Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1682 | 1683 | (Page 1684) | 1685 | 1686 | .... | 3272 | newer

  0 0


  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Viattel Tanzania (Halotel) Do Manh Hong, kampuni amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka saba likiwemo la uhujumu uchumi.

  Mshtakiwa Do Manh Hong amefikishwa mahakamani hapo na kuunganishwa na washtakiwa wengine saba waliofikishwa mahakamani hapo mapema Mwaka huu.

  Wote kwa pamoja wanakabiliwa ma mashtaka kumi, kula njama. Kisimika mitambo ya mawasiliano bila kibali cha TCRA, kutoa nyaraka za uongo, kusababisha hasara kwa serikali ya Tanzania,  ya milioni 459, kutumia mitambo ya mawasilino ambayo haijathibitishwa na namba za simu.

  Mbali na Hong, washtakiwa wengine ni Dilshad Ahmed (36), Rohail Yaqoob(47), Khalid Mahmood (59), Ashfaq Ahmad (38), Muhamad Aneess(48), Imtiaz Ammar (33) wote raia wa Pakistan na Ramesh Kandasamy (36) raia wa Sri-Lanka.

  Kabla ya kusoma kwa mashtaka, wakili wa Serikali, Jehovanea Zacharias aliiomba mahakama kumuunganisha mshtakiwa Hong na kuwasomea washtakiwa wote makosa yao.

  Imedaiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa mshtakiwa Ahmed, Yaqoob,  Mahamood, Ahmad, Anees, Kandasamy na Qammar Novemba 2016 Dar es Salaam walikula njama ya kutumia vifaa vya mtandao.

  Imedaiwa kuwa, watuhumiwa walitengeneza mfumo wa kutumia huduma za mtandao kwa lengo la kukwepa kodi ya  kupokea na kusambaza simu za kimataifa bila kibali cha TCRA.

  Aidha imedaiwa kuwa Novemba 20, 2016 waliingiza vifaa vya kielektroniki  bila ya kuwa na leseni na kuvisimika  bila ya kuwa na kibali cha  TCRA.

  Imedaiwa, washtakiwa waliunganisha  vifaa hivyo na huduma za mitandao kwa lengo la kupokea na kusambaza mawasiliano bila ya kuthibitishwa na TCRA.

  Kwa upande wa Kampuni ya Viettel Tanzania Limited na Do Hong wanadaiwa kati ya Novemba 2016 na Februari 2017 maeneo ya ofisi za Halotel Victoria Kinondoni walishindwa kuthibitisha taarifa iliyotolewa na Unex Company Ltd kwa lengo la kusajili lakini za simu 1000.

  Kwa upande wa washtakiwa Ahmed na wenzake sita wanadaiwa kuwa Januari 5 ,2016 walitoa Cheti chakughushi cha usajili wa kodi chenye namba 100-864-210 kuonyesha imetolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania wakati si kweli.

  Mbali na mashtala hayo, watuhumiw wote kwa pamoja wanadaiwa kuisababisha hasara TCRA na serikali ya Tanzania kiasi cha milioni 459.

  Hata hivyo, washtakiwa wote hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mshtaka yanayowakabili yako nchini ya sheria ya uhujumu uchumi.

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 29,2017.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Viattel Tanzania (Halotel) Do Manh Hong, akipandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mapema leo jijini dar,kujibu mashtaka saba likiwemo la uhujumu uchumi. 

  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Chalinze

  TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services, jana iliikomboa Halmashauri mpya ya wilaya Chalinze kwa kuipatia kompyuta mbili kwa ajili ya kupunguza changamoto za upungufu wa vifaa vya kiutendaji, ikiwa ni miezi michache tangu kuanzishwa kwa Halmashauri hiyo mpya.

  Kompyuta hizo zilipokewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Edes Lukoa katika ofisi yake, ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa Halmashauri hiyo inatimiza wajibu wake wa kuwatumikia wana Chalinze na Watanzania kwa ujumla kwa kutumia kompyuta hizo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Edes Lukoa akipokea kompyuta mbili kutoka kwa Taasisi ya Bayport Financial Services ikiwakilishwa na Mratibu wa Masoko Mercy Mgongolwa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri mpya ya Chalinze mkoani Pwani, Edes Lukoa mwenye koti jeusi, akipokea msaada wa kompyuta mbili kutoka kwa Mratibu wa Masoko wa Bayport Fiancial Services, Mercy Mgongolwa. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Kanda ya Kati Christopher Kihwele kushoto kwa Mercy na Meneja wa wa Bayport Bagamoyo Francis Sumila na Katibu wa Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete Idd Swala kulia kwa Mkurugenzi wa Chalinze.

