Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MAY 12,2017


KAIMU JAJI MKUU WA TANZANIA AKAMILISHA ZIARA YAKE MKOANI ARUSHA KWA KUONGEA NA WATUMISHI WA MAHAKAMA WA KANDA HIYO

$
0
0



Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akisamiliana na Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Arusha alipowasili katika viwanja vya Mahakama Kuu-Arusha kukamilisha ziara yake ya siku mbili mkoani humo. A
Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,Mhe. Kamugisha akimsomea taarifa ya hali ya utendaji kazi wa Mahakama katika mkoa huo. Lengo la ziara ya Mhe. Kaimu Jaji Mkuu katika Kanda hiyo ni kujifunza na kuona hali halisi ya mazingira ya kazi na utekelezaji wa majukumu.
 A 1
Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Rumisha (wa kwanza kulia) akimuonesha Mhe. Kaimu Jaji Mkuu, moja ya kumbi za Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha pindi alipokuwa akikagua ofisi mbalimbali za Mahakama ya Mkoa na Mahakama Kuu katika Kanda hiyo.
 A 2
Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Juma akiwa katika Kompyuta Mpakato akikagua Mfumo wa Kuratibu takwimu za Mashauri kwa njia ya Kielektroniki (JSDS) kuhakikisha kama inafanya kazi ipasavyo, pembeni ni Afisa TEHAMA, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha, Bw. Athuman
 A 4
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, akiongea na Mahakimu na Watumishi wengine wa Mahakama (hawapo pichani), katika maongezi yake na Watumishi hao Mhe. Jaji Prof. Juma amewataka na kuwasisitiza Watumishi hao kufanya kazi kwa kuzingatia Maadili ikiwa ni pamoja na kuwa na lugha nzuri kwa Wateja/Wananchi wanaowahudumia. kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha na kushoto ni Mhe. Rumisha, Naibu Msajili-Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha.

MAMA JANETH MAGUFULI AMKARIBISHA MAMA SIZAKELE ZUMA OFISINI KWAKE DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa ameongozana na Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma, wakati  wakielekea kwenye ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na  kusaidia wazee walemavu na wale walioathirika na ugonjwa wa ukoma jijini Dar es salaam siku ya Alhamisi. Mama Zuma alikuwa ameongozana na mumewe aliyekuwa katika ziara ya kikazi nchini.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma,  kwenye ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na  kusaidia wazee walemavu na wale walioathirika na ugonjwa wa ukoma jijini Dar es salaam siku ya Alhamisi. Mama Zuma alikuwa ameongozana na mumewe aliyekuwa katika ziara ya kikazi nchini.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa katika mazungumzo na Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma,  kwenye ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na  kusaidia wazee walemavu na wale walioathirika na ugonjwa wa ukoma jijini Dar es salaam siku ya Alhamisi. Mama Zuma alikuwa ameongozana na mumewe aliyekuwa katika ziara ya kikazi nchini.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akipeana mikono na Mke wa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Mama Sizakele Zuma,  kwenye ofisi yake anayoendeshea shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na  kusaidia wazee walemavu na wale walioathirika na ugonjwa wa ukoma jijini Dar es salaam siku ya Alhamisi. Mama Zuma alikuwa ameongozana na mumewe aliyekuwa katika ziara ya kikazi nchini.

CCM Z’BAR YAWAFARIJI WALIOATHIRIWA NA MAFURIKO.

$
0
0


NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

ZAIDI ya Nyumba 300 katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Mjini Magharibi zimeathiriwa na Mvua za masika zinazoendelea kunyesha hivi sasa.

Akizungumza katika mtaa wa ziwa maboga sheha wa shehia ya Tomondo, Bw. Mohamed Omar Said alisema zaidi ya nyumba 200 katika eneo hilo zimeathiriwa na mvua kwa kujaa maji na zingine kuporomoka.

Bw. Said alifafanua kwamba baadhi ya wakaazi wa eneo hilo wamehama katika makaazi yao na kuomba hifadhi katika maeneo mengine yaliyokuwa salama, huku idadi ya nyumba zinazoathiriwa na mvua hizo zikiendelea kuongezeka kadri mvua zinavyioendelea kunyenyesha.

Mbali na maeneo hayo pia katika mitaa ya Meli nne, Fuoni janga mizini na Fuoni Migombani kuna nyumba zaidi ya 100 zimeathiriwa na mvua hizo.

