Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1684 | 1685 | (Page 1686) | 1687 | 1688 | .... | 3284 | newer

  0 0


  0 0


  Na Nuru Juma & Husna Saidi-Maelezo.  Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) linajiandaa kushiriki mashindano ya kanda ya Zone 5 Kimataifa kwa watoto chini ya umri wa miaka 16 yatakayofanyika mjini Mombasa nchini Kenya kuanzia tarehe 1-6 Juni mwaka huu.  Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es salaam leo, Kaimu Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Michael Mwita alisema mashindano hayo yatatumika kupata timu  itakayowakilisha kanda ya Zone 5 na baadaye kuwakilisha  bara la Afrika katika mashindano ya Dunia ya mchezo huo.  Alifafanua kuwa zimeundwa timu kutoka Mikoa mbali mbali ambapo mazoezi rasmi ya mchujo wa wachezaji kupata timu itakayowakilisha Taifa yataanza tarehe 20 mwezi  huu katika viwanja vya JMK sports Complex jijini Dar es Salaam.  “Tumeshathibitisha ushiriki wa timu yetu na vijana wameshaanza mazoezi tangu mwezi Januari na tumeandaa bajeti ya mil.30 ili kuweza kufanikisha mashindano hayo ambayo kwa Tanzania ni mara ya kwanza kushiriki”, alieleza Mwita.  Aliongeza kuwa mshindi atakaepatikana kwa kanda ya Zone 5 atakutana na washindi wengine wa kanda sita kwa upande wa bara la Afrika na kisha kupata timu itakayowakilisha bara la Afrika na kukutana na bara la Amerika, bara  la Ulaya na bara la Amerika ya Kusini ili kumpata mshindi wa Dunia.  Kwa upande wake kocha wa timu hiyo, Bahati Mgunda alisema ameamua kuteua makocha wasaidizi katika Mikoa mbali mbali ili mchezo huo wa kikapu uweze kuenea nchi nzima.  Mgunda alisema wanahitaji kuwalea watoto wa jinsia zote wenye umri kuanzia miaka 11 hadi 14  watakaopenda kujiunga na mchezo huo wa mpira wa kikapu na baadaye kuwaunganisha katika timu kubwa na kuweza kushiriki mashindano ya Kitaifa.
  Katika kanda ya Zone 5 nchi zitakazoshiriki mashindano hayo ni Tanzania, Kenya, Sudan, Sudani Kusini, Uganda, Burundi, Rwanda, Misri na Somalia. 


   Kaimu Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) Michael Mwita akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuwaomba wadau kuichangia shilingi milioni 30 kwa timu ya Vijana U-16 wa mchezo ikiwa ni ghalama ya kwenda kushiriki mashindano ya 2016 Zone 5 Mombasa Kenya.

  Kocha wa Timu ya Taifa ya Mchezo wa kikapu chini ya umri wa miaka 16, Bahati Mgunda akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akielezea programu nzima ya maandalizi ya hiyo inayojiandaa kwenda kushiriki mashindano ya 2016 Zone 5 Mombasa Kenya. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni , George Manyama amesema kuwa manispaa imejipanga katika katika kutoa elimu bora kwa wanafunzi.

  Manyama ameyasema hayo katika kilele cha wiki ya elimu kwa Manispaa ya Kinondoni iliyofanyika leo katika shule ya Sekondari ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam amesema watakuwa bega kwa bega na shule zilizo katika manispaa hiyo katika kutoa elimu bora kwa wanafunzi.

  Amesema kuwa katika awamu wa tano wamejipanga katika kutatua changamoto ambazo zinakabili manispaa hiyo ikiwa ni vyumba vya madarasa baada kwa kuisha kwa changamoto ya madawati.

  Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana kwa kupata ufaulu wa juu katika shule ya Msingi Mikocheni Islamic , Taus Amiri amesema kuwa alijituma na kuweza kupata ufaulu huo.

  Taus amesema kuwa wanafunzi wenzake wajitume waweze kuwa na ufaulu utaofanya wawe na malengo ya kuendelea kufanya vizuri,Mwalimu Mkuu Msaidizi Mikocheni Islamic, Maulid Omari amesema kuwa shule yao ilikuwa ya pili katika manispaa ya kinondoni kwa kubebwa na Taus kwa kupata alama kubwa katika masomo yote .

