Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1674 | 1675 | (Page 1676) | 1677 | 1678 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 
  Waziri wa nyumba ardhi na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema ataendelea kuwachukulia hatua wale wote ambao watakwenda kinyume cha sheria katika umiliki wa ardhi hapa nchini. 
   Mhe. Lukuvi alitoa kauli hiyo mbele ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akijibu hoja za baadhi ya wajumbe wakati wa mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara ambao walizungumzia changamoto kadhaa katika sekta ya ardhi. 
   “Kuna tatizo sana katika umiliki wa ardhi yetu, hasa haya mashamba makubwa, maana kuna baadhi ya watu wamechukua mashamba makubwa na kwenda kukopa katika mabenki na ukija katika hayo mashamba hakuna ambacho kimewekwa shambani kulingana na mikopo yao.
  "Hivyo sasa sitasita kumchukulia hatua mtu yoyote ambaye atakwenda kinyume na na sheria za ardhi kwa kumnyang’anya hati yake na kuirudisha serikalini” amesema Waziri Lukuvi. Mhe. Lukuvi.
  Pia ameweka wazi kuwa yupo radhi kutoa ardhi yenye hati ndani ya siku moja kwa mtu yoyote anayetaka kuwekeza viwanda hapa nchini na sio wababaishaji ambao wamegeuza ardhi kama mtaji wa kununulia mabasi kwa kukopa kwenye mabenki. 
  Mhe. Lukuvi alimalizia kwa kusema kwa sasa wizara yake imeandaa vitabu ambavyo vinaonyesha watu wote wale ambao wanamiliki ardhi bila ya kufanya shughuli yoyote .

   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akielezea jambo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akielezea jambo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. William Lukuvi akizungumza na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania  Profesa Beno Ndulu
  wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo Ikulu Jijini Dar es Salaam Jumamosi.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 
   WAZIRI Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema Serikali imejipanga katika kuimarisha sekta ya kilimo hili kuimarisha sekta ya Viwanda nchini. 
  Amesema hayo alipokuwa akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyabiashara nchini Ikulu jijini Dar es Salaam Jumamosi wakati akijibu hoja mbalimbali juu ya upatikanaji wa mbolea na malighafi. “Tayari kuna kiwanda cha utengenezaji matrekta hapahapa nchini kinajengwa pale Kibaha (mkoa wa Pwani) hivyo gharama za ununuaji wa matrekta utapungua na yatakuwa yanapatikana kwa urahisi hili kuweza kuboresha kilimo kwa sekta hii ambayo ni tegemeo kubwa katika kuimarisha uchumi wa viwanda” amesema Waziri Mkuu.
  Ameeleza kuwa katika uimarishaji wa uzalishaji mazao mashambani tayari serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha kumpa mzabuni mmoja awe ndio muagizaji mkuu wa mbolea za DAP na UREA hili kuondoa urasimu wa bei kwa wakulima. 
  Ametaja kitendo cha kila wakala kuagiza mwenyewe mbolea kumepelekea bei ya mbolea kutofautiana nchi nzima hali inayochangia katika kuzorota kwa uzalishaji mashamabani kwa mbolea kutofika kwa wakati. 
  Mhe. Majaliwa pia amesema ofisi yake inafanya mapitio upya ya tozo za mbolea ili kuweza kupunguza gharama kwa mkulima kwani aoni haja ya kuwepo kwa tozo mbalimbali kwenye mbolea ambazo zinamkandamiza mkulima moja kwa moja. 
  Amesema kuwa moja ya jitihada zingine za kumsaidia mkulima nchini ni pamoja na ufunguzi wa benki ya kilimo ambayo wakulima wataweza kunufaika na mikopo mbalimbali ambayo itakuwa ikitolewa na benki hiyo. 
   Aidha Waziri Mkuu Majaliwa alitumia fursa hiyo kuwaambia Wafanyabiashra hao kuwa serikali inatambua mchango wa sekta binafsi na ipo pamoja nao na kusema anawashukuru wafanyabiashara hao wanavyotambua kwa jinsi gani serikali ilivyopambana na rushwa katika maeneo mbalimbali ya kazi.
   Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara katika  ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam . Kushoto kwake ni Waziri  
  Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TSPF) Dkt. Reginald Mengi, Rais Dkt John Pombe Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu ) Mhe. Jenista Mhagama

   Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba  Akizungumza katika
  mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara katika  ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam

  Wajumbe  katika mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara katika  ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam

  0 0  0 0

   Unapomuongelea MAKEKE si jina geni kwenye Tasnia ya mitindo nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla. Mwaka jana alikuja na collection ya aina yake iliyoitwa TABID - The African Beauty in The darkness, ( uzuri wa Afrika gizani) collection hio imefanya vizuri sana 2016/2017 kwani imeoneshwa kwenye Majukwaa mbalimbali makubwa ya mitindo. Na mwaka huu mwanamitindo huyu asiyeishiwa MAKEKE amekuja na kitu kipya kabisa, kinachoitwa OTOSIM2017 - ON THE OTHER SIDE OF MAKEKE, akiwa na maana ya ladha/ubunifu  wa aina Nyingine. Kwa Mara ya kwanza OTOSIM imeoneshwa kwenye jukwaa kubwa la ZANZIBAR SWAHILI FESTIVAL  mwezi uliopita na kufanya maajabu makubwa jukwaani. Kwa watu waliokuwepo pale walijionea utamu wa show hiyo  ya Ki - MAKEKE. Msanii huyu wa mitindo ameahidi mambo mengi matamu zaidi kwa mwaka huu 2017. Tuendelee kusubiri.


  0 0

  Na Profesa Mbele
  Leo, mwanahabari na mwanaharakati maarufu Amy Goodman amehutubia chuoni Carleton hapa Northfield. Mada yake ilihusu "threats to freedom of the press and the importance of independent media," yaani mambo yanayotishia uhuru wa vyombo vya habari na umuhimu wa media zisizo chini ya mamlaka yoyote. Ninaamini tafsiri yangu inaweza kuboreshwa.

  Amy Goodman ni maarufu kama mwendesha kipindi kiitwacho Democracy Now!, ambacho kinachambua masuala kwa mtazamo tofauti na ule wa watawala wakandamizi na propaganda zao za kurubuni watu na kuhalalisha hali iliyopo. Mtazamo wa Amy Goodman ni wa kichochezi kwa maslahi ya walalahoi, wavuja jasho, na wale wanaoonewa na kudhulumiwa. Ni mwana harakati ambaye hasiti kujitosa sehemu ambapo watu wanadhulumiwa ili kuwaunga mkono na kuwezesha sauti zao kusikika ulimwenguni.
  Katika mhadhara wake wa leo, ameongelea zaidi hali ya Marekani, akiainisha madhaifu ya vyombo vya habari na media kwa ujumla. Alianza hotuba yake kwa kauli ya kusisimua na kufikirisha ya Thomas Jefferson, "were it left to me to decide whether we should have a government without newspapers or newspapers without a government, I should not hesitate a moment to prefer the latter," yaani "ingekuwa ni mamlaka yangu kuamua kama tuwe na serikali bila magazeti au magazeti bila serikali, nisingesita hata dakika moja kuchagua hilo la pili."

  Baada ya hotuba yake, Amy alisaini nakala za kitabu chake, Democracy Now: Twenty Years of Covering the Movements Changing America. Wakati ananisainia, aliniuliza ninatoka wapi. Nilipomtajia Tanzania, alitabasamu, akasema "Julius Nyerere." Niliguswa, ingawa sikushangaa, kuwa Amy ni mmoja wa watu wa ughaibuni wanaomwenzi Mwalimu Nyerere. 

