Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1723 | 1724 | (Page 1725) | 1726 | 1727 | .... | 3284 | newer

  0 0  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd , Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
  Picha ya pamoja 

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda jana Alhamisi June 1, 2017 amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo katika dhifa ya Makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1 tayari kwa kuelekea Mafia Mkoani Pwani.

  Mwenge wa Uhuru ni chombo kilichoasisiwa na baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni Tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika.

  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo  Mhe Paul C. makonda  amesema kuwa jumla ya Miradi 40 imepitiwa na Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2017 katika Mkoa wa Dar es salaam yenye thamani ya Shilingi 244,392,530,334 huku akibainisha kuwa Miradi 12 imezinduliwa, Miradi 15 imewekewa mawe ya Msingi, Miradi miwili imefunguliwa na Miradi 11 imetembelewa.

  Rc Makonda alisema kuwa Mbio za Mwenge wa Uhuru tangu mwanzo zimekuwa kichocheo kikubwa katika kuhamasisha Maendeleo , uzalendo, Umoja , Mshikamano na kudumisha Amani ndani na nje ya nchi.

  Alisema kuwa Mwenge wa Uhuru Mwaka 2017 wenye kauli mbiu isemayo Shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu pia umebeba jumbe mbalimbali ikiwemo kupiga Vita Maambukizi mapya ya UKIMWI na Malaria sambamba na kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya.

  Katika mapambano dhidi ya Dawa za kulevya jitihada ya kudhibiti ni ajenda muhimu kwa mustakabali wa maisha ya mtanzania kwa kuwa linagusa nguvu kazi ya Taifa.
  Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda kwenye dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. jana Alhamisi June 1, 2017

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akitoa taarifa ya Miradi iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wake mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kwenye dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. jana Alhamisi June 1, 2017
  Baadhi ya Wananchi waliozuru katika dhifa ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. jana Alhamisi June 1, 2017
  Viongozi mbalimbali wa serikali na wadau akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakifatilia dhifa ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Terminal 1. jana Alhamisi June 1, 2017.


  0 0

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza

  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufungua rasmi semina kwa wastaafu watarajiwa iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na kufanyika kwenye ukumbi wa chuo cha mafunzo kwa watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), jijini Mwanza.

  Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, kwenye ufunguzi wa semina hiyo iliyoanza leo Juni 2, 2017, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Bw. Gabriel Silayo alisema, semina hiyo inalenga kuwandaa kwa kuwapa mafunzo watumishi wa umma ambao wanatarajiwa kustaafu hivi karibuni, ili hatimaye wastaafu kwa amani.

  “Na kwa kufanikisha hilo, tunao maafisa wetu watatoa mada mbalimbali, wapo washirika wetu, SIDO, na mabenki kama vile NMB, CRDB, TPB, MCB na UTT, ambao watatoa elimu ya namna bora ya kutunza na kutumia fedha zako za mafao.” Alibainisha Bw. Silayo.

  Bw. Silayo pia alisema, kwa kutambua kipaumbele cha serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake, Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kauli mbiu ya semina hiyo ni “Mafao ni Mtaji wa Uwekezaji Sahihi”. “Na ndio maana tumewaleta SIDO hapa ili wawaelimishe jinsi mtakavyoweza kuanzisha viwanda vidogo vidogo baada ya kustaafu utumishi wa umma na ndugu zangu napenda niwahakikishie hilo linawezekana.” Alisema

  Alisema semina hiyo itakuwa ya siku mbili na kwamba, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ataifungua rasmi kesho Jumamosi Juni 2, 2017.

  Zaidi ya watumishi 300 kutoka sekta mbalimbali za utumishi wa umma kwenye wilaya zote za mkoa wa Mwanza wanahudhuria semina hiyo ya mafunzo.
  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ya mafunzo kwa wastaafu watarajiwa 
  Afisa Mwandamizi wa Utafiti wa PSPF, Bw. Mapesi Maagi, akigawa vitendea kazi kwa washiriki wa semina mwanzoni mwa mafunzo hayo
  Baadhi ya wadau wa PSPF, na washiriki wa semina wakifuatilia mada zilziokuwa zikitolewa
  Washiriki wa semina wakiwa kwenye ukumbi wa chuo cha mafunzo BoT jijini Mwanza
  Bw. Silayo, (Kushoto), akimsikiliza kwa makini Meneja wa Fedha wa Mfuko huo, Bw.Lihami Masoli.


