Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

bwawa la maini oye!


Kitabu Kimependekezwa na Africa International University

$
0
0

Na Profesa Joseph Mbele
Nimeona leo kuwa kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, kimependekezwa na Africa International University (AIU) kwa ajili ya wanafunzi wa kigeni. Chuo hiki kiko Karen, nchini Kenya.
Nimevutiwa na maelezo yaliyotolewa kama Information for International Students juu ya hali halisi anayokumbana nayo mtu anapojikuta katika utamaduni wa kigeni:
Moving to a different cultural environment is a very stressful experience – that’s why it is sometimes referred to as “culture shock”. You will likely go through a difficult period of adjustment and homesickness after the initial excitement wears off. This is normal. As you learn your way around the campus and its unique culture, you will be more comfortable at AIU. Soon you will be helping other new international students adjust to AIU and Kenya. If you are willing to learn, you will learn a great deal about yourself and others who are different from you. You will leave here enriched and transformed.

Still, it is wise to take time before coming to prepare yourself and your family for the cultural adjustments that will be necessary. By reading as much as you can about cultural adjustment and talking to other international students, you can learn what to expect. Then you will better understand the feelings and frustrations you deal with as you adjust to your new environment. Since academics will demand a great deal of you at AIU, any preparation you can do before coming will help all of your adjustments once you arrive on campus....Due to cultural differences, you may feel somewhat confused when talking with fellow students. “What do they mean?” Communication in Africa is inferential rather than direct, so you will need to become adept at listening for what is being communicated between the lines.... Students at AIU are coming from all over Africa and the world. They will appreciate the time you invest in learning about the uniqueness of their own cultures—e.g. what communicates respect.

Maelezo na mawaidha haya yanahusiana na yaliyomo katika kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. Ni masuala yasiyokwepeka, hasa katika dunia ya utandawazi wa leo. Yanawahusu sio tu wanafunzi, bali pia wafanya biashara, wanadiplomasia, na kadhalika, kama ninavyoelezea mara kwa mara katika blogu hii.

Wanawake Watakiwa Kujiamini Ili Wafanikiwe Katika Uongozi

$
0
0
Spika Mstaafu Anne Makinda akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Mradi wa “Wanawake Viongozi -Nguvu ya Mabadiliko” leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo wa miaka mitatu unalengo la kuwajengea uwezo wanawake 200 katika medani za uongozi wa kisiasa ili kufikia idadi ya asilimia 40 ya wanawake katika uongozi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020. unashirikisha asasi tatu ambazo ni Women Fund Tanzania, Kituo cha Utawala Bora na Maendeleo ya Uchumi (CGG & ED) na Taasisi ya Hanns Seidel Foundation (HSF) chini ya udhamini wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU).
Mkurugenzi wa Taasisi ya Hanns Seidel Foundation (HSF), Dkt. Susanne Luther akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Mradi wa “Wanawake Viongozi - Nguvu ya Mabadiliko” leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo wa miaka mitatu unalengo la kuwajengea uwezo wanawake 200 katika medani za uongozi wa kisiasa ili kufikia idadi ya asilimia 40 ya wanawake katika uongozi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020. Kulia ni Mkuu wa Sehemu ya Uchumi na Utawala kutoka Umoja wa Ulaya (EU), Oliveier COUPLEUX na Mwakilishi Mkazi wa HSF Tanzania na Uganda, Bi. Julia Berger.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Spika Mstaa Anne Makinda (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa “Wanawake Viongozi - Nguvu ya Mabadiliko” leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo wa miaka mitatu unalengo la kuwajengea uwezo wanawake 200 katika medani za uongozi wa kisiasa ili kufikia idadi ya asilimia 40 ya wanawake katika uongozi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020. unashirikisha asasi tatu ambazo ni Women Fund Tanzania, Kituo cha Utawala Bora na Maendeleo ya Uchumi (CGG & ED) na Taasisi ya Hanns Seidel Foundation (HSF) chini ya udhamini wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU).