Akizungumza juu ya athari hizo, Mjumbe wa sheha wa shehia ya kibondeni, Bi. Zuhura Ame alisema hali za baadhi ya wananchi waliopata maafa hayo sio nzuri hivyo wanahitaji msaada wa dharura.

Alisema kwamba licha ya viongozi wa majimbo hasa Wabunge, wawakilishi na madini baadhi yao tayari wameanza kutoa msaada na wengine ndio wanajipanga kufika kwa ajiri ya kuwafariji wananchi lakini bado panahitajika nguvu za pamoja baina ya wananchi, vyama vya kisiasa na serikali ili kuinusuru nchi kuingia katika maafa makubwa.

Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma akipokea maelezo kutoka kwa viongozi wa mtaa akiwemo sheha wa shehia ya Tomondo, Mohamed Omar katika eneo la Ziwa maboga ambapo zaidi ya nyumba 200 zimeathiriwa na mvua za masika zinazoendelea kunyesha. 
Nyumba mbali mbali zilizoathiriwa na maji ya mvua katika eneo la Tomondo Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.  
Katibu wa Tawi la CCM Tomondo, Hassan Kipanga Abdalla akimweleza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar hali ya waakazi wa shehia hiyo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Abdalla Juma Saadala akiwafariji wananchi wa eneo la Mwanakwerekwe Meli nne, waliopata maafa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa. 

TADB, TAHA WAPANGA KUSAIDIA SEKTA YA MALI MBICHI NA MATUNDA (HORTICULTURE)

$
0
0

Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) na Asasi Kilele ya wakulima wa Malimbichi na Matunda Tanzania (TAHA) zinajipanga kusaidia sekta Malimbichi na Matunda (horticulture) ili kuongeza tija kwa kilimo hicho.

Watendaji wakuu wa taasisi hizo wamesema kuwa kuna haja ya makusudi ya uwekezaji mkubwa katika sekta ya Malimbichi na Matunda (horticulture) ili kuchagiza na kusaidia mapinduzi katika sekta hiyo na kilimo kwa ujumla nchini.

“Tunajipanga kuchochea ukuaji wa sekta hii ili kuwakwamua wakulima wa malimbichi kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini,” anasema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa ushirikiano kati ya TADB na TAHA kwa kuwa taasisi zote ni za Kilele (apex institutions) zenye kulenga katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kutoka kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha kibiashara na uzalishaji wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
 
Timu ya Maandalizi ya Makubaliano ya ushirikiano katika kuisaidia sekta ya malimbichi na matunda nchini wakiwa katika majadiliano.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Francis Assenga (kulia) akimuelezea Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi (hayupo pichani) nafasi ya TADB katika kuleta mapinduzi ya kilimo nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara, Augustino Chacha. 
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Francis Assenga (kushoto) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi (kulia) nafasi ya TADB katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAHA, Jijini Arusha. 
Timu ya Maandalizi ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya TADB na TAHA katika kuisaidia sekta ya malimbichi na matunda nchini wakiwa katika majadiliano wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano wao. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAHA, Jijini Arusha.

KAMPUNI YA TANCOAL ENERGY YATEKELEZA AGIZO LA SERIKALI

$
0
0
KAMPUNI ya kuzalisha makaa ya mawe nchini, Tancoal Energy Limited imetekeleza kwa zaidi ya asilimia 100 agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa ya kuongeza uzalishaji wa makaa ya mawe maradufu.

Taarifa hiyo iliyotolewa jana na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bw. James Shedd wakati alipokutana na Waandishi wa habari waliotembelea mgodi huo uliopo eneo la Ngaka katika wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

Bw. Shedd amesema kwamba, kampuni yake kwa sasa inazalisha kiasi kikubwa cha makaa ya mawe kukidhi mahitaji ya soko la ndani ya tani 60,000 kwa mwezi na ziada ya tani nyingine 20,000 ambazo pia zinauzwa katika nchi za Uganda, Kenya na Rwanda.

