Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

TANZANIA ALL STAR - TUNAWAOMBEA


RAMBIRAMBI

TFF YAOMBOLEZA

Kamishna Mkuu TRA atembelea Ubalozi wa Tanzania, London

0
0
Mheshimiwa Balozi Asha-Rose Migiro (wanne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna Mkuu wa TRA, Bwana Charles E. Kichere (watatu-kushoto). Kamishna Mkuu wa TRA na ujumbe wake wapo nchini Uingereza kwa safari ya kikazi, Ijumaa tarehe 5 Mei 2017 walipata nafasi ya kutembelea Ofisi za Ubalozi na kufanya mazungumzo na Mhemiwa Balozi. Wengine katika picha ni msaidizi wa Kamishna Bwana Masumbuko Mwaluko (watatu kulia), Bwana Said Kiondo(wpili kulia) Kaimu Mkuu kitengo cha  Utafiti cha Mamlaka ya mapato, Mkuu wa Utawala Ubalozini, Bibi Rose Kitandula, Mwambata wa Fedha Ubalozini Bwana Wema Kibona na Mwambata wa Uhamiaji Bwana Magnus Ulungi

WAZIRI MWIGULU NA WATENDAJI WAKE WAKUU WAJADILI BAJETI YAKE IKIWA NI MAANDALIZI YA MWISHO KABLA YA KUIWASILISHA KWENYE BUNGE LA BAJETI MJINI DODOMA JUMANNE

0
0
 Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Lameck Nchemba  wa pili kushoto akitoa Maelekezo kwa  Watendaji Wakuu wa  Wizara yake wakati wa Kikao cha cha maandalizi ya mwisho cha kupitia Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara yake, kabla ya kuiwasilisha Bajeti ya Wizara yake katika Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Jumanne. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamadi Masauni na wa kwanza kulia ni  Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Wizara mjini Dodoma. 

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu aliyenyanyua mkono akitoa ufafanuzi wa jambo fulani kuhusu bajeti  ya Jeshi la Polisi nchini mbele ya Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba  wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni maandalizi  ya mwisho kabla ya Bajeti ya Wizara hiyo kuwasilishwa kwenye  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,siku ya  jumanne.Kikao hicho kilichowashirikisha Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo na Maafisa Mipango wa Wizara kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  wizara hiyo mjini Dodoma. 

 Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba  akipokea taarifa mbalimbali zilizotolewa na watendaji wakuu wa Wizara yake wakati wa Kikao cha Maandalizi ya mwisho ya kupitia ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara yake,  kabla ya kusomwa kwa Bajeti ya Wizara yake katika Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Jumanne. Kushoto kwake ni  Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamadi Masauni, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  wizara mjini Dodoma. 

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza  nchini, Dkt. Juma Malewa wa pili kulia akitoa ufafanuzi mbele ya Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba  wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni maandalizi  ya mwisho kabla ya Bajeti ya Wizara hiyo kuwasilishwa kwenye  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,siku ya Jumanne.Kikao hicho kilichowashirikisha Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo na Maafisa Mipango wa Wizara kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Wizara hiyo mjini Dodoma. 

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye wa tatu kulia  akitoa ufafanuzi kuhusu Jeshi lake mbele ya Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba  wakati wa Kikao cha maandalizi ya mwisho ya kupitia ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  kabla ya Bajeti ya Wizara hiyo kusomwa kwenye Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,siku ya Jumanne.Kikao hicho kilichowashirikisha Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo na Maafisa Mipango wa Wizara kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Wizara hiyo mjini Dodoma. 