  0 0


  0 0

  MUS1
  Mfanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Raymond Mushumbusi akiwa pamoja na Mkewe Bi.Susan Barnabas jana wakati walipofunga ndoa takatifu na kuwa mwili mmoja kwenye kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam wakisindikizwa na wasimamizi wao Benedict Mwakasindile na Bi. Leticia Mwakaila . Ndoa hiyo ilifungwa na Padri Padri Haule wa Kanisa hilo.
  MUS2
  Bibi harusi Susan Barnabas na msimamizi wake Leticia Mwakaila wakiwa kwenye gari kabla ya kuingia kanisani tayari kwa tukio la kufungwa kwa ndoa hiyo jana.
  MUS3
  Mfanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Raymond Mushumbusi akimvisha pete Mkewe Susan Barnabas wakati walipofunga ndo katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jana jijini Dar es salaa.
  MUS4
  Mfanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Raymond Mushumbusi akiwa pamoja na Mkewe Susan Barnabas wakishiriki sala wakati wa ibada ya kufungwa kwa ndoa yao jana.
  MUS5
  Padri Haule wa kanisa la Mtakatifu Petro akiziombe pete za maharusi huku maharusi hao wakiwa wamezishikilia.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa amenunua hisa za kampuni ya Vodacom Tanzania PLC zenye thamani ya Tsh. milioni 10 pamoja na nyingine za Tsh. milioni 10 kwa ajili ya mke wake, Mary Majaliwa ili kuwahamisha watanzania kuwekeza katika uchumi unaokuwa kwa kasi.
  Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo Ijumaa, Mei 5, mwaka huu wakati akizungumza na waandishi wa habari mbele ya wakuu wa Masoko ya Hisa na Dhamana; Soko la Hisa la Dar es Salaam, viongozi wa Baraza la Uwezeshaji na kampuni ya Vodacom katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam. 
  Waziri Mkuu amewasihi Watanzania walioko ndani na nje ya nchi wachangamkie fursa ya kununua hisa hizo ili waweze kuwa wamiliki wa kampuni kupitia hisa zao. “Hii ni fursa kwa Watanzania kumiliki kampuni. Ukinunua hisa, unashiriki kikamilifu kumiliki kampuni na pia unaboresha uchumi wako binafsi. Ninawasihi Watanzania wote tumieni fursa hii kununua hisa hizo kabla muda haujaisha ili kuboresha uchumi wetu,” alisisitiza.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alimhakikishia Waziri Mkuu kuwa Vodacom Tanzania itaendelea kuimarisha teknolojia yake ili kuwaunganisha watanzania na kuwezesha kukuza uchumi binafsi. Vodacom Tanzania ilianza kuuza hisa za awali mwezi Machi mwaka huu na mwisho wa kuuza hisa hizo itakuwa ni Mei 11, 2017.
  Makundi mbalimbali ya watu wanaendelea kununua hisa za vodacom kwa ajili ya maisha ya baadae. Uuzwaji wa hisa za awali bado unaendelea hadi tarehe 11/05/2017. Waziri Mkuu kaonesha amechangamkia fursa nasi tusibaki nyuma tuwekeze katika uchumi unaokuwa kwa kasi.  

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  akiongea wakati wa hafla ya ununuzi wa hisa za Vodacom Tanzania PLC iliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ambapo alinunua hisa  zake pamoja na mke wake Mary Majaliwa zenye thamani ya shilingi Milioni 20, wapili kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwekezaji Bi. Beng’i Issa , Mkurugenzi  Mtendaji  wa Vodacom Tanzania  PLC, Bw. Ian Ferrao na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Bi. Rosalynn Mworia.

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  akielekezwa jinsi ya kujaza fomu  za kununua hisa  za Vodacom Tanzania PLC na Mkurugenzi wa wakala wa hisa wa Orbit Securities, Bw. Gerase Kamugisha  (kushoto) wakati alipokuwa akinunua hisa zake na mke wake Mary Majaliwa(hayupo pichani)zenye thamani ya shilingi milioni 20 katika hafla fupi  iliyofanyika ofisini kwake  jijini Dar es Salaam leo.Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwekezaji, Bi.Beng’i Issa  na Mkurugenzi  mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Bw. Ian Ferrao.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akikabidhiwa fomu ya kununua hisa za Vodacom Tanzania PLC   na Mkurugenzi wa wakala wa hisa wa Orbit Securities, Bw. Gerase Kamugisha   wakati wa hafla fupi ya kununua hisa zake na mke wake Mama Mary Majaliwa (hayupo pichani) zenye thamani ya shilingi Milioni 20.Hafla hiyo ilifanyika  ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo,Anaeshuhudia kulia ni Mkurugenzi  Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC,Ian Ferrao.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akipongezwa na Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao  baada ya kununua hisa zake na za mke wake Mary Majaliwa(hayupo pichani) kutoka Vodacom Tanzania PLC kampni hiyo zenye thamani ya Shilingi Milioni 20.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na wadau wakati wa hafla fupi ya ununuzi wa hisa Vodacom Tanzania PLC iliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ambapo alinunua hisa  zenye thamani ya shilingi Milioni 20 pamoja na mke wake  Mama Mary Majaliwa.

