Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1698 | 1699 | (Page 1700) | 1701 | 1702 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akizungumza na wafanyabishara katika hafla ya Msaada wa Chakula kwa waathirika na maafa ya Mvua za Masika na upepo mkali uliotokea hivi karibuni, vilivyotolewa na Wafanyabiashara mbali mbali katika viwanja vya Ikulu Mjini Z
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)akipokea fedha taslimu za Kitanzanuia Shilingi Millioni kumi kutoka kwa Mwakilishi wa kuteuliwa na Rais na Mfanyabishara Mhe,Ahmada Yahya Abdulwakil katika hafla ya Msaada wa Chakula kwa waathirika na maafa ya Mvua za Masika na upepo mkali uliotokea hivi karibuni vilivyotolewa leo na Wafanyabiashara mbali mbali katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar,(wa pili kulia) Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mhe,Mohamed Raza Daramsi,[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akipokea msaada wa Chakula kutoka kwa Hassan Mohamed Raza kwa waathirika na maafa ya Mvua za Masika na upepo mkali uliotokea hivi karibuni,chakula hivyo vikiwemo Unga wa Ngano,Mafuta,Mchele na Sukari, vilivyotolewa leo na Wafanyabiashara mbali mbali katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar (wa pili kulia) Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mhe,Mohamed Raza Daramsi na (kushoto) Mfanyabiashara Said Bophar,[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.
  Baadhi ya Waandishi wa habari na Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya kukabidhi ya Msaada wa Chakula kwa waathirika na maafa ya Mvua za Masika na upepo mkali uliotokea hivi karibuni, vilivyotolewa leo na Wafanyabiashara mbali mbali katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) ,[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na wafanyabishara mbali mbakli katika hafla ya kukabidhi Msaada wa Chakula kwa waathirika na maafa ya Mvua za Masika na upepo mkali uliotokea hivi karibuni,mazungumzo hayo yalifanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.

  0 0

  Wachimbaji wadogo wa madini, wachuuzi na madalali wa madini nchini wanatarajia kufanya mdahalo wa kitaifa juu ya umuhimu wa sekta ya madini na namna ya kuwanufaisha zaidi.

  Mkurugenzi wa shirika la Haki Madini Amani Mhinda, akizungumza mji mdogo wa Mirerani na viongozi wa chama cha wachimbaji madini mkoani Manyara (Marema) alisema mdahalo huo utafanyika mkoani Geita.

  Mhinda alisema lengo la mdahalo huo ni kuwaleta wadau mbalimbali kwa pamoja ili kuzungumzia changamoto zinazoikabili sekta hiyo kwa wachimbaji wadogo na kutafakari kitaifa maono ya wachimbaji. 

  Alisema wanatarajia kufanya mdahalo huo mwishoni mwa mwezi Juni kwa kushirikiana na shirika kiongozi duniani la maendeleo la International Institute for Environment and Development (IIED). 

  “Haki madini tunarajia mpango huu utatoa jukwa hitajika kwa wadau kushirikiana na kubadilishana ujuzi na kukuza utawala bora kuwa sauti kubwa, usalama na utengenezaji,” alisema Mhinda.

  Alisema uchimbaji mdogo wa madini unaweza kutoa mchango chanya wenye umoja na usawa wa maendeleo endelevu na ukuaji wa uchumi, kwani husaidia mamilioni ya watu hasa wanawake na watoto. 

  Katibu wa Marema Tawi la Mirerani, Abubakari Madiwa alisema kupitia mdahalo huo wanatarajia wachimbaji mdogo kunufaika kwa kujengewa uwezo hivyo wamejiandaa kushiriki mara utakapofanyika.

  “Haki madini imekuwa msaada mkubwa kwa wachimbaji madini wadogo kwani tumekuwa pamoja bega kwa bega kwa kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapata haki zao,” alisema Madiwa.
  Viongozi wa chama cha wachimbaji madini Mkoani Manyara, Marema Tawi la Mirerani Wilayani Simanjiro, wakizungumza na viongozi wa shirika la Haki Madini juu ya mdahalo wa kitaifa wa madini unaotarajia kufanyika Mkoani Geita
  Mtafiti wa shirika la IIED la Uingereza, Fitsum Weldegiorgis akizungumza juzi na viongozi wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Manyara, Marema (kushoto) ni Mkurugenzi wa shirika la Haki Madini, Amani Mhinda.
  Viongozi wa chama cha wanunuzi na wachuuzi wa madini ya Tanzanite Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuzungumza na viongozi wa shirika la Haki Madini juu ya mdahalo wa kitaifa wa madini unaotarajia kufanyika Mkoani Geita. 