NEWS ALERT: Mwili wa Mzee Francis Maige Kanyasu ‘Ngosha’ Wasafirishwa Mwanza leo

$
0
0
Mwili wa marehemu Mzee Francis Maige Kanyasu umeagwa leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kusafirishwa na serikali kwenda kijijini kwao Igokero wilayani Misungwi. 
 Shughuli ya kuuaga mwili huo imeongozwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamaii , Jinsia , Wazee na Watoto, Marcel Katemba ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk. Mpoki Ulusubisya. 
 Akizungumza katika shughuli hiyo Bwana Katemba ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa jitihada kubwa walizofanya za kumpatia tiba na kumuhudumia kwa kipindi alichokuwa amelazwa hospitalini hapo. 
 “Nawapongeza Muhimbili kwa juhudi zenu ni kweli mlitaka kuokoa maisha ya mzee wetu, lakini kazi ya Mungu haina makosa, Pia sina budi kuwashukuru majirani zake na uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Malapa kwa kujitoa - naomba mfanye hivyo hata kwa wazee wengine’’ amesema Katemba. Naye Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dk. Juma Mfinanga amesema walimpokea Mzee Kanyasu Mei 25, 2017 akitokea Hospitali ya Amana alikokua akipatiwa matibabu na walipomfanyia vipimo vya awali waligundua kwamba ana maradhi ya Kifua Kikuu ambayo alikuwa nayo kwa muda mrefu kutokana na mazingira aliyokua akiishi. 
 Hivyo Dk. Juma ametoa rai kwa wananchi kujenga tabia ya kwenda hospitalini mapema pindi mtu anapoona hali yake ya kiafya si nzuri kwani ukiwahi hospitali ni rahisi kupata tiba na kupona kuliko kusubiri hadi ugonjwa uwe sugu. 
 Mzee Francis Maige Kanyasu alizaliwa 1931 na kufariki dunia Mei 29 , 2017 saa mbili na nusu usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
 Waombolezaji wakiongozwa na  Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Godfrey Mungereza (kushoto) na Bw. Eric Shigongo wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu  tayari kwa safari ya kuelekea Misungwi mkoani Mwanza ambako mazishi yatafanyika.

Baadhi ya wafanyakazi wa Muhimbili wakisubiri kuuaga mwili huo leo. Kulia ni Zuhura Mawona ambaye amemwakilisha Mkurugenzi wa Uuguzi, Agness Mtawa na Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk Julieth Magandi. Pembeni yao kushoto ni Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Godfrey Mungereza
 Baadhi ya wanahabari na wawakilishi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiaga mwili wa marehemu Francis Maige Kanyasu (86) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo. Marehemu alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo na wakati akiendelea na matibabu mauti yakamkuta.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Marcel Katemba ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Mpoki Ulusubisya akizungumza kabla ya shughuli za kuaga mwili huo leo.
 Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali wa Muhimbili, Dk Juma Mfinanga akieleza kwa wanahabari jinsi Hospitali ya Muhimbili ilivyokuwa ikimpatia matibabu mzee Francis Maige Kanyasu.
 Mkurugenzi wa Huduma na Upasuaji wa Muhimbili, Dk Julieth Magandi akiwashukuru watu mbalimbali walofika kuuaga mwili huo leo.
 Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali wa Muhimbili, Dk Juma Mfinanga akieleza jinsi Hospitali ya Muhimbili ilivyokuwa ikimpatia matibabu mzee Francis Maige Kanyasu.
PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI 

Mwili wa Mzee Francis Maige Kanyasu ‘Ngosha’ Wasafirishwa Mwanza leo

$
0
0
Mwili wa marehemu Mzee Francis Maige Kanyasu  umeagwa leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)  na kusafirishwa na serikali kwenda kijijini kwao Igokero wilayani Misungwi.

Shughuli ya kuuaga mwili huo imeongozwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamaii , Jinsia , Wazee na Watoto, Marcel  Katemba ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk. Mpoki Ulusubisya.

