Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

SIMANZI YATAWALA JIJI LA ARUSHA KATIKA KUAGA MIILI YA WANAFUNZI 32, WALIMU WAWILI NA DEREVA

$
0
0
 Umati wa wakazi wa Jiji la Arusha na maeneo ya jirani ukiwa umefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid wakati wa zoezi la kuaga miili ya Wanafunzi 32 wa Shule ya Sekondari ya Lucky Vicent, Walimu wao wawili na Dereva waliopoteza maisha kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la Rhotia Wilayani Karatu hivi karibuni. Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan ndie aliongonza zoezi hilo la kuaga.
Sehemu ya Jeneza zenye miili ya Wanafunzi 32, Walimu wawili na Dereva waliopoteza maisha kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la Rhotia Wilayani Karatu hivi karibuni, zikiwa Uwanja wa Kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid wakati wa zoezi la kuaga lililoongozwa na Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan. 



UMISSETA COPA COCA-COLA 2017 YAZINDULIWA JIJINI MWANZA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dk Leonard Masale akikagua timu ya ya mpira wa miguu ya Nyamagana baada ya kuzindua michuano ya Copa Cocacola kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dk Leonard Masale akikabidhi vifaa vya michezo kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bugogwa baada ya kuzindua michuano ya Copa Cocacola kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Mkurugenzi wa Nyanza Bottling, Christopher Gachuma na wa pili kushoto ni Afisa Msaidizi wa Masoko wa kampuni hiyo nchini, Pamela Lugenge.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dk Leonard Masale akikabidhi vifaa vya michezo kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bugogwa baada ya kuzindua michuano ya Copa Cocacola kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Mkurugenzi wa Nyanza Bottling, Christopher Gachuma na wa pili kushoto ni Afisa Msaidizi wa Masoko wa kampuni hiyo nchini, Pamela Lugenge.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

INVITATION TO ATTEND TANZANIA – SOUTH AFRICA BUSINESS FORUM

$
0
0
Tanzania Investment Centre (TIC) in collaboration with the Ministry of Foreign Affairs and East Africa Corporation and The South African High Commission in Tanzania, are pleased to invite local companies/entrepreneurs to a business forum to be held on 11 th May 2017, at the Julius Nyerere International Conference Centre in Dar-es- salaam.

The Tanzania-South Africa Business Forum will coincide with the State visit of the South African President, HE. Jacob Zuma whereby more than 80 companies from South Africa are expected to attend the forum and meet Tanzanian Companies engaging in the following sectors ; -

 Manufacturing, Agriculture and agro processing, Mining, Textile and Apparel, Energy, Construction, Services, Pharmaceuticals, Water, Infrastructure development, Information Technologies, Telecommunications, Oil and Gas. The Tanzania- South Africa business forum will be a good platform for local companies to meet with counterpart from South Africa to discuss various business opportunities you can do together.

Companies are advised to prepare detailed profiles of their projects for easy promotion and marketing.

Interested companies are advised to register with TIC through Mr. Ayoub Magarya Mobile no. 0654862931 email ayoub.magarya@tic.co.tz

2 or Mr. Ajelandro Sindano Mobile no. 0786660777 email ajelandro.sindano@tic.co.tz before 09 th May, 2017.

Please note
1. No registration cost but participants will be required to register prior to the event.

2. A tentative program and other information will be sent to you immediately after confirmation.

3. For further details, please contact TIC on Tel. number 2116328/31 Item; Tanzania- South Africa Business Forum. before 11 th May, 2017

ISSUED BY TANZANIA INVESTMENT CENTRE- PUBLIC RELATIONS

Bunge Sports Club yaibuka mshindi katika mechi za kirafiki dhidi ya NMB

$
0
0
Spika wa Bunge Job Ndugai akimkabidhi kikombe Naodha wa timu ya Bunge Sports Club ambaye ni Mbunge wa Mbiga, Sixtus Mapunda baada ya timu hiyo kuifunga NMB Magori 2-0 wakati wa mchezo wa kirafi uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. 
 
