Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1699 | 1700 | (Page 1701) | 1702 | 1703 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea kwa masikitiko taarifa za kupata ajali kwa msafara wa timu ya Ruvu Shooting FC iliyotokea leo barabara ya Manyoni mkoani Singida wakati kikosi hicho kikitokea Shinyanga kwenda Pwani.

  Taarifa kutoka Singida zinasema gari hilo lilipata ajali baada ya kupasuka tairi moja la mbele hivyo kuyumba na kuacha njia eneo la Itigi - kilometa 200 kutoka Singida mjini kuelekea Manyoni hivyo kutoka barabarani kuu kabla ya kugonga mti.

  Taarifa hizo zilizothibitishwa na Masau Bwire, zinasema wachezaji watatu akiwamo Bwire mwenyewe ndio waliopata majeraha na kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Singida kwenda kutibiwa. Wachezaji hao ni Yussuf Nguya, Abdul Mpambika na Saidi Dilunga.

  Timu hiyo ilikuwa mkoani Shinyanga ilipocheza mechi ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17 dhidi ya Stand United na kupoteza kwa mabao 2-1, hata hivyo imebaki kucheza Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao baada ya kushika nafasi ya saba. 

  Mara baada ya kupata taarifa hizo, Rais wa TFF Jamal Malinzi mara moja ametuma salamu za kuwapa pole uongozi wa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania pamoja na timu nzima ya Ruvu Shooting.

  “Nawapa pole viongozi wote, makocha na wachezaji. Na kwa wachezaji ambao wamejeruhiwa na viongozi wote waliojeruhiwa akiwamo ndugu yetu Masau Bwire, nawaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone haraka,” amesema Malinzi.

  Rais Malinzi alimshukuru Mungu kwa kuepusha vifo kwa wanafamilia hao wa mpira wa miguu hasa wakati huu Watanzania wakiwa makini kufuatilia maendeleo ya timu za taifa.

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, ametuma salamu za pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida ulioingia madaraka jana Mei 20, 2017.

  Mbunge wa Singida Mjini, Mheshimiwa Mussa Sima amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa SIREFA baada ya kuwashinda wenzake Erasto Sima, Hussein Mwamba, Said Mnyampanda na Samwel Nakei.

  Katika salamu zake kwa SIREFA, Rais Malinzi amesema anashukuru kwa uamuzi wa kidemokrasia uliofanywa na wajumbe wa mkoa huo na kwamba ana imani na uongozi ulioingia madarakani.

  “Kwa namna ya wanafamilia wa mpira wa miguu wa Mkoa wa Singida walivyodhamiria kutaka kuleta maendeleo ya mpira wa miguu, nina imani na uongozi wa Mheshimiwa Sima katika kutekeleza mipango ya maendeleo ya soka mkoani huo,” amesema Malinzi.

  Katika uchaguzi huo mdogo uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) mjini Singida na kusimamiwa na Mwenyekiti Stella Maila, pia ulimchagua Katibu Mkuu Rashid Koba wakati Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF ni Nurfus Ndee huku Hamza Ntoga akichaguliwa kuwa Mweka Hazina Msaidizi.

  Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilikwenda kwa Ally Ramadhani Nkhangaa aliyekuwa mgombea pekee wakati Koba alimshinda Edward Ihonde na Ndee alimshinda Manase Abel.

  Uchaguzi wa SIREFA ulifanyika baada ya viongozi wengine walioingia madarakani mwishoni mwa mwaka jana, kujiuzulu kutokana na kubanwa na majukumu mbalimbali.

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

  0 0
   Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakitia saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017.

  Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakipongezana  baada ya kukamilika zoezi la utiaji saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017
  Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni na wajumbe zao katika mazungumzo ya mwisho  kabla ya kutia saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017
   Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakiwa na Mawaziri na  maafisa waandamizi wa pande zote mbili baada ya kukamilika zoezi la utiaji saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017

  Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakiwa na watendaji wa pande zote mbili baada ya kukamilika zoezi la utiaji saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 21, 2017

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
 • 05/21/17--08:45: TUZO ZA LIGI KUU 2016/17
 • SHEREHE za Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kufanyika Mei 24 mwaka huu ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.