  0 0

  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai leo ameendelea kuwaadhibu wabunge ambao wamekwenda kinyume na taratibu na ukosefu wa nidhamu baada ya kumuamuru Mbunge wa Kibamba , Mhe. John Mnyika wa CHADEMA kutoka nje ya bunge kwa utovu wa nidhamu.
  Spika Ndugai aliamuru walinzi wa Bunge kumtoa nje mbunge huyo na kusema hataruhusiwa kushiriki katika vikao vya bunge kwa siku 7, jambo ambalo limepelekea wabunge wengine wa upinzani kutoka nje ya ukumbi wa Bunge kupinga kitendo hicho.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Mkoani Singida Mwingulu L. Nchemba, amekabidhi gari la kubebea wagonjwa mpya na la kisasa ambalo limetolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kituo cha afya cha Ndago kilichopo Wilayani Iramba.

  Mwigulu ameagiza gari hilo lisitumike kama taksi au gari la kubebea mkaa, bali litumike kwa kazi iliyokusudiwa ambayo ni kubebea wagonjwa na akina mama wajawazito tu.

  Mbunge huyo ameyasema hayo juzi wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi ‘ambulance’ hiyo iliyofanyika katika kijiji cha Ndago jimbo la Iramba na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.

  Aidha, amesema ni marufuku wagonjwa kuombwa kuchangia mafuta ya ambulance hiyo au gharama yo yote ile, gari hili wagonjwa walitumie bure.

  “Gari hilo lipatikane kituoni wakati wote. Liwe na mafuta ya kutosha na dereva awepo. Gari hili ambalo ni la kisasa, litunzwe na kulindwa ili liweze kutumika kwa miaka mingi ijayo”, alisema Mwigulu.

  Mbunge huyo ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya rais Magufuli na waziri Ummy kwa msaada huo ambao utaokoa wapiga kura wake na wananchi kwa ujumla.

  Awali mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha Ndago, Dkt Lyoce Mgelwa, alisema kituo hicho kinahudumia tarafa nzima ya Ndago yenye wakazi 89,882.

  Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Mkoani Singida Mwigulu Nchemba akiwasha gari la kubebea wagonjwa (ambulance), katika kijiji cha Urughu tarafa ya Ndago jimbo la Iramba.
  Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba mkoani Singida Mwigulu Nchemba akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa (ambulance) katika kijiji cha Urughu tarafa ya Ndago jimbo la Iramba.
  Mkazi wa kijiji cha Urughu jimbo la Iramba mkoani Singida Jumanne Hatibu akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya gari la kubebea wagonjwa lililotolewa na serikali kupitia wizara ya afya jinsia, wazee na watoto.


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu akipata picha ya pamoja na Makamishna, makamanda wa Wakuu wa Vikosi wa Jeshi la Polisi baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu akipata picha ya pamoja na Makamanda wa Polisi wa mikoa baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu akipata picha ya pamoja na Makamanda wa Vikosi vya  Polisi baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu akipata picha ya pamoja na Makamanda wa Vikosi vya  Polisi baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga baada ya kufungua kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi katika Bwalo la Maafisa wa polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Juni 2, 20. Picha na IKULU

  0 0

   Umma unaarifiwa kuwa Serikali imefanya jitihada za kuwatafuta na hatimaye kuwapata  ndugu wa marehemu Mzee Francis Maige Kanyasu (86) anayetajwa kuwa mmoja wa wachoraji wa nembo ya Taifa. Mzee Kanyasu alifariki dunia usiku wa tarehe 29 Mei, 2017 saa mbili na nusu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Mwili wa marehemu utaagwa rasmi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanzia saa mbili na nusu asubuhi  Jumamosi ya tarehe 3 Juni, 2017 na mara baada ya kuagwa mwili marehemu atasafirishwa na Serikali kwenda kijijini kwao Igokero, Wilaya ya Misungwi kwa ajili ya mazishi.

  Taarifa zaidi kuhusu mazishi ya Mzee Kanyasu zitaendelea kutolewa kwa umma kadiri inapobidi.

   Imetolewa na:

  Bi. Sihaba S. Nkinga
  KATIBU MKUU
  Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
  (MAENDELEO YA JAMII)

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mgeni wake Balozi wa Morocco katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Abdelilah Benryane wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akizungumza na mgeni wake Balozi wa Morocco katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Abdelilah Benryane wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo. (Picha na Ikulu)

  0 0

  Na Veronica Kazimoto,  Morogoro

  Uratibu wa Mfumo wa Taifa wa Takwimu umesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha uzalishaji takwimu rasmi nchini.

  Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Mpango Kabambe wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu nchini, Philemon Mahimbo wakati wa mafunzo kwa Wanasheria wa Wizara na Taasisi za Serikali kuhusu Sheria mpya ya Takwimu No. 9 ya Mwaka 2015 yaliyofanyika leo mkoani Morogoro.

  Mahimbo amesema mfumo huu unaoratibiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu Na 9 ya mwaka 2015, umeweza kusaidia upatikanaji wa takwimu rasmi ambazo zinatumika katika kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo na kupunguza changamoto ya kukinzana kwa takwimu zilizokuwa zinatolewa na taasisi mbalimbali.

  Kwa upande wake Mwanasheria wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Oscar Mangula amesema Sheria mpya ya Takwimu No. 9 ya Mwaka 2015 haimzuii mtu ama taasisi kufanya utafiti bali inamtaka mtu au taasisi kuwasiliana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kupata kibali na miongozo kama anataka takwimu anazozikusanya ziwe rasmi.

  “Sheria hii mpya ya Takwimu No. 9 ya Mwaka 2015 sio kwamba inazuia watu ama taasisi kuendesha shughuli za utafiti au za kukusanya takwimu kwa matumizi ya mtu binafsi au taasisi husika nchini bali inawataka kutumia miongozo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu ili takwimu wanazozikusanya ziwe rasmi,” amesema Mangula.

  Oscar Mangula amebainisha kuwa ni kosa kisheria kwa mtu ama taasisi kuendesha utafiti wenye miongozo isiyothibitishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu na kuzitangaza kama takwimu rasmi.

  Ofisi ya Taifa ya Takwimu imepewa mamlaka kisheria ya kuratibu, kusimamia, kuchambua na kusambaza takwimu rasmi nchini.
  Mratibu wa Mpango Kabambe wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu nchini (Tanzania Statistical Master Plan-TSMP) kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Philemon Mahimbo akiwasilisha mada wakati wa mafunzo kwa wanasheria kuhusu sheria mpya ya Takwimu ya Mwaka 2015 yaliyofanyika leo mkoani Morogoro.
  Meneja wa Idara ya Mbinu za kitakwimu, Viwango na Uratibu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Emilian Karugendo akiwasilisha mada kuhusu takwimu na takwimu rasmi wakati wa mafunzo kwa wanasheria kuhusu sheria mpya ya Takwimu ya Mwaka 2015 yaliyofanyika leo mkoani Morogoro.
  Baadhi ya wanasheria kutoka Wizara na taasisi za Serikali wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa mada zinazohusu sheria mpya ya Takwimu ya Mwaka 2015 wakati wa mafunzo kwa wanasheria kuhusu sheria hiyo yaliyofanyika leo mkoani Morogoro.
  Baadhi ya wanasheria kutoka Wizara na taasisi za Serikali wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa mada zinazohusu sheria mpya ya Takwimu ya Mwaka 2015 wakati wa mafunzo kwa wanasheria kuhusu sheria hiyo yaliyofanyika leo mkoani Morogoro.

  0 0

  MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) imeshiriki kufanya usafi katika maeneo yanayozunguka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku mazingira duniani.

  Wafanyakazi wa mamlaka hiyo wameshiriki shughuli hizo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani, ambayo kitaifa inaadhimishwa kesho katika Wilaya ya Butiama, mkoani Mara.

  Akizungumza leo wakati wa kufanya usafi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Salim Msangi amesema, ndege za abiria zimekuwa zikizalisha hewa ya ukaa kwa asilimia mbili duniani kote, hivyo ni muhimu kupanda miti maeneo ya viwanja vya ndege ili kutunza mazingira.

  Amesema kila mwaka wamekuwa wakipanda miti katika maeneo ya viwanja vya ndege ili kufyonza hewa ya ukaa ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia kuharibu mazingira na kuongeza joto.

  "Lakini pia nimeagiza mameneja wote kuhakikisha wanapanda na nitakuwa natoa zawadi kila mwaka kwa meneja atakayeonekana kufanya vizuri," amesema Msangi.

