Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1724 | 1725 | (Page 1726) | 1727 | 1728 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na waandishi wa habari baada ya Kuzindua Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi, Harrison Mseke. 
   Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Kigoma (CCM), Mhandisi  Atashasta Nditiye (kushoto), akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Daniel Nsanzugwako pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi, Harrison Mseke, wakifuatilia Mada inayohusu Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi iliyokuwa inatolewa na Mratibu wa Mpango huo kutoka Idara ya Huduma za Wakimbizi, Dk. John Jingu (hayupo pichani), muda mfupi kabla ya Uzinduzi wa Mpango huo.
   Sehemu ya Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi zake nchini  pamoja na Wawakilishi wa Taasisi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga, akijibu maswali ya waandishi wa habari  wakati wa uzinduzi wa  Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamadi Masauni (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Katavi, Tabora, Kagera na Kigoma, watendaji wa serikali na Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa yanayofanya kazi nchini, wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 

  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI –WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0

   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akifurahia zawadi ya 'Hotpot' baada ya kukabidhiwa na Umoja wa Vijana wa CCM, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Buhigwe, mkoani Kigoma, leo, kuendelea na ziara yake ya Kichama mikoani.
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akiwasalimia baadhi ya viongozi kabla ya kuingia ofisini, katika Ofisi ya CCM wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma leo
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo (kushoto) akiwaunga mkono kuselebuka, wana CCM waliokuwa wakijimwayamwaya kwa nyimbo za mapokezi, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, leo
   Wana CCM wakihanikiza shamrashamra nje ya Ofisi ya CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Ahaj Abdallah Bulembo alipowasili kwenye Ofisi hiyo,leo.
   Mbunge wa Viti Maalum Josephine Ngezabuke, akishiriki kuselebuka na wana CCM waliokuwa wakijimwayamwaya kwa nyimbo za mapokezi ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa CCM, Alhaj Abdallah Bulembo kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, leo. PICHA: BASHIR NKOROMO


  0 0


  0 0  Mkurungezi Mtendaji na Muanzilishi wa IswapMyBooks.Com Shafiq Mpanja akifafanua jambo kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa Mtandao huo unaowezesha wasomaji wa vitabu kubadilishana vitabu mara tu wanapomaliza kuvisoma kwa njia ya mtandao huo.Hafla ya uzinduzi huo zilifanyika mapema jana katika makao makuu ya SOMA BOOK Cafe iliyopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.


  Meneja Uendeshaji wa IswapMyBooks.com Viola Massawe akifafanua taratibu za matumizi ya mtandao huo , wakati wa uzinduzi wa Mtandao huo unaowezesha wasomaji wa vitabu kubadilishana vitabu mara tu wanapomaliza kuvisoma kwa njia ya mtandao huo.Hafla ya uzinduzi huo zilifanyika mapema jana katika makao makuu ya SOMA BOOK Cafe iliyopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.

  Mkurungezi Mtendaji wa Soma Book Cafe Demera Kitunga akielezea umuhimu wa kujisomea kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi  wakati wa uzinduzi wa Mtandao wa IswapMyBooks.com, Mtandao huo unaowezesha wasomaji wa vitabu kubadilishana vitabu mara tu wanapomaliza kuvisoma kwa njia ya mtandao huo.Hafla ya uzinduzi huo zilifanyika mapema jana katika makao makuu ya SOMA BOOK Cafe iliyopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.  Mdau akichangia jambo wakati wa uzinduzi wa IswapMyBooks.com , Mtandao huo unaowezesha wasomaji wa vitabu kubadilishana vitabu mara tu wanapomaliza kuvisoma kwa njia ya mtandao huo.Hafla ya uzinduzi huo zilifanyika mapema jana katika makao makuu ya SOMA BOOK Cafe iliyopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.
  Mkurungezi Mtendaji wa Koncept Krantz Mwantepele (mwenye koti la suti) na wadau wa usomaji wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa mtandao wa IswapMyBooks.com , Mtandao huo unaowezesha wasomaji wa vitabu kubadilishana vitabu mara tu wanapomaliza kuvisoma kwa njia ya mtandao huo.Hafla ya uzinduzi huo zilifanyika mapema jana katika makao makuu ya SOMA BOOK Cafe iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
  Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Wavuvi wakiwa katika Mwalo wa Katonga Mkoani Kigoma wakijiandaa kuingia katika Ziwa Tanganyika kuvua Dagaa kama walivyokutwa na mdau Raymond Mushumbusi leo

