Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1697 | 1698 | (Page 1699) | 1700 | 1701 | .... | 3282 | newer

  0 0


  0 0

   YaraLIVA NITRABOR ni mbolea maalumu yenye Calcium inayoyeyuka pamoja na boron kwa ajili ya uchevushaji wa maua, kurefusha muda wa mazao kutokuharibika  kwa haraka na huongeza ubora wa mazao ya mbogamboga na matunda.
  Matumizi:
  1.       Weka gramu 145 kwenye bomba la lita 15
  Zingatia:
  ·         Pulizia kwenye majani na sio kwenye udongo
  ·         Tafadhali wasiliana na bwana shamba wa kampuni ya Yara kwa maelekezo na mahitaji maalumu
  Wasiliana na wataalamu wa Yara Tanzania Ltd kwa kupiga *149*50*31# BURE au +255 22 2112965/6

   Bw. Bagalama, mkulima wa tikiti na karanga mkoani Tabora alienufaika na mbolea aina ya YaraLiva NITRABOR


  0 0

  Na Immaculate Makilika- MAELEZO 
  WAKUU wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatarajia kufanya mazungumzo ya pamoja baina yao katika Mkutano wa kawaida wa 18 utakaofanyika kesho Mei 20 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam. 
   Mkutano huo unatarajiwa kupokea ripoti ya usuluhishi ya kamati inayoongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamini William Mkapa kuhusu mgogoro wa nchini Burundi. Mambo mengine yatakayozungumzwa katika mkutano huo ni pamoja na taarifa na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa katika mkutano wa 17 wa Wakuu wa nchi za Jumuiya hiyo. 
   Masuala hayo ni pamoja na namna ya kuwezesha uundaji wa magari katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kupunguza uagizaji wa magari yaliyotumika kutoka nje ya Jumuiya, mapitio kuhusu sekta ya nguo na ngozi. 
   Aidha masuala mengine ni pamoja na kuzuia ama kuondoa uagizaji wa nguo na viatu vilivyotumika kutoka nje. 
   Wakuu hao wa Nchi pia wanatarajia kujadili namna endelevu ya uchangiaji wa bajeti ya Jumuiya hiyo kwa nchi wananchama. 
   Aidha, katika Mkutano huo wa 18 Tanzania itakabidhi nafasi ya mwenyekiti wa Jumuiya hiyo iliyoishika kwa muda wa miaka miwili kwa nchi ya Jamhuri ya Uganda.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizungumza wakati akifungua Semina ya Bodi ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, iliyoandaliwa na Jumuiya ya Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini (TSSA), iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Gold Crest, Jijini Arusha leo Mei 19, 2017.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizungumza wakati akifungua Semina ya Bodi ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, iliyoandaliwa na Jumuiya ya Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini (TSSA), iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Gold Crest, Jijini Arusha leo Mei 19, 2017.
  Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini (TSSA), akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kufungua semina hiyo, itakayowajengea uwezo Wajumbe wa Bodi ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, kuhusu sekta ya Viwanda kuwa kama fursa ya Uwekezaji, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Gold Crest, Jijini Arusha leo Mei 19, 2017.
  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini (TSSA), Meshack Bandawe akizungumza machache wakati akitoa muongozo wa Semina hiyo, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Gold Crest, Jijini Arusha leo Mei 19, 2017.


  0 0


  Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imejenga uwezo zaidi wa kukabiliana na vitendo vya rushwa katika azma yake ya kujenga uchumi imara utakaostawisha Taifa kwa kuongeza Mapato kupitia Sekta ya Utalii sambamba na Ujenzi wa Viwanda vipya vya kudumu. 
  Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi anayemuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwenye Jukwaa la Dunia la Uchumi { world Economy Forum } wakati akiwasilisha Muelekeo wa Tanzania katika uimarishaji wa Sekta ya Utalii hapo katika Ukumbi wa Mfamle Hassan Bin Talal pembezoni mwa Bahari Nyeusi Mjini Amma Nchini Jordan. 
  Balozi Seif alisema zipo jitihada za ziada zilizochukuliwa katika ujenzi wa miundombinu ndani ya Sekta ya Utalii kutokana na Rasilmali nyingi zilizopo ikiwemo Mbuga za Wanyama, Ardhi yenye Rutba, Fukwe za kuvutia pamoja na Mlima wa Pili kwa urefu Duniani Kilimanjaro zilizoifanya Tanzania kujikita zaidi katika uimarishaji wa Seklta hiyo. 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameuongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Tamasha la Uchumi la Dunia linalofanyika Mjini Amman Nchini Jordan akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli. 