  Mama wa Taus , Hiba Msasi amesema mwanae amekuwa na bidii katika masomo ndio maana ilimuwezesha kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni , George Manyama akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha maadhimisho ya elimu yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana kwa kupata ufaulu wa juu katika shule ya Msingi Mikocheni Islamic , Taus Amiri akizungumza na waandishi habari juu ya ufaulu wake katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, George Manyama akitembelea maonesho ya shule katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya elimu .
  Wanafunzi wakifanya maonesho ya kilele cha wiki ya elimu leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Andrew Chenge akiongoza kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.
  Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi akijibu hoja Mbalimbali za Wabunge katika kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angelina Kairuki akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.


  0 0

  Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

  Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji imesema kuwa Serikali ya India imeahidi kutoa dola milioni 500 kwa ajili utekelezaji wa miradi ya maji katika miji 16 ya Tanzania Bara na Zanzibar katika awamu ya tatu katika mwaka wa fedha 2017/18.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Eng.Isack Kamwelwe akijibu Swali la Mbunge wa Tumbatu Mhe.Juma Othman Hija leo Bungeni Mjini Dodoma.

  “Katika bajeti ya mwaka 2016/17 Wizara yangu ilitoa taarifa ya mchango mkubwa inaoupata kutoka Serikali ya India ili kuboresha huduma ya Maji nchini kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali hiyoa”,Aliongeza Mhe.Kamwelwe.

  Aidha katika awamu ya tatu hatua inayoendelea kwa sasa ni kufanya manunuzi ya Mhandisi Mshauri atayefanya mapitio ya usanifu wa miradi na uandaaji wa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya ujenzi ambapo kazi ya ujenzi zinatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2017/18.

  Amesema kuwa katika awamu ya kwanza Serikali ilipata dola za kimarekani Milioni 178.125 ambapo kazi zilizotekelezwa katika awamu hiyo ni upanuzi wa mradi mkubwa wa Ruvu Juu,Ujenzi wa bomba kuu kutoka Mlandizi hadi Kimara,Pia Ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji katika Jiji la Dar es Salaam pamoja na ujenzi wa mradi Chalinze.

  Katika awamu ya Pili Serikali ya India itatoa dola milioni 268.35 kwa ajili ya mradi mkubwa wa kutoa maji katika mradi wa KASHWASA kutoka kijiji cha Solwa kwenda katika miji ya Tabora,Igunga,Nzega,Tinde na Uyui pamoja na Vijiji 89 vinavyopitiwa na bomba kuu umbali wa kilomita 12 kila upande uku wakandarasi wa kutekeleza mradi huo wamepatikana na wapo katika hatua za utekelezaji.

  0 0

  Katika kukuongezea burudani wewe msikilizaji wa 93.7fm Dar es salaam, Pwani na 91.3fm Mwanza, kituo cha E- fm redio kinakuletea kipindi kipya cha The chart show kitakacho husisha ngoma kali zinazoshikilia chart na stori kemkem za wanamuziki kutoka ndani na nje ya nchi kiitwacho KARATA 15 kaa tayari kukutana na watangazaji wako Jabir Salehe“KUVICHAKA- Bonge Tozz” na Allen Mushi “BIG ALLEN” kila Jumamosi kuanzia tarehe 13/05/2017, saa 6:00 – 8:00 Mchana.

  “E-FM NI KWIKWI”


  0 0


  0 0

  Wauguzi wilayani Kishapu wamepongezwa kwa kazi nzuri na kutakiwa kuendelea kuipenda kazi yao kuchapa kazi katika mazingira yoyote waliopo kwani wao ni chachu ya afya katika jamii.

  Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Talaba wakati kwenye kilele cha Siku ya Wauguzi Duniani iliyofanyika katika viwanja vya Hospitali ya Wilaya ya DK. Jakaya Kikwete. 