“Kampuni yetu imeongeza uzalishaji wa makaa ya mawe kwa zaidi ya asilimia 100 na tayari magari yatumikayo katika ubebaji na uchimbaji wa makaa ya mawe yako njiani kufika huku katika eneo la mgodi ili kuzidi kuongeza uzalishaji na hatimaye tani za uzalishaji wa madini haya zitazidi kuongezeka”, alisema Bw. Shedd.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tancoal Energy Tanzania Limited Bw. James Shedd (kushoto) akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu makaa ya mawe katika moja ya ofisi zilizopo katika mgodi wa makaa yam awe wa Liganga uliopo Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma 10 Mei, 2017.
Meneja Udhibiti Ubora wa Makaa ya Mawe wa Kampuni ya Tancoal Energy Tanzania Limited Bw. Bosco Mabena akielezea moja ya majukumu wayafanyayo katika Kitengo cha Udhibiti Ubora wa makaa ya mawe yanayochimbwa kutoka mgodi wa makaa hayo uliopo Ngaka, Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma 10 Mei, 2017.
Kijiko kikifanya kazi ya kuchimba makaa ya mawe katika mgodi wa makaa ya mawe uliopo eneo la mgodi wa Ngaka Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma 10 Mei, 2017.
Malori maalum yakibeba vifusi yakielekea kupakia vifusi vya udongo katika eneo linaloandaliwa kuanza kuchimbwa makaa ya mawe katika eneo la mgodi wa Ngaka Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma 10 Mei, 2017.
Mashine ya kusaga makaa ya mawe katika eneo la mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma ikifanya kazi ya kusaga makaa ya mawe yaliyochimbwa 10 Mei, 2017.



Mbolea za Yara zanufaisha wakulima wa Viazi, Mbeya

$
0
0
Afisa kilimo kutoka kampuni ya Yara Tanzania Ltd ambao ni wazalishaji na wasambazaji wa mbolea nchini, Maulid Mkima (kushoto) akiwa na mmoja wa wakulima wa viazi katika kijiji cha Simambwe Wilaya ya Mbeya, Furaha Ngala alipotembelea shambani kwake na kuona matokea ya zao hilo baada ya kutumia mbolea aina ya YaraMila WINNER, YaraLiva NITRABOR na YaraVita TRACEL BZ.
Afisa kilimo kutoka kampuni ya Yara Tanzania Ltd ambao ni wazalishaji na wasambazaji wa mbolea nchini, Maulid Mkima (kushoto) akitoa elimu juu ya matumizi bora ya mbolea ya YaraMila WINNER, YaraLiva NITRABOR na YaraVita TRACEL BZ kwa ajili ya zao la viazi kwa wakulima katika kijiji cha Simambwe Wilaya ya Mbeya.
Afisa kilimo kutoka kampuni ya Yara Tanzania Ltd ambao ni wazalishaji na wasambazaji wa mbolea nchini, Maulid Mkima (katikati) akiwa shambani kwa mkulima wa viazi katika kijiji cha Simambwe Wilaya ya Mbeya, Furaha Ngala (kulia) kwa ajili ya kukagua maendeleo ya zao hilo baada ya kutumia mbolea ya YaraMila WINNER, YaraLiva NITRABOR na YaraVita TRACEL BZ mpangilio wa lisha linganifu kwenye viazi. Kushoto ni bwana shamba msaidizi wa kampuni hiyo kutoka Mbeya, Medson Joseph

MTANZANIA KUTOKA NORTH CAROLINA NCHINI MAREKANI AZINDUA CHARLES NEWA GOLF ACADEMY ATOA MSAADA WA VIFAA VYA GOLF KWA WATOTO LUGALO, JIJINI DAR

$
0
0
 Kushoto ni Liban Newa mchezaji wa Golf kutoka Durham, North Carolina akikabidhi vifaa vya mchezo wa golf kwa watoto katika viwanja vya mchezo huo Lugalo jijini Dar ikiwa kama sehemu ya uzinduzi wa Charles Newa Golf Academy itakayo saidi katika muendeleza vipaji vya watoto wanaopenda mchezo huo. Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na fimbo, mipira, gloves vikiwemo vifaa vingine. Anayepokea vifaa hiyo ni Japhet Masai timu kapteni wa Lugalo golf Club na mwalimu wa watoto hao.
 Liban Newa (kulia) akikabidhi moja ya vifaa vya mchezo wa golf katika viwanja vya Lugalo jijini Dar ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Charles Newa Golf Academy. Anayepokea msaada huo ni Juma Likuli ambaye ni mwalimu msaidizi wa watoto hao.
 Watoto wapenda mchezo huo waliojitokeza kwenye makabidhiano ya vifaa vya mchezo wa golf wakiwa katika picha ya pamoja.
Watoto wakipata mapochopocho mara baada ya makabidhiano hayo.

