Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

JUMUIYA YA MADOLA YA WAPIGA MSASA WABUNGE KUTOKA NCHI 16

0
0
Wajumbe wa Bunge la Umoja wa Bunge la Jumuiya ya Madola wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza kwa Mafunzo ya wiki moja yalioandaliwa na Bunge hilo, katika mafunzo hayo Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania limewakilishwa na Naibu Spika Dr. Tulia Ackson na Baraza la Wawakilishi Zanzibar limewakilishwa na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Tulia Ackson akitoa nasaha zake za shukrani kwa niaba ya Wabunge kutoka nchi za Jumuiya ya Madola walioshiriki mafunzo hayo yaliofanyika katika ukumbi wa University of Witwaterstrand, Johannesburg South Africa.
Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano Dr Tulia Ackson pamoja na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Simai Mohammed Said wakishiriki katika masomo ya wiki pamoja huko Afrika Kusini University of Wits ambapo jumla ya Wabunge kutoka nchi 16 kutoka Jumuiya za Madola wameshiriki masomo hayo. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akiwasilisha kazi ya kikundi wakati wa mafunzo hayo ya wiki moja yanayofanyika Nchini Afrika Kusini yalioandaliwa na Umoja wa Bunge la Jumuiya ya Madola, akieleza kuhusiana na umuhimu wa kamati za kudumu za mabunge ya Jumuiya Madola kuelekea karne 21. 

Kutoka kushoto ni Mbunge kutoka India Ajay Misra, Naibu Spika Tanzania Dr Tulia Ackson, Seneta kutoka Jamaica Charles Pearnel na Mussa Dlamini Swaziland. Masomo hayo yanafanyika Johanessberg University of Witwatersrand kwa wiki moja na kudhaminiwa na Commonwealth Wealth. 
Wawakilishi kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Naibu Spika Dr.Tulia Ackson pamoja Simai Mohammed Said kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa masomomi South Africa University of Witwatersrand wakibadilishana mawazo na Mbunge wa Swaziland Mhe Mussa Dlamini


BILLNAS JIWE LA MWEZI XXL YA CLOUDS FM NA MAKAMUZI YA SHOO YA NGUVU NA MZEE WA MBEYA LEO.

Menejimenti Ya DCC Yapongezwa kwa Kurejesha Uhai wa Shirika.

0
0

Nuru Juma – MAELEZO.

Serikali imeipongeza Bodi na Menejimenti nzima ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) kwa juhudi zao zakurejesha uhai wa Shirika hilo richa ya changamoto wanazo kumbana nazo.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –TAMISEMI), George Simbachawene wakati akipokea taarifa fupi ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) na Shirika la Masoko Kariakoo alipokutana na menejinti ya mashirika hayo leo.

Waziri Simbachawene alisema kuwa amepitia taarifa ya Shirika hilo na kuridhika nayo hivyo hana budi kuipongeza timu nzima ya uongozi kwani kwa muda mfupi imeweza kufanya mabadiliko na kuweza kuliinua tena Shirika hilo.

“Pamoja na kuipongeza bodi hii lakini napenda kuwashauri kuangalia maeneo mengine ya kuwekeza kama kufungua maeneo mengi zaidi ya burudani kwani hilo ndilo lilikuwa lengo la kuanzishwa kwa DDC,ikiwa ni pamoja na kuweka mahali ambapo watoto wataweza kucheza ili kuhakikisha shirika linajiongezea kipato na kuiongezea Serikali kipato pia,” alisema Waziri Simbachawene.

Simbachawene alitumia nafasi hiyo kuwaagiza Wakuu wa Mashirika ya Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanaandaa taarifa nyingine itakayohusisha mali zote za mashirika hayo.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akipokelewa na wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam alipokuwa katika ziara ya kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC).Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam  Sipora Liana na Mstahiki Meya wa Jiji hilo Isaya Mwita.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akizungumza na menejimenti za Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) wakati wa ziara yake katika ofisi za mashirika hayo leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo.
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Sipora Liana akifafanua jambo wa mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (mbele) alipokuwa katika ziara ya kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akisisitiza jambo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo katika Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KUTOKA MAKTABA