  0 0


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Dodoma


  Tafiti mpya iliyozinduliwa leo inasema serikali inapoteza fedha zaidi ya Sh trillion 4 kwa mwaka kutokana na misamaha na ukwepaji wa kodi.

  Pia repoti inasema serikali inasema serikali inapoteza Dola za kimarekani 1.3 biloni (2.9 trilion) kutokana na rushwa na ufisadi katika bajeti ya Taifa.

  Hayo yamesemwa na Profesa Honest Ngowi alipokuwa akiwasilisha matokeo ya utafiti na mapitio ya ripoti ya swali la dola bilioni moja na kuja na swali Tanzania inapoteza kiasi gani cha fedha?.

  Profesa Ngowi katika mapitio hayo amepata kutaja kuwa , Mfumo wa ulipaji kodi , Mlipa kodi,Misamaha ya kodi ,Utroshwaji wa fedha nje ya nchi na upotevu wa mapato,Ukwepaji kodi, Madhara na Gharama za upotevu na kutokusanywa kodi ipasavyo ni moja ya mambo yanayochangia kupotea kwa fedha hii.

  “Tatizo la utoroshwaji wa fedha nje ya nchi na upotevu wa mapato limeangaliwa upya katika utafiti huu na kubaini kuwa Tanzania bado inapoteza mapato kwa njia ya utoroshaji fedha zilizopatikana kwa njia zisizo halali ,Zinaondoshwa nchini visivyo na kutumiwa isivyo halali” amesema Prof Ngowi.

  Ametaja kuwa fedha hizo zinaweza kuwa ni fedha zitokanazo na biashara haramu kama biashara ya kulevya , biashara haramu mipakani ,uharamia ,usafirishaji binadamu ,mapato kutokana na ukwepaji kodi na mapato yatokanayo na rushwa.

  Amesema kuwa sambamba na utoroshwaji wa fedha ,tatizo la kutoa taharifa za uongo wa bei.
  Kamati ya Viongozi wa dini ya Masuala ya haki za Binadamu ,Kiuchumi na uadilifu katika Uumbaji wakizindua Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani? wakizindua Ripoti hiyo, wakiwa na Wabunge
  Kamati ya Viongozi wa dini ya Masuala ya haki za Binadamu ,Kiuchumi na uadilifu katika Uumbaji wakizindua Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani? wakiwa na wabunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakionyesha Vitabu juu mara baada ya uzinduzi.


  0 0

  Mkuu wa mkoa Mhe. Mrisho Gambo mapema leo amezindua mradi mkubwa wa maji wa maji kwaajili ya kunyweshea mifugo(cattle trough) na matumizi ya binadamu katika kata ya Ndepes wilayani Ngorongoro.

  Mradi huo mkubwa wa maji umetumia takribani milioni 200 ikiwa ni gharama nzima za mradi huo, utekelezaji wa mradi huo umesimamiwa na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ikiwa ni utekelezaji wa agizo la waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alilolitoa mapema mwezi wa Desemba 2016, moja ya maagizo yake ilikua ni wananchi kujengewa mfumo wa maji kwa matumizi yao na mifugo yao ili kuzuia  uingizwaji wa mifugo katika crater ya Ngorongoro.

  Aidha Mhe. Gambo ameipongeza mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwa kuutekeleza mradi huo kwa wakati na kuendelea kutoa msisitizo kwa wananchi kuwa agizo la kutoingiza mifugo ndani ya crater linaendelea na amezitaka mamlaka kuanza mchakato wa kuligeuza agizo hilo kuwa sheria ili liweze kutekelezeka kwa vitendo zaidi.

  Wananchi wa eneo la Ndepes wameishukuru sana serikali ya awamu ya tano kwa kutekeleza ahadi yake ya kuhakikisha wananchi hawafuati maji umbali zaidi ya mita mia nne kama ilivyo ahidiwa katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
   

   


  0 0


  0 0

  Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata), umelalamikia tozo, ushuru wa masoko na tozo za kusafirisha kwa gunia badala ya kutozwa kwa uzito, kwani hujenga mazingira shawishi kwa wanunuzi na madalali kuzidisha uzito wa vifungashi zaidi ya kiwango stahiki. 