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza Makatibu Mahsusi nchini kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na waache tabia ya kutoa siri za ofisi zao kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anafungua mkutano wa Tano wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Mji Dodoma.
  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema uadilifu na uaminifu ni njia pekee ya kuaminiwa na viongozi wao hivyo ni muhimu kwa makatibu mahsusi nchini kufanya kazi kwa bidii na ubunifu mkubwa katika maeneo yao ya kazi.
  Makamu wa Rais pia amewahimiza makatibu mahsusi kufanya tathmini ya utendaji wao wa kazi na wawe tayari katika kujifunza mbinu mpya za utendaji zinazoendana na mabadiliko ya teknolojia.
  “Sote tunafahamu kuwa dunia imekuwa ni kijiji kutokana na utandawazi unaoletwa na mifumo ya teknolojia hivyo kutokana na mabadiliko haya hamna budi nanyi kubadilika na kwenda na wakati ili msiangaliwe kwa mtazamo hasi wa kuwa wapiga cha tu”
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa mwaka wa 5  wa Chama cha Makatibu Mahususi Tanzania (TAPSEA) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Jakaya Kikwete ,mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

   Sehemu ya wajumbe waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) ambao mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0


  0 0
 • 05/19/17--14:34: Article 1


 • 0 0


  0 0  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori, katika Ukumbi wa CCM Manzese, wakati wa ziara yake ya kuimarisha Chama kwa kuzungumza na Wenyeviti, Makatibu na Wenezi wa Kata, Makatibu wa Jumuiya  ya ngazi za Kata, Wenyeviti wa Mitaa na Mabalozi wa Jimbo hilo la Ubungo jijini Dar esSalaam , jana. 
   Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori, akizungumza kutoa tathmini ya usalama wa kisiasa katika Wilaya yake mbele ya mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick  Mpogolo, aliyekuwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama katika Jimbo la Ubungo, jijini Dar es Salaam, jana. 
   Naibu  Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Makatibu na Wenezi wa Kata, Makatibu wa Jumuiya  ya ngazi za Kata, Wenyeviti wa Mitaa, Mabalozi na Wanachama wa CCM wa Jimbo la Ubungo, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana katika Ukumbi wa CCM manzese jijini Dar Es Salaam. 
   Baadhi ya Viongozi wa Kata ya Salanga Jimbo la Kibamba, wakiwa bize kutunza kumbukumbu ya elimu iliyokuwa ikitolewa kwao na Naibu Katibu Mkuu jana.

  KUSOM ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
  0 0

  Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, wakifatilia Mkutano huo wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dk. Charles Kimei akitoa taarifa ya matokeo ya utendaji wa Benki hiyo pamoja na Kampuni zake Tanzu kwa mwaka uliopita. Mkutano huo unafanyika leo Mei 20, 2017 kwenye Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dk. Charles Kimei akiwasilisha taarifa ya matokeo ya utendaji wa Benki hiyo pamoja na Kampuni zake Tanzu kwa mwaka uliopita, katika Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, unaofanyika leo Mei 20, 2017 kwenye Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB PLC, Ally Hussein Laay akiwasilisha taarifa ya Mwaka na Matokeo ya Kifedha ya Benki hiyo pamoja na Kampuni zake Tanzu kwa mwaka ulioishia Disemba 2016, katika Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, unaofanyika leo Mei 20, 2017 kwenye Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
   Meza kuu katika katika Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB.
   Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambwa akitoa muongozo kwa wajumbe wa Mkutano huo, unaofanyika leo Mei 20, 2017 kwenye Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
  Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, Abeid Mwasajone akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Mkutano huo, unaofanyika leo Mei 20, 2017 kwenye Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, 
  Globu ya Jamii,Mwanza.
  Ligi Kuu Tanzania Bara imemalizika leo kwa timu ya Yanga kutawazwa ubingwa wa msimu wa 2016/17 ikiwa ni  mara 27 toka ligi kuanzishwa.

  Yanga waliokuwa ugenini dhidi ya Mbao iliweza kupoteza mechi hiyo ya mwisho lakini walitawazwa ubingwa kwa idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa dhidi ya Mahasimu wao wakubwa Simba.
  Katika mechi hiyo iliyoanza sa  10 Mbao waliandika goli lao la kwanza na la ushindi katika kipindi cha kwanza  ambapo liliweza kudumu mpaka dakika 90 kumalizika.
  Mechi hiyo iliyochezeshwa na mwamuzi Ludovic Charles kutoka Tabora ilikuwa ya kukamiana kwa kila upande huku akionekana kushindwa kuuhimili mchezo huo.
  Baada ya kumalizika kwa mechi nane za Ligi zilizochezwa kwa mda mmoja timu ya Toto Afrika ya Mwanza na African Lyon zimeshuka daraja zikiungana na JKT Ruvu iliyokuwa tayari imeshajikatia tiketi ya kurudi daraja la kwanza.
  Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Wakiwa wanashangilia baada ya kutawazwa mabingwa leo Jijini Mwanza ikiwa ni mara ya tatu mfululilzo.
   wachezaji nwa Yanga wakipokea medali zao za ubingwa baada ya kutawazwa mabingwa kwa mara ya 27 na mara ya tatu mfululizo.
  Kikosi cha Mbao kilichocheza dhidi ya Yanga leo katika Uwanja wa CCM Kirumba na kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
              Kikosi cha Yanga kilichocheza dhidi ya Mbaoleo katika Uwanja wa CCM Kirumba.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Unguja – Zanzibar akitokea mkoani Dodoma ambapo hapo kesho anatarajiwa kuzindua ya kampeni maalum inayojulikana kama Mimi na Wewe mjini Unguja.