Timu ya kwanza ya Bunge kushinda kikombe ilikuwa timu ya mpira wa pete ambaye iliifunga timu ya pete ya NMB magoli 19 kwa 2, ikifuatiwa na timu ya mpira wa kikapu kwa wanaume ambayo iliwafunga wapinzani wao timu ya mpira wa kikapu ya NMB kwa jumla ya vikapu 37 kwa 28.

Kikombe cha tatu kwa timu ya Bunge kilipatikana kwa timu ya mpira wa miguu ambayo iliwafunga NMB goli 2-0 na hivyo kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo wowote ambao timu hizo zimekutana.

Timu ya Bunge Sports Club na NMB Sports Club zimekuwa zikikutana zikicheza michezo mbalimbali ikiwa na lengo ya kuboresha uhusiano baina ya Bunge na NMB ambapo kwa mwaka huu bonanza hilo limefanyika katika uwanja wa Jamhuri uliopo makao makuu ya nchi, Dodoma.
Abdulmajid Nsekela- Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na wa kati NMB akisalimiana na mchezaji wa Bunge Sports Club mpira wa Pete ambaye ni Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kabla ya mchezo wa kirafiki wa Pete kati ya Bunge na NMB.TIMU ya Bunge Sports Club inayojumuisha timu ya mpira wa miguu, mpira wa pete na kikapu imeibuka washindi na kunyakua vikombe vitatu katika bonanza lililozikutanisha timu ya Bunge na timu ya Benki za NMB.
Meneja wa Kanda ya Kati wa NMB, Straton Chilongala akimkabidhi nahodha wa mpira wa Pete wa Bunge Sports Club ambaye pia ni Mbunge wa Tarime Esther Matiko.
Abdulmajid Nsekela akikabidhi kikombe cha mpira wa Kikapu kwa washindi Bunge Sports Club.
Wachezaji wa Bunge Sports Club na NMB mpira wa pete wakiwania mpira wakati wa mchezo wa kirafi uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma. 

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI APRILI HAUJAONGEZEKA UMEBAKI ASILIMIA 6.4

$
0
0
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii ,Epraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei nchini kwa mwezi Arili, 8 kwaka huu.

Na Dotto Mwaibale

MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Sensa za watu na takwimu wa Ofis ya Taifa ya Takwimu,(NBS), Ephraim Kwesigabo, alisema hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha March 2017 imekuwa sawa na kasi ya upandaji ilivyokuwa mwaka ulioisha.

Kwesigabo, alisema fahirisi za bei zimeongezeka hadi 109.4 mwezi April 2017 kutoka 1o2 mwezi April 2016.

"Mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi marchi 2017 kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha mwezi Aprili imekuwa sawa na mwezi Marchi 2017,"alisema

Pia alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Aprili 2017 umeongezeka hadi 11.8 kutoka asilimia 11.0 ilivyokuwa mwezi Marchi.

Aidha mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Aprili 2017 umeongezeka hadi asilimia 12.0 kutoka asilimia 11.7 mwezi Marchi 2017.

Alisema badiliko la fahirisi za bei kwa bidhaa sisizo za vyakula umepungua kidogo hadi asilimia 3.4 mwezi Aprili kutoka asilimia 3.6 mwezi Machi.

Akizungumzia kuhusu ukuaji wa dhamani ya shilingi, Kwesigabo alisema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 91 na senti 71, mwezi Aprili 2017 ikilinganisha na shilingi 92 na senti 21 ilivyokuwa mwezi Marchi 2017.

SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI UJENZI WA KITUO CHA MABASI MBEZI LUIS

BENK YA WANAWAKE TAWI LA MKWEPU WAUNGANA NA TAIFA KUOMBOLEZA VIFO VYA WANAFUNZI 32, WALIMU 2 NA DEREVA

$
0
0
Kwa niaba Benki ya Wanawake wametuma salamu za pole kwa wazazi, walezi, familia na jamii yote ya Arusha na Tanzania kwa ujumla, kwa kupoteza watoto wetu ambao walikuwa waliokuwa wanandaliwa kuwa nguvu kazi ya Taifa letu katika Sekta mbalimbali.