  Amesema utunzaji wa mazingira ni muhimu kwani binadamu wote na viumbe hai vingine vinahitaji mazingira na kwamba hata kaulimbiu ya kitaifa ya mwaka huu ya “Hifadhi mazingira, Muhimu kwa Tanzania ya Viwanda” haiwezekani kuwa na viwanda katika mazingira ambayo si salama.
   Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Salim Msangi wa (kwanza kushoto) akiongoza ufanyaji  katika maeneo yanayozunguka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
   Wafanyakazi wa Mamlaka Viwanja vya Ndege nchini (TAA), wakiendelea na  usafi.
  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka Viwanja vya Ndege nchini (TAA),Salim Msangi akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

  0 0

  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers Siang'a (wa pili kulia) akiangalia sehemu ya kemikali bashirifu katika eneo la bandari kavu ya Ami Tabata jijini Dar es Salaam.

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii


  Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya imekamata kontena mbili zilizobeba kemikali bashirifu zilizokuwa tayari kwa kuingizwa nchini katika eneo la Bandari Kavu ya Ami Tabata Relini, Jijini Dar es salaam.


  Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa Kulevya , Rogers Siang’ a ameendesha operesheni  ya ukamataji wa Kemikali  bashirifu ambazo zilikuwa zikiingia nchini na kuanza kwa matumizi yake.  Akizungumza wakati wa  ukaguzi wa kemikali hizo, Kamishna Msaidizi wa Ukaguzi wa Kemikali Jinai ,  Bertha Mamuya, amesema  mzigo huo ni mwendelezo wa mzigo wa kampuni ya Tecno Scientific ambayo ilikuwa ikifanyia shughuli zake katika eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam.

  Amesema hapo awali waliweza kukamata lita 10,000  za Kemikali Bashirifu na katika Bandari ya Dar es Salaam zaidi ya  lita  6000 zimekamatwa zikitokea nchini Ufaransa.

  Ametaja kuwa mamlaka inaendelea na uchunguzi wa kuzichunguza kemikali hizo hili kubaini kama zimefuata njia sahihi ya kuingia nchini na iwapo  itabainika kuwa Kemikali hizo zimeingia kinyume cha sheria wahusika watapelekwa mahakamani.
  Baadhi ya watendaji wa Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), wakikagua kemikali ziliozopo ndani ya maboksi na kuchukua sampluli.
  Mzigo wa kemikali bashirifu ukipakuliwa ndani ya kontena katika eneo la bandari kavu ya Ami tabata jijini Dar es Salaam.
  Kamishna Msaidzi wa ukaguzi kemikali jinai wa Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Bertha Mamuya
  akiweka alama maboksi yaliyokutwa na kemikali bashirifu.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers Siang'a akiangalia mzigo wa kemikali bashirifu.
  Mmiliki wa Kiwanda cha Tecno Scientific akiwa amekaa katika eneo la bandari kavu akiangalia mzigo wake unavyokaguliwa.
  Wafanyakazi wa TRA na Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), wakikagua siri za kufungia kontena hili waweze kulifungua.

  0 0  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo alipofika kujitambulisha leo Ikulu Mjini Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na  Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo baada ya mazungumzo alipofika kujitambulisha leo Ikulu Mjini Zanzibar (Picha na Ikulu)

  0 0

   Muonekano wa Kiwanja. Ni Kuanzia mwanzo wa Picha mpaka mwisho wa Ukuta upande wa kushoto
  Mwanzo wa Picha Mpaka kwenye ukuta wa Ghorofa kule 

  Kiwanja Kipo KIGAMBONI KIBADA

  Ukubwa wa Kiwanja ni Mita za Mraba (Sqmeter) 1088

  Kiwanja kina hati safi na hakina mgogoro

  Bei ni Milioni 65 Maongezi kidogo yapo na Kiwanja hiki kinauzwa Na Mwenye Nacho 

  Kwa Mawasiliano 0786 821 613

  Karibu mwenye Uhitaji. Biashara Maelewano Hata 

  0 0

  Na Atley Kuni - Mwanza.

  Jumla ya mizani 3,070 Iliyo Hakikiwa katika mikoa ya kanda ya ziwa kwa ajili ya matayarisho ya ununuzi wa pamba kwa msimu wa 2017/2018 imekutwa salama baada ya kuhakikiwa na wakala wa Vipimo nchini.

