Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 170 | 171 | (Page 172) | 173 | 174 | .... | 3285 | newer

  0 0
 • 06/21/13--04:25: GARI INAUZWA
 •  Make: IVECO 4x4
  Kilometer:  16000 - 20000
  Sitting capacity: 23 pamoja na dereva
  Extras: Ina fridge (chumba) kikubwa kinachoweza kuhifadhi jeneza.
  Price: Sh.55 milioni (mazungumzo yapo) bila dalali wala mpambe.
  Contact: 0784 400044

  0 0

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman ( wa pili kulia), Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Fakih Jundu (wa kwanza kulia),na Majaji wa Mahakama ya Rufani pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju wakiwa Katika picha ya pamoja na kundi la baadhi ya Mawakili wapya walioapishwa Leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania)

  0 0

  Na. Jeshi la Polisi Dodoma.

  Jeshi la Polisi Mkoa Dodoma linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumvamia na kumshambulia Mheshimiwa MOSES S/O MACHALI, miaka 31, Muha, Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia NCCR – Mageuzi wakati anaelekea nyumbani kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw. David. A. Misime alisema Tukio hilo limetokea tarehe 20/06/2013 majira ya 19.00 hrs katika eneo la Area ‘E’ katika Manispaa ya Dodoma.

  “alikutana na vijana wanne (4) walikouwa amesimama katikati ya barabara akapiga honi lakini hawakupisha. Aliamua kuwauliza “Jamani mnasimama katikati ya barabara si nitawagonga?” Nao wakamjibu: “Wewe si unajifanya mtto wa Mbunge, tutakupiga sasa”. Alisisitiza Kamanda Misime.

  Kamanda Misime alisema Mheshimiwa alipojaribu kupita vijana hao walipiga gari lake. kitu ambacho kilimfanya ashuke ili atazame kama gari hilo limepata uharibifu.wowote, ndipo vijana hao wakaanza kumshambulia kwa ngumi na mateke huku naye akijitahidi kujihami.

  Hata hivyo Bw.Misime alisema, walitokea vijana wawili (2) na kumsaidia. Mheshimiwa mbunge ambapo kijana mmoja kati ya waliokuwa wanamshambulia Mheshimiwa Machali ‘alimng’ata’ mgongoni kijana aliyekuwa anamsaidia Mheshimiwa Mbunge.

  Bw. Misime alisema Watuhumiwa baada ya kuona wamezidiwa nguvu walitimua mbio. Ambapo pia Mheshimiwa Machali aligundua kuwa simu yake ya mkononi wameondoka nayo vijana hao.

  Kamanda David. A. Misime alisema jeshi la Polisi mkoani Dodoma lilifanya Msako mkali ulifanyika usiku wa manane ambapo watuhumiwa wawili (2) walikamatwa ambao aliwataja kuwa ni JEREMIA LAWRENT MKUDE@ JERRY, Miaka 18, Mkaguru Mkazi wa Chaduru, Manispaa ya Dodoma. aliyekutwa akiwa na jeraha usoni alilopata wakati anapambana na Mheshimiwa Mbunge na vijana waliokuwa wanamsaidia.

  Kamanda huyo wa Polisi Mkoa wa Dododoma alimtaja mtuhumiwa mwingine anayeshikiliwa na jeshi la polisi kuwa ni CHARLES CHIKUMBILI, Miaka 22, Mkulima, Mkazi wa Swaswa, katika Manispaa ya Dodoma.

  Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Bw. David Misime alisema askari walipowafanyia upekuzi wa mwili watuhumiwa usiku huo wa manane wamekutwa na misokoto miwili (2) ya bhangi.

