Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

MAMIA YA WAKAZI WA KIGOMA WAJITOKEZA KUPATA MATIBABU YA MADAKTARI BINGWA.

$
0
0
 
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma.


MAMIA ya wananchi wa mkoa Kigoma wamejitokeza katika kupata matibabu kutoka kwa madaktari bingwa katika mpango unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa bima ya afya nchini (NHIF).

Matibabu hayo yanayotolewa katika hospitali ya mkoa Kigoma Maweni yanahusisha magonjwa ya kina mama ,magonjwa ya moyo,magonjwa ya watoto ambayo madaktari bingwa wake watafanya kazi hiyo moja kwa moja huku magonjwa mengine ambayo hayana madaktari bingwa utatolewa ushauri wa hatua za kuchukua.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya mfuko huo,Anne Makinda alisema kuwa hakuna mtanzania atakayekufa kwa sababu ya kukosa pesa za matibabu kutokana na serikali kuweka mfumo mzuri unaohakikisha wananchi wote wanapata matibabu kwa gharama nafuu.

Makinda alisema kuwa kwa sasa wananchi wote wataweza kujiunga na huduma za matibabu za mfuko huo kupitia makundi mbalimbali yalipo kwenye jamii na mitaa na wananchi watapata huduma za matibabu nchi nzima bila kubagua hospitali.

Alisema kuwa pamoja na hilo mfuko huo unatambua kuwepo kwa changamoto za uhaba wa madawa,vitendea kazi,uchache wa majengo na vifaa vingine vya kutolea tiba na kwamba mfuko huo umzingatia changamoto hiyo na kwa sasa mfuko unatoa mikopo kwa vituo vya afya,zahanati na hospitali ili kuwezesha huduma bora kupatikana wakati wote.
 Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa bima ya afya(NHIF) Anna Makinda akiongea na mmoja wa wagonjwa waliofika katika hospita ya Mkoa wa Kigoma (maweni) kwa ajili ya kupata huduma za madaktari bingwa. 
 Anna Makinda ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya bima ya afya (NHIF) akiongea na wagonjwa waliofika leo hospital ya Mkoa wa kigoma kwaajili ya kupata matibabu toka kwa madaktari bingwa.
 Anna Makinda akikata utepe katika hospitali ya Mkoa wa Kigoma kuzindua zoezi la utoaji wa huduma kwa madaktari bingwa kwa hospitali za pembezoni.


TRA Yatoa siku 39 kodi ya majengo iwe imelipwa Mwanza

$
0
0

Na Atley Kuni- Afisa habari Mwanza.

Mamlaka ya mapato nchini imetoa muda hadi kufikia  Juni 30, mwaka huu wananchi wote wanaodaiwa kodi ya majengo kuhakikisha wanailipa kodi hiyo ilikuepuka kufikishwa mahakamani na kutozwa faini.

Kauli hiyo imetolewa na kamishina mkuu wa TRA nchini ndugu Charles Kichere, alipokuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Mwanza hii leo.

“Mwisho wa kulipa kodi ya majengo bila adhabu ni tarehe 30 Juni, 2017. Hivyo wenye majengo yaliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana), na Manispaa ya Ilemela wafike ofisi za TRA zilizopo karibu nao kuchukua ankara zao endapo hawajazipokea kutoka kwa viongozi wa serikali za mitaa yao au kujisajili  na kulipa kupitia benki yoyote ya biashara” alisema Kichere. 

Kichere amefafanuakuwa kwa walioko sehemu ambazo nyumba zimethaminishwa watalipa kiwango cha asilimia ya thamani ya jengo kama inavyoonesha kwenye ankara zao na walioko maeneo ambayo hayajapimwa au kuthaminishwa watalipa viwango maalum vilivyopitishwa na mabaraza ya madiwani na kutangazwa na TRA kwenye vyombo vya habari.