  Mratibu wa Mviwata mkoani Manyara, Martin Pius alisema hayo mjini Babati kwenye warsha ya uboreshaji matumizi ya vipimo na kuzingatia vipimo sahihi vya ujazo na matumizi ya mizani wakati wa kufanya biashara ya mazao ya kilimo. 

  Pius alisema lengo lao ni kutafuta hatua za pamoja kwenye kuboresha biashara ya mazao ya kilimo kwa kuzingatia vipimo sahihi vya ujazo ili kuongeza tija kwa wakulima, wanunuzi na halmashauri kwa ujumla. 

  Alisema inatakiwa kuandaa mpango wa pamoja unaotekelezeka kwa ajili ya kuwezesha matumizi ya vipimo katika wilaya ya Babati na kupashana habari ya maboresho katika sheria ya vipimo, kanuni zake na marekebisho yaliyofanywa. 

  “Matumizi sahihi ya vipimo ni muhimu sana katika kuhakikisha uwazi na uhakika wa vipimo vinavyotumika, ili wazalishaji, wanunuzi na watumiaji walindwe na serikali ikusanye mapato inayostahili na takwimu sahihi za uzalishaji na mauzo zipatikane,” alisema. 
  Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Manyara, Mhandisi Munis Weransari akifungua warsha ya matumizi sahihi ya vipimo kwenye mazao iliyoandaliwa na Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata) na kufanyika mjini Babati 
  Katibu Tawala Msaidizi Mkoani Manyara, (Huduma za Uchumi na Uzalishaji) Felix Mwasenga akifunga warsha ya matumizi sahihi ya vipimo kwenye mazao iliyoandaliwa na Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata) na kufanyika mjini Babati . 


  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  TGNP Mtandao imesema kuwa changamoto inayowakabili wanafunzi wa vyuo  vikuu nchini ni rushwa ya ngono.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwapongeza wasichana 38  waliofanya vizuri katika elimu ya Juu kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa  TGNP,  Lilian Liundi amesema wanawake wengi wanashindwa kufikia malengo kutokana na changamoto ya ngono na kufanya wanawake kuwa wanyonge.

  Amesema kuwa wanawake wanaonekana daraja la pili hali ambayo inafanya kuendelea kuweka mfumo dume wa maamuzi kufanywa na wanaume.Lilian amesema kuwa wasichana ambao wamefanya vizuri  katika vyuo mbalimbali inaonyesha ukombozi wa wanawake katika kuleta maendeleo ya kumuokoa mwanamke mwezie.

  Aidha amesema kuwa TGNP Mtandao imekuwa katika mstari wa mbele katika kuendesha harakati za kumkomboa mwanamke katika changamoto mbalimbali.Mmoja wahitimu wa waliofanya vizuri , Aisha Soudy  kutoka  Chuo cha  Teku, amesema kuwa wasichana wanachangamoto nyingi ikiwemo na mila na tamaduni ambayo unampendelea zaidi mtoto wa kiume.
  Amesema kuwa yuko tayari katika kufanya ukombozi wa mwanamke kwa kutoa msaada pale anapoona anawajibu wa kufanya kwa ajili ya kumuinua Mwanamke.

  Kwa upande wa Mhitimu aliyefanya vizuri katika matokeo ya Chuo Kikuu cha Dodoma, Sara Mgonela amesema kuwa msichana ana nafasi yake kama  akijitambua anataka kufanya nini katika jamii yake katika kuleta tofauti  kuliko vile wanavyofikiria.Sara amesema kuwa licha kukabiliwa na changamoto kama mtoto wa kike lakini ameweza kufanya vizuri na kuwataka wasichana kujiamini kuwa wanaweza.
   Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi akizungumza na waandishi habari kuhusu kuwapongeza wahitimu waliofanya vizuri katika vyuo mbalimbali nchini katika ukumbi wa TGNP  leo jijini Dar es Salaam. 
   Msichana aliyefanya vizuri katika Chuo Kikuu cha Dodoma, Sara Mgonela akizungmza na waandishi habari juu umahiri wake ambao ulimuwezesha kufanya vizuri katika matokeo ya mwisho katika chuo katika hafla ya kuwapongeza wasichana waliofanya vizuri katika matokeo uliofanyika leo katika Ukumbi wa TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam.
   Msichana aliyefanya vizuri katika Chuo Kikuu cha  Kairuki, Flora Njiku akizungmza na waandishi habari juu rushwa ya ngono kwa watoto wa kike vyuoni katika hafla ya kuwapongeza wasichana waliofanya vizuri katika matokeo ya vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini uliofanyika leo katika Ukumbi wa TGNP jijini Dar es Salaam.


