Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1709 | 1710 | (Page 1711) | 1712 | 1713 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitoa risala ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla na kuwatakia kheri katika mwezi huo,pia amewataka kujitahidi kufanya ibada kwa wingi,ikiwemo kusima Quran,kuswali sana hasa swala za Suna na kutoa zaka.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Chama cha Wafanyabiashara wa Pikipiki na Vipuri  vyake pamoja na baadhi ya wabunge, ofisini kwake, Bungeni mjini Dodoma Mei 26, 2017. Kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Philip Mpango. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbulu  Vijijini, Fratei Massay kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 26, 2017. Wapili kulia ni Mbunge wa Iramba Mashariki, Allan Kiula. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Wabunge wa Viti Maalum, Amina Makiragi na Anna Lupembe kwenye jengo la utawala la Bunge mjini Dodoma Mei 26, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wa Chuo Kikuu cha Makumira kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 26, 2017. Kushoto ni  Mbunge wa Newala Mjini, Capt. George Mkuchika. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Na Tiganya Vincent

  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri amesema wachimbaji wadogo wadogo waliofichua maovu yanayofanywa na Watendaji wa Ofisi ya Madini kwa kushirikiana na Kampuni zilizopewa leseni za kuchimba madini katika eneo la Kitunda wilayani Sikonge wasiwe na wasiwasi kwani Serikali itawashika mkono ili wasidhurike.

  Bw. Mwanri alitoa kauli hiyo jana katika eneo la Kitunda wilayani Sikonge kwenye Mkutano wa hadhara uliowahusisha wachimbaji wadogo wadogo , Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Wilaya ya Sikonge na viongozi wa Kampuni zenye leseni ya uchimbaji wa madini kufuatia malalamiko kuwa wachimbaji hao wanaosema ukweli wamekuwa wakipata vitisho kutoka kwa wamiliki wa migodi na baadhi ya watendaji.

  Alisema kuwa wamesema ukweli na kufichua maovu yanayoendelea katika eneo la machimbo hayo, Serikali inawahakikishia ulinzi wa kuhakikisha kuwa hakuna mtu yoyote atayenyanyaswa kwa kufichua uovu unafanywa na Kampuni za Uchimbaji Madini katika eneo hilo.

  Mkuu huyo wa Mkoa alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Sikonge washirikiane na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Sikonge kuhakikisha kuwa vijana wote walieleza uovu wa watendaji wa Ofisi ya Madini ya Mkoa kwa kushirikiana na Kampuni za madini wanakuwa salama na kuendelea na kazi zao.

  Alisema kuwa kiongozi yoyote awe wa Serikali au Kampuni ya Madini asijaribu kuwagusa vijana wote walioeleza matatizo mbalimbali yanayowakabili vingine atakayewagusa atakuwa anakosa sifa za kuendelea kuwa mtumishi wa umma au kuendelea na kazi zake za uchimbaji madini.

  Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa Serikali hii iko makini inataka kila mtu au Kampuni itekeleza wajibu wake kama ni kulipa kodi za Serikali ilipe na sio kuendesha shughuli zake kiujanjanja tu na hivyo kuikosesha Serikali mapato.
  0 0


    KAMPUNI inayojishughulisha na uuzaji wa Vilainishi Duniani ( SINOPEC) imefanya Semina ya kuwaelimisha na kuwafundisha wateja wake mbalimbali namna ya kutumia ,kwa lengo la kulinda na kutunza Mazingira.

  Akizungumza hayo mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,Mkurugenzi mtendaji wa SINOPEC amesema kuwa,wameamua kuwekeza nchini Tanzania kutokana na Serikali ya awamu ya Tano,kupunguza vikwazo kwa wawekezaji kama ilivyokuwa awamu zilizopita.

  " Kwa Afrika tumeanza kutoa Semina nchini Tanzania, yote hiyo imetokana na mazingira ya uwekezaji kuwa rafiki,hali nzuri ya Usalama pamoja na urafiki wetu wa muda mrefu na Tanzania" alisema Wang

  Amesema kutokana kuweko kwa mazingira rafiki na wezeshi ya uwekazaji,wanaamini kampuni yake itajitanua zaidi kibiashara katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania,ikiwa sambamba na kuhakikisha serikali inajipatia mapato stahiki kwa kulipa kodi .