SIKU YA WAUGUZI KITAIFA KUFANYIKA ITIGI KWA UFANISI MKUBWA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameridhishwa na maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani ambayo kitaifa yatafanyika katika Hospitali ya St. Gasper halmashauri ya Wilaya ya Itigi tarehe 12 Mei, 2017.

Dkt. Nchimbi amesema hayo mara baada ya kukagua eneo la maadhimisho hayo pamoja na kukutana katika kikao kifupi na watendaji wa chama cha wauguzi Tanzania na watendaji wa hospitali ya St Gasper ambapo maadhimiyo hayo yatafanyika.

Amesema ana imani na uhakika kwa maadhimisho hayo yatafanyika kwa ufanisi mkubwa kutokana na maandalizi mazurri yaliyofanyika huku mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye atawakilishwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Ummy Mwalimu.

Dkt. Nchimbi amewataka wauguzi kuitumia siku yao kuonyesha jinsi fani ya uuguzi ilivyokuwa ni fani ya upendo, huruma na kujitoa sadaka katika kuhudumia jamii hivyo wauguzi hao  wajitokeze kwa wingi.

Ameongeza kuwa wananchi wote wa mkoa wa Singida na wale wa halmashauri ya Itigi wajitokeze kwa wingi ili waweze kushirki maadhimisho hayo kwa kupata huduma bure na ushauri juu ya masuala ya afya zao.

Kwa upande wake Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Singida Bi Theresia Ntui amesema maadhimisho ya siku ya wauguzi yatatanguliwa na shughuli ya maonyesho ya shughuli za wauguzi.

Amesema maonyesho yatafanyika katika viwanja vya hospitali ya St. Gasper kuanzia tarehe 10 mpaka 11 Mei 2017 ambapo kutakuwa na huduma za bure kwa wananchi ambazo zitahusisha upimaji wa sukari, shinikizo la damu, Virusi vya Ukimwi na mafunzo kwa vitengo juu ya utengenezaji wa uji wa lishe kwa watoto.

Ameongeza kuwa wananchi wote hasa wazazi wote kuhudhuria mafunzo hayo ya bure ambapo wataelekezwa hatua kwa hatua namna ya utengenezaji wa uji bora wa lishe kwa kutumia vyakula asilia ambapo uji huo utawasaidia watoto pamoja na watu wazima kuwa na afya njema.

Bi Theresia Ntui amewasihi wauguzi wote Mkoani Singida na Mikoa ya jirani kuhudhuria maadhimsiho hayo ambapo wauguzi wote watarudia kiapo chao cha uuguzi pia kutakuwa na  maandamano ambapo watakuwa na fursa ya kuonyesha maoni yao.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiteta jambo na Makamu wa Rais wa chama cha Wauguzi Tanzania Ibrahim Mgoo mara baada ya kukagua maandalizi ya siku ya Wauguzi kitaifa katika Hospitali ya St. Gasper Itigi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akishauri jambo wakati wa kikao kifupi cha maadalizi ya siku ya Wauguzi kitaifa katika Hospitali ya St. Gasper Itigi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiagana na Makamu wa Rais wa chama cha Wauguzi Tanzania Ibrahim Mgoo mara baada ya kukagua maandalizi ya siku ya Wauguzi kitaifa katika Hospitali ya St. Gasper Itigi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiagana na Mjumbe wa chama cha Wauguzi Tanzania Alphonsina Kaduma mara baada ya kukagua maandalizi ya siku ya Wauguzi kitaifa katika Hospitali ya St. Gasper Itigi.

Waziri Mkuu Majaliwa kuongoza mkutano wa Tasnia ya Korosho

$
0
0


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Wadau wa Tasnia ya Korosho utakaofanyika kwa siku mbili kuanzia Jumamosi, Mei 13, 2007, mjini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho (CBT) Hassan Jarufu, amesema ya kuwa Mkutano huo Mkuu wa Wadau wa Tasnia ya Korosho utawajumuisha washiriki wapatao 600 na utafanyika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango, Dodoma.

