Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1708 | 1709 | (Page 1710) | 1711 | 1712 | .... | 3278 | newer

  0 0


  0 0  0 0  0 0

  MSHINDI wa droo ya nane ya Bahati Nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’, Daniel Mwakaboko, jana amepokea fedha zake jumla ya Sh Milioni 10, huku akisema kuwa zawadi aliyoshinda kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko itamkomboa kiuchumi na kumuondoa kwenye hatari ya umasikini inayowakumba vijana wengi.

  Akizungumza jana katika makabidhiano ya fedha zake, Mwakaboko alisema kwamba zawadi ya fedha taslimu Sh Milioni 10 ni nyingi kwa wakati huu anaposaka maisha bora kwa kutafuta mtaji mara kadhaa bila mafanikio.
  Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven kulia akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 10 mshindi wa droo ya nane ya Biko, Daniel Dancan Mwakaboko aliyetangwa Jumatano ambapo jana alikabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam.
  Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven kulia akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 10 mshindi wa droo ya nane ya Biko, Daniel Dancan Mwakaboko aliyetangwa Jumatano ambapo jana alikabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Kushoto ni afisa wa NMB aliyesimamia zoezi la kuingiza fedha hizo katika akaunti ya mshindi huyo wa Milioni 10 na Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko Grace Kaijage.

  Alisema kwa sasa anafanya kazi ya kuchapisha majarida na vitu tofauti tofauti vya kiofisi katika ofisi ya mtu mwingine, hivyo ni wakati wake wa kuangalia namna gani atazitumia vizuri fedha za ushindi alizokabidhiwa baada ya kuibuka na ushindi kartika droo ya nane ya Biko iliyochezeshwa Jumatano.

  “Biko ni mchezo mzuri usiochosha na unaoweza kumpa kila mmoja wake ushindi kwa sababu hata uchezaji wake wa kuweka muamala kwa simu za Tigo Pesa, MPESA na Airtel Money kwa kuanzia Sh 1000 na kuendelea ni rahisi maana unachotakiwa ni kuingiza namba ya kampuni 505050 na kumbukumbu 2456 tayari kusubiri zawadi ya papo kwa hapo au droo kubwa ya Sh Milioni 10.

  “Nina ndoto ya kufanikiwa kiuchumi lakini pia sitahasahau kiwanja maana vitu vyote hivi vilikuwa vikisisumbua kwa siku nyingi na nadhani Mungu amejibu maombi yangu maana hapo kabla hali yangu ilikuwa ngumu,” Alisema Mwakaboko mkazi wa Tabata na mwenye asili ya mkoani Mbeya.

  Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba kampuni yao imejipanga ipasavyo kuhakikisha kwamba kila mtu anavuna mamilioni ya Biko kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni Moja ambayo hulipwa papo kwa hapo dakika chache baada ya mshindi kupatikana.

  “Nawaomba Watanzania wote bila kuangalia unapatikana eneo gani la Tanzania kucheza Biko mara nyingi zaidi ili kujiwekea mazingira mazuri ya ushindi na kupata suluhu ya changamoto za kimaisha kwa kupitia mchezo wa Biko maarufu kama Nguvu ya Buku,” Alisema Heaven.

  Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema kwamba njia ya ushindi ni kucheza mara nyingi zaidi ambapo pindi mtu anaposhinda hupewa zawadi yake kwa haraka, ambapo mpaka sasa zaidi ya wateja 32000 wamepatikana na jumla ya Sh Milioni 80 zimelipwa kwa washindi nane tu.

  “Mpaka sasa tumefanya droo kubwa za kuwania Sh Milioni 10 nane na tayari wateja wameshapewa stahiki zao hivyo kuifanya Biko kutoa Sh Milioni 80 kwa washindi wake nane ukiacha wale wanaolipwa papo kwa hapo ambao ndio wengi na wanatoka kila mikoa ya Tanzania,” Alisema.

  Droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 10 inayochezeshwa na Biko inafanyika mara mbili kwa wiki ambapo ni Jumatano na Jumapili, huku mshindi wa zawadi za papo kwa hapo akipatikana kila baada ya dakika chache.

  0 0

  Na Shamimu Nyaki - WHUSM

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameipongeza timu ya vijana chini ya miaka 17 “Serengeti Boys” kwa hatua nzuri waliyofikia katika kiwango cha Soka la Afrika kwa kushika nafasi ya pili katika kundi B walilokuwa wanacheza wakati wa michuano ya AFCON iliyomaliziki hivi karibuni Mjini Gabon.