  Akizungumza nami Jijini Mwanza, kaimu Meneja Sehemu ya Elimu, Habari na Mawasiliano Bi. Irene John, amesema, Wakala wa vipimo Tanzania ( WMA) chini ya usimamizi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeendelea kutoa elimu kwa wakulima pamoja na kuhakiki mizani itakayotumika kununulia zao la Pamba ikiwa ni maandalizi ya msimu wa ununuzi wa Pamba kwa mwaka huu.
  Wakulima mkoani Shinyanga wakipatiwa elimu kuhusu matumizi sahihi ya Mizani kabla ya msimu kuanza. 

  Bi. Irene amesema, Dhumuni kuu la utoaji elimu kwa wakulima wa zao la Pamba Kanda ya Ziwa ni kuwawezesha wakulima kutambua mizani iliyosahihi (inayoruhusiwa kwa biashara) na ile iliyochezewa (isiyoruhusiwa kwa biashara) ili waweze kujilinda wenyewe pindi maafisa vipimo wanapokuwa hawapo katika vituo vya kuuzia Pamba yao, lakini pia ni kuwawezesha wakulima kupata faida ya thamani kamili ya jasho lao.

  Ameongeza kuwa, katika maandalizi ya msimu mpya wa ununuzi wa Pamba zaidi ya mizani 1,402 imekaguliwa katika mkoa wa Shinyanga, mkoa wa Simiyu wamekagua zaidi ya mizani 302, mkoa wa Geita jumla ya mizani 40 tayari imekaguliwa, ilihali katika mkoa wa Mwanza wamekagua mizani 448, mkoa wa Mara mizani 690, mkoa wa Tabora wamekagua mizani 164 pamoja na mkoa wa Kagera wamekagua jumla ya mizani 24 ikiwa ni maandalizi ya ununuzi wa zao la Pamba.
  Wakulima mkoani Geita wakipatiwa Elimu. 

  Katika hatua nyingine Irene amesema, sheria ya Vipimo Sura 340 inawataka Wakala wa Vipimo kuhakiki na kupiga chapa vipimo vyote vinavyotumika katika biashara ikiwa ni pamoja na kuweka sticker kwa kipimo kitakachokuwa tayari kimehakikiwa na kukutwa kikiwa sahihi ili iwe rahisi kwa wakulima kuona na kutambua mizani iliyokaguliwa na kuruhusiwa kwa biashara kwa mwaka husika.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kuliombea Taifa ili liendelee kudumu katika hali ya amani na utulivu.

  Amesema suala la kudumisha amani na utulivu ni jukumu la kila mmoja, hivyo kila mwananchi kwa imani yake ahakikishe anashiriki kutunza hali hiyo.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Juni 2, 2017) baada ya kumaliza kuswali sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al-Gadaf, mjini Dodoma.

  Amesema ni vema kila mwananchi akajivunia hali ya amani na utulivu iliyoko nchini kwa kuwa ndiyo inayowezesha kufanyika kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo. “Tuendelee kudumisha amani, tufanye ibada kila mtu kwa imani yake. Serikali inaheshimu dini zote kwa sababu ndizo zinazojenga amani na mshikamano,” amesema.

  Pia amewataka wazazi wahakikishe wanawalea watoto wao katika mazingira ya kidini ili wanapokuwa watu wazima waje kuwa raia wema. “Tuendelee kuhamasisha watoto wetu wasikilize mahubiri ya dini; ni jukumu letu sisi kama wazazi kuwahimiza wahudhurie mahubiri ya viongozi wa dini ili waweze kujijenga vyema kimaadili na kiimani pia.”

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewakumbusha Waislamu wahakikishe wanautumia vizuri mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kuzidisha ibada na kusaidia watu wenye mahitaji. “Leo ni Ijumaa ya kwanza katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, nawaomba tutumie vizuri mwezi huu ili tupate baraka,” amesema.

  Ibada hiyo ya sala ya Ijumaa iliongozwa na Sheikh Nurdin Kishki ambaye ni Imamu wa Msikiti wa Vetenari, wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam.

  Sheikh Kishki katika hotuba yake, aliwasisitiza Waislamu waendelee kufanya mambo mema yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu ikiwemo kuwatunza wazazi wao, kumswalia Mtume Mohammed (S.A.W) na kufunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Sheikh Nurdin Kishik ambaye ni Mhadhiri wa Kimataifa wa Dini ya Kiislaam, (kulia) na ujumbe wake, ofisini kwake bungeni mjini Dodoma  Juni  2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki katika sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa  Al- Gadaf mjini Dodoma Juni 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Na Ashraf Said, Globu ya Jamii .