  Lengo la kampeni hiyo ni kuhamasisha jamii kuchangia kwa hali na mali katika uboreshaji wa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo elimu, afya, mazingira na kusaidia watu wasiojiweza katika Mkoa wa Mjini Magharibu, Unguja.

  Katika uwanja wa ndege wa Zanzibar, Makamu wa Rais amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud pamoja na Viongozi Mbalimbali wa Serikali na wa Vyama vya siasa.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Mjini Magharibi,Borafya Silima mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege  wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume. #Picha na Adam H. Mzee/ VPO 

  0 0

  Akielezea furaha hiyo wakati akipokea sehemu ya msaada huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 6 kwa hospitali ya mkoa wa Morogoro, Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Zainab Chaula amesema kumekua na chanagamoto mbalimbali za vifaa tiba katika hospitali mbalimbali hapa nchini. 

  Kwa upande wake meneja wa uhusiano wa PPF, Lulu Mengele amesema pamoja na kutoa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendana na hayo kwa wanachama wake kutoka kwenye sekta rasmi na isiyokuwa rasmi. Mfuko wa Pensheni wa PPF katika sera yake ya uchangiaji na udhamini ambapo moja kati ya sehemu wanayochangia ni upande wa sekta ya afya ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi milioni 99,983,700 zimetolewa kununulia vifaa tiba vinavyogawiwa katika hospitali na vituo vya afya 16 vya serikali nchini. 

  Sehemu ya vifaa hivyo vilivyotolewa ni muendelezo wa zoezi la kukabidhi vifaa tiba lilizinduliwa na waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wa 26 wa wanachama na wadau wa PPF uliofanyika machi 2017 jijini Arusha. 

  Naye meneja wa PPF kanda ya mashariki na kati, Bw. Michael Christian alisema kuwa PPF wanao mfumo wa uchangiaji wa hiari 'WOTE SCHEME' ambapo aliwakaribisha wananchi waliokatika sekta isiyo rasmi kujiunga ili kunufaika na mafao ya uzeeni, huduma za bima za afya pamoja na mikopo ya elimu na mikopo ya maendeleo. Vile vile wale walio sekta rasmi wanakaribishwa kujiunga kama mfumo wa hiari ili kuweza kujiwekea akiba na kunufaika na mikopo ya elimu na mikopo ya maendeleo.
  Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (kulia) akimkabidhi msaada wa mashuka Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa Bi. Zainab Chaula (kushoto) kwa ajili ya hospitali ya Rufaa ya Morogoro. Msaada huo ni sehemu ya vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko huo ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi milioni 99,983,700 zimetolewa kununulia vifaa tiba vinavyogawiwa katika hospitali na vituo vya afya 16 vya serikali nchini. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali ya mitaa Bi. Zainab Chaula (kushoto) akimkabidhi mashuka ambayo ni sehemu ya vifaa tiba kwa Meya wa Manispaa ya Morogoro, Paschal Mahanga (kulia) kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Morogoro. Wengine wanaoshuhudia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (wa kwanza kushoto) na Meneja wa PPF Kanda ya Mashariki na Kati, Bw. Michael Christian.
  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mkoa na Serikali ya Mitaa Bi. Zainab Chaula akitoa shukrani kwa PPF kwa kuweza kurudisha sehemu ya mapato yake kwa jamii kwa kutoa vifaa tiba.  Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele akizungumza mbele ya wageni waliofika katika hafla ya kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi mil. 6,077,800 kwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambapo PPF imetoa sehemu ya mapato yake kwa jamii kulingana na sera ya uchangiaji na udhamini ya Mfuko huo.
  Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya Morogoro, Frank Jacob akitoa shukrani wa PPF. 


  0 0


  0 0

  Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umefikia tamati leo Ikulu Jijini Dar es Salaa. Mkatano huu ulikuwa na ujumbe na uwakilishi kutoka nchi zote sita zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki. . 