  Akizungumza jana katika makabidhiano hayo wilayani Chalinze, Mratibu wa Masoko wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, alisema kwamba lengo la kuipatia kompyuta hizo linatokana na dhamira ya kuona wilaya hiyo inasonga mbele kimaendeleo.

  Alisema kugawa kompyuta hizo ni mwendelezo wa nia yao baada ya kuzindua ugawaji wa kompyuta hizo 205 zilizoanza kusambazwa katika ofisi mbalimbali za serikali baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki.


  0 0

  Uwanja wa Namfua uliopo manispaa ya Singida ambao ukarabati wake umefikia hatua ya kuridhisha umeanza kutoa matumaini kwa wananchi wa Singida ambao wamekuwa wakifuatilia kwa karibu ukarabati wake.

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwa pamoja na Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa Singida wamefanya ziara ya kushtukiza kujionea hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa uwanja huo ambao utatumika kama uwanja wa nyumbani wa timu ya Mpira wa Miguu iliyobeba jina la mkoa ‘Singida United’.

  Dkt. Nchimbi amesema anaridhishwa na kasi ya utengenezaji wa uwanja wa Namfua unaomilikiwa cha chama cha Mapinduzi Mkoa wa Singida huku akiupongeza uongozi wa CCM mkoa wa hatua ilipofikia uwanja huo kwakukwa ni tegemeo la fursa nyingi hasa za wajasiriamali wadogo.

  “Chama cha Mapinduzi kimetengeneza fursa na ajira nyingi kwa wajasirimali mkoani Singida kwa kuukarabati Uwanja huu ili uweze kutumika na timu ya Singida United ambayo inatupa heshima kubwa wana Singida”, ameongeza Dkt. Nchimbi.

  Ameongeza kuwa wananchi wa Singida wana hamu kubwa ya kuziona timu kubwa zinazocheza ligi kuu Tanzania bara zikicheza katika uwanja wa Namfua na hivyo kuitumia fursa hiyo kufanya biashara mbalimbali.

  Aidha Dkt. Nchimbi amesema kuwa uwanja huo utakuwa ni chanzo cha mapato kwa mmiliki wa uwanja huo ambaye ni CCM Mkoa wa Singida, huku timu zitakazocheza, TFF na Manispaa ya Singida watapata mgao wao kulingana na taratibu zilizopo.

  Kwa upande wao vijana waliokuwa wakishuhudia ukarabati wa uwanja huo wamesema wamejiandaa kuuza bidhaa kama jezi na vipeperushi vya timu kubwa huku wakisema watatoa kipaumbele katika kuuza na kuvaa jezi za timu yao ya Singida United.

  Wameongeza kuwa uwanja huo ni faraja kwa kila mjasirimali mkoani Singida wakitoa mfano kwa wamiliki wa hoteli, nyumba za kulala wageni, wauzaji wa vinywaji na bidhaa ambazo zinapatikana mkoani Singida kwa ubora mkubwa ambazo ni asali, mafuta ya alizeti, kuku wa kienyeji, vitunguu bora na Viazi vitamu watapata wateja wa kutosha.  
   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akikagua ujenzi wa uwanja wa Namfua uliopo Manispaa ya Singida, kulia kwake ni Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa Singida.
   Uwanja wa Namfua uliopo Manispaa ya Singida ukiendelea kukarabatiwa.
    Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akikagua ujenzi wa uwanja wa Namfua uliopo Manispaa ya Singida, kulia kwake ni Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa Singida.
  Uwanja wa Namfua uliopo Manispaa ya Singida ukiendelea kukarabatiwa.

  0 0


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii


  Kamati ya Miss Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Grace Product na Gift Jewelers wamekabidhi gari kwa Mrembo wa Shindano hilo Diana Edward Lukumai  ambaye alishinda taji la Miss Tanzania 2016/2017.


  Akizungumza wakati wa kukabidhiwa zawadi hiyo Miss Diana amesema kuwa  anaishukuru sana kamati hiyo kwa kumsaidia kupata zawadi hiyo ambayo ameisubiri kwa hamu na kwa muda mrefu .