Kichere amevitaja viwango hivyo vilivyopitishwa kuwa, ni shilingi za kitanzania (20,000) kwa Jiji la Mwanza na kumi na tano elfu (15,000) kwa Manispaa ya Ilemela. 
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akiogea katika kikao hicho cha TRA na Waandishi wa habari Jijini Mwanza, katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Kamishna Mkuu wa TRA nchini,Charles Kichere, akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani ( Picha zote na Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza)
 Viongozi wa Tanzania Chamber of Commerce Mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Kamishna wa TRA nchini wakati wa kikao hicho na waandishi wa habari Mkoani Mwanza.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UHALIFU UNAOVUKA MIPAKA KUJADILIWA ARUSHA.

$
0
0
Na. Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Arusha.

Mkutano mkuu wa  mwaka wa Shirikisho la wakuu wa Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) unatarajia kufanyika Jumatano Mei 24, 2017 mkoani Arusha chini ya mwenyekiti wa Shirikisho hilo kwa kipindi hiki ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu. 

Taarifa iliyotoilewa na Msemaji wa Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Advera Bulimba imesema mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba na utahudhuruwiwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi kutoka SADC na wale wa Shirikisho la Polisi wa kimataifa INTERPOL ambapo tayari kamati tendaji za shirikisho hilo zinaendelea na mikutano yake kwa ajili ya maandalizi ya mkutano huo mkuu.

Bulimba alisema katika mkutano huo mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo jinsi ya kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kwa kufanya Operesheni za pamoja katika kubaini na kukabiliana na makosa  mbalimbali yakiwemo  dawa za kulevya, wizi wa magari, usafirishaji haramu wa binadamu na ugaidi.

“Vilevile, mkutano huu utajadili utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa na Wakuu wa Upelelezi wa SARPCCO pamoja na kamati tendaji za sheria, Mafunzo na kamati tendaji ya Jinsia na watoto baada ya mkutano wao uliofanyika mwezi Machi mjini Bagamoyo” Alisema Bulimba.

SARPCCO iliundwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu. Shirikisho hilo linaundwa na Nchi kumi na tano ambazo ni Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Lesoto, Mauritius, DRC, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Madagascar na Syshelis.
 Naibu Inspekta jenerali wa polisi, Abdulrahmani Kaniki, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kamati tendaji za shirikisho la wakuu wa polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika, (SARPCCO)  ikiwa ni maandalizi ya mkutano mkuu wa mwaka wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika  jumatano tarehe 24/05/2017 mkoani Arusha. 

Baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji za shirikisho la wakuu wa polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika, (SARPCCO) wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kamati hizo ikiwa ni maandalizi ya mkutano mkuu wa mwaka wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika  Jumatano tarehe 24/05/2017 mkoani Arusha. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi

MTULE AMCOS WAJIPANGA KUCHANGAMKIA FURSA ZA TADB

$
0
0

Na mwandishi wetu, Zanzibar.

Chama cha Ushirika cha Msingi cha Masoko cha Mtule (Mtule AMCOS) kinachojishughulisha na kilimo cha mbogamboga na matunda  kimeweka bayana nia yake ya kuchangamkia fursa za mikopo nafuu inayotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kuwasaidia katika kuendeleza kilimo chao.

Akizungumza wakati ugeni kutoka TADB ulipotembelea kijijini Mtule, Mwenyekiti wa Mtule AMCOS, Mzee Mgana Zidi Khamis amesema kuwa Chama chake kimejidhatiti katika kufikia soko kubwa la matunda na mboga mboga ila wanarudishwa nyuma na uduni wa mtaji pamoja miundombinu ya masoko.

“Tulisikia uwepo wa Benki ya Kilimo ila hatukuwa tunajua namna ya kuwapa, leo tunaamini kuja kwenu kijiji hapa kumefufua matumaini yetu ya kupatiwa mikopo ili kuongeza tija kilimo chetu na kipato chetu kwa ujumla,” alisema.