  0 0


  0 0

  Wachezaji wa timu ya Tusker ya Kenya wakiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, tayari kwa ajili ya michuano ya Sportpesa itakayo anza kutimua vumbi Juni 5 mwaka huu katika uwanja wa Uhuru maalufu kama shamba la bibi. Michuano hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya Sport Pesa kwa kuzishirikisha timu zinazo dhaiminiwa na kampuni hiyo za nchi ya Kenye na Tanzania.  Wachezaji wa timu ya Tusker ya Kenya wakiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, tayari kwa ajili ya michuano ya Sportpesa itakayo anza kutimua vumbi Juni 5 mwaka huu katika uwanja wa Uhuru maalufu kama shamba la bibi.Michuano hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya Sport Pesa kwa kuzishirikisha timu zinazo dhaiminiwa na kampuni hiyo za nchi ya Kenye na Tanzania. 

  Picha na Mafoto Blog

  0 0

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza
  MFUKO wa Pensheni wa PSPF umewaleta poamoja watumishi wa umma kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza zaidi ya 450, ambao wanatarajiwa kustaafu hivi karibuni ili kuwapatia semina ya mafunzo itakayowawezwesha kujiandaa kustaafu kwa amani.
  Katika semina hiyo iliyoanza leo Juni 2, 2017 kwenye ukumbi wa chuo cha BoT Capri-point  jijini Mwanza, wadau wa PSPF ambao ni taasisi za fedha nao wametumia fursa hiyo kutangaza fursa mbalimbali ambazo wastaafu hao wanaweza kuzitumia ili kuendeleza maisha yao ya baadaye.
  Wadau hao ni pamoja na Mwalimu Commercial Bank, (MCB), NMB, CRDB, TPB na Mfuko wa UTT-AMIS, pia Shirika la Viwanda Vidogovidogo SIDO.
  Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko, Mwalimu Commercial Bank, (MCB),Bw. Valence Luteganya, akizungumzia huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo. "Beni hii imeanzishwa hivi karibuni na wamiliki wa benki hii kwa karibu asilimia 30 ni walimu. na huduma tunazozitoa ni pamoja na utoaji mikopo nafuu, ushauri wa kifedha lakini pia katika jiyihada za kurahisisha huduma za kibenki, MCB imo kwenye mtandao wa Umoja Switch ambao umetapakaa nchi nzima." hayo ni baadhi ya maneno ya Bw. Lutenganya
   Bw. Lutenganya, akifafanua zaidi huduma zitolewazo na benki ya MCB

  Mkuu wa kitengo cha  wateja binafsi benki ya NMB, Bw.Omary Mtiga, akitoa somo kuhusu fursa mbalimbali ambazo wastaafu hao watarajiwa wanaweza kuzipata. "Benki ya NMB ina matawi kote nchini na hivyo inaweza kukufikishia huduma hapo ulipo pasina shaka, kwenu nyinyi ambao wengi wenu ni wateja wetu, mnayo fursa ya kufungua Bonas account ambayo inakuwezesha kufikia malengo mbalimbali uliyojiwekea na inaweza kutunza amana zako kwa usalama na kufikia malengo yako ya baadaye uliyojiwekea, lakini kubwa zaidi hakuna gharama za kuendesha akaunti hii." alisema
   Mkurugenzi wa idara ya mikopo benki ya Posta Tanzania, (TPB), Bw. Henry Bwogi, akizoa mada kwa washiriki ambapo alisema, "TPB ndiyo benki kongwe kuliko zote hapa nchini ikiwa na matawi yaliyosambaa kila kona ya nchi na hivyo kuwa rahisi kwa wateja kufikiwa na huduma zake, lakini pia benki hiyo tayari imeonyesha nia ya dhati ya kuwajali wastaaafu ambapo imekwisha toa mikopo ya mabilioni ya shilingi kwa wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
   Bi Doris Mlenge, Afisa Masoko wa Mfuko wa UTT-AMIS, akiwapatia vipeperushi vyenye maelezo ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo. "Kwa mtu yeyote anayetegemea kupata kipato kwa mkupuo kutokana na pensheni au chanzo kingine cha fedha anatakiwa kuwekeza kwenye Mfuko huo ili aweze kupata kipato cha mara kwa mara na akasema kuwekeza kwenye mifuko ya kujikimu kama UTT-AMIS kunatoa faida kubwa ukilinganisha na uwekezaji wa namna hiyo kwenye masoko ya fedha.

