Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1702 | 1703 | (Page 1704) | 1705 | 1706 | .... | 3270 | newer

  0 0


  HUU NI UJUMBE WA MWALIMU HUYO.  HABARI KAKA-Kuna mwanafunzi wangu anaitwa Mariam Ibrahimu Mwema wa shule ya sekondari Kawe ukwamani kidato cha 4 mwenye umri wa miaka 16 tu ana matatizo makubwa ya tumbo. Alifanyiiwa opereshen ya kwanza  akiwa darasa la 3. Baadae  upasuaj uliendelea takriban mara 9.    
                     

  Hali yake kiafya imezorota tena baada ya kuimarika katika miezi 2 Iliyopita kufuayia operation aliyofanyiwa pale Muhimbili .Ilikuwa ni operation ya kumi kwa huyu binti mwenye umri chini ya miaka 18                       

  Dogo kwa sasa ni wa kutapika tu, tumbo limevimba tena na kitu kiumizacho zaidi ni kuwa FAMILIA YAKE IPO TAABANI KIUCHUMI KWA SASA...!                     Anaumwa kiukweli dogo hata kukaa hawez..!   
   
  Habari Ndugu Mtanzania Mzalendo,Kwa majina Naitwa Exaud Mtei,Mwandishi wa Habari nchini Tanzania,kwa Masikitiko makubwa Imebidi niwe Balozi wa Kusambaza Ujumbe huu ambao nimeupata kutoka kwa mwalimu wa shule ya Kawe Ukwamani akinieleza Kuhusu maisha ya mwanafunzi wake wa Kidato cha Nne ambaye anashindwa kundelea na masomo kutokana na Matatizo yanayomkumba-                   

  Pleeeeease wadau hebu kila mmoja wetu afikirie nini anachoweza kumfanyia malaika huyu kunusuru kiza  kinene cha mustakabali wake kimaisha. Kiukweli wazazi wake wamefikia hatua ya kutokujua hatma ya mtoto wao kipenzi. 
                        

  Wazazi hawana kitu imebaki ni kumtazama tu, mtoto Analia wazazi wanalia basi ni tafrani Inaumiza sana pale Mariam anapokuambia japo kama ingekuwa inawezekana basi yeye akupatie nafsi yake nawe umpatie yako japo kwa masaa 2 ( dakika 120) japo naye apumzike maumivu kwa muda huo.
    

  Msaada unaohitajika kwa sasa ni Matibabu ya haraka nje ya nchi kwa mujibu wa maelezo ya madaktari. Na kwa msaada wa madaktari wa Tmj, Sanitas na Shree Hindumabdal hospital tulifanikiwa kupata mawasiliano, hospital na daktari ambaye alitupatia gharama za natibabu ya tatizo la mtoto wetu sambamba na gharama nyingine kuwa ni takriban dola elfu nane ( 8000) za marekani.    

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Aliyekuwa Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Fedha, Utawala na Masoko ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Stanley Mahembe akiwaaga wafanyakazi wa kurugenzi yake leo akielekea katika kituo chake kipya cha kazi cha Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Fedha, Utawala na Masoko ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Lilian Karumuna.
  Aliyekuwa Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Fedha, Utawala na Masoko ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Stanley Mahembe akifurahia jambo na wafanyakazi wa kurugenzi yake wakati akiwaaga leo kuelekea katika kituo chake kipya cha kazi cha Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
  Aliyekuwa Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Fedha, Utawala na Masoko ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Stanley Mahembe (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kurugenzi hiyo mara baada ya kuwaaga leo akielekea katika kituo chake kipya cha kazi cha Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (Mbele) akihutubia maelfu ya wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Arusha zinazoshiriki michuano ya Copa/UMISSETA, katika ufunguzi wa mashindano hiyo mkoani Arusha kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid iliyofanyika mwishoni mwa wiki. Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (Mbele) akiambatana na Meneja wa Mauzo wa Coca-Cola kwa Jiji la Arusha Boniface Mwasi, wakisalimia wachezaji wa moja ya timu za sekondari zinazoshiriki michuano ya Copa/UMISSETA, katika ufunguzi wa mashindano hiyo mkoani Arusha kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (Kushoto) akisalimia moja ya timu ya shule za sekondari kutoka mkoa wa Arusha, katika ufunguzi wa mashindano ya Copa Umisseta mkoani hapa yaliyofanyika mwisho wa wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, ambapo kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola iligawa vifaa mbali mbali vya michezo kwa shule za serikali na binafsi kwa ajili ya ushiriki wa michuano yam waka huu.