  Pongezi hizo zimetolewa jana Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuipokea timu hiyo katika viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Mwalimu Nyerere ambapo Waziri Mwakyembe aliwataka walimu na wachezaji hao kuendelea kujiandaa kwa ajili ya mashindano mengine yaliyo mbele yao.

  “Nimefurahi kwa hatua mliyoifikia na watanzani wote wanawapongeza kwa kuwa mmeshindana kwa uwezo wenu na kuirudisha Tanzania katika ramani ya soka baada ya kukaa nje ya michezo ya AFCON kwa takribani miaka 30 alisema” Mhe Mwakyembe.

  Aidha aliongeza kuwa hapo walipofika wao ni mashujaa na Serikali inaahidi kushirikiana nao katika kuhakikisha kuwa vipaji hivyo vinaendelezwa kwa ajili ya ngazi nyingine za kisoka.

  Naye Kocha wa Serengeti Boys Kim Paulsen ameiomba Serikali na wadau wa michezo nchini kuendelea kuisadia timu hiyo katika maandalizi mbalimbali ili kuipa motisha zaidi katika kufanikisha ndoto ya Tanzania katika mchezo wa soka.

  Kwa upande wake kapteni wa timu ya Serengeti Boys Bw. Dickson Job amewashukuru watanzania kwa mchango mkubwa walioutoa kwao katika maandalizi mpaka hapo walipofikia ingawa hawakufanikiwa kurudi na ushindi.

  “Mchezo una matokeo matatu kushinda, kushindwa au kutoka sare ingawa hatukutarajia kushindwa kwa kuwa tulitamani sana kurudi na ushindi kama ambavyo tuliwaahidi watanzania ila mwaka huu bahati haikuwa yetu ila tunaahidi kuendeleza mapambano katika hatua zijazo” alisema Bw. Job

  Timu ya Serengeti Boys imerejea nyumbani baada ya kumalizika kwa michuano ya AFCON ambapo watapumzika na kuingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na michuano inayofuata ya chini ya miaka 20 inayounda timu ya Ngorongoro Heroes.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akimpa mkono wa kumkaribisha nyumbani mchezaji wa Serengeti Boys Bw. Abdul Sulemani (kushoto) katika hafla ya kuwapokea wachezaji hao waliorejea nchini kutoka katika michuano ya AFCON nchini Gabon jana Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Serengeti Boys pamoja na viongozi wa timu hiyo katika hafla ya kuwakaribisha baada ya kurejea kutoka katika michuano ya AFCON nchini Gabon jana Jijini Dar es Salaam.
  Wachezaji wa timu ya vijana chini ya miaka 17 “Serengeti Boys” wakimsikiliza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika picha) katika hafla ya kuwakaribisha baada ya kurejea kutoka katika michuano ya AFCON nchini Gabon jana Jijini Dar es Salaam. (Picha na: Lorietha Laurence - WHUSM).

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula (pichani) amewataka wananchi wa Kijiji cha Losoito, kuitunza na kutohujumu miundombinu ya maji yaliyowezeshwa na kampuni ya TanzaniteOne.

  Mhandisi Chaula aliyasema hayo juzi alipofanya ziara ya siku moja kwenye kijiji hicho baada ya kupatiwa taarifa kuwa kuna baadhi ya watu wameharibu miundombinu hiyo kwa kukata mabomba.

  Alisema miundombinu hiyo imewezeshwa kwa pamoja na kampuni ya TanzaniteOne na Serikali kwani wanamiliki mgodi huo kwa asilimia 50 kwa 50 hivyo jamii inapaswa kuyatunza kuyathamini na kuyalinda maji.

  Alisema atamchukulia hatua mtu yeyote atakayekamatwa akiharibu miundombinu ya maji kwani wananchi wa eneo hilo kwa muda mrefu waliteseka kufuata huduma hiyo umbali mrefu hadi Mirerani.

  “Nimeambiwa awali kuna mama alishajifungua njiani wakati akifuata maji na baba wa kimasai akakata kitovu cha mtoto kwa kutumia sime kasha leo mtu anaharibu miundombinu hii,” alisema mhandisi Chaula.

  Mkazi wa Kijiji hicho, Magdalena Peter alisema anashukuru kampuni ya TanzaniteOne kwa kuwezesha mradi huo wa maji ila bado kuna changamoto ya upatikanaji kwani wanayapata mara mbili kwa wiki.

  “Awali tulikuwa tunapata maji hayo kwa wakati fofauti na tulivyokuwa tunatembea kilomita 40 hadi Mirerani ila hivi sasa tunawakati mgumu baada ya tenki hilo kupasuka,” alisema Peter.