PICHA ZOTE NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

SALAAM ZA RAMBIRAMBI KUTOKA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

0
0

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea kwa huzuni na masikitiko  makubwa taarifa ya vifo vya watoto 32, walimu 2 na dereva mmoja wa shule ya Lucky Vicent ya Arusha, vilivyosababishwa na ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu - Arusha. 
Tunasikitika sana kwa kuwa ajali hii imetokea wakati wazazi, walezi na walimu wakitekeleza wajibu wao wa msingi wa kumpatia mtoto haki ya kuendelezwa Kielimu.
Kufuatia msiba huu mkubwa, kwa niaba ya Wizara na kwa niaba yangu mwenyewe ninatoa pole kwa wazazi, walezi, familia na jamii yote ya Arusha na Tanzania kwa ujumla, kwa kupoteza watoto wetu ambao walikuwa wanaandaliwa kuwa nguvu kazi ya Taifa letu katika Sekta mbalimbali. Tunamuomba 
Mwenyezi Mungu awapatie Faraja na Moyo wa Subira  katika kipindi hiki kigumu cha huzuni, uchungu na simanzi kwa familia za marehemu na Taifa kwa ujumla. 
Tunaziombea roho za watoto wetu wapendwa zipumzishwe mahali pema peponi, Amiin. Ni maombi yetu pia kuwa Majeruhi waliopo hospitalini watapata nafuu ili waweze kuendelea na masomo.

Ummy Mwalimu, Mb
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
07/05/2017

Emmanuel Macron ashinda kwa kishindo kiti cha urais Ufaransa

0
0

Na Sultani Kipingo

Emmanuel Macron (pichani) leo ameshinda kwa kishindo kinyang'anyiro cha Urais wa Ufaransa na kumweka kando Marine Le Pen kwenye mbio hizo za kuingia Ikulu ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa, Macron kashinda kwa kupata asilimia 64.78 za kura dhidi ya mpinzani wake Le Pen aliyeambulia asilimia 35.22 za kura. 

Akiwa na umri wa miaka 39, Macron anakuwa kiongozi kijana zaidi kutawala nchi hiyo tangia enzi za utawala wa Napoleon Bonaparte.

"Nimempigia simu Emmanuel Macron usiku huu kumpongeza kwa kushinda kiti cha urais wa Jamhuri ya Ufaransa, " rais anayemaliza muda wake Francois Hollande amesema katika taarifa yake.

Rais Hollande amesema ushindi wa kishindo wa Macron unathibitisha kwamba raia wengi wa Ufaransa wanakubaliana na mustakabali wa Jamhuri hiyo na kuthibitisha uungaji mkono wa Jumuiya ya Ulaya - ambayo Le Pen alikuwa ametangaza kufikiria kujitenga.Mama huyo pia alikuwa anapiga vita sana sera za uraia za Ufaransa ambapo alisema endapo atachaguliwa ataangalia namna ya kuzuia wahamiaji na wakimbizi kukanyaga nchi hiyo.

Marine Le Pen amekubali matokeo na kumpongeza Macron kwa ushindi wake mnono wa kupata asilimia 31 ya kura zaidi ya zake.





WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI ARUSHA


SAIGON social club ya jijini Dar es salaam imefanya khitma ya kurehemu waliotangulia mbele ya haki

0
0
Jana Jumapili Saigon social club ya jijini Dar es salaam imefanya khitma ya kurehemu wazee na ndugu  wa Kariakoo waliotangulia kwa Mwenyenzi Mungu. Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilali. Kila mwaka klabu hii hufanya khitma ikiwa ni mojawapo ya shughuli katika kalenda yake
 Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilali akikaribishwa makao makuu ya Saigon Social Club kuhudhuria khitma hiyo
 Sehemu ya wanachama wa Saigon Social club na wageni waalikwa
 Baadhi ya viongozi wa Saigon Social club
 Mashekhe wakiongoza khitma
Khitma inaendelea. Picha kwa hisani ya Mohamed Said.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

PICHA ZA WANAFUNZI (32),WALIMU (2) NA DEREVA (1) WALIOFARIKI KWA AJALI YA GARI HUKO KARATU MKOANI ARUSHA

MAGAZETI YA LEO JUMATATU MAY 8, 2017

MAADHIMISHO YA NNE YA UMOJA WA MATAIFA KWA WIKI YA USALAMA BARABARANI (UN ROAD SAFETY WEEK)

0
0
Na Mary Richard (Advocate)