  “Wasichana wanatakiwa kuwa wavumilivu na kujiandaa kisaikolojia kwani kushinda taji la urembo la Miss Tanzania sio kitu kidogo, watu wengi watakufuatilia, hivyo lazima ujitambue kuwa ukiwa Miss Tanzania ni mtu ambaye anatakiwa kuwa msiri,  hivyo wasichana wajiandae sana kisaikolojia katika hili.” Amesema Miss Diana.


  Amesema kuwa gari hiyo itaweza kumsaidia katika matumizi yake binafsi hasa katika kipindi hiki ambacho anaendelea na kampeni yake ya Dondosha wembe ambayo ina lengo la kumkomboa  mtoto wa kike juu ya mila potofu za kuozeshwa mapema na ukeketaji.


  Kwa upande wake mkuu wa itifaki wa kamati ya Miss Tanzania, Albart Makoye amesema mara baada ya kukabidhi kwa zawadi hiyo kunafungua pazia la shindano jipya la mwaka 2017/2018 .


  Amesema kuwa warembo wanatakiwa kujiweka sawa hili waweze kunyakuwa taji hilo ambalo mashindano yake yataanza kuanzia ngazi ya votongoji mpaka taifa.
   Ofisa wa Basata akikabidhi funguo kwa Miss Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai  kama ishara ya kumkabidhi mrembo  huyo gari yake aina ya Suzuki Swift pembeni yake Mkurugenzi wa Grace Products Ltd Elizabeth Kilili.
   Miss Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai akiingia ndani ya gari yake mara baada ya kukabidhiwa
   Miss Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai akifurahi mara baada ya kuingia ndani ya gari yake
   Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania , Arbart Makoye akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi gari
   Mkurugenzi wa Grace Products Ltd Elizabeth Kilili na Mumewe  wakikabidhi kadi ya gari kwa Miss Tanzania 2016/217 Diana Lukumai
   Mkurugenzi wa Grace Products Ltd Elizabeth Kilili. akizungumza na Miss Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai katika duka la ke lililopo City Mall jijini Dar es Salaam.

  0 0


  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said.

  SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limewaomba wateja wake na wananchi kwa ujumla kutoa taarifa mapema mara inapotokea hitilafu ya umeme iliyosababishwa na mvua au sababu nyingine.
  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2017, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (pichani juu), alisema, sambamba na hilo pia wananchi wasifanye shughuli au kukaa chini ya miundombinu ya umeme.
  “Lakini tunawaomba wananchi watoe taarifa haraka maeneo yenye mafuriko au mkusasnyiko wa maji mengi ili wataalamu wetu waweze kuchukua hatua za haraka.” Alisema.
  Dkt. Mwinuka pia alisema endapo kuna nyaya, nguzo au kifaa chochote cha umeme kimepata hitilafu na kinahatarisha maisha ni vema uangalizi au alama ikawekwa ili kuwapa hadhari wapiti njia na watoto wasikaribie eneo hilo wakati mafundi wa TANESCO wakichukua hatua za marekebisho.
  Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA), katika taarifa yake iliyotoa Mei 9, 2017 imeonya kuwa maeneo ya Pwani ya Kaskazini ikiwemo visiwa vya Unguja na Pemba, yatakabiliwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24 kuanzia Mei 10 hadi 12, 2017. 

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (katikati), akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Me11, 2017. Dkt. Mwinuka ametoa hadhari kwa wananchi kutogusan miundombinu ya Tanesco hususan nyaya zilizoanguka, au kufanya shughuli yoyote karibu na miundombinu yab umeme katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendela kunyesha nchini. Kulia ni Mhandisi Simon Kihiyo, na kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji.
   Mhandisi Simon Kihiyo, akitoa ufafanuzi wa kitaalamu kuhusu hatua za kuchukua pindi hitilafu ya umeme inapotokea
   Dkt. Mwinuka akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Wito umetolewa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuchangamkia fursa za uwekezaji katika serkta ya kilimo na mifugo kwa kuwapatia mikopo wakulima wanaojishughulisha katika sekta hizo.

  Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega wakati akizungumza na ugeni kutoka TADB walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha.

  Bw. Kwitega amesema kuwa mkoa wa Arusha una fursa nyingi za uwekezaji hasa katika maeneo ya kilimo na ufugaji.

  Akizungumza wakati wa mazungumzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga alisema uanzishwaji wa TADB unatokana na Serikali kutambua umuhimu wa uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya Kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo.