  Ofisa mahusiano wa kampuni ya TanzaniteOne, Halfan Hayeshi alisema anaomba apewe muda wa wiki mbili ili ahakikishe anafanyia matengenezo sehemu za miundombinu iliyoharibika eneo hilo.

  “Nitakuja na mafundi wiki ijayo ili waangalie na kuikarabati miundombinu hiyo na pia tutanunua tenki lenye ujazo wa lita 10,000 tofauti na hili la lita 5,000 linalotumika hivi sasa,” alisema Hayeshi.

  0 0

  Hyasinta Kissima-Njombe
  Miongoni mwa changamoto zinazoikumba sekta ya afya hususani katika maeneo ya pembezoni mwa Miji ni ukosefu wa huduma bora za afya na za kisasa pamoja na ukosefu wa vifaa tiba.

  Katika Halmashauri ya Mji Njombe Kituo cha afya cha Mtakatifu Anna kinachomilikiwa na shirika la masista wa Benedictine kilichopo Uwemba, takribani KM 30 kutoka yalipo makao makuu ya Halmashauri ni miongoni mwa vituo vya afya 08 katika Halmashauri vinavyotoa huduma za afya kwa zaidi ya Kata 5 zinazoizunguka Halmashauri ya Mji Njombe.

  Miongoni mwa changamoto iliyokua inakikabili kituo cha Mtakatifu Anna Uwemba tangu mwaka 1997 ambapo kilipandishwa hadhi na kuwa kituo cha afya ni ukosefu wa chumba cha Upasuaji. Wazo la uanzishaji wa chumba cha upasuaji lilianza mwaka 2008 na kufikia 2013 kituo hicho kilipata ufadhili kutoka Uholanzi kupitia Mfadhili wao Monique Derrez na Leon Van ambao wao walijitolea kuhakikisha ujenzi na utoaji wa vifaa vya kisasa katika  chumba cha upasuaji.

  Muonekano wa ndani wa Chumba cha Upasuaji.

  Akizungumza wakati wa ibada ya shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kufanikisha ujenzi wa Chumba hicho cha upasuaji Kaimu Naibu Askofu Jimbo Katoliki la Njombe Padre Exavery Mlelwa amesema kuwa ni jambo la heri kumshukuru Mungu kwa Ujenzi wa chumba hicho lakini pia kuwashukuru na kuwaombea Wamisionari waliotangulia na kuanzisha huduma za afya katika maeneo mbalimbali nchi ambazo leo hii huduma hizo zimekuwa ni za msaada kwa jamii ya Watanzani wote na amewasisitiza wazazi kuhakikisha wanawasomesha watoto wao ili kuweza  kupata wataalamu wazuri zaidi katika sekta ya afya kwa siku za mbeleni.

  “Ni vyema kuuenzi uhai tuliojaliwa na mwenyezi Mungu kwa kulinda afya zetu, kufanya vipimo lakini pia kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wetu wa afya na kufuata maelekezo ya madaktari. Uwepo wa Chumba cha Upasuaji Uwemba ni habari njema ya kuimarisha huduma ya afya. Hivyo ni jukumu letu kuhakikisha huduma zinaendelezwa kwa kuhakikisha mnasomesha watoto na kutoa ulinzi wa kutosha kwa kulinda kituo chetu cha afya ili kiweze kuwa na manufaa vizazi na vizazi.” Alisema.
  Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe Gualbert Mbujilo akikata Utepe Kuashiria Uzinduzi wa chumba cha upasuaji.Nyuma yake ni Mganga Mkuu Halmashauri ya Mji Njombe Dkt. Samwel Thomas Ndalio

  Akionesha hali halisi ya vifo vinavyosababishwa na ukosefu wa huduma za upasuaji kwa kina mama Mganga Mkuu Halmashauri ya Mji Njombe Dkt. Samwel Thomas amesema kuwa idadi ya watoto waliopoteza maisha kutokana na kuchelewa kupata huduma kwa kinamama wanaojifungua (Infant Death) kwa kipindi cha Mwezi Januari hadi Machi 2017 katika Halmashauri yake  ni vifo 37 vilivyoripotiwa ambapo kwa kiasi kikubwa vifo hivi vimesababishwa na ukosefu wa huduma za upasuaji katika maeneo jirani na amepongeza uzinduzi huo wa chumba cha upasuaji kwani itapunguza idadi ya kinamama wengi hususani wa maeneo ya Uwemba na Kata za jirani kusafiri hadi mijini kutafuta huduma za upasuaji jambo ambalo limekua likihatarisha maisha yao na watoto wanaozaliwa.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Gualbert Mbujilo, amesema kuwa Halmashauri kwa sasa inasubiri mifumo mipya ya mikataba kati ya Serikali na sekta binafsi juu ya uendeshaji wa vituo vya afya na ameahidi pindi itakapokuwa tayari Halmashauri itatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha yale yaliopo kwa mujibu wa miongozo yanatekelezwa ipasavyo.