NAHREEL'S PRODUCTION NEVER STOPS TO AMAZE US,COKE STUDIO AFRICA 2017

0
0
Nahreel, the recipient of 2015 KTMA 2015 “Producer of the year” award, The Industry Studios record producer and a Navy Kenzo recording artist have been invited to the Coke Studio season five. Nahreel will work with 6 superstar artists from 6 different countries to produce their original tracks. Within a 3 weeks’ timeline he will work with 2 artists in a weekly basis. Nahreel made their Debut on Coke Studio Africa in the season 4, apparently its Nahreel’s second appearance.
 About Nahreel:
Emmanuel Mkono (born 12 December 1989, in dar es salaam), known by his stage name Nahreel,is a Tanzanian nominated record producer, singer, rapper and entrepreneur. He is the founder and current C.E.O of The Industry Studios. Nahreel was co-founder and member of the music group Navy kenzo. He has produced albums and hit single for and overseen the careers of many rappers, including Joh makini, Nikki wa pili, Vanessa Mdee, Izzo bizness, G nako, and more. He is credited as a key figure in the popularization of English rap, Afropop & dancehall in Tanzania, which is a Swahili speaking nation.

WANAHABARI WA ISRAEL WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA GOMBE, WAAHIDI KUTANGAZA VIVUTIO VYA TANZANIA NCHINI HUMO

0
0

Kundi la waandishi kumi wa habari kutoka nchini Israel wakiwa katika hifadhi ya Taifa ya Gombe hivi karibuni kwa ajili ya kurekodi vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana katika hifadhi hiyo kwa ajili ya kuvitangaza nchini kwao ikiwa ni mkakati wa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa kushirikiana na Hifadhi za Taifa (TANAPA). Kwa sasa soko la utalii la mashariki ya kati limeanza kufunguka kwa kasi ambapo hivi karibuni Waziri Mkuu Mstaafu wa Israel Ehud Barak ametembelea hifadhi za Ngorongoro na Serengeti.

HAMZA TEMBA - WMU

Kundi la wanahabari kumi akiwemo muigizaji mmoja na maofisa wa kampuni ya utalii ya Safari kutoka nchini Israel limetembelea hifadhi ya Taifa ya Gombe iliyopo mkoani Kigoma na kufurahia vivutio lukuki vya utalii vinavyopatikana katika hifadhi hiyo na kuahidi kuvitangaza watakaporudi nchini kwao ikiwa ni mkakati wa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia TANAPA na Bodi ya Utalii kutangaza vivutio hivyo nchini humo.


Akizungumza hivi karibuni mara baada ya kukamilika kwa ziara hiyo ya siku mbili, Kiongozi wa kundi hilo, Ronit Hershkovitz alisema ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa ambapo wamefurahia kuona vivutio vya kipekee katika hifadhi hiyo na kuahidi kuwa mabalozi wazuri wa vivutio hivyo nchini Israel. 


Timu maalum ya wanahabari kutoka nchini Israel ikiwa na wajumbe kumi ilipowasili katika uwanja wa ndege wa Kigoma tayari kwa ajili ya ziara ya kitalii ya siku mbili katika hifadhi ya Taifa ya Gombe. Ziaza hiyo iliandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kushirikiana na Shirika ya Hifadhi za Taifa Tanzani (TANAPA) kwa ajili ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nchini Israel ikiwa ni mkakati maamlum wa kukamata soko la Mashariki ya Kati. Kutoka kulia wanaongoza msafara huo ni Meneja Mawasiliano TANAPA, Paschal Shelutete na Meneja Mahusiano wa TTB, Geofrey Tengeneza.

“Ni furaha kubwa kuwa hapa Gombe, tumeona makundi ya Sokwe na fukwe nzuri za Ziwa Tanganyika, tuko hapa kwa ajili ya kwenda kueleza kivutio hiki na vivutio vingine vya Tanzania nchini Israel, Waisrael wanaipenda Tanzania na wanapenda kutembelea Tanzania, tumeona ongezeko kubwa la watalii katika miaka ya hivi karibuni kutoka Israel baada ya kazi ngumu ya muda mrefu, sasa tuna furaha kuona watalii wengi wanaongezeka na tungependa kuona pia Watanzania wengi wakitembelea Israel,” Alisema Ronit.