  Kwa taarifa zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya (wapili kushoto), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Dk. Juma Malewa (kulia), Mwenyekiti wa  Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, William Mkombozi (kushoto) na Katibu wa Baraza hilo, Amani Mashaka wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima kabla ya Waziri Mwigulu kufungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara kilichojadili Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2016/2017 na malengo ya mwaka 2017/2018, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam jana. Katika hotuba yake, Mwigulu aliwataka wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati mahitaji yao yanapofanyiwa kazi na viongozi wao, pia aliwataka Watendaji wa Wizara hiyo kusimamia haki za wafanyakazi pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali ya kufanya kazi. 
   Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara yake kabla ya kufungua Kikao Baraza hilo kilichojadili Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2016/2017 na malengo ya mwaka 2017/2018, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mwigulu aliwataka Wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati mahitaji yao yanapofanyiwa kazi na viongozi wao, pia aliwataka watendaji wa wizara hiyo kusimamia haki za wafanyakazi pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali ya kufanya kazi. 

   Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akizungumza katika Kikao kilichojadili Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2016/2017 na malengo ya mwaka 2017/2018 cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Naibu Inspekta Jenerali  wa Polisi, Abdulrahman Kaniki na kulia ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga
   Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati waliokaa), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya (wa pili kushoto), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Dk. Juma Malewa (kulia), Mwenyekiti wa  Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, William Mkombozi (kushoto), Katibu wa Baraza hilo, Amani Mashaka  wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza hilo, mara baada ya Waziri Mwigulu kufungua Kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mwigulu aliwataka wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati mahaitaji yao yanapofanyiwa kazi na viongozi wao, pia aliwataka watendaji wa wizara hiyo kusimamia haki za wafanyakazi pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali ya kufanya kazi. 
  Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati waliokaa), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya (wapili kushoto), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Dk. Juma Malewa (kulia), Mwenyekiti wa  Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, William Mkombozi (kushoto), Katibu wa Baraza hilo, Amani Mashaka  wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo, mara baada ya Waziri Mwigulu kufungua Kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mwigulu aliwataka wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati mahitaji yao yanapofanyiwa kazi na viongozi wao, pia aliwataka Watendaji wa Wizara hiyo kusimamia haki za wafanyakazi pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali ya kufanya kazi. 
  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  0 0  0 0


  0 0

  MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) unakusudia kuwafikia wananchi kwenye vijiji na kata mbalimbali mkoani hapa ili kutoa elimu juu ya umuhimu wa huduma ya afya kwa watoto (Toto Afya  Kadi) ambapo uelewa wake umekuwa sio mzuri.

  Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu (Pichani Juu)wakati akizungumza na mtandao huu ofisini kwake ambapo alisema wameamua kufanya hivyo ili kuipa uelewa jamii kuhusiana na umuhimu na faida za huduma hiyo.

  Alisema wakiwa huko watapita kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo mashuleni na kufanya mikutano ya nje kwa wananchi ili kuweza kuwapa uelewa juu manufaa ya kuwaingiza watoto hao kwenye mfuko huo.

  “Unajua hii huduma Toto Afya Kadi hasa kwa maeneo ya vijijini uelewa wake umekuwa sio mzuri hivyo sisi tumepanga kuanza kuhamasisha na kuipa uelewa jamii ili waweze kuitambua na kujiunga nayo “Alisema.