Mwenyezi Mungu awapatie Faraja na Moyo wa Subira  katika kipindi hiki kigumu cha huzuni, uchungu na simanzi kwa familia za marehemu na Taifa kwa ujumla. 

Wafanyakazi wa Benki ya Wanawake Tawi la Mkwepu wameungana na Taifa kuombolea vifo vya wanafunzi 32, walimu 2 na dereva mmoja  vilivyotokana na ajali iliyotokea Karatu mkoani Arusha tarehe 6 May,  mwaka huu.

SERIKALI KUFUTA USHURU NA TOZO MBALIMBALI KWA WAKULIMA


Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini kufanya ziara ya siku tatu nchini Tanzania

$
0
0

Taarifa kuhusu ziara ya Rais wa Afrika Kusini nchini

1. UTANGULIZI

(i) Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mheshimiwa Jacob Gedleyihlekisa Zuma anatarajiwa kufanya Ziara ya Kitaifa ya siku tatu hapa nchini, kuanzia tarehe 10 hadi12 Mei 2017, kwa mwaliko wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(ii) Ziara hii inafanyika baada ya Mheshimiwa Rais Magufuli na Mheshimiwa Rais Zuma kukutana mjini Addis Ababa, Ethiopia wakati wa Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU).

(iii) Mheshimiwa Rais Zuma anatarajiwa kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tarehe 10 Mei 2017, jioni na kupokelewa na mwenyeji wake, Mheshimiwa Rais Magufuli. 

(iv) Ziara hii itatoa fursa kwa Viongozi wetu kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi hizi mbili, ya kikanda na kimataifa pamoja ‎na kujadili fursa zaidi za ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji na biashara. Ujio wa Mheshimiwa Rais Zuma ni fursa nzuri sana ya kuendelea kukuza na kuimarisha zaidi mahusiano mazuri naya kihistoria kati ya nchi zetu mbili. 

(v) Mheshimiwa Rais Zuma anafuatana pia na wafanyabiashara takribani 80. Hii ni fursa muhimu sana katika kukuza mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini. Hivyo, tarehe 11 Mei 2017, kutakuwepo na Kongamano la Wafanyabiashara katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JINCC).

(vi) Ziara ya Mheshimiwa Rais Zuma inaenda sambamba na vikao vya Tume ya Pamoja ya Marais (Bi-National Commission - BNC) kati ya Tanzania na Afrika Kusini. Mkutano wa Marais umepangwa kufanyika tarehe 11 Mei, 2017. Mkutano huo utatanguliwa na Kikao cha Mawaziri kitakachofanyika tarehe 10 Mei, 2017 na kikao cha Makatibu Wakuu kitafanyika tarehe 8 na 9 Mei, 2017.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu Ziara ya Rais wa Afrika Kusini nchini Mhe. Jacob Zuma, ambaye atawasili nchini kwa ziara ya siku 3. Pamoja na mambo mengine, Rais Zuma pia atatembelea Hospitali ya Muhimbili Kitengo cha tiba ya ugonjwa wa moyo (Jakaya Kikwete Cardiac Institute), na pia kufungua rasmi Ubalozi wao hapa nchini. 
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Suleiman Salehe, akimsikiliza Waziri Mahiga (Hayupo pichani) katika mkutano na waandishi wa Habari 
Sehemu ya waandishi wa habari wakinukuu maeneo mbalimbali yaliyotajwa na Waziri Mahiga kwenye mkutano na waandishi wa habari. 
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea. 

Tanzania na Afrika Kusini za dhamiria kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi

$
0
0

Wataalamu wa Tanzania na Afrika Kusini wapo katika mkutano wa siku nne wa kuandaa mpango bora wa kushirikiana kwenye maeneo mbalimbali kwa madhumuni ya kukuza uchumi wa nchi hizo.

Mkutano huo unaojulikana kama Tume ya Ushirikiano ya Marais (Bi-National Commission-BNC) umefunguliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima jijini Dar Es Salaam leo.