  Rais Mhe. Dkt. Magufuli akizungumza katika Mkutano huu wakati wa kukabidhi kiti cha Uwenyekiti amesema katika kipindi cha miaka miwili ya Uwenyekiti wa Tanzania, Jumuiya ya Afrika Mashariki imepata mafanikio makubwa na kuifanya istawi zaidi katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara kutokana na kupunguzwa kwa vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiforodha, kuboreka kwa mfumo wa elimu ya Juu ndani ya Jumuiya na kuongezeka kwa Sudan Kusini katika Jumuiya. 

  Aidha mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Mhe. Museveni akiongea mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo amesema kunakila sababu ya kulinda na kudumisha Mtangamano kwa kuwa unaharakisha kasi ya maendeleo ya nchi wanachama na watu wake, unaimarisha ulinzi na usalama wa nchi wanachama, na kudumisha undugu wa kihistoria uliodumu kwa muda mrefu miongoni mwa nchi wanachama. 

  Pia Mkutano huu wa 18 wa Wakuu wa nchi umeshuhudia viapo vya viongozi wapya wawili katika ngazi ya Jumuiya ambao ni Jaji wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Sudan Kusini, Jaji Charles Oyo Nyawezo na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Eng. Steven Mrote kutoka Tanzania. Katika Kutano huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekabidhi rasmi uwenyekiti kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni. 
  Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia hadhira iliyohudhuria Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaa.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaini moja ya nyaraka ya makabidhiano ya uwenyekiti wakati wa Mkutano wa 18 wa Kaiwa wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mshariki. 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wakwanza kulia) akifuatilia Mkutano. Wengine ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip Mpango (katika) na Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kushoto).
  Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Jaji Charles Oyo Nyawezo kutoka Sudan Kusini kwa kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya kula kiapo. 
  Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mwanafunzi wa kitado cha nne aliyejishindia nafasi ya nne katika mashindano ya uandishi wa insha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Shule ya Sekondari Kibaha, Tanzania Bw.Joseph Mbogo 
  Picha ya pamoja 


  0 0  Na Richard Mwaikenda, Mtama.

  WALIMU na Wanafunzi Mkoa wa Lindi, wamefurahishwa na Kampeni ya Kitaifa ya Hedhi Salama kwa Wasichana iliyofanyika kwa uwazi katika Shule ya Sekondari Mtama.
  Kampeni hiyo iliyozinduliwa juzi na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), mjini Lindi, yalishirikisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari pamoja na walimu katika Jimbo la Mtama.

  Akielezea kuhusu kampeni hiyo, Mwanafunzi Fasda Mahamudu wa Shule ya Sekondari Mtama, alisema kuwa mafunzo aliyoyapata yamemfanya aelewe vizuri kuhesabu siku zake za hevi na jinsi ya kuwa msafi ikiwemo kuoga mara tatu kwa siku na kila baada ya kupata haja.

  Naye Amana Amah mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Likongopele, alisema amefurahishwa na kampeni hiyo iliyoendeshwa kwa njia ya uwazi na kwamba imemfumbua mambo mengi ikiwemo kuzijua aina mbalimbali za pad za kisasa na jinsi ya kuzivaa wakati wa hedhi. Aliomba TGGA kuieneza kwa uwazi elimu hiyo katika shule mbalimbali vijijini.

   Naye Mratibu Elimu Kata ya Mtama, Marcelinus Lukanga, aliwataka wasichana kujiunga kwa wingi TGGA ili waondokane na woga, hofu na kutokuwa na aibu jambo ambalo pia litawasaidia kuwa huru, safi, salama na kutopata kirahisi maambukizi hasa wakati wa hedhi.
   Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Mkoa wa Lindi, Sharifa Mkwango akitoa elimu kwa wanafunzi kuhusu Hedhi salama kwa wasichana  (Manustretion Hygiene) wakati wa kampeni iliyoendeshwa na chama hicho  katika Shule ya Sekondari Mtama, Lindi Vijijini juzi. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG

  Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Zuhura Mohamed akimkabidhi zawadi ya pad Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtama, Asha Namjupa.
   Mratibu Elimu  Kata ya Majengo, Marsenus Lukanga (kulia) akimkabidhi kasha la vihifadhi (Pad),  Mwanafunzi wakati wa Kampeni ya Kitaifa ya Hedhi Salama (Manustretion Hygiene) kwa Wasichana iliyoendeshwa na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), katika Shule ya Sekondari Mtama, Lindi Vijijini juzi.
   Wanafunzi wakishangilia baada ya kufurahishwa na elimu ya hedhi salama.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1697 | 1698 | (Page 1699) | 1700 | 1701 | .... | 3282 | newer