Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1677 | 1678 | (Page 1679) | 1680 | 1681 | .... | 3285 | newer

  0 0  0 0

   Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta  katika picha ya pamoja na viongozi wa UN Habitat na wakuu na wawakilishi wa mataifa mbalimbali katka Mkutano huo. Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Chana ni wa pili kutoka kushoto mbele
  Kutoka kushoto ni Bw. Abilah Hassani Namwambe Afisa Mambo ya Nje kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Chana pamoja na  Bw. Martin Barugahare  Kiongozi kutoka UN Habitat Nairobi.

  0 0  0 0  0 0


  Na Beatrice Lyimo na Fatma Salum-MAELEZO

  MAKAMUwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaongoza maelfu ya Watanzania kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa Shule ya Msingi Lucky Vicent waliofariki kwa ajali ya gari Mei 6 mwaka huu Mkoani Arusha.

  Katika tukio hilo lililofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Makamu wa Rais ametoa salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa Mkuu wa Mkoa, Wazazi na wote walioguswa na msiba huu.

  “Shukrani kwa Rais wa Kenya na Wakenya wote kwa ujumla kwa kujumuika na Watanzania katika kuomboleza msiba huu ulioukumba taifa, ambapo Rais Uhuru Kenyata amemtuma Waziri wa Elimu wa nchi hiyo kuwakilisha Wakenya katika kuomboleza msiba huu” anasema Makamu wa Rais.

  Aidha Makamu wa Rais ametoa wito kwa Wizara ya Elimu, Jeshi la Polisi na wazazi kulinda Sheria za Usalama barabarani ili kulinda maisha na ndoto za watoto.

  “Msiba huu umegusa kila Mtanzania, hivyo tuzidi kuwaombea Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, hivyo tujipe moyo na nguvu kwamba hili limetokea na kwa Mwenyezi Mungu tujirudishe” ameongeza Makamu wa Rais.

  Hata hivyo Makamu wa Rais ametoa wito kwa madereva wa magari mbalimbali kuwa makini na waangalifu katika vyombo vya moto wanavyovitumia.

  Aidha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako ametoa pole kwa wazazi wote waliondokewa na watoto na ndugu zao, wafiwa na watanzania wote walioguswa na msiba huo.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amewapa pole wazazi na wanajumuia wote na kusema kuwa kama kuna kitu kinatuunganisha sote ni kifo kwani kila binadamu ana mwisho wake.

  Naye Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema kuwa Mwenyezi Mungu ametoa nafasi ya kutafakari umoja wetu na ushirikiano wetu kama taifa kupitia msiba huo.

  Vilevile Waziri wa Elimu kutoka nchini Kenya Dkt. Fred Matiang’I amesema kuwa Kenya itaendelea kuwa pamoja na Watanzania kwenye kipindi hiki kizito cha msiba huo mzito ulioukumba taifa.

  Mbali na hayo Rais Dkt. John Magufuli kwenye ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa amepatwa na uchungu na majonzi makubwa alipoyaona majeneza ya watoto na walezi wao waliopoteza maisha katika ajali ya basi huko Arusha.

  “Tumepoteza mashujaa wetu katika elimu, tuwaombee na tuendelee kuwa na subira, uvumilivu na ustahimilivu” amesema Rais Magufuli.

  Wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja wa shule ya Lucky Vicent walipata ajali ya basi Mei 6, mwaka huu Mkoani Arusha walipokuwa wakienda kufanya mtihani wa ujirani mwema.

  0 0

  Ngoma Africa Band inaungana na watanzania wote katika kipindi hiki cha msiba wa wanafunzi, walimu na dereva kilichotokea mkoani Arusha,Tanzania.
  Mungu awalaze pema peponi
   - AMINA

