Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1710 | 1711 | (Page 1712) | 1713 | 1714 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Soka Duniani, Gianni Infantino ameandika Barua ya kuipongeza timu ya Yanga kwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo. isome barua hiyo hapo chini.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameiagiza halmashauri ya Manispaa ya Singida kusimamia upatikanaji wa mizinga hamsini ya nyuki kwa ajili ya timu ya mpira wa Miguu ya Misuna Stand kwakuwa imekua ni timu yenye lengo la kuwa kituo cha mafunzo na marekebisho ya tabia.

  Dokta Nchimbi ametoa agizo hilo mapema leo asubuhi alipokutana na wananchama wa klabu hiyo ambapo amewaomba radhi kwakuwa Mkoa, wilaya na Halmashauri ya manispaa imekuwa haitoi ushirikiano wa kutosha kwa timu hiyo.

  Amesema timu hiyo ambayo imeundwa na umoja wa Mawakala wa Mabasi Singida, imekuwa mstari wa mbele wa kubadilisha tabia mbaya kuwa njema hasa kutokana na mazingira ya stendi nyingi nchini kutawaliwa na vitendo vya uvunjaji wa sheria.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na wanachama wa timu ya Stand Misuna mapema leo asubuhi alipowatembelea na kuwahamasiha kuendeleza timu hiyo ili ipande daraja la kwanza katika msimu ujao.

  Dkt. Nchimbi ameongeza kuwa sasa serikali ya Mkoa, wilaya na halmashauri imewatambua na kwa kuthibisha hilo yeye kama mkuu wa mkoa amejiunga ramsi kama mwananchama wa timu hiyo ya mpira wa miguu na kutoa michango ya miezi mitatu ambapo kila siku mwanachama anatakiwa kuchangia shilingi miatano.

  “Nimetoa ada ya uanachama kuonyesha kuwa tupo pamoja na tutashirikiana kuhakikisha timu yetu ya Misuna Stand inapanda daraja, kwa sasa nawaomba wanachama wote tushirikiane katika kuiboresha timu yetu”, amesisitiza.

  Dkt. Nchimbi amesema lengo la Mkoa ni kuwa na timu mbili za mpira wa miguu ambazo zinashiriki ligi kuu na kwakuwa tayari uwanja wa nyumbani wa Namfua Stadium uko katika hatua za mwisho za ukamilishaji huku akiwahakikishia mashabiki wa Singida United kuwa wataishuhudia timu yao ikicheza nyumbani.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akionyesha ada ya uanachama wake katika timu ya mpira wa miguu ya Stand Misuna mapema leo asubuhi alipowatembelea wanachama wa timu hiyo, pembeni yake ni Mwenyekiti wa timu hiyo Yahya Said Kisiu.

  Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo ambaye ameteuliwa kuwa Mlezi wa Timu hiyo amesema stendi zimekuwa ni mahala pa wizi, uvutaji wa madawa ya kulevya na vitendo viovu lakini jitihada za Misuna Stand FC zitabadilisha tabia hizo na kuwa njema.

  Tarimo amesema wanachama watakuwa wachapakazi kwakuwa kila siku wanatakiwa kulipa kiasi cha shilingi miatano lakini pia wamejipanga kuhakikisha wanaelimishana juu ya madawa ya kulevya jambo ambalo litaufanya Mkoa na Mji wa Singida kuwa wa Amani sana.

  Ameongeza kuwa atahakikisha anasimamia utekelezaji waq agizo la Mkuu wa Mkoa La kuipatia timu hiyo Mizinga hamsini pamoja na kuhakikisha halmashauri inatoa eneo la utundikaji wa miznga hiyo pamoja na kuitunza.
  Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo ambaye pia ni mlezi wa timu ya mpira wa miguu ya stand Misuna akizungumza na wanachama wa timu hiyo mapema leo alipowatembelea akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Singida.


  Naye Mwenyekiti wa tawi la Misuna stand FC Yahya Said Kisiu amesema wanachama wa timu hiyo wamepata faraja kubwa sana kwa kutembelewa na Mkuu wa Mkoa pamoja na kuwapatia mizinga hamsini.