  Kamati Maalum iliyoundwa kusimamia tuzo hiyo imefanya mabadiliko kiasi kwa kuongeza baadhi ya tuzo ambazo hazikuwepo msimu uliopita lengo ikiwa ni kuboresha tuzo.

  Tuzo zilizoongezwa ni: Tuzo ya Heshima (ambayo itatolewa kwa mwanasoka nguli wa zamani mwenye historia nzuri kwa soka la Tanzania).

  Nyingine ni: Tuzo ya Kikosi Bora cha Msimu (Itatolewa kwa wachezaji Bora 11 wa Ligi Kuu (VPL XI 2016/2017) walioteuliwa kutokana na ufanisi wao katika ligi hiyo msimu huu.

  Pia imeongezwa Tuzo ya Mchezaji Bora mwenye chini ya umri wa miaka 20 (Hii itatolewa kwa wachezaji waliofanya vizuri katika ligi ya vijana ya timu za Ligi Kuu ya Vodacom.

  Tuzo hiyo ya Mchezaji Bora wa Ligi ya Vijana itajulikana kama Tuzo ya Ismail Khalfan ikiwa ni heshima ya kumbukumbu ya mchezaji Ismail Khalfan wa Mbao FC aliyefia uwanjani katika mashindano hayo yaliyofanyika mkoani Kagera.

  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limefikiria kutoa tuzo hiyo kama njia mojawapo ya kuonesha kuthamini kipaji cha mchezaji huyi wakati wa uhai wake.

  Kutokana na mabadiliko hayo tuzo zitakazotolewa katika sherehe hizo pamoja na Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya VPL ambayo ndiyo tuzo kuu, pia ni Bingwa wa Ligi Kuu, Mshindi wa Pili, Mshindi wa Tatu, Mshindi wa Nne na Mfungaji Bora.

  Nyingine ni Mchezaji Bora wa Ligi Kuu, Golikipa Bora, Kocha Bora, Mwamuzi Bora, Mchezaji Bora wa Heshima, Mchezaji Bia anayechipukia, Goli Bora la Msimu, Mchezaji Bora wa Kigeni, Mchezaji Bora wa Chini ya Umri wa Miaka 20 na Timu Yenye Nidhamu.

  Tuzo za Bingwa, mshindi wa pili, wa tatu na wa nne na Mfungaji Bora hizi zipo kulingana na msimamo wa ligi ulivyo.

  Hata hivyo Mfungaji Bora safari hii kuna wachezaji wawili wamefungana, hivyo kamati itapitia vigezo vilivyopo katika Kanuni za kumpata Mfungaji Bora w Ligi Kuu Tanzania Bara ili kupata mshindi ambaye atatangazwa siku hiyo ukumbini.

  Wafuatao wameteuliwa kuwania tuzo hizo kutokana na vigezo mbalimbali:  0 0

   Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuendeleza Quraan na Sunna Tanzania (JAQUSUTA) Sheikh Hassan Kabeke (kushoto aliyesimama) akizungumza kwenye Maulid iliyofanyika jijini Mwanza juzi. Waliokaa kushoto ni Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania Mkoa wa Mwanza (BAKWATA) Sheikh Salum Mohamed Balla, Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella, kulia wa kwanza ni Sheikh Khatm kutoka Malindi Kenya na wa pili ni Kaimu Mufti Othman Issa Othman.
   Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania Mkoa wa Mwanza (BAKWATA) aSheikh Salum Mohamed Balla na Mkuu wa mkoa huo  Mhe. John Mongella (wa pili kutoka kushoto) wakifuatilia mawaidha kwenye Maulid iliyofanyika jijijni Mwanza  juzi.Kulia wa kwanza ni Sheikh Khatm kutoka Malindi Kenya na wa pili ni Kaimu Mufti Othman Issa Othman.
  Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania Mkoa wa Mwanza (BAKWATA) Sheikh Salum Mohamed Balla na Mkuu wa mkoa huo  Mhe. John Mongella (wa pili kutoka kushoto) wakifuatilia mawaida kwenye Maulid iliyofanyika jijijni Mwanza.Kulia wa kwanza ni Sheikh Khatm kutoka Malindi Kenya na wa pili ni Kaimu Mufti Othman Issa Othman. Picha na Baltazar Mashaka.
  Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

   Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Mhandisi Atashasta  Ndetiye akiongoza semina ya Wabunge wote  inayohusu umuhimu wa uhifadhi wa Maliasili Malikale na Maendeleo ya Utalii nchini Tanzania, iliyofanyika leo Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma. kushoto kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Prof. Jumanne Maghembe
  Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa Amina Mollel akizungumza jambo wakati wa semina ya Wabunge wote iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii inayohusu umuhimu wa uhifadhi wa Maliasili Malikale na Maendeleo ya Utalii nchini Tanzania, iliyofanyika leo Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0

  TAASISI isiyo ya kiserikali ya The Desk & Chair Foundation (TD&CF) tawi la Tanzania imekabidhi misaada ya baiskeli za miguu mitatu (wheel chair)  na visaidizi kwa watu mbalimbali wenye ulemavu pamoja na vifaa vya mazishi.
  Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 7.6 vilikabidhiwa jana kwa walengwa na Naibu Meya wa Jiji la Mwanza Bhiku Kotecha ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mbugani Wilaya ya Nyamagana.
   Mwenyekiti wa taasisi hiyo Sibtain Meghjee akimkaribisha mgeni rasmi kukabidhi msaada huo alisema walipokea maombi mengi kutoka kwa wahitaji lakini kutokana na maombi wamefanikiwa kuwapa wachache na kuahidi waliokosa watapa awamu nyingine.
  “Niwashukuru wafadhili wanaotuwezesha kuwasaidia watu wasio na uwezo pamoja na vyombo vya habari. Misaada hii ni endelevu , niwaombe ndugu zangu mliokosa kwa sababu ya wingi wa maombi muwe wavumilivu endapo ufadhili utapatikana tutawasaidia kulingana na mahitaji ya kila mmoja,” alisema Meghjee.
  Aliitaja misaada hiyo kuwa ni Wheel Chair nne, baiskeli 10 za magurudumu matatu, magongo seti moja,visaidizi viwili vya kuwawezesha  watoto kutembea (baby walker), vifaa vya mazishi (chepeo 4, sululu 2 na majembe 4), sahani na vikombe 204.
  Akizungumza kabla ya kuikabidhi misaada hiyo Kotecha aliipongeza taasisi hiyo kwa kazi kubwa inayoifanya ya kusaidia jamii pamoja na serikali kwenye sekta za elimu, afya na maji.
  Alisema kuwepo kwa taasisi hiyo Watanzania wengi hasa wa mikoa ya Kanda ya Ziwa na mingine, wataendelea kunufaika na laiti tungepata taasisi nyingi kama The Desk & Chair Foundation nchi ingepata maendeleo ya haraka.
  “Naamini uadilifu wenu katika kutekeleza kazi zenu zinazotokana na fedha za wafadhili zimewafanya muendelee kuaminika kwao.Mgekuwa wapigaji msingefanikiwa,” alisema Kotecha.
  Naibu Meya huyo na Diwani wa CCM Kata ya Nyamagana alisema taasisi hiyo imefanya mengi kwenye sekta za elimu,maji na afya  kwa kutengeneza madawati, kuchimba visima vya maji , kulipa gharama za matibabu na ada za masomo kwa wanafunzi mbalimbali.
  Alisema taasisi hiyo imekuwa ikijenga miradi ya vyoo na kuchimba visima vya maji vyenye ubora kwa gharama nafuu,vinavyokidhi thamani ya fedha na kuiomba serikali kuisaidia na kuiunga mkono kutokana na kufanya kazi kubwa ya kusaidia jamii.  
  “Nakosa maneno ya kusema juu ya Desk & Chair, wanayoyafanya hawayafanyi kwa kujionyesha,lengo ni kuwasaidia watanzania maana  hawaangalii dini, rangi wala kabila.Si kama wengine wanofanya kwa kujinufaisha wao.Nawashukuru sana,”alisema Naibu Meya huyo wa Jiji.
  Naye Skeih Hashim Ramadhan wa Bilal Muslim Mission Of Tanzania Tawi la Mwanza alieleza kuwa ni jambo jema kutoa kitu chochote ili kusaidia watu  wenye mahitaji lakini pia ni sadaka na thawabu
   Mtoto Teddy Shirikale mkazi wa Kisesa Magu, mwenye ulemavu uliotokana na kipigo kutoka kwa mama yake aliyefahamika kwa jina moja la Enjoy na kusababisha mguu wa kushoto uoze na kupata kilema cha kudumu.Mama huyo baada ya kutenda unyakiwa akiwa amekaa kwenye Wheel Chair aliyokabidhiwa na The Desk & Chair Foundation. Anayemsukuma ni Naibu Meya wa Jiji la Mwanza Mstahiki Bhiku Kotecha ambaye alikuwa mgeni rasmi  muda mfupi baada ya kumkabidhi. Anayemrekebisha mkanda ni Mkurugenzi wa taasisi ya Nitetee Flora Lauwo.
   Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation Sibtain Meghjee wa pili kutoka kulia waliosimama akiwa katika picha ya pamoja na walemavu waliopokea msaada wa baiskeli, wa kwanza kushoto ni mgeni rasmi Bhiku Kotecha.
   Mmoja wa walemavu walipoata baiskeli Bw. Mwanza Lima akizungumza na 

  Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation Sibtain Meghjee, Mwanza Lima alipata ulemavu baada ya kupigwa kichwani na mkewe.

   Mgeni Rasmi Naibu Meya wa Jiji la Mwanza Bhiku Kotecha akimkabidhi Bw. Mwanza Lima baiskeli ya magurudumu matatu baada ya kupata ulemavu wa kudumu uliosababishwa na kipigo kutoka kwa mkewe ambaye baada ya tukio hilo alitoroka. 
  Bi. Batika Kilaka mkazi wa Bunda akiwa amekaa kwenye Wheel chair aliyokabidhiwa na Naibu Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Bhiku Kotecha (nyuma yake ) iliyotolewa  na The Desk & Chair Foundation. 
  Habari na picha na Baltazar Mashaka


  0 0

  Na Is-haka Omar, Zanzibar
  NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,  Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” amesema atalinda na kusimamia kikamilifu mali na miradi mbali mbali inayomilikiwa na chama hicho ili iwanufaishe wananchi wote badala ya watu wachache wanaojimilikisha baadhi ya  rasilimali hizo kinyume cha sheria.
  Msimamo huo ameutoa wakati akikagua shamba la CCM lenye zaidi ya hekta 200 huko katika Kijiji cha Kilombero Wilaya Kaskazini “B” Unguja, alisema CCM haiwezi kufikia dhamira yake ya kuimarika kiuchumi endapo kama kuna baadhi ya watu wanaotumia rasilimali hizo kwa maslahi binafsi.
  Alisema lengo la CCM kupitia mabadiliko ya muundo wa taasisi hiyo yaliyofanyika hivi karibu ni kuhakikisha rasilimali zinatumika vizuri na kwa maslahi ya wengi kwa lengo la kufikia dhamira chama hicho kujitegemea kiuchumi.
  Dkt. Mabodi alisema CCM itasimamia Utekelezaji wa Ilani yake ya  Uchaguzi ya mwaka 2015/2020 kama ilivyowahidi wananchi kwa kuhakikisha inaondosha mianya yote ya ubadhirifu  wa mali za chama hicho.
   Kulia ni Ni Afisa milki wa CCM Zanzibar Nd. Mwenemzi Omar Said aliyevaa fulana ya njano akionyesha ramani na mipaka ya Shamba hilo kabla ya kuanza ziara hiyo (katikati) ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi”  na kushoto aliyevaa kanzu na kofia ni Kaimu Mkuu wa Utawala Afisi Kuu CCM Zanzibar  Nd. Mohamed Sijaamini pamoja na watendaji wa CCM Wilaya hiyo na wamiliki wa mashamba yaliyopakana na shamba hilo.
   Msafara wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.  Abdalla Juma Saadala "Mabodu" na baadhi ya wananchi wakiongozwa na Viongozi wa CCM Wilaya ya  CCM Kaskazini “B”, wakikagua shamba hilo.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.  Abdalla Juma Saadala "Mabodi" akishauriana masuala mbali mbali na baadhi ya wananchi wakiwa ndani ya shamba hilo.

  0 0

  Na Ofisa Habari Mufindi 
