Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 168 | 169 | (Page 170) | 171 | 172 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania, Grace Rubambey (katikati) akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya ugonjwa wa Sikoseli Duniani jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mfuko huo, Dk Julie Makani, Balozi wa Canada nchini, Alexandre Leveque na mmoja wa watu wanoishi na ugonjwa huo, Arafa Salim Said.
  Balozi wa Canada nchini, Alexandre Leveque (katikati) akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya ugonjwa wa Sikoseli Duniani jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania Dk Julie Makani na Mwenyekiti wa mfuko huo, Grace Rubambey na mmoja wa watu wanoishi na ugonjwa huo, Arafa Salim Said.
  Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania, Dk Julie Makani (kushoto) akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya ugonjwa wa Sikoseli Duniani jijini Dar es Salaam leo. Tanzania ni nchi ya nne duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaougua ugonjwa wa sikoseli.
  Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Msimbazi, Philipo Pilla (kulia) akizungumza wakati wa maadhjimisho hayo. Benki ya KCB ni mmoja wa wadhamini wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania.
  Mratibu wa Huduma za Ugonjwa wa sikoseli katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Deogratias Soka (kulia) akizungumza kuhusu hali ya ugonjwa huo katika hospitali hiyo katika maadhimisho hayo. Inakadiriwa kuwa katika ya watoto 8,000 hadi 10,000 kuzaliwa na ugonjwa huo nchini Tanzania kila mwaka.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, wakati alipowasili kwenye Hoteli ya Double Tree, kwa ajili ya kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mawakala wa Usafirishaji wa Majini kwa nchi za Mashariki ya Kati kwa Afrika, uliaoanza jijini Dar es Salaam leo Juni 19, 2013 unaofanyika kwa siku nne.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mawakala wa Usafirishaji wa Majini kwa nchi za Mashariki ya Kati kwa Afrika, uliaoanza jijini Dar es Salaam leo Juni 19, 2013 unaofanyika kwa siku nne. 
  Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua mkutano huo.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi rasmi wa mkutano huo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe,wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo.Picha na OMR

  0 0

  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Angella Kairuki (mwenye koti la pink) akimsikiliza Bw. Paschal Mayumba Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Mvumi Makulu anayehudumia Mahakama ya Mwanzo Mvumi Makulu na Mahakama ya Mwanzo ya Handali akitoa ufafanuzi wa jambo kuhusu kiwanja ambacho Mahakama ya Mwanzo ya Handali imepewa na Uongozi wa Kijiji kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Mahakama hiyo. Kushoto kwa Mhe. Kairuki ni Mhe. Livingstone Lusinde, Mbunge wa Jimbo la Mtera, ambaye aliambatana na Naibu Waziri katika kutembelea Mahakama za Mwanzo za Wilaya ya Chamwino. Wengine katika picha hiyo ni viongozi wa Mahakama na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Handali.
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Angella Kairuki akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Makang’wa Wilayani Chamwino na kuwahamasisha kujenga majengo ya Mahakama kwa nguvu zao ili waweze kupata huduma hii muhimu karibu na maeneo yao na kuacha kutembea umbali mrefu kuzifuata mahakama ili kupata haki zao. Aidha,Mhesjhimiwa Kairuki aliwaahidi wananchi hao kwamba Serikali kupitia Mahakama itashirikiana nao katika kujenga jengo la Mahakama katika eneo hilo.
  Mbunge wa Jimbo la Mtera, Mhe. Livingstone Lusinde akiuelezea ujumbe wa Mhe. Angellah Kairuki namna ambavyo uongozi wa Mahakama umepewa kiwanja na uongozi wa Kata ya Mvumi Mission kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo. Hadi sasa eneo hilo lenye wakazi wengi halina huduma ya Mahakama na hivyo kuwalazimu wananchi wa eneo hilo kutembea umbali mrefu kutafuta haki zao.

  0 0

  Diamond akilonga na Sauda kuhusu shoo kali atakayotoa Usiku wa Matumaini 2013.