  Kisiu ameongeza kuwa timu hiyo iliyoanzishwa mwaka 2014 ilifanikiwa kufika ligi daraja la pili lakini kwa sasa imeshuka tena daraja huku akisisitiza kuwa ari mpya waliopatiwa mkuu wa Mkoa itawezesha timu hiyo kupanda tena daraja.
  Wanachama wa timu ya mpira wa miguu ya Stand Misuna wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi mapema leo alipowatembelea.

  0 0  0 0  0 0

  Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), imesisitiza kuwa wapiga kura wa Lesotho wanatarajia kuwa Serikali itakayochaguliwa na wananchi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Wabunge wa mwaka 2017 itasimamia na kutekeleza mageuzi yanayohitajika nchini humo. 

  Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi ya SADC, Kiongozi wa Timu hiyo Balozi Dkt. Augustine Mahiga alisema japo mazingira ya upigaji kura yameandaliwa na kukamilika, lakini huu ni uchaguzi wa tatu ndani ya miaka mitano na wapiga kura wamechoka. Ni matumaini ya SADC na ya wananchi wa Lesotho kuwa Serikali ijayo itajipanga vizuri na kusimamia kikamilifu mageuzi ya kikatiba na kimfumo ambayo yataleta uimara wa kisiasa na unaotabirika nchini humo.  "Jumuiya yetu imejiwekea misingi imara ya kidemokrasia ambayo ikijumuishwa na ile ya nchi, na kimataifa kama Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa tunapata vigezo tisa ambavyo timu yetu itaviangalia wakati huu wa uchaguzi" alisema Balozi Mahiga.

  Baadhi ya vigezo vitakavyoangaliwa kwenye uchaguzi huo ni ushiriki wa wananchi kwenye michakato ya siasa, fursa sawa kwa vyama vyote vya siasa, uhuru wa taasisi zinazosimamia uchaguzi, elimu ya mpiga kura na wajibu wa wagombea na vyama vya siasa kukubaliana na matokeo kama yatakavyotangazwa na tume huru ya uchaguzi kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za nchi husika. 

  Wadau mbali mbali waliohudhuria hafla hiyo wakiwemo Viongozi wa vyama vya Siasa na Jumuiya ya Diplomasia nchini Lesotho, walielezwa kuwa SADC imepongeza hatua ya vyama vya siasa kuweka makubaliano yaliyosainiwa na Viongozi wa vyama kukubali matokeo ya uchuguzi iliyoratibiwa na Umoja wa Makanisa Lesotho. 

  Uchaguzi Mkuu wa Wabunge nchini Lesotho unatarajiwa kufanyika tarehe 3 Juni 2017 ambapo Chama au Muungano wa Vyama vyenye ushindi mkubwa wa viti vya ubunge, wataunda Serikali ambayo itaingozwa na Waziri Mkuu. 

  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  Maseru, Lesotho 26 Mei, 2017


  0 0


  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe, akitoa ufafanuzi mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari,kuhusiana na namna mfuko huo unavyoweza kuhudumia wateja wake,katika semina iliyofanyika leo mapema leo jijini Dar.Pichani kati ni
  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Theophil Makunga pamoja na Katibu wa Jukwaa hilo Neville Meena. 
  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Theophil Makunga akichokoza Mada zilizowasilishwa na wataalamu wa mfuko huo wa LAPF,mbele ya Wahariri wa Vyombo vya Habari,zikiwemo mada zilizohusu Afya,mambo ya Uzazi kwa akina mama,Mafao mbalimbali ikiwemo fao la Elimu,fao la Kujitoa.Pichani kulia ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe,kushoto ni Ofisa Mwandamizi Mipango na Uwekezaji, Eliya Shola pamoja na Meneja Mafao wa LAPF, Ramadhan Mkeyenge kutoka LAPF
  Mmoja wa Wahariri akiuliza swali kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo na mfuko huo wa LAPF.
  Meneja Mafao wa LAPF, Ramadhan Mkeyenge, akitoa mada katika semina hiyo.Mkeyenge alisema kuwa mfuko huo mpaka sasa umeweza kutoa mafao na mikopo kama vile,mafao ya uzazi ambapo zimetolewa zaidi ya bilioni 12,mkopo wa elimu zaidi ya bilioni moja zimetolewa,mkopo wa kujikimu zaidi ya bilioni 5,mikopo ya nyumba zaidi ya bilioni 2,pamoja na hayo akaongeza kusema kuwa pia kuna waliolipwa kabla ya muda wa kustaafu Zaidi ya bilioni moja.
  Ofisa Mwandamizi Mipango na Uwekezaji, Eliya Shola, akitoa ufafanuzi kuhusiana na uwekezaji mbalimbali unaofanywa na mfuko huo,ikiwemo katika suala la viwanda na namna ambavyo imechukua tahadhari katika suala zima la usimamizi wa viwanda hivyo
  Ofisa Habari wa Mfuko wa LAPF, Rehema Mkamba (kushoto), akiwa na baadhi ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kwenye semina hiyo.