  Mkurugenzi huyo amewaomba Watanzania kwa ujumla wao kuvitumia vilainishi hivyo vyenye ubora wa Kimataifa,katika mitambo yao,mashine mbalimbali,magari na vifaa vinginevyo vinavyohitaji kutumia vilainishi.

  Kwa upande wake Meneja Masoko wa kampuni hiyo ya SINOPEC, Jafali Mswahili amesema wateja wote pamoja na mainjinia watakuwa na utaratibu wa kupewa elimu ili kuwahikikishia wateja wao wanapata na kutumia vilainishi vilivyo bora zaidi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya SINOPEC, Andy Wang akionesha baadhi ya bidhaa kwa waandishi wa habari.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima (wa kwanza kulia), akimkabidhi zawadi Afisa Mambo ya Nje, Bi. Eva Ng'itu kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa. Bi. Ng'itu amekuwa Mfanyakazi Hodari wa Wizara ya Mambo ya Nje kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. Dkt. Mlima aliwapongeza na kuwasihi wafanyakazi waliofanya vizuri kuwa zawadi walizokabidhiwa iwe chachu ya kuongeza juhudi na ufanisi katika utumishi wao. 
  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akimpongeza Bi. Ng'itu kwa kuwa mfanyakazi Hodari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
  Bw. Mohammed Kheri kutoka Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar akipokea zawadi yake kwa kuwa mfanyakazi bora wa Idara hiyo. 
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora na Mratibu wa Mafunzo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Tagie Daisy Mwakawago naye akipokea zawadi ya ufanyakazi bora wa Idara ya Diaspora 


  0 0


  Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

   Mtafiti wa masuala ya Uchumi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam  Dkt.Haji Semboja anasema kuwa amefurahishwa na ripoti ya Kamati Maalum iliyoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  John Pombe Magufuli  ya  kuchunguza mchanga wa madini kwenye makontena 277 yaliyozuiwa na serikali kusafirishwa kwenda nje kwaajili ya uchenjuaji.

  Akizungumza Jijini Dar es Salaam  katika mahojiano na mwandishi wa habari hii, Dkt.Semboja alisema kuwa, hatua hiyo ni nzuri na ya kuridhisha  kwa vile Rais Magufuli amefanyia kazi suala hilo ambalo limekua likizungumzwa kwa muda mrefu na baadhi ya wasomi,wanaharakati na hata wanasiasa hapa nchini.

  “Mimi ni kati ya Watanzania waliofurahishwa na maamuzi ya Rais, nina furaha kubwa hasa ukizingatia niliwahi kushiriki katika uandaaji wa sera za madini na uwekezaji, na ni wazi kuwa tumekuwa tukiibiwa kwa kiwango kikubwa katika sekta ya madini” alisema  Dkt.Semboja.

  Malalamiko haya  ya wizi na utoroshaji wa madini yamekuwepo kwa muda mrefu,  kitu ambacho tulikua tukizungumza    sasa  kimethibitishwa , baada ya Rais Magufuli  kupokea ripoti hiyo ya mchanga”, aliongeza Dkt.Semboja.

  Aidha, Dkt.Semboja amemshauri  Rais Magufuli  kuendelea kuwatumia wataalamu mbalimbali waliopo nchini na kuiomba Serikali iwe na utaratibu wa kuwatumia watu wake ambao wengi ni wazalendo na wana uchungu na nchi yao.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  Rais Dkt John Pombe Magufuli

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kulia akimkabidhi vitanda moja kati ya 25 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani,Sabas Chambasi ambavyo ni miongoni mwa mgao wa vifaa tiba walivyopewa na Rais John Magufuli kwa ajili ya wilaya ya Pangani kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Issa
  Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kulia akimkabidhi Mgao wa mashuka 50 kutoka kwa Rais John Magufuli Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani,Sabas Chambasi kwa ajili ya kusaidia huduma za afya kwenye wilaya ya Pangani katika halfa iliyofanyika kwenye hospitali ya wilaya ya Pangani juzi wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Issa 
  Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kushoto akiwa ameambatana na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa wakitembelea hospitali ya wilaya ya Pangani kabla ya kukabidhi Msaada wa vifaa tiba ambavyo vimetolewa na Rais John Magufuli
  Mganga Mkuu wa wilaya ya Pangani,Dkt Juma Mfanga kulia akimueleza Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Changamoto zinazowakabili wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba ambavyo vimetolewa na Rais John Magufuli kwa Mbunge huyo kwa ajili ya wilaya ya Pangani ambayo ni mashuka 50 na vitanda 25


