Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Diamond kumtambulisha msanii mpya wa WCB leo

$
0
0
Rais label ya WCB, Diamond Platnumz Jumatatu hii atamtambulisha msanii mpya wa label hiyo.
Msanii huyo atakuwa msanii wa 5 kutoka ndani wa label hiyo ambayo ina wasanii 4 akiwemo Rich Mavoko, Harmonize, Rayvanny pamoja na Queen Darleen.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Marry You, amesema anafanya hivyo ili kuwasaidia wasanii wachanga ambao wanavipaji lakini wanashindwa kufikia malengo yao.
“Panapo majaaliwa siku ya Jumatatu kesho (leo), ntakuwepo kwenye Leo tena ya Clouds Fm na familia nzima ya WCB Wasafi tukimtambulisha Kijana mwenzetu mwingine mpya toka mtaani, ndani ya WCB,” aliandika Diamond Instagram.
Aliongeza, “Sisi ni vijana ambao tumekulia kwenye umaskini na bado tupo kwenye kupambana namna ya kujikwamua kwenye umasikini na ndiomaana tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kila tukiona kijana yoyote mwenye nia na kipaji kumsaidia kwa kadri ya uwezo wetu, ili nae aweze kutambulisha kazi zake, na Pengine Mwenyez Mungu akimjaalia nae awe mkombozi kwenye Familia yake. Sio jambo Rahisi ni gumu, lakini kwa Sapoti yenu naamini tunaweza lifanikisha. Siku zote naomba mkumbuke WCB_Wasafi sio ya Diamond, ni ya vijana wote wapambanaji…na ndiomaana kila siku nawaomba Muendelee kuniombea na Kunisapoti, kwani Sapoti yenu ndio itayo nifanya hata kesho niweze kukuchukua wewe ama ndugu yako ili aje kukitambulisha kipaji chake na Mwenyez Mungu akijaalia kufikia Malengo…… USIKOSE kusikiliza Leo tena ya @Cloudsfmtz saa nne Asubuhi…Shukran🙏

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATOA SEMINA KWA WABUNGE JUU YA UMUHIMU WA UHIFADHI WA MALIASILI, MALIKALE NA MAENDELEO YA UTALII NCHINI

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta  Ndetiye (kushoto) akizungumza wakati wa semina hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na kufanyika katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana. Kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Prof. Jumanne Maghembe. Semina hiyo ilihusu umuhimu wa uhifadhi wa Maliasili Malikale na Maendeleo ya Utalii nchini.
Baadhi ya viongozi na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania muda mfupi kabla ya kuanza kuwasilishwa kwa mada mbalimbali katika semina hiyo. Mada zilizowasilishwa katika semina hiyo ni Kwanini Watanzania tuhifadhi uoto wa asili na Wanyamapori, Athari za Muingiliano wa Mifugo na Wanyamapori, Maendeleo ya Utalii na umuhimu wake katika uchumi wa Tanzania na Umuhimu wa Uhifadhi wa Misitu Nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jeneral Gaudence Milanzi akizungumza katika semina hiyo iliyoandaliwa na Wizara kwa ajili ya wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkurugenzi wa Idara wa Wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Alexander Songorwa askiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa Watanzania kuhifadhi uoto wa asili na Wanyamapori katika semina hiyo. Kushoto waliokaa ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe na baadhi ya viongozi na wakurugenzi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

SHUKRANI

$
0
0
Bi. Vicky Joan Msina wa Benki Kuu Dar es Salaam, kwa niaba ya ndugu zake wote na familia za Msina, Lyimo, Kiiza na Mbuya wa Dar es Salaam, Kilema, Moshi, na Tabora; wanapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki wote walioshiriki kwa namna moja ama  nyingine katika kipindi chote cha kumuuguza na kushiriki shughuli ya msiba wa Mama yao mpendwa Mwalimu Petronella Peter Lyimo, aliyefariki Ijumaa tarehe 28 Aprili, 2017 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam na kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele tarehe 04 Mei, 2017Mbweni, Dar es Salaam.


Shukran za pekee ziwafikie Madaktari na Wauuguzi wa Hopitali ya St. Joseph- Mbweni, Rabininsia na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili za Dar es Salaam.


Pia Shukran ziwafikie Majirani wote wa Mbweni wakiongozwa na Bwana na Bibi Mutegeki, Bi Sandra na wengine wote, pamoja na Wana Jumuiya ya mtakatifu Joseph Mfanyakazi – Mbweni kwa kutufariji kwa hali na mali. Vile vile shukran ziende kwa Baba Paroko, Paroko msaidizi na Katekista na wanakwaya wa Parokia ya Mtakatifu Rafael - Mbweni kwa huduma ya kiroho waliyotoa kwa marehemu wakati wa uhai wake na pia kwa kufanikisha Ibada ya Maziko kwa kushirikiana na kaka wa Marehemu Fr. Henry Zawadi wa Kristo Mfalme Moshi.