  Wakati huo huo amewasisitiza viongozi wa Vijiji, Kata na Watendaji kuhakikisha wanawahamasisha Wananchi kujiunga na Mfumo wa afya CHF  kwani kwa kipindi cha mwaka mmoja familia itatibiwa kwa kiasi cha shilingi elfu kumi na hii itasaidia si tuu upande wa familia bali pia kupitia CHF kituo cha afya kitaweza kujiendesha kwa ufanisi zaidi.

  Kwa sasa kituo hicho kinakabiliwa na ukosefu wa Jokofu la kuhifadhia damu, jenerator la dharura pindi umeme unapokatika ghafla na wameiomba serikali, makampuni binafsi  na watu wenye mapenzi mema  kuona ni jinsi gani inaweza kuwasaidia upatikanaji wa vifaa hivyo kwani kwa sasa vinaumuhimu mkubwa kutokana na uwepo wa chumba hicho cha upasuaji.
  Sister Scholastika ni Daktari katika kituo hicho cha Afya akitoa ufafanuzi wa kazi za vifaa mbalimbali katika chumba cha upasuaji kwa wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.

  0 0

  Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Daniel Kidega (wa pili kulia) akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Mabalozi wa vijana wanaoiwakilisha Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, waliomtembelea ofisini kwake kumuaga, baada ya kumaliza muda wake wa ukongozi katika Bunge la Afrika Mashariki unaofikia ukomo wiki ijayo. Kutoka kushoto ni Reginald saria, Kamala Dickson, Suzane Mollel pamoja na Evas.
  Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Daniel Kidega (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa vijana wanaoiwakilisha Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, waliombelea ofisini kwake kumuaga, baada ya kumaliza muda wake wa ukongozi katika Bunge la Afrika Mashariki. Kutoka kushoto ni Reginald Saria, Kamala Dickson, Suzane Mollel pamoja na Evas.

  0 0


  Mkuu wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amemhakikishia Mfalme Letsie wa III wa Lesotho kuwa Asasi ya Ushirikiano ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama imethibitisha pasipo mashaka utayari wa wapiga kura wa nchi hiyo kupiga kura siku ya Jumamosi tarehe 3 Juni 2017. 

  Hayo yamesemwa kwenye mazungumzo ya viongozi hao ambapo Mhe. Dkt. Mahiga alimuelezea Mtukufu Mfalme Letsie wa III, hatua mbalimbali za uangalizi wa uchaguzi zilizochukuliwa na Jumuiya ya SADC tangu alipofika nchini Lesotho. Jumuiya hiyo mbali na kupeleka waangalizi 41 wa uchaguzi kutoka kwenye nchi tisa wanachama, pia ina wajumbe wawili wa Baraza la Ushauri wa Masuala ya Uchaguzi ambapo mmoja wa wajumbe hao ni Jaji Mstaafu John Tendwa wa Tanzania. 

  Mhe. Mahiga pia alisifu jitihada za Serikali na Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho ambao kwa pamoja wamehakikisha kuwa mazingira mazuri yameandaliwa yatakayoruhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu kufanyika kama ilivyopangwa.

  Kwenye mazungumzo yao, Mhe. Mahiga alitumia pia nafasi hiyo kumpelekea Mfalme Letsie salaam za heshima kutoka kwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama ambayo inaundwa na nchi za Tanzania, Msumbiji na Angola kwa sasa. 

  Kwa upande wake, Mtukufu Mfalme Letsie wa III wa Falme ya Lesotho alimshukuru Mhe. Rais Magufuli kama kiongozi wa asasi hiyo muhimu ya Jumuiya ya SADC na kuongeza kuwa ni matarajio yake kuwa chini ya uongozi wake makini na mahiri, nchi wanachama wa Jumuiya watatekeleza kwa ufanisi majukumu yao muhimu ya kuendeleza jumuiya. 