  0 0

  Benki ya Dunia kupitia washirika wake wa Maendeleo imeamini ya kuridhika na hatua kubwa iliyochukuliwa na Jamii ya Wananchi wa Visiwa vya Zanzibar katika kusimamia miradi yao kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania{TASAF} Awamu ya Tatu katika kujiondolea Umaskini.


  Viongozi wa Ujumbe wa Washirika hao wa Maendeleo ulitoa kauli hiyo wakati ukitoa tathmini ndogo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua miradi ya Jamii inayotekelezwa kupitia Tasaf Tatu katika maeneo mbali mbali ya Mjini na Vijijini Unguja na Pemba.

  Kiongozi wa Ujumbe huo kutoka Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdulah alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba ziara ya Ujumbe wake imeshuhudia maendeleo makubwa yaliyopatikana katika Jamii kutokana na kundi kubwa la Wananchi lilivyoamua kutekeleza kwa ufanisi mkubwa miradi yao waliyoianzisha. 

  Bwana Moderes alisema Zanzibar imeonyesha mfano bora katika uendelezaji wa miradi ya Maendeleo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF} awamu ya Tatu kiasi kwamba Uongozi wa Benki ya Dunia kupitia Washirika wake imefurahia hatua hiyo ya mafanikio.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdula aliyeuongoza Ujumbe wa Washirika wa Maendeleo ulikuwepo Zanzibar kwa siku Nne kukagua miradi ya Tasaf Awamu ya Tatu. Kati kati yao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania Bwana Ladislas Mwamanga.
  Balozi Seif akizungumza na Ujumbe wa Benki ya Dunia ulioambatana na washirika wa Maendeleo hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar uliofika kukagua miradi ya Tasaf.
  Balozi Seif kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Viongozi wa Benki ya Dunia na washirika wake wa maendeleo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.  Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma Nhunga, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Nd. Joseph Abdulla Meza na Bibi Azzah Ammin kutoka Shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA).  Kushoto ya Balozi Seif ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Jamii Tanzania (TASAF) Nd. Ladislas Mwamanga, Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bwana Moderes Abdula na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim Haji.


  0 0


  Na Fatma Salum (MAELEZO)

  Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) imeanzisha mfumo mpya wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement System) kutoka nje ya nchi utakaosaidia kupunguza bei na kuhamasisha matumizi ya mbolea kwa wakulima.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Lazaro Kitandu alisema uamuzi huo wa kuanzisha mfumo mpya umekuja baada ya Serikali kugundua kuwa kwa muda mrefu matumizi ya mbolea hapa nchini si ya kuridhisha kutokana na bei ya mbolea kuwa juu.

  “Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wadau wa masuala ya mbolea imeanzisha mfumo huu baada kupitia tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalam waelekezi wa ndani na nje ya nchi na kutumia uzoefu wa taasisi nyingine zinazofanya ununuzi wa bidhaa kwa pamoja” Alisema Kitandu.

  Kitandu alieleza kuwa katika nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SSA), Tanzania ni mojawapo ya nchi zenye matumizi ya chini ya mbolea kwa kutumia kilo 19 za virutubisho hivyo kwa hekta katika ngazi ya wakulima wadogo ambapo kiasi hicho hakiendani na malengo ya azimio la Maputo la nchi za SADC linalotaka kufikia angalau kilo 50 kwa hekta moja.
  Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Bw. Lazaro Kitandu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mfumo mpya wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement System). Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Bw. Richard Kasuga. Picha na Fatma Salum- MAELEZO   0 0