“Mkutano huu ni muhimu sana kwa kuwa licha ya nchi zetu kuwa na uhusiano na ushirikiano mzuri tokea enzi za ubaguzi wa rangi, lakini bado utakuwa chachu ya kuimarisha na kuharakisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii katika maeneo tutakayokubaliana na wenzetu” Balozi Mlima alisema. 

Balozi Mlima alieleza kuwa Tanzania na Afrika Kusini zilikubaliana kuanzisha Tume ya Marais ya Uchumi (Presidential Economic Commission-PEC) mwaka 2005 na mwaka 2011 nchi hizo zilisaini BNC ambayo ilichukuwa nafasi ya PEC. Tokea uwekaji saini wa makubaliano hayo, chombo hicho hakikuweza kukutana licha ya kuwa, makubaliano hayo ndiyo yatakuwa mwongozo katika majadiliano yatakayoendelea hadi tarehe 11 Mei 2017.

Kwa mujibu wa Balozi Mlima, uhusiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Afrika Kusini unaendelea kuimarika kadri siku zinavyokwenda. Kwa takwimu zilizopo takribani makampuni 226 ya Afrika Kusini yamewekeza nchini mtaji wa jumla ya Dola za Marekani milioni 803.15 na kuajiri zaidi ya watu 20,917. Alisema idadi ya makampuni inaweza kuongezeka kwani kuna makampuni mengi mapya kutoka Afrika Kusini yameshaonesha dhamira ya kuwekeza nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Tume ya Marais ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini unafanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. 
Sehemu ya Makatibu Wakuu nao wakifuatilia kwa makini Hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Dkt. Mlima.
Dkt. Mlima akiendelea kuzungumza .


KUMBUKUMBU YA MAREHEMU AKANASHE MAKERE

$
0
0

ILIKUWA NI SEKUNDE, DAKIKA, SAA, WIKI, MWEZI  MWAKA NA SASA NI MIAKA MITANO UMETIMIZA TANGU BIBI YETU KIPENZI AKANASHE SHEDRACK MAKERE UTUTOKE GHAFLA TAREHE 08/05/2012 SAA 10 JIONI BILA YA KUTUAGA KUTOKANA NA MARADHI YALIYOKUWA YAKIKUSUMBUA.

UNAKUMBUKWA SANA KWA UCHESHI, UPENDO NA KUWAJALI KILA KIUMBE CHA HAPA DUNIANI. HALIDHALIKA UNAKUMBUKWA SANA NA WANAO, WAJUKUU, VITUKUU, KILEMBWE, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ZAKO. UMETUACHIA HUZUNI NA PENGO KUBWA KATIKA UKOO.

MWENYEZI MUNGU, MUUMBA WA MBINGU NA NCHI AENDELEE KUKUPA MWANGA NA RAHA YA MILELE HUKO ULIPO KWANI YEYE NDIYE ALIYETOA NA YEYE NDIYE ALIYETWAA. JINA LA BWANA DAIMA LIHIMIDIWE. AMEN!

BALOZI ASHA-ROSE MIGIRO AWATEMBELEA WANADIASPORA READING

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Asha-Rose Migiro alifanya ziara ya kuwatembelea watanzania waishio Reading na Bekshire tarehe 6/5/2017. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Balozi Migiro alipata fursa ya kufanya mkutano na kuwatembelea baadhi ya watanzania hao kwenye maeneo yao ya kazi.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Asha-Rose Migiro akiwa pamoja na baadhi ya wana diaspora waishio Reading na Bekshire waliohudhuria mkutano.
 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Bw. Daniel Samwenda mmoja wa wamiliki wa kampuni ya McDaan Finance inayojishughulisha na shughuli mbali mbali za kifedha kama kutoa mikopo ya muda mfupi.
 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Asha-Rose Migiro akipata maelezo kutoka kwa Bw. Hassan Abdula Mkurugenzi wa Kampuni ya Hill View Family Co. Ltd inayojishughulisha na usafirishaji wa mizigo.