  0 0
 • 06/21/13--04:37: mapitio ya magazeti leo

 • 0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimuaga Sheha wa Shehia ya Tomondo Mohd Omar Said { Kidevu } anayekwenda Nchini India kwa Uchunguzi na Matibabu zaidi baada ya kumwagiwa Tindi kali usiku wa Tarehe 22 Mei 2013. Sheha Kidevu alikuwa akipatiwa huduma ya matibabu katika Hospitali Kuu ya Rufaa Mnazi Mmoja kwa takriban Mwezi mmoja baada ya tukio hilo.
  Sheha wa Shehia ya Tomondo Moha Omar Said Kidevu akitoa shukrani kwa SMZ kwa kufanikisha safari yake ya kwenda matibabuni Nchini India mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ambae hayupo pichani wakati alipokwenda kumuuga rasmi kwa safari hiyo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  Sheha wa Shehia ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Bwana Mohd Omar Said { Maarufu Kidevu } ameondoka Zanzibar kuelekea Nchini India kwa ajili ya Uchunguz na matibabu zaidi baada ya kumwagiwa Tindi kali { Acid } na mtu asiyejuilikana Usiku wa tarehe 22 Mei Mwaka huu wa 2013.

  Sheha Mohd Kidevu alikuwa akipatiwa huduma zamatibabu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kwa takriban Mwezi Mmoja sasa kutokana na kuathirika sehemu ya kulia ya kifua chake, Bega pamoja na baadhi ya maeneo ya mapaja.

  Mgonjwa huyo ameondoka na Ndege ya shirika la ndege la Oman kwa kupitia Muscut na amewasili Mjini Chenai Nchini India mapema leo tarehe 21/6/2013 saa 12.30 za asubuhi akiambatana na Daktari wake.

  Akimuaga sheha huyo hapo katika wadi yake ya Mapinduzi Kongwe Mnazi Mmoja Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alimuombea sheha Mohd Kidevu safari ya mafanikio itakayomletea hafaja njema.

  Bwana Mohd Kidevu alisema Mtu huyo alianza kutimua mbio baada ya kufanikiwa kufanya dhambi hiyo kitendo ambacho akalazimika kuomba msaada kwa wasamaria wema lakini hatimae ilishindikana kutokana na kuzidiwa kwa maumivu makali yenye kuchoma kama moto.

  Sheha huyo wa Shehia yaTomondo aliendelea kumfahamisha Balozi Seif kwamba hali yake hivi sasa inaendelea vyema na ameshaanza kupatamatumainikufuatiajicho lake kuanzakuonaingawabadoanakabiliwanamaumivukatikasehemuyakeyausoni.

  Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alimuomba Sheha huyo wa Tomondo kuwa na moyo wa subra wakati wa kipindi hichi kigumu cha huduma za matibabu.

  Balozi Seif alimuhakikishia Bwana Mohd Kidevu kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kufuatilia matibabu ya afya yake hadi atakapopata nafuu na kurejea nyumbani kuendelea na harakati zake za kimaisha kama kawaida.

  Naye sheha wa shehia ya Tomondo Mohd Omar Said { Kidevu } aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada zake zilizosaidia kufanikisha kwa safari yake ambayo imempa faraja kubwa.

  Sheha Kidevu alisema maumivu yaliyokuwa yakimkabili ndani ya wiki hii hasa wakati wa kula imepunguwa kidogo kufuatia huduma za karibu alizokuwa akipatiwa na madaktari wanaomuhudumia.

  Akizungumza na vyombo vya Habari nje ya Wodi ya Mapinduzi Kongwe hivi karibuni wakati alipomkagua sheha huyo kwa mara ya kwanza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali Kuu imesikitishwa na vitendo hivyo viovu vinavyoleta athari kwa Binaadamu.

  Balozi Seif alisema tabia hiyo mbaya inayoonekana kuanza kuchipua hapa Nchini ikibeba ufinyu wa imani inaanza kuleta hofu miongoni mwa wananchi katika kuendelea na harakati zao za kimaisha za kila siku.

  Alisema Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi itaendelea na uchunguzi wa kufuatilia matukio hayo na kamwe haitasita kuwachukulia hatua za kisheria kwa kuwafikisha katika mkondo wa sheria wale wote watakaobainika kuhusika katika vitendo hivyo.

  Hili ni tukio la tatu kuwahi kutokea la kumwagiwa watu tindili kali ndan ya mkoa wa mjini Magharibi likiwahusisha aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Ndugu Rashid Ali Juma pamoja na Katibu wa Fufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhil Suleiman Soraga.