Akizungumza katika shughuli hiyo Bwana Katemba ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa jitihada kubwa walizofanya za kumpatia tiba na kumuhudumia kwa kipindi alichokuwa amelazwa  hospitalini hapo.

“Nawapongeza Muhimbili kwa juhudi zenu ni kweli mlitaka kuokoa maisha ya mzee wetu, lakini kazi ya Mungu haina makosa , pia sina budi kuwashukuru majirani zake na uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Malapa kwa kujitoa naomba mfanye hivyo hata kwa wazee wengine’’ amesema Katemba.

Naye Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dk. Juma Mfinanga amesema walimpokea Mzee Kanyasu Mei 25, 2017 akitokea Hospitali ya Amana alikokua akipatiwa matibabu na walipomfanyia vipimo vya awali waligundua kwamba ana maradhI ya Kifua Kikuu ambayo alikuwa nayo kwa muda mrefu kutokana na mazingira aliyokua akiishi.

Hivyo Dk. Juma ametoa rai kwa wananchi kujenga tabia ya kwenda hospitalini mapema pindi mtu anapoona hali yake ya kiafya si nzuri kwani ukiwahi hospitali ni rahisi kupata  tiba na kupona kuliko kusubiri hadi ugonjwa uwe sugu.

Mzee Francis Maige Kanyasu alizaliwa 1931 na kufariki dunia Mei 29 , 2017 saa mbili na nusu usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Baadhi ya wawakilishi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiaga mwili wa marehemu Francis Maige Kanyasu (86) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo. Marehemu alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo na wakati akiendelea na matibabu mauti yakamkuta.
Mwili wa marehemu ukiwa umebebwa tayari kwa safari ya kuelekea Misungwi mkoani Mwanza ambako mazishi yatafanyika. 0003: Baadhi ya wafanyakazi wa Muhimbili wakisubiri kuuaga mwili huo leo. Kulia ni Zuhura Mawona ambaye amemwakilisha Mkurugenzi wa Uuguzi, Agness Mtawa na Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk Julieth Magandi.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Marcel Katemba ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Mpoki Ulusubisya akizungumza kabla ya shughuli za kuaga mwili huo leo.

HUWEZI KWENDA MBINGUNI BILA KUFA - KANALI NGELEMA LUBINGA

$
0
0
Wazazi wametakiwa kuwa mstari wa mbele kwa kutoa elimu kwa vijana wao, ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa katika maadili mabaya, yanayopelekea wengi wao kujiingiza katika mazingira hatarishi ambayo yanaviashiria vya uvunjifu wa Amani.

A TRIBUTE TO LINDA KAAYA MAGOMBE (RIP)

$
0
0
LINDA:  June 2, 1965 - June 2, 1995
Linda, the ever smiling princess, the shining candle that lit the family, the extended family, friends and admirers alike; blown by the wind too early and too soon.
In heaven you are not alone. In the avenue of everlasting tranquility you are with Uncle George, Aunt Edith, Uncle Ostia, Cousin Georgina, and Cousin George Jr. 
We derive solace in the knowledge that you are together, holding hands, and at peace. 
We remember you all. 
RIP.
Mark Mwandosya, Lucy Akiiki, Godfrey Mwandosya, Max Mwandosya, Digna Mwandosya, Sekela Mwandosya, and Emmanuel Mwandosya

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA SEMINA KWA WASTAAFU WATARAJIWA WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza waajira wasiopeleka au kuchelewesha michango ya wanachama kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii nchini wachukuliwe hatua za kisheria ili kukomesha tabia hiyo.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo 3-June-2017 Jijini Mwanza wakati anafungua semina ya maisha baada ya kustaafu,fursa ya mafao,uwekezaji iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kwa ajili ya wastaafu watarajiwa 450 kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa waajiri wakichangia kwa mujibu wa sheria kwenye mifuko hiyo watawezesha wanachama wao kupata mafao kikamilifu na kwa wakati.