  0 0

    NI BAADA YA WAKULIMA 18 KUKAIDI AGIZO LA WAZIRI MKUU.
  ·        ATAKAYEKAMATWA TUMBAKU YAKE KUTAIFISHWA
   
  Na Tiganya Vincent
   RS-Tabora

   
  Mkuu wa  Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri amepiga marufuku usafirishaji wa  tumbaku kutoka Wilaya moja kwenda nyingine ili kudhibiti utoroshaji unaotarajiwa kufanya na baadhi ya wakulima wasio waaminifu ambao hadi hivi sasa wamekaidi agizo la Waziri Mkuu la kuwataka wakulima wote kuuza  tumbaku yao kupitia Vyama vya Msingi vilivyopo katika maeneo yao.
   
  Marufuku hiyo inafuatia wakulima wa kujitegemea (IF) zaidi ya 16 kutoka Wilaya ya Urambo na Uyui kukataa kujisajili katika Vyama vya Msingi na hivyo kutoonyesha kuwa watauzia tumbaku yao kupitia  Chama gani cha Msingi.
   
  Mkuu wa Mkoa huyo alitoa agizo hilo jana mjini Tabora wakati wa kikao cha wadau wa tumbaku, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa , ambapo pamoja na mambo mengine kupitia Bodi ya Tumbaku Tanzania kimejadili tarehe ya kuanza kwa  masoko ya tumbaku ambayo yataanza siku ya Ijumaa wiki hii (26.5.2017) katika meneo mbalimbali.
   
  Alisema kuwa Serikali iliamua wakulima wote kuuzia tumbaku yao kupitia Vyama vya Msingi katika maeneo yao na sio vinginevyo ili kuepuka watu wanatumia mwanya wa kujitegemea kuwarubuni  tumbaku ya wakulima wadogo wadogo walipo katika vyama vya msingi na kuwauzia baadhi ya tumbaku yao na kusababisha madeni katika vyama vyao vya Msingi.
   
  Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa hadi hivi sasa baadhi ya wakulima hao wamekata kujisajili katika Vyama vya Msingi vilivyopo katika maeneo yao na hata kwingine ni ishara tosha kuwa wanampango wa kutorosha tumbaku hiyo kwenda kuuzia wanakujua kinyume na agizo la Waziri Mkuu.
   
  Alisisitiza kuwa yeye akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa , hawezi kukubali watu wakaidi agizo la Waziri Mkuu kwa nia ya kutaka kuwanyonya wakulima wengine.
   
  Kufuatia hali hiyo aliagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa , Wilaya kushirikiana na Watendaji ngazi za chini na kuwakamata wao na mizigo yote itakayokuwa inasafirisha nje ya eneo la Chama cha Msingi la Mkulima anapokaa kama bidhaa hiyo haijanunuliwa na kupata hati inayotambulika na Bodi ya Tumbaku ya Tanzania (TTB) na wanunuzi rasmi wa tumbaku wenye vibali vya kufanya kazi hiyo mkoani Tabora.


  0 0

  NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

  KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amewahamasisha wananchi wenye majengo katika Jiji la Mwanza kuhakikisha wanalipa kodi ya majengo kwa wakati ili kuepuka kutozwa faini au kufikishwa mahakamani.

  Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa kodi jijini Mwanza jana Kichere alisema kodi ya majengo ipo kwa mujibu wa sheria na italipwa mara moja kwa mwaka, hivyo ni muhimu wananchi wakailipa mwaka huu wa fedha kabla ya Juni 30 .

  Alisema TRA haina sababu ya kufikishana mahakamani an wananchi lakini watakaoshindwa kulipa ndani ya muda wa kisheria watalazimika kulipa na tozo au kufikishwa mahakamani na kulingana na matakwa ya sheria za mamlaka hiyo watalipa sh. 70,000 badala ya viwango vya sh. 20,000 (Nyamagana) na sh. 15,000 (Ilemela) vya sasa.