  0 0

   Mshauri wa Taasisi ya Mama’s & Papa’s For Community Reform Rehabilitation Center (MPFCR) Balozi Patrick Chokala akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utoaji wa TUZO kwa baadhi ya watu wenyemkachango katika jamii leo Jijini Dar es Salaam. Tuzo hizo zitatolewa tarehe 12 mwezi huu. Watakaopewa tuzo hizo ni Dkt. Reginald Mengi, Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatale, Mhe. Agustino Lyatonga Mrema, Mustafa Sabodo, na Mohamed Gulam Dewji. Kulia ni Mjumbe wa Taasisi hiyo Omary Kombe.
   Msanii wa muziki wa Bongo Fleva ambaye pia ni Balozi wa Taasisi ya Mama’s & Papa’s For Community Reform Rehabilitation Center (MPFCR), Nurdin Bilal maarufu kama Shetta (baba Kaira) akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu yeye kuwa Balozi wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuunga mkono jitihada za kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya leo Jijini Dar es Salaam.Taasisi hiyo pia imetoa Tuzo za heshima kwa baadhi ya watu wenye mchango katika jamii. Kutoka kulia ni Mshauri wa Taasisi hiyo Balozi Patrick Chokala na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bibi. Emmi Ally Ghahae. 
  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wao na wawakilishi wa Taasisi ya Mama’s & Papa’s For Community Reform Rehabilitation Center (MPFCR) leo jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo inatarajia kutoa Tuzo za heshima kwa baadhi ya wadau wanajali na kuthamini jamii.Watakaopewa tuzo hizo ni Dkt. Reginald Mengi, Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatale, Mhe. Agustino Lyatonga Mrema, Mustafa Sabodo, na Mohamed Gulam Dewji.

  0 0

  a


  0 0

   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Jaquiline Materu akizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu cha Mkwawa katika semina elekezi ya umuhimu wa uwekezaji na ununuzi wa hisa za Vodacom Tanzania PLC wakiwa bado wanafunzi,Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki chuoni hapo.
   Baadhi ya wanachuo wa chuo kikuu kishiriki cha Mkwawa wakisoma vipeperushi vinavuhusu uwekezaji na ununuzi wa hisa za Vodacom Tanzania PLC katika mafunzo yaliyofanyika chuoni hapo mwishoni mwa wiki.
   Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa Masuala ya Fedha  kutoka kampuni ya Orbit Securities Limited,Godfrey Gabriel, akizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu cha Mkwawa juu ya umuhimu wa kuwekeza na ununuzi wa hisa za Vodacom Tanzania katika mafunzo yaliyofanyika chuoni hapo juzi.

   Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa Masuala ya Fedha  wa Orbit Securities Limited,Godfrey Gabriel, akizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu cha Mkwawa juu ya umuhimu wa kuwekeza na kununua hisa za Vodacom Tanzania PLC katika mafunzo yaliyofanyika chuoni hapo juzi mwishoni mwa wiki.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Jaquiline Materu akizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu cha Mkwawa katika semina elekezi ya umuhimu wa uwekezaji na ununuzi wa hisa za Vodacom Tanzania PLC wakiwa bado wanafunzi,Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki chuoni hapo.

  0 0
  0 0


  Mwakilishi wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya GARWARE ya Nchini India  Bwana Kedar Chapekar amesema Zanzibar ina uwezo wa kuwa kituo cha Kimataifa cha Kibiashara kinachofanana na Dubai kutokana na rasilmali ya kimazingira iliyonayo.
  Bwana Kedar alieleza hayo akiambatana na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa  Taasisi inayojishughulisha na Masuala la Sekta ya Elimu ya Arun { U } ltd ya Nchini India Bwana Jatinder Sehgal wakati wakizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
  Viongozi hao wa Taasisi za Uwekezaji za Nchini wapo Zanzibar kwa ziara ya Wiki moja kuangalia fursa mbali mbali za Uwekezaji zilizopo Zanzibar kufuatia mualiko wa Balozi Seif wakati wa ziara yake ya hivi karibuni Nchini India.
  Alisema Zanzibar iko katika mazingira mazuri ya Kibiashara ndani ya mwambao wa Afrika Mashariki pamoja na Ukanda wa Kusini Mashariki mwa Bara la Afrika ambayo bado haijatumika vyema kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
  Bwana Kedar alimueleza Balozi Seif kwamba  Taasisi zao za uwekezaji zimepata fursa nzuri ya kuangalia hali halisi ya kimazingira iliyopo Zanzibar na Uongozi wa Taasisi hizo utaangalia maeneo ambayo wanaweza kuwekeza Visiwani Zanzibar.
  Naye Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa  Taasisi inayojishughulisha na Masuala la Sekta ya Elimu ya Arun { U } ltd ya Nchini India Bwana Jatinder Sehgal alisema upo uwezekano wa Zanzibar kuwa na Ukumbi mkubwa wa Kimataifa unaoweza kutoa huduma za Mikutano ya Kimataifa.
  Bwana Jatinder Sehgal alisema ukumbi huo kwa upande mwengine unaweza kuhamasisha kasi ya uwekezaji ambayo tayari imeshachaguliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa muhimili wa Uchumi wake utakaoweza kusaidia kunyanyua Mapato ya Taifa.
  Akitoa shukrani zake kufuatia ujio wa Ujumbe huo wa Wawekezaji kutoka Nchini India kufuatia ziara yake ya hivi karibu Nchini India Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanziba  imejiwekea malengo ya kuwa kituo na kitovu cha Utalii katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
  Balozi Seif alisema uimarishaji wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar pamoja na miundombinu ya mawasiliani ya bara bara  ni jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuona Sekta hiyo inaanza muelekeo mzuri wa kuimarika Kiuchumi.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alizipongeza Taasisi na Makampuni ya Nchini India yaliyoonyesha nia ya kutaka kuwekeza miradi yao ya Kiuchumi Visiwani Zanzibar katika azma yao ya kuunga mkono jitihada za SMZ za kuimarisha mipango ya Maendeleo.
   Kaimu Balozi wa Tanzania Inchini India Balozi Mohamed  Hija kulia akifafanua jambo wakati wa mazungumzo ya Viongozi wa Kampuni za Kimataifa ya Ujenzi ya GARWARE na Taasisi inayojishughulisha na Masuala la Sekta ya Elimu ya Arun { U } ltd ya Nchini India walipokutana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa  Taasisi inayojishughulisha na Masuala la Sekta ya Elimu ya Arun (U)Ltd. ya Nchini India Bwana Jatinder Sehgal na wa kwanza kushoto ni Balozi Seif.
  Balozi Seif akibadilishana mawazo na Ujumbe huo wa Makampuni na Taasisi za Uwekezaji kutoka Nchini India mara baada ya mazungumzo yao.
  Picha na – OMPR – ZNZ.