   Serikali Wilayani Mufindi Imewataka wajumbe wa kamati za Shule na viongozi wa Serikali za vijiji kwa kushirikiana na wazazi, kutekeleza mpango wa utoaji chakula cha mchana kwa wanafunzi wanapokua shuleni kwa lengo la kuongeza ufanisi wakati wa kujifunza na kuleta matokeo chanya. 
   Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William, wakati wa maadhimisho ya siku ya kusoma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi iliyofanyika Kata ya Nyololo Wilayani humo. 
   Mkuu huyo wa Wilaya amesema, mpango wa utoaji wa chakula Shuleni ambao wazazi hutakiwa kuchangia kwa mujibu wa sera ya Elimu pasipo malipo, husaidia kuleta usawa kati ya walionacho na wasionacho, kuimarisha mahudhurio na kutunza muda wa ratiba za shule na kusisitiza kuwa endapo mambo haya yote yatafanyika kiusahihi yanamchango mkubwa wakati wa ujifunzaji ulio bora kwa wanafunzi darasani. 
   Maadhimisho ya siku ya kusoma katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi yanalengo la kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji wa stadi za msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) huku yakiambatana na maonyesho ya Elimu na utoaji zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye kuandika, kusoma na kuhesabu. 
   Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imekua miongoni mwa Halmashauri ambazo shule zake zinafanya vizuri katika mitihani ya kitaifa kwani mapema mwaka jana Halmashauri ya Mufindi ilishika nafasi ya sita  kwenye mitihani ya darasani la nne  kati ya Halmashauri 185.
  Pia mwaka 2014 iliweka rekodi ya kukumbukwa ambapo shule yake ya kata ya Igowele iliongoza kitaifa kwa kushika nafasi ya kwanza kwenye mtihani wa kidato cha sita
  Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya kusoma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi iliyofanyika Kata ya Nyololo Wilayani humo.


  Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William akimvisha zawadi ya Begi la shule mmoja kat ya Wanafunzi wa darasa la kwanza  waliofanya vizuri kwenye stadi za kuandika ,kusoma na kuhesabu

  0 0

   Sehemu ya umati uliohudhuria katika Mkutano wa Sheikh shariff Majini  katika ukumbi wa Kamanda Mbogo uliopo jirani na chuo cha CBE mjini Dodoma wikiendi hii
   Sheikh Shariff Majini  akiendesha mkutano huo katika ukumbi wa Kamanda Mbogo uliopo jirani na chuo cha CBE mjini Dodoma wikiendi hii
   Sheikh Shariff Majini  akiendesha mkutano huo katika ukumbi wa Kamanda Mbogo uliopo jirani na chuo cha CBE mjini Dodoma wikiendi hii
  Sheikh Shariff Majini  akiombea wahudhuriaji kwenye  mkutano huo katika ukumbi wa Kamanda Mbogo uliopo jirani na chuo cha CBE mjini Dodoma wikiendi hii

