Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Afisa Mazingira wa Kinondoni aongoza zoezi la Upandaji Miti Shule ya Msingi Mlimani jijini Dar leo

$
0
0
 Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni,Bi. Merry Komba akishirikiana na Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah kupanda mti kwenye eneo la Shule ya Msingi Mlimani ilipo ndani ya eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Kampeni ya Exel With Grand Malt inayoendeshwa na kinywaji cha Grand Malt.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mlimani,Hanifa Mponji akiongea na waandishi wa habari wakati akitoa shukrani zake kwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Grand Malt kwa kuweza kupanda miti katika Shule yake.
 Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni,Bi. Merry Komba akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kupanda miti katika Shule ya Msingi Mlimani ilipo ndani ya eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Kampeni ya Exel With Grand Malt inayoendeshwa na kinywaji cha Grand Malt.Bi. Komba aliwaasa walimu na wanafunzi wa shule hiyo kuanzisha klabu ya kutunza Mazingira kwani faida yake wataiona baadae.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mlimani wakishiriki zoezi la upandaji miti.

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu mawali Bungeni Mjini Dodoma leo Juni 20,2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Kuteuliwa, Joseph Mbatia, Bungeni Mjini Dodoma Juni  20,2013.
Wabunge wa CUF wakimsindikiza Yussuf Salim Hussein (wapili kushoto) wakati alipoapa kuwa Mbunge, Bungeni Mjini Dodoma Juni 20,2013.
Yussuf Salim Hussein wa CUF akiapa kuwa mbunge Bungeni Mjini Dodoam Juni 20,2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi kwenye viwanja vya Bunge MjiniDodoma Juni 20, 2013.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na Wageni wa Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya kutoka Kata ya Silambo walioy temlea Bunge, Ofisini kwake, BungeniMjini Dodoma Juni20, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

President Kikwete meets African Pioneers Against AIDS Scourge

$
0
0
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete pose for a group photograph with some members of African leaders who are pioneers of War against AIDS pandemic in Africa. From left a Kenyan Public Health advocate and academic Prof. Miriam Were, Former Botswana President Festus Mogae(Second left) and Right is Retired President Benjamin William Mkapa. The pioneers held a meeting with President Kikwete at Dar es Salaam State House and discussed the progress made so far in combating the AIDS scourge in the continent and the way forward.(Photo by Freddy Maro).

(COSTECH) IN COLLABOLATION WITH RESEARCH AFRICA FROM SOUTH AFRICA FACILITATE A TWO DAY SCIENCE COMMUNICATION TRAINING FROM 19TH -20TH JUNE 2013 AT COSTECH CONFERENCE ROOM

$
0
0
The Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH) in collaboration with Research Africa from South Africa has conducted a two day science communication training from 19th -20th June 2013 at COSTECH conference room .The training is aiming at improving Journalists and Scientists skills to communicate effectively Science and Technologies issues to the majority of Tanzanians. It is also aiming at providing guidance on reporting scientific controversies. The trainer in that program is Ms Linda Nordling, an editor and Journalist based in Cape Town. The training is also facilitated by Gerald Ralph from South Africa
COSTECH Director General Dr Hassan Mshinda(right) giving his opening remarks to officiate the science Communication training at COSTECH Conference room .Left is the Research Africa trainer from South Africa,Miss Linda Nordling.The two day science communication training is intended to bring together scientists and science Journalists with opportunities for dialogue and mutual learning between these communities.
Participants in group dfiscussions doing some assignments about the science communication organized by Tanzania Commission for Science and Technologies and Research Africa from South Africa.
Mr Gerald Ralphs(left) from South Africa handing over a Vuvuzela gift to the COSTECH Director General Dr Hassan Mshinda as a sign of his appreciation for being invited to facilitate a Science Communication Training.
Participants from different parts of Tanzania standing outside the COSTECH Building to mark the opening of the two day Science communication training organized by COSTECH and Research Africa on 19th June 2013.
Group photo.