  Bw. Assenga mkoa wa Arusha utaingizwa rasmi katika mpango wa biashara wa Benki na ametoa wito kwa wakulima na wafugaji wa mkoa wa Arusha kuchangamkia fursa zinazotolewa na TADB.
  Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (kushoto) akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kulia) wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha.
  Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (katikati) akizungumza na ugeni kutoka TADB wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha. Ugeni uliongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe, bungeni mjini Dodoma Mei 11, 2017    
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi,  Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama bungeni mjini Dodoma Mei 11, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Rombo Roman Joseph Selasini, kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 11, 2017, katikati ni Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Francis Mbatia, (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wafanyabiashara mbalimbali wa nchini pamoja na Afrika ya Kusini wakati aliposhiriki pamoja na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma katika Jukwaa hilo  la Wafanyabiashara  jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akisoma hotuba yake katika Jukwaa hilo la Wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika Kusini lililofanyika jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kutoka kwenye Jukwaa hilo la Wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika Kusini lililofanyika jijini Dar es Salaam.
   Sehemu ya Wafanyabiashara mbalimbali wa Tanzania na Afrika Kusini waliohudhuria katika Jukwaa hilo la Wafanyabiashara jijini Dar es Salaam.

  PICHA NA IKULU


  0 0


  0 0


  Na Mathias Canal, Iringa 

  Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela amefungua warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028.

  Alisema kuwa ili kukuza na kuendeleza sekta ya kilimo nchini wataalamu wote nchini wanapaswa kubadilishana ujuzi na kushauriana namna ya kuwa na kilimo chenya tija kuliko kuficha ujuzi walionao kwa muktadha wa maeneo husika pekee waliyopo hivyo ni vyema kutumia ujuzi wao kwa makubaliano na maelekezano kwani jambo hilo litachochea zaidi ukuzaji wa sekta ya kilimo nchini Tanzania.

  Dc Kasesela ameyasema hayo wakati Akizungumza kwenye ufunguzi wa warsha hiyo inayofanyika katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa, warsha inayowahusisha Makatibu Tawala wasaidizi upande wa uchumi kutoka mkoa wa Iringa na Pwani na Maafisa kilimo wa mikoa, Meya wa Manispaa/Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa halmashauri za Manispaa/wilaya, Wachumi wa Manispaa/Wilaya na Maafisa Kilimo wa Manispaa/Wilaya kutoka Katika Halmashauri za Manispaa na Wilaya kutoka Mkoa wa Pwani na Dar es salaam.

  Dc Kasesela ameeleza kuwa Programu hii ya ASDP 2 imeandaliwa baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya ASDP 1 iliyotekelezwa kuanzia mwaka 2006/2007 hadi 2013/201 huku akiwapongeza waandaaji wa warsha hiyo ambao ni OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kutaraji kutekelezwa na wadau mbalimbali kama vile Wizara za sekta ya kilimo, Wahisani, Sekta binafsi, Taasisi zisizo za kiserikali, Wakulima Wafugaji, na Wavuvi.
  Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela akizungumza wakati wa kufungua warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
  Meya wa Manispaa ya kinondoni Mheshimiwa Benjamini Sitta ambaye pia ni mwenyekiti wa warsha akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa


  0 0

   Aliyekuwa  kuwa Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Steven  Wassira  akiwa katika jengo la Mahakama ya Rufaa jijiji Dares Salaam akizungumza jambo na baadhi ya mawakili kabla ya kusikiliza kwa Rufaa ya kesi yake dhidi ya Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya.  Katika kesi hiyo jopo la majaji watatu  wa Mahakama ya Rufaa limepanga kuendelea na kesi hiyo Jumatatu ijayo ya Aprili 15, mwaka huu. Uamuzi huo umetolewa  leo  Aprili 11, mwaka huu katika Mahakama hiyo  baada ya  Pande zote mbili  kutoa maelezo  ya sababu za rufaa.
  Wakili wa Mbunge  wa Jimbo la Bunda Mjini, Tundu Lissu  akizungumza  jambo na mara baada kikao kilichokuwa kinasikiliza ombi la rufaa lilifunguliwa na  wapigakura wanne wa Jimbo la Bunda, kupinga  hukumu ya  Mahakama Kuu Kanda ya  Mwanza, kuhusu ushindi wa mbunge wa jimbo hilo, Ester Bulaya.