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
  UONGOZI wa Klabu ya Azam umethibitisha rasmi kuachana rasmi na winga wake Khamis Mcha ‘Vialli’ na Ame Ally, aliyekuwa kwa mkopo Kagera Sugar ikiwa ni baada ya mapema wiki kutoa taarifa ya kuachana na mshambuliaji wao John Raphael Bocco.
  Akizungumza na waandishi wa habari, Msemaji wa timu ya Azam Jaffar Iddy  (pichani) amesema kuwa wachezaji  wote mikataba yao imemalizika na hawapo katika mipango ya kocha mkuu kwa sasa kwahiyo wameona ni bora watoe taarifa mapema.
  Taarifa iliyotolewa leo na msemaji wa klabu hiyo, imeeleza kuwa kuelekea msimu ujao na kuendelea, Azam FC itaweka msisitizo na kufanya uwekezaji ipasavyo kwenye kituo chake cha kukuza vipaji ‘Azam Academy’ ili kuvuna wachezaji bora watakaopandishwa katika kikosi cha timu kubwa.Kwa kuanzia katika kutekeleza malengo hayo, kuelekea msimu ujao Azam FC imewapandisha wachezaji sita kutoka kwenye kituo chake, ambao ni mabeki Abbas Kapombe, Abdul Haji, Godfrey Elias, kiraka Ramadhan Mohamed, kiungo Stanslaus Ladislaus na mshambuliaji Yahaya Zaid, aliyekuwa mfungaji bora wa Ligi Daraja Kwanza (FDL) msimu uliopita kwa mabao 12 aliyofunga alipokuwa kwa mkopo Ashanti United.

  Mbali na hilo klabu ya Azam imefanya mabadiliko kwenye mfumo wa uongozi na katika  hatua nyingine, Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC imefanya mabadiliko ya mfumo wa kiuongozi ya timu hiyo kwa kukifuta cheo cha Ofisa Mtendaji Mkuu, na sasa cheo cha juu kitakuwa ni Meneja Mkuu, nafasi inayoshikiliwa na Abdul Mohamed.

  Kutokana na mabadiliko hayo ya kiutendaji, aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu, Saad Kawemba, amemaliza mkataba wake na pande zote mbili zimekubaliana kuachana, na sasa majumuku yake yote yatafanywa na Abdul Mohammed, akiwa ndio Meneja Mkuu wa klabu.
  Azam FC imekuwa na utaratibu mzuri wa kulea wachezaji wake vijana kwa kuwapandisha kwenye timu kubwa, ambao wamekuwa wakifanya vizuri na kuibeba timu, ambapo wengine waliopo katika kikosi cha wakubwa ni makipa Aishi Manula, Metacha Mnata, mabeki Gadiel Michael, Ismail Gambo, kiungo Mudathir Yahya, Abdallah Masoud, Himid Mao, Joseph Mahundi na mshambuliaji Shaaban Idd.Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, aliyeongezewa mkataba wa mwaka mmoja, anaamini ya kuwa wachezaji hao vijana watazidi kukiimarisha kikosi chake kwa kushirikiana na wachezaji wazoefu waliopo kikosini, hadi anafikia uamuzi huo wa kuwapandisha aliwafuatilia katika mechi mbalimbali za timu ya vijana ikiwemo na baadhi ya siku kuwajumuisha katika mazoezi ya timu kubwa.Aidha kuhusiana na wachezaji waliomaliza mikataba yao,

