Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1673 | 1674 | (Page 1675) | 1676 | 1677 | .... | 3272 | newer

  0 0  0 0
 • 05/06/17--08:49: YANGA YAIPIGA PRISONS 2-0
 •  Wachezaji wa Yanga wakishangilia ushindi wa bao la pili dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo. (PICHA NA KHAMISI MUSSA)
   Mchezaji wa Yanga, Geofrey Mwashiuya (kulia), akigombea mpira na Nurdin Chona katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam . Yanga ilishinda mabao 2-0.


  Wanayanga wakishangilia ushindi


  0 0

  EFM redio kwa mara nyingine imehitimisha shindano la shika ndinga leo siku ya Jumamosi ya tarehe 6/5/2017 katika viwanja vya Tanganyika Packers - Kawe Jijini Dar es salaam ambapo washindi wawili wameondoka na magari aina ya Suzuki Carry maarufu kama Kirikuu ikiwa mmoja ni wa kiume na mwingine wa kike. 
  Shindano hili lilianza tarehe 25/03/2017 ambapo lilifanyika katika wilaya 6 ambazo ni Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala, Bagamoyo na kibaha ambapo washindi wawili kutoka katika kila wilaya walizawadiwa Pikipiki kila mmoja aina ya Sanmoto. 
  Efm redio kupitia shindano hili kwa ujumla limetoa pikipiki 12 pamoja na magari mawili ambayo hutumika katika shughuli za kiuchumi ikiwa kama njia ya kuwawezesha washindi kujiongezea kipato chao na kufanya maisha yao kukua kiuchumi.
   Burudani kutoka kwa Man Fongo, Sholo Mwamba, Madada 6, Virus, Yuda Msaliti na Chemical.
   Umati wa watu wakishuhudia shindano zima na burudani iliyoandaliwa na kituo cha E fm radio.

   Micheal Peter mshindi wa gari kwa upande wa wanaume akikabidhiwa mkataba na funguo wa gari lake na Bw Suleima Malele mkurugenzi wa uchumi na utawala alie mwakilisha Bi. Being’I Isaa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC)

  Joyce Daniel mshindi wa Gari aina ya Suzuki Caryy aka Kirikuu kwa upande wa wanawake.
  Washindi kutoka wilaya ya Kigamboni, Temeke, Kinondoni, Ilala ,Kibaha na Bagamoyo wakiwa kwenye Pikipiki 12 aina ya San moto ambazo walikabidhiwa.

  0 0

  Na Dotto Mwaibale
  VILIO na majonzi vilitawala wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa mwanahabari Revocatus Bulizya wa Kituo cha Televisheni cha Star TV wakati wa ibada ya kumuaga iliyofanyika Kanisa Katoliki la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam leo asubuhi.
  Ibada hiyo ilihudhuriwa na ndugu jamaa na marafiki wa marehemu pamoja na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali akiwepo aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam toka mwaka 2010/2015, Shelymar Kweygia ambaye ni ndugu ya mke wa Bulizya.
  Akitoa mahubiri wakati wa ibada hiyo Katekista wa Paroko ya Kanisa Katoliki MNH, alisema ni wakati wa kila mmoja wetu kutafakari juu ya maisha yake ya kimungu.
  Alisema hakuna njia ya kukutana na mungu bila ya kifo na ndio maana wakati wote tunatakiwa kujiandaa kwa sababu hatui ni lina tutatoweka duniani kama alivyotuacha ndugu yetu Revocatus Bulizya.
  Recocatus Bulizya alzaliwa tarehe 29-10-1979 na kufariki dunia tarehe 2-5-2017 kwa kugongwa na pikipiki 'bodaboda' maeneo ya Pugu jijini Dar es Salaam wakati akirejea nyumbani kwake akiwa ameongoza na mke wake.
  Mazishi ya marehemu yamefanyika Mwandege Kongowe Barabara ya Kilwa nje kidogo ya jijini Dar es Salaam na mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu.
  Marehemu Revocatus Bulizya enzi za uhai wake
  Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mwanahabari Revocatus Bulizya wakati ukiingizwa katika Kanisa la Katoliki Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya ibada ya kuuaga kabla ya kwenda kwenye mazishi yaliyofanyika Mwandege Kongowe Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
  Mjane wa marehemu na mtoto wao (katikati), akisaidiwa na dada yake aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam toka mwaka 2010/2015, Shelymar Kweygia kuingia katika kanisa hilo kwa ajili ya ibada ya kuuaga mwili huo.


  Jeneza likiingizwa kanisani.

  Waombolezaji wakiwa katika ibada ya kuuaga mwili katika Kanisa Katoliki la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam leo asubuhi.