  0 0


  SIMU.TV: Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi taifa Abdallah Bulembo, amemsimamisha kazi katibu msaidizi wa CCM wilayani Mbulu kutokana na ubadhirifu wa fedha; https://youtu.be/5Cdji3IKmOU

  SIMU.TV: Mkoa wa Kagera umeanza kuchukua tahadhari kujikinga na ugonjwa hatari wa Ebola ambao umeanza kushambulia maeneo kadhaa nchini Congo DRC; https://youtu.be/IxVGRPd_Q18

  SIMU.TV: Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo, macho na masikio wamewasili mkoani Kigoma kwa ajili ya kutoa huduma ya magonjwa hayo kwa wakazi wa mkoa huo; https://youtu.be/Zu3nPcQe_Mc

  SIMU.TV: Mwenge wa uhuru umekamilisha mbio zake mkoani Mtwara kwa kufungua miradi kadhaa yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 10; https://youtu.be/AhD1kK-USRM

  SIMU.TV: Baadhi ya wakulima wa zao la Tumbaku mkoani Tabora wameiomba serikali kuingilia kati tabia ya baadhi ya watumishi wa vyama vya msingi kuwabambikia madeni; https://youtu.be/4xyTkr1yWvM

  SIMU.TV: Fahamu serikali ya Tanzania ilichoahidi kukifanya kwa wakazi wa kanda ya ziwa katika kumbukumbu ya vifo vya mamia ya watanzania kwenye ajali ya Mv Bukoba; https://youtu.be/UTdvPLf-nDM

  SIMU.TV: Timu ya taifa ya vijana Serengeti boys inashuka dimbani usiku huu kuvaana na timu ya taifa ya vijana ya Niger kuwania nafasi ya kucheza nusu fainali; https://youtu.be/YAOM5WC6UDE

  SIMU.TV: Tazama sehemu ya mapokezi waliyoyapata timu ya soka ya Yanga walipowasili jijini Dar Es salaam wakitokea mkoani Mwanza; https://youtu.be/MQQ_OB9SQrU

  SIMU.TV: Rais wa Zanzibar Dkt Alli Shein amezindua rasmi kampeni ya kuchangia fedha kwa lengo la kufufua michezo mashuleni visiwani humo; https://youtu.be/TwqRifhTIxM

  SIMU.TV: Timu ya Azania ya Tanzania itashuka dimbani usiku huu katika uwanja wa Liverpool nchini Uingereza kuwania kombe la Standard Chartered; https://youtu.be/PHklpeoVOw8
  0 0

  Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba  wakiyarudi magoma wakati walipokuwa wakiingia ukumbini katika tafrija maalum ya kuwapongeza kwa kuungana kwao iliyofanyika Jumamosi katika ukumbi wa Tausi uliopo Kiluvya kata ya Kisarawe mkoani Pwani.
   Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba wakipewa mikono ya pongezi
   Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba wakipongezwa

  Maharusi katika picha ya pamoja na wazazi na ndugu wa karibu
   Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba na Mama mdogo Zamaradi Kawawa
   Maharusi  Zuberi Senzota Msemo na mkewe Bi Khadija Khamis Lyoba na mama wakubwa. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameunga mkono jitihada zinazofanywa na Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar za kusaidia wananchi wanaokabiliwa na hali duni ya maisha kwa kuahidi kutoa mifuko ya saruji 1000 na mabati 600 kwa ajili ya kusaidia wananchi hao.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa ahadi hiyo mjini Unguja wakati anazindua kampeni maalum ya MIMI NA WEWE inayolenga kuhamasisha wananchi kuungana pamoja katika kutoa misaada ya hali na mali ili kuboresha huduma za kijamii katika sekta za afya, elimu,mazingira,maji safi na salama, matumizi bora ya ardhi na kusaidia watu wasiojiweza.