  Wahariri wa Vyombo vya habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye Semina hiyo ilioandaliwa na LAPF,na kufanyika mapema leo jijini Dar.Picha na Michuzi JR.


  0 0

  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema iwapo Mpango wa Huduma ya Afya ngazi ya Jamii utatumika vizuri utasaidia kuokoa Afya na maisha ya wananchi wengi Mkoani humo.

  Mtaka ameyasema hayo katika kikao kilicho wahusisha Viongozi ngazi ya Mkoa,Wilaya, watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Halmashauri ya Wilaya Bariadi, Itilima na Mji wa Bariadi, ambacho kililenga kutoa elimu kuhusu utekelezaji wa mpango wa huduma ya Afya ngazi ya Jamii mkoani humo.

  Mtaka amesema mwamko wa kupata huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa wananchi katika maeneo mengi mkoani humo uko chini, hivyo mpango huu wa kutoa huduma ngazi ya kaya utasaidia kuhamasisha wananchi kutafuta huduma za afya katika vituo hivyo badala ya kutegemea tiba za kienyeji.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji katika kikao cha kutoa elimu kwa viongozi hao kilichofanyika Mjini Bariadi kuhusu utekelezaji Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii ngazi ya Jamii Mkoani humo.

  “Tukitumia huduma hii ya Afya Majumbani vizuri itasaidia sana, tukifika mahali ambapo jamii yetu itapata mwamko wa kupata matibabu katika vituo stahiki vya afya tutakua tumeokoa jamii yetu, kwa sababu bado wapo wanaoamini kupata matibabu katika tiba za kienyeji; tungehitaji wananchi wetu huduma ya kwanza kwenye afya iwe vituo vyetu kutolea huduma za afya na siyo tiba mbadala” amesema Mtaka.

  “........kwa sisi ambao tunatengeneza Mkoa wetu katika Uchumi, Uchumi ni Afya wananchi hawawezi kufanya kazi wakajenga uchumi kama hawatakuwa na afya njema” alisisitiza. Aidha, Mtaka amewataka Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji kufanya utambulisho wa kutosha wa wahudumu wa afya ya Msingi ngazi ya jamii watakaokuwa wakitoa huduma kwa wananchi katika maeneo yao ili wataalam hao wasije wakapata madhara yoyote wakati wakitekeleza majukumu yao.
  Dkt.Ama Kasangala kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, akizungumza na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji katika kikao cha kutoa elimu kwa viongozi hao kilichofanyika Mjini Bariadi kuhusu utekelezaji Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii ngazi ya Jamii Mkoani Simiyu.

  Mkuu huyo wa Mkoa pia amewataka wananchi kuachana na taratibu za kimila zinazoathiri utendaji wa watumishi wa Umma ikiwemo kutumia mahakama za kimila (dagashida) na akawataka viongozi hao kuwasaidia wananchi kubadilika ili wahudumu wa afya ngazi ya Jamii watakaopelekwa katika maeneo yote ya mkoa huo watekeleze majukumu yao bila vikwazo vyovyote.