SPIKA WA BUNGE ATEMBELEWA NA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI PAMOJA NA UJUMBE WA MWENYEKITI WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA NCHINI TANZANIA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akisalimiana na Msajili wa Vyama vya siasa nchini Tanzania, Jaji Francis Mtungi (kulia) aliemtembelea leo Ofisini kwake katika Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akisisitiza  jambo mbele ya ujumbe wa Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa nchini Tanzania ukiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa nchini Tanzania, Mhe. John Shibuda (Kushoto) na kulia ni Msajili wa Vyama vya siasa nchini Tanzania, Jaji Francis Mtungi katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake katika Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa nchini Tanzania, Mhe. John Shibuda (Kushoto), pale ujumbe wa Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa ulipomtembelea leo Ofisini kwake katika Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa nchini Tanzania, Mhe. John Shibuda (Kushoto), Msajili wa Vyama vya siasa nchini Tanzania Jaji Francis Mtungi (kulia) pale walipomtembelea na ujumbe wa Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa nchini Tanzania, katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake katika Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.

KATIBU MKUU WIZARA YA UCHUKUZI, DKT LEONARD CHAMURIHO AKEMEA UDOKOZI NA WIZI KATIKA USAFIRI WA ANGA.

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamuriho amewakumbusha wadau wa usafiri wa anga kusughulikia na kumaliza tatizo la wizi na udokozi katika usafiri wa anga, hali ambayo amesema inahatarisha usalama na ustawi wa sekta hii hapa nchini.

Katika hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa 42 wa kamati ya Kitaifa ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga (National Air Transport Facilitation Committee) iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchukuzi - Sekta ya Uchukuzi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Rogatus Hussein Mativila, Dkt. Chamuriho ametoa mfano wa taarifa za hivi karibuni katika vyombo vya habari kuhusu wizi wa mafuta ya ndege hali ambayo amesema itajenga hofu kwa watumiaji wa uchukuzi wa anga . 

"Matukio kama haya hayaatarishi usalama tu, lakini pia ustawi wa sekta kwa vile yatajenga hofu kwa wasafiri na kusababisha wachague njia nyingine". Alisema Katibu Mkuu na kuongeza ustawi wa usafiri wa anga katika nchi yoyote, unategemea na upatikanaji wa huduma bora katika viwanja vya ndege, usalama wa abiria na mali zao, ndege na miundombinu mbali mbali .
Kaimu Mkurugenzi Udhibiti Masuala ya Kiuchumi , Mamlaka ya Usafiri wa Anga Dan Malanga (wa kwanza Kushoto) akimsikiliza Meneja wa uwanja wa ndege wa Dodoma, Julius K. Mlungwana,(wa Pili Kushoto) wakati kamati ya kitaifa ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ilipotembelea kiwanja cha ndege Dodoma May, 8 2017.
Kaimu Mkurugenzi Udhibiti Masuala ya Kiuchumi, Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Dan Malanga (Amesisima) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha 42 cha wajumbe wa kamati ya kitaifa ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga kilichofanyika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma May, 8 2017.
Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchukuzi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Rogatus Hussein Mativila akifungua kikao cha 42 cha wajumbe wa kamati ya Kitaifa ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga Kilichofanyika Ukumbi wa Hazina mijini Dodoma May, 8 2017.

Makamu wa Rais aongoza Watanzania kuaga miili ya wanafunzi waliopata ajali Mkoani Arusha

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan leo tarehe 8-May-2017 ameongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Arusha na Mikoa ya Jirani katika kuaga miili ya wanafunzi 32,walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha waliopata ajali katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.

Katika hotuba yake kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi katika tukio la kuaga miili hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahakikishia waombolezaji kuwa Serikali ipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu na chenye majonzi mazito kwa kuondokewa na wapendwa wao.

Amehimiza wananchi kote nchini kuungana katika msiba uliotokea kwa kuwafiriji wafiwa katika kipindi hiki kigumu na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali peponi.