We are now in the Final Countdown to Global 2013 Dar es Salaam

$
0
0
DR MIHAELA SMITH CHIEF EXECUTIVE/JOINT CONVENER

News alert: Mbunge wa Kasulu Mjini Mhe. Moses Machali ashambuliwa na watu wasiojulikana, alazwa hospitali Dodoma

$
0
0
Habari kutoka Dodoma zinasema Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, Mhe. Moses Machali (pichani), amelazwa katika hospitali ya mkoa ya Dodoma kuuguza majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na Mbunge wa kuteuliwa, Mhe James Mbatia, watu takriban wanane hivi walimshambulia Mhe Machali mnamo saa mbili za usiku akielekea kupumzika baada ya kuhudhuria vikao vya Bunge.

Mhe Mbatia amesema leo mjini Dodoma kwamba amemtembelea Mhe. Machali asubuhi hii na kumkuta anaendelea vyema na matibabu. 
Habari zaidi tutawaletea kwa kadri zitapopatikana.


tujikumbushe wosia wa baba wa taifa

miondoko ya kumeremeta kwenya mnuso


WADAU TUCHANGAMKE HAPA: NAFASI ZA AJIRA ZA KADA ZA AFYA KWA MWAKA 2012/2013

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

NAFASI ZA AJIRA ZA KADA ZA AFYA KWA MWAKA 2012/2013

Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, anapenda kuwaarifu Wataalamu wa Kada za Afya kuwa wamepangiwa vituo vya kazi kutokana na maombi ya kazi waliyowasilisha kwake kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

Watalamu wote wanatakiwa kuripoti katika vituo walivyopangiwa kabla ya tarehe 30 Juni, 2013. Baada ya muda huo kumalizika waajiri wanatakiwa kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili wale ambao hawajaripoti nafasi zao ziweze kujazwa.

Aidha, Waajiri wote wanakumbushwa kukagua vyeti halisi (Original) vya kidato cha nne na kidato cha Sita pamoja na vyeti vya taaluma kabla ya kuwaajiri wataalamu hawa wa kada za afya.

Orodha ya majina ya Wataalamu waliopangiwa kazi na vituo walivyopangiwa inapatikana kwenye tovuti ya Wizara www.moh.go.tz. Wizara haitatoa barua za kupangiwa vituo vya kazi kama ilivyokuwa hapo awali.

Nawapongeza kwa kupata nafasi hii ya kutumia utaalamu wenu katika kuwahudumia wananchi, na ninawatakieni kazi njema na utumishi uliotukuka.

20 Juni, 2013

Article 18

Makampuni ya simu kupandisha gharama Julai Mosi - MOAT

$
0
0
Kufuatia kuongezwa kwa kodi katika huduma za simu za mkononi , gharama za huduma hizo zinatajiwa pia kuongezeka kuanzia Julai Mosi mwaka huu.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa jijini Dar es salaam na Umoja wa Makampuni ya Simu za Mkononi Tanzania – MOAT imesema pendekezo la serikali la kuweka kodi ya 14.5 kwenye huduma za simu za mkononi hazotoweza kukwepesha kupanda kwa gharama za simu kwa watumiaji.

MOAT inasema awali kodi ilikuwa ikitozwa asilimia 12.5 katika huduma ya mawasiliano ya simu na kwmaba ongezeko la kufiikia asilimia 14.5 tofauti na nchi za jirani Kenya na Uganda ambazo zimeendelea kutoza viwango vya ushuru vya asilimia 10 na 12.5 tu ni mzigo kwa watumiaji wa huduma za simu za mkononi.

Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2013 unaainisha, huduma za mawasiliano kuwa ni; “huduma yoyote ya maelezo inayotolewa na makampuni ya mawasiliano ya simu kwa njia ya mawasiliano kwa kutoa au kupokea sauti, maandishi, na picha au taarifa ya aina yoyote kupitia mfumo wa kielektronikia.

”Imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na Vodacom, Airtel, Tigo na Zantel MOAT imesema eneo mojawapo litakaloathirika ni huduma za Intaneti eneo amablo linahitaji kuwekewa mikakati ya kulikuza kutokana na umuhimu wake katika maisha ya sasa kiuchumi na kijamii na wala sio kulizorotesha kwa kusababisha ongezeko la gharama na hivyo kuendelea kuwa na kiwango cha cha matumizi kilinganishwa na baadhi ya nchi nyengine zikiwemo za Afrika Mashariki. “Hatua hii ya kuongeza kodi itakwenda kinyume na mipango iliyopo yenye lengo la kuibadili jamii kwa kuipatia maarifa ya msingi kupitia huduma ya intaneti sambamba na mawasiliano ya simu.”

Kwa mujibu wa MOAT, Tanzania ni kati ya nchi zenye kiwango cha chini ya matumizi ya huduma ya mtandao wa intaneti katika bara la Afrika ambapo watumiaji wa huduma hiyo ni asilimia 10 pekee ikilinganishwa na nchi jirani ya Kenya ambayo ina zaidi ya watumiaji asilimia 40.

Aidha, MOAT imeongeza kuwa, “mawasiliano ya simu si anasa bali ni huduma muhimu katika Tanzania ya leo, sasa tunawezaaje kuwatozakodi mara kwa mara watu hao hao ambao wanaitegemea huduma hiyo ili kuboresha maisha yao? Ilihoji taarifa hiyo ya MOAT. Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa kwa tozo la kodi ya mapato ya asilimia 35 kwenye sekta hiyo ya mawasiliano ya simu linatosha kiasi ya kwamba sekta hiyo isngeweza kubeba mzigo zaidi wa ongezeko jingine.

Hivi sasa, upanuzi wa mawasiliano na miundombinu vijijini ndiyo kipaumbele cha sekta nzima. Tunaamini hapa ndipo ukuaji wa sekta ya mawasiliano ya simu itakapoonekana katika miaka ijayo. Ongezeko lolote la kodi litazorotesha uwezo wetu wa kutanua huduma zetu za mawasiliano na miundombinu maeneo ya vijijini, imesema MOAT.

“Tunaelewa kuwa serikali inayafanya haya yote ili kuweza kupata fedha kwa ajili ya kusaidia kwenye huduma za jamii katika maeneo muhimu. Ni bahati mbaya kwamba sekta ya huduma ya mawasiliano ya simu inaendelea kubeba mzigo mkubwa wa ongezeko hili ambapo wateja watalazimika kuubeba mzigo wa ongezeko hilo,” ilihitimisha taarifa hiyo ya MOAT.

Mh. January Makamba kuwa mgeni rasmi Redd's Miss Tanga 2013

$
0
0
NAIBU Waziri wa Sayansi na Tekinolojia January Makamba,anatarajia kuwa mgeni rasmi, katika shindano la umsaka malikia wa Redd's Miss Tanga 2013 linalotimua vumbi katika uwana wa Mkwakwani Mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Mkurugenzi wa DATK Intertainment Asha Kigundula alisema, maandalizi yamekamilika kilichosalia ni muda kufika na mrembo kuwekwa hadharani.

“Nashukuru mungu mambo yameenda sawa, kilichokuwa kimesalia ni kumtangaza mgeni rasm na nashuuru tumeisha mpata tayari mh;Makamba na hakuna kingine, cha muhimu mungu atuongoze katika shughuli yetu esho mambo yaende sawa,”alisema Kigundula.

Aidha Kigundula alisema, ameamua kutoa zawadi ya fedha taslimu kwa warembo na sio vitu ili warembo wake waweze upata fursa ya ujichagulia kitu cha kununua wenyewe uliko ununuliwa na kudai uwa mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha sh 500,000, wa pili sh 300,000 na wa tatu sh 250, 000.

Huku wa nne na tano wakipata sh.200, 000 kila mmoja na warembo wengine watakaosalia watapata kitita cha sh 100,000 kila mmoa kama kifuta jasho pamoja na zawadi kwa mrembo mwenye nidhamu ili kuweza kuboresha shindano hilo.

