Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1737 | 1738 | (Page 1739) | 1740 | 1741 | .... | 3270 | newer

  0 0


  Na Mathew Kwembe, Mtwara

  Waganga wafawidhi wa vituo vya afya, na Waratibu elimu kata kutoka Halmashauri 93 zilizo katika mikoa 13 nchini inayotekeleza Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) nchini wameanza mafunzo ya siku mbili juu ya namna ya kutumia mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS).

  Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Tehama na Mawasiliano kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) bwana Desderi Wengaa, mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo watoa huduma katika vituo vya kutolea huduma na kusaidia upatikanaji wa taarifa sahihi katika mahesabu ya mapato na matumizi ya halmashauri.

  Bwana Wengaa alisema kuwa kuunda kwa mfumo huo kutasaidia kuhakikisha fedha za ruzuku zinasimamiwa vizuri na taarifa za matumizi yake zinatolewa kwa usahihi tofauti na ilivyokuwa mwanzo.Alisema kuwa FFARS itawapatia watoa huduma mfumo sanifu uliorahisishwa ambao utawawezesha kutunza taarifa za fedha zinazotolewa na zilizopo katika vituo vyao. 

  Bwana Wengaa aliongeza kuwa FFARS itaweza kufuatilia matumizi ya fedha hizo katika kufikia malengo ya utoaji huduma na kuhakikisha yanaendana na sheria za manunuzi na utoaji taarifa. “Taarifa hizi zitasaidia Serikali kuimarisha Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma na kuongeza uwazi, na hivyo watoa huduma wa afya kuwa na wajibu kwa jamii wanayoihudumia,” alisema.
  Mkuu wa Kitengo cha Tehama na Mawasiliano kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) bwana Desderi Wengaa akizungumza na waratibu elimu kata na waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka Manispaa ya Mtwara Mikindani na Mtwara DC (hawapo pichani) kuhusu malengo ya kuanzishwa kwa mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS).
  Baadhi ya Waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka Manispaa ya Mtwara Mikindani na Mtwara DC wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Mhandisi Sambwe Sijabaje (hayupo pichani) wakati alipofungua mafunzo ya siku mbili kuhusu namna ya kuutumia mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS).
  Baadhi ya Waratibu wa Elimu Kata kutoka Manispaa ya Mtwara Mikindani na Mtwara DC wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Mhandisi Sambwe Sijabaje (hayupo pichani) wakati alipofungua mafunzo ya siku mbili kuhusu namna ya kuutumia mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS).


  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya mpira kutoka kwa Afisa Masoko Msaidizi wa kampuni ya soda ya Coca Cola Bi. Pamela Lugenge kama ishara ya kuendeleza michezo nchini na pia kwa ajili ya kumsaidia kuendeleza mazoezi yake binafsi wakati wa ufunguzi wa mashindano ya 38 ya UMISSETA na ya 22 ya UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa mashindano ya 38 ya UMISSETA na ya 22 ya UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassanakirusha mpira kuashiria ufunguzi wa mashindano ya 38 ya UMISSETA na ya 22 ya UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
  Vijana wakionesha utayari wao wa kushiriki michezo wakati wa mashindano ya 38 ya UMISSETA na ya 22 ya UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.


  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 

  0 0

  Shirika linaloongoza katika kutoa huduma za malipo Direct Pay Online ni mdhamini wa maonyesho makubwa ya utalii na biashara kanda ya Afrika Mashariki ya KILIFAIR 2017. Maonyesho hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Ushirika tarehe 2 hadi 4 mwezi Juni mwaka huu yalikusanya wafanyabiashara zaidi ya 300 kutoka Tanzania na nchi jirani na kuwa na wageni zaidi ya 3000 kutoka nje na ndani ya nchi. 

  “Tunajivunia kuwa wadhamini wa kiwango hiki cha platinamu katika maonyesho makubwa kama haya. Hii ni fursa muhimu kwa kampuni yetu ya DPO kujitangaza kwa kazi kubwa tunayofanya ya kurahisisha malipo haswa kwa sekta ya safari,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa DPO Eran Feinstein. 