Makamu wa Rais pia ameiagiza Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia, Jeshi la Polisi nchini,walimu, wazazi na walezi wawe makini katika kuhakikisha kuwa sheria za usalama barabarani zinazingatiwa kwa kuchukua hatua stahiki za kulinda watoto hasa wanapotumia vyombo vya moto kwenye shughuli zao za kimasomo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa zoezi la kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akitoa pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu waliofika katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili hiyo.
Miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent ikiwa katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuombewa pamoja na kuagwa leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwenye miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwafariji ndugu na jamaa wa marehemu waliofika kuaga miili ya ndugu zao leo katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Kiserikali na chama wakiwa kwenye 
uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha wakati wa kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent.

Wanafunzi wa shule ya Lucky Visent wakiwa kwenye majonzi wakati wa kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.

Baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha wakiwa 
 katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent waliofariki kwenye ajali.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana ateta jambo na Wazir pamoja na Pole pole jijini Arusha leo.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Katibu wa Makamu wa Rais, Wazir Salum mapema leo jijini Arusha walipokuwa wakielekea kwenye tukio la kuaga miili ya Wanafunzi 32,waalimu wawili na dereva mmoja ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini humo,ambapo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alishiriki kuongoza tukio hilo,kushoto ni katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu  Pole Pole
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalamiana na Katibu wa Makamu wa Rais, Wazir Salum mapema leo jijini Arusha walipokuwa wakielekea kwenye tukio la kuaga miili ya Wanafunzi 32,waalimu wawili na dereva mmoja ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini humo,ambapo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alishiriki kuongoza tukio hilo,kushoto ni katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu  Pole Pole
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo na Katibu wa Makamu wa Rais, Wazir Salum mapema leo jijini Arusha walipokuwa wakielekea kwenye tukio la kuaga miili ya Wanafunzi 32,waalimu wawili na dereva mmoja ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini humo,ambapo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alishiriki kuongoza tukio hilo,kushoto ni katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu  Pole Pole

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA TATU AFRIKA KWA SHERIA BORA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA KEMIKALI

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Tanzania imeshika nafasi ya tatu barani Afrika ikiongozwa na nchi ya Afrika Kusini na Nigeria kwa kuwa na Sheria bora ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Prof. Samweli Manyele alipokua akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkutano wa Kimataifa wa Udhibiti wa Kemikali na Kemikali Taka uliofanyika Geneva, Uswisi kuanzia Aprili 24 hadi Mei 5 mwaka huu.

Prof. Manyele amesema kuwa katika Bara la Afrika Tanzania ndio nchi pekee ambayo ina taasisi ya Serikali inayosimamia kemikali wakati nchi zingine usimamizi wa masuala ya kemikali upo katika taasisi za mazingira kitu ambacho kinapelekea usimamizi hafifu wa kemikali hizo.
“Tanzania ni nchi pekee Afrika ambayo taasisi inayohusika na masuala ya kemikali ipo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na pia ni taasisi yenye kusimamiwa na wataalamu wa kemikali waliobobea pamoja na kuwa na maabara kubwa inayojulikana kimataifa,”alisema Prof. Manyele.
Akiongelea kuhusu mkutano huo, Prof. Manyele amesema kushiriki katika mkutano huo ni jambo la kisheria hivyo kupeleka watumishi watatu kutoka kwenye taasisi hiyo inadhihirisha kuwa Tanzania imetimiza majukumu yake kama Taifa.
Amefafanua kuwa mkutano huo unaisaidia taasisi kutoa taarifa kuhusu utendaji kazi, kujifunza nchi zingine wanafanyaje kazi zao, kupata majibu ya moja kwa moja pamoja na kujadiliana namna ambavyo wataboresha utendaji kazi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma ya Ubora wa Bidhaa, Daniel Ndiyo ametaja wadau wanaotakiwa kupata taarifa na maamuzi ya mkutano huo kuwa ni wafanyabiashara, watumiaji wa kemikali hizo pamoja na mamlaka mbali mbali za usimamizi wa kemikali. 