Kwa namna ya kipekee tunawashukuru sana Uongozi na Wafanyakazi wa Benki Kuu Tanzania, Wizara ya Fedha na Mipango, NMB- Makao Makuu na Tawi la Bank House, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Shule ya Msingi za  Pwani- Tegeta na Kiumbageni-Mbweni pamoja na Shule maalum ya wasiosikia- Njombe. 
Ni ngumu kumtaja kila mmoja kwa namna mlivyoshiriki kutufariji katika kipindi hiki kigumu. Tunasema kwenu nyote Asanteni sana na Mungu awabariki daima. 

PUMZIKA KWA AMANI MAMA YETU MPENDWA Mwl. PETRONELLA LYIMO.



“BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE”.

Mashine za Discovery , Defender na Range Rover zinauzwa

$
0
0
Pia tunaweza kukupatiya Spare ya aina yoyote kutoka Europe kwa bei nafuu.
Bei ya hiyo Land Rover Discocery  Engine Td5 ni T.sh.4.7 Milion, tunaleta kutoka U.K. zipo Dar es Salaam kwa maelezo zaidi wasiliana nasi Tel.+255674782666 +255652444311  on whatswap +447723550406

TAFITI INAONYESHA SERIKALI INAPOTEZA MABILIONI KUTOKANA RUSHWA NA UFISADI KWENYE BAJET

$
0
0
Kamati ya Viongozi wa dini ya Masuala ya haki za Binadamu, Kiuchumi na uadilifu katika Uumbaji wakizindua Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani? wakizindua Ripoti hiyo, wakiwa na Wabunge.


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii - Dodoma

Tafiti mpya iliyozinduliwa hivi karibuni inasema serikali inapoteza fedha zaidi ya Sh trillion 4 kwa mwaka kutokana na misamaha na ukwepaji wa kodi. Pia repoti imesema serikali inapoteza Dola za kimarekani 1.3 biloni (2.9 trilion) kutokana na rushwa na ufisadi katika bajeti ya Taifa.

Hayo yamesemwa na Profesa Honest Ngowi alipokuwa akiwasilisha matokeo ya utafiti na mapitio ya ripoti ya swali la dola bilioni moja na kuja na swali Tanzania inapoteza kiasi gani cha fedha?.

Profesa Ngowi katika mapitio hayo amepata kutaja kuwa, Mfumo wa ulipaji kodi , Mlipa kodi, Misamaha ya kodi, Utoroshwaji wa fedha nje ya nchi na upotevu wa mapato, Ukwepaji kodi, Madhara na Gharama za upotevu na kutokusanywa kodi ipasavyo ni moja ya mambo yanayochangia kupotea kwa fedha hii.

“Tatizo la utoroshwaji wa fedha nje ya nchi na upotevu wa mapato limeangaliwa upya katika utafiti huu na kubaini kuwa Tanzania bado inapoteza mapato kwa njia ya utoroshaji fedha zilizopatikana kwa njia zisizo halali, Zinaondoshwa nchini visivyo na kutumiwa isivyo halali” amesema Prof Ngowi.

Ametaja kuwa fedha hizo zinaweza kuwa ni fedha zitokanazo na biashara haramu kama biashara ya Dawa za kulevya, biashara haramu mipakani, uharamia, usafirishaji binadamu, mapato kutokana na ukwepaji kodi na mapato yatokanayo na rushwa.

Amesema kuwa sambamba na utoroshwaji wa fedha, tatizo la kutoa taharifa za uongo wa bei.
Kamati ya Viongozi wa dini ya Masuala ya haki za Binadamu ,Kiuchumi na uadilifu katika Uumbaji wakizindua Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani? wakiwa na wabunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakionyesha Vitabu juu mara baada ya uzinduzi.
Profesa Honest Ngowi akifafanua juu ya Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani?
Askofu Stephene Munga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani?

Her Initiative yawakutanisha pamoja wasichana katika Tamasha la ujasiriamali, uvumbuzi na ajira (PANDA)

$
0
0
Her Initiative iliyojulikana hapo awali kama Teen Girls Supportive Initiative (TGSI) iliandaa mkutano ujulikanao kama Panda, uliowakutanisha pamoja wanafunzi wakike kutoka vyuo mbalimbali nchini pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na biashara, ujasiriamali na wanahabari, lengo likiwa ni kukuza upeo na uelewa wa wasichana katika maswala mbalimbali ya maendeleo.