  Makamu wa Rais katika hotuba yake kwa mamia ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa kampeni hiyo amekemea vikali tabia ya ubinafsi kwa baadhi ya viongozi inayosababisha wananchi kutopatiwa taarifa muhimu za maendeleo yao hali inayopelekea uduni katika uchangiaji wa shughuli za maendeleo.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ni muhimu kwa viongozi katika maeneo mbalimbali kujenga tabia ya kuweka wazi mapato na matumizi ya fedha wanazopata na jinsi zilivyotumika ili kuwapa moyo wananchi katika kuchangia kwenye shughuli za maendeleo kwa sababu watakuwa na imani kuwa fedha zao walizochanga zinatumika vizuri.

  “Maendeleo endelevu ni lazima yazingatie Utu na heshima ya mtu, mshikamano wa dhati na mafungamano ya Kijamii,” Amesisitiza Makamu wa Rais.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mimi na Wewe uliofanyika kwenye uwanja wa Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge, mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar. 
  Bila kujali mvua iliyokuwa inanyesha wananchi walijitokeza na kumsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mimi na Wewe kwenye uwanja wa Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge, mkoa wa mjini Magharibi, Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi,Wafadhili waliochangia kufanikisha kampeni ya Mimi na Wewe inaleta tija kwa wananchi wa mkoa wa Mjini Magharibi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).


  0 0

   Wakulima wa mahindi katika kijiji cha Ihemi mkoani Iringa pamoja na Bwana Shamba wa Yara Tanzania Ltd, Andrew Ndundulu (kati-chini) katika picha ya pamoja baada ya mafunzo ya matumizi bora ya mbolea za mahindi kutoka kampuni hiyo. Mafunzo hayo yalifanyika katika shamba darasa la Yara Tanzania kama njia ya kuelimisha waondokane na fanya kilimo cha mazoea na kuelekeza fikra zao kwenye kilimo cha kisasa.
  Moja ya picha iliyopigwa kwenye shamba darasa la Yara katika kijiji cha Ihemi mkoani Iringa 

  0 0

  Meneja Chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa (mwenye kofia nyeusi kulia) na Meneja Mwajiri Zantel, Frank Jackson (mwenye kofia nyeusi kushoto) wakikabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa uongozi wa soko la Samaki la Kunduchi mara baada ya wafanyakazi wa Zantel kumaliza zoezi la kufanya usafi katika soko hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Zoezi hilo ni moja ya hatua ya uwajibikaji wa Kampuni hiyo kwa jamii katika kuweka mazingira safi na salama ambapo kampuni hiyo iliwataka wadau hao kuendeleza utamaduni huo.
  Wafanyakazi wa Kampuni ya mawasiliano ya Zantel wakishiriki kufanya usafi katika soko la Samaki la Kunduchi ikiwa ni moja ya hatua ya uwajibikaji wa Kampuni hiyo kwa jamii katika kuweka mazingira yao safi na salama. Zeozi hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam ambapo kampuni hiyo ilikabidhi pia vifaa vya kufanyia usafi kwa uongozi wa soko hilo ili kuendeleza utamaduni huo. 
  Wafanyakazi wa Kampuni ya mawasiliano ya Zantel wakishiriki kufanya usafi katika soko la Samaki la Kunduchi ikiwa ni moja ya hatua ya uwajibikaji wa Kampuni hiyo kwa jamii katika kuweka mazingira yao safi na salama. Zeozi hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam ambapo kampuni hiyo ilikabidhi pia vifaa vya kufanyia usafi kwa uongozi wa soko hilo ili kuendeleza utamaduni huo. 
  Meneja Chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa (Kulia) akishiriki kufanya usafi katika soko la Samaki la Kunduchi ikiwa ni moja ya hatua ya uwajibikaji wa Kampuni hiyo kwa jamii katika kuweka mazingira yao safi na salama. Zeozi hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam ambapo kampuni hiyo ilikabidhi pia vifaa vya kufanyia usafi kwa uongozi wa soko hilo ili kuendeleza utamaduni huo.