  0 0

                      
   WANAKIKUNDI cha upakasaji mikoba, makawa, vipochi vya ukili na upandaji miti cha ‘Subira njema’ kilichopo kijiji cha Changaweni Wilaya ya Mkoani Pemba, ambao wengi wao ni watu wenye ulemavu, wakiwa kazini katika kazi yao hiyo ambapo mkoba mmoja wa kisasa wenye zipu ni shilingi 20,000 hadi shilingi 25,000, (picha na Haji Nassor, Pemba)
  WAJASIRIAMALI kisiwani Pemba, wakiwa na sabuni za michi, nje ya ukumbi wa kiwanda cha mafuta ya Makonyo Wawi Chakechake baada ya kuhitimu mafunzo hayo. Picha na Haji Nassor, Pemba.

  0 0  0 0


  0 0
  0 0

  Je, wajua kwamba Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na ya maingiliano yao na makabila mengine?  Basi kaa chonjo ufahamishwe!
  Kabila la Kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogomadogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia mashariki (Tarakea, Rombo) hadi magharibi kwa Kilimanjaro (Siha, Machame). Makabila ya Kichagga ni Wa-Rombo, Wa-Vunjo ambao wanajumuisha watu wa Mwika, Mamba, Marangu, Kilema na Kirua ambayo ndio inajulikana na wengi kama Kirua Vunjo. 
  Ukipenda unaweza kuwagawa watu hawa wa Vunjo kama Wa-Mwika, Wa-Mamba ,Wa-Marangu,Wa-Kilema,na Wakirua.Makabila mengine ni Wa-Old Moshi, Wa-Kibosho, na Wa-Machame, Wa-Uru, na Wa-Siha. 
  Usipate shida ndugu yangu. Ukitaka kujua mengi zaidi juu ya Wachagga, ama kupanda Mlima Kilimanjaro, ama kutembelea mbuga za wanyama za Kaskazini, tembelea MOSHI ambao unasifika nchini kuwa ni mji msafi kuliko yote. 
  Na unapokuwa hapo fikia EASTPOINT HOTTEL iliyopo kona ya mitaa ya Swahili na Liwali katikati ya mji wa Moshi. Ni hoteli mpya na ya kisasa inayoongoza kwa huduma bora na mandhari nzuri za Mlima Kilimanjaro.  0 0

  Na Pamela Mollel, Arusha .