Naye Meneja wa Kanda ya Kaskazini GCLA , Christopher Anyango amesema mkutano huo unawasaidia wananchi kupata msaada wa haraka kutoka katika Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuwa wana uelewa pamoja na kupata mafunzo ya kemikali zinazoruhusiwa na zisizoruhusiwa kulingana na mahitaji kwa wakati husika.
Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ilishiriki katika mkutano huo wa utekelezaji wa mikataba mitatu ikiwemo ya usafirishaji wa taka sumu kimataifa (Basel), mkataba unaohusu kemikali zenye madhara na zinazochukua muda mrefu kuoza katika mazingira (Stockholm) pamoja na mkataba wa Rotterdam unaohusu upashanaji taarifa juu ya kemikali hatari na viuatilifu katika biashara ya kimataifa.

 Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu Tanzania kushika nafasi ya tatu barani Afrika kwa kuwa na Sheria bora ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali hali iliyopelekea Taasisi hiyo kuwa moja ya Taasisi bora zenye maabara ya kisasa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma ya Ubora wa Bidhaa, Bw. Daniel Ndiyo na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara, Bw.  George Kasinga.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma ya Ubora wa Bidhaa, Bw. Daniel Ndiyo akiwaeleza waandishi wa habari umuhimu wa wananchi kupata taarifa na maamuzi ya mkutano wa Kimataifa kuhusu Udhibiti wa kemikali na kemikali taka uliofanyika hivi karibuni  Geneva, Uswisi kuanzia Aprili 24 hadi Mei 5 mwaka huu.
Meneja wa Kanda ya Kaskazini GCLA, Bw. Christopher Anyango akifafanua kuhusu mkakati wa Serikali kuwajengea uwezo wananchi kuelewa madhara yatokanayo na kemikali ambazo zimepigwa marufuku.
Picha na Frank Mvungi-Maelezo


YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA KUMI NA TISA MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 8, 2017.

$
0
0
Spika  wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai  akiongoza  kikao cha kumi na Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 8, 2017.
Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA)  Mhe.Catherine Nyakao Ruge  akila kiapo cha uaminifu mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa katika  kikao cha kumi na Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 8, 2017.
Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Mariam Kisangi(CCM) akiuliza swali katika  kikao cha kumi na Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 8, 2017.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Mhe.Selemani  Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha kumi na Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 8, 2017.
Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Angelina Malembeka (CCM) akiuliza swali katika  kikao cha kumi na Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 8, 2017.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI WA FEDHA ZANZIBAR AZUNGUMZA NA WAANDISHI LEO.

$
0
0

Waziri wa Fedha Zanzibar Dk Khalid Salum Mohd akifafanua jambo kwa  Waandishi wa Habari kuhusiana na Mipango Mapendekezo ya Bajeti (Mapato na matumizi) ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017-2018.Katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha Vuga Mjini Unguja.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika mkutano wa waandishi wa habari na  Waziri wa Fedha Zanzibar Dk Khalid Salum Mohd kuhusiana na Mipango Mapendekezo ya Bajeti (Mapato na matumizi) ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017-2018.Katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha Vuga Mjini Unguja.PICHA NA YUSSUF SIMAI /MAELEZO ZANZIBAR.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS AWATEMBELEA MAJERUHI WA AJALI YA KARATU HOSPITALI

$
0
0
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali  Godfrey Tarimo mwenye umri wa miaka 11 ambaye ni mmoja wa majeruhi waliolazwa kwenye hospitali mkoa wa  wa Arusha ya Mt. Meru, Godfrey ni mmoja ya waliojeruhiwa katika ajali waliopata wanafunzi wa Lucky Vincent (Picha na Ofisi ya Maku wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali  Doreen Mshana mwenye umri wa miaka 13ambaye ni mmoja wa majeruhi waliolazwa kwenye hospitali mkoa wa  wa Arusha ya Mt. Meru, Doreen ni mmoja ya waliojeruhiwa katika ajali waliopata wanafunzi wa Lucky Vincent (Picha na Ofisi ya Maku wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali  Sadia Isamel Awadhi mwenye umri wa miaka 11 ambaye ni mmoja wa majeruhi waliolazwa kwenye hospitali mkoa wa  wa Arusha ya Mt. Meru, Sadia ni mmoja ya waliojeruhiwa katika ajali waliopata wanafunzi wa Lucky Vincent (Picha na Ofisi ya Maku wa Rais)
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live


Latest Images