  Katika bidhaa zilizokuwa katika maonyesho kwende banda la DPO ni pamoja na huduma ya bure inayoitwa MarketPlace ambayo iko wazi kwa wafanyabiashara na wateja wote wa hoteli, safari, mawakala na maduka wa DPO wanaotumia tovuti hiyo na huduma nyingine kuuza bidhaa zao na pia kuwapatia fursa ya kujitangaza ulimwenguni bure. DPO pia ilionyesha jinsi ya kutumia programu ya DumaPay ambayo inawezesha wafanyabiashara kuwatoza wateja wao kutumia teknolojia inayosoma kadi kwa usalama mahali popote na muda wowote. Mteja huweza kulipa kupitia kadi au simu kwa sarafu wanayopendelea.  Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Direct Pay Online Group, Eran Feinsten (kushoto) jinsi wanavyotumia mfumo wa mawasiliano kutuma na kupokea fedha katika banda la kampuni hiyo katika maonesho ya Utalii na Viwanda ya Kili Fair yaliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi katikati ni Mkuu wa wilaya ya Moshi, Kippi Warioba.


  Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na maafisa wa kampuni ya Direct Pay Online, Kate Gathii (kushoto) ambaye ni Mkuu wa Masoko na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Eran Feinsten (wa pili kushoto) alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya Utalii na Viwanda ya Kili Fair yaloyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi kuanzia taerehe 2 Juni, wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na Mkuu wa wilaya ya Moshi, Kippi Warioba. 

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) akikaribishwa na Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Direct Pay Online, Kate Gathii (kushoto) alipotembelea banda la kampuni hiyo ambao ni platnimu sponsor wa maonesho ya Utalii na Viwanda ya Kili Fair yaliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi kuanzia tarehe 2 June. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo,Eran Feinsten,wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na Mkuu wa wilaya ya Moshi.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Balozi wa Morocco nchini, Mheshimiwa Abdelilah Benrwayane katika futari aliyoiandaa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Juni 8, 2017.
  Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza na Mwenyekiti wa Bunge, Azan Mussa Zungu (kulia kwake), Mbunge wa Mbarali, Haroon Mulla Pirmohamed (wapili kushoto) na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa, Valentino Mlowola katika futari iliyoandaliwa wa Waziri Mkuul Kassim Majaliwa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 8, 2017
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mbunge wa Nsimbo, Mhandisi Richard Mbogo baada kufuturisha kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 8, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  ‘SHIRAWADU’ ni ngoma mpya kabisa ya mduara ambayo wiki hii imeachiwa rasmi kutoka kwa msanii anayekuja juu kwa kasi ya ajabu, Shania Kabeya.

  Studio ya 442 Music iliyoko Karakata, Kipawa, jijini Dar es Salaam chini ya Mtayarishaji Tamimu Hamis ‘Mabanga’ ndipo ilipopikwa ngoma hiyo iliyobeba ujumbe mzito juu ya wapenzi wanavyotakiwa kutoyafuatilia maneno ya watu wa pembeni.

  Kwa upande wake Shania mwenyewe, hii ndio ngoma yake ya kwanza ambapo hata hivyo yuko mbioni kuandaa kazi nyingine ‘sumu’, anazoamini kuwa zitabamba zaidi na kutokea kufunika nyingine zitakazozikuta.
  Video ya kibao ‘Shirawadu’ iko jikoni na itatoka mwishoni mwa mwezi huu, ikiwa sambamba na kibao chake kingine kipya cha mduara. 


  0 0


  0 0  Mratibu wa Masoko wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa akimkabidhi kompyuta mbili Kaimu Mkurugenzi wa Mbulu, mkoani Manyara, Deogratias Kashasha.


  Na Mwandishi Wetu, Mbulu
  KWA miezi kadhaa sasa mvua imeendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, hali inayoonyesha kukidhi kiu ya watu wengi waliokuwa wakiiomba inyeshe katika maeneo yao.

  Hata hivyo, licha ya mvua hiyo kunyesha, lakini baadhi ya maeneo imekuwa na matokeo mabaya kutokana na kuezua nyumba, kuharibu miundo mbinu muhimu ikiwamo ya barabara.