  Wakili  Constantine  Mutalemwa  akifafanua  jambo kwa baadhi  ya waandishi  wa habari  mara baada kikao kilichokuwa kinasikiliza ombi la rufaa lilifunguliwa na  wapigakura wanne wa Jimbo la Bunda, kupinga  hukumu ya  Mahakama Kuu Kanda ya  Mwanza, kuhusu ushindi wa mbunge wa jimbo hilo, Ester Bulaya.(PICHA NA MAGRETH  KINABO)

  0 0


  Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Mussa A. Zungu akifafanua jambo wakati wa semina ya pamoja iliyoandaliwa na Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya dhidi ya Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge, ikilenga kubadilishana uzoefu wa kiutendaji wa kazi, katika kikao kilichofanyika leo katika Hoteli ya Dodoma Mjini.
  Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mary Nagu akizungumza jambo katika semina ya pamoja iliyoandaliwa na Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya dhidi ya Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge, ikilenga kubadilishana uzoefu wa kiutendaji wa kazi, katika kikao kilichofanyika leo katika Hoteli ya Dodoma Mjini.
  Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Naghenjwa Kaboyoka akizungumza jambo wakati wa semina ya pamoja iliyoandaliwa na Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya dhidi ya Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge, ikilenga kubadilishana uzoefu wa kiutendaji wa kazi, katika kikao kilichofanyika leo katika Hoteli ya Dodoma Mjini.
  Mjumbe wa Wabunge Vijana wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Abdallah Ulega akifafanua jambo wakati wa semina ya pamoja iliyoandaliwa na Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya dhidi ya Wabunge Vijana wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kikao kilichofanyika leo katika Hoteli ya Dodoma Mjini.
  Mwenyekiti wa Wabunge Vijana wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Upendo peneza akizungumza wakati wa semina ya pamoja iliyoandaliwa na Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya dhidi ya Wabunge Vijana wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, katika kikao kilichofanyika leo katika Hoteli ya Dodoma Mjini.
  Mwenyekiti Mwenza, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni akiongoza semina ya pamoja ya iliyoandaliwa na Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya dhidi ya Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati ya Kudumu za Bunge, katika kikao kilichofanyika leo katika Hoteli ya Dodoma Mjini.

  (PICHA NA OFISI YA BUNGE)


  0 0

  TANZANIA needs to end open defecation and have all people using improved toilets, to reflect the status of a middle-income country. 

  The Minister for Health, Community Development, Gender, Elderly and Children, Honorable Ummy Mwalimu (MP) and stakeholders conveyed this in Dodoma during a Call to Action event. The minister called for the national sanitation campaign, “To carry out a much bigger campaign far beyond the dimensions of the Mtu ni Afya.”

  The National Sanitation Campaign launched in 2012 is ramping up its efforts to accelerate household sanitation improvements. The use of poor quality toilets and the practice of open defecation is a leading cause of illness and death from cholera, diarrheal diseases, and costs the country 1% of its GDP each year. Poor sanitation is also a major contributor to stunted growth of about 2.7 million children in Tanzania. Children who are more likely than their peers to struggle in school and earn less as adults.

  The campaign is setting out new activities ranging from promoting improved toilets, hand washing with soap, water treatment at point of use, sanitation in schools and health care facilities to the provision of adequate toilets on highways and bus stops.

  “I would request each one of you to join the government efforts of ensuring access to improved sanitation and hygiene,” said the Minister,to the assembled government staff, development partners, the private sector and public.
  Minister for Health, Community Development, Gender, Elderly and Children, Honorable Ummy Mwalimu (MP) speaks during the launches of sanitation campaign in Dodoma.  MORE NEWZ CLICK HERE


  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Kutokana na mvua zinazoendelea katika maeneo tofauti barabara mbili zimekata mawasiliano na kufanya baadhi huduma za kijamii kushindwa kufanyika.

  Barabara zilizokata mawasiliano ni barabara ya Chamanzi kwenda Kibamba pamoja na barabara ya barabara ya Mkuranga kwenda Hoyoyo.

  Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Dodoma, Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa hali ya barabara katika jimbo lake ziko katika hali mbaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

  Amesema kuwa ameomba barabara ya Kimazichana kwenda Kibamba kuingizwa katika barabara za Tanroads ili ziweze kuangaliwa kutokana umuhimu wake katika uchumi wa nchi.

  Diwani wa Kata ya Tengerea , Shaban Manda amesema kuwa barabara ya Mkuranga kwenda Hoyoyo makaravati yaliyowekwa hayawezi kuhimili mvua ikiwa kubwa.