  Mfalme huyo mrithi wa baba yake Mfalme Moshoeshoe wa II anayetawala Lesotho tangu mwaka 1996 kama Falme ya Kikatiba, alisema anaiheshimu sana Tanzania kwa mchango mkubwa kwa nchi hiyo hususan kwenye kuendeleza taaluma mbalimbali nchini humo. Alisema kwa miaka mingi sasa wataalamu wa masuala ya afya na elimu kutoka Tanzania wameendelea kufanya kazi Lesotho na kuongeza kuwa hata yeye binafsi alifundishwa Chuo Kikuu cha Lesotho na Mtanzania masomo ya Sheria na Sayansi ya Siasa. 

  Mtukufu Mfalme Letsie alimaliza kwa kuahidi kuendeleza ushirikiano wa karibu uliopo baina ya Lesotho na Tanzania ambapo chimbuko lake ni kuwa nchi zote mbili ni wanachama waanzilishi wa Jumuiya ya SADC. Aidha alionesha nia kubwa ya kuzuru Tanzania siku za usoni, na kumuomba Mhe. Dkt. Mahiga, kufikisha salamu za heshima na ushirikiano kwa Rais na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
  Maseru, Lesotho 25 Mei, 2017 
  Mfalme Letsie wa III wa Falme ya Lesotho 
  Mkuu wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akisalimiana na Mfalme Letsie wa III wa Falme ya Lesotho, alipo kutana nae na kufanya mazungumzo. 

  0 0

  Mkataba wa mradi wa Bomba la Mafuta kati ya Serikali ya Tanzania na Uganda (Intergovernmental Agreement- IGA) umesainiwa leo tarehe Mei 26, 2017 katika Hotel ya Serena Jijini Kampala, Uganda. Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Paramagamba Kabudi na Uganda ni Waziri wa Nishati wa nchi hiyo Engineer  Irene Nafuna Muloni.
   Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Paramagamba Kabudi na Uganda ni Waziri wa Nishati wa nchi hiyo Engineer  Irene Nafuna Muloni, wakiwa katika Mkutano huo unaofanyika leo Mei 26, 2017 katika Hotel ya Serena Jijini Kampala, Uganda. 
  Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Paramagamba Kabudi akizungumza katika Mkutano huo unaofanyika leo Mei 26, 2017 katika Hotel ya Serena Jijini Kampala, Uganda. 

  0 0

  MAONESHO ya Vyuo Vikuu vya nchini India yanatarajiwa kufanyika kesho huku yakitarajiwa kutoa fursa kwa wanafunzi wa Kitanzania kuvifahamu vyuo vilivyopo nchini humo na ubora wa taaluma zake.

  Maonesho hayo ambayo yameandaliwa na Global Education Link (GEL) kwa kushirikiana na Ubalozi wa India nchini yatafanyika kesho katika ubalozi huo uliopo jirani na Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC).

  Akizungumzia maonesho hayo, Mkurugenzi wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel amesema, wanafunzi wa kitanzania wamekuwa wakikumbana na changamoto kubwa ya kudsoma katika vyuo ambavyo havina ifa.

  “Unakuta mwanafunzi anapewa taarifa ambazo si sahihi hata katika vyuo anachokwenda, na ndio sababu tumeamua kuandaa maonesho hayo ili kubaini vyuo sahihi,” alisema.

  Amesema wanafunzo wengi wamejikuta wakisoma katika vyuo ambavyo havina hadhi sawa na ile waliyotegemea, hatua inayowawia vigumu katika kutambulika na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU).

  Kwa upande wake Balozi wa India nchini, Sandeep Arya amesema maonesho hayo yatafanyika Kesho na keshokutwa katika ubalozi wa India na kwamba lengo kubwa ni kuwaunganisha wanafunzi wa kitanzania wanaolenga kusoma katika nchi hiyo na vyuo vyenye ubora.

  Arya amesema maonesho hayo yatashirikisha taasisi 20 za vyuo vikuu ambazo zinazotoa fani tofauti katika ngazi zote za elimu ya juu.

  01.Mkurugenzi wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel akizungumzia juu ya maonesho hayo ya Vyuo Vikuu vya nchini India yanatarajiwa kufanyika kesho katika ubalozi huo uliopo jirani na Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC).jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Kampuni ya Jumia Travel imeanzisha kampeni iliyopewa jina la 'Democratize Travel',ya kuwakomboa waafrika kusafiri ndani na nje ya mipaka yao kwa ghrama nafuu kupitia mtandao wa kampuni hiyo .

  Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Mkazi wa Jumia Travel nchini, Fatema Dharsee amesema bara la Afrika limekuwa katika mabadiliko ya matumizi ya Mtandao na kufanya kuongezeka kwa mapato ndani katika sekta ya Utalii.