  0 0

  Meneja wa Idara ya Malipo ya Kabla wa Vodacom Tanzania, Yvonne Maruma (katikati) pamoja na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu (kushoto) wakichezesha droo kubwa ya Promosheni ya Cheka Nao ambapo washindi watano walipatikana na kujishindia shilingi Milioni 2 kila mmoja,Promosheni hiyo inawawezesha wateja kuongea na mitandao yote bila mipaka kwa bei nafuu,na Ili kujiunga mteja anatakiwa kupiga *149*01#.akishuhudia ni Ofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania Bi.Chiku Saleh.
  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu akimpigia mmoja wa washindi miongoni ya watano waliojishindia shilingi milioni mbili kila mmoja kwenye droo kubwa ya Promosheni ya Cheka Nao,inayowezesha wateja kuongea na mitandao yote bila mipaka kwa bei nafuu. Ili kujiunga mteja anatakiwa kupiga *149*01#.wanaoshuhudia ni Meneja wa Idara ya Malipo ya Kabla wa kampuni hiyo, Yvonne Maruma (kati kati)pamoja na Ofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania Bi.Chiku Saleh.
  Meneja wa Idara ya Malipo ya Kabla wa Vodacom Tanzania, Yvonne Maruma (kati kati) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kuchezesha droo kubwa ya Promosheni ya Cheka Nao ambapo washindi watano waliojishindia shilingi milioni 2 kila mmoja,Promosheni hiyo inawawezesha wateja kuongea na mitandao yote bila mipaka kwa bei nafuu. Ili kujiunga, mteja anatakiwa kupiga *149*01#.wanaoshuhudia kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu (kushoto) pamoja na Ofisa wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini Bi.Chiku Saleh.

  0 0
 • 06/21/13--05:15: SHULE INAUZWA MKOANI GEITA
 •  MKURUGENZI WA KADI'S INVESTIMENT LTD ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA ANAUZA SHULE YAKE YA KADI'S ENGLISH MEDIUM PRIMARY SCHOOL ILIYOPO WILAYANI BUKOMBE MKOANI GEITA. 

  SHULE INAENEO LA HEKA KUMI LILOSAJILIWA KWA NAMBA 20588 L.O NAMBA 186857. INAVYUMBA VYA MADARASA KUMI OFISI YA UTAWALA NA YA WATUMISHI. KUNA BWENI LA KULAZA WANAFUNZI 150 AMBALO HALIJAKAMILIKA NA KUNA VIWANJA VYA MICHENZO.

  SHULE IMESAJILIWA KWA NAMBA SH.07/7/E.A001 TAREHE 2.12.2004 KWA SHULE YA AWALI NA NAMBA SH.07/7/001 KWA SHULE YA MSINGI. 

  KWA MAWASILIANO PIGA NAMBA 0713922890 na 0789499563.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wakazi wa jijini Tanga, wakati alipofika eneo la Pongwe jijini Tanga leo Juni 21, 2013 kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Viwanda katika eneo hilo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, linalosimamiwa na Wawekezaji kutoka nchini Korea Kusini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Juni 21, 2013 jijini Tanga. Kushoto kwa Makamu ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga Economic Corridor Ltd, Chris Incheul Chae.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa, Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga Economic Corridor Ltd, Chris Incheul Chae na viongozi wengine kwa pamoja wakifurahia baada ya Makamu kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Juni 21, 2013 jijini Tanga.


  0 0

  Dr. Asha-Rose Migiro
  NAIBU Katibu Mkuu Mstaafu wa Umnoja wa Mataifa, Dk. Ash-Rose Migiro amesifiwa kwa umahiri wa wake wa kutoingiza athari za kiingereza katika kiswahili, anapozungumza au kuhutubia, licha ya kuishi na kufanya kazi nje ya Tanzania kwa miaka mingi.

  Amesifiwa kwamba amekuwa akizungumza kiswahili fasaha kisichochanganywa na kiingereza, kwa athari za maneno au utamkaji kwenye mikutano ya hadhara au katika mazungunzo ya kawaida na watu.

  Sifa hizo zimetolewa leo na Mtaalam wa Kiswahili kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Mussa Kaoneka, katika kipindi cha lugha ya Kiswahili, kilichokuwa kikitangazwa na Kituo cha Radio One kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam.