  “ TRA na Serikali ya Mkoa wa Mwanza inalenga kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kulipa kodi hii bila adhabu ifikapo Juni 30, mwaka huu ambayo ni mwisho.Wenye majengo kwenye Halmashauri ya Jiji na Manispaa ya Ilemela ambao hawajapokea Ankara zao za kodi wakazichuke ofisi za TRA au kwa viongozi wa serikali za mitaa yao ama wajisajili na kulipia benki yoyote ya biashara,”alisema Kichere.

  Alisema TRA mkoa wa Mwanza inasimamia kodi ya majengo yaliyokamilika na kutumika kwa makazi na biashara yaliyothaminishwa au la,yaliyopimwa na yasiyopimwa katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na Manispaa ya Ilemela.

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akizungumzia umuhimu kodi ya majengo kwenye mkutano wa wadau wa kodi uliofanyika Ukumbi wa Ofisi yake.Kulia kwake ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Kamishna wa Polisi Cloudwing Mtweve na wa kwanza kulia ni Richard Kayombo Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi makao makuu TRA.Picha zote na BALTAZAR MASHAKA
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akielezea umuhimu wa wananchi kulipa kodi ya majengo kwenye mkutano wa wadau wa kodi uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi yake.Kulia kwake ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Kamishna wa Polisi Cloudwing Mtweve na wa kwanza kulia ni Richard Kayombo Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi makao makuu TRA.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles E. Kichere akizungumza na wadau wa kodi pamoja na waandishi wa habari jijini Mwanza kuhamasisha ulipaji kodi ya majengo kwa wakati bila shuruti.Watatu kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, Katibu Tawala mkoa, CP Cloudwing Mtweve (wa pili kulia) naRichard Kayombo,Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi makao makuu TRA wa kwanza kulia , kushoto wa kwanza ni Ernest Dundee,Meneja wa mamlaka hiyo mkoani humu .


  0 0


  0 0

  Vijana kutoka mataifa mbalimbali waliokusanyika katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN), mjini Arusha wametakiwa kuchambua masuala yaliyopo mbele yao kwa makini ili kutoa jawabu kwa matatizo ya dunia yanayohitaji ushiriki wao.

   Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi wa serikali katika mkutano huo Ngusekela Karen Nyerere, Ofisa anayeshughulikia dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

  Aliwataka vijana wanaoshiriki TIMUN kuhakikisha wanaangalia kwa makini mambo yanayogusa nchi zao na kuyatafutia ufumbuzi kwa kuwa ndio njia pekee ya kutekeleza malengo endelevu ya dunia ambayo yanahitaji ushirikiano wa ndani na wa kimataifa. TIMUN ambayo kirefu chake ni Tanzania International Model United Nations hufanyika kila mwaka na ujumbe mbalimbali na mwaka huu ujumbe wa TIMUN ni: “kuwawezesha vijana katika diplomasia na uongozi” Picha juu na chini ni Ofisa wa dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ngusekela Karen Nyerere akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017) unaofanyika kwenye Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) mjini Arusha.

  TIMUN huandaliwa na Shirikisho la vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) taasisi ya vijana isiyotengeneza faida inayotangaza shughuli za Umoja wa Mataifa na kushirikisha vijana katika utekelezaji wa shughuli hizo. 

  Aidha aliwashukuru waandazi wa mkutano huo kubwa unaofanana na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (General Assembly) wenye lengo la kukutanisha vijana kujadili mustakabali wa malengo ya dunia. 

  Alisema vijana wana nafasi muhimu katika utekelezaji wa malengo hayo ya maendeleo endelevu jukumu ambalo dunia imejipa kwa miaka 15 hadi mwaka 2030. Pamoja na kuwashukuru Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha (NM-AIST) kwa kukubali kuwa mwenyeji wa kambi hiyo, hali iliyoonesha kwamba wanajali vijana, mwakilishi huyo wa serikali alisema kwamba Tanzania ipo tayari kusukuma mbele ajenda ya ushirikishaji vijana katika maendeleo endelevu kwa kuwa inaamini juu ya hilo. “Wakati serikali inafanyakazi kwa karibu na taasisi nyingine kuhakikisha kwamba malengo ya maendeleo yanatekelezeka, baraza la vijana ambalo litakutana litakuwa na kazi kubwa ya kutengeneza sauti ya pamoja namna ya kukabiliana na changamoto zilizopo” Alisema kwamba malengo ya dunia ambayo yapo 17 yanagusa kila sehemu ya maisha na hivyo ni vyema kama vijana watatoka na majibu ya maswali yanaoumiza vichwa kuhusu malengo hayo hasa mazingira na dunia endelevu. 