  “Nia kubwa ni kutaka kuona jamii waliochini ya miaka 18 wana jiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwani itawasaidia kupunguza gharama za matibabu kwa sababu akishajiunga anaweza kupata matibabu bure “Alisema.

  Sambamba na hilo alisema pia hivi sasa wanaihamasisha jamii kuendelea kujiunga nao ikiwemo wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa ili kuweza kunufaika na huduma zinazotolewa na mfuko huo.

  “Lakini pia tunaendelea kuhamasisha wakina mama kujiunga na mradi wa KFW mradi ambao unaendelea kwenye mikoa ya Mbeya na Tanga  kwani itawasaidia kupata matibabu pindi wanapokuwa wameugua “Alisema.

  Akizungumzia changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo,Meneja huyo alisema ni uelewa mdogo wa wananchi hasa maeneo ya vijijini na katakuchangamkia fursa za mfuko huo.
  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha 

  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Djibouti Ismail Omar Guelleh ambapo katika mazungumzo hayo viongozi hao wamekubaliana kuanzisha uhusiano na ushirikiano kati ya pande mbili hizo hasa katika sekta za maendeleo na uchumi.

  Viongozi walifanya mazungumzo katika ukumbi wa Ikulu ya Djibouti ambapo Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi na shukurani kwa Rais Guelleh kwa mwaliko wake huo nchini mwake.

  Katika mazungumzo hayo viongozi hao kwa kauli moja walieleza haja ya kuanzisha uhusiano na ushirikiano katika sekta mbali mbali za maendeleo na uchumi kwa manufaa ya pande mbili hizo.

  Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh kwa upande wake alimuhakikishia Dk. Shein kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Zanzibar katika kuimarisha sekta za mawasiliano, utalii, uwekezaji pamoja na usafiri na usafirishaji sambamba na utayari wa kujifunza mambo mbali mbali kutoka Zanzibar ikiwemo sekta ya utalii.

  Rais Guelleh, alieleza kuwa nchi yake inathamini sana uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Tanzania ambao una historia nzuri na kueleza kuwa Djibout iko tayari kujifunza mbinu zilizotumika na Zanzibar katika kuimarisha sekta ya utalii.


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Djbout Mhe.Ismail Omar Guelleh alipofika katika Ikulu ya Djbout leo akiwa katika ziara ya kiserikali na ujumbe wake,Picha na Ikulu.07/05/2017 
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Rais wa Djbout Mhe.Ismail Omar Guelleh alipofika katika Ikulu ya Djbout leo akiwa katika ziara ya kiserikali na ujumbe wake,Picha na Ikulu.07/05/2017 

  0 0  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa Km 45 inayojengwa na Mkandarasi M/S Sinohydro Corporation.

  Akizungumza mkoani Geita jana, mara baada ya kukagua  barabara hiyo ikiwa ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga-Biharamulo KM 112, Naibu Waziri Eng. Ngonyani amemtaka mkandarasi huyo kahakikisha wanamaliza sehemu iliyobakia kwa muda uliopangwa.
  “Nimeridhishwa na kasi yenu, hakika mmepiga hatua sana kwani awali nilipopita kukagua barabara hii haikuwa hivi”, amesema Naibu Waziri Ngonyani.

  Aidha,  Eng. Ngonyani, amewapongeza wasimamizi wa barabara ya Biharamulo – Bwanga kutoka wakala wa barabara nchini (TANROADS) kupitia kitengo chake maalum cha wahandisi washauri wazawa (TECU),  kwa kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi M/S Sinohydro Corporation  kujenga barabara hiyo kwa viwango vilivyomo kwenye mkataba.

  Kwa upande wake, Mhandisi mkazi wa barabara hiyo Eng. Juma Msonge, amemhakikishia Waziri huyo kumaliza barabara hiyo kwa wakati.
  Eng. Msonge ameongeza kuwa kwa sasa mradi huo umefika asilimia 60 ambapo mkandarasi anaendelea na kazi ya kuweka matabaka ya lami ambapo ameshaweka km 30 kati ya 45 zilizopo kwenye barabara hiyo.