  Vijana wazalendo wampongeza Rais, Dk. John Pombe Magufuli juu ya hatua stahiki anazoendelea kuchukua dhidi ya unyonyaji uliokithiri katika sekta ya Nishati na Madini.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa vijana hao, Mwita Nyarukururu amesema jitihada za Rais Dk. John Pombe Magufuli zinawapeleka watanzania katika uchumi wa kati wa nchi kuweza kujitegemea na kuachana na wanyonyaji wa rasilimali katika sekta ya nishati na madini kutokana na misaada wanayoitoa .

  Amesema kuwa Rais Dk. John Pombe Magufuli ameonyesha dhamira ya kweli katika kuhakisha watendaji waliopewa mamlaka wanawajibika na wanaposhindwa kufanya hivyo hatua zinachukuliwa alivyoweza kuiwajibisha Wizara ya Madini pamoja na Bodi ya Ukaguzi wa Madini (TMAA).

  “Unyonyaji na Uhujumu uchumi katika sekta ya madini umekuwa ukipigiwa kelele na wananchi kutokana na Mikataba kuwa ya siri na mibovu isiyonufaisha Taifa,”Amesema.


  Aidha wamemuomba Rais Dk. John Pombe Magufuli na Serikali yake kupeleka upya bungeni mswada wa sheria zote zinazohusu sekta ya Nishati na Madini kwa lengo la kujadiliwa upya kwa maslahi ya taifa na wananchi wote.

  Mwenyekiti wa vijana Vijana Wazalendo, Mwita Nyarukururu katikati akizungumza na waandishi wa habari juu hatua ambazo anazichukua Rais Dk. John Pombe Magufuli katika sekta ya Nishati na Madini leo jijini Dar es Salaam. Kushoto Halima Makoroganya kulia ni Rose Manumba

  0 0


  0 0


  Katibu Mkuu wa Baraza la Waganga Shaka Mohamedi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na serikali kutoa elimu ya ugonwa wa Ebola na dalili zake kwa waganga wa Tiba asilia leo Jijini Dar  es salaam.

  Na Ashraf Said.

  Baraza la Waganga laiomba serikali kutoa mafunzo maalum kwa waganga wa tiba asilia kuwapa elimu na kuufahamu ugonjwa wa Ebola na dalili zake ili kuweza kushiriki katika kutoa taarifa pindi watakapokutana na mgonjwa mwenye dalili za ugonjwa huo

  Mapema wiki hii Wizara ya Afya,maendeleo ya jamii, jinsia,wazee na watoto kupitia kwa Waziri Ummy Mwalimu walitoa taarifa rasmi zinazohusu ugonjwa wa Ebola na kusema kuwa bado haujaingia nchini na watanzania wasiwe na hofu kwani serikali iko makini katika kuhakikisha wanapambana nao.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Baraza la Waganga Shaka Mohamedi ameiomba Wizara ya Afya,maendeleo ya jamii, jinsia,wazee na watoto kuangazia zaidi kwenye utoaji wa elimu dhidi ya ugonjwa wa Ebola kwa waganga wa tiba asilia ikizingatia na wao ni moja ya watoaji huduma za kiafya kwa jamii inayowazunguka.

  Shaka amesema waganga wa tiba asilia watakapofahamu dalili za ugonjwa wa Ebola itakuwa ni rahisi sana kuweza kutoa taarifa kwa Serikali kulingana na huduma wazitoazo na ukaribu uliopo baina yao na jamii

  "Naipongeza wizara ya Afya kwa kuchukua hatua za haraka na mapema ikiwa ni tahadhari za kuzuia ugonjwa wa Ebola kuingia nchini kutoka nchi jirani ya Congo DRC,lakini pia naomba wizara hii kuchukua hatua za ziada kuhakikisha wananchi kuwa na uelewa mpana wa dalili za ugonjwa wa Ebola,'' Amesema.

  Licha ya hayo,katibu mkuu wa baraza la waganga BAWATA ameonya vikali waganga wote wanaohudumia au kujinadi kutoa tiba asilia kwa jamii hali ya kuwa hawatambuliki kwenye Baraza hilo,ni kosa kisheria.

older | 1 | .... | 1723 | 1724 | (Page 1725) | 1726 | 1727 | .... | 3284 | newer