  "Hizi athari zinatokana na watu wengi kupenda kutukuza mno lugha za wenzetu, na tatizo limekuwa likidhaniwa kwamba huenda ni kitokana na mtu kuwa ughaibuni kwa mda mrefu, lakini mbona wapo baadhi ya Watanzania ambao wamekaa na kufanya kazi kwa muda mrefu nje, lakini wakizungumza Kiswahili utasuuzika moyo kwa jinsi wanavyokienzi wanapoongea", alisema Kaoneka na kuongeza;

  "Mmoja wa Watanzania hawa naomba  nimtaje, ni Dk. Asha-Rose Migiro aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, huyu ukimkuta anazungumza kwenye mikutano ya hadhara hata kwa kutumia hotuba ambayo hakuiandika, huwezi kumsikia amechanganya hata neno moja la kiingereza katika mazungmzo yake au kuzungumza kwa haiba ya kizungu.

  Kaoneka alisema, mbali ya hotuba, hata katika mazungumzo ya kawaida Dk. Asha-Rose ambaye kwa sasa ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, akiamua kuzungumza kiswahili ni kiswahili fasaha kisicho na mchanganyiko wa neno la Kiingereza hata moja.

  Katika kipindi hicho kilichorushwa kuanzia saa mbili asubuhi, kikiongozwa na mtangazaji Lugendo Madege, walikuwa wanajadili athari mbaya na nzuri za lugha nyingine kwenye Kiswahili katika zama hizi za utandawazi.

  Walisema, athari nzuri ni pamoja na Kiswahili kuweza kupata maneno mapya hasa ya majina ya vitu na teknbolojia ambavyo kabla ya udandawazi havikuwepo Tanzania na hivyo kulikuwa hakuna majina rasmi ya kuvitaja na athari mbaya ni baadhi ya watu kuchukua maneno ya Kiingereza na kuyapa tafsiri  ya 'sisisi' ambayo yanakiharibu Kiswahili.

  Kaoneka aliyataja baadhi ya maneno yanayotokana na tafsiri za aina hiyo kuwa ni 'Mwisho wa siku' linalotokana na neno la Kiingereza 'at the end of the day' ambalo kwa mujibu wa mtaalam huyo tafsiri yake sahihi ni 'hatimaye', na mtu kusema "siku hizi nafanyakazi na Benki, wakati usahihi ni "nafanyakazi benki".

  Alifafanua kuwa kusema, "nafanyakazi na Benki" ikimaanisha kuajiriwa Benki, siyo sahihi, kwa kuwa kutamka hivyo kuna maanisha kwamba mhusika na benki wanafanya kazi pamoja. 
  IMEYATARISHWA NA BASHIR NKOROMO

  0 0

   Kutoka kushoto, katibu mkuu ofisi ya makau wa raisi bwana Sazi Salula, waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais Muungano mh. Samia Suluhu Hassan, mwenyekiti wa mkutano,Mh Ali Juma shamhuna waziri wa Elimu Zanzibar, akimuwakilisha  Wazri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa Rais zanzibar kama mwenyekiti mwenza katika kikao cha kamati ya pamoja cha Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya mapinduzi zanzibar cha kujadili changamoto za Muungano.
   Baadhi ya mawaziri wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar katika kikao cha pamoja cha kujadili changamoto za muungano mjini Dodoma Leo
  Baadhi ya wakurugenzi kutoka Ofisi ya makamu wa rais wakifuatilia mazungumzo katika kikao cha pamoja cha kujadili changamoto za muungano kinachoendelea mjini Dodoma. Picha zote na Evelyn Mkokoi

  0 0


  TUNAHITAJI MADEREVA WAWILI WA MAGARI MAKUBWA
  GOOD NEWS FOR TANZANIA
  HUDUMA MPYA YA KIFURUSHI 
  NEW DOOR TO DOOR SERVICE
  TUNACHUKUA MZIGO MLANGONI KWAKO UK NA TUTAUFIKISHA MLANGONI KWAKO DAR
  UKILIPA HAPA UK HAULIPI TENA DAR, SISI TUTAKULETEA MZIGO NYUMBANI KWAKO!
  Baada ya kushughilikia kwa kina mapungufu yaliyojitokeza mwanzo, 
  sasa tumerudi na huduma ya kifurushi tena ikiwa imeboreshwa zaidi.
  BEI ZETU KAMA KAWAIDA HAZINA KIGUGUMIZI NA SI ZA KUUMIZA