  Amesema kampeni hiyo ina dhumuni la kuondoa mawazo yaliyojengeka miongoni linapokuja suala la mchakato mzima wa kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine pamoja kupunguzwa kwa gharama za malazi.

  Fatema amesema idadi ya watumiaji wa internet imezidi kuongezeka kwa bara la Afrika na kufikia watumiaji milioni 300 sawa na asilimia 27.7. Matumizi ya Internet yameweza kuchochea ukuaji wa shughuli za utalii kwa njia ya mtandao ikiwemo na usafiri wa anga.

  Fatema amesema kutokana na takwimu hizo zinafanya kuamini Bara la Afrika lina fursa katika ukuaji wa sekta ya Utalii kwa njia ya mtandao.

  Amesema ripoti ya utalii Afrika 2017 iliyowasilishwa na Jumia Travel inajihusisha na huduma za hoteli kwa njia ya mtandao , ambapo inaonyesha kuwa huduma za simu zimeiingizia Bara la Afrika mapato ya ndani kwa asilimia 6.7 kwa mwaka 2015 sawa na dola za Kimarekani bilioni 150 na itaongezeka kufikia dola za Kimarekani bilioni 210 sawa na asilimia 7.6 ya jumla ya pato la ndani la kitaifa kufikia 2020.

  "Jumia Travel nimeona ujio wa Internet na kupokelewa vizuri na waafrika ni ishara kwamba sekta ya utalii itakua ukizingatia ina mchango mkubwa kwenye kuchangia pato la Taifa",alisema Fatema.

  Meneja Mkazi wa Jumia Travel nchini, Fatema Dharsee akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari,wakati wa uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina la 'Democratize Travel',ya kuwakomboa waafrika kusafiri ndani na nje ya mipaka yao kwa ghrama nafuu kupitia mtandao wa kampuni hiyo,kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma,Godfrey Kijanga .

  Meneja Uhusiano wa Umma-Jumia Travel ,Godfrey Kijanga akitoa ufafanuzi kuhusiana na kampeni hiyo 'Democratize Travel' inavyoweza kurahisisha mambo mbalimbali kwa wateja wao,ikiwemo suala la kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine,kulia ni Meneja Mkazi wa Jumia Travel nchini, Fatema Dharsee 
  Mwakilishi kutoka hoteli ya Hong Kong ya jijini Dar Es Salaam,Dusa Suleiman akielezea namna Jumia Travel inavyoweza kurahisisha ufanyikaji wa shughuli za kila siku za hoteli,amebainisha kuwa wao wamenufaika kwa kiasi kikubwa kuliko hapo awali kupitia mtandao huo wa Jumia Travel,amesema kupitia mtandao huo wateja wameweza kujua huduma zao mbalimbali,hivyo wateja wao wameongezeka .

  Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa na  Meneja Mkazi wa Jumia Travel nchini, Fatema Dharsee kuhusiana na uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina la 'Democratize Travel',ya kuwakomboa waafrika kusafiri ndani na nje ya mipaka yao kwa ghrama nafuu kupitia mtandao wa kampuni .Picha na Michuzi JR.

  0 0


  Na Benny Mwaipaja, WFM.

  Serikali za Tanzania na Uganda zimetiliana saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania lenye urefu wa Kilometa 1,443, uliokadiriwa kugharimu zaidi ya Dola bilioni 3 nukta 55, mjini Kampala Uganda, leo.

  Mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi na Waziri wa Nishati wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni.

  Tukio hilo limekuja siku chache baada ya Marais wa Nchi hizo mbili, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni, kutia saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano ya vipengele vya mkataba, Ikulu Jijini Dar es salaam.

  Hafla ya kutia saini Mkataba huo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, Jijini Kampala, Uganda imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi zote mbili wakiwemo Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wanasheria Wakuu wa Serikali, Wakurugenzi na Viongozi wa taasisi mbalimbali zinazohusika katika mradi huo.

  Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima-Uganda hadi Tanga Tanzania, unatarajia kusisimua uchumi wa nchi hizo mbili na katika mchakato wa ujenzi wake zaidi ya watu 10,000 wanatarajiwa kunufaika na ajira.