Akiwasilisha malengo ya safari yao na umuhimu wa Benki hiyo kwa wakulima nchini, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi katika  kilimo nchini.
 Katibu wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Masoko cha Mtule (Mtule AMCOS), Bw. Ali Fadhil Ali akiongea wakati Benki ya Kilimo ilipotembelea Kijiji cha Mtule kukagua miradi ya kilimo inayohitaji mikopo.
 Mwenyekiti wa Mtule AMCOS, Mzee Mgana Zidi Khamis (kulia) akiwaonesha eneo linaloendelezwa la Chama chao linalojengwa kwa michango wa wanachama. Alioongozana nao ni Mjumbe wa Bodi ya TADB, Bw. Hussein Mbululo (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati).
 Mjumbe wa Bodi ya TADB, Bw. Hussein Mbululo (kushoto) akitoa ushauri kwa Mwenyekiti wa Mtule AMCOS, Mzee Mgana Zidi Khamis (kulia) kuhusu uendelezaji wa miundombinu ya Ofisi ya Chama.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Wanawake na Vijana wapewe Zabuni – Dc Daqaro

$
0
0
Na Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqaro amesema wanawake na vijana wanaokidhi vigezo wapewe Zabuni za Halmashauri ya Jiji ili kuweza kuwainua kiuchumi na kuboresha maisha yao kwa kazi mbalimbali zinazotolewa kila mwaka.

Daqaro ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wanawake na vijana ambao ni wajasiriamali wanaonufaika na mikopo yenye riba nafuu kutoka Jiji ambayo hutolewa kwa mujibu wa sheria.

 “Ni wakati wa wanawake na vijana kuchangamkia fursa mbalimbali katika Jiji la Arusha ikiwa ni pamoja na zabuni ambazo zitasaidia kuinua mitaji na kuongeza pato la familia zenu, hizi kazi ni zenu hakikisheni mnafuata taratibu zote ili mzichukue wasije watu toka mbali wakapewa wakati ninyi ambao ni wakazi wa Mji huu mkakosa kwa kukosa vigezo vidogo watumieni wataalamu wa Jiji wawaelimishe”amesema Daqaro.

Wakati akisema hayo Mkuu wa Wilaya Mhe. Daqaro amekabidhi hundi za mfano ya Tsh Mil 390 kwa vikundi vya wanawake 78 huku vikundi vya vijana 67 vimekabidhiwa hundi ya Tsh Mil 336.

Mhe. Daqaro amesema kuwa kutokana na changamoto iliyoko katika taasisi za fedha ambazo hutoa mikopo kwa riba kubwa na kuhitaji dhamana ya nyumba na ardhi jambo ambalo linawakwamisha wakopaji hivyo Serikali imeamua kutoa mikopo ya masharti nafuu ambayo ni asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri.

Pia amewasihi wanufaika wa mikopo hii kuwa mikopo itumike katika malengo maalumu na katika miradi inatakayoleta tija kama vile uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo ambavyo vitasaidia kutengeneza ajira na kukuza uchumi.

Kwa upande wao kinamama na vijana waliopokea mikopo hiyo wamesema kuwa mikopo hiyo itawainua kiuchumi na kuwawezesha kufanya shughuli za uzalishaji mali na kuachana na kuwa tegemezi pamoja na matumizi ya dawa za kulevya  na wizi.

Mpaka kufikia robo ya tatu Machi 2017 Halmashauri ya jiji la Arusha imetoa mikopo ya Tsh Bil 1.3 kwa ajili ya wanawake  na vijana kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.

  Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Fabian Daqarro (katikati) akifungua mafunzo ya wajasiriamali yanayoenda sambamba na utoaji wa mikopo ya wanawake na vijana kwa robo ya tatu.

Mkurugezi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia (tatu kulia) akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo kwa wajasiriamali ambao ni wanufaika wa mikopo ya Halmashauri ya Jiji kwa robo ya tatu.

  Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Fabian Daqarro (katikati) akiwakabidhi hundi ya mfano ya Tsh Mil 390 kwa vikundi vya wanawake Jiji la Arusha.
 Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Fabian Daqarro (katikati) akikabidhi hundi ya mfano ya Tsh Mil 336 kwa vikundi vya vijana, Jiji la Arusha.
 Washiriki wakifuatilia mafunzo ya ujasiriamali kabla ya kukabidhiwa mikopo ya riba nafuu toka Jiji la Arusha.

DC UBUNGO MHE KISARE MAKORI AAGIZA KUJENGWA DARAJA LA MBEZI MSUMI

$
0
0
Na Nasri Bakari, Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori Leo Jumamosi, Mei 20, 2017 ameagiza kujengwa kwa daraja  jipya kutokana na kuharibika kwa daraja la awali katika eneo la Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam.
Agizo hilo amelitoa mapema hii leo wakati akizungumza Na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa Hadhara uliowajumuisha pia Mtendaji wa Kata,  wajumbe wa mitaa na wataalamu mbalimbali kutoka Manispaa ya Ubungo.
Mhe Makori amesema kuwa amejionea adha  iliyopo katika daraja hilo ambapo sio ubovu wa miundombinu pekee bali pia ni swala la usalama hasa kwa watoto wanaopita katika daraja hilo waendapo shuleni na sehemu mbalimbali.
"Mimi kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika Wilaya hii sitojisikia vizuri kuona tunahatarisha maisha ya binadamu kwa namna yoyote ile, lazima nihakikishe mnakuwa salama wakati wote" 
"Hivyo nakuagiza Mkurugenzi kuanza haraka ujenzi wa daraja hili ambalo kwa kiasi kikubwa litasaidi wananchi Wetu hawa  kupita kwa usalama zaidi" Alisema Mhe Makori.
Aidha amesisitiza kuwa kodi zinazokusanywa na serikali  ni kwa ajili ya kugharamia na kuimarisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kama vile kuboresha Sekta ya Elimu, Afya na huduma nyingine za kijamii, hivyo ni lazima  serikali ishughulikie na kusimamia mahitaji ya Msingi kwa wananchi wake.
Sambamba na hayo pia Mhe Makori amewaomba wananchi kufika kwa viongozi wao pindi wanapopata kadhia mbalimbali zinazowasumbua katika jamii inayowazunguka kwani wameajiriwa kwa ajili yao na serikali ya awamu ya tano inajali wananchi wote hususani wanyonge.
Kwa upande wake Injinia wa Ujenzi Manispaa ya Ubungo Ndg Goodluck Mbanga amesema kuwa daraja lililokuwa limejengwa awali lilikuwa Dogo ukilinganisha Na wingi wa Maji Jambo lililopelekea kuharibika haraka.
Mbanga Alisema utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Wilaya nitaanza haraka iwezekanavyo ili kufikia mwanzoni mwa mwaka 2018 lianze kutumiwa Na wananchi hao ambao wamepata adha kubwa kwa muda mrefu.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Msumi Ndg Hemed Abdallah Gulamu amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwa Kazi kubwa anayoifanya tangu alipoteuliwa kuongoza Wilaya hiyo.
Pia amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa ufanisi katika utendaji Na kusema kuwa uongozi wake utaacha alama kubwa na kukumbukwa na watanzania wote.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisikiliza malalamiko ya wananchi wa Mtaa wa Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam wakielezea adha wanayokumbana nayo kutokana na uharibifu wa Daraja
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori  sambamba na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Ally wakikagua daraja lililovunjika eneo la Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam.
Muonekano wa Daraja la Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam likiwa limeharibika
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA
 

Marriott International to Debut The Ritz-Carlton in the Zanzibar Archipelago

$
0
0

DUBAI, United Arab Emirates, May 22, 2017/ -- Marriott International (NASDAQ: MAR) (www.Marriott.com) today announced the signing of an agreement with Pennyroyal Gibraltar Limited, to debut The Ritz-Carlton brand (www.RitzCarlton.com) in the exotic Zanzibar Archipelago. 