Aliongeza kuwa, “Tunaenda kueleza taarifa hizi kwenye mitandao ya kijamii, magazeti, televisheni na popote tutakapoweza, lakini kubwa zaidi ni kuwaeleza marafiki zetu ana kwa ana uzuri wa Tanzania kwasababu tunaipenda Tanzania, nakupenda sana”.


Wanahabari kutoka Israel wakipanda kwenye boti kwa ajili kunza safari kuelekea hifadhi ya Taifa ya Gombe. Msafara huo ulikuwa na wanahabari kutoka vyombo maarufu nchini humo ikiwemo kituo cha Televisheni cha Channel 2, Jarida la Atmosphere, Jarida la National Geographic, Jaria la wiki la Yediot Acharanot -7 Yamim na waandishi wawili wa mitandao ya kijamii. Wengine ni maofisa wawili wa kampuni ya Utalii ya Safari  ya nchini humo.

Walfson Noa, ambaye ni Mwandishi wa Mitandao ya Kijamii na Meneja Masoko wa Kampuni ya Utalii ya Safari ya Israel alisema, “Tulifanya matembezi kuwaona Sokwe wanaovutia sana huku wakiishi katika mazingira yao ya asili, hili ziwa ni la maajabu sana (Ziwa Tanganyika), hata nyani nao walikuwa wakijaribu kuingia kwenye mahema yetu ni jambo la kuvutia, katika mtizamo wa kimasoko hili ni eneo ambalo nitawashauri wateja wangu watembelee, ni kitu ambacho watu wanatakiwa kukifahamu, kugundua siri ya uzuri wa hifadhi ya Taifa ya Gombe”

BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI

SALAAM ZA RAMBIRAMBI KUTOKA TCRA


MKULIMA IDDY MLUKA AELEZEA MAFANIKIO YAKE YA KILIMO KUPITIA MBOLEA ZA YARA TANZANIA

NHIF TANGA KUPELEKA HUDUMA YA TOTO AFYA KADI VIJIJINI

0
0
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) unakusudia kuwafikia wananchi kwenye vijiji na kata mbalimbali mkoani hapa ili kutoa elimu juu ya umuhimu wa huduma ya afya kwa watoto (Toto Afya  Kadi) ambapo uelewa wake umekuwa sio mzuri.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu (Pichani Juu)wakati akizungumza na mtandao huu ofisini kwake ambapo alisema wameamua kufanya hivyo ili kuipa uelewa jamii kuhusiana na umuhimu na faida za huduma hiyo.


Alisema wakiwa huko watapita kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo mashuleni na kufanya mikutano ya nje kwa wananchi ili kuweza kuwapa uelewa juu manufaa ya kuwaingiza watoto hao kwenye mfuko huo.

“Unajua hii huduma Toto Afya Kadi hasa kwa maeneo ya vijijini uelewa wake umekuwa sio mzuri hivyo sisi tumepanga kuanza kuhamasisha na kuipa uelewa jamii ili waweze kuitambua na kujiunga nayo “Alisema.

“Nia kubwa ni kutaka kuona jamii waliochini ya miaka 18 wana jiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwani itawasaidia kupunguza gharama za matibabu kwa sababu akishajiunga anaweza kupata matibabu bure “Alisema.

Sambamba na hilo alisema pia hivi sasa wanaihamasisha jamii kuendelea kujiunga nao ikiwemo wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa ili kuweza kunufaika na huduma zinazotolewa na mfuko huo.

“Lakini pia tunaendelea kuhamasisha wakina mama kujiunga na mradi wa KFW mradi ambao unaendelea kwenye mikoa ya Mbeya na Tanga  kwani itawasaidia kupata matibabu pindi wanapokuwa wameugua “Alisema.