0
0
Mwaka 1972, Rais Nyerere aliwaita nyumbani mabalozi wote wa Tanzania waliokuwa nchi za nje kuja kuchukua mafunzo mafupi ya kijeshi kupunguza "nundu" zao baada ya uvamizi wa awali kabisa wa nduli Idi Amin dhidi ya Tanzania. 
Mwishoni mwa mafunzo hayo, mabalozi walipiga picha ya pamoja na wakufunzi wao. Kutoka kushoto walioketi mstari wa mbele: Philip Nhigula, Idris Abdulwakil, Cecil Kallaghe, Ahmed Hassan Diria, mkuu wa mafunzo hayo Gideon Sayore, Chifu Michael Lukumbuzya, Daniel Mloka, Abdalla Sued na Richard Wambura. Mstari wa kati toka kushoto: Anthony Nyaki, Philemon Muro, mkufunzi, Abdul Faraji, mkufunzi, Frederick Rutakyamirwa, mkufunzi, Chifu George Batega Rusimbi na mkufunzi. Mstari wa nyuma toka kushoto: Abbas Kleist Sykes, mkufunzi, Christopher Ngaiza, mkufunzi, Sebastian Chale, wakufunzi wawili, Raphael Lukinda na mkufunzi (Picha kwa hisani kubwa ya Balozi Ngaiza, Rai toleo la Desemba 2001)

Bamiza Music Chart 27th May 2017

The East African Crude Oil Pipelie (EACOP) in a nutshell

IYK-Columbus, Ohio: Karibuni Ibada ya Kiswahili Kusheherekea Miaka Minane 8 ya Ibada ya Kiswahili na Sikukuu za Waliozaliwa Mwezi wa Mei

0
0
IYK Columbus inawakaribisha wote kwenye ibada ya Kiswahili Jumapili hii 5/28 kuanzia saa kumi kamili alasiri(4:00pm). Ibada itafanyika katika kanisa la Ascension. Baada ya ibada kutakuwa na chakula cha jioni cha pamoja kusherehekea miaka 8 ya IYK na wale wote wanaosherehekea siku za kuzaliwa mwezi huu wa tano. Wote tunakaribishwa.

TRA Watoa Somo la Ulipaji Kodi kwa Wafanyabiashara wa Kichina

0
0




Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.   

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa somo la masuala ya kodi kwa wafanyabiashara kutoka China wanaoishi nchini kwa lengo la kuwaongezea uelewa juu ya sheria na taratibu za ulipaji kodi katika semina kuhusu mafunzo hayo leo Jijini Dar es Salaam.

Akiwasilisha mada wakati wa mafunzo hayo, Meneja wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Gabriel Mwangosi amesema kuwa Tanzania ya sasa ina fursa nyingi za uwekezaji hivyo wafanyabiashara hao watakapokuja kuwekeza lazima wafahamu kanuni na taratibu za ulipaji kodi nchini ili waweze kuendana na sheria zilizopangwa na nchini.

“Semina hii mahususi imeandaliwa kwa ajili ya wafanyabiashara wa kichina wanaoishi nchini kupata mafunzo ya kodi zikiwemo za zuio, majengo pamoja na ushuru na forodha ambazo ni lazima wazifahamu kwa manufaa ya Taifa letu na wao pia,”alisema Mwangosi. 
Meneja wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Gabriel Mwangosi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu semina juu ya Kodi, Utaratibu na Sheria kwa wafanyabiashara kutoka China iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na Kampuni ya Jiteng Consultancy Ltd na kufanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
2
Mrakibu wa uhamiaji na Afisa Vibali vya Ukazi, Eliud Ikomba akitoa semina kwa wafanyabiashara kutoka China (hawapo pichani) juu ya sheria za uhamiaji katika semina iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na Kampuni ya Jiteng Consultancy Ltd na kufanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
3
Baadhi ya wafanyabiashara kutoka China wanaofanya biashara zao nchini wakisikiliza mafunzo mbalimbali juu ya Kodi, Utaratibu na Sheria katika semina iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na Kampuni ya Jiteng Consultancy Ltd na kufanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.




CHAMA CHA WAONGOZA WATALII TANZANIA (TTGA) WALIA NA MIUNDO MBINU MIBAYA YA BARABARA NDANI YA HIFADHI

0
0
Na.Vero Ignatus ,Arusha

Chama cha waongoza Watalii nchini Tanzania (TTGA) wameiomba Serikali iwapatie eneo huru kati ya Hifadhi ya Ngorongoro na ile ya Serengeti ,kwani katika eneo hilo la Ndutu katika upande wa Serengeti hakuna barabara za kufanyia mizunguko za kwenda kuangalia wanyama .