Her Initiative ni asasi ya wasichana ambapo wao wenyewe ndio mhimili wa maongezi, ambayo inawapa wasichana nafasi ya kuwakilisha na kusimamia maswala yao wenyewe ya kiuchumi, kielimu, kiutamaduni na kiafya. Zaidi inamjengea uwezo msichana kwa kutafuta suluhu ya changamoto zake mwenyewe bila kutegemea watu wengine. Vyote hivi hufanyika kupitia kampeni, matamasha, semina na kuwapa msaada wa mahitaji ya kielimu, kiuchumi na kiafya kwa kushirikiana na wadhamini mbalimbali.
Faraja Nyalandu mmiliki wa Shule Direct ambaye ndie alikuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano huo akiwsihi wanafunzi kuwa na nidhamu ya pesa kwa kutumia kidogo na kuwekeza zaidi. 

Akizungumza katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Her Initiative, Maureen Richard aliwataka Wasichana kujishughulisha na vitu mbali mbali, kwani Uwezo wanao na Panda ni mwanzo wa maendeleo mengi zaidi kwa wasichana. "Nina wasihi wasichana wajitambue, wajithamini na wachakarike pia watumie fursa walizonazo kujikwamua kiuchumi" alisema Maureen Richard.

Mkutano huo ulifanyika mapema wiki iliyopita katika ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam. Watu mbalimbali mashuhuri walikuwepo kuwapatia motisha na ushauri wasichana hao, wakiongozwa na Faraja Nyalandu mmiliki wa Shule direct (mgeni rasmi), Elizabeth Muro  "mshauri mkuu wa Commercial Bank of Africa ", Jokate Mwegelo mmiliki wa "Kidoti", Martin Kadinda "mshindi wa ubunifu wa mavazi" , Philip Makoye "mmiliki wa Mak Juice".
Mwanzilishi wa Her Initiative ambaye kwa sasa ni Kiongozi wa Nguvu ya Binti na Mtangazaji wa vipindi vya Fema, Lydia Charles akitoa neno kwa wasichana wenzake.

Mkutano huo wa PANDA 2017 ulidhaminiwa na  TECNO MOBILE , EFM , RACHEL'S CHOICE Pamoja na MICHUZI MEDIA GROUP.
Baadhi ya wasichana walioshiriki katika tamasha hilo.  
Jokate Mwegelo alimpongeza Lydia kwa ujasiri na Moyo wa kufanya kazi ingawa alipitia changamoto nyingi. Pia alitoa wito kwa wasichana kuiga mfano kutoka kwa muanzilishi wa taasisi hiyo, Lydia Charles ambaye kwa sasa ni mtangazaji wa vipindi vya Fema.
Mwenyekiti mpya wa Her Initiative Moureen Richard (Kati) akiwa pamoja na mzungumzaji Elizabeth Muro (kulia) na Lydia Charles (kushoto). 

MV KAZI YAFANYIWA MAJARIBIO

$
0
0
Na Alfred Mgweno, TEMESA 
 Kivuko cha MV KAZI hatimaye kimefanyiwa majaribio ya kubeba abiria na magari kwa mara ya kwanza baada ya kukamilika kwa matengenezo yake. 
Majaribio hayo yalifanyika kulingana na sheria na taratibu za vyombo vya majini ambayo inavitaka vyombo vyote vya majini kufanyiwa majaribio kabla ya kuanza kazi ili viweze kupatiwa cheti cha ubora “Seaworthiness Certificate”.
Awali wataalam kutoka Chuo cha Ubaharia Dar es Salaam (DMI) waliweza kupima ubora na uimara wa kivuko hicho kwa kutumia utaratibu wa kuweka mawe yenye kilo zinazolingana na uwezo wa kivuko pamoja na magunia ya mchanga ili kuweza kupima uwezo wa kivuko kulingana na mahitaji yaliyoainishwa kabla hakijabeba abiria na mizigo. 
Zoezi hili pia lilihusu kufanyika kwa kipimo cha kuhakikisha kuwa kivuko hakilali upande mmoja yaani “Inclination test” ambapo kilionyesha Kivuko kiko sawa. Taarifa ya zoezi hili itakuwa sehemu ya vitu vya makabidhiano wakati wa upokeaji wa Kivuko.
Miongoni mwa waliokuwepo kushuhudia majaribio hayo alikuwa Mkuu wa Vivuko Magogoni/Kigamboni, Mhandisi Lukombe King’ombe ambaye alisifu uwezo wa kivuko hicho na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuhakikisha wanakitunza kivuko hicho kwani kitawasaidia kupunguza msongamano wa abiria na magari hasa majira ya asubuhi na jioni.Ujenzi wa MV KAZI umegharimu Shilingi Bilioni 7.3 za Kitanzania na kina uwezo wa kubeba abiria 800 magari 22 sawa na jumla ya tani 170. 
Kivuko hicho kitakabidhiwa rasmi hivi karibuni kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa ajili ya kuanza kutoa huduma. Aidha ujio wa kivuko hicho utaongeza idadi ya vivuko kufikia vitatu vitakavyotoa huduma ya kuvusha abiria na magari katika eneo la Magogoni/Kigamboni.
Abiria wakiingia katika kivuko cha MV KAZI tayari kwa kuvuka kuelekea upande wa Kigamboni. Kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio ya kubeba abiria kwa mara ya kwanza baada ya ujenzi wake kukamilika hivi karibuni.
Abiria wakiingia katika kivuko cha MV KAZI tayari kwa kuvuka kuelekea upande wa Kigamboni. Kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio ya kubeba abiria kwa mara ya kwanza baada ya ujenzi wake kukamilika hivi karibuni.
Kivuko cha MV KAZI kikielea kwa mara ya kwanza majini huku kikiwa na abiria na magari, kivuko hicho kilikua kikifanyiwa majaribio baada ya ujenzi wake kukamilika hivi karibuni.
Kivuko kipya cha MV KAZI kikiwasili kwa mara ya kwanza upande wa Magogoni tayari kwa majaribio ya kubeba abiria na magari. 