Akizungumzia changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo,Meneja huyo alisema ni uelewa mdogo wa wananchi hasa maeneo ya vijijini na katakuchangamkia fursa za mfuko huo.

WANANCHI WAIOMBA SERIKALI KUKAMILISHA DARAJA LA SIBITI

0
0
Wananchi wa kata ya Mpambala, wilaya ya Mkalama mkoani Singida wameiomba Serikali kuhakikisha inamaliza ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti haraka iwezekanavyo ili kurahisisha huduma za mawasiliano kati ya wilaya ya hiyo na mikoa jirani ya Simiyu, Manyara na Mara.

Wananchi hao wamemweleza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, alipofika kukagua daraja hilo mkoani humo jana, ambapo pamoja na mambo mengine wamesema kuwa kukamilika kwa daraja hilo kutatatua changamoto za usafiri hususan katika kipindi cha masika.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), mkoa wa Singida, Eng. Yohanes Mbegalo, akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa kwanza kulia), kuhusu maendeleo yaliyofikiwa ya ujenzi wa Daraja la Sibiti lenye urefu wa M 82 linalounganisha Mikoa ya Singida, Simiyu, Manyara na Mara.

"Tunaomba Mheshimiwa Naibu Waziri utusaidie  kukamilisha daraja hili mapema ili  tupate huduma muhimu kama usafiri hasa kipindi cha masika", amesema mmoja wa wananchi.

Aidha, wananchi hao wameipongeza Serikali kwa kuendelea na jitahada za ujenzi wa barabara za maingilio zenye urefu wa KM 25 katika daraja hilo ambapo kwa sasa mradi wote umefika asilimia 43.9.

Kwa upande wake Naibu Waziri Eng. Ngonyani ameuagiza Uongozi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani humo kuhakikisha kuwa wanamsimamia mkandarasi na kuhakikisha anamaliza ujenzi wa daraja hilo pamoja na barabara hizo kufikia mwezi Machi mwakani.
Mhandisi Mshauri Mr. Sunil Singh, akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kulia), nguzo za Daraja la Sibiti zilizosimamishwa wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa Daraja hilo na barabara za maingilio kwa kiwango cha changarawe KM 25, mkoani Singida jana.

Kuhusu deni la mkandarasi huyo analoidai Serikali, Eng. Ngonyani amesema kuwa watahakikisha wanamlipa mapema ili kufanikisha mradi kumalizika kwa muda uliopangwa.

"Tutahakikisha tunalipa deni lote linalodaiwa ili kurahisisha mradi huu kuisha haraka kwa ajili ya wananchi kuweza kutumia daraja hili pamoja na barabara yake kwa kuwa ni kiungo muhimu kwao", amesisitiza Naibu Waziri.

ANGALIA HAPA SHUGHULI YA KUAGWA KWA MIILI YA WANAFUNZI, WALIMU NA DEREVA WA SHULE YA LUCKY VINCENT-ARUSHA

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA MKWAWA IRINGA WAYAFURAHIA MAFUNZO YA KUWEKEZA KATIKA HISA

0
0
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Jaquiline Materu akizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu cha Mkwawa katika semina elekezi ya umuhimu wa uwekezaji na ununuzi wa hisa za Vodacom Tanzania PLC wakiwa bado wanafunzi,Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki chuoni hapo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Jaquiline Materu akizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu cha Mkwawa.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa Masuala ya Fedha kutoka kampuni ya Orbit Securities Limited,Godfrey Gabriel, akizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu cha Mkwawa juu ya umuhimu wa kuwekeza na ununuzi wa hisa za Vodacom Tanzania katika mafunzo yaliyofanyika chuoni hapo juzi.
Baadhi ya wanachuo wa chuo kikuu kishiriki cha Mkwawa wakisoma vipeperushi vinavuhusu uwekezaji na ununuzi wa hisa za Vodacom Tanzania PLC katika mafunzo yaliyofanyika chuoni hapo mwishoni mwa wiki.
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images