  0 0
  0 0


    Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi (AQRB) , Dkt6543W2 Geraldine Kikwasi akizungumza na Wanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya Sekondari Majani ya Chai iliyoko wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kuwahamasisha Wanafunzi wa kidato cha pili wa shule hiyo kuwapa elimu kuhusiana na fani mbili za ubunifu majengo na Wakadriaji Majenzi kwa masomo ya sayansi.
  ARCH. Daniel Matondo kutoka Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi akiwaelezea Wanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya Sekondari Majani ya Chai shughuli mbalimbali zinazofanywa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi katika sekta ya ujenzi. 
  Afisa Uhusiano kutoka Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi (AQRB) Bw.Hamis Sungura. akiwatambulisha viongozi wa Bodi.
  Wanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya Sekondari Majani ya Chai iliyoko wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam wakifuatilia elimu ya fani mbili ya ubunifu majengo na Wakadriaji Majenzi kwa masomo ya sayansi. 


  0 0

                          We are a group of companies currently looking to expand and now we are looking for Commission based sales representatives in Dar es salaam (30) all other regions 2.

  The ideal candidates will possess a high energy level, outgoing personality, confident, smart, must be results oriented with demonstrated success in sales or have the ability to sale, ready to learn. A go getter on the whole.


  QUALIFICATIONS

   • 1 or more years of successful  commission based sales experience or if you feel you are born to sale with no experience you may apply.

   • Customer service, Meeting sales goals, closing skills, territory management

  • cold calling, market research  and securing sales from small/big business accounts that you were be allocated.

  • Capable of seeking out and participating in local networking events.

  • Identifies prospects, customers, and referral sources, while developing and maintaining excellent relationships

  • Strong interpersonal and communication skills (oral, written, presentation) in English and Kiswahili.

  • Must be highly organized and self motivated

   •Positive and energetic attitude

   • Knowledge of Word, Outlook, Excel.

     On-going sales training will be provided.

  NB:This is a commission  based position only with a start up transport allowance ONLY. The best candidates will get permanent jobs after  a probation period of 3 months.
  Send your CV only to  kccsm@turkysgroup.co.tz 


  Deadline 24.5.2017


  0 0
 • 05/21/17--23:28: Article 14


 • 0 0
 • 05/21/17--23:35: KUKUA KWA UHALIFU MTANDAO

 • Na Yusuph Kileo
  Kumeendelea kukua kwa uhalifu mtandao maeneo mengi duniani – Huku baadhi wakitafsiri hili linatokana na wana usalama mtandao kuonekana kulemewa (Kuzidiwa) na wahalifu mtandao. Hili limepingwa katika kikao kilicho kamilika mwishoni mwa wiki iliyopita, Nchini Afrika kusini ambapo binafsi nilishiriki na kuzungumza na wenzangu kuhusiana na namna sahihi ya uchunguzi wa makosa ya kimtandao – Kubwa nililozungumzia ilikua ni kuwa rudisha wenzangu kwenye mstari kwa kuwakumbusha juu ya taratibu tulizojiwekea na zinazo takiwa kufatwa na mataifa yote duniani. Pamoja na mambo mengine, nilikumbusha umuhimu kuhakiki hatua zote za uchunguzi zinakua katika maandishi – Zaidi, nilicho zungumza pia kinaweza kupatikana katika Habari inayoweza kusomeka: BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1699 | 1700 | (Page 1701) | 1702 | 1703 | .... | 3272 | newer