Star TV - Tuongee Asubuhi: Mahojiano na RC Makonda


Nafasi Art Space Preview

Vodacom kumwaga zawadi kwa washindi ligi kuu

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
Wadhamini wa kuu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC inatarajia kutoa zawadi kwa washindi wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa 2016/2017 siku ya Jumatano.

Pamoja na kutoa zawadi mbali mbali kwa timu washiriki, kampuni hiyo ambayo ni mdhamini mkuu wa ligi, imezipongeza timu zote zilizoshiriki msimu huu wa ligi na itatoa zawadi kwa timu ambazo zimefanikiwa kushika nafasi ya kwanza hadi ya tatu.

Meneja uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu  (pichani) aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, kampuni ya Vodacom inafurahi kuona msimu wa ligi ukimalizika kwa mafanikio makubwa huku timu ya Yanga ikiweza kuibuka mshindi kwa miaka miwili mfululizo.


“Tunaipongeza timu ya Yanga pamoja na mshindi wa pili na wa tatu,Ligi ilikuwa na msisimko pamoja na ushindani mkubwa,” alisema


Nkurlu aliongeza, “waswahili husema chanda chema huvishwa pete, tunapenda kuwatangazia wadau wa soka na timu zilizoshiriki ligi kuu kuwa tarehe 24 siku ya Jumatano tutakuwa na sherehe kubwa itakayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city ya kukabidhi zawadi yao mabingwa. Pamoja na mabingwa, timu nyingine zilizoshiriki zitaweza kuzawadiwa zawadi mbali mbali kwa kuwa zawadi zao zipo tayari pia kamati Maalum iliyoundwa kusimamia tuzo hizi imefanya mabadiliko kiasi kwa kuongeza baadhi ya tuzo ambazo hazikuwepo msimu uliopita lengo ikiwa ni kuboresha tuzo hizi.

Tuzo zilizoongezwa ni: Tuzo ya Heshima (ambayo itatolewa kwa mwanasoka nguli wa zamani mwenye historia nzuri kwa soka la Tanzania).”
Alisema Vodacom Tanzania mwaka huu imetoa zawadi mapema kwa kuwa ni utaratibu wa kawaida kwa kampuni hiyo kukabidhi zawadi mara tu baada ya msimu wa ligi kwisha.

“Uchelewaji wa kutoa zawadi hutokana na sababu mbali mbali ambazo zinakuwaga nje ya uwezo wao ikiwamo baadhi ya timu kuwa zinashiriki mashindano mengine kama Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Sababu nyingine ni pamoja na mfungo wa mwezi mtuku wa Ramadhani,” alieleza Meneja Uhusiano huyo.
Nkurlu alisema utoaji wa zawadi mapema pia utazisaidia timu kuwa na muda wa kutosha kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujoa.

Emirates Offers Special Fare and Free Visa to Dubai for Tanzanian Travellers

$
0
0
Dar es Salaam, Tanzania, 22 May 2017 – Award-winning Emirates is offering travellers in Tanzania a limited time only fare of just USD399 for an Economy Class ticket to Dubai including a visa.

The special offer is only available for Economy Class travel to Dubai, and must be purchased between 22 May and 2 June 2017, with travel completed between 22 May and 22 July 2017. The USD399 offer includes airport taxes and a visa for the United Arab Emirates.

Dubai is one of the world’s most popular tourism and business destinations and offers visitors a wide range of activities and attractions. This includes several new and exciting attractions, such as the world’s largest indoor themed entertainment destination, IMG Worlds of Adventure, and the Dubai Parks and Resorts, the Middle East’s largest integrated theme park. Dubai also offers world class shopping at its many malls and other well-known attractions for visitors, such as the Burj Khalifa, the tallest building in the world, traditional souks and the clear water beaches of the Arabian Gulf.

A wide range of accommodation to suit all budgets is available throughout the city.

On all Emirates’ flights, customers can look forward to hours of entertainment on the airline’s ice system, which offers over 2500 channels of on demand audio and visual entertainment, from the latest movies, music, audio books and games, as well as family friendly products and services for children, including complimentary toys, kids’ meals and movies, priority boarding for families and the use of free strollers at Dubai International Airport.