  Na Wilbert Molandi

  MKALI wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ ametamba kufanya shoo kali ikiwemo kumfunika msanii wa Uganda, Prezzo katika Tamasha la Matumaini 2013 litakalofanyika Sikukuu ya Sabasaba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

  Diamond ametoa majigambo hayo wakati wa mahojiano na Mtangazaji wa kituo cha Star TV, Sauda Mwilima.

  “Nimeahidi kufanya bonge la shoo kwenye Tamasha la Matumaini siku hiyo, mashabiki wangu na wapenzi wa muziki wajitokeze kwa wingi.
  “Ninataka kudhihirisha ubora wangu siku hiyo kwa kumfunika vibaya Prezzo,” alisema Diamond.

  0 0
 • 06/19/13--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Ngoma ya Oliver Ngoma (RiP) 'ADIA' ni balaa

  0 0


  0 0

  .Airtel Tanzania has handed over jerseys, shin guards, balls and socks to teams taking part in this year's  U-17 talent scouting football tournament known as Airtel Rising Stars whose regional level matches are set to commence on Monday June 23rd 2013. 
  Soccer regions of Ilala, Temeke and Kinondoni will enter both boys and girls in the annual event while Morogoro, Mwanza and Mbeya will only participate in the boys category as opposed to Tanga, Ruvuma and Kigoma regions which will feature in the girls category alone. 
   All the teams have sounded optimistic that they are well prepared to compete and win their matches. The regional matches will be used to pick the best players to form a combine team for the national ARS finals slated for July at the Karume Memorial Stadium in Dar es Salaam. 
  Speaking at the kits handover press conference held at the Tanzania Football Federation (TFF) today, Airtel Tanzania Public Relations Manager Jackson Mmbando said that Airtel is proud to be part and parcel of the youth football program which is aimed to accelerate football development in Tanzania. “We believe that our combined forces with Manchester United FC and TFF will facilitate football development in Tanzania. We have confidence in the youth that given chance and support, they are able to excel in football’, he said. TFF Technical Director Sunday Kayuni said that he was highly impressed by the overwhelming response by the youngsters to take part in this year’s Airtel Rising Stars championships. 
   “The turnout has been highly impressive and encouraging and I thank Airtel for coming up with this initiative which helps us to indentify more hidden soccer talents”, he said. Airtel Rising Stars football program is an initiative designed for the entire African continent which is aimed to provide a platform for upcoming soccer talent to showcase their skills to leading scouts, coaches and have an opportunity to further their football skills.
   In the previous two years of this program, Manchester United sent its school coaching staff to conduct international football clinics in Tanzania, South Africa, Gabon and Kenya where selected participants got opportunity to learn how to play football the Manchester United way. 
  To further motivate and excite the youngsters, Airtel has introduced an inter-country tournament that was held in Nairobi for the first time last year where the boys and girls had an opportunity to showcase their football talents.
   The inter-continental tournament brought together ARS stars from 14 countries where Airtel does business. The ARS stars are selected at the national finals which are held by each of the participating countries under the supervision of respective national football federations. Both the clinic and the inter-country will be held again this year round and more details regarding these two events will be released next month.
   Airtel Tanzania Public Relations Manager Jackson Mmbando(L) hands over footnall  kits to TFF Technical Director Sunday Kayuni and DRFA Chairman Almasi Kasongo for  regional teams taking part in this year’s U-17 Airtel Rising Stars football  tournament. The handover event was held at TFF conference hall in Dar es Salaam

   Airtel Tanzania Public Relations Manager Jackson Mmbando(L) hands over footnall  kits to TFF Technical Director Sunday Kayuni and DRFA Chairman Almasi Kasongo for  regional teams taking part in this year’s U-17 Airtel Rising Stars football  tournament. The handover event was held at TFF conference hall in Dar es Salaam

  Airtel Tanzania Public Relations Manager Jackson Mmbando speaks to the media at a press conference held at TFF conference hall to hand over soccer kits to regional teams taking part in this year’s U-17 Airtel Rising Stars football  tournament.