  Hivi Karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliuelezea mradi huo kuwa ni mkubwa kwakuwa Uganda imegundua shehena kubwa ya mafuta katika eneo la Hoima kiasi cha mapipa bilioni 6 na laki 5 na kwamba Tanzania inatarajia pia kupata mafuta kule ziwa Tanganyika na ziwa Eyasi, ambayo yatapitishwa katika bomba  hilo hilo.
   Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi (kulia) na Waziri wa Nishati wa Uganda, Bi. Irene Muloni (kushoto) wakitia saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda
   Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi (kulia) na Waziri wa Nishati wa Uganda, Bi. Irene Muloni (kushoto) wakitia saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda
   Ujumbe wa Tanzania na Uganda ukishuhudia tukio la utiwaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.
   Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi, akihutubia baada ya kutia saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.
   Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Bw. George Masaju (kulia) na Mwanasheria wa Uganda Bw. Milliam Byaruhanga (kushoto), wakionesha nakala za Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.
  Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi (kulia) na Waziri wa Nishati wa Uganda, Bi. Irene Muloni (kushoto) wakionesha Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, baada ya kuusaini, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.

  0 0
 • 05/26/17--05:05: TAARIFA KWA UMMA.


 • 0 0


  Na Daudi Manongi, MAELEZO,DODOMA.

  Serikali kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeanzisha dawati la wepesi wa kufanya biashara ambao lina jukumu la kuondoa ugumu wa kuanzisha na kuendesha biashara  nchini.

  Hayo yamesemwa leo Bungeni na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Magomeni Mhe. Jamal Kassim Ali.

  “Ujenzi wa Viwanda nchini unategemea zaidi mazingira ya uwekezaji yaliyopo ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa ardhi yenye miundombinu wezeshi,sera mbalimbali,mifumo ya kodi na mifumo ya upatikanaji wa vibali  vinavyotakiwa kisheria ambayo ni majukumu ya Serikali”Alisema Mhe.Mwijage.

  Aidha Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji imeweka mikakati mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara wa kitanzania ili kuwekeza kwenye viwanda hapa nchini.

  Miongoni mwa Mikakati hiyo ni Mafunzo yanayotolewa kwa watanzania wenye nia ya kuwekeza katika viwanda juu ya kuibua mawazo ya kibiashara,kuanzisha ,kuendesha na kusimamia biashara kupitia SIDO,kutoa ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kuchagua teknolojia sahihi inayoendana na wazo la ujenzi wa kiwanda alilonalo Mtanzania kupitia TIRDO,TEMDO na CAMARTEC na namna ya kupata ama kukuza mtaji wa ujenzi wa viwanda kupitia NEDF,SIDO na TIB.

  Pamoja na hayo Wizara imeandaa mwongozo kwa Mikoa,Wilaya,Kata na Vijiji kutenga maeneo ,kusimamia sheria,kanuni,taratibu na kutoa maelekezo kwa wawekezaji.

  “Watanzania wnaaotaka ama walio na mitaji mikubwa wanaweza kuwekeza kupitia maeneo ya EPZA ambayo yametengwa mahsusi kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zinazouzwa nje ya nchi,Pia wanaweza kuwasiliana na TIC kupata vivutio mbalimbali vilivyowekwa na Serikali kwa ajili ya uwekezaji,Alisisitiza Mhe.Mwijage.

  Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage.


  0 0


  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM wilaya ya Kiteto baada ya kusaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM, Wilayani humo leo. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Manyara Pazo Mwamlima na Kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo, Injia Shekue Pashua
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM wilaya ya Kiteto baada ya kusaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM, Wilayani humo leo
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akiwasili kuzungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya, Mabaraza ya Jumuia za CCM na Mabalozi wa CCM wa kumi zilizo karibu na Makao Makuu ya Wilaya ya Kiteto, leo
  Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya, Mabaraza ya Jumuia za CCM na Mabalozi wa CCM wa kumi zilizo karibu na Makao Makuu ya Wilaya ya Kiteto wakimshangilia Bulembo alipowasili ukumbini kuzungumza nao leo.


  0 0

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakifurahia jambo na Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nassari katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.  
    Mbunge wa Kaliua (CUF) Mhe. Magdalena Sakaya akiuliza swali katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.    
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijadiliana jambo na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.
   Naibu waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anstazia Wambura(kulia) pamoja na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe(katikati) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt Medred Kalemani wakati wakijadiliana jambo katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017.  
   Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Mhe. Joseph Haule (Kulia) pamoja na Mbunge wa Mikumi Mhe. Joseph Haule (wa pili kulia) na Mbunge wa Tunduma (CHADEMA) Mhe. Frank Mwakajoka (aliyeipa kisogo kamera) wakimsikiliza Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charels Mwijage wakati wakijadiliana jambo katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 26, 2017. 