  Aliwataka vijana kutumia nafasi yao vyema katika jukwaa hilo kwani maisha ya watu bilioni 7 duniani wanategemea namna ambavyo wanajengwa na vijana, wenye mchango muhimu wa kulinda mazingira na kuhakikisha maendeleo endelevu. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017), unaofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) mjini Arusha.

  Awali Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alisema kwamba zaidi ya vijana elfu 20 nchini Tanzania wamefunzwa malengo endelevu ya dunia, toka ulipofanyika uzinduzi Juni, 2016. 

  Akizungumza katika hafla ya kambi ya mwaka huu ya Tanzania International Model United Nations (TIMUN), inayofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha (NM-AIST), Bw. Rodriguez alielezea kufurahishwa na idadi hiyo ya vijana waliohamasishwa na kusema kwamba malengo ya maendeleo endelevu 2030 yanahitaji kila mmoja kushiriki. Aidha alielezea umuhimu wa ushiriki wa vijana katika masuala ya maendeleo kutokana na uwingi wao hapa nchini. Asilimia 67 ya watu nchini ni vijana. Mkutano ukiendelea katika ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) jijini Arusha. Bw. Rodriguez alishukuru machampioni kwa kuwezesha vijana wenzao kutambua malengo endelevu ya dunia na kuwataka kuendelea kufanya vizuri zaidi katika kuwashawishi vijana wenzao kuelewa na kushiriki katika malengo hayo. 


  0 0  0 0


  0 0

  Mke wa Mbunge wa Mkuranga Bi Mariam Abdallah Kwa niaba ya mume wake Ndugu Abdallah Ulega akikabidhi vifaa vya ofisi,'Photocopy machine' na 'Rim papers' Kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya CCM Mkuranga vyenye thamani ya milioni tatu na laki tano, kwa Naibu Katibu Kuu wa CCM,Ndg Rodrick Mpogolo katika ziara yake leo mkoani Pwani.
  Naibu Katibu Kuu wa (CCM),Ndg Rodrick Mpogolo akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa katika ziara yake hapo jana mkoani Pwani.
  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Firbato Sanga akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa katika ziara ya Naibu Katibu Kuu wa CCM,Ndg Rodrick Mpogolo mkoani Pwani.
  Muonekano wa Photocopy machine.


  0 0

  Kikosi cha kwaya ya Usharika wa Mabibo (waliovaa jezi za Dark Blue) na kwaya ya Usharika wa Kinondoni (waliovaa jezi nyekundu) wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi kuanza
  Mpira ukiwa unaendelea ambapo kwaya ya Kinondoni waliibuka kuwa washindi.


  0 0

  Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

  Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Sophia Mjema amewaomba wananchi hasa wa wilaya ya Ilala kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 29 mwezi huu katika kuukaribisha na kupokea Mwenge wa uhuru unaotaraji kukesha eneo la Kariakoo .

  Mjema ameyasema hayo leo wakati akitembelea miradi mbali mbali inayoendelea na ujenzi katika manispaa ya Ilala kwa kuanzia eneo la Kivukoni ambapo mwenge utupokelewa na kuelekea sanamu ya askari uliopo katikati ya jiji, bustani ya Kaburi moja, na miradi mingineyo.

  Amesema mwenge huo mwaka huu una kauli mbiu isemayo,’ mwenge ni kushiriki katika uchumi wa Viwanda’ na mwenge huu utakuwa unaongelea viwanda zaidi katika ukuzaji wa viwanda na ili kufanikisha hilo tutaenda maeneo ya gerezani ambapo kuna viwanda vidogo vidogo ambavyo tutavisaidia kukuza uchumi.