Kuhusu madeni ya Serikali kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini, Makamu wa Rais amewahakikishia Wakurugenzi wa mifuko hiyo kuwa Serikali inashughulikia madeni hayo na baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa madeni hayo basi malipo yatafanyika haraka iwezekanavyo.


Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, (kulia), akipokea mfuko wenye vipeperushi na machapisho mbalimbali yenye maelezo ya kina ya huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu, Bw. Adam Mayingu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Semina kwa wastaafu watarajiwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza
Baadhi ya washiriki wa Semina ya Wastaafu Watarajiwa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha Vitabu vya PSPF kwenye kutoa elimu kwa Wanachama wa mfuko huo.
Baadhi ya washiriki wa Semina ya Wastaafu Watarajiwa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Mwanza.
Baadhi ya Wadau wakifuatilia ufunguzi wa Semina kwa Wastaafu Watarajiwa.


Rais Dkt. Magufuli amteua bi. Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Pia afanya uteuzi wa Mabalozi wawili

Tunaungana na Ulimwengu Kuokoa Bahari- Tizeba

$
0
0

Na Boss Brown

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Chares Tizeba ataongoza ujumbe kutoka Tanzania kushiriki katika Kongamano la Bahari Duniani linalotarajiwa kuanza Jumatatu tarehe 5 hadi 9 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York nchini Marekani.

“Changamoto inayoikabili bahari ni kubwa kutokana na uchafuzi utokanao na taka sugu ambazo zinahatarisha uhai wa Bahari yetu, tunaunagana katika kushilikiana na wadau mbalimbali katika juhudi za kuiokoa bahari kwa pamoja.” Alisisitiza Tizeba.

Akifafanua amesema kama nchi wanachama tanaadhimia kutekeleza kipengele cha 14 cha Malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ya agenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa Kinacholenga matumizi bora ya rasilimali za baharini.

Kongamano hili ni la muhimu katika kuokoa bahari na litakutanisha Serikali, Umoja wa Mataifa, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Mashirika yanayoshughulikia mazingira, Taasisi za elimu na wanasayansi ya Jamii, Asasi za Kirai, watu binafsi, makampuni na viwanda.
Sehemu ya fukwe wa Bahari ya Hindi maeneo ya Jiji la Dar es Salaam ikiwa imeathiriwa na uchafu .


WAZIRI MKUU AAGIZA KILOSA WAILIPE GAIRO DENI LA0

$
0
0
* Ni la sh. milioni 213/- la fedha za maendeleo.
*Ataka apewe taarifa ifikapo Juni 30. 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Clifford Tandari aitishe kikao na uongozi wa Halmashauri ya Kilosa na kupata kauli yao ni lini watalipa zaidi ya sh. milioni 210 wanazodaiwa na Halmashauri ya Gairo.

“Katibu Tawala itisha kikao cha Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri, waseme ni lini watazileta fedha hizo ambazo zilitumwa kwao wakati Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ikiwa haijafungua akaunti zake,” amesema.

Ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Juni 3, 2017) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Morogoro, wilaya ya Gairo na watumishi wa Halmashauri ya Gairo mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa na wilaya katika kikao kilichofanyika Gairo mjini

“Kilosa ni lazima wazilipe hizo fedha. Katibu Tawala simamia zoezi hilo na kama watachelewa, uzikate moja kwa moja kwenye fedha yao wanayoletwa kutoka Ofisi ya Rais (TAMISEMI). Nataka nipewe taarifa ya maamuzi hayo kabla Juni haijaisha,” amesema.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi na watumishi wa Wilaya ya Gairo (hawapo pichani) katika mkutano aliouitisha mjini Gairo Juni 3, 2017.
Viongozi na watumishi wa Wilaya ya Gairo wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) katika mkutano aliouitisha mjini Gairo Juni 3, 2017. (Picha na OWM).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Cliford Tandari mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero. (Picha na OWM).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipanda mti nje ya Ofisi ys Mkuu wa Wilaya ya Gairo mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Upandaji Miti Kitaifa. Wengine ni viongozi wa Mkoa na Wilaya wakishuhudia. (Picha na OWM).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimwagilia mche alioupanda nje ya Ofisi ys Mkuu wa Wilaya ya Gairo mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Upandaji Miti Kitaifa. Wengine ni viongozi wa Mkoa na Wilaya wakishuhudia. (Picha na OWM).