  Mkutano uliendelea 

  0 0

  Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) anakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya ngazi za Cheti na Diploma katika kampasi za Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya katika kozi zifuatazo:

  Uhasibu (Accountancy),  Utawala katika Biashara (Business Administration), Masoko (Marketing), Manunuzi na Ugavi (Procurement & Supplies Management), TEHAMA (ICT) na Vipimo na Mizani (Legal & Industrial Metrology).Katika mwaka wa masomo 2017/18 Chuo kitatumia mitaala mipya inayoendana na hali halisi ya mahitaji ya soko la ajira.
  SIFA ZA KUJIUNGA
  CHETI - Mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne na kupata ufaulu wa angalau "D" nne.
  DIPLOMA - Mwanafunzi aliyemaliza kidato cha sita na kupata angalau, principal pass
  moja na subsidiary pass moja, Au mwenye elimu ya ngazi ya cheti kutoka katika Chuo kinachotambulika na NACTE
  NAMNA YA KUFANYA MAOMBI
  - Online kupitia www.cbe.ac.tz
  - Au fika katika Kampasi yoyote ya CBE na Vyeti halisi, pamoja na  Ada ya maombi 25,000/=

   Pia Chuo kinatoa Bachelor degree, Postgraduate diploma na Masters degree. Maombi ya kujiunga yanaendelea.
  MASTER'S DEGREE NI HIZI ZIFUATAZO
  1) ICT Project Management - DAR Campus
  2) ICT for Development - DAR Campus
  3) Supply Chain Management - DAR, DODOMA
  4) International Business Management - DAR na DODOMA
  VILEVILE, kampasi za Dar na Dodoma, kuna kozi nzuri ya Ualimu wa Masomo wa Biashara, yaani Bachelor of Business Studies with Education (BBSE), Changamkia


  ADA ZETU NI NAFUU NA ZITALIPWA KWA AWAMU
  Kumbuka, Chuo ni cha Serikali na kinao uzoefu wa miaka 52 katika Elimu ya Biashara

  Imetolewa na
  Kitengo cha Uhusiano na Masoko,
  Chuo cha Elimu ya Biashara
  0715 722 467

  0 0


  Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umefikia tamati katika ukumbi wa mikutano wa Kikwete  Ikulu Jijini Dar es Salaam, ukiwa umehudhuriwa na  ujumbe kutoka nchi zote sita wanachama.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika mkutano huu wakati wa kukabidhi kiti cha Uwenyekiti amesema katika kipindi cha miaka miwili ya Uwenyekiti wa Tanzania, Jumuiya ya Afrika Mashariki imepata mafanikio makubwa na kuifanya istawi zaidi katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara kutokana na kupunguzwa kwa vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiforodha, kuboreka kwa mfumo wa elimu ya Juu ndani ya Jumuiya na kuongezeka kwa Sudan Kusini katika Jumuiya. 
  Aidha, mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais wa  Uganda Mhe. Yoweri Museveni akiongea mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo amesema kuna kila sababu ya kulinda na kudumisha mtangamano uliopo kwa kuwa unaharakisha kasi ya maendeleo ya nchi wanachama na watu wake, unaimarisha ulinzi na usalama wa nchi wanachama, na kudumisha undugu wa kihistoria uliodumu kwa muda mrefu miongoni mwa nchi wanachama. 
  Mkutano huo pia  umeshuhudia viapo vya viongozi wapya wawili katika ngazi ya Jumuiya ambao ni Jaji wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Sudan Kusini, Jaji Charles Oyo Nyawezo na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  Mhandisi Steven Mrote kutoka Tanzania.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni kwenye Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto
  Meza kuu ya viongozi ikiwa imesimama wakati wa wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mkutano huo.
  Wajumbe wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribishwa kitini pake Mwenyekiti mpya Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayemaliza muda wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli na anayeingia Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakirekebisha mpangilio wa majina.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.Semina hiyo, itafuatiwa na Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki hiyo, utakaofanyika kesho Mei 20, 2017.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha. Semina hiyo, itafuatiwa na Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki hiyo, utakaofanyika kesho Mei 20, 2017.
  Mwenyekiti wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB, Mwasajuni akiongoza semina hiyo
  Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambwa akipitia moja ya vitabu vya mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
  Mkurugenzi wa Masoko, Utafitii na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB PLC, Tully Mwambapa akifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
  Naibu Wakurugenzi  Watendaji wa Benki ya CRDB PLC,  Saugata Bandyopadhyay (kulia) na Esther Kitoka wakiteta jambo, wakati wa ufunguzi wa semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.