In addition to the on-board comforts and products, customers will experience the world famous hospitality from Emirates’ multinational cabin crew while enjoying chef prepared regional and international cuisine, using the freshest ingredients, accompanied by a wide range of complimentary wines and beverages.

Emirates flies once a day from Julius Nyerere International Airport (JNIA) to Dubai. To book, or for more information on fares, terms and conditions, please visit www.emirates.com/tz  or visit the local Emirates office or your travel agent.

Vodacom kumwaga zawadi kwa washindi ligi kuu

$
0
0
Wadhamini wa kuu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC inatarajia kutoa zawadi kwa washindi wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa 2016/2017 siku ya Jumatano.

Pamoja na kutoa zawadi mbali mbali kwa timu washiriki, kampuni hiyo ambayo ni mdhamini mkuu wa ligi, imezipongeza timu zote zilizoshiriki msimu huu wa ligi na itatoa zawadi kwa timu ambazo zimefanikiwa kushika nafasi ya kwanza hadi ya tatu.

Meneja uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, kampuni ya Vodacom inafurahi kuona msimu wa ligi ukimalizika kwa mafanikio makubwa huku timu ya Yanga ikiweza kuibuka mshindi kwa miaka miwili mfululizo.


“Tunaipongeza timu ya Yanga pamoja na mshindi wa pili na wa tatu,Ligi ilikuwa na msisimko pamoja na ushindani mkubwa,” alisema

Nkurlu aliongeza, “waswahili husema chanda chema huvishwa pete, tunapenda kuwatangazia wadau wa soka na timu zilizoshiriki ligi kuu kuwa tarehe 24 siku ya Jumatano tutakuwa na sherehe kubwa itakayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city ya kukabidhi zawadi yao mabingwa. Pamoja na mabingwa, timu nyingine zilizoshiriki zitaweza kuzawadiwa zawadi mbali mbali kwa kuwa zawadi zao zipo tayari pia kamati Maalum iliyoundwa kusimamia tuzo hizi imefanya mabadiliko kiasi kwa kuongeza baadhi ya tuzo ambazo hazikuwepo msimu uliopita lengo ikiwa ni kuboresha tuzo hizi.

Tuzo zilizoongezwa ni: Tuzo ya Heshima (ambayo itatolewa kwa mwanasoka nguli wa zamani mwenye historia nzuri kwa soka la Tanzania).”
Alisema Vodacom Tanzania mwaka huu imetoa zawadi mapema kwa kuwa ni utaratibu wa kawaida kwa kampuni hiyo kukabidhi zawadi mara tu baada ya msimu wa ligi kwisha.

“Uchelewaji wa kutoa zawadi hutokana na sababu mbali mbali ambazo zinakuwaga nje ya uwezo wao ikiwamo baadhi ya timu kuwa zinashiriki mashindano mengine kama Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Sababu nyingine ni pamoja na mfungo wa mwezi mtuku wa Ramadhani,” alieleza Meneja Uhusiano huyo.

Nkurlu alisema utoaji wa zawadi mapema pia utazisaidia timu kuwa na muda wa kutosha kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujoa.

UJENZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU UNAENDELEA MKOANI DODOMA

$
0
0
Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikikagua ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya ofisi hiyo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo iliyofanyika hivi karibuni mkoani Dodoma. Ujezi wa jengo hilo unatarajia kumalizika mwanzoni mwa mwaka 2018.
Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikikagua ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya ofisi hiyo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo iliyofanyika hivi karibuni mkoani Dodoma. Ujezi wa jengo hilo unatarajia kumalizika mwanzoni mwa mwaka 2018.
Taswira ya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mkoani Dodoma. Ujezi wa jengo hilo unatarajia kumalizika mwanzoni mwa mwaka 2018.
Taswira ya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mkoani Dodoma. Ujezi wa jengo hilo unatarajia kumalizika mwanzoni mwa mwaka 2018. 

SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI VIWANGO VYA RIBA KATIKA TAASISI ZA FEDHAWa

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Dkt. Ashatu Kijaji
Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma

Serikali imesema kuwa mabadiliko ya sekta ya fedha ya mwaka 1991 yalipelekea Serikali kujitoa katika uendeshaji wa  moja kwa moja wa shughuli za kibenki nchini ili kuruhusu mfumo wa Soko Huria, hususan nguvu ya soko kuamua viwango vya riba za mikopo, riba za amana na gharama zingine za huduma za kibenki.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu  swali la  msingi la Mbunge wa  Viti Maalumu Mhe. Jesca David Kishoa (CHADEMA), aliyehoji licha ya kuwa na benki nyingi zaidi kuliko nchi zote Kusini na Mashariki mwa Afrika, kwa nini wingi huo bado haujaleta unafuu katika tozo ya riba.