  Wakati huo huo Mtaka ameomba Shirika lisilo la Kiserikali la AMREF lisaidie katika kuajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii walipewa mafunzo, ili wasaidie kutoa huduma na kupunguza changamoto ya upungufu wa watoa huduma wakati Serikali ikiendelea kushughulikia suala hilo.
  Baadhi ya Watendaji Kata, Mitaa na Vijiji kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka katika kikao cha kutoa elimu kwa viongozi hao kilichofanyika Mjini Bariadi kuhusu utekelezaji Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii ngazi ya Jamii Mkoani humo.

  Vile vile ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa afya ikiwemo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kushughulikia suala la upatikanaji wa vifaa ili watoa huduma ngazi ya jamii watakapowafikia wananchi waweze kutoa huduma stahiki kwa wakati.


  0 0  0 0  Lori lililopakia Boti ya MV MKONGO likipita chini ya daraja la Furahisha jijini Mwanza. Boti hiyo inayomilikiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) inasafirishwa kuelekea mkoa wa Pwani kwa ajili ya kutoa huduma ya kusafirisha abiria kati ya Utete na Mkongo
  Boti ya MV MKONGO inayomilikiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ikiwa imepakiwa kwenye lori, Boti hiyo inasafirishwa kwa njia ya barabara kuelekea Utete Pwani kwa ajili ya kutoa huduma ya kusafirisha abiria kati ya Utete na Mkongo.
  Lori lililobeba Boti ya MV MKONGO inayomilikiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) likiwa njiani kuelekea mkoa wa Pwani, boti hiyo inatarajiwa kutoa huduma ya kusafirisha abiria kati ya Utete na Mkongo.PICHA ZOTE NA THERESIA MWAMI (TEMESA)

  0 0

  Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) kwa kushirikiana na ActionAid Tanzania waliandaa mafunzo ya siku tatu kwa wanachama wa chama cha walimu na asasi za kiraia za elimu mkoa wa Singida kuhamasisha upatikanaji wa haki za mtoto shuleni na maendeleo ya sekta ya elimu kwa kushawishi serikali kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu kwa kutumia rasilimali za ndani. 

  Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Meneja Mradi kutoka ActionAid Tanzania Karoli Kadeghe alielezea katika bajeti ya elimu 2016/17, takribani bilioni 277 sawa na asilimia 31% ilitarajiwa kukusanywa kutoka kwa wahisani na washirika wa maendeleo. 

  Hata hivyo, hadi kufikia mwezi Machi 2017, wahisani walikuwa wametoa kiasi cha shilingi bilioni 132 tu sawa na asilimia 47.6%. Alisisitiza kuwa ni vyema serikali iimarishe  vyanzo vyake vya mapato vya ndani ili kuepuka aibu hii na sisi wadau wa elimu tunalo jukumu la kuisimamia serikali katika kutimiza wajibu wake. 

  Kila mtu akilipa kodi stahiki kadiri ya kile anachozalisha na pia serikali ikidhibiti mianya ya upotevu wa kodi, hata kodi ya PAYE itapungua na kumpa mwalimu ahueni katika makato hayo.
   Mkufunzi wa Mafunzo, Wakili Dominic Ndunguru akielezea kuhusu ripoti ya utafiti ya shirikisho la dini (Interfaith standing committee) iliyozinduliwa Mwezi Mei mwaka 2017 kwa kuwashirikisha kamati ya kudumu ya Bunge ya Uchumi na Fedha inaliyoonyesha kuwa Tanzania kwa sasa inapoteza takribani dola bilioni 1.83 sawa na Tsh trilioni 4.09 kwa mwaka kupitia misamaha ya kodi, uhamishaji wa fedha nje ya nchi bila kufuata utaratibu, kushindwa kutoza kodi sekta isiyo rasmi na aina nyingine za ukwepaji kodi.
    Meneja Mradi Wa Elimu ActionAid Tanzania, Karoli Kadeghe akiwasilisha mada kuhusu mtazamo wa upatikanaji wa elimu nchini Tanzania wakati wa Mafunzo ya wanachama na viongozi wa Chama cha Walimu na Asasi za Kiraia waliokutana mkoani Singida yaliyofanyika kwa siku tatu.
   Mdau wa Elimu kutoka asasi za kiraia, Lucy Mkosamali akichangia mada ya umuhimu wa uwekezaji katika maendeleo ya sekta ya elimu kwenye mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida ulioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kuwa mgeni kwenye maonyesho ya kimataifa yatakayoanza kesho kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga 
  Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akikagua mabanda mbalimbali kuelekea uzinduzi wa maonyesho ya kimataifa yatakayofunguliwa kwenye na Waziri Mwijage
  Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akisalimiana na wanawake wajasiriamali wakati akikagua mabanda mbalimbali kuelekea uzinduzi wa maonyesho ya kimataifa yatakayofunguliwa kwenye na Waziri Mwijage
  Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akisalimia na baadhi ya wajasiriamali wakati apokuwa akikagua mabanda mbalimbali kuelekea uzinduzi wa maonyesho ya kimataifa yatakayofunguliwa na Waziri Mwijage