        Shule ya msingi Sing’isi iliyopo katika wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha iliyokuwa ikikabiliwa  na changamoto ya madarasa kujaa maji imepatiwa msaada wa kiasi cha shilingi Milioni nne na benki ya biashara ya Africa (CBA) kwa ajili ya ukarabati wa baadhi ya madarasa

  Akikabidhi hundi katika shule hiyo juzi Mkurugenzi wa CBA Gifti Shoko alisema kuwa lengo la msaada huo ni kusaidia wanafunzi kuondokana na changamoto ya kutoa maji katika madarasa pindi mvua zinaponyesha hali inayosababisha kukosa vipindi viwili hadi vitatu kwa siku

  Alisema kuwa msaada huo utumike kama ulivyokusudiwa kuboresha madarasa hayo kwani ubora wa elimu unaletwa na mazingira mazuri ya watoto  kusomea  

  ‘’Hapa nawaona Marais, mawaziri wa kesho pamoja na wafanyakazi wazuri wa benki yetu hivyo hatuna budi kutuoa msaada huu ikiwa kama mchango wetu wa kuboresha sekta ya elimu na tunawahidi hatutaishia hapa tutaendelea kuwasaidia kadri ya uwezo wetu ‘’

  Mwalimu mkuu wa shule hiyo Faith Mushiro akitoa neno la shukrani alisema kuwa wanafunzi wa darasa la tano na la sita ndiyo hasa walikuwa wakipata hadha hiyo ya kuondoa maji madarasani pindi mvua zinapoanza kunyesha

  Aidha alisema kuwa zaidi ya vipindi viwili hadi vitatu vya asubuhi hushindwa kuhudhulia kutokana na changamoto hiyo hivyo kupitia msaada huo wanafunzi watasoma katika vyumba  vya madarasa vizuri tofauti na kipindi cha nyuma 

  Awali akisoma Risala mwalimu wa shule hiyo Bw.Simon Mbawala  kwa niaba ya shule hiyo alisema kuwa pamoja na msaada waliopatiwa bado shule inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa makataba ya kuhifadhi vitabu, kuharibika kwa sakafu za madarasa pamoja na kupasuka kwa vioo vya madirisha 

  Hata hivyo tunatoa shukrani zetu za dhati kwa mssada huu wa ujenzi wa vyumba vinne ambayo vilikuwa na tatizo la kuvuja kwa maji kutokana na bati zake kuwa chakavu hali iliyokuwa ikiwathiri sana wanafunzi na walimu hasa ikifika wakati wa kufundisha

   Mkurugenzi wa Benki ya biashara ya Africa (CBA) Gifti Shoko akikabidhi hundi ya kiasi cha shilingi Milioni nne kwa Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Sing’isi iliyopo katika wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha juzi Bi.Faith Mushiro kwaajili ya kukarabati madarasa manne ambayo hujaa maji kipindi cha mvua hali ambayoilikuwa ikiwasababishia wanafunzi kukosa vipindi viwili hadi vitatu kwa siku.
   Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sing'isi Bi.Faith Mushiro akionyesha sehemu ambayo husababisha maji kujaa ndani ya madarasa pindi mvua inaponyesha, wakatikati ni Mkurugenzi wa Benki ya biashara ya Africa(CBA)Gifti Shoko pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Wabunge wa Nkasi, Tabora na Shinyanga wakiwasili tayari kukabidhiwa magari la kubebea wagonjwa waliyopewa msaada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiwakaribisha  Wabunge Mhe Ali Mohamed Kessy (Nkasi Kaskazini)  Mhe. Munde tambwe (viti maalumu - Mkoa wa Tabora) na Mhe Lucy Mayenga (viti maalumu-mkoa wa Shinyanga) kupokea magari ya kubebea wagonjwa waliyopewa saada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akimwangalia Mbunge wa Nkasi Mhe Ali Mohamed Kessy baada ya kumkabidhi gari la kubebea wagonjwa alilopewa msaada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akimwangalia Mbunge wa Viti Maalumu Mhe Lucy Mayenga baada ya kumkabidhi gari la kubebea wagonjwa alilopewa msaada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akimwangalia Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Munde baada ya kumkabidhi gari la kubebea wagonjwa alilopewa msaada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (kati) akiwa na Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Alphayo Kidata (Kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma Ikulu  Bw. Charles Mwankupili (kulia) na  Wabunge Mhe Ali Mohamed Kessy (mbunge wa Nkasi Kaskazini)  Mhe. Munde tambwe na Mhe Lucy Mayenga (wabunge viti maalumu)  baada ya kuwakabidhi magari la kubebea wagonjwa waliyopewa msaada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017.


  PICHA NA IKULU

  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza mamia ya wakazi wa kata ya Mnacho, wilayani Ruangwa kwenye mazishi ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Bw. Daniel Mtawa ambaye alifariki dunia Mei 7, 2017. 