Akijibu swali hilo Mhe. Dkt. Kijaji alisema kuwa, viwango vya riba za mikopo hupangwa kwa kuzingatia gharama za upatikanaji wa fedha, uendashaji, bima, sifa za mkopaji na hatari ya mkopaji kutolipa mkopo, pamoja na kasi ya mfumuko wa bei.

“Dhana ya uhitaji na utoaji wa mikopo siyo kigezo pekee kinachoweza kupunguza viwango vya riba hapa nchini, hatari ya kutolipa mkopo ni kigezo kikubwa kinachotumiwa na benki kupanga viwango vya riba za mikopo, hususan kwa wajasiriamali wadogo”. Alisema Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji aliongeza kuwa, uzoefu uliopo  unaonesha kuwa, benki zinapendelea kukopesha wajasiriamali waliojiunga katika vikundi kuliko mjasiriamali mmoja mmoja ili kupunguza kiwango cha mikopo isiyolipika.

Aidha, Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Jesca David Kishoa, alihoji ni kwa nini Serikali isiweke  ukomo wa riba kisheria kwa benki hizo ili kumsaidia mjasiriamali wa sekta binafsi kama ilivyofanya nchi ya Kenya.

Dkt. Kijaji alifafanua kuwa,  kwa mujibu wa Sheria ya Taasisi za Fedha ya Mwaka 1991, iliyotungwa kwa kuzingatia misingi ya mfumo wa soko huria,  Benki Kuu imepewa jukumu na mamlaka ya kusimamia na kuzichukulia hatua taasisi za fedha zinazoendesha shughuli zao kwa hasara.

Aliongeza kuwa, kutoa maelekezo kwa benki kutumia viwango fulani vya riba, kutaifanya Benki Kuu kukosa nguvu na mamlaka ya kuzichukulia benki hatua endapo zitapata hasara kwa kutumia riba ambayo Benki Kuu imeelekeza.

Katika swali la nyongeza Mbunge huyo, alieleza kuwa mikopo isiyolipika imekua kwa kiwango kikubwa tangu mwaka 1991 huku akitaja sababu kubwa mbili ambazo ni mazingira magumu ya biashara pamoja na riba kubwa kwa wafanyabiashara hao.

‘’Je Serikali haioni umuhimu wa kuwasaidia kwa kuwapa riba nafuu ili iweze ‘Kustimulize’ (kuchochea) biashara zao’’. Alihoji Mhe. Kishoa.

Akijibu swali hilo la nyongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alisema kuwa kutokana na mabadiliko ya mfumo wa mwaka 1991 ya sheria ya Mabenki na Taasisi za fedha, Benki Kuu au Serikali haiwezi kutoa mweleko au ukomo wa Taasisi za fedha.

NEEC, UN, HDIF wazindua mafunzo kwa wajasiriamali

$
0
0
Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Umoja wa Mataifa (UN) na shirika la Human Development Innovation Fund (HDIF) leo wameungana na kuzindua mafunzo ya aina tano za ujuzi kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata mbinu bora za ujasiriamali mdogo na wa kati hapa nchini Tanzania.

Misingi ya ujuzi na mbinu hizi inalenga kukuza na kuboresha uzoefu wa vijana katika ujasiriamali. Ujuzi huu utawasaidia kuwa imara na kuweza kuhimili ushindani wa kiuchumi.

Mafunzo haya yenye mbinu tano yatalenga ukuzaji wa bidhaa, mauzo, kumbu kumbu za mauzo, ujuzi wa kawaida pamoja na taratibu na sheria za kufanya kazi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Bw. Beng’i Issa alisema anaamini ya kwamba uzinduzi wa mafunzo haya yatasaidia Taifa kufanikisha malengo ya kuwa nchi ya viwanda ifikapo 2015.

Kuendeleza wajasiriamali ni muhimu sana kama kweli Tanzania ina lengo la kuwa nchi ya viwanda. Wajasiriamali watajenga fursa nyingi ambazo zitatoa ajira kwa watanzania na kuinua uchumi wa nchi. "Uzinduzi wa mafunzo ya mbinu tano za kukuza ujasiriamali ni njia mojawapo sahihi itakayoleta mafanikio katika Taifa letu", alisema Issa.

"Kigezo kikubwa kinachohitajika kuwa mshiriki wa mafunzo hayo ni kuwa na ujuzi wa ujasiriamali na kuwa na malengo endelevu ya kukua kibiashara", alisema Issa.