  “Tunaomba wananchi washiriki zaidi katika kuukaribisha mwenge na katika mkesha ambao utakuwa pale kariakoo, tunapeleka mkesha kariakoo kwa sababu pale tunajaribu na tunataka kuwatambua wamachinga rasmi, tunataka kuwafugulia ofisi yao rasmi ili wawe wanatambulika na serikali”.

  Ameongeza kuwa ili kukuza uchumi wa viwanda serikali itamsaidia kila mwananchi mwenye kiwanda kidogo katika kukuza uchumi wake ili baadae nao waweze kuja kuwa wajasiliamali wakubwa na hata kumaliza kabisa biashara ya wamachinga kama siyo kupunguza,.

  Aidha amesema Wilaya ya Ilala itatenga mitaa kama vile, Kongo, Mchikichi, Sikukuu na Nyamwezi kutumika zaidi kwa shughuli za umachinga na mingine itakuwa kwa ajiri ya maegesho ya magari ya mizigo, Tax na huduma zingine kama hizo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akijadili jambo na Katibu tawala wa Wilaya hiyo Edward Mpogolo .
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akizungumza na afisa Mazingira wa Ilala , Abdon Mapunda juu ya umuhimu bustani hiyo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akipata Maelekezo ya bustani ya Kaburi moja kutoka kwa Mhandisi Faizer Mbange.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema, akikagu sehemu itakayopandwa miti na majani kwa ajili ya watu kupumzika.


  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama moja kati ya mtrekta aina URSUS yanayounganishwa kwenye karakana ya TAMCO mjini Kibaha Mei 23, 2017.Kulia kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akikagua matrekta aina ya URSUS yanayounganishwa katika karakana ya TAMCO mjini Kibaha Mei 23, 2017. Wengine pichani kutoka kulia kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NDC Mlingi Elisha Mkucha, Waziri wa Viwanda, Biahara na Uwekezaji, Charles Mwijage, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evaresti, Ndikilo na kulia kwake ni Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama moja kati ya mtrekta aina URSUS yanayounganishwa kwenye karakana ya TAMCO mjini Kibaha Mei 23, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo akizungumza wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrial Estate lililopo Kerege Bagamoyo Mei 23, 2017.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka baada ya kutembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrual Estate lililopo Kerege, Bagamoyo Mei 23, 2017
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi, wabunge na wananchi waliohudhuria wakati alipotembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrial Estate lililopo Kerenge, Bagamoyo Mei 23, 2017.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi, wabunge na wananchi waliohudhuria wakati alipotembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrial Estate lililopo Kerenge, Bagamoyo Mei 23, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

    Mstahiki meya wa Jiji la Dar es salaam Mheshimiwa Isaya Mwita Charles leo amekabidhi rasmi magari mawili aina ya Suzuki Carry maarufu kama (Kirikuu) kwa washindi wa shindano la shika ndinga linaloandaliwa na kuendeshwa na kituo cha utangazaji cha EFM redio, washindi waliopatikana katika fainali iliyofanyika tarehe sita mwezi wa tano mwaka huu katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe Jijini Dar es Salaam.

  Mstahiki Meya Mheshimiwa. Isaya Mwita akijiandaa kukabidhi magari hayo.

  Mstahiki Meya akitoa pongezi zake kwa washindi Kutoka Kulia ni Meneja mkuu Dennis Busulwa, Mshindi (Michael Peter), akifuatiwa na Mshindi Joyce Daniel pamoja na Rukia Mtingwa Meneja masoko Zantel
  Washindi wa shindano hilo wakiwa wameshikilia kadi za gari Kutoka kulia ni Michael Peter na Joyce Daniel
  Shamla Shamla zikiendelea
  Wasindikizaji wa mshindi Michael Peter kutoka Salasala

  0 0

  Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

  Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora kuhakikisha wanakarabati upya Jengo la utoaji wa huduma ya Upasuaji katika Zahanati ya Ilolanguru lilojengwa chini ya kiwango na Mradi wa Mbola Melenia.Hatua hiyo inalenga kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza kwa mgongwa wakati anapata huduma ya upasuaji kutoka madaktari.