  0 0


  Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) imewahakikisha kuwapatia mikopo wakulima wa Zao la Karafuu visiwani Zanzibar katika kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta Mapinduzi yenye tija katika wakulima hao.

  Hayo yalielezwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga wakati akitoa mada juu ya fursa zinazopatikana kwa ajili ya wakulima na wadau wa kilimo cha karafuu visiwani Zanzibar katika Kikao cha Wadau wa Karafuu kilichokuwa kinafanyika mjini Unguja.

  Bw. Assenga alisema kuwa Serikali inatambua changamoto wanazokutana nazo wakulima nchini na hivyo uanzishwaji wa TADB unalenga kutekeleza hatua mbalimbali zikilenga kuharakisha mapinduzi na maendeleo katika Sekta ya Kilimo ikiwemo uendelezaji wa zao la karafuu ambalo ni zao kuu la biashara visiwani Zanzibar.

  “Tunatambua kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) iliweka Mkakati Maalum wa miaka 10 (2011 -2021) wa kuongeza uzalishaji, usafirishaji, ubora na tija wa zao la karafuu kwa kutambua hilo Benki inakuja kuongeza kasi juhudi hizi za Serikali,” alisema.

  Alisema kwa kutambua juhudi za SMZ zao la karafuu lilipewa kipaumbele cha pekee miongoni mwa minyororo ya thamani ya kwanza kuanza kupatiwa mikopo na Benki hiyo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao mbalimbali nchini.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) akimsikiliza Katibu na Mwanasheria wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC), Bw. Ali Hilali Vuai (kulia) wakati wa Kikao cha Wadau wa Karafuu ambapo TADB ilialikwa kuwasilisha mada. 
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC), Bw. Kassim Maalim Suleiman (kushoto) akizungumza wakati wa Kikao cha Wadau wa Karafuu ambapo TADB ilialikwa kuwasilisha mada juu ya fursa zinazopatikana kwa ajili ya wakulima na wadau wa kilimo cha karafuu. 
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga akiwasilisha mada juu ya fursa zinazopatikana kwa ajili ya wakulima na wadau wa kilimo cha karafuu wakati wa Kikao cha Wadau wa Karafuu visiwani Zanzibar. 
  Meneja wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC), Bw. Ali Usi (kulia) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha (katikati).


  0 0

  Na Veronica Simba - Arusha

  Jumla ya wanawake 18 kutoka mikoa mbalimbali nchini, jana (Mei 19, 2017) wamehitimu mafunzo ya ukataji na ung'arishaji madini ya vito katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), kilichopo jijini Arusha. 

  Wahitimu hao wa awamu ya nne, wamefanya idadi ya waliohitimu tangu kuanzishwa mafunzo husika katika Kituo hicho kufikia 65.

  Akizungumza katika sherehe za Mahafali hayo, Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, alitoa wito kwa wadau wa madini ya vito nchini, kuwapa ajira na ushauri wa kitaalam wahitimu, ili waweze kujiajiri katika shughuli za uongezaji thamani madini. 

  "Lengo ni kuhakikisha kuwa ukataji unafanyika kwa viwango vya kimataifa ili kuweza kuuza zetu kwenye masoko ya nje."

  Aidha, Dkt. Pallangyo alitoa changamoto kwa wadau wote wa madini ya vito kuendelea kukuza shughuli za uongezaji thamani madini kwa kubadilishana uzoefu na wakataji wa madini ya vito mahiri duniani. 

  "Kwa wale wafanyabiashara wa madini ya vito, mlioajiri wataalam wa kigen, natoa rai muendelee kuwahimiza watoe mafunzo kwa watanzania wanaofanya nao kazi, ili kuhawilisha utaalam huu adimu," alisisitiza. 

   Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mwenye koti la mauamaua), akikagua kazi za uongezaji thamani madini ya vito, zinazofanywa katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), kilichopo jijini Arusha.
   Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, akisoma historia ya Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), kwa Mgeni Rasmi (hayupo pichani).
  Mwanafunzi bora, Happiness Ernest, akipokea zawadi yake kutoka kwa Mgeni rasmi.

  Mgeni Rasmi katika sherehe za mahafali ya Nne ya Mafunzo ya uongezaji thamani madini ya vito nchini, Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mwenye koti la mauamaua – walioketi) na Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (kulia kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir, akisoma taarifa ya shule kwa Mgeni rasmi katika mahafali hayo ya 29 ya kidato cha Sita, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Hamis Mataka (kulia), wakati wa mahafali hayo. Kushoto ni Mwalimu wa Taaluma, Mwalimu Rashid Kassim.
  Mgeni rasmi katika Mahafali ya 29 ya kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Hamis Mataka, akizungumza na wahitimu hao, wakati wa mahafali hayo, jijini Dar es Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir na kulia ni Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Al- Haramain, Mwalimu Suleiman Urassa.
  Mgeni rasmi katika Mahafali ya 29 ya kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Hamis Mataka, akimkabidhi cheti cha Kiongozi Bora, mhitimu Khadija Mashaka, wakati wa mahafali hayo, jijini Dar es Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir.
  Mgeni rasmi Sheikh Hamis Mataka, akimkabidhi cheti Mwanafunzi Bora katika somo la Geography, mhitimu Mussa Baruti, wakati wa mahafali hayo, jana, jijini Dar es Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuh Jabir.


  0 0

  DROO ya saba ya mchezo wa Kubahatisha wa Biko, Ijue Nguvu ya Buku imechezeshwa leo jijini Dar es Salaam, huku Sospeter Muchunguzi akifanikiwa kuibuka kidedea na kuzoa Sh Milioni 10.

  Mkazi huyo wa jiji alifanikiwa kujinyakulia zawadi hiyo ya juu ya Sh Milioni 10 kutoka Biko, katika droo iliyochezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa ushirikiano na Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.

  Akizungumza katika droo hiyo ya saba, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba Watanzania wameendelea kupata hamasa kubwa na kujitokeza kwa wingi kuwania zawadi mbalimbali za fedha taslimu kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni 1,000,000. 
  Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akizungumza jambo wakati wa kuchezesha droo ya saba ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10 ambapo bwana Sospeter Muchunguzi wa Ubungo, jijini Dar es Salaam alitangazwa mshindi.
  Kajala Masanja akionyesha namba ya mshindi.

  “Ni furaha kwetu kuona idadi kubwa ya Watanzania inajitokeza kwa wingi kucheza Biko na kupata zawadi mbalimbali kutoka kwetu kwa kucheza bahati nasibu yetu kwa kufanya miamala kuanzia Sh 1000 ambapo kwenye namba ya kampuni wataingiza 505050 na namba ya kumbukumbu ni 2456.

  “Biko bado inaendelea kuchanja mbuga ambapo sasa tutakuwa tunachezesha droo kwa siku ya Jumatano na Jumapili kwa ajili ya kuhakikisha kwamba kila mtu anaibuka na ushindi wa Biko na kuzoa mamilioni kutoka kwenye bahati nasibu yetu,” Alisema Heaven.

  Naye Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe, aliwataka Watanzania kuendelea kuchangakia zawadi za Biko kwa kucheza kwa wingi kutokana na utaratibu mzuri na urahisi wa mchezo wa Biko.

  “Bodi yetu ipo makini kufuatilia kwa kina uchezaji wa bahati nasibu, hivyo tunawaomba watu wacheze kwa sababuBiko ni mchezo salama na unafuata kanuni, sheria na taratibu zote,” Alisema Chiku ambaye pia aliwaasa akina mama kujitokeza kwa wingi ili nao washinde mamilioni ya Biko.

  Akizungumza kwa simu, mshindi huyo wa droo ya saba ya Biko, Sospeter Muchunguzi, alishukuru kwa kuibuka na ushindi huo, akisema ni mchezaji mzuri wa bahati nasibu hiyo ambapo mbali na kushinda Sh Milioni 10, pia amewahi kushinda zawadi za papo hapo mara kadhaa.