  Amesema wakandarasi wanatakiwa kushirikisha wananchi katika uwekaji wa madaraja na makaravati kutokana na wao ndio wanajua sehemu zenye matatizo.Manda amesema kuwa wakati mwingine sehemu zinazowekwa makaravati hayana umuhimu ndio maana mvua zikinyesha nayo yanakwenda na maji .

  Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimazichana , Omary Ndeu amesema hali mbaya kwa wananchi wa Mbezi na Kibamba hawawezi kufika kimazichana ambapo huduma za kijamii na biashara ndio zinafanyika.
  Wananchi wakishuka katika daladala inayofanya safari zake Kibamba , Kimazichana na Dar es Salaam kwa ajili ya kuvuka kutokana na barabara hiyo kukatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
  Vijana wakitengeneza barabara ya dharula kwa ajili ya kupitisha magari na kupata kipato kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
  Barabara ya Mkuranga kwenda Hoyoyo ikiwa imekatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
  Diwani wa Kata ya Tengerea, Shaban Manda akizungumza na Michuzi Blog juu ya barabara hiyo kukatika na kukatika kwa mawasiliano.

  0 0


  Na Ramadhani Ali-Maelezo

  Taasisi zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) na ukimwi Zanzibar zimetakiwa kuelekeza nguvu katika makundi maalum ambayo maambukizi bado ni makubwa.

  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo alitoa ushauri hao alipokuwa akifungua mkutano wa siku moja wa wadau wa mapambano ya ukimwi uliotayarishwa na Taasisi ya kuimarisha huduma za afya Tanzania (THPS) na kuzindua mpango mkakati wa miaka mitano wa taasisi hiyo katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni.

  Alisema wakati Zanzibar inajivunia kuwa na asilimia chini ya moja ya maambukizi ya VVU, katika makundi maalumu maamukizi yapo kwa asilimia 10 hadi 19 ambapo ni hatari.

  Aliyataja makundi hayo kuwa ni vijana wanaojidunga sindano za madawa ya kulevya, wanawake wanaofanya biashara ya ngono na wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao.
  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akifungua mkutano wa wadau wa mapambano ya ukimwi Zanzibar katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni.
  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizindua Mpango Mkakati wa miaka mitano wa THPS katika mkutano wa wadau wa mapambano ya ukimwi uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni, anaeshirikiana nae katika uzinduzi huo ni Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Redempta Mbatia.
  Mkurugenzi Mtendaji wa THPS Dkt. Redempta Mbatia akizungumza na wadau wa mapambano ya ukimwi Zanzibar katika mkutano wa siku moja uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni.
  Muhudumu Mkuu wa huduma za mama na mtoto na huduma za upimaji vvu kwa jamii kutoka Hospitali ya Mwembeladu Mwanakhamis Alawi Nguzo akipokea zawadi maalum kutoka Waziri wa afya Mh. Thabit Kombo baada ya kuwa kituo bora katika mapambano ya ukimwi kipindi cha miezi mitatu Octoba – Disemba.  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani maarufu kama Prof Maji Marefu akitoa msaada wa kuwaokoa wananchi wa Jimbo lake kwenye mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mengi ya Mji wa Korogwe na maeneo mengine mengi ya nchi. 
  Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani akijadiliana jambo na baadhi ya wananchi wake.  0 0   Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akipunga mkono wakati akiwasili Ikulu akiwa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kabla ya kuanza kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akisoma hotuba yake wakati akizungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akipiga ngoma wakati alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akizungumza jambo na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji LG Electronics Afrika Logistics, Janghoon Chung akingumza na waandishi habari juu ya ubora wa viyoyozi vya LG iliyofanyika leo  katika Hoteli ya Hyatt Legency jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Masoko Afrika Mashariki LG Electronics , Moses Marji  akizungumza wakati wa  uzinduzi wa bidhaa mpya kutoka LG 
  Meneja wa bidhaa za LG Afrika Mhandisi , Singh Chana  akizungumza juu ya umuhimu wa bidhaa za LG katika uhifadhi wa Mazingira .
   Mkurugenzi Mtendaji LG Electronics Afrika Logistics, Janghoon Chung Akimkabidhi zawadi ya Televisheni mmoja wa washindi wa bahati nasibu  iliyochezeshwa katika semina ya uzinduzi wa bidhaa mpya za Lg Tanzania , Ramachandran  Veeraman. Habari kamili BOFYA HAPA

  0 0


older | 1 | .... | 1682 | 1683 | (Page 1684) | 1685 | 1686 | .... | 3272 | newer