Slated to open in 2021, the 90 room all-suite and villa resort will bring the defining luxury experience of The Ritz-Carlton to one of the most magical destinations in the world. Located within a convenient 45-minute drive from Zanzibar International Airport, The Ritz-Carlton, Zanzibar will provide easy access to the fabled and magnificent UNESCO World Heritage Site, Stone Town, often referred to as the cultural heart of Zanzibar. 

The signing of The Ritz-Carlton, Zanzibar took place at an intimate ceremony attended by the owners, Mr. Saleh Said and Mr. Brian Thomson, Directors of Pennyroyal Gibraltar Limited and Mr Alex Kyriakidis, President and Managing Director, Middle East and Africa, Marriott International, along with other executives from both companies.
.Mr. Saleh Said, Directors of Pennyroyal Gibraltar Limited and Mr Alex Kyriakidis, President and Managing Director, Middle East and Africa, Marriott International, along with other executives from both companies.

UTEUZI: ADOLF HYASINTH MOHONDELA NDUNGURU TEULIWA KUWA NAIBU KAMISHNA MKUU TRA


WAKULIMA WA NDIMU BWEJUU, ZANZIBAR, WALILIA SOKO

$
0
0
Umoja wa Wakulima wa Ndimu wa Kikundi cha Juhudi Zetu kilichopo Bwejuu, mjini Unguja wametoa kilio chao cha kukosa soko la ndimu wanazozalisha kwa uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).
Wakizungumza na ugeni huo, wakulima hao wamesema kwa muda mrefu sasa wamekosa soko la uhakika la mazao yao kwa kukosa mnunuzi wa uhakika licha ya kulima kisasa na kupata mazao mengi.
Mmoja wa wakulima hao Bw. Shafi Hamadi Mussa amesema kuwa kwa muda mrefu sasa wamekosa soko la uhakika la mazao ya hali inayorudisha nyuma ari ya kuendelea kulima zao hilo.
“Tunakatishwa tamaa kwa kukosa soko la uhakika licha uwekezaji mkubwa tunaoufanya katika kulima kisasa,” Bw. Mussa alisema.
Bw. Mgana Khatibu Mgana, mkulima mwengine wa Umoja huo amesema changamoto ya ukosefu wa masoko inaweza kutatuliwa kwa kupatiwa mkopo nafuu wa kununulia mitambo ya uchakataji wa mazao ambayo itatumika kuongeza thamani kwa mazao yao.
 Ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wakikagua mashamba ya midimu wakati walipotembelea mashamba ya Umoja wa Wakulima wa Ndimu wa Kikundi cha Juhudi Zetu kilichopo Bwejuu, mjini Unguja.
 Ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wakikagua mashamba ya midimu wakati walipotembelea mashamba ya Umoja wa Wakulima wa Ndimu wa Kikundi cha Juhudi Zetu kilichopo Bwejuu, mjini Unguja.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akioneshwa miundombinu ya umwagiliaji ya kilimo cha ndimu. Anayemuonesha ni Bw. Mgana Khatibu Mgana na (kushoto) na Bw. Kombo Haji Mussa (katikati).
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akiangalia namna midimu inavyomwagiliwa maji.
Meneja wa Mikopo wa TADB, Bw. Samuel Mshote (kushoto) akiangalia ndimu zilizoanguka kwa kukosa wateja. Kwa mujibu wa wakulima wa ndimu, ndimu huuzwa ikiwa katika hali ya kijani lakini changamoto za kukosa soko hupelekea ndimu za wakulima wa Kijiji cha Bwejuu kuivia mtini. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

SERIKALI KUFUTA TOZO 108 KATIKA KILIMO,MIFUGO NA UVUVI - MHE.WILLIAM OLE NASHA

SERIKALI YAIHAKIKISHIA SEKTA BINAFSI KUENDELEA KUPATA MIKOPO

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LEO TAREHE 22.05.2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 31, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 22, 2017

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Andrew Chenge akiongoza  kikao cha thelathini na Moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 22, 2017.
 Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha thelathini na Moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 22, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo na Naibu wake Mhe.Anthony Mavunde katika  kikao cha thelathini na Moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 22, 2017.