  Talaba ambaye aliwaongoza wauguzi hao na watumishi wa halmashauri kutoa misaada na kufariji wagonjwa hospitalini hapo aliwapongeza kwa huduma nzuri kwa wagonjwa.  Alisema kuwa bila ya wauguzi afya haijakamilika na kuwa uuguzi ni zaidi ya wito na ni huduma inayohitaji upendo na huruma kwa wale unaowahudumia.  “Kama huna upendo na ukarimu basi wewe siyo muuguzi na ukionesha ukarimu na upendo ndiyo mwanzo wa kupona kwa mgonjwa ukifika tu pale mgonjwa anapona hata kabla hujampa dawa,” alisisitiza.Aidha, aliwataka wauguzi waendelee kuwa na ushirikiano baina yao huku akiwapongeza kwa mafanikio katika sekta ya afya pamoja na kuwa wana changamoto ya mazingira ya kazi.
   Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akiwa amembeba mtoto aliyezaliwa katika Hopsitali ya Wilaya (Dk. Jakaya Kikwete) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani kiwilaya.
   Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Talaba akimpa msaada mmoja wa mama anayeuguza mtoto katika hopsitali ya wilaya.
   Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akizungumza na wauguzi (hawapo pichani) katika sikukuu ya Wauguzi Duniani viwanja vya hospitali ya wilaya.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Na Lorietha Laurence  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe  ameupongeza uongozi wa Klabu ya michezo ya Afrika Lyon kwa kutumia  mchezo wa mpira wa miguu kuelimisha jamii kupambana na ujangili wa tembo.  Waziri Mwakyembe ametoa pongezi hizo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na uongozi wa klabu hiyo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO.  Katika kikao hicho uongozi wa timu hiyo ulimueleza Waziri kuwa timu yao imeamua kushiriki vita dhidi ya vitendo vya mauaji ya tembo kwa kuandika ujumbe maalum katika jezi za timu hiyo kuelimisha jamii dhidi ya vitendo hivyo.    “ni jambo zuri kuhakikisha jamii inapata burudani ya mpira wakati huo huo inaelimika kupitia ujumbe unatolewa na wachezaji katika jezi zao”Dkt Mwakyembe alisema.  Kwa hivyo, aliushukuru uongozi wa timu hiyo kwa juhudi zao hizo na kukieleza kitendo hicho kuwa ni “cha mfano na kujivunia”.

  Aliongeza kuwa Serikali inajivunia na kuthamini mchango wa wananchi wazalendo wanaojitolea kujenga taifa na kulinda rasilimali zake kama timu ilivyofanya timu hiyo.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akipokea jezi kwa niaba ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya afrika Lyon Bw.Rajuu Kagenzi (kushoto) mara baada ya kikao na uongozi huo leo Jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akionyeshwa michora ya ramani za viwanja vya michezo vinavyotarajiwa kujengwa kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya afrika Lyon Bw.Rajuu Kagenzi (kushoto) leo Jijini dar es Salaam.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa timu ya Taifa Stars itafanya vizuri katika mashindano mbalimbali itakayoyakabili  hapo baadae,kutokana na wadau wanavyojitokeza kuiunga mkono.

  Mwakyembe ameyasema hayo wakati kishuhudia utiaji saini mkataba kati kampuni ya ya Bia ya Serengeti (SBL) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) wenye thamani ya sh.bilioni 2.1,utakaodumu kwa miaka mitatu na  kuifanya SBL kuwa mdhamini mkuu wa timu ya Taifa Stars.

  “Kwa niaba ya serikali,tunaishukuru sana kampuni ya SBL kwa kurejea tna kuwa mdhamini mkuu wa Taifa Stars,lakini pia tunatoa wito kwa kampuni zingine na watu binafsi wenye mapenzi na michezo kujitokeza na kutoa michango ya hali na mali ili kuendeleza sekta hiyo hapa nchini”,aliesema Waziri Mwakyembe.

  Nae Mkurugenzi Mtendaji wa SBL ,Helene Weesie amesema kuwa SBL imekuwa mdhamini kwa kipindi cha pili baada ya kampuni hiyo kufanya udhamini wa timu ya taifa stars mwaka 2007 hadi 2011.

  Amesema timu ya Taifa Stars itakuwa inapokea sh.milioni 700 kila mwaka ambapo itakuwa ni pamoja na kutangaza chapa ya SBL wakati wa mechi za ndani na ugenini zitakazochezwa na timu hiyo.

  Kwa upande wa Rais wa TFF, Jamal Malinzi ameishukuru SBL kwa kuunga mkono katika kusaidia maandalizi ya timu ya taifa Stars,akaongeza kusema kuwa udhamini huo utasaidia katika kufanikisha maandalizi mazuri na ushiriki kikamilifu wa timu hiyo katika mashindano mbalimbali, ndani na nje ya nchi.

  “Udhamini wa SBL umekuja kwa wakati mwafaka, wakati ambapo timu yetu ya taifa ipo katika hatua za maandalizi kwa mashindano ya kikanda na kimataifa,” alisema Malinzi.

  Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Helene Weesie (kulia ) akipeana mkono na Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) mara baada ya kukabidhiana
  mfano wa hundi ya Sh. Bilioni 2.1,Pichani kati anaeshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.

  Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Helene Weesie (kushoto) na Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kulia) kwa pamoja wakionesha mikataba waliowekeana saini, leo mbele ya Waandishi wa habari,kwenye hafla fupi iliofanyika jioni ya leo jijini Dar.Pichani kati anaeshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
   

  Wakiweka  saini mikataba hiyo.

  Pichani kati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jioni,kwenye hafla fupi ya uwekaji saini mkataba kati ya kampuni ya ya Bia ya Serengeti (SBL) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) wenye thamani ya sh.bilioni 2.1 .

  Baadhi ya Waandishi wa Habari na baadhi ya wafanyakazi wa TFF na Wizara wakishuhudi tukio la uwekaji saini mkataba wa udhamini kwa timu ya Taifa Stars wenye thamani ya sh.bilioni 2.1 uliotolewa na kampuni ya SBL  na hatimaye kuifanya kampuni hiyo kuwa mdhamini mkuu wa timu ya Taifa Stars,hafla hiyo imefanyika jioni ya ya leo jijini. Picha na Michuzi Jr.

  0 0


  0 0

  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imesema kwamba huduma ya kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto wenye matatizo ya masikio na watu wengine itaanza kutolewa Juni, mwaka huu.Huduma ya upandikizaji huo utaipunguzia serikali gharama za kuwapeleka wagonjwa wenye matatizo hayo nchini India.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Daktari Bingwa wa Masikio, Pua na Koo katika Hospitali ya Muhimbili, Edwan Liyombo wakati wa kutoa elimu kwa wazazi wa watoto wenye matatizo ya masikio jinsi ya kutunza vifaa vya usikivu kwa watoto waliopatiwa huduma hiyo.

  Dk Liyombo amesema kwamba huduma itaanza kutolewa nwezi Juni, mwaka huu na kwamba Hospitali ya Muhimbili imeboresha miundombinu na tayari imenunua vifaa kwa ajili ya kuanza kwa huduma hiyo.

  Kuhusu gharama za mtoto mmoja kuwekewa kifaa cha usikivu amesema ni ndogo kuliko akiachwa bila kupatiwa huduma hiyo kwani maisha yake yote atakuwa hasikii wala hataweza kupata uelewa wa masomo shuleni.

  “Sisi tunaona hakuna gharama ya mtoto kuwekewa kifaa cha usikivu kwa sababu huduma hii ataitumia katika maisha yake yote na akipelekwa shule atakuwa na uwezo wa kusikia na kuzungumza, kwa kifupi atakuwa sawa kama watoto wengine ambao hawana matatizo ya kusikia,” amesema Dk Liyombo.

  Akizungumzia lengo la kuwaita wazazi wa watoto wenye matatizo ya kutokusikia, Dk Liyombo amesema ni kuwaelekeza jinsi ya kutunza vifaa hivyo na endapo vina matatizo wanapaswa kutoa taarifa ili virekebishwe.
  Amewataka wazazi wenye watoto wenye matatizo ya kusikia kuwapeleka katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa huduma na pia amewataka kinamama wajawazito kuudhuria kliniki ili kuchunguzwa afya zao pamoja na mtoto kwa lengo la kuzuia mtoto kuzaliwa na tatizo la usikivu.

   Daktari Bingwa wa Masikio, Pua na Koo, wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Edwin Liyombo akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu huduma ya upandikizaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto wenye matatizo ya masikio. Kutoka kushoto ni Maneja wa Bidhaa, Shalini Srivatsan wa Kampuni ya Vanguard (T) Limited na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Nitesh Patel.
   Baadhi ya wazazi wenye watoto ambao wana matatizo ya usikivu wakimsikiliza Dk. Liyombo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
  Maneja wa Bidhaa, Shalini Srivatsan wa Kampuni ya Vanguard (T) Limited akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu namna wanavyosaidia jamii
   Watoto wenye matatizo ya usikivu wakiwa kwenye mkutano huo leo.
    Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha (kulia), Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanguard (T) Limited, Nitesh Patel na Maneja wa Bidhaa wa kampuni hiyo, Shalini Srivatsan (kushoto) wakimsikiliza Dk Liyombo wa Muhimbili kabla ya kuanza kwa mkutano na waandishi wa habari wakiwamo wazazi wa watoto wenye matatizo ya usikivu. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Kampuni ya SportPesa imeingia mkataba wa miaka mitano wa kuidhamini klabu ya Simba ukiwa na thamani ya Bilion 4.9 .