  Wasanii wa kizazi kipya Fid Q, Snura, Madee, Dogo Njaja, Stamina na Navy Konzo wanatarajia kutoa burundani katika matamasha ya Taifa Moja ambayo yatafanyika kesho (Jumamosi) kwenye mikoa mine tofauti hapa nchi.
  Burandani hio itaenda sambasamba na kutoa elimu kwa Wananchi wa mikoa husika juu ya uhuru wa kutuma pesa bila mipaka ambayo ni ushirikiano wa makampuni matatu ya simu za mkononi kupitiia huduma zao Tigo Pesa, Airtel Money na Ezy Pesa.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Liginiku Milinga ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Fern Tanzania ambao ndio waratibu na waandaaji wa matamasha hayo alisema wasanii wote washathibitisha kushiriki kwao kwenye matamasha hayo na kwamba maandalizi yote yamekamilika huku akiwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kupata burundani toka kwa wasanii wakali hapa nchini na pia kupata elimu juu ya kutuma na kupokea pesa kwenda mtandao wowote hapa Tanzania kwa gharama ile ile.

  Wasanii Stamina na Fid Q watambuiza kwenye tamasha litakalofanyika kwenye uwanja wa Mwembetongwa mjini Iringa wakati Dogo janja na Baba Levo wakifanya ya kwao kwenye uwanja wa Community Center grounds uliopo mjini Kigoma huku Snura na Madee wakiwashika vilivyo wakazi wa mji wa Tanga kwenye uwanja wa Tangamano. Navy Kenzo huku akitamba na wimbo wake wa kamati ya chini, atakuwa kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Sabasaba iliyopo mjini Morogoro.


   

  Tangu tuanze kampeni yetu ya Taifa Moja tumekuwa tukitumia wasanii wetu kutoa elimu kwe Wananchi kupitia burudani na tumetapata mafanikio makubwa sana ya kufikisha ujumbe wetu wa uhuru wa kutuma pesa bila mipaka kupitia burudani kwa Watanzani. 

  Naomba nitoe wito wangu kuwaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi kesho kushuhudia wasanii wetu ambao wamehaidi kutoa burundani ya uhakika.

  Bali na kupata burundani, Watanzania wataweza kufahamu jinsi ya kujikwamua kiuchumi kwani kwa njia ya kutuma pesa kwenda mtandao wowote ule kwa gharama ile ile imetoa urahisi kwa kuongeza watumiaji wengi wa huduma ya kutuma pesa na hivyo kuwa rahisi Wananchi kupata huduma za kifedha.


  Taifa Moja ni kampeini ambayo imedhaminiwa na taasisi za Financial Sector Deepening Trust of Tanzania (FSDT) pamoja na Bill & Melinda Gates Foundation huku ikiratibiwa na International Finance Corporation (IFC) chini ya muungano ya makampuni matatu ya simu za mkononi za Airtel Tanzania, Tigo Tanzania na Zantel kupitia huduma zao za Airtel Money, Tigo Pesa na Ezy Pesa. 

  0 0

  Na Lorietha Laurence-WHUSM.

  Dhana ya kuwekeza katika sekta ya michezo kwa vijana wadogo wa shule za Sekondari imekua ikileta manufaa makubwa kwa Taifa katika kuzalisha wachezaji mahiri ambao wamekua wakipeperusha bendera ya Tanzania ndani na nje ya chini.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe alipokua akifungua michezo ya COPA UMISSETA ambayo inashirikisha shule za Sekondari za Serikali na Binafsi leo katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

  “Nimefurahishwa na juhudi zinazofanywa na Kampuni ya CocaCola katika kuhakikisha tunaimarisha sekta ya michezo kwa vijana wadogo wa sekondari kwani kwa kufanya hivyo tunaibua vipaji na kuviendeleza kwa  kupata  wanamichezo mahiri wa baadaye” amesema Waziri Mwakyembe.

  Aidha aliongeza kuwa Serikali itahakikisha kuwa inawekeza katika michezo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa kuwa michezo ni ajira inayowapatia vijana riziki pamoja na kuchangia katika uchumi wa nchi.