  0 0


  0 0
 • 06/02/17--14:44: IFTAR YA PAMOJA NEW YORK


 • 0 0


   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na waandishi wa habari baada ya Kuzindua Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi, Harrison Mseke. 
   Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Kigoma (CCM), Mhandisi  Atashasta Nditiye (kushoto), akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Daniel Nsanzugwako pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi, Harrison Mseke, wakifuatilia Mada inayohusu Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi iliyokuwa inatolewa na Mratibu wa Mpango huo kutoka Idara ya Huduma za Wakimbizi, Dk. John Jingu (hayupo pichani), muda mfupi kabla ya Uzinduzi wa Mpango huo.
   Sehemu ya Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi zake nchini  pamoja na Wawakilishi wa Taasisi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga, akijibu maswali ya waandishi wa habari  wakati wa uzinduzi wa  Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamadi Masauni (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Katavi, Tabora, Kagera na Kigoma, watendaji wa serikali na Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa yanayofanya kazi nchini, wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 

  0 0


  Marehemu Mzee Francis Maige Kanyasu Ngosha enzi za uhai wake

  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amekutana na Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo aliyefika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu mpya wa  Brigedi ya Nyuki Zanzibar. 
  Dk. Shein alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia, ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kwa kumteua Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo kushika wadhifa na kumpongeza Brigedia huyo huku akimuhakikishi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wake itampa mashirikiano makubwa kama ilivyofanya kwa viongozi waliokuwepo kabla yake. 
  Nae, Brigedia Jenerali Nondo alimuahidi Dk. Shein kuwa ataendeleza uhusiano na ushirikiano mwema ulipo kati ya Majeshi ya Ulinzi Tanznia  pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar huku akisifu mashirikiano mazuri anayoyapata kutoka kwa viongozi wa Serikali na viongozi wa vikosi vya ulinzi vya SMZ na kuahidi kutoa ushirikiano kwao pamoja na kwa wananchi wote wa Zanzibar. 
  Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo anashika nafasi ya Marehemu Bregedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki, aliyekuwa Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar, ambaye alifariki dunia tarehe 13, Disemba mwaka 2016 huko katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Lugalo jijini Dar-es-Salaam na kuzikwa Mkoani kwao Ruvuma. 
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo alipofika kujitambulisha leo Ikulu Mjini Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na  Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo baada ya mazungumzo alipofika kujitambulisha leo Ikulu Mjini Zanzibar
   (Picha na Ikulu)

  0 0
  0 0


  0 0


  0 0


  Tanga, SERIKALI imeshauriwa kuweka kanuni ya majengo ya gorofa na taasisi za huduma za kijamiii kujenga miundombinu maalumu kwa walemavu lengo ikiwa ni kuzifikia huduma kama ilivyo kwa wengine.  Wakizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali vilivyokabidhiwa kwa uongozi wa Kituo cha Watoto Walemavu (YDPC), na kuishauri kutoruhusu ujenzi wa majengo ya huduma za kijamii bila kuwepo kwa miundombinu ya walemavu.


  Imesemwa kuwa majengo mengi ya huduma za kijamii hayana miundombinu kwa walemavu hivyo kunyimwa fursa ya kupata huduma kama ilivyo kwa wengine. Imesemwa katika kongamano hilo, kuwa kutokuwepo kwa sheria watu wengi hujenga majengo bila kuweka miundombinu ya walemavu.


  Imesemwa kuna baadhi ya walemavu wa viungo wenye elimu hupoteza nafasi ya kazi kutokana na majengo wanayopangiwa kazi kutokuwa na njia maalumu kwa walemavu wa viungo na kuwa kero kwao.
  Mtaalamu wa tiba sanifu kwa njia ya Mazoezi kwa njia ya Mazoezi na Vitendo, Amina Mbowe, akitoa maelekezo ya kazi wanazozifanya katika kitengo chake ikiwa na pamoja na kuwaonyesha vifaa vya mazoezi kwa watoto wenye ulemavu.
  Mwanafunzi mlemavu kituo cha Watoto wenye Ulemavu wa viungo na ngozi, Imamu Amir, akipanda mbegu ya muhongo katika shamba la kituo hicho kijiji cha Mleni Amboni Tanga, ujumbe huo pia ulitembelea katika shamba hilo ambalo watoto walemavu wamekuwa wakiendesha kilimo cha chakula na mbogamboga.
  Mtaalamu wa kilimo kwa watoto walemavu kituo cha Walemavu, Sabra Swai akitoa maelekezo kwa ujumbe wa umoja wa wanawake wa Makanisa ya Free Pentacostal Church of Tanzania wakati walipotembelea shamba la Mleni ambalo watoto walemavu wa viungo, ngozi, viziwi na wengineo huendesha kilimo shamba lililoko kilometa 20 kutoka Tanga mjini.
  Mkurugenzi wa kituo cha Watoto Walemavu (YDPC) William Hendry wa pili kulia akiongoza maombi na kutoa shukurani kwa Ujumbe wa Umoja wa Wanawake Makanisa Free Pentacoastal Church of Tanzania wakati alipopokea zawadi mbalimbali kwa kituo hicho.