“Kama tulivyokwishakueleza, Mkutano huu Mkuu utafunguliwa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa na watakuwapo pia Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Charles Tizeba, Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa inayolima Korosho ya Lindi, Pwani, Tanga, Mtwara na Ruvuma.

“Tumealika pia waheshimiwa Wabunge wanaotoka katika Mikoa hiyo, wakulima wa Korosho na watendaji wa Vyama vya Ushirika vya zao la Korosho. Mkutano huu utajadili kwa kina changamoto zinazoikabili Tasnia ya Korosho nchini,” alisema Jarufu.

Mkutano huu Mkuu wa Wadau wa Tasniaya Korosho unakuja katika wakati ambao Tasnia ya Korosho imepata mafanikio muhimu katika msimu uliopita ambayo ni pamoja na kuweka udhibiti uliosababisha Korosho nyingi kuuzwa kwa kutumia mfumo wa Stakabadhi Ghalani na hivyo kupunguza matumizi ya Kangomba, kipimo ambacho kwa muda mrefu kimekuwa kikimnyonya mkulima.

Udhibiti huo ulisababisha makusanyo ya Korosho kuongezeka kutoka tani 155, 244.645 msimu wa 2015/2016 hadi tani 264, 887. 527 katika msimu wa 2016/2017.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

CHAMA CHA CCM CHATOA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA MZEE PAUL SOZIGWA

RAIS WA AFRIKA KUSINI JACOB ZUMA ALIVYOSHIRIKI KATIKA DHIFA YA KITAIFA ALIYOANDALIWA JANA USIKU NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. MAGUFULI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali (hawaonekani pichani) waliohudhuria katika Dhifa ya Kitaifa aliyomwandalia Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Mama Janeth Magufuli (Mke wa Rais), Mama Sizakele Zuma wakwanza kulia (Mke wa Rais wa Afrika Kusini) wakati nyimbo ya Taifa ikipigwa katika Dhifa ya Kitaifa aliyomwandalia Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akizungumza katika Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akiwa amemshika mkono Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim wakati akizungumza jambo na Rais Msaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa mara baada ya kumalizika kwa Dhifa ya Kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati Bendi ya Kilimanjaro “Wana njenje” ilipokuwa ikitumbuiza katika Ukumbi wa Ikulu katika Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa Rais Zuma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati Bendi ya Kilimanjaro “Wana njenje” ilipokuwa ikitumbuiza katika Ukumbi wa Ikulu katika Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa Rais Zuma.
 Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Anna Mghwira mara baada ya Dhifa ya Kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam, Pembeni ni Rais Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa Rais huyo wa Afrika Kusini Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Viongozi mbalimbali wa Kisiasa na Serikali wakiwa katika Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma Ikulu jijini Dar es Salaam. 

PICHA NA IKULU

BENKI KUU YA TANZANIA YAFUTA LESENI YA MBINGA COMMUNITY BANK PLC

$
0
0
Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuifunga Mbinga Community Bank Plc, kusitisha shughuli zake zote za kibenki na kufuta leseni yake ya biashara ya kibenki kuanzia tarehe 12 Mei, 2016.


Aidha Benki Kuu ya Tanzania imeiweka Mbinga Community Bank Plc chini ya ufilisi na kuiteua Bodi ya Bima ya Amana kama mfilisi kuanzia tarehe 12 Mei, 2017, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Benki Kuu leo asubuhi imeeleza.

Uamuzi huu umechukuliwa baada ya Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa Mbinga Community Bank Plc ina upungufu mkubwa wa mtaji na ukwasi kinyume na matakwa ya Sheria ya Mabenki an Taasisi za Fedha ya wmaka 2006 na kanuni zake.

“Upungufu huu wa mtaji na ukwasi unahatarisha usalama wa sekta ya fedha, na kwamba kuendelea kwake kutoa huduma za kibenki kunahatarisha usalama wa amana za wateja,” taarifa hiyo imeeleza.

Aidha, Benki Kuu ya Tanzania imeuhakikishia umma kuwa “itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.”

Benki Kuu ya Tanzania imechukua uamuzi wa kuifunga benki hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 56(1) (g), 56(2) (a), (b) na (d), 58(2) (i), 11(3) (j), 61(1) na 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.