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho ndugu Halifa Msangi kwamba changamoto kubwa wanayoipata kama waongoza watalii ,ni kipindi ambacho wanyama pundamilia na Nyumbu wanapohama kuelekea upande mwingine hawawezi kuwapeleka wageni kwenda kuwaona wanyama hao upande wa pili

"Katika eneo la Ndutu wananyama pundamilia na nyumbu huwa wanatabia ya kuhama na kuelemea upande mwingine,sasa unakuta wewe muongozaji ukiwa na kibali cha upande mmoja tu huwezi kuwapeleke wageni mahali wanyama walipo kwani hakuna barabara ya kufanyia mizunguko kwenda kuwaona wanyama jambo ambalo tumekuwa tukipata changamoto kubwa na maswali mengi kutoka kwa wageni tumeizungumzia changamoto hii kwa muda mrefu sasa."alisema Halifa.

Kwa upande wake Katibu wa chama hicho cha waongoza watalii Emanuel Alfayo Mollel amesema kuwa changamoto nyingine kubwa ni barabara zilizopo ndani ya Hifadhi haswa kutoka Ngorongoro kuelekea Serengeti ,barabara hizo zimejazwa vifusi kwa ya km 10 ambavyo havijasambazwa jambo ambalo wakati mwingine vinaweza vikapelekea hata kusababisha ajali pale ambapo dereva anahangaika kuvikwepa.
Chama cha waongoza Watalii wakiwa kwenye banda lao ndani ya viwanja vya magereza katika maonyesho ya Karibu Fair yaliyo beba kauli mbiu isemayao Utalii endelevu kwa Maendeleo.

Wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa chama cha waongoza Watalii Halifa Msangi,Wakwanza kushoto ni Katibu wa umoja huo Emanuel Mollel,Haji Mbuguni Mjumbe wa (TTGA)Omari Rajabu mjumbe,Apolinary Kiwhili M/Msaidizi wakiwa katika maonyesho ya utalii ya 18 ya Karibu Fair 2017Picha na Vero Ignatus Blog.

Wa pili kulia ni mwenyekiti wa Chama cha waongoza Utalii Nchinni Tanzania Halifa Msangi,Wa kwanza kushoto Katibu wa chma hicho Emanuel Mollel,wakiwa na wajumbe wa chama hicho ,pamoja na Hosiana F. Siao.Picha na Vero Ignatus Blog. 

MAGAZETI YA LEO JUMALIPI MAY 28, 2017

MAONESHO YA UCHORAJI WA MWILI YA HABA NA HABA YAVUTIA WATU WENGI

0
0
--
 Msanii wa Sanaa za Ufundi Maarufu kama Ngosha  akimchora mmoja wa wanamitindo katika Tamasha la kuchora mwili lililofanyika katika ukumbi wa Nafasi Art Space jijini Dar es salaam
 Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam walijitokeza katika Tamsha hilo wakishiriki kuchora miili ya wanamitindo hao
 Baadhi ya wanafunzi wa program ya Women Express wakiwa Darasani katika kituo cha Nafasi Art Space wakijufunza namna ya kuchora michoro mbalimbali
  Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam walijitokeza katika Tamsha hilo wakishiriki kuchora miili ya wanamitindo hao
 Mmoja wa wasanii akichora picha ya wanamitindo wa kiume ambao walikuwa wamefikia hatua ya kulala kama sehemu ya onyesho hilo la uchoraji wa mwili
  Mmoja wa wasanii akichora picha ya wanamitindo wa kiume ambao walikuwa wamefikia hatua ya kulala kama sehemu yaonyesho hilo la uchoraji wa mwili
  Msanii wa Sanaa za Ufundi Maharufu kama Ngosha  akimchora mmoja wa wanamitindo wa kike katika Tamasha hilo la uchoraji lililofanyika katika ukumbi wa Nafasi  Art Space
Wanamitindo wa michoro ya mwili wakiwa katika pozi mbalimbali mara baada ya kumalizwa kuchorwa