  0 0

   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiagana na Viongozi wa Serikali na Wazee wa CCM uwanja wa Ndege wa Kimataifa Zanzibar akielekea Nchini Djibout kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiagana na Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akielekea Nchini Djibout kwa ziara ya kiserikali.
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiteta jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kabla ya kuaza safari yake Nchini Djibout kwa ziara ya kiserikali.(Picha na Ikulu)  


  0 0

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeeleza kuwa nafasi za Wabunge wa Viti Maalum wanaoteuliwa zipo kwa mujibu wa Sheria na zimeainishwa katika  Ibara ya 78 (1) na (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
  Akitoa ufafanuzi huo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani amesema kuwa Ibara ya 78 (1) na (4) ya Katiba inaeleza utaratibu mzima wa kuwapata Wabunge wanawake wa Viti maalum.
  Amesema  kila Chama cha Siasa kinachoshiriki katika Uchaguzi Mkuu na kupata angalau asilimia 5 ya Kura zote halali za wabunge kitapata Wabunge wa Viti Maalum kulingana na Kura ambazo chama husika kimepata. 

  Amefafanua kuwa Chama kinachopata asilimia 5 ya Kura zote halali za Wabunge katika Uchaguzi Mkuu kinatakiwa kuwasilisha orodha ya wanachama wanaopendekezwa kuwa wagombea wa Viti Maalum ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
  Aidha, ameeleza kuwa endapo inatokea nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na sababu mbalimbali, Spika wa Bunge humtaarifu Mwenyekiti wa Tume juu ya uwepo wa nafasi hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.
  Amesema kuwa  Mwenyekiti wa Tume hukiandikia barua chama husika kukitaarifu juu ya uwepo wa nafasi wazi ya viti maalum ili kiweze kuwasilisha pendekezo la jina katika orodha kiliyowasilishwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwaka 2015,  ikiambatanishwa na Fomu namba 8 D ya kuomba jina lililopendekezwa  liteuliwe na Tume katika nafasi ya Ubunge kulingana na sifa zilizoainishwa kwa mujibu wa Sheria.  0 0  0 0  0 0


  Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU e.V unapenda kuwaalika watanzania wote wanaoishi Ujerumani (TANZANIA DIASPORA) kwenye mkutano mkuu wa umoja wetu 2017. Mkutano wetu mkuu utafanyika Siku ya Jumamosi, terehe 13.05.17 saa 13:00 Mchana  katika Address ifuatayo:
  Bob's Cafe,
  Altendorfer Straße 375
  45143 Essen
  Ili kufanikisha mkutano wetu tunawaomba Watanzania kufika kwa wingi mno, mkutano huu ni muhimu sana kwani  kuhudhuria kwenu ndio mafanikio ya umoja wetu na mafanikio yako wewe mtanzania unayeishi hapa ujerumani . Umoja wa Tanzania Ujerumani ( UTUe.V) ‘’Ndio mwavuli  na Sauti ya Watanzania Ujerumani’’

  0 0


  0 0

   Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na viongozi wa CCM na Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, katika Ofisi ya CCM mkoa huo, mwanzoni mwa ziara yake, kukagua uhai wa chama na mwenendo wa mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa CCM. Waliokaa kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe na Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa  huo, Lugano Mwafongo
  Wanachama wakiwa ukumbini
  Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mAlhaj Abdallah Bulembo akizungumza na viongozi wa Jumuia ya Wazazi kwenye kikao hicho

  Wanachama wa CCM ambao ni kutoka Jumuia ya Wazazi wakishangilia wakati wa kikao hicho
  Katibu wa CCM wilaya ya Ilala akikabidhi taarifa ya mchakato wa uchaguzi katika maeneombalimbali wilayani humo kwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo.


  0 0

  Daktari bingwa wa pua na masikio kutoka China Dk. Fei Jie, akimfanyia uchunguzi wa pua Bi. Amina Himid katika siku ya Afya ya kijiji iliyofanyika Skuli ya Kwamtipura. 
   Wananchi waliojitikeza kupatiwa huduma katika siku ya Afya ya Kijiji huko Skuli ya Kwamtipura.
  Watoto wakinywa Uji mara baada ya kupatiwa huduma za afya.
   Wananchi waliojitikeza kupatiwa huduma katika siku ya Afya ya Kijiji huko Skuli ya Kwamtipura.
  Daktari bingwa kutoka Jamhuri ya Watu wa China Dk. Gao, akimpima kifua mtoto Salma Mohammed mkaazi wa Kilmahewa, katika siku ya Afya ya Kijiji iliyofanyika Skuli ya Kwamtipura Wilaya ya Mjini Unguja.

  0 0


  0 0
  0 0

   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk .Ali Mohamed Shein, akisalimiana wafanyakazi wa Ofisi  ya Ubalozi wa Ethiopia mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nchini Humo akiwa