BALOZI MPYA WA JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN AJITAMBULISHA KWA RAIS WA ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekikti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Moussa Ahmad Farhangaliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo kujitambulisha.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekikti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mgeni wake Balozi mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Moussa Ahmad Farhang baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kujitambulisha.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekikti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Mgeni wake Balozi mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Moussa Ahmad Farhang baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kujitambulisha.Picha na Ikulu, Zanzibar.

KISHAPU YAZINDUA MASHINDANO YA UMISETA

$
0
0
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imezindua mashindano ya Michezo ya Sekondari Tanzania (UMISETA) kwa mwaka 2017 kitarafa katika viwanja vya shule ya sekondari Shinyanga.

Mashindano hayo yamehusisha mpira wa miguu, netiboli, kikapu, wavu na riadha ambapo yatashirikisha shule za tarafa mbalimbali wilayani humo ambapo washindi watashindanishwa kupata timu za wilaya.

Akizungumza na wachezaji kutoka shule za Shinyanga sekondari, Maganzo Songwa, Mwadui ufundi, Idukilo na Mwadui Lutheran kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji, Ofisa elimu sekondari, Paul Kasanda aliwataka kuwa wamoja.

Alisema pamoja na kuwa wachezaji hao wanatoka shule mbalimbali wilayani humo wanapaswa kushirikiana na kupata ushindi pindi watakapocheza na wilaya zingine kutafuta wawakilishi ngazi ya taifa.

Kasanda aliongeza kwa kusema kuwa michezo ni upendo, furaha, huleta furaha na pia huweza hata kutoa ajira kama zingine endapo wachezaji watajituma vizuri wataweza kufika mbali.

“Pamoja na kuwa ninyi ni wamoja mnatoka wilaya moja lakini tunataka mtuoneshe ufundi wenu, vipaji na ushindani ili tupate timu bora zitakazoshindana na wilaya zingine,” alisema Kasanda.

Mashindano ya UMISETA kiwilaya yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 21 ambapo kimkoa ni Mei 22 hadi Juni 5 wakati kitaifa ni Juni 6 hadi 15 mwaka huu.
Ofisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Paul Kasanda akizungumza na wachezaji wanafunzi kutoka shule mbalimbali washiriki wa mashindano ya UMISETA ngazi ya wilaya katika viwanja vya Shinyanga Sekondari.
Wachezaji wasichana wakionesha vipaji vyao katika kusakata soka (mchezo wa mpira wa miguu) kupata timu itakayowakilisha wilaya katika mashindano hayo.
Timu za netiboli kutoka shule mbalimbali zikitoana jasho kupata washindi kwa ajili ya kushindana ngazi ya mkoa.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

UZINDUZI WA LIGI YA MABENKI "BRAZUKA KIBENKI" WAFANYIKA, TIMU 16 KUSHIRIKI MWAKA HUU

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


UZINDUZI wa ligi ya mabenki umefanyika huku timu zikiongezeka na kufikia 16 kushiriki katika mchezo wa mpira wa miguu na mpira wa pete (netball) huku droo ya makundi ikifanywa.

Ligi hiyo inayotambulika kama 'Brazuka Kibenki' inatarajiwa kuanza Julai Mosi mwaka huu zikiwashirikisha timu 16 kutoka mabenki tofauti nchini huku mwaka huu kukiwa na ingizo jipya ya benki ya UBA.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ligi hiyo ya Mabenki mratibu Raymond Bunyinyiga amesema kuwa huu ni mwaka wa tatu toka waanze kuwa na ligi ya mabenki ila mwaka huu ushindani utakuwa mkubwa zaidi kwani kila timu imeonekana kujipanga kuchukua ubingwa mwaka huu.

Raymond amesema kwa mwaka huu timu zimeongezeka mpaka kufika 16 kwani mwaka jana zilikuwa timu 14 pamoja kila timu kupewa sheria 17 zinazoendesha shindano hilo ambapo ziliweza kupitishwa waandaji wa ligi hiyo kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).

"Tumeweza kufikisha timu 16 mwaka huu kukiwa na maingizo mapya ya mabenki pia kila timu inatakiwa kufuata sheria zilizowekwa ili kuepuka kuondolewa katika ligi hiyo kwa kutokufuata sheria ikiwemo ya kuwachezesha wachezaji ambao ni mamluki na iwapo utatambulika umefanya hivyo utaondolewa moja kwa moja pamoja na kulipa faini,"amesema Raymond.