  0 0


    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mabalozi wateule wa Tanzania, wanaokwenda kuripoti kwenye Vituo vyao vya kazi nje ya nchi, wakati mabalozi hao walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kumuaga mhe. Makamu. Kutoka Kushoto ni Balozi Modest Mero, anayekwenda Umoja wa Mataifa, Geneva, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, anayekwenda, Abu Dhabi UAE, Balozi Chabaka Kilumanga, anayekwenda Comoro, Balozi Wilson Masilingi, anayekwenda The Hague, Uholanzi na Balozi Liberata Mulamula, anayekwenda Washington D.C, Marekani.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wateule wa Tanzania, wanaokwenda kuripoti kwenye Vituo vyao vya kazi nje ya nchi, wakati mabalozi hao walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kumuaga mhe. Makamu. Kutoka Kushoto ni Balozi Chabaka Kilumanga, anayekwenda Comoro, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk, anayekwenda, Abu Dhabi UAE, Balozi Modest Mero, anayekwenda Umoja wa Mataifa, Geneva (kulia) ni Balozi Wilson Masilingi, anayekwenda The Hague, Uholanzi na Balozi Liberata Mulamula, anayekwenda Washington D.C, Marekani.Picha Zote na Ofisi ya Makamu wa Rais

  0 0

   Mkuu wa Idara ya Uendelezaji Biashara ya M-pesa Jackson Kiswaga akionesha jinsi M-pesa inavyoweza kuboreshwa kukidhi mahitaji zaidi ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu ambayo huitumia huduma hiyo kama njia kuu ya kukusanyia ada ya maombi ya mkopo tangu mewaka 2010. Wanaomuangalia ni Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim (kulia) na Naibu Mkurugenzi wa Tehama wa bodi Cuthbeth Simalenga. Vodacom ilitembelea makao makuu ya bodi hiyo jana kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa taasisi hizo mbili.

   Mkuu wa Idara ya Mawasiliano, Habari na Elimu kwa Umma wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Cosmas Mwaisbwa akifafanua jambo wakati wa kikao baina ya bodi na kampuni ya Vodacom Tanzania kuangalia namna ya kuimarisha na kubioresha zaidi uhusiano wa biashara baina ya taasisi hizo mbili. Wengine pichani kutoka kulia ni Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Naibu Mkurugenzi wa Tehama wa bodi Cuthbeth Simalenga,
  Mkuu wa Idara ya Uendelezaji Biashara ya M-pesa Jackson Kiswaga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati Vodacom ilipotem,ebela makao makuu ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu jana jijini Dar es salaam kwa lengo la kukuza uhusiano wa biashara baina ya taasisi hizo mbili. Kulia ni Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi Juma Chagonja na Naibu wa Tehama wa bodi hiyo Cuthbeth Simalenga. Bodi ya mikopo kwa miaka mitatu sasa imekuwa ikiitumia huduma ya M-pesa kama njia kuu ya kukusanyia ada ya mamombi ya mkopo kutoka kwa waombaji wake.