TECNO YAWAALIKA WADAU WA SIMU HIYO SINEMA

0
0
--
 Afisa uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya  Tecno,, Erick Mkomoye akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika kutazama sinema iliyoandaliwa na kampuni ya Tecno kwa watu wanaotumia simu za kampuni hiyo ambao waliweza kualikwa kufika katika ukumbi Century Cinema Dar Free Market
 Afisa uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya  Tecno,, Erick Mkomoye akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari vilivyofika katika ukumbi huo.
 Balozi wa simu za Tecno nchini Tony Albert (TBWAY) akizungumza na wana habari juu ya uzuri wa simu za Tecno kwa waandishi wa habari
 Afisa huduma kwa wateja Christina Simbano  akikabidhi tiketi kwa mshindi wa kuingia sinema Christiner Christopher
Baadhi ya wadau wa Tecno wakisheherekea  na Selfie ya Tecno Cam C9

WAZIRI MWIJAGE AZINDUA DUKA KUBWA LA VIFAA VYA UJENZI DAR ES SALAAM

0
0
 Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara  na uwekezaji Charles Mwijage(katikati) akiongoza jopo la Viongozi kuzindua duka kubwa la kisasa litakalokuwa linauza vifaa vyote vya  vya ujenzi kwa bei nafuu  lililopo eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam
 aibu Waziri wa Viwanda, Biashara  na uwekezaji Charles Mwijage akikagua sehemu ya bidhaa zilizopo ndani ya duka hilo ambazo zinazalishwa hapa nchini.
 Rais wa umoja wa wafanyabiashara wa china wanaotengeza vifaa vya ujenzi,Thomas Cao akitoa maelezo  kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam jinsi duka hilo lilivyosheheni bidhaa kutoka makampuni mbalimbali hapa nchini
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni  Mstahiki Ben Sitta akiwa na viongozi wa duka hilo katika picha ya pamoja. Picha zaidi BOFYA HAPA



Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha azindua Wiki ya Unywaji maziwa Kitaifa

0
0
Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha akisaidiwa na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kagera  akikata utepe kuashiria Kuanza kwa Wiki ya Unywaji maziwa Kitaifa. Maadhimisho haya yanafanyika katika viwanja vya Kyakairabwa, Manispaa ya Bukoba. 


Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha akizungumza na mfugaji wa ng'ombe wa kisasa kutokea wilayani Misenyi Bi Haulath Athumani Mfugaji 

Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha  akipata maelezo katika Banda la NARCO
 Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nashaakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wawakilishi Shirika la Maendeleo ya Wakulima (MAYAWA). Picha na Abdullatif Yunus

HABA NA HABA DANCE FESTIVAL ILIVYOBAMBA KATIKA UKUMBI WA NAFASI ARTS SPACE, DAR ES SALAAM

0
0
 Wasanii wa mchezo wa jukwaani kutoka kundi la Haba na haba wakitumbuiza mchezo uliokwenda kwa jina la There is no Future Word for in Swahili?
 Wasanii wa mchezo wa jukwaani kutoka kundi la Haba na haba wakitumbuiza mchezo uliokwenda kwa jina la There is no Feture Word for Fiture in Swahili?
 Wasanii wa kundi la Nantea Dance Company  Tanzania wakionyesh mchezo wao jukwaani
 Wasanii wa kundi la Haba na haba wakionyesha mchezo wa WD Forest Tanzania katika Tamasha la Haba na Haba
watu mbalimbali wakijumuika katika kucheza ngoma za asili katika Tamasha la Haba na haba. Picha zote na Humphrey Shayo

yale yaleeeeeeee......

0
0
Mkaazi wa jiji la Dar es Salaam akiwa  juu ya mzigo uliobebwa na Baiskeli ya magurudumu matatu (Guta) akitokea katika soko la Mabibo  kuelekea mtaani kama alivyokutwa katika barabara ya Mandela jijini Dar es Salaam leo hasubuhi,  jambo ambalo ni hatari kwa usalama wake 
Picha na Humphrey Shao wa Globu ya Jamii

MKUU WA WILAYA YA MBOGWE AONGOZA ZOEZI LA USAFI WA MAZINGIRA.

0
0

Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mh Martha Mkupasi ameongoza wakazi wa Mbogwe kwenye Zoezi la Usafi wa Mazingira kwa kufanya usafi eneo la Kituo cha Afya Masumbwe na maeneo yanayozunguka kituo hicho.

Akiongea na wananchi baada ya zoezi la usafi, mh Mkupasi amewataka wananchi kujijengea tabia ya kufanya usafi wa mazingira yanayowazunguka kila siku na wasisubiri mwisho wa mwezi kwani kwa kupenda usafi itawasaidia kujiepusha na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu. Pia amewasisitiza wananchi kutunza mazingira na kuepuka kukata miti ovyo badala yake wapande miti ya kutosha .