  Baada ya kutangazwa mshindi wa Sh Milioni 10, Biko watamkabidhi mshindi huyo fedha zake mapema wiki hii kama walivyokabidhiwa wengine ili waziweke katika mipango yao ya kimaisha.

  0 0


  Serikali imefurahishwa na na juhudi za Mfuko wa Pensheni PPF kwa kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 99,983,700 kwa hospitali 16 hapa nchini ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini. 

  Akielezea furaha hiyo wakati akipokea sehemu ya msaada huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 6 kwa hospitali ya mkoa wa Morogoro, Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Zainab Chaula amesema kumekua na chanagamoto mbalimbali za vifaa tiba katika hospitali mbalimbali hapa nchini. 

  Kwa upande wake meneja wa uhusiano wa PPF, Lulu Mengele amesema pamoja na kutoa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendana na hayo kwa wanachama wake kutoka kwenye sekta rasmi na isiyokuwa rasmi. Mfuko wa Pensheni wa PPF katika sera yake ya uchangiaji na udhamini ambapo moja kati ya sehemu wanayochangia ni upande wa sekta ya afya ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi milioni 99,983,700 zimetolewa kununulia vifaa tiba vinavyogawiwa katika hospitali na vituo vya afya 16 vya serikali nchini. 

  Sehemu ya vifaa hivyo vilivyotolewa ni muendelezo wa zoezi la kukabidhi vifaa tiba lilizinduliwa na waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wa 26 wa wanachama na wadau wa PPF uliofanyika machi 2017 jijini Arusha. 

  Naye meneja wa PPF kanda ya mashariki na kati, Bw. Michael Christian alisema kuwa PPF wanao mfumo wa uchangiaji wa hiari ‘WOTE SCHEME’ ambapo aliwakaribisha wananchi waliokatika sekta isiyo rasmi kujiunga ili kunufaika na mafao ya uzeeni, huduma za bima za afya pamoja na mikopo ya elimu na mikopo ya maendeleo. Vile vile wale walio sekta rasmi wanakaribishwa kujiunga kama mfumo wa hiari ili kuweza kujiwekea akiba na kunufaika na mikopo ya elimu na mikopo ya maendeleo.
  Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (kulia) akimkabidhi msaada wa mashuka Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa Bi. Zainab Chaula (kushoto) kwa ajili ya hospitali ya Rufaa ya Morogoro. Msaada huo ni sehemu ya vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko huo ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi milioni 99,983,700 zimetolewa kununulia vifaa tiba vinavyogawiwa katika hospitali na vituo vya afya 16 vya serikali nchini. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG. 
  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali ya mitaa Bi. Zainab Chaula (kushoto) akimkabidhi mashuka ambayo ni sehemu ya vifaa tiba kwa Meya wa Manispaa ya Morogoro, Paschal Mahanga (kulia) kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Morogoro. Wengine wanaoshuhudia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (wa kwanza kushoto) na Meneja wa PPF Kanda ya Mashariki na Kati, Bw. Michael Christian. 
  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mkoa na Serikali ya Mitaa Bi. Zainab Chaula akitoa shukrani kwa PPF kwa kuweza kurudisha sehemu ya mapato yake kwa jamii kwa kutoa vifaa tiba.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mkewe  Mama Mwanamwema Shein (kushoto) pamoja na Mshauri wa Rais Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Uchumi pia Mwenyekiti wa Kamati ya Uchangiaji Vifaa vya Michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar Mhe.Mohamed Ramia wakiangalia picha ya zamani wakati Dk.Shein alivyokuwa akishiriki mchezo wa Riadha katika Skuli ya Lumumba picha hiyo iliyofikishwa katika hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika viwanja vya  Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja.
  haf3
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (katikati) wakiwa na Viongozi mbali mbali katika hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika  Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  Mnazi Mmoja Mjini Unguja akiwepo Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi (wa pili kulia),[Picha na Ikulu.] 20/05/2017. 
  haf8
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma alipokuwa akitangaza mchango wake wa Milioni moja kumdhamini Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika viwanja vya  Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.
  haf9
  Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein alipokuwa akitangaza mchango wa Millioni nane kwa niaba ya familia yake kumdhamini Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa mgeni rasmi katika hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika viwanja vya  Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja.
  haf10
  Picha  ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipiga mpira wakati wa Uzinduzi wa Mashindano ya Vyuo Vikuu ikinadisha wakati wa hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika viwanja vya  Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja.
  haf4
  Viongozi na Wafanyabiashara mbali mbali wakiwa katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja wakiwa hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.]  20/05/2017. 