Mbali na hilo pia ameishukuru Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa jitihada kubwa wanazozionesha katika kuinua michezo ikiwemo na kushirikiana na kuwapa ushauri katika kuandaa ligi hiyo ya Brazuka Kibenki.

Ligi hiyo itakayoanza Julai Mosi itafanyija katika Viwanja vya Gymkhana na inatarajiwa kuwa katika hatua ya makundi 4 kwa kila kundi kuwa na timu 4 na zitachezwa kila Jumamosi kwa kipindi cha miezi minne na zawadi ya Mshindi wa kwanza itakuwa ni kombe huku kukiwa na zawadi zingine zaidi ya mia moja kwa washiriki ambao ni mabenki pamoja na wachezaji na ada ya kuingia ni kiasi cha Shilingi milion moja na laki mbili kwa kila timu (1,200,000).

 Mratibu wa Ligi ya Mabenki Raymond Bunyinyiga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ligi hiyo inayojulikana na Brazula Kibenki inayotarajiwa kuanza Julai Mosi mwaka huu na timu 16 kutoka mabenki tofauti kushirki katika michezo ya soka na netboli.Kushoto ni Nahodha wa timu ya DTB  Iddy Yakoub.
 Mratibu wa Ligi ya Mabenki Raymond Bunyinyiga akionyesha timu shiriki zitakazoumana kwne ye ligi ya Mabenki Brazuka Kibenki Julai Mosi mwaka huu.
Wawalishi wa mabenki wakiwa wanaonyesha vikatarasi vya makundi walivyokuwa wamechagua jana katika Uzinduzi wa ligi ya Mabenki Brazuka Kibenki itakayoanza Julai Mosi mwaka huu.

Picha na Zainab Nyamka.

WADAU WA MIFUGO WAOMBA ‘SAPOTI’ YA TADB

$
0
0
Na mwandishi wetu, Arusha

Wadau wa sekta ya mifugo mkoani Arusha wameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuwasaidia katika kuendeleza sekta hiyo kwa kuwapatia mikopo na mahitaji mengine kwa ajili ya kuongeza tija katika ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa nyama na maziwa.

Akizungumza katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika Kampuni ya Nyama ya Arusha, kwa niaba ya wafugaji wa mkoa wa Arusha, Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Nyama cha Arusha, Bw. Fabian Kissiagi amesema ukosefu na ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha za mtaji kwa ajili ya maendeleo ya kilimo hasa katika sekta ya mifugo inawapa changamoto katika uendelezaji wa sekta ya mifugo nchini.

Bw. Kissiagi ameongeza ukosefu wa mikopo ya uhakika inarudisha nyuma ukuaji wa sekta ya mifugo na kurudisha nyuma juhudi za serikali katika kuendeleza sekta ya mifugo.

“Hali ya ukosefu wa mitaji ya uhakika inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa na kutusahau sisi wakulima na wafugaji, hivyo tunaiomba TADB kutusaidia kutatua changamoto hii,” alisema.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi katika  kilimo nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya TADB na Wadau wa Mifugo mkoani Arusha kuhusu fursa za mikopo ya TADB. Kikao hicho kilifanyika katika Kampuni ya Nyama ya Arusha, jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha (aliyesimama) akizungumza kuhusiana na mikopo na huduma zinazotolewa na TADB katika kikao cha pamoja kati ya TADB na Wadau wa Mifugo. Kikao hicho kilifanyika katika Kampuni ya Nyama ya Arusha, jijini Arusha.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

FILBERT BAYI AFUNGA KOZI YA MAFUNZO YA UTAWALA BORA KWA WADAU WA MPIRA WA MIGUU

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. 

KATIBU mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi amefunga kozi ya utawala bora iliyoendeshwa na mkufunzi wa FIFA Henry Tandau iliyokuw ainafanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam 

Kozi hiyo inayosimamiwa na Kamati ya Olimpiki ilianza Mei 08 na kufungwa Mei 12 huku kukiwa na washiriki 15 kutoka klabu mbali mbali za ligi kuu na taasisi za michezo. 

Akizungumza wakati wa kufunga kozi hiyo Bayi amesema kuwa hii ni kwa mara ya kwanza kwa wawakilishi kutoka klabu mbalimbali za Ligi Kuu kushiriki katika mafunzo haya ambayo ni muhimu sana kwa maendeleo ya michezo nchini. 