  Na Mwandishi wetu.
  Bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini - HESLB imesema huduma ya M-pesa inayowawezesha waombaji wa mikopo ya elimu juu kwenye bodi hiyo kulipia ada ya uombaji kwa kiasi kikubwa imesaidia kurahisisha uendeshaji ikwemo usimamizi na ufuatiliaji wa malipo hayo.
  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini Bw. Cuthbeth Simalenga wakati wa kikao cha urafiki mwema kati ya uongozi wa Bodi na Kampuni ya Vodacom kilichofanyika makao makuu ya bodi hiyo yaliyopo Msasani Jijini Dar es salaam kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa taasisi hizo.
  Bw. Simalenga amesema bodi hiyo ilianza kutumia huduma ya M-pesa kwa malipo ya ada ya maombi miaka mitatu iliyopita na kwamba tangu wakati huo huduma hiyo imekuwa ikiimarika na kutoa tija zaidi kwa upande wa uendeshaji wa shughuli za uombaji wa mikopo.
  "Kwa miaka mitatu sasa tumekuwa tukitumia huduma ya M-pesa kukusanyia ada za malipo ya maombi ya mikopo, kwa sasa waombaji wote wanatumia huduma hii na tumekuwa tukiboresha mifumo yetu ya ndani mara kwa mara kukabiliana na changamoto za hapa na pale zinazojitokeza."Alisema Bw. Simalenga
  Zaidi ya waombaji 50,000 wakiwemo waombaji wapya na wale wanaaondelea na elimu ya juu hutuma maombi ya mikopo kwenye  bodi hiyo kwa mwaka, na wote kwa sasa wanatumia huduma ya M-pesa kulipia ada ya malipo ya maombi ambayo ni Sh 30,000.
  Bw. Simalenga amesema changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa katika mfumo huo wa malipo kuwa ni uaminifu wa waombaji hasa wanafunzi ambao baadhi yao hulalamika kushindwa kulipia au na kudai kutaka kurejeshewa fedha zao wakati huohuo wakiwa tayari wameshakamilisha mchakato wa uombaji na fedha hizo kupaswa kutumika kama ada ya uombaji.
  "Wamekuwepo baadhi ya waombaji ambao wamekuwa wakisababisha usumbufu wa hapa na pale kwa kutuma maombi na kufanya malipo baadae wanarudi na kupiga simu Vodacom kudai kurejeshewa fedha zao kwa madai kuwa wamebadili mawazo ya kuomba mkopo wakati sio kweli." Aliongeza Bw. Simalenga
  "Tunaomba waombaji wote na umma kwa ujumla kutambua kuwa mamlaka ya kurejeshewa fedha Sh 30,000 ya ada ya uombaji yapo nje ya Vodacom, hilo ni la Bodi na kwamba sasa tumeweka utaratibu wa kurudisha fedha hizo mwishoni mwa zoezi la uombaji tukizinagtia taratibu za kiuhasibu za bodi baada ya kujiridhsiha kuwa utambulisho wa muamala (Transaction ID) wa mwombaji haijatumika kuendelea na zoezi la uombaji mkopo."Alifafanua
  Aidha ametumia nafasi hiyo kuzungumzia uhusiano wa bodi na kampuni ya Vodacom ambao amesema una kila nafasi ya kuwa imara zaidi huku akiishauri Vodacom kuongeza ubunifu zaidi kwenye mfumo wa malipo ya M-pesa ili mfumo huo uweze kuwa na tija zaidi kwa wadau wake hasa wabia wakubwa.
  "Vodacom imekuwa karibu na sisi na bado kuna fusra zaidi ya ubunifu kwenye huduma hii itakayotoa tija zaidi kwetu."Alisema Bw Simalenga na kuongeza "Tunafurahia uhusiano wetu wa kibishara kwa kipindi chote hiki kwani tumepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Vodacom pekee hivyotumejikuta tukiwa na M-Pesa pekee."
  Kwa upande Mkuu wa Idara ya Ukuzaji Biashara ya M-pesa wa Vodacom Bw Jackson Kiswaga amesema kiasi cha Sh. Bilioni Moja na Milioni Mia Nne kinapitia katika mfumo wa M-pesa kama ada ya uombaji wa mikopo kila mwaka.
  "Tumekuja kubadilishana uzoefu na wenzetu juu ya uhusiano wetu unaotuunganisha kupitia huduma ya M-pesa, bodi hii imekuwa sehemu muhimu kwetu kibiashara na tunatarajia kuimarisha zaidi huduma hii siku zijazo."Kiswaga aliwaambia waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo.
  Kiswaga amewakumbusha waombaji wa mikopo wa bodi hiyo ya elimu ya Juu kuendelea kuitumia huduma ya M-pesa katika kulipia ada ya uombaji kwa kuwa ndio njia rahisi na ya kuaminika zaidi kwao inayowapunguzia gharama za usafiri,muda na usumbufu.
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi hiyo Bw. Juma Chagonja amesema bado zipo fursa nyingi bodi inazoweza kuzitumia kwenye huduma ya M-pesa na kuwataka wananchi kuvuta subira kuona mambo mazuri zaidi siku chache zijazo.