  Akizungumza na waombolezaji katika ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye kijiji cha Nandagala, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi jana (Jumatatu, Mei 8, 2017), Waziri Mkuu alisema msiba uliowapata wana-Mnacho ni mkubwa, na akatumia fursa hiyo kuwapa pole wanafamilia na wanakijiji wenzake.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ruangwa, anatoka katika kijiji cha Nandagala, kwenye kata hiyohiyo ya Mnacho.

  Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kufikisha salamu za rambirambi ambazo zilitolewa na Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Mheshimiwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan. “Mheshimiwa Rais ametoa salamu za pole kwa mke wa marehemu, familia na wana-Ruangwa wote. Pia Mheshimiwa Makamu wa Rais, anawapa pole wana-Ruangwa wote kwa msiba huu mzito,” aliongeza.

  “Ndugu yetu Mtawa amemaliza safari yake na ametangulia mbele ya haki. Tuendelee kumuombea marehemu Mtawa, kila mtu kwa imani yake. Ninatoa pole kwa familia, kwa Mwenyekiti wa Halmashauri na madiwani wenzangu wote,” alisema.

  Akitoa salamu za rambirambi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ruangwa, Bw. Rashid Nakumbya, alisema Bw. Mtawa alikuwa diwani wa kata hiyo tangu mwaka 2015 lakini alianza kupata tatizo la shinikizo la damu Desemba mwaka jana. “Alilazwa katika hospitali ya Nyangao kwa mwezi mmoja, na baadaye akahamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alilazwa kwa miezi miwili kabla ya kupata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani kuendelea na dawa,” alisema.

  Marehemu Mtawa ameacha mjane, watoto saba (wa kiume watano na wa kike wawili) na wajukuu wanane.
  Waziri  Mkuu Kassim  Majaliwa  na Mbunge wa Ruangwa,  akiweka mchanga  kwenye kaburi la aliyekuwa  Diwani wa  CCM Kata ya Mnacho ,Kijij cha Nandagala , Bw.  Daniel Petro  Mtawa ambaye amefariki tarehe   May 7,2017 na kuzikwa  kijijini  kwake  Nandagala  Wilaya ya Ruangwa  Mkoani  Lindi May 8 ,2017. (PICHA NA OWM)
   Waziri Mkuu Kassim  Majaliwa  akitoa salamu za Pole  Katika  Msiba kwa  aliyekuwa Diwani wa  CCM Kata ya Mnacho ,Kijij cha Nandagala , Bw.  Daniel Petro  Mtawa aliyefariki tarehe May 7,2017 na kuzikwa  kijijini  kwake  Nandagala  Wilaya ya Ruangwa  Mkoani  Lindi May 8 ,2017. (PICHA NA OWM)

  Waziri  Mkuu  Kassim  Majaliwa  akiwa ameongozana na  Viongozi  wa Mkoa  wa  Lindi na Mtwara   pamoja na wananchi kuelekea makaburini kwa ajili  ya  mazishi ya aliyekuwa Diwani wa  CCM Kata ya Mnacho, Kijiji cha Nandagala , Bw.  Daniel Petro  Mtawa aliyefariki tarehe May 7,2017 na kuzikwa  kijijini  kwake  Nandagala  Wilaya ya Ruangwa  Mkoani  Lindi May 8,2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego na wa pili kulia, ni Mkuu  wa Mkoa  wa Lindi,  Bw.  Godfrey  Zambi. Kushoto  ni Kaimu   Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa , Bi. Rukia Mhango. (PICHA NA OWM)


  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mhe. Fatma Mohammed Rajab, Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Qatar akiwa katika mazungumzo na Mhe. Sultan bin Saad Al Muraikhi, Waziri wa Nchi, Mambo ya Nje wa Qatar. Mazungumzo hayo yalifanyika baada ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho. Wawili hao walizungumza masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar.
  Balozi Mteule wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma Mohammed Rajab akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Sultan bin Saad Al Muraikhi, Waziri wa Nchi, Mambo ya Nje wa Qatar ofisini kwa Mhe. Waziri. Mhe. Fatma Rajab anakuwa Balozi Mkazi wa kwanza kuiwakilisha Tanzania katika Taifa la Qatar. Mhe. Balozi alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Doha alipokelewa na Idara ya Itifaki ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar. Aidha, wawakilishi wa Watanzania wanaoishi nchini humo walifika Uwanja wa Ndege kumlaki.
  Mhe. Balozi Fatma Mohammed Rajab, akiwa na viongozi wa Watanzania wanaishi nchini Qatar. 

older | 1 | .... | 1677 | 1678 | (Page 1679) | 1680 | 1681 | .... | 3285 | newer