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez alisema ni muhimu kwa taifa lolote lenye nia ya kujiendeleza kufikia kuwa nchi ya viwanda halina budi kuwathamini na kuwaendeleza wajasiriamali wadogo na wa kati. Bw. Rodriguea alisisitiza kuwa wajasiriliamali ndio wenye nafasi kubwa ya kutoa ajira pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

Naye mwanzilishi wa Taasisi ya Fursa Tanzania, Bw. Ruge Mutahaba alisema uzinduzi wa mafunzo ya mbinu tano za kukua kijisiriamali kutafungua nafasi pana kwa taasisi na watu binafsi watakaotaka kuunga mkono na kuwa sehemu ya kuendeleza mradi huu. Hii itawapa nafasi pekee ya kushirikiana na vijana wajisiriliamali kutatua changamoto zinazowakabili katika kufikia malengo yao.


Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji,Bengi Issa, akizungumza na waandishi wa habarai Dar es Salaam jana wakati wa semina kwa vijana kuhusu namna ya kutumia Fursa kujikwamua kiuchumi. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez,Mkurugenzi wa Fursa, Ruge Mutahaba na Kiongozi wa Shirika la Maendeleo ya Jamii na Ubunifu Endelevu (HDIF),David McGinty.


,Mkurugenzi wa Fursa, Ruge Mutahaba akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habarai jijini pichani kati ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji,Bengi Issa 

TASAF NA WADAU WA MAENDELEO WAKUTANA JIJINI DAR KUTATHIMINI UTEKELEZAJI WA MFUKO HUO.

$
0
0
NA ESTOM SANGA-TASAF.

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- na wadau wa maendeleo wameanza mkutano wa kutathimini utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa kipindi cha miezi SITA iliyopita.

Mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za TASAF mjini Dar es salaam pia unawajumuisha maafisa wa serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar,pamoja na mambo mengine umefahamishwa juu ya mafanikio na changamoto zilizopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini kwa kipindi cha kuishia mwezi Marchi mwaka huu.

Katika mawasilisho ya shughuli zilizotekelezwa na TASAF katika kipindi kilichopita, imeonyeshwa kuwa zaidi ya kaya milioni MOJA za walengwa zimeendelea kunufaika na Mpango kupitia ruzuku na utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyoibuliwa na walengwa kupitia utaratibu wa ajira ya muda ambapo hulipwa ujira baada ya kutekeleza kazi hizo.

Aidha taarifa hiyo imeonyesha kuwa kumekuwa na mwitikio chanya wa walengwa katika kuanzisha shughuli za kiuchumi kwa kutumia fedha zinazotolewa na TASAF chini ya utaratibu wa uhawilishaji fedha, na hivyo kusaidia kwa kiwango kikubwa ongezeko la kipato kwa kaya zilizoandikishwa kwenye Mpango.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akifungua mkutano wa wadau wa maendeleo kwenye ukumbi wa mikutano wa Mfuko huo jijini Dar es salaam. 


Msimamizi wa shughuli za TASAF (Benki ya Dunia) Bwana Muderis Mohamed (aliyesimama) akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa maendeleo na TASAF .
Baadhi ya wadau wa Maendeleo na Maafisa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF – wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Mfuko huo katika mkutano wa kujadili utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MBUNGE LUSHOTO AWAPA POLE WAKULIMA WA MBOGAMBOGA NA KUWATAKA KUONGEZA UZALISHAJI

$
0
0
  Mbunge wa Jimbo la Lushoto Mkoani Tanga (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia katika  akizungumza na wakulima wa mbogamboga kwenye Jimbo lake  hivi karibuni ambao bidhaa zao ziliharibika kutokana na miundombinu ya barabara ya Mombo hadi Lushoto kudondokewa na vifusi na mawe kabla ya kuondolewa na wakala wa barabara mkoani Tanga (Tana Road ) ambapo aliwapa pole wakulima na kuwataka kuongeza uzalishaji
 Kushoto ni mmoja wafanyabiashara wakimuelezea Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia hasara walizozipata kutokana na ubovu wa miundombinu
 Baadhi ya bidhaa za mbogamboga ambazo zimeharibika kama zinavyoonekana
 Mbunge wa Jimbo la Lushoto(CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia kulia akiwa na mfanyabiashara mara baada ya kuangalia namna alivyopata hasara kutokana na ubovu wa miundombinu ambapo pia alitumia nafasi hiyo kuwapa pole
Mbunge wa Jimbo la Lushoto(CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia katika akiwa na wananchji wa Jimbo hilo wakati alipowatembelea hivi karibuni kuona athari za mafuriko kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Lushoto Ramadhani Mahanyu.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MANGULA AKUTANA NA MKURUGENZI WA TAASISI YA KIMAREKANI INAYOSHUGHULIKIA MASUALA YA DEMOKRASIA DUNIANI

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Phili Mangula akikmkaribisha Mkurugenzi wa Tasisi ya Kimarekani inayoshughulikia masuala ya Demokrasia Duniani (NDI), Kanda ya Mashariki na Kusini Mwa Afrika, Dk. Keith Jennings, kwa ajili ya mazungumzo, Ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.