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Zephania Chaula, amefanikiwa kutatua mgogoro wa ardhi uliokuwa unafukuta kwenye Kata ya Terrat, kwa kupiga marufuku matumizi mengine ya sehemu ya kulishia mifugo na wanyamapori.

  Akizungumza kwenye mkutano wa wananchi wa eneo hilo, Chaula ameuagiza uongozi wa Kijiji cha Terrat kupima eneo lote lililotengwa kwa ajili ya mifugo na wanyamapori na mipaka yake ibainishwe.

  Pia, ametoa miezi miwili kwa wakulima waliovamia na kulima sehemu ya eneo hilo kuondoka kwa hiyari yao wenyewe ifikapo Julai 31 mwaka huu na endapo watakaidi agizo hilo wataondolewa kwa nguvu.

  Alisema eneo la kingo ya mifugo libainishwe ukubwa wake na pia mipaka yake ipimwe baina ya vijiji vya Terrat na Loiborsiret ili kuondokana na sintofahamu ya mwishilio wa eneo hilo.

  Alisema serikali ya kijiji ibainishe maeneo ya wazi yaliyowekwa kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi na kuonyesha maeneo ya kilimo na mifugo na kutolewa mapendekezo kupitia mikutano ya kijiji.

  “Pamoja na hayo nahitaji hadi Juni 15 mwaka huu, niletewe taarifa juu ya uvamizi wa watu watano ambao wanalima kwenye sehemu hiyo ambayo wananchi wa Terrat wanailalamikia,” alisema Chaula.

  Alisema serikali ya kijiji hicho pia, iangalie namna ya kukutana na watu 527 wa Terrat ambao wana mgogoro wa ardhi wakidaiwa kuinga kwenye sehemu ya malisho na kutumia eneo hilo kwa kilimo.

  Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Yefred Myenzi alisema ardhi ni mali ya wananchi wote na endapo kutatokea mgogoro wa ardhi sheria ya ardhi inaagiza namna ya kuutatua.

  Myenzi alisema kupitia sheria hiyo wamefanya jitihada ya kupata suhulu juu ya mgogoro wa kijiji cha Terrat na Loiborsiret na atatoa taarifa kwa mkuu wa wilaya hiyo ifikapo Juni 15 mwaka huu.

  “Kunapotokea mgogoro wa ardhi tunafanya jitihada na kuhakikisha unamalizika hivyo wale watu 25 wanahitajiwa wahudumiwe na upande wa Terrat na wale wengine wakahudumiwe kule,” alisema.

  Diwani wa Kata ya Terrat Jackson Materi alipongeza jitihada za mkuu wa wilaya hiyo kuhakikisha anamaliza mgogoro huo ambao ulitaka kusababisha mpasuko na mshikamano wa wananchi wa eneo hilo.

  “Pamoja na hayo bado tutaendelea kuwa pamoja na wananchi wangu na nilishawaeleza tangu hapo awali kuwa mimi sina ardhi hivo matumizi ya ardhi yenu mtajipangia ninyi wenyewe,” alisema Materi.

  Wakazi wa Kijiji cha Terrat Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mhandisi Zephania Chaula, aliyeutatua mgogoro wa ardhi wa wakulima na wafugaji wa eneo hilo.

older | 1 | .... | 1724 | 1725 | (Page 1726) | 1727 | 1728 | .... | 3272 | newer