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  By Said Ameir

  When President John Pombe Magufuli took over the chairmanship of EAC Heads of State Summit during the 17th EAC ordinary summit held early March, 2016 at Ngurdoto, Arusha, none expected that he would give shocking plea to EAC secretariat- stop your lavish spending and spare the community funds to serve the poor!.

  His first summit after being elected in power, President Magufuli never showed any newness to the occasion and instead showed his true color by hammering what was unexpected to any of his fellow Heads of State and government.

  In his acceptance speech, he never wasted time to pin point that he was of the opinion that the regional body was unwisely spending community funds something which does not reflect the actual state of the economies of the member states.

  President Magufuli urged the Secretariat to take cost- cutting measures to rid the regional body from wasting its hard fought resources from their poor citizens and strongly warned members of the secretariat not to mess around with community money!

  He pledged to take same measures implementing in his country to reduce government spending including curbing lavish spending on travels and meetings and went further to question as to why the secretariat favors convening meets in expensive resorts instead of using conference halls at the regional body’s headquarters.

  The President challenged the Secretariat to become problem solver instead of being always ‘moaners’ and restrict them from being parasitic at the detriment of the poor citizens of member states.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Na Mathias Canal, Dar es salaam


  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori Leo Mei 26, 2017 ameiagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo inayoongozwa na Ndg John Lipesi Kayombo kuanza haraka ujenzi wa Shule ya Sekondari kwa ajili ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam.


  Agizo hilo amelitoa wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mvurunza mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Kata hiyo ili kujionea hali ya maendeleo ya elimu sambamba na kubaini changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ubungo na hatimaye kuzitatua.


  Katika ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo imehudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo, Afisa Tarafa ya Kibamba, Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ubungo, Diwani wa Kata ya Kimara, Mtendaji Kata ya Kimara, Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa sambamba na Baadhi ya Wananchi wa eneo hilo.


  Agizo la Mkuu wa Wilaya ya Ubungo linakuja zikiwa ni siku chache zimepita tangu kutoa maagizo kama hayo katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza, Shule ya Msingi Kawawa na Shule ya Sekondari Mburahati ambapo kote huko ameelekeza kuanza haraka ujenzi wa Madarasa sambamba na Vyoo kwa ajili ya wanafunzi na walimu.
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori (Kulia), Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota wakikagua eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akikagua ukarabati wa Zahanati ya Mavurunza mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017 ambapo ameahidi kusaidia kukamilika haraka kwa ujenzi huo.
   Hali ya ukarabati wa Zahanati ya Mavurunza iliyopo katika Mtaa wa Mavurunza Kata ya KImara
  Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota akimuongoza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori kukagua ukarabati wa Zahanati ya Mavurunza mara baada ya kuzuru kukagua eneo hilo. Leo Mei 26, 2017 ambapo ameahidi kusaidia kukamilika haraka kwa ujenzi huo.


  0 0


  Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, inawashikilia watu wanne wakiwemo wahudumu wawili wa chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mwananyamala kwa kosa la kupasua maiti na kuiba dawa za kulevya kisha kwenda kuziuza.

  Kamanda wa kanda Maalum, Kamishna Simon Sirro amesema, mbali na wahudumu hao wa chumba cha kuhifadhia maiti, mtuhumiwa mwingine ni Ally Mahamud Nyundo (41) ambaye ni miongoni mwa watu waliotajwa katika orodha ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kujihusisha na biashara hiyo.

  “Watuhumiwa walikamatwa kutokana na kuwepo taarifa ya kupokelewa kwa mwili wa raia wa Ghana katika hospitali hiyo, aliyedaiwa kufariki katika nyumba ya kulala wageni kutokana na kumeza dawa za kulevya,” amesema Kamanda Sirro.

  Amesema mtu huyo ambaye bado hajafahamika jina lake alifariki dunia Machi 14 mwaka huu katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Red Carpet iliyoko Sinza, wilaya ya kinondoni.

  Kamanda Sirro amewataja waliokamatwa kuwa ni Omari Rukola (47) na Athuman Mgonja (48) wote wahudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti na katika mahojiano walikiri kuuchana mwili wa marehemu na kuchukua kete 32 za dawa za kulevya ambapo alimkabidhi Omary Wagile (47) mfanyabiashara ambaye naye aliziuza kwa Nyundo.

  Kamanda Sirro amesema watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na baada ya uchunguzi kukamilika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

older | 1 | .... | 1708 | 1709 | (Page 1710) | 1711 | 1712 | .... | 3278 | newer