  Vilevile aliwataka walimu kufuata ratiba za vipindi vya michezo kwa kuhamasisha michezo mashuleni ikiwemo kuwapatia wanafunzi nafasi ya kujifunza na sio kuvitumia vipindi hivyo kwa shughuli nyingine.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akiimba wimbo wa Taifa wakati wa kufungua mashindano ya COPA UMISSETA uliofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yussuph Singo na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya CocaCola Eric Ongara na anayefuatia ni Rais wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) Bw.Vitalus Shija.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akiongea na wanafunzi wa shule za Sekondari za Jijini Dar es Salaam wakati wa kufungua kwa mashindano ya COPA UMISSETA katika uwanja wa mpira wa Taifa.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia) akisalimiana na washiriki wa michezo ya COPA UMISSETA inayoshirikisha shule za Sekondari za Serikali na Binafsi iliyofunguliwa leo Jijini Dar es Salaam.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini , Dk. Juliana Palangyo amewaagiza wahandisi wa Shirika la umeme nchini Tanesco na Wakala wa barabara nchini Tanroads kufanya nguvu kwa pamoja ili kuweka alama za miundombinu ya mradi wa kuboresha umeme wa Dar es Salaam itapita katika barabara ya Mandela mpaka kurasini.

  Dk .Palangyo amesema hayo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akikagua sehemu ya miundombinu hiyo itakayopita kwa kushirikiana na Tanroads .

  “Tanesco wamekubaliana na Wakala wa Barabara nchini kupitisha sehemu ya miundombinu ya umeme kando kando mwa barabra ya Mandela hili kuweza kuongeza nguvu katika kituo cha kurasini na mkoa mzima wa Dar es Salaam.Makabuliano haya yamefikiwa leo mara baada ya mimi kutembelea katika ofsi za Tanroads na sehemu ambapo miundombinu hiyo itatakiwa kupita”.

  Dkt. Palangyo amesema kuwa wameamua kufanya mazungumzo na Tanroads hili kufikia muafaka kwakuwa wao nao walitaka kutumia eneo hilo katika moja ya miradi yao hivyo kufikia muafaka wa hili kumewezesha mradi wa tanesco kwenda kwa kasi zaidi ya awali.

  0 0

  Kampuni ya simu ya Mkononi ya itel imemtambulisha Msanii Bongo Movis, Irene Uwoya kuwa Balozi wa kampuni hiyo hapa nchini.

  Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Irene amesema amejisikia faraja kuwa balozi na kuahidi kuitendea kazi katika kutangaza kampuni hiyo kupitia bidhaa zao za simu.

  Amesema kuwa amekuwa akifanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja na kuweza kufanya makubaliano ya kuwa balozi katika kuunganisha itel na watanzania  kwa ujumla.

  Kwa upande  Mkurugenzi wa itel, Coopeer Chan amesema kuwa wanatarajia  jamii itafaidika kwa kupata elimu kuhusu bidhaa za kampuni hiyo kupitia kwa balozi Irene Uwoya katika matukio ya kuonyesha ukarimu kwa baadhi ya makundi kwa utoaji wa misaada.

  Amesema kuwa wanamkaribisha balozi mpya itel Tanzania Irene Uwoya kuungana na familia ya kubwa ya itel.

  "Sote tunafahamu mchango wa Irene Uwoya kwenye jamii amekuwa akielimisha kupitia filamu zake na kutambua umuhimu wake sisi itel Mobile tutashirikiana naye kikamilifu kuhakikisha jamii inapata kile inachotarajia kukipata kwetu na kwake pia" amesema Chan.
   Mkuruegenzi wa itel, Coopeer Chan akisaini makubaliano  na Msanii Bongo Movis, Irene Uwoya kuwa balozi wa kampuni hiyo leo katika ukumbi wa Hoteli ya Hyaat Legency  jijini Dar es Salaam.
   Msanii Bongo Movis ,Irene Uwoya akizungumza na waandishi wa habari juu kuwa balozi wa Kampuni ya Simu ya Mkononi leo jijini Dar es Salaam.
   Mkuruegenzi wa itel , Coopeer Chan akibadilishana hati ya makubaliano  na Msanii Bongo Movis ,Irene Uwoya kuwa balozi wa kampuni hiyo leo katika ukumbi wa Hoteli ya Hyaat Legency  jijini Dar es Salaam.
  Msanii Bongo Movis ,Irene Uwoya akiwa katika picha ya pamoja wafanyakazi itel leo jijini Dar es  Salaam.

  0 0

  Timu nzima ya MMG chini yake Ankal Issa Michuzi, inawatakia mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ndugu wote katika Imaan ya Dini ya Kiislam, Duniani kote. Hiki ni kipindi muhimu sana kwa waislam wote katika Ibada ya Toba, hivyo tujitahidi kuhimizana kufanya ibada na kumcha Allah Sub Hannahu Wataala. 