Amesema kuwa, ana imani kubwa sana kuwa elimu hii waliyoipata wataenda kuitumia vizuri katika kuziendesha klabu zao na kuzieletea maendeleo kwani msingi mkubwa wa maendeleo ya soka ni kuwa na utawala bora. 

"Elimu hii mliyoipata leo nina imani kubwa sana mtaitumia vizuri kwani wengi wenu mnatoka katika klabu za Simba, Yanga na Azam na maendeleo ya mpira wa miguu yanaletwa na utawala bora na wasiende kuweka vyeti ndani bali wanatakiwa kuvitumia kwa ajili ya manufaa ya vizazi vijavyo,"amesema Bayi. 

Mkufunzi wa FIFA Henry Tandau amemshukuru Bayi kwa kuweza kukubali kuwa mgeni rasmi kaika mafunzo hayo na kumuahidi kuwa elimu hii waliyoipata wanaimani kuwa washiriki wote wataenda kuelimisha na wengine na kuleta utawala bora kwenye klabu zao. 

Mafunzo hayo ya siku 5 yameratibiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini huku ikiwa ni kwa mara ya kwanza tofauti na miaka mingine kufanyika mikoani pia yameweza kuleta tija kwa washiriki kufahamu mambo mbalimbali yanayohusu michezo ikiwemo riadha. 
Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akizungumza wakati wa kufunga kozi wa mafunzo ya utawala bora iliyoendesha na Shirikisho la Mpia wa Miguu (FIFA) kupitia kamati ya Olimpiki iliyoanza Mei 08 mpaka Mei 12 Jijini Dar es salaam.
Mkufunzi wa FIFA Henry Tandau akizungumza wakati wa kufunga kozi wa mafunzo ya utawala bora iliyoendesha na Shirikisho la Mpia wa Miguu (FIFA) kupitia kamati ya Olimpiki iliyoanza Mei 08 mpaka Mei 12 Jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi.
Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akitoa cheti cha mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka Kituo cha JKM Park Kassim Liogope mafunzo yaliyomaliza leo Jijini Dar es salaam.

WADAU WAOMBWA KUICHANGIA TIMU YA KIKAPU YA VIJANA U-16 INAYOJIANDAA KUSHIRIKI MICHUANO YA 2016 ZONE 5 MOMBASA KENYA

$
0
0
 Kaimu Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) Michael Mwita akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuwaomba wadau kuichangia shilingi milioni 30 kwa timu ya Vijana U-16 wa mchezo ikiwa ni ghalama ya kwenda kushiriki mashindano ya 2016 Zone 5 Mombasa Kenya.
Kocha wa Timu ya Taifa ya Mchezo wa kikapu chini ya umri wa miaka 16, Bahati Mgunda akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akielezea programu nzima ya maandalizi ya hiyo inayojiandaa kwenda kushiriki mashindano ya 2016 Zone 5 Mombasa Kenya. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.

BALOZI DK.MAHIGA AKABIDHIWA MAGARI NA SERIKALI YA KUWAIT

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa  Balozi Dk. Augustine Mahiga amepewa msaada wa magari kutoka serikali ya Kuwait ilikuweza kusaidia katika shughuli mbalimbali za kiutendaji.

Balozi Mahiga amesema hayo wakati akipokea msaada wa magari kwa ajili ya wizara yake amesema wizara yake sio yenye tatizo ya usafiri bali ni suala wizara mbalimbali na taasisi zingine za serikali .

Amesema serikali ya Kuwait inatoa msaada katika serikali ya Tanzania zaidi ya dola za kimarekani milioni 200 kwa kila mwaka.Balozi Mahiga amesema ubalozi wa Kuwait nchini amekubali kusaidia magari kwa sekta zingeni kwa kutaka kuorodhesha mahitaji ya usafiri ili kuweza kusaidia serikali ya Tanzania Kiutendaji.
 Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukabidhiwa magari kutoka ubalozi wa Kuwait nchini leo Jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhii magari yenye thamani ya dola za Kimarekani 100,000 leo jijini Dar es Salaam.picha zote na Emmauel Massaka,Glob ya Jamii.
  Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akikabidhi funguo za Magari kwa Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiteta jambo na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem
 Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa wizara hiyo.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images