  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka akfungua mkutano wa mwaka wa Chama hicho ulioshirikisha wanachama wake ambao ni wanasheria wanawake, Mkutano huo umefanyika leo kwenye Hoteli ya New Afrika jijini Dar es salaam na kujadili mambo kadhaa yakiwemo mafanikio na changamoto zinazokabili chama chao pamoja na jamii kwa ujumla wake.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
  Kutoka kulia ni Maria Matui Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania ( TAWLA), Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka, Tike Mwambipile Mkurugenzi Mtendaji wa (TAWLA) na Lulu Ngwanakilala Mtoa mada katika mkutano huo wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyojadiliwa na washiriki wa mkutano huo.


  0 0


  Na Mathias Canal, Dar es salaam

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda Leo Me 27, 2017 amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi katika dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma na kuukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke tayari kwa kumulika miradi ya Maendeleo.

  Mara baada ya kukagua Miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Temeke Mwenge wa Uhuru utazuru katika Wilaya ya Kigamboni Tarehe 28/05/2017, Siku ya Tarehe 29/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Ilala, Tarehe 30/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Kinondoni na Tarehe 31/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Ubungo.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda amesema kuwa Mwenge wa uhuru ni chombo kilichoasisiwa na baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni Tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika hivyo kuzuru katika Mkoa wa Dar es salaam itakuwa ni kichocheo kikubwa katika kuhamasisha Maendeleo, Uzalendo, Umoja , Mshikamano na kudumisha Amani ndani na nje ya Taifa letu.

  Mhe Makonda alisema kuwa Mwaka huu utakuwa mwaka wa 24 tangu mbio za Mwenge wa Uhuru zirejeshwe chini ya utaratibu wa usimamizi wa serikali kutokana na mabadiliko ya kidemokrasia baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992.

  Katika mapambano dhidi ya Dawa za kulevya Mhe Makonda alisema kuwa jitihada ya kudhibiti kusambazwa na Matumizi ya Dawa za Kulevya ni kuifanya kuwa ajenda muhimu kiutekelezeji kwa mustakabali wa maisha ya watanzania kwa kuwa Jambo hilo linagusa nguvu kazi ya Taifa.
   
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda (Kushoto) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi (Kulia) katika dhifa ya Makabidhiano iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017. 

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda (Kushoto) akizungumza jambo na Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Simon Sirro katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017. 

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda (Kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017. 
  Wananchi waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.   0 0
 • 05/27/17--13:30: Article 0


 • 0 0

  Na Lydia Churi, Mahakama, Songea
  Mahakama Kuu, Kanda ya Songea imefanikiwa kwa asilimia 100 kumaliza kesi zote zenye umri unaozidi miaka miwili Mahakamani.
  Akitoa taarifa ya hali ya kesi katika Mahakama Kuu, Kanda ya Songea, Jaji Mfawidhi wa Kanda hiyo Mhe. David Mrango alisema hadi kufikia Desemba 2016, Kanda yake ilikuwa na kesi 28 za jinai.
  Alifafanua kuwa kesi za jinai zilizofunguliwa kati ya Januari na Mei mwaka huu zilikuwa 51na zilizomalizika na kutolewa hukumu ni 52 na zilizobaki kesi 27.
  Kwa upande wa kesi za madai , Jaji Mrango alisema mpaka Desemba 2016, kulikuuwa na kesi 46 za madai kwenye Kanda yake , jumla ya kesi za madai zilizofunguliwa kati ya Januari na Mei 2017ni 42 na zilizosikilizwa na kutolewa hukumu ni 47 wakati zilizobaki ni kesi 41.
  Alisema kati ya Januari na Mei, vikao viwili vya kesi za mauaji vilifanyika ambapo kesi 22 zilisikilizwa na 18 zilitolewa hukumu huku 2 zikibaki.
  Kuhusu upatikana wa nakala za hukumu, Jaji Mfawidhi huyo alisema licha ya changamoto zilizopo, Kanda yake imekuwa ikitoa nakala za hukumu pamoja na mienendo ya kesi kwa wakati.
  Mahakama kuu, Kanda ya Songea ni moja ya Kanda za Mahakama Kuu 13 nchini, Kanda hii ina jumla ya Majaji wawili.
  IMAGE