  Amin


  Ramadhan Kareem.

  0 0
  0 0  0 0  0 0


  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi aahidi ongezeko la Upimaji wa Ardhi Nchini baada ya kuwasilisha bajeti ya Wizara - Bungeni. 
  Akitoa ufafanuzi kuhusu kupatikana kwa vifaa zaidi vya upimaji, baada ya hoja za wabunge; Mhe. Lukuvi amesema Wizara imejipanga kutoa mafunzo kwa wapima wa Ardhi nchini na hivyo kasi ya upimaji itaongezeka nchini kwani vifaa hivyo vya aina ya RTK vina uwezo wa kupima ekari elfu 30 kwa wakati mmoja. Alisema, vifaa hivyo vitatolewa kwa Halmashauri nchini bila gharama. Aliongeza kuwa Serikali itanufaika kwa kupata ongezeko la mapato ya Kodi ya Pango la Ardhi zaidi. 
  Aidha, katika mwaka wa fedha 2016/17, Serikali iliahidi kuidhinisha ramani za Upimaji zenye viwanja 200,000 na mashamba 400. Hadi kufikia 15 Mei, 2017; ramani za upimaji zenye jumla ya viwanja 118,502 na mashamba 374 ziliidhinishwa. Katika mwaka wa fedha 2017/18 Wizara itaidhinisha ramani za upimaji zenye jumla ya viwanja 200,000 na mashamba 400.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Naibu wake; Angeline Mabula wakiwa na watendaji wa Wizara na Taasisi katika picha ya pamojabaada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi. 

   Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akipongezwa na baadhi ya Watendaji wa Wizara baada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi. 

   Waziri wa ardhi; Mhe. William Lukuvi na viongozi wakuu wa Wizara; Naibu wake; Angeline Mabula, Katibu Mkuu; Dkt. Yamungu Kayandabila na Naibu Katibu Mkuu; Dkt. Moses Kusiluka wakijadili jambo nje ya ukumbi wa bunge, baada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi.

   Waziri wa ardhi; Mhe. William Lukuvi wakifurahia na watendaji wa Wizara na Taasisi baada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi.

  Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini; Edwin Ngonyani akipata maelezo ya matumizi ya vifaa vya upimaji Ardhi vya kampuni ya Surveying Equipment Service Centre (EA) LTD/ SESC (EA) LTD katika eneo la bunge baada tu ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi.

   Na kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

  0 0

  Baadhi ya wauguzi na madaktari wakimpandisha kwenye ambulance Mtoto Antonia kwa ajili ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imemsafirisha mtoto, Antonia Justine Msoka anayeongezeka uzito kwenda India kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

  Mtoto Antonia mwenye umri wa miaka 17 alikuwa amelazwa Muhimbili tangu Novemba mwaka jana na kuanza kupatiwa matibabu.

  Akizungumzia afya yake, Antonia amesema kuwa afya yake inaendelea vizuri na amewashukuru madaktari na wauguzi wa Muhimbili kwa kumpatia matibabu.

  “Nashukuru kwa msaada kwani sasa naenda Hospitali ya India kwa matibabu zaidi, naishukuru pia serikali kwa kunisadia,” amesema mtoto Antonia.

  Awali Antonia alifikishwa Muhimbili akiwa na uzito wa Kilo 250, lakini sasa zimepungua na kufikia kilo 230.

  Mama wa mtoto huyo, Salome Manyirizu Kisusi ameishukuru wizara hiyo kwa msaada fedha za matibabu na kumsafirisha kwenda India kwa ajili ya matibabu zaidi.

  “Nawashukuru watu waliokuwa wakiniombea na pia wote walionichangia fedha za matumizi, Mungu awabariki. Pia, nawashukuru madaktari, wauguzi na uongozi wa Muhimbili kwa ushirikiano mzuri walionipatia,” amesema Mama Salome.
  Mtoto Antonia akiwa amepumzika kwenye gari ya kubebea wagonjwa leo kabla ya kupanda ndege kuelekea India.


older | 1 | .... | 1709 | 1710 | (Page 1711) | 1712 | 1713 | .... | 3272 | newer