 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe.Martha Mlata akiuliza swali katika  kikao cha thelathini na Moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 22, 2017.
Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi akizungumza jambo na Mbunge wa Kawe Mhe.Halima Mdee katika  kikao cha thelathini na Moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 22, 2017. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

CANDY IMAX KURUDISHA HADHI YA BONGO MOVIE

$
0
0
BAADA ya kuonekana hali ya kuashiria kupoteza mvuto kwenye tasnia ya filamu hapa Bongo, hatimaye Candyimax imekuja kwa kasi ya kurudisha hadhi ya filamu za hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Kupitia ‘Candyimax online streaming Tv’ imetoa fursa kwa kiwanda cha filamu hapa nchini na wadau wote kupeleka miongozo ya filamu (script)  mbalimbali ambazo zitakuwa kwenye ubunifu wa hali ya juu na kuhakikisha wanafanya kazi nzuri zenye viwango ambazo zitaipeleka tasnia hiyo kimataifa.

Katika kutilia mkazo suala hilo Candyimax Tv imejipanga kugharamia muongozo wa filamu (script) ambazo zimepitishwa na uongozi wa Tv hiyo yenye mpango na kusudio kubwa la kuinasua tasnia hiyo ambayo haifanyi vizuri sokoni kwa sasa.

Pia mfumo huo mpya wa kuangalia Tv hiyo online utasaidia filamu hizo kuonekana duniani kote,kwa wahusika wa tasnia hiyo wanatakiwa kuwasilisha kazi zao (script) ofisi zao zilizopo Masaki,barabara ya Umoja wa Mataifa,na kwa mawasiliano zaidi wapigie kwa namba +255765802457.
Baadhi ya wadau wa filamu wakiwa kwenye harakati za maandalizi ya movie mpya


HATUA ZA KUFUATA BAADA YA KUACHWA NA NDEGE

$
0
0

Na Jumia Travel Tanzania
Ni jambo la kawaida kuachwa na usafiri kama vile basi, boti, treni au ndege licha ya kufanya maandalizi ya kutosha. Baadhi ya sababu zinazoweza kuchangia mtu mpaka kuachwa na usafiri ni kama vile foleni barabarani, ajali au usafiri kupata matatizo na kukosea muda wa kuwasili.
Hali ya kuachwa na usafiri ni ngumu sana kama haijawahi kukutokea kabla na hauna mbinu mbadala ya kukuwezesha kusafiri kama ulivyokukusudia. Zipo hatua kadhaa za kufuata pindi uchelewapo ndege ambazo Jumia Travel ingependa uzifahamu na kuzizingatia pindi utakapokumbwa na changamoto kama hii.
Wasiliana na shirika la ndege unalosafiri mara moja. Kitu cha kwanza kabisa baada ya kugundua kwamba utachelewa au umechelewa ndege ambayo ulitakiwa kusafiri nayo ni kuwasiliana na shirika husika. Mara nyingi mawasiliano huwemo kwenye tiketi au tovuti ya shirika. Kwa kufanya hivyo utajua ni msaada gani wanaweza kukupatia kulingana na hali uliyopo.

wateja wote wa Airtel money kaeni tayari kupokea gawio kwa kutumia Airtel money!