  0 0

  Na mwandishi wetu, Zanzibar 

  Chama cha Ushirika cha Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane kilichopo eneo la Maruhubi mjini Unguja kimeiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuwasaidia katika kuendeleza ushirika wao kwa kuwapatia mikopo na mahitaji mengine ili kuboresha huduma zao. 

  Akizungumza katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika eneo la ushirika huo mjini Unguja, Mwenyekiti wa Tusiyumbishane, Bw. Haji Omar Haji amesema licha ya fursa kubwa iliyopo kwenye eneo la ukaushaji wa madagaa, ushirika wao unakabiliwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu na ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha za mtaji kwa ajili ya kuboresha huduma zao. 

  Bw. Haji ameongeza ukosefu wa mikopo ya uhakika imekuwa ni changamoto kubwa inayochangia kurudisha nyuma ukuaji wa biashara hiyo hivyo kuwa kikwazo katika kupambana na umaskini wa kipato miongoni mwa washirika wa umoja huo hivyo akaiomba benki hiyo kuwawezesha ili kuongeza tija ya shughuli zao. 

  “Uduni wa mitaji ya uhakika inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mabenki na taasisis nyingine za kifedha kushindwa kutuwezesha sie wajasiriamali wa hali ya chini kwa kukosa sifa wazitakazo, hivyo tunaiomba TADB kutuwezesha ili tuongeze tija katika shughuli zetu,” Bw. Haji aliongeza. 
  Wajumbe wa Kikao cha Pamoja kati ya Chama cha Ushirika cha Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane kilichopo eneo la Maruhubi mjini Unguja na ugeni wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). Kikao kilijadilia changamoto zinazozikabili Ushirika huo na namna TADB inavyoweza kuwasaidia katika kuendeleza ushirika huo. 
  Mtaalamu wa Ushirika kutoka Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Bw. Khamis Mkanga (katikati) akiendesha Kikao cha Pamoja kati ya Chama cha Ushirika cha Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane kilichopo eneo la Maruhubi mjini Unguja na ugeni wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia). 
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (wapili kulia) akizungumza na Wanaushirika wa Chama cha Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane wakati alipofanya kikao na umoja huo. Kikao hicho kilifanyika eneo la Maruhubi mjini Unguja. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Ushirika huo Bw. Haji Omar Haji na Mtaalamu wa Ushirika kutoka Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Bw. Khamis Mkanga (wapili kushoto). 
  Mmoja wa Wanaushirika wa Chama cha Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane, Bibi Bahati Shabani (kulia) akitoa maelezo kuhusu shughuli za uchakataji wa dagaa. Bibi Bahati alimuelezea Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) changamoto wanazokabiliana nazo katika shughuli hiyo. 


  0 0


  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Graceana Shirima, akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Mradi wa Ukarabati wa Shule ya Sekondari Pugu, iliyopo Wilaya ya Ilala Dar es Salaam (katikati) Kaimu Mkurugenzi TEA, Dk. Erasmus Kipesha, na Kaimu Mwanasheria TEA Igenge Edwin. (Picha na Francis Dande).
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela, akizungumza katika makabidhiano ya Mradi wa Ukarabati wa Shule ya Sekondari Pugu, iliyopo wilaya ya Ilala Dar es Salaam (kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA Graceana Shirima (kulia), Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu, Jovinus Mutabuzi.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Graceana Shirima, akimkabidhi baadhi ya nyalaka Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Miliki Shirika la Nyumba la Taifa, Hassan Mohamed, katika hafla ya makabidhiano ya Mradi wa Ukarabati wa Shule ya Sekondari Pugu, iliyopo wilaya ya Ilala Dar es Salaam. 
  Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa TEA, Sylvia Lupembe akijadiliana jambo na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Pugu wakati wa hafla hiyo.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa wakati alipomtembelea  Rais huyo Mstaafu nyumbani kwake jijini Dar es salaam Mei 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa wakati alipomtembelea Rais huyo Mstaafu  nyumbani kwake jijini Dar es salaam Mei 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


older | 1 | .... | 1698 | 1699 | (Page 1700) | 1701 | 1702 | .... | 3270 | newer