  0 0
 • 06/20/13--00:58: Article 14


 • 0 0

  Kwa katuni kedekede, tembelea jarida lako la katuni la mtandaoni, 'nathan cartoon magazine' kila Alhamis. Leo lipo angani kupitia chochoro hii,www.nathanmpangala.blogspot.com

  0 0

  An illustrious panel of football experts has been assembled by SuperSport to provide unprecedented coverage of the Confederations Cup, that recently started in Brazil.
  They include Sunday Oliseh, Shaun Bartlett, Gary Bailey, Samuel Kuffour, Neil Tovey, Doctor Khumalo, Mark Fish and Andre Arendse, who will offer analysis of the traditional “dry run” ahead of the 2014 World Cup.
  African champions Nigeria will fly the continent’s flag, but have been drawn in a tough Group B that includes World Cup winners Spain and South American champions Uruguay.
  The tournament will be staged at six venues across Brazil from June 15-30 and will be used to test the country’s readiness for the World Cup this time next year.
  It is the second appearance at the competition for the Super Eagles, who finished fourth in 1995 when the tournament was held in Saudi Arabia and still known as the King Fahd Cup.
  Coach Stephen Keshi will be relishing taking his side onto the global stage after their success at the 2013 Africa Cup of Nations in South Africa in February.
  That victory might have been unexpected, but was fully deserved as the side grew in stature as the tournament progressed, getting better with each game.
  They got the chance to ease into the Confederations Cup as well with an opening match against tiny Oceania champions Tahiti on June 17.
  Tahiti are easily the smallest country ever to appear in a FIFA finals with a population of just 180 000 and are not expected to provide much resistance to their pool opponents.
  Nigeria face a talented, but largely out of sorts of late Uruguay side in their second group game on June 20, warming up to a big finish against Spain on June 23.
  It is likely the Uruguay clash will be the key one in the pool for Keshi and his charges if they are to finish in the top two and advance to the semifinals.
  Group A has a fascinating look about it with hosts Brazil, European Championship runners-up Italy, crowd favourites Mexico and an ever-improving Japan battling it out for the top two places. 
  Brazil got their campaign under way against the Asian champions on June 15 and finish off against Italy on June 22. 
  The top side in Group A meets the runners-up of Group B and vice-versa in the semifinals, with the final to be staged at the refurbished Maracanã in Rio de Janeiro on June 30.
  Cameroon are the only African side to reach the final of the competition, but lost 1-0 to France in 2003, a tournament that was overshadowed by the death of Indomitable Lions midfielder Marc-Vivien Foé.
  Aside from Nigeria’s fourth-place finish almost two decades ago, South Africa also claimed that position on home soil in 2009, as did Cote d’Ivoire in 1992.
  SuperSport’s coverage, to be anchored by Robert Marawa, Neil Andrews and Charles Anazodo, will include one-hour buildups per match, plus a magazine show – Ola Brazil –screening on Saturdays and Sundays at 10am CAT. Master Plan will air on Sundays at 6pm CAT.
  Apart from English, language options include Sotho, Zulu and Portuguese.

  BROADCAST DETAILS


  ·        Please note that all times are in CAT


  0 0

  Wanabiafra pamoja na marafiki wengine kwa pamoja walijumuika nyumbani kwa Mwenyekiti wa Biafra Bw. Abdul Mollel pamoja na mkewe Bi. Evelyine katika arobaini ya mtoto wao Mollel Jr. Fuatilia matukio pichani.
  Mama mzaa chema Evelyne akiwa na mtoto Mollel Jnr.
  kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina O. Kombani akisani kitabu cha wageni. Picha zote na Scola Malinga – Hazina- Tanzania.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina O. Kombani alipotembelea banda la Wizara ya fedha na kuelezea jinsi alivyofurahishwa na ushiriki wa Wizara ya fedha katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
  Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Wizara ya Fedha kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi. Christine Ngonyani akiwa na watumishi wa wizara ya fedha walipotembelewa na Bw. Pascal Mugabe ambaye ni Afisa Tawala Rasilimali Watu wa Idara ya Utawala, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye yupo Nchini Ghana kwa masomo ya elimu ya juu(Phd) .