$
0
0
Mambo vipi! Mr. Money anarejesha gawio la Tshs billioni 3.1 kwa wateja wote wa Airtel money. Hivyo basi kaa tayari kupokea gawio lako kwa kutumia Airtel money. Endelea kutumia na kufurahia huduma za Airtel money Piga*150*60#  FOLLOW: @airtel_tanzania

UJUMBE KUTOKA KWA OFIS YA MAKAMU WA RAIS

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MAY 23,2017

Muchunguzi: Kuogopa kucheza Biko ni dalili ya kukaribisha umasikini

$
0
0
MSHINDI wa droo ya saba ya Sh Milioni 10 kutoka kwenye Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Sospeter Muchunguzi, amekabidhiwa fedha zake huku akisema kuwa kuogopa kucheza Biko ni dalili ya kukaribisha umasikini.



Muchunguzi aliyasema hayo jana katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam wakati anakabidhiwa fedha zake na Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage.



Akizungumza kwa msisitizo mkubwa, Muchunguzi mwenye ndoto za ujasiriamali alisema kwamba watu wote waliofanikiwa katika maisha yao walithubutu katika mambo waliyokusudia kuyafanya, hivyo ni budi kila mmoja kupita njia hiyo.
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, kulia akimkabidhi nyaraka halali za Benki ya NMB zinazoonyesha kuingizwa kwa fedha za mshindi wao Sospeter Muchunguzi pichani kushoto jumla ya Sh Milioni 10 alizoshinda katika Bahati Nasibu yao ya Ijue Nguvu ya Buku, droo iliyochezeshwa Jumapili. Makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini Dar es Salaam.
Sospeter Muchunguzi katikati akisaini nyaraka za benki ya NMB kwa ajili ya fedha zake kuingizwa kwenye akaunti yake katika benki hiyo jana baada ya kuibuka kidedea katika droo ya Biko ya Sh Milioni 10. Kulia ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko Grace Kaijage na kushoto ni Afisa wa NMB.


Alisema uhakika wa kushinda ni mkubwa ikiwa mtu ameamua kweli kuingia katika sekta ya michezo ya kubahatisha, hususan mchezo wa Biko ambao hata uchezaji wake upo wazi na hakuna dalili zozote za kudanganya washindi.



“Nilipoona utaratibu wa Biko ni mzuri nikathubutu kucheza huku nikiamini kwamba endapo naweza kuibuka na ushindi naweza kusogea katika hatua moja kwenda nyingine hivyo Watanzania wenzangu hakuna haja ya kuogopa ili tusonge mbele.



“Nimefurahi kupata fedha hizi kutoka Biko maana hata uchezaji wao kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo, Vodacom na Airtel kwa kuandika kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kumbukumbu namba ya 2456 ni rahisi hali inayoweza kumfanya kila mtu amudu kucheza mahala popote na wakati wowote,” Alisema Muchunguzi.



Naye Grace Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, aliwataka Watanzania kila pembe za nchi kucheza kwa wingi ili wajiwekee mazingira ya kushinda zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazotoka kila wakati, huku pia donge nono la Sh Milioni 10 likitolewa katika droo ya Jumatano na Jumapili.



“Lengo letu ni kutoa zawadi nono kwa kila mshindi wetu, hivyo umnachotakiwa kufanya ni kucheza Biko kwa wingi kwa kununua tiketi kuanzia Sh 1000 na kuendelea ili mshinde, maana kucheza mara nyingi zaidi ndio njia ya kufanikisha ushindi,” Alisema Grace na kuongeza kuwa tiketi moja inatoa nafasi mbili, ikiwamo ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na nafasi ya kuingia kwenye droo ya kuwania Sh Milioni 10.



Kwa mujibu wa Grace, washindi wao wanaoshinda zawadi za papo kwa hapo wanatumiwa fedha zao kwa kupitia simu walizocheza na wale wa droo kubwa wakikabidhiwa katika benki ili kuleta usalama wa fedha wanazotoa kwa washindi wao.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>