Kigundula alisema, kwa upande wa Burudani msanii wa kizazi kipya, Tunda Man, ataongoza safu ya burudani, ambapo itakuwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Dr John, Nabisha kutoka kundi la THT, Fady Dady na wasanii chipukizi kutoka mkoani hapa.

Kigundula alisema shindano hilo linatarajiwa kuanza majira ya saa mbili usiku na kushirikisha warembo 12 ambao watachuana ili kuweza kumpata malkia wa mkoa huu ambaye atauwakilisha mkoa katika mashindano hayo ngazi ya kanda.

Warembo hao ni Hawa Ramadhani (18),Hazina Mbaga (19)Like Abdulraman (19), Irene Thomas(20), Tatu Athumani (19), Winfrida Gutram (21)Lulu Mbonela (19) ,Hazina Daniel (19),Lulu Matawalo(22),Judithi Moleli (21),Neema Jonas na Hawa Twaybu(21).

Aliongeza wa kuwataka wakazi wa Tanga na Mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kushuhudia shindano hilo la aina yake, ambalo litajenga historia mypa kwa Mkoa huu, Shindano la Redds Miss Tanga 2013 limedhaminiwa na  Redds, Miss Tanga, imedhaminiwa na Al Hayat Investment Limited, Dodoma Wine, CXC Africa,Executive Solutions,Busta General Supply, Mkwabi Interprises,Lusindic Investment LTD, Lavida Pub,Jambo Leo,Staa Spoti,Five Brothers Cloud's Media Group, pamoja na Blog Michuzi Media Group,Bongostaz.com, Saluti5,Kajuna, JaneJohn, na Kidevu na assengaoscar.blogspot.com.

Article 15

$
0
0
CENTURY CINEMAX MLIMANI CITY 
 NOW SHOWING:
(21 - 27 JUNE 2013)

 MAN OF STEEL 3D
[PG-13]*Henry Cavill
2 pm* / 4:30 pm / 7:15 pm  & 10 pm

YALIYOJIRI KATI YA TIMU YA BENKI YA NMB NA WABUNGE JIJINI DODOMA MWISHONI MWA WIKI

$
0
0
Katika kuendeleza na kuimarisha mahusiano mazuri kati ya Benki ya NMB na waheshimiwa wabunge, Benki ya NMB iliandaa mtanange wa kukata na shoka ambao ulihudhuriwa na washabiki wa timu hizo mbili ambao ni wakazi wa manispaa ya Dodoma.

Hiki ndicho kikosi kamili cha timu ya benki ya NMB kilichong’ara siku hiyo katika kutimua kivumbi kwenye uwanja wa jamhuri.

Na hii ndio timu ya waheshimia wabunge iliyowatikisa wachezaji wa timu ya NMB

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mhe. George Mkuchika ambae alikua ndiye mgeni rasmi akikagua kikosi cha timu ya NMB kabla ya mpambano huo.

Naibu waziri wa habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.Amos Makalla (Jezi ya njano na Bluu) akipigwa chenga na Afisa mkuu wa fedha NMB Waziri Waziri katika mtanange huo uliokuwa wa kukata na shoka.

Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azan ambae ndiye mlinda mlango wa timu ya wabunge (Jezi ya rangi ya chungwa) akiongoza wanatimu kufurahia goli moja walilolipata kwa taabun sana na kuwapa ushindi wa bahati dhidi ya timu ya NMB

Hawa ni sehemu ya mashabiki wa timu hizi mbili wakifurahia mtanange huu

Article 13


Mhe. Jaji Mkuu awaapisha Mawakili wapya 127 jijini Dar es Salaam Leo

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akimpongeza mmoja wa Mawakili wapya 127 walioapishwa  leo asubuhi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Picha na Mary Gwera

MHE. ALI HASSAN MWINYI MGENI RASMI, MASANJA, SHILOLE KUFANYA MAKAMUZI MIAKA 3 YA VIJIMAMBO NA TAMASHA LA UTAMADUNI WA KISWAHILI MAREKANI

$
0
0

Blog ya Vijimambo ikishirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Washington, DC, Marekani na Jumuiya ya Watanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia wanapanga kusherehekea miaka 3 ya Vijimambo na kukuletea tamasha la kiswahili. Tamasha hili ni kuendeleza lugha na utamaduni wa Kiswahili hapa Marekani ili watoto wanaoishi huku waweze kuendeleza matumizi ya lugha hii na utamaduni wake kizazi hadi kizazi. 