  Dkt. Ntara ametoa agizo hilo jana Wilayani Uyui wakati alipokwenda kukagua vifaa vya kisasa vya upasuaji ambavyo vipo katika Zahanati hiyo toka mwaka 2013 lakini havijaanza kutumika kwa sababu mbalimbali ikiwemo ubovu wa jengo lililojengwa na Mradi wa Mbola na ambalo halina ubora kwa mujibu wa Madaktari.

  Alisema kuwa wajenzi wa jengo hilo waliamua kujenga hata bila kuwashirikisha Wataalamu wa Afya na Wahandisi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wala Mkurugenzi wa Wilaya ya Tabora na hivyo majengo yao mengi kuwa mabovu na ambayo yana nyufa kabla hayajaanza kutumika.

  Dkt. Ntara aliongeza kuwa haiwezekani kwa muda mfupi baada ya kujengwa jengo liwe limeshapasuka na madirisha kuruhusu vumbi kuingia katika Chumba cha upasuaji , jambo ambalo ni hatari kwa mgongwa kupata maambukizi mengine.


  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara hiyo kwa mwaka 2017/2018 leo  mjini Dodoma. UNAWEZA KUSOMA HOTUBA ALIYOIWASILISHA HAPO CHINI.


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na  Bw. Zhang Xin, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya China National Machinery Industry Federation (CBMIF) na mjumbe wa National Congress ya China Bw. Zhang Xin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 23, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza Kaimu Balozi wa Korea Kusini nchini Mhe. Songwon Shin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 23, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 23, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Kaimu Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Yunus Belei aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 23, 2017.

  0 0

  Nenda Yusuf,Imetosha na ahsante sana,najua ni maamuzi magumu lakini naamini sasa ni wakati wa akili kubwa kufanya kazi kwa bidii na nina wakati wa kumrudisha kundini Dr Jonas Tiboroha na kuja kuongeza nguvu na Katibu mKuu Mkwassa na hakika tutasogea mbele zaidi
  Mengi yemeongewa na kusemwa na naamimi mengine ni ukweli mtupu na mengine ni porojo ila naamini kuna mapungufu makubwa katika uongozi wako uliopita na kubwa zaidi ya yote ni kamati ya utendaji kukosa meno ya nguvu ya kuhoji mambo kadha wa kadha juu ya matumizi na udhamini,mara kadhaa wale waliokuwa wanahoji tumeona wakifanyiwa fitina na kutolewa nje,wapo wakina Aaron Nyanda,Bin Kleb,Seif Magari,Salum Mkemi nk hapo haikuwa sawa,lazima ifike pahali tukubali kutofautiana mawazo ili tuweze kupiga hatua.
  Kamati ya utendaji isiyoweza kumuhoji Mwenyekiti na maamuzi binafsi ya kukataa wadhamini na kujipa udhamini mkuu kwa bei aliyopanga yeye haikuwa sahihi.

  Yanga Sc hii ya Sportpesa inamuhitaji @drjonastiboroha na kamati ya utendaji makini ipige hatua na kuachana na kuomba omba as a super brand it will attracts sponsors all over the places,its all about having the right people.

  Yanga needs to be restructured ili kuweza kwenda sawa na speed ya masoko,inahitaji the right person kwa nafasi ya Mkuu wa masoko anayeweza kuja na challenges na kuleta mawazo mapya na ku adopt marketing skills ambazo wenzetu majirani wanafanya mfano Zesco au Sofapaka.
  Yanga ina watu wanaoitwa wakuu wa idara za magazetini ambazo hazina tija katika day to day operations na hawa add value kwenye maendeleo ya Yanga.Hii ni timu kubwa sio ya kuomba udhamini,hii ni klabu yenye miaka 82 lets have new ways na kutumia weledi katika uendeshaji.

  Yanga inahitaji msemaji na kurugenzi ya mawasiliano makini inayoweza kusimamia social media links na kuweza kufanya kazi bega kwa bega na kurugenzi ya masoko kuuza bidhaa za yanga online pia.

  Its time tuwape proffessionals wafanye kazi na kuleta ufanisi...tuache blah blah bana Manji kapita kama walivyopita wakina Gulamali,Verani.

  By Mac Temba - Fan wa Yanga Sc

  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  MAOFISA Ugani wametakiwa kuwa na mashamba ya mfano ili kutoa fursa kwa wakulima kujifunza masuala ya kilimo kutoka kwao.