  Matokeo hayo yameibua changamoto mpya hususan za kufikika kwa urahisi katika maeneo hayo yanayoendelea kukumbwa na mvua kubwa. Mbali na mvua hiyo kunyesha, hata hivyo uwajibikaji unaendelea kufanyika kwa sekta na watu mbalimbali kuendelea na maisha yao ya kila siku ili wakuze uchumi.
  Zoezi la kutoa msaada wa kompyuta lilivyokuwa linaendelea katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.


  Licha ya maeneo mengi kukumbwa na mvua, lakini Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services imeendelea na usambazaji wa kompyuta katika ofisi za serikali mikoani kama ilivyozindua utaratibu huo mwishoni mwa mwaka jana.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akitia saini kitabu cha maombolezi kufuatia kifo cha Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia idadi ya Watu Duniani Dr. Babatunde Osotimehin kilichotokea tarehe 4/06/2017.
  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani Batula Abdi wakati alipokwenda kutia saini kitabu cha maombolezi kufuatia kifo cha Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia idadi ya Watu Duniani Dr. Babatunde Osotimehin kilichotokea tarehe 4/06/2017.

  PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

   Naibu Gavana Dkt. Yamungu Kayandabila akilakiwa na afisa uhusiano Bi. Victoria Msina alipowasili kuanza kazi rasmi Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es salaam

   Naibu Gavana Dkt. Yamungu Kayandabila akilakiwa na maofisa alipowasili kuanza kazi rasmi Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es salaam
   Naibu Gavana Julian Banzi Raphael(katikati) akifanya mazungumzo mafupi na Naibu Gavana Dkt. Kayandaliba alipotembelea ofisini kwake.

  Naibu Gavana Julian Banzi Raphael(katikati) akifanya mazungumzo mafupi na Naibu Gavana Dkt. Kayandaliba alipotembelea ofisini kwake.


  0 0


    Wageni wilayani Muheza Mkoani Tanga wakipata futari iliyoandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza, Mhandisi Hajat Mwanasha Tumbo 
    Wageni wilayani Muheza Mkoani Tanga wakipata futari iliyoandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza, Mhandisi Hajat Mwanasha Tumbo 
   Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi katikati anayefuatia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza (DAS) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza, Luiza Mlelwa wakipata futari iliyoandaliwa na mkuu huyo wa wilaya nyumbani kwake.
   Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi wakipata futari iliyoandaliwa na Mkuu huyo wa wilaya.Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na waandishi wa habari ambapo alitoa shukrani kwa kuitikia mwitikio wa futari hiyo.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Massauni, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu utekelezaji wa mpango mkakati wa kupunguza ajali za barabarani nchini katika kipindi cha miezi sita, mjini Dodoma leo, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani.
   Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia), akifafanua jambo katika mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu hatua za utekelezaji wa mpango mkakati wa kupunguza ajali za barabarani nchini katika kipindi cha miezi sita, mjini Dodoma leo, kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhandisi  Hamad Massauni.
   Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Julius Chambo (Kushoto), akisikiliza kwa makini taarifa ya utekelezaji wa mpango mkakati wa kupunguza ajali za barabarani nchini katika kipindi cha miezi sita, iliyotolewa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhandisi Hamad Massauni (hayupo pichani), mjini Dodoma leo.
  Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Massauni, akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango mkakati wa kupunguza ajali za barabarani nchini katika kipindi cha miezi sita kwa wajumbe na waandishi wa habari, mjini Dodoma leo. 