MAKAMU WA RAIS AWASILI BUTIAMA,KESHO KUWA MGENI RASMI KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Mara alasiri ya leo 3-June-2017 akitokea mkoani Mwanza ambapo hapo kesho atakuwa ni mgeni rasmi katika kilele cha Siku ya Mazingira Duniani.

Alipowasili kijijini Butiama, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Viongozi wa vyama vya siasa na watendaji mbalimbali wa Serikali ambao wameongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba.

Makamu wa Rais pia amepokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Mara na amepata fursa ya kuwasha mshumaa na kuweka shada la maua katika kaburi la baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere lililopo Mwitongo kijijini Butiama.

Hapo kesho tarehe 4-June-2017 Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ataongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Mara na mikoa ya Jirani katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambapo kitaifa sherehe hizo zitafanyika katika kijiji cha Butiama mkoani Mara. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua juu ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada ya kuwasili Butiama ambapo atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za siku ya mazingira Duniani ambazo Kitaifa zinafanyika Butiama mkoani Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima mbele ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada kuweka shada la maua,Makamu wa Rais yupo Butiama kuhudhuria sherehe za siku ya mazingira Duniani ambazo Kitaifa zinafanyika Butiama mkoani Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye kikao cha kupokea taarifa ya mkoa wa Mara mara baada ya kuwasili Butiama kwenye makazi ya Hayati Baba wa Taifa.


Waziri Mavunde azindua mpango wa mafunzo ya ufundi wa kisasa wa kutengeneza viatu na bidhaa za ngozi jijini Mwanza

$
0
0
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu anaeshughulikia kazi, jira na maendeleo ya Vijana Mh Anthony Mavunde akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa mafunzo ya ufundi wa kisasa wa kutengeneza viatu kwa njia za kisasa uliofanyika kwenye chuo cha DIT Karakana ya Viatu jijini Mwanza leo.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika uzinduzi huyo uliofanyika kwenye cho cha DIT Karakana ya Viatu jijini Mwanza.
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu anaeshughulikia kazi, jira na maendeleo ya Vijana Mh Anthony Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na waalikwa waliohudhuria katika uzinduzi huo wa mpango wa mafunzo ya ufundi wa kisasa wa kutengeneza viatu kwa njia za kisasa.

……………………………………………………
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu anaeshughulikia kazi, jira na maendeleo ya Vijana Mh Anthony Mavunde amefungua mpango wa mafunzo ya ufundi wa kisasa wa kutengeneza viatu kwa njia za kisasa kwa vijana 1000 wanaotaka mikoa zaidi ya kumi nchini.

Akizundua mpango huo, Mhe Mavunde, amesema mpango huo unalenga kuwajengea uwezo wa kujiajiri vijana na pia kutumia bidhaa zitokanazo na mazao ya mifugo kwa ajili ya kuzalisha viatu na bidhaa za ngozi nchini.

Amesema, serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha inatekeleza azma ya ujenzi wa viwanda kwa kuwajengea uwezo vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa katika kujiandaa na mfumo wa mapinduzi ya viwanda ambavyo vimeshaanza kujengwa nchini.

Aidha amewataka vijana kutochagua kazi au kubweteka kuwa kazi rasmi ni zile za ajira ya moja kwa moja serikali au sekta binafsi, amewataka vijana kubadilisha mtazamo wa maaana ya Ajira kwa kutokukaa na kusubiri nafasi za ajira.