  Kampuni hiyo inayojishughulisha na masuala ya michezo ya bahati nasibu nchini Kenya imeweza kuingia nchini Tanzania na kuja kufanya uwekezaji kwa klabu mbalimbali za mpira wa miguu.

  Utiaji saini wa makubaliano ya mkataba huo umefanyika jioni hii katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa na kushuhudiwa na wadau mbalimbali wa mpira nchini.

  Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva amesema mkataba huu utaweza kuwasaidia katika kuendelea kutoa hamasa kwa timu yao kufanya vizuri zaidi.

  Kwa upande wa Mkurugenzi wa SportPesa nchini Abbas Tarimba amesema kuwa wamefurahi sana kuingia mkataba na Timu ya Simba na mkataba wao utakuwa katika hatua tofauti kulingana na makubaliano waliyoyaingia.

  Amesema kwa mwaka wa kwanza Klabu ya Simba watapata milioni 880 na katika miaka mitatu inayofuata watapata nyongeza ya asilimia 6  huku mwaka wa mwisho wa mkataba huo klabu hiyo itafaidika kwa kupata bilioni 1.08.

  Mbali na hilo Tarimba amesema kuwa klabu ya Simba itafaidika kwa kupata fedha mbalimbali kama hamasa iwapo wataweza kupata ubingwa kwa kupewa bonus ya milioni 100 au kushiriki michuano ya kimataifa.

  Kabla ya utiaji saini wa mkataba huo Simba iliweza kutoka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya stand United magoli yakifungwa na Laudit Mavugo na Juma Luizio huku la Stand likifungwa na Kasim Selembe.
  Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya SportPesa Pavel Slavkov akikabidhiana hati ya makubaliano ya mkataba na Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva ukiwa ni mkataba wa udhamini wa kipindi cha miaka mitano wenye thamani ya Bilion 4.9 uliofanyika leo katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa
  Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya SportPesa Pavel Slavkov pamoja na Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva wakisaini hati ya makubaliano ya mkataba na ukiwa ni mkataba wa udhamini wa kipindi cha miaka mitano wenye thamani ya Bilion 4.9 uliofanyika leo katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa. Kulia ni Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania Abbas Tarimba

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Yara Tanzania, Alexandre Macedo (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ghala la kuhifadhi mbolea nchini Rwanda, uliofanyika hivi karibuni. Macedo ni msimamizi pia wa Yara Rwanda na Burundi ambapo hupata huduma zake za mbolea kupitia Tanzania.

  0 0  0 0
  0 0


  0 0

  Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Umoja wa Afrika katika Usuluhishi wa Mgogoro wa Libya, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefanya ziara Mashariki mwa Libya tarehe Mei, 11 2017.

  Katika ziara hiyo, Rais Mstaafu Kikwete amekutana na Spika wa Baraza la Wawakilishi (House of Representative), Agila Saleh Essa Gwaider  nyumbani kwake Al-Qubba, Libya.

  Katika mazungumzo yao, Rais Mstaafu amemuhakikishia utayari wa Umoja wa Afrika kushirikiana na pande zote za Libya kuwezesha kufikiwa kwa suluhu ya kudumu. Amempongeza kwa dhamira na utayari wake wa kutafuta suluhu kwa njia ya mazungumzo katika muktadha wa Mkataba wa Amani wa Libya (Libya Political Agreement).

  Kwa upande wake, Spika Aguila amemshukuru Rais Mstaafu Kikwete kwa kufanya ziara kwa mara ya kwanza Mashariki mwa Libya tokea kutokea kwa mapinduzi nchini humo. Ameelezea imani yake kubwa kwa Umoja wa Afrika na mchango wake katika kutafuta suluhu ya kudumu ya tofauti zilizopo miongoni mwa wadau wa siasa wa Mashariki na Magharibi mwa Libya. Amemuhakikishia Rais Mstaafu utayari wake na wenzake wa kupitia upya baadhi ya vipengele vya Mkataba kwa lengo la kuuimarisha na si kuandikwa kwa Mkataba mpya.
  Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Umoja wa Afrika katika Usuluhishi wa Mgogoro wa Libya, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Libya (House of Representative),Agila Saleh Essa Gwaider baada ya mazungumzo yao.

  0 0


older | 1 | .... | 1684 | 1685 | (Page 1686) | 1687 | 1688 | .... | 3284 | newer