  Naibu waziri  Ngonyani, amemaliza ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Geita ambapo pamoja na mambo mengine ametembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akipokea taarifa ya maendeleo kutoka kwa Mhandisi Mkazi Eng. Juma Msonge, kuhusu ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami wakati alipokagua barabara hiyo jana, mkoani Geita

  A
  Mhandisi Mkazi Eng. Juma Msonge, akitoa taarifa ya maendeleo yaliyofikiwa ya ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami jana, mkoani Geita kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani.
  A 1
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akitoa maelekezo kwa Mhadisi Mkazi Eng. Juma Msonge, baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami jana, mkoani Geita.
  A 2
  Sehemu ya barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami na Mkandarasi Synohdro, mkoani Geita. Hadi sasa ujenzi wake umefikia asilimia 60.
  A 3
  Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Geita, Eng. Harun Senkuku, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, ambae alikuwa mkoani humo kwa ajili ya kukagua miradi inayotekelezwa na Wizara yake

  0 0

  Watanzania wenzangu,  ninaungana na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, pamoja na Mheshimiwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kutoa pole nyingi sana kwa uongozi wa shule ya Lucky Vicent pamoja na wazazi wa watoto waliopoteza maisha kwenye ajali ya jana. 

  Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Tunamuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. 
  Amina. 

  Mhe. Kassim Majaliwa (MB.)
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  0 0

  Na Othman Khamis Ame, OMPR
  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa mkono  wa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Mrisho Gambo kutokana na vifo vya Wafanuzi 32, Walimu pamoja na Dereva  wa Skuli ya Mchepuo wa Kingereza ya Luck Vicent kufuatia  Basi walilokuwa wakisafiria kupinduka katika Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.
  Salamu hizo za pole zimetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein na Wananchi wote wa Zanzibar kufuatia msiba huo mzito kwa Taifa.

  Balozi Seif Ali Iddi alisema Wananchi wa Zanzibar wamepokea kwa huzuni, masikitiko na mshtuko mkubwa taarifa ya ajali hiyo iliyotokea katika Kijiji cha Rhotia, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha na kusababisha  vifo hivyo pamoja na Majeruhi kadhaa.
  Alisema huo ni msiba mkubwa siyo tu kwa Wazazi, Ndugu na Jamaa wa Watoto hao bali pia ni kwa Taifa zima, kwani Watoto hao walikuwa nguvu kazi kubwa iliyotumainiwa kuja kulitumikia Taifa laWatanzania baada ya kumaliza Masomo yao.
  Balozi Seif  alimuomba Mwenyezi Mungu awape wazazi na familia za Watoto hao moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hichi kigumu cha msiba na Wananchi wote Nchini Tanzania wako pamoja katika msiba huo.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia alimuomba Mwenyezi Muungu mola wa viumbe wote azilaze roho za marehemu wote mahali pema pepono amin na wale majeruhi awaponyeshe haraka ili warudi kuendelea na maisha yao ya kila siku.

  0 0  0 0
 • 05/07/17--13:32: Article 15


 • 0 0

  images
  Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) umepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu 36 ambao ni wanafunzi 33, walimu wawili na dereva wa gari la shule ya msingi Lucky Vicent ya Arusha vilivyotokea jana tarehe 6 Mei 2017 katika ajali ya gari katika eneo la Rhotia Marera Wilayani Karatu, Arusha.
  Katibu Mkuu wa UWT Ndg Amina Makilagi ametoa salamu za pole na rambi rambi kwa familia, wazazi, ndugu na walezi waliopoteza wapendwa wao hasa watoto wadogo waliokuwa wakilelewa kuwa raia wema na nguvu kazi bora ya Taifa letu hapo baadae. Katika salamu zake Ndg Makilagi amesema UWT inaungana na wanawake, wazazi na waombolezaji wote nchini kuwaombea majeruhi kupona haraka na kumuomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahala pema peponi. Amina 
  Imetolewa na:- 

  AMINA MAKILAGI
  KATIBU MKUU WA UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA 
  07/05/2017.

older | 1 | .... | 1674 | 1675 | (Page 1676) | 1677 | 1678 | .... | 3278 | newer