Amesema mpango huu wa miaka mitano unalenga kuwafikia vijana zaidi ya milioni 4 nchini katika kuwajengea uwezo ambao utawafanya kujiajiri au kuajiriwa katika Tanzania ya viwanda.


Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano.
Wizara ya kazi,ajira, ulemavu na maendeleo ya vijana
03/06/2017

KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA KUFANYIKA KESHO MKOANI MARA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akitoa maelezo ya awali ya ufunguzi katika mijadala ya kuadhimisha siku Mazingira Duniani Wilayani Butiama Mkoni Mara. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mahusiano Endelevu Kati ya Binadamu na Mazingira.”
Wanajopo wa mada ya kwanza ya “Tanzania Bila Mkaa na Kuni Inawezekana?” kutoka kushoto ni Ndugu Charles Meshack Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo Mkurugenzi Mkuu, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Eng. Estomih Sawe Mkurugenzi Mtendaji TaTEDO (Center for Sustainable Modern Energy Initiative in Tanzania). Mjadala unaendelea Butiama katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.
Mjadala ukiendelelea pichani, Wanajopo wa mada ya kwanza ya “Tanzania Bila Mkaa na Kuni Inawezekana?” kutoka kushoto ni Ndugu Charles Meshack Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo Mkurugenzi Mkuu, wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Bi. Maria Sarungi (Mwendesha Mada) na Eng. Estomih Sawe Mkurugenzi Mtendaji TaTEDO (Center for Sustainable Modern Energy Initiative in Tanzania). Kongamano linaendelea Butiama katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. January Makamba akifuatilia mjadala katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki Butiama- Mara. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora. Mijadala mbalimbali inaendelea katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mahusiano Endelevu Kati ya Binadamu na Mazingira.”

WELCOME TO DANUBE HOME!


Toyota Corolla X (Popular as Corolla Police ) for sale

$
0
0
 Make : Toyota Corolla X (Popular as Corolla Police )
Mileage : 200,000Km
Condition : Good condition,Original Seats ,Ac,Tyres.
Insurance : Comprehensive to June 2018.
Price : 6M (Negotiations allowed)
Location : Around UDSM /Mlimani City.
Contacts : 076 61 12445 / 078 56 70829

BAMIZA MUSIC CHART TOP 20, JUNE 3RD 2017

Sheikh Shariff Majini atikisa jiji la Arusha

$
0
0
Sheikh Shariff Majini ambaye yupo ziarani Jijini Arusha leo Jumamosi tarehe 03 Juni 2017 amefanya mkutano mkubwa katika Stand ya Hiace jirani na soko la Kilombero Jijini Arusha. 
 Mkutano wa Sheikh Shariff utaendelea kesho  Jumapili tarehe 04 kuanzia saa mbili asubuhi hapo hapo katika viwanja vya Stendi ya Hiace Soko la Kilombero. Baada ya Arusha Sheikh Shariff atafanya ziara Mkoani Tanga siku ya Jumamosi tarehe 10 na Jumapili tarehe 11 mwazi huu wa Juni.
 Sehemu ya umati wa wakaazi wa Arusha waliojitokeza kwenye mkutano wa Sheikh Shariff Majini katika Stand ya Hiace jirani na soko la Kilombero Jijini Arusha.
 Sheikh Shariff Majini akimuombea Mzee mwenye maradhi ya miguu..
 Sheikh Shariff Majini akimuombea mtoto mwenye matatizo
 Sehemu ya umati wa wakaazi wa Arusha waliojitokeza kwenye mkutano wa Sheikh Shariff Majini katika Stand ya Hiace jirani na soko la Kilombero Jijini Arusha.