Pamoja na hayo mh Mkupasi aliongea na Vijana wa Kikundi cha Scout walioungana na wananchi kwenye zoezi la usafi , nakuwahimiza kupenda masomo yao ya kila siku na kuweka bidii kwani bila elimu hawezi kutimiza ndoto zao .

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya, Afisa Mazingira wa Wilaya Charles Karibu Tuyi aliwashukuru wananchi na kikundi cha scouti kwa kujitolea kuja kufanya usafi wa mazingira kwenye kituo cha afya Masumbwe na kuwahimiza kuendelea kusafisha mazingira wanayoishi na kuwataka waepuke kutupa uchafu kwenye mitaro kwani utupaji wa taka ngumu unaweza kuziba mitaro na kusababisha mafuriko .

TANZIA TANZANIA

0
0
TANZIA.
Familia ya Marehemu Mh. Samuel Sitta,inawatangazia Ndugu,jamaa,na Marafiki imepata Pigo la kuondokewa na Mdogo wa Marehemu Mh.Samuel Sitta, ambaye alikuwa Meya wa mji mdogo wa Urambo Ndg.Peter Sitta ambaye amefariki Usiku wa Leo jumamos trh 27/5 katika hospital ya Hindu Mandal..Msiba upo Masaki Nyumbani kwa Hayati Samuel Sitta Mtaa wa Twiga , Karibu na Makao makuu ya UNHCR .
Bwana ametoa, Bwana ametwaa Jina lake lihidiwe.

TIMU YA WATAALAM YAAGIZA KUANDA RIPOTI YA KUMALIZA MGOGORO WA BWAWA LA ULUWA WILAYANI SIKONGE.

0
0

Na Tiganya Vincent, Sikonge 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ameteua timu ya Maafisa watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kwa ajili ya kuandaa taarifa(ripoti) itakayowasilishwa kwake Jumatano(wiki inayoanza kesho) ili imwezeshe kutoa maamuzi yatakaondoa kuondoa mgogoro uliosababisha ujenzi Mradi wa Bwawa la Umwagiliaji la Uluwa ushindwe kuendelea kwa sababu ya maji yake kuelekezwa katika Msitu wa Hifadhi wa Ipembampazi. 

Hatua hiyo itasaidia kuokoa zaidi ya shilingi milioni 313 ambazo hadi hivi sasa zimeshatumika katika ujenzi wa mradi huo ambao ni kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji wa mpunga katika vijiji viwili vya Mtakuja na Kiloleni kama mradi utaendelea. Profesa Maghembe alichukua uamuzi huyo jana wilayani Sikonge baada ya kutembelea Mradi huo huku akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri ili kujionea hatua ulipokuwa umefikia na hiyo mifereji ilijengwa kuelekea katika Msitu wa Hifadhi. 

Alistaja wataalam hao kuwa ni Ofisa wa Maliasili, Misitu, Kilimo na Mhandisi wa Maji, Mhandishi wa Ujenzi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mteandaji wa Halmashauri ya Sikonge ambao aliwapa jukumu la kuandaa taarifa itakayoonyesha mambo mbalimbali ikiwemo kupima na kuonyesha kiasi cha eneo ambalo wananchi wanalohitaji kwa ajili ya kilimo hicho na eneo lilobaki katika Msitu huo wa Hifadhi. 

Profesa Maghembe aliwaambia kuwa uharaka na ubora wa ripoti ya Halmashauri ndio utakaoisaidi Wizara ya Maliasili na Utalii kufikia maamuzi haraka ambayo baada ya wataalam wake kuipitia atawalisha mapendekezo na hatua waliofikia kwa Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya hatua zaidi. 

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe
 

RAIS DKT. MAGUFULI AWAJULIA HALI WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Mzee Francis Maige Kanyasu(Ngosha) aliyelazwa Wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa ajili ya Matibabu leo. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru pamoja na Dkt. Juma Mfinanga Daktari Bingwa wa magonjwa ya Dharura na Ajali katika hospitali hiyo.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali mtoto Shukuru Kisonga aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mtoto Shukuru alikuwa akidaiwa kuishi kwa kula Sukari, Maziwa na mafuta ya kula lakini hali yake imeimarika zaidi na kuanza kula vyakula vya kawaida. Katikakati ni Mama yake Shukuru Mwanahabibi Mohamed Mtei.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Angalia video hapo chini

Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images