“SERIKALI KUSAMBAZA VIFUKO VYENYE VIFAA MAALUM VYA KUJIFUNGULIA KWA WANAWAKE 500,000 NCHI NZIMA”-MHE.KIGWANGALLA

$
0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imesema kuwa inategemea kusambaza  vifuko maalum vya kujifungulia vyenye vifaa vya kujifungulia  kwa wanawake  500,000 ambavyo vitasambazwa nchi nzima kulingana na uhitaji.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mhe.Dk Khamis Kigwangalla wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Munira Mustafa Khatibu leo Bungeni Mjini Dodoma.

“Sera ya Afya ya mwaka 2007 inaeleza kuwa Huduma za kina Mama wajawazito katika vituo vya ngazi zote zinapaswa kutolewa bila malipo”,Alisisitiza Mhe.Kigwangala.Aidha amesema kuwa Serikali haijawahi kuweka tozo na gharama za vifaa vya kujifungulia na upasuaji na hivyo huduma hizo zitaendelea kutolewa katika ngazi zote katika vituo vya umma vya kutolea huduma kwa gharama za Serikali.

Aidha kwa upande mwingine Mhe,Kigwangala ametoa rai kwa Wabunge kusaidia  kusimamia utekelezaji wa Sera walizokubaliana katika katika maeneo yao husika ili kuhakikisha huduma hizi za kina mama zinapatikana kwa Gharama za Serikali kama ilivyopangwa.

“Ili azma ya Serikali ya Kuhakikisha akina mama wajawazito wanapata huduma nzuri na lengo la kupunguza vifo vya mama na watoto inafanikiwa ni lazima usimamizi uwe wa karibu sana”,Aliongeza Mhe.Kigwangalla.
Aidha jumla ya kina mama 1,900,000 hujifungua kila mwaka nchini na kumekuwa na changamoto katika upatikanaji wa vifaa ambapo kwa sasa Serikali imeliwekea mkazo suala hilo ili kuhakikisha kina mama hao wanajifungua salama.

Naibu Waziri wa WWizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,  Mhe. Mhe.Dk Khamis Kigwangalla wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Munira Mustafa Khatibu leo Bungeni Mjini Dodoma.

MAHAKAMA YAWAASA MAWAKILI KESI YA 'MALKIA WA MENO YA TEMBO'

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo imewaasa mawakili wa upande wa utetezi katika kesi ya kukutwa na meno ya tembo ya bilioni 5.4 inayomkabili Raia wa China maarufu kama 'malkia wa tembo' Feng Glan (66), na wenzake, kuheshimu mahakama, pindi inapopanga tarehe ya kusikiliza kesi hiyo

Hayo yamesemwa na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi base's ya Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi kudai kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa na kwamba walikuwa na shahidi mmoja.

Nchimbi akadai washitakiwa wapo mahakamani lakini mawakili wanaowatetea hawapo licha ya kuwaona mahakamani hapo na kuzungumza nao kabla ya kesi hiyo kuitwa.

 Kutokana na hali hiyo, Hakimu Shaidi alisema amewasubiri mawakili hao ambao ni Jeremia Ntobesya na Nehemia Nkoko kwa  zaidi ya saa moja licha ya kuwa na majalada mengine ya kuandikia hukumu, ili waendelee na kesi hiyo lakini wameshindwa kutokea mahakamani.

Amesem ni mara nyingi upande huo wa utetezi umekuwa ukilalamika kwamba kesi hiyo haiendi kwa wakati  na kueleza kuwa leo shahidi ambaye alitoka Singida ameweza kufika.

 Hakimu shahidi akawauliza washitakiwa huenda hawajawalipa mawakili wao na wamefanya mgomo wa kuingia katika kesi hiyo kwa kuwa wameshindwa kutoa udhuru.

 Hata hivyo, Wakili Hassan Kiangio alidai kuwa shahidi aliyekuja ni kwa ajili ya mshitakiwa wa pili ambaye ni Philemone na kwamba anawakilishwa na Ntobesya na Nkoko ambao walikuwa kwenye kesi nyingine.

 Washitakiwa hao wamekanusha na kusema  wamewalipa mawakili wao na wanaomba muda kwa ajili ya kuwatafuta ili kuendelea na kesi kwani wanataka iishe.

Wakili Nchimbi, ameiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kusikilizwa ili washitakiwa waweze kuzungumza na mawakili wao.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni Mosi.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22,2014  kwa makusudi  raia wa China, China, Yang Feng Glan aliongoza na kufadhiri vitendo vya kijinai kwa kukusanya na kusafirisha vipande hivyo 706 vya Meno ya Tembo bila ya kuwa na kibali chochote kile kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama Pori.

Kwa upande wa washtakiwa Salvius na Manase  wanadaiwa kuongoza makosa ya uhujumu uchumi kwa kusaidia biashara ya nyara za serikali kwa kukusanya, Kusafirisha na Kuuza Meno ya Tembo kwa nia ya kujipatia faida.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images