  0 0


  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa daraja la Kelema lenye urefu wa mita 220 linalounganisha wilaya ya Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.  Akizungumza leo mkoani Dodoma, mara baada ya kukagua daraja hilo lililopo katika barabara ya Mayamaya-Mela KM 99.35, Naibu Waziri Ngonyani  amesema kuwa kukamilika kwa daraja hilo na  barabara za maingilio katika daraja hilo kutarahisisha  huduma ya usafiri kwa wananchi wa mkoa huo na mikoa jirani ya  Manyara na Arusha.  "Daraja hili na barabara zake ni kiungo muhimu kati ya mkoa huu na mikoa  ya Manyara na Arusha  na pia inaunganisha  nchi ya Tanzania, (Cape Town) South Afrika hadi (Cairo) Misri, hivyo kurahisisha huduma za  usafirishaji wa abiria na mizigo kutoka hapa kuelekea maeneo mengine", amesema Eng.Ngonyani.  Aidha, Naibu Waziri ameitaka kampuni ya ujenzi ya Chico kuhakikisha inamaliza daraja hilo ifikapo mwezi wa Kumi mwaka huu kama ilivyoandikwa kwenye mkataba ili wananchi kuweza kulitumia.

  Kwa upande wake Mhandisi Mshauri wa mradi huo, Eng. Leornado Licari, amesema kuwa kwa sasa mradi umefika asilimia 87 ambapo hivi karibuni wanatarajia kuweka lami.  "Nakuhakikishia kumaliza mradi huu kwa wakati kwani kazi zilizobaki kwa sasa hivi ni chache, kwa hiyo hadi kufikia mwezi Septemba tutakuwa tumeshakamilisha kazi zote", amesisitiza Mhandisi Mshauri Licari.  Naibu Waziri Ngonyani yupo katika ziara ya kikazi ya siku moja katika mikoa ya Dodoma na Manyara ambapo pamoja na ukaguzi wa daraja hilo pia amekagua madaraja mengine matatu likiwemo la Msui, Kingali na Mela pamoja na ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga KM 88.8.  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
   Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35 Eng. Leornado Licari akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, kuhusu hatua za ujenzi zilizofikiwa za Daraja la Kelema Mita 220 linalounganisha wilaya ya Chemba na kondoa mkoani Dodoma, leo.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), akikagua hatua za ujenzi zilizofikiwa za Daraja la Kelema Mita 220 linalounganisha wilaya ya Chemba na kondoa mkoani Dodoma, leo. Kulia ni Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35 Eng. Leornado Licari.
   Mkandarasi wa Kampuni ya Chicco, Li Jianzheng, akimounesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (wa pili kulia), namna ya usukwaji nondo katika Daraja la Kelema lenye urefu wa mita 220 wakati alipokagua daraja hilo mkoani Dodoma leo.
   Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35 Eng. Leornado Licari akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, kuhusu ujenzi wa Daraja la Msui lenye urefu wa mita 45 lililopo katika barabara hiyo, mkoani Dodoma, leo.
   Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mela – Bonga Km 88.8 Eng. Kini Kuyonza akimuonesha taarifa ya mradi Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, wakati alipokuwa akikagua barabara hiyo, mkoani Manyara, leo.