  Mwito huo umetolewa na Mtaalamu wa magonjwa ya pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru, Stellah Chirimi wakati akitoa mada katika mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa la Wazi la Bioteknolojia kwa manufaa ya kilimo (OFAB). 

  "Ni vema kila ofisa ugani akawa na shamba la mfano ambalo litasaidia wakulima kwenda kwao kujifunza kilimo bora badala ya kuwaacha bila ya kuwasaidia kupitia mashamba hayo ya mfano.

  Katika hatua nyingine Chirimi alisema uzalishaji wa zao la pamba umeshuka kutokana na maofisa kilimo kushindwa kuwafikia wakulima kwa ajili ya kuwapa elimu ya kilimo bora na cha kisasa.

  Alisema kuna kila sababu ya kutolewa elimu kwa wakulima kuhusu mbegu bora ya pamba ambayo ikitumika itaongeza tija katika uzalishaji hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda hapa nchini.
   Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus (kulia), akitoa mada katika mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa hilo.
   Mtaalamu wa magonjwa ya pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Stella Chirimi akitoa mada katika mafunzo hayo.
   Ofisa Ushauri wa Kilimo wa Wilaya ya Buchosa, Sospeter Obwago (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Kaimu Ofisa Kilimo wa Wilaya hiyo, Paul Misana. Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon na Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0


  Na Mathias Canal, Dar essalaam

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo tarehe 23, Mei 2017 amefanya mazungumzo na Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo ulioongozwa na Mchungaji kiongozi wa usharika huo, Katibu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ya Pwani, Kiongozi wa Kamati ya Ujenzi wa kanisa hilo na baadhi ya wazee wa kanisa.

  Kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za usharika wa KKKT Ubungo kilikuwa na Agenda ya kujadili nanma bora ya uvunjaji wa Ukuta wa eneo la kanisa hilo ambao umeingia katika eneo la Shule ya Msingi Ubungo Plaza Jambo linalopelekea Kushindwa kuanza ujenzi wa madarasa nane mapya kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo ambao kwa sasa wanasoma katika madarasa ambayo majengo yake si rafiki kwa ajili ya usomaji.

  Alisisitiza kuwa ujenzi huo utakuwa maalumu kwa ajili ya kutekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori alilolitoa Mei 19, 2017 wakati wa mkutano wake na walimu wa shule hiyo sambamba na wananchi wa Mtaa huo ukiwajumuisha Afisa mtendaji wa Kata na wajumbe wa mitaa.

  MD Kayombo alisema kuwa baadhi ya shule katika Manispaa ya Ubungo hazifanyi vizuri katika matokeo ya mitihani ya taifa kutokana na uduni wa miundombinu ikiwemo madarasa Jambo ambalo pia limepelekea Manispaa ya Ubungo kuona umuhimu wa kuboresha miundombinu ili kuwa rafiki kwa wanafunzi kujifunzia. 
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa kikao na Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo ulioongozwa na Mchungaji kiongozi wa usharika huo, Katibu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ya Pwani, Kiongozi wa Kamati ya Ujenzi wa kanisa hilo na baadhi ya wazee wa kanisa. Leo tarehe 23, Mei 2017 
  Darasa lililokabidhiwa na Uongozi wa kanisa la kiinjili la Kilutheli Tanzania Usharika wa Ubungo kwa Uongozi wa Manispaa ya ubungo mbele ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg john Lipesi Kayombo
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua majengo ambayo yamejengwa na kanisa la KKKT yakiwa yameingia katika eneo la shule ya Msingi Ubungo Plaza sambamba na viongozi wa kanisa hilo baada ya kikao cha pamoja na Uongozi wa Kanisa hilo Usharika wa Ubungo. Leo tarehe 23, Mei 2017 
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua majengo ambayo yamejengwa na kanisa la KKKT yakiwa yameingia katika eneo la shule ya Msingi Ubungo Plaza sambamba na viongozi wa kanisa hilo baada ya kikao cha pamoja na Uongozi wa Kanisa hilo Usharika wa Ubungo. Leo tarehe 23, Mei 2017.
older | 1 | .... | 1702 | 1703 | (Page 1704) | 1705 | 1706 | .... | 3270 | newer