Siku ya July 6, 2013  hapa DMV kwenye Hall la Hampton Conference Center lililopo 
207 w Hampton Pl, 
Capitol Height, MD

Mambo mengi yatakayokuwepo ni Vikundi mbalimbali vya utamaduni, wanamitindo wa mavazi mbalimbali kuwakilisha, vyakula vya Kitanzania, Wasanii kutoka nyumbani ambao ni Shilole na Masanja Mkandamizaji wakishirikiana na wa hapa Marekani yote hayo ni kudumisha utamaduni wetu wa kiswahili

HOTEL KWA WAGENI 
Tumeongeza vyumba 35 Hotel ya Country Inn & Suites 
Na unapopiga simu uliza SWAHILI CULTURE IN USA kusudi upate unafuu wa bei nambari ya simu ni 301 350 8088 na Address ni
8850 Hampton Malls Drive North
Capitol Heights, MD 20843

Hotel za jirani na hapa ni
Hampton Inn
9421 Largo Dr West,
Largo, MD 20774
simu ni 301 499 4600

Extended Stay American

9401 Largo Drive West,
Largo, MD 20774
simu ni 301 3339139

Confort Inn
56 Hampton Park Blvd
Capitol Heghts, MD20743
Simu ni 301 336 8900

MAVAZI 
10:00 am - 5:00 pm Vazi la Kitanzania
7:00 pm - 3:00 am Vazi lolote lakini uwe umependeza
KARIBU

TANGAZO LA MKUTANO WA WANA TABORA GIRLS (WARSAW) Juni 22, 2013

$
0
0
Ndugu uliyesoma Tabora Girls mwaka wowote ule, unakaribishwa katika kikao cha kupanga mikakati mbalimbali ya kuinuana. 
Mchango wa mawazo yako ni muhimu sana pia ni msingi imara wa umoja utakao anzishwa baada ya mchakato huo kukamilika.

Tukutane Landmark Hotel, Riverside, Dar es salaam  Saa 9 kamili mchana tarehe 22/6/2013.
Tafadhali mjulishe na mwenzio.


 "Divided we fall together 
we stand against all odds"

Karibuni sana.
MRATIBU

Tanzanite yawa kivutio Ghana.

$
0
0
Madini ya vito aina ya Tanzanite yanayopatikana na kuchimbwa Tanzania pekee duniani hapa yamekuwa kivutio kwa wananchi katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma-Afrika yanayoaendelea jijini Accra-Ghana. 
Wananchi wengi waliotembelea banda la Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) wameeleza kuwa pamoja na kuyaona madini hayo sehemu mbalimbali duniani lakini walikuwa hawana ufahamu wa kutosha kuwa ni Tanzania pekee ndiyo yenye hazina ya madini hayo. 
Msemaji wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Eng. Yisambi E.Shiwa ameeleza kuwa maonesho yamekuwa yakitumika kama nyenzo ya kutoa elimu kuhusu uendelezaji wa sekta ya madini Tanzania ili kuweza kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya Tanzania kuwekeza kwenye rasimali hiyo.
Kamishina wa Tume ya Utumishi wa Umma Ghana Bw.Robertson Akwei Allotey akiangalia madini ya tanzanite yanayoonyeshwa katika banda la Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) jijini Accra
Wananchi wa Ghana wakiwa kwenye banda la Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) ili kupata elimu kuhusu sekta ya madini Tanzania jijini Accra

TAARIFA TOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images