  Imetolea na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano


  0 0

  Na Stella Kalinga, Simiyu
  Shirika la Kidini la Madhebu ya Kikristo la Life Ministry limetoa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 40 kwa Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu, Mjini Bariadi.
  Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.  Anthony  Mtaka ameishukuru Life Ministry kwa msaada huo na kuwahakikishia kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi katika hospitali hiyo.
  Aidha, amesema Serikali iko tayari kushirikiana na madhehebu ya dini katika  kuhakikisha kuwa afya za wananchi zinakuwa salama, hivyo akawahakikishia kuwa  milango iko wazi kwa taasisi nyingine za dini zinazotaka kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za afya.
  Mtaka ameongeza kuwa ili Madaktari na wauguzi waweze kutekeleza majukumu yao vizuri ni lazima wawezeshwe vifaa, hivyo msaada huo utawatia moyo na kuongeza ari ya kufanya kazi.
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Life Ministry hapa nchini, Dismas Shekalaghe amesema vifaa hivyo vimetolewa kama sehemu ya kuisaidia jamii ambavyo vitawawezesha madaktari na wauguzi kuwahudumia wananchi.
  Shekalaghe ameongeza kuwa wao wanaamini kuwa ili mtu aweze kumtumikia Mungu  ni lazima awe na afya njema, hivyo kupitia msaada huo wa vifaa wagonjwa watahudumiwa na kurudi katika hali zao kawaida na kuendelea kumtumikia Mungu na kufanya shughuli za maendeleo.
   Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.  Anthony Mtaka(katikati), Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Mkoa, Dkt. Fredrick Mlekwa(kushoto) wakipokea baadhi ya vifaa vilivyotolewa  Life Ministry kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika hilo la dini, Bw. Dismas Shekalaghe(Kulia).

   Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.  Anthony  Mtaka(katikati), Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Mkoa, Dkt. Fredrick Mlekwa(kushoto) wakikabidhiwa viti vya kubebea wagonjwa na Mkurugenzi wa Life Ministry Bw. Dismas Shekalaghe (kulia).  ambavyo ni miongoni mwa vifaa vilivyotolewa  Shirika hilo la Kikristo kwa Hospitali Teule  ya Mkoa wa Simiyu.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Semina ya Mtandao wa Wabunge Afrika Tawi la Tanzania walio katika Mapambano Dhidi ya Rushwa (APNAC). Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Naibu Spika, Dkt. Tulia Akson na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki, Kulia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge Tawi la Tanzania walio katika Mapambano Dhidi ya Rushwa (APNAC) Kepteni Mstaafu (MB) John Mkuchika, na Mbunge wa wa Manyoni Mashariki Daniel Mtuka Nyuma walio simama ni waBunge wanao shiriki Semina hiyo ya siku Mbili ambayo inaendeshwa na UNDP. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimina na Mshauri wa Maswala ya Bunge kutoka ofisi ya Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa Tawi la Tanzania ,Bibi Anna Hovhannesyan , baada ya kufungua Semina ya Mtandao wa Wabunge Africa Tawi la Tanzania walio katika Mapambano Dhidi ya Rushwa (APNAC) Semina hiyo ya siku mbili inafanyika Mkoani Dododma katika ukumbi wa Hoteli ya African Dreams . June 9, 2017 na June10,2017 nakuendeshwa na UNDP.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki ,baada ya kufungua Semina ya Mtandao wa Wabunge wa Africa Tawi la Tanzania walio katika Mapambano Dhidi ya Rushwa (APNAC) katikati ni Naibu Spika Dr Tulia Akson, Semina hiyo ya siku mbili inafanyika Mkoani Dododma katika ukumbi wa Hoteli ya African Dreams . June 9, 2017 na June10,2017 nakuendeshwa na UNDP.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

  Wadau na wachumi mbalimbali wametoa maoni tofauti kuhusu bajeti ya serikali ya mwaka 2017/2018 iliyowasilishwa jana Bungeni na Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango na kusema kuwa ni mapema mno kuisherehekea.

  Wakizungumza katika mkutano wa kujadili bajeti hiyo ulioandaliwa na kampuni ya ukaguzi ya Ernst and Young (EY),wamesema, ni vema kusubiri mabadiliko ya sheria ya fedha ili kuja kuona mpango wa utekelezaji wake.
  Mkurugenzi wa Utawala na Kodi wa Kampuni ya Ukaguzi ya EY (Ernest & Young), Laurian Justinian akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau na Wachumi mbali mbali wa kujadili Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18, ulioandaliwa na Kampuni ya Ukaguzi ya EY (Ernest & Young), katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam Juni 9, 2017.

  Wameongeza kuwa, uzoefu unaonyesha kuwa, mara nyingi bajeti inakuwa na mambo mazuri lakini utekelezaji wake unakuwa ni tofauti kwani hata ile iliyopita utekelezaji wake haukuridhisha.
  Wamesema kuwa, ni vizuri wananchi wakaacha kusherehekea badala yake kuona utekelezaji na kama ikibidi  waje washerehekee mwezi Juni mwakani.