  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akikagua zege lililowekwa katika barabara ya Mela-Bonga KM 88.8 eneo la Mlima Kolo uliopo wilaya ya Kondoa, wakati alipokagua ujenzi wake, leo. Kulia ni Mhandisi Mshauri wa mradi huo Eng. Kini Kuyonza

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  WANAFUNZI wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya nje wanatakiwa kupita katika Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) kwa ajili ya kuangalia vigezo ambavyo vinahitajika.

  Hayo yamesemwa na Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Dk. Fabian Mahundu wakati wa maonesho ya vyuo vikuu vya nchini India yaliyofanyika katika ubalozi wa nchi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
  Dk. Mahundu amesema mwanafunzi anayekwenda kusoma vyuo vya nje anatakiwa kuwa na ufaulu wa D mbili ambazo ni viwango vilivyowekwa.

  Amesema kuwa mwanafunzi anayekwenda kusoma nje bila kupita katika tume hiyo ilivyowekwa kwa ajili ya kuratibu,  akirudi anakuwa anakosa sifa katika mfumo wa elimu nchini.

  Kwa upande wa Balozi wa India nchini, Sandeep  Arya amesema kuwa Tanzania na India zimekuwa na mahusiano mazuri katika nyanja mbalimbali. Amesema India imekuwa ikitoa elimu bora na kwamba Tanzania ni nchi ambayo inanufaika kwa kupata ufadhili wa watu 25 kila mwaka.
  Naye, Mkurugenzi wa Global Education Link  (GEL), Abdulmalik Mollel amesema kuwa nchi ya India  iangalie uwezekano wa kuongeza idadi ya ufadhili hadi kufikia 100 kutokana na mahitaji yaliyopo.

  Amesema kuwa GEL imekuwa katika msisitizo wa mara zote katika kuhakikisha wanafunzi wote wanapita TCU  kwa ajili ya kuhakikiwa..
  Maonesho vya vyuo vikuu vya nchini India yamefadhiliwa a kampuni ya Global Education Link (GEL).
   Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Dk.Fabian Mahundu akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozi wa India Jijini Dar es Salaam.
   Balozi wa India Nchini Tanzania, Sandeep Arya  akizungumza akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozini  Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
   Mkurugenzi Mtendaji wa  Global Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozi wa India Jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Udahili wa Global Education Link (GEL), Zakia Nassor akitoa elimu kwa wanafunzi waliotembelea banda  katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozini  Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
   Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Dk.Fabian Mahundu akiwa na Balozi wa India nchini, Sandeep  Arya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa  Global Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel wakitembelea  mabanda katika  maonesho ya vyuo vikuu vya nchini India.leo jijini Dar es Salaam. 
   Balozi wa India nchini, Sandeep  Arya akiwa katika picha ya  watanzania  25 waliopata ufadhili wa Serikali ya India wa kusoma katika vyuo vikuu vya nchi hiyo leo jijini Dar es  Salaam.

  0 0

   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Abdallah Bulembo akipewa na Wazee, heshima ya Kiongozi Mkuu wa Kabila la Wamasai la Ulaigwanani, alipowasili ukumbini kuzungumza na Watendaji na viongozi na wanachama wa CCM wakiwemo mabalozi, katika mji mdogo wa Mererani mkoani Manyara, leo, May 27, 2017. (Picha na Bashir Nkoromo).
    Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Abdallah Bulembo akizungumza ukumbini na Watendaji wa serikali, viongozi na wanachama wa CCM wakiwemo wajumbe wa nyumba kumi, katika mji mdogo wa Mererani mkoani Manyara, leo May 27, 2017.
   Viongozi na wanachama wa CCM wakiwemo wajumbe wa nyumba kumi wakishangilia wakati Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa CCM, Abdallah Bulembo alipozunumza nao ukumbini katika mji mdogo wa Mererarini mkoani

  0 0

  Na Lydia Churi, Mahakama, Songea

  Mahakama ya Tanzania itashirikiana na Wadau wake ili kuhakikisha inawajibika ipasavyo na kufikika kirahisi ili wananchi wapate haki kwa wakati.

  Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma jana, Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali alisema Mahakama haitaweza kufanya kazi ya kutoa haki bila kushirikisha wadau wake.