KIKAO CHA BULEMBO NA WAJUMBE WILAYANI KIBONDO CHANOGA

$
0
0
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akiingia ukumbini kuzungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kibondo, Mabalozi, watendaji wa CCM na wa Serikali, leo Wilayani Kibondo akiwa katika mwendelezo wa ziara zake za Kichama mikoani
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akiwa amewasili ukumbini tayari kwa kikao hicho. Kushoto ni Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Kigoma Nicholaus Zakaria, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou na kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Kigoma, Mbunge wa Viti Maalum Josephine Ngezabuke, Mbunge wa Mbambwe Atashasta Nditiye na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibondo Josephat Ntabindi.
 Wajumbe wakishangilia bada ya Bulembo kuingia ukumbini 
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kibondo Josephat Ntabindi akifanya utambulisho kabla ya kufungua kikao hicho
 Wajumbe wakishangilia ukumbini.

MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA BUKOBA KWENYE MKAKATI WA KUHAMIA RUBALE.

$
0
0
Na Abdullatif Yunus, Kasibante Fm.
Halmashauri  ya Wilaya Bukoba, Ipo katika Mkakati na Hatua za Awali  za kuyapeleka Makao Makuu ya Wilaya Bukoba, katika tarafa ya Rubale, Kata Rubale.
Hayo  yamebainika katika Mkutano wa Hadhala wa Wananchi pamoja na wadau wa Elimu, uliofanyika katika Kata ya Rubale Juni 3, 2017.
Akihutubia katika mkutano huo, Mwenyekiti  wa Halmashauri  ya Wilaya ya Bukoba, Mh. Murshidi Hashim Ngeze amesema,  tayari  Halmashauri imekwishatuma timu ya Wataalamu kukagua maeneo wapi  panafaa kuwekwa Makao Makuu hayo ya Wilaya, Rubale ikiwa ni eneo mojawapo linalopewa kipaumbele, hivyo wananchi wawe tayari kuyapokea  maamuzi hayo pale yatakapopitishwa.
Akifafanua zaidi kuhusu suala hilo, Mwenyekiti Ngeze  amesema kuwa  tayari  mazungumzo ya awali yameanza kufanyika ikiwa ni pamoja na kuanza  mipango  ya kuanza kuifanya  Rubale kuwa Mji mdogo, huku akitoa Rai kwa Wananchi  kukubali usumbufu na uharibifu utakaojitokeza  kuhusiana na mali zao, kwani Maendeleo pia huambatana na hasara.
Awali mwenyekiti  Ngeze ambae pia ni Diwani wa Kata ya Rukoma, amewapongeza wananchi kwa kujitolea kuchangia vifaa vya ujenzi wa Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari ya Rubale, na kuahidi kuendelea kutafuta wahisani mbalimbali ili kuchangia Ujenzi wa Shule hiyo, na kusisitiza kuwa Shule hiyo  ambayo inapendekezwa kuwa ya Wasichana  pekee ni lazima itajengwa Rubale.
Kwa upande wake Diwani wa viti maalumu Tarafa Rubale kupitia CCM,  Bi Asuma Kokugonza Bantanuka  amewaomba akina mama kujitokeza kwa wingi kuunga mkono Ujenzi huo, na kuwataka wnawake ikibidi kujitoa na kujitolea kufanikisha zoezi hilo, lengo likiwa ni kumsomesha mtoto wa kike kwa maendeleo ya Baadae.
Bi Asuma aliefuatana na Mwenyekiti Ngeze Katika ziara hiyo ameongeza kuwa, mwanamke ana nafasi na jukumu kubwa katika jamii hasa katika suala la maendeleo hivyo, hana budi kubaki nyuma ili kujikwamua kiuchumi.
 Diwani viti maalum Tarafa Ruabale - CCM Bi Asuma Kokugonza Bantanuka akizungumza na wananchi waliohudhuria katika mkutano huo..
 Mwenyekiti  wa Halmashauri  ya Wilaya ya Bukoba, Mhe. Murshidi Hashim Ngeze akizungumza na hadhara iliyohudhuria mkutano wake eneo la Katani, Rubale.
Wananchi waliohudhuria mkutano huo wakiendelea kufuatilia hotuba. 
Picha zote na Allawi Kaboyo
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images