  Akitoa maoni yake katika majadiliano hayo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha  Mzumbe na  Mshauri wa Uchumi, Profesa Honest Ngowi amesema bajeti ya mwaka jana haikutimia kabisa, malengo yalikuwa kukusanya Tirioni 29.5 lakini ilipatikana  Tirioni 20.1 ambayo ni sawa na asilimia 70.1 na bajeti ya mwaka huu ni Tirioni 31.6 ongezeko la tirioni 11. je nini kitafanyika kupata fedha hizo za mwaka huu.

  Amesema kuwa kuna masuala mengi ambayo ni lazima yaelezewe sheria ya fedha kwa jinsi itakavyokuwa inatekelezwa ikiwa ni pamoja na kupunguza misamaha isiyokuwa ya lazima.
  Amesema bajeti hii inaleta neema kwa wakulima ambao walikuwa wanalipa tozo kwa ukomo wa asilimia tano lakini sasa watakuwa wakilipia ukomo wa asilimia tatu tu.
   Aidha ameongeza pia kuondolewa kwa kodi ya leseni Ya magari kutawapunguzia wananchi mzigo mkubwa, hasa wale ambao magari yao hayakuwa yakitumia klwa muda mrefu lakini bado yalikuwa yanahesabiwa kodo kama kawaida.

  Ameongeza kuwa, uchumi wa Tanzania na Africa Mashariki kwa ujumla unaenda kwenye viwanda, na kuna mambo mengi ya kikodi yamejitokeza ya  kulinda viwanda vya ndani kwa maana hiyo kuongezeka kwa kodi kwenye vitu vitakavyokuwa vinaingia ndani yan chi hizo kutakuwa kunalinda soko la ndani.

  “Changamoto kubwa itakuwa namna ya kupata fedha zote hizo Tilioni (31.6) hatujajua ni nini cha tofauti kimefanywa tofauti na miaka mingine kusudi kuweza kupata fedha hizo ambazo kwa mwaka jana tulishindwa kupata 29.5 tukaishia kugonga kwenye Trn 20.

  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe na Mshauru wa Maswala ya Fedha na Uchumi, Prof. Honest Ngowi akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau na Wachumi mbali mbali wa kujadili Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18, ulioandaliwa na Kampuni ya Ukaguzi ya EY (Ernest & Young), katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam Juni 9, 2017.

  Ameongeza kuwa ili kuweza kujaribu kufikia lengo hilo TRA wanatakiwa kukusanya kodi kistaarbu bila ya kutumia nguvu na mabavu, Mkurugenzi wa kodi wa EY Laurian Justinian amesema bajeti inamuelekeo mzuri, inaaanza kuonyesha picha ya kuingia kwenye viwanda but kunamasuala yanatakiwa kuwa na wiano.

  Muanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Pangani group Heri Bomani amesema Serikali imekuwa ikiwekeza zaidi kwenye miundombinu na sasa inahama kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
  Muanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Pangani Group, Heri Bomani akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau na Wachumi mbali mbali wa kujadili Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18, ulioandaliwa na Kampuni ya Ukaguzi ya EY (Ernest & Young), katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam Juni 9, 2017. Wengine pichani kutoka kulia ni Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Mzumbe na Mshauru wa Maswala ya Fedha na Uchumi, Prof. Honest Ngowi, Mkufunzi, Mtafiti na Mshauri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dkt. Faisal Issa pamoja na Mkurugenzi wa Utawala na Kodi wa Kampuni ya Ukaguzi ya EY (Ernest & Young), Laurian Justinian. 