  Alisema Mahakama kupitia Mpango Mkakati wake wa miaka mitano hivi sasa iko kwenye Mpango maalum wa kumaliza kesi zote za zamani ambapo awamu ya kwanza ya Mpango huo iliyoanza mwezi Aprili, itamalizika leo Mei, 26.

  Alisema ili kumaliza kesi hizo wadau wa Mahakama ni muhimu kwa kuwa wataharakisha na kurahisisha utendaji wa shughuli za Mahakama .

  Akizungumza na Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Songea, Mhe. Wambali amewataka kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na kuachana na vitendo vya rushwa na lugha mbaya kwa wananchi wanaofika mahakamani kutafuta haki zao.

  Alisema kwa kufanya hivyo taswira ya Mahakama kwa jamii itakuwa ni chanya na Mahakama kuendelea kuwa kimbilio la wengi.

  Jaji Kiongozi ameanza ziara katika Mahakama Kuu, Kanda ya Songea na Mtwara yenye lengo la kukagua shughuli za Mahakama na kusisitiza utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama (2015-2020).

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Binilith Mahenge amesema endapo Mahakama itatekeleza kwa vitendo nguzo tatu za Mpango Mkakati wake ni dhahiri kuwa dhana ya Tanzania kuwa na uchumi wa kati.

  0 0


  NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Sadala amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya kimarekani inayoshughulikia masuala ya Demokrasia Duniani (NDI), kanda ya mashariki na kusini mwa afrika, Dkt. Keith Jennings, huko Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.

  Katika mazungumzo hayo Naibu Katibu Mkuu huyo alieleza kwamba CCM imekuwa mdau mkubwa wa kutekeleza dhana ya demokrasia kwa vitendo, sambamba na kutoa fursa za uongozi kwa makundi yote ya kijamii.

  Alisema ujio wa taasisi hiyo Zanzibar utafungua fursa mbali mbali kwa vijana na wanawake kupata ujuzi wa kukabiliana na changamoto za kisiasa na kiuchumi.

  Pia Dkt. Mabodi aliishauri Taasisi hiyo kufungua Ofisi hapa nchini kwa lengo la kuratibu masuala mbali mbali yakiwemo kuwapatia Vijana fursa za kimasomo nchini marekani ili waweze kujifunza na kupata ujuzi wa fani zinazokubalika katika soko la ajira hapa nchini.

  “Vijana na Wanawake wa Zanzibar wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa ajira, hivyo taasisi yenu ikitoa fursa za mafunzo ya ujasiria mali itasaidia kukabili tatizo hilo.”, alisema Dkt. Mabodi.

  Naye Mkurugenzi wa taasisi ya kimarekani inayoshughulikia masuala ya Demokrasia duniani (NDI), kanda ya mashariki na kusini mwa afrika, Dkt. Keith Jennings alieleza kuwa taasisi hiyo inajishughulisha na masuala ya Demokrasia na kutoa mafunzo ya ujasiria mali kwa vijana na wanawake duniani.

  Dkt. Keith alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni taasisi hiyo kujitambulisha kwa CCM Zanzibar na kubadilishana mawazo yatakayosaidia kufanya kazi za kisiasa kwa pamoja.

  ” Taasisi yetu imekuwa ikitoa mafunzo ya ujasiriamali pamoja na mbinu za kutumia fursa zinazopatikana katika mifumo ya Kidemokrasia kwa vijana na wanawake, hivyo tunatarajia hata kwa Zanzibar makundi hayo yatanufaika na mpango huo.”, alieleza Dkt. Keith.

  Dkt. Keith alisema Zanzibar ina historia kubwa ya kisiasa hivyo taasisi hiyo ina dhamira ya kuwajengea uwezo vijana mbali mbali hapa nchini ili waweze kutumia vizuri fursa zilizopo katika michakato ya kidemokrasia.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala ” Mabodi” akizungumza na Mkurugenzi wa taasisi ya kimarekani inayoshughulikia masuala ya Demokrasia duniani (NDI), Dkt. Keith Jenningspamoja na ujumbe wake


older | 1 | .... | 1710 | 1711 | (Page 1712) | 1713 | 1714 | .... | 3278 | newer