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0
 • 06/20/13--03:08: Article 9

 • 0 0


  0 0
 • 06/20/13--04:47: msaada tutani
 • Ankal,

  Habari, naitwa Upendo, naomba uniweke katika blog hii ya jamii natafuta mchumba hatimae tufike katika ndoa, mchumba ninaehitaji awe na umri kati 49-55.

  Pia hii ni mara ya pli kukuandikia je naomba nikuulize nimekiuka maadili kwani sikupata maelezo yoyote kama nimekosea naomba muongozo.

  Ahsante.

  Napatikana kwenye email: siamini.sudi63@gmail.com

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Benki ya kiarabau kwa maendeleo ya Afrika BADEA wakati wajumbe hao walipomtembelea na kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam.(picha na Freddy Maro).

  0 0

  Mahmoud Ahmad,Arusha

  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Freeman Mbowe na Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini,Godbless Lema wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa ilikuweza kutoa ushahidi wa tukio la bomu lililotokea kwenye mkutano wa kampeni wa chama hicho.

  Viongozi hao wanashikiliwa baada ya Mwenyekiti huyo kudai anawajuwa waliolipua bomu na wanao mkanda wa tukio zima la ulipuaji huo wa Bomu kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Udiwani ulikuwa ufanyike Juni 16 jijini hapa.

  Akizungumza na wanahabari kwenye ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi mkoani hapa jana,Kamishna wa Upelelezi wa Jeshi hilo,Paul Chagonja alisema kuwa jeshi hilo linawataka viongozi hao waweze kuwasilisha ushahidi huo na kuwa kama hawatakubali kwa hiyari basi litawatafuta popote walipo.

  Kamishna Chagonja alisema kuwa ushahidi wa tukio hilo ni muhimu kwa amani ya nchi yetu na kuwa machafuko yanayotokea kwenye jiji hili hayakubaliki kwani nchi yeyote iliyoingia kwenye machafuko ilichangiwa na vyombo vya habari kuripoti kwa ushabiki badala ya kutumia taaluma.


  “Matukio ya ulipuaji wa mabomu kwenye nchi yetu hayakubaliki na kuwa mtu mwenye ushahidi wa tukio la bomu kwenye mkutano wa chadema atusaidie kuweza kufanya upelelezi wa tukio hili nawaombeni wanahabari kuacha ushabiki na kujikita katika taaluma yenu”alisema Chagonja.


  Wakati huo huo Mwili wa aliekuwa Katibu wa Kata ya Sokoni 1 wa Chama hicho,Marehemu Judith William Mushi imepelekwa kuzikwa kwenye kata hiyo kwa heshima zote za chama hicho wakiwemo wabunge mbali mbali wa chama hicho waliopo mkoani hapa baada ya mwenyekiti wao kuwataka kushiriki kwenye tukio hilo.

  Baadhi ya wabunge wa chama hicho waliopo mkoani hapa kushiriki msiba huo ni pamoja na mch.Peter Msigwa,Joseph Mbilinyi,Theresia Pareso,Ezekie Wenje,John Mnyika,na viongozi mbali mbali wa chama hicho kutoka makao makuu na mikoa ya jirani.

  Aidha baadhi ya wananchi waliongea na mwanahabari hii waliieleza kuwa tumekuwa tukitafuta vipaji vya riadha hapa nchini lakini kumbe wapo hadi wabunge wanaoweza kutuwakilisha vizuri nchi yetu na tukapata hadi medali akiwemo mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema.

  “unajua ndugu mwandishi mabomu sio mchezo yalimfanya mbunge kutimua mbio hadi maeneo ya sanawari hapa vipaji vipo ila hatujaweka mkazo kwenye kutafuta vipaji “alisema Yusuph.

  Msafara wa kuupeleka mwili wa katibu wa kata ya Sokon 1 ulipitia kwenye barabara za Sokoine kuelekea Esso hadi Pallotkwenye nyumba yake ya milele na kuhudhuriwa na wafuasi wa chama hicho wengi wakitembea kwa miguu umbali wa kilometa sita kutoka Hospital ya mkoa ya Mout Meru.

  0 0older | 1 | .... | 168 | 169 | (Page 170) | 171 | 172 | .... | 3272 | newer