  0 0

  Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya tatu, Ali Hassan Mwinyi (kushoto) akiagana na Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas (katikati) mara baada ya kumalizika kwa tafrija ya futari maalumu kwaajili ya Wateja wa NMB walio kwenye mfungo Mtufu wa Ramadhani. Hafla hii ya Futari ilifanyika Jijini Dar es Salam juzi. Kulia ni Mkurugenzi wa wateja wadogo na wakati wa NMB, Abdulmajid Nsekela. Rais Mstaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto) akiagana na baadhi ya wateja wa Benki ya NMB baada ya kumalizika kwa tafrija ya futari maalumu kwa ajili ya Wateja wa NMB walio kwenye mfungo Mtukufu wa Ramadhani. Baadhi ya wateja wa Benki ya NMB wakijumuika katika tafrija ya futari maalumu kwa ajili ya wateja wa benki hiyo walio kwenye mfungo Mtukufu wa Ramadhani jijini Dar es Salaam. Baadhi ya maofisa waandamizi wa Benki ya NMB wakiwa na viongozi mbalimbali waalikwa katika hafla hiyo.

  0 0

   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Balozi mdogo wa Marekani nchini Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Inmi Patterson, pale alipomtembelea  leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza jambo pale alipotembelewa na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini Tanzania, wakiongozwa na Balozi wa Uingereza nchini, Mheshimiwa Sarah Cooke(kulia kwake) katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati)akimsikiliza Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mheshimiwa Sarah Cooke (wa pili kushoto) pale Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini Tanzania walipomtembelea leo ofisini kwake Mjini Dodoma.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Benjamin Sawe

  MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Mei, 2017 umepungua hadi asilimia 6.1 kutoka asilimia 6.4 ilivyokuwa mwezi Aprili, 2017. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo amesema kupungua kwa mfumuko wa bei kunatokana na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwezi Aprili, 2017.

  “Mfumuko wa Bei wa Taifa umepungua kutoka asilimia 6.4 kwa mwezi Aprili, 2017 hadi kufikia asilimia 6.1 kwa mwezi Mei , 2017 kutokana na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Mei, 2017,” amesema Kwesigabo. Kwesigabo amesema Mfumuko wa Bei wa mwezi Mei, 2017 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.2 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.5 ilivyokuwa mwezi Aprili, 2017.

  Amesema Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 109.26 kwa mwezi Mei, 2017 kutoka 109.04 mwezi Aprili, 2017 kutokana na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.

  Kwesigabo ametaja bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi kuwa ni pamoja na mahindi yaliyoongezeka kwa asilimia 4.2, maharage mabichi kwa asilimia 2.9, maharage ya soya kwa asilimia 2.2, unga wa mtama kwa asilimia 1.5, viazi mviringo kwa asilimia 2.0, mihogo mikavu kwa asilimia 2.3, na magimbi kwa asilimia 2.5.

  Aidha bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na mkaa ulioongezeka kwa asilimia 2.5. Ameongeza kuwa Mfumuko wa Bei kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Mei, 2017 umepungua hadi asilimia 11.8 kutoka asilimia 12.0 mwezi Aprili, 2017. Aidha, badiliko la Fahirisi za Bei kwa bidhaa zisizo za vyakula umepungua hadi asilimia 3.0 mwezi Mei, 2017 kutoka asilimia 3.4 mwezi Aprili, 2017.
  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo akiongea na wanahabari kuhusu Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Mei 2017 jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Honorius Mpangala

  Moja ya misemo ya kiswahili inayopendwa kutumuwa na watanzania ni "usijisifie una mbio bali msifie na anayekukimbiza" msemo huu ungekuwa bora sana kuwa elezea klabu ya Simba kuwa walikua vyema msimu tofauti na msimu uliopita.

  Msimu wa 2016/17 kwa upande wa klabu ya Yanga unaweza kusema ulikua mgumu sana na huenda ungewanyima taji kama tu wasingechukua maamuzi magumu baada ya kuona watu wanapangwa katika kikosi kwa mazoea,binafsi naamini taji la Yanga ni kwa marekebisho makubwa yaliyofanyika na Kocha George Lwandamina.

  Tathimini yangu kwa msimu mzima kwa klabu ya Yanga.

  Moja ilianza ligi ilikuwa na mchoko wa hali ya juu baada ya kuumaliza mwaka mzima wa kalenda wa 2016 kwa kufululiza kucheza mechi ikiwa ni kitu ambacho haikuzoeleka kwa wachezaji wake.

  Mbili kiburi cha kujiona wakimataifa  kulisababisha Yanga iweza kuona michezo kama dhidi ya Stands Utd, Ndanda, Mbeya City kuwa migumu kwao tofauti na ilivyokua msimu uliopita.