  AIR CARGO TO DAR NOW £3.50 INCLUSIVE CLEARANCE!
  AIR CARGO TO ZANZIBAR NOW £3.00 INCLUSIVE CLEARANCE!
  AIR CARGO TO NAIROBI/MOMBASA NOW £2.80 INCLUSIVE CLEARANCE!
  KIFURUSHI KWA KONTENA DAR/ZANZIBAR NOW £2.20 INCLUSIVE CLEARANCE!
  NDEGE ZINAONDOKA KILA WIKI MARA MBILI
  MZIGO WOWOTE LETE TU
  MINIMUM WEIGHT IS 40KILOS
  KAMA UNATAKA KUAGIZA KITU AU KUFANYA BOOKINGS TUWASILIANE KWA NAMBA HAPA CHINI
  40'HC CONTAINER TO DAR/MOMBASA £1,800
  CHEZEA SERENGETI WEWE!
  CHRIS LUKOSI +44 07903828119  & 07404279633 
  SIMON LOUIS (MOHSIN) +44 07950689243
  HASSAN   +44 07404672873
  HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
  Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477

  0 0

  Wakazi wa Mkungugu tarafa ya  Isimani  wilaya ya  Iringa vijijini  wakipita  jirani na mnala  wa aliyekuwa mkuu  wa mkoa  wa Iringa marehemu Dkt.  Wilbert Kleruu  aliyeuwawa kwa  kupigwa  risasi na marehemu Saidi Mwamwindi  ambayeb aliyehukumiwa  kunyongwaPicha na Francis 

  0 0

   Mshindi wa Redds Miss Kinondoni 2013, Lucy Tomeka akivalishwa taji lake na mrembo aliyekuwa akilishikilia taji hilo Redds Miss Tanzania 2012/2013, Bright Alfred. Lucy Tomeka aliweza kuchukua taji hilo kwa kuweza kuwagalagaza wenzake wapatao 12 katika kinyang'anyiro hicho kilifanyika jana ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip jijini Dar.    
   Akivalishwa utambulisho wake.
   Showlove...
   Warembo waliofanikiwa kuingia katika tano bora wakifurahia kwa pamoja, katikati ni Redds Miss Kinondoni 2013 Lucy Tomeka, (shoto kwake) ni Prisca Clement, (kulia kwake) ni Phillios Lemi. Wengone ni Sarah Paul (kwanza kulia) na Linda Joseph (kwanza kushoto).

    Tatu bora ni katikati ni Redds Miss Kinondoni 2013 Lucy Tomeka, (shoto kwake) ni Prisca Clement, (kulia kwake) ni Phillios Lemi. 

  0 0
 • 06/22/13--02:53: lango kuu la mji wa singida
 • Unapoingia mji wa Singida ukitotokea Babati unakaribishwa na majabali haya ambayo wajenzi wa barabara wameamua kuyaacha ili kupendezesha mandhari na kutunza mazingira halisi. 

  0 0


  Na Vicky Kimaro, Mwananchi

  Dar es Salaam. “Madaktari waliponiambia kuwa watoto wangu wameungana nilichanganyikiwa, niliona dunia imenigeuka, sikuwahi kuwaza nitakutana na kitu cha namna hii katika maisha yangu.”
  Ni maneno ya binti kutoka kabila la Wandali ambalo asili yake ni Mbeya, Grace Joel (19), ambaye Februari 20 mwaka huu, alijifungua mapacha wa kiume ambao wameungana katika sehemu ya kiunoni.
  Mwanadada huyo anasema hakuamini macho yake pale madaktari wa Hospitali ya Uyole iliyopo mkoani humo walipomwambia kuwa watoto wake wameungana na hivyo kupewa rufaa ya kwenda kwenye Hospitali Kuu ya Mkoa wa Mbeya.
  "Wakati wa ujauzito wangu sikuwahi hata siku moja kuhisi kuwa ningeweza kuzaa watoto wakiwa kwenye tatizo hili, sikuwahi kuumwa zaidi ya kuvimba miguu tu na  hiyo ni hali ya kawaida kwa mjamzito yeyote." anasema Grace ambaye kwa sasa anahitaji msaada wa hali na mali ili kuokoa maisha ya watoto wake.
  Licha ya umri huo mdogo, amejikuta kwenye hali ya mateso na uchungu mwingi baada ya familia yake, hususani mume wake, Erick Mwakyusa kumtelekeza kwa kile alichodai kuwa hana haja na watoto walioungana.

  Kwa msaada ili kuokoa maisha ya 
  watoto hawa piga namba 


  0 0

   Kamera Man wa Globu ya Jamii,leo amefanikiwa kuzinasa taswirazz hizi za Wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga katika Mataa ya Kuongozea Magari,Ubungo Jijini Dar.Vijana wengi hapa mjini,wamekuwa  wakijishughulisha na kazi mbali mbali ili kuweza kujikimu kimaisha.
   Hapa ni Machinga akiuza mipira ya kucheza.
  Mishale na mikuki yake pia inapatikana Ubungo Mataa.

  0 0

  Meza kuu wakati wa hafla hiyo
  Spika wa bunge Anne Makinda akizungumza katika hafla ya kumuaga Spika Mstaafu Samuel Sitta kwenye viwanja vya bunge Mjini Dodoma juni 21, 2013.
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na Mheshimiwa Dr. Maua Daftari ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya hafla ya kumuaga Spika wa zamani,Mh. Samuel Sitta kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 21, 2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi zake pichani kwa Spika mstaafu. Samuel Sitta katika hafla ya kumuaga Spika huyo kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 21, 2013.Kushoto kwake ni mkewe Tunu na wengine kutoka kulia ni Mke wa Spika wa Zamani Margareth Sitta, Spika wa zamani Samuel Sitta na Spika wa Bunge Anne Makinda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0
 • 06/22/13--05:03: Article 15

 • 0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almas Kassongo (kushoto) akimkabidhi Sh 500,000, Meneja wa Friends Rangers, Shaaban Marsila mara baada ya timu hiyo kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa.

  TIMU ya Friends Rangers ya jijini Dar es Salaam imetamba kuibuka na ushindi dhidi ya Stand United ya mkoani Shinyanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa (RCL) itakayochezwa kesho Juni 23 kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi.

  Akizungumza leo hii Juni 22, Meneja wa Friends Rangers, Shaaban Marsila alisema wamejipanga vyema kuhakikisha wanashinda mechi hiyo ili iwe rahisi kwao katika mechi ya marudiano itakayochezwa Juni 30.

  “Kikubwa mabacho naweza kusema ni kwamba timu imendaliwa vizuri kwa ajili ya kushinda na mechi dhidi ya Stand United, tunaamini tukishinda mechi hiyo itakuwa rahisi kwetu katika mechi ya marudiano.

  “Tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kwenye Uwanja wa Azam Complex kuishangilia kwa nguvu timu yao ili ipate ushindi,” alisema Marsila.

  Friends Rangers ndio timu pekee iliyosalia katika ligi hiyo ya mabingwa kutoka jijini Dar es Salaam huku timu za Abajalo na Red Coast zikiaga mashindano hayo ambayo timu tatu zitafuzu kucheza Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.

  Katika kuelekea katika mechi hiyo, tayari Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kupitia kwa Ofisa Habari wake, Mohamed Mharizo kimeitakia kila la kheri Friends Rangers ili iweze kuibuka na ushindi dhidi ya Stand United.

  “Kwa niaba ya DRFA nachukua fursa hii kuwatakia kila la khri Friends Rangers katika mechi hiyo, kwani wamekuwa wawakilishi wetu wazuri na naamini wataendelea kutuwakilisha vyema,” alisema Mharizo.

  0 0
 • 06/22/13--05:18: Matofali yakipigwa sop sop
 •  Mdau akipiga sop sop Matofali ikiwa ni sehemu ya kuyafanya yaimarike,kwani bila hivyo tofali ni sawa na bure kabisa.


older | 1 | .... | 170 | 171 | (Page 172) | 173 | 174 | .... | 3285 | newer