  Tatu,klabu ya yanga kukumbwa na changamoto ya mishahara ilikua ni moja ya sababu iliyowafanya wachezaji kukutwa na visununu kama Yale yaliyotokea kwa Vincent bossou aliyekuja kutofautiana na uongozi kwasababu ya malipo ya mshahara wake kama ilivyokua kwa Obrey Chirwa.

  Majeruhi ya key player kama Juma Abdul, Donald Ngoma,Thaban Kamusoko, Amis Tambwe kwa nyakati tofauti watu waliochukua nafasi zao hawakuweza kuwa fit na kuisaidia klabu kucheza kwa kasi na kiwango kama cha waliopata majeruhi.
  Nne, Matatizo ya Mwenyekiti wa klabu kulimfanya kukaa mbali na kushindwa kuwa karibu na wachezaji ambao waliamini uwepo wake katika kuwasapoti kulitoa hamasa kubwa kwao.

  Tano, kuna haja kubwa ya kuandaa mikakati ya kuweza kufanikiwa katika michezo ya kimataifa kwani japo msimu uliopita timu iliishia hatua ya robo fainali ila mapungufu yalikuwa mengi kwasababu ya maandalizi ya klabu katika kuwakabili wapinzani wao.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  HALMASHAURI ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam imetiliana saini ya mikataba 30 yenye thamani ya Sh. bilioni nne na Wakandarasi kutekeleza shughuli mbalimbali katika halmashauri hiyo.

  Akizungumza wakati wa utilianaji saini hizo uliofanyika katika Ofisi za Halmashauri hiyo Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, John Kayombo alizitaja shughuli zitakazohusika katika mikataba hiyo kuwa ni pamoja na usafi, barabara  na miradi ya maji.

   Meya wa Ubungo, Boniface Jacob (katikati)na  Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, John Kayombo (wa kwanza kulia ) wakisani mkatamba na Mkurungenzi wa Kampuni ya Invostment , Rukia Punzi leo jijini Dar es Salaam.

   “Manispaa yetu ina miezi minane tu lakini tumefanikiwa kusaini mkataba 30 ya miradi mbalimbali, tunaposaini mikataba hii inaonesha wazi kuwa Manispaa yetu inakua.

  “Ombi langu kwenu, nendeni mkatekeleze kile kilichopo kwenye mikataba na bahati nzuri siwafahamu sitaweza kusita kuchukua hatua kama Meya, nitasimamia sheria sitapindisha pale nitakapoona kazi imeenda ovyo sitakuwa tayari kufungwa pingu” amesema Kayombo.

  Kayombo aliwataka wakandarasi hao kuhakikisha wanatekeleza miradi waliokubalia isiishie kusaini kisha wakapotelea mitini.

  Naye  Meya wa Manispaa hiyo, Boniphace Jacob, aliwataka wakandarasi hao kuhakikisha wanatekeleza miradi hiyo katika kiwango walichokubaliana na kuwa atakayetekeleza kinyume atanyang’anywa na kupewa mtu mwingine fedha zitarudishwa .

  “Ukipewa miezi miwili ikiisha kabidhi mradi, mkurugenzi ukikuta mtu anayefanya kazi ya usafi hajasafisha au  mtu yeyote atakayekiuka mkataba tusiwe na aibu ya kumwajibisha” amesema Jacob.
   Meya wa Ubungo,  Boniface Jacob (kushoto)  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, katika hafla ya kusaini mikataba 30 yenye thamani ya Sh.bilioni Nne na wakandarasi kutekeleza shughuli mbalimbali katika Halmashauri hiyo. kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, John Kayombo,
  Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, John Kayombo akizungumza katika hafla ya kusani mikataba 30 yenye thamani ya Sh bilioni nne na wakandarasi kutekeleza shughuli mbalimbali katika halmashauri hiyo.
   Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, John Kayombo akibadilishana hati za makubalino na Mkurungenzi wa Kampuni ya Invostment Rukia Punzi leo jijini Dar es Salaam.,katikati ni Meya wa Ubungo Mh. Boniface Jacob.

older | 1 | .... | 1737 | 1738 | (Page 1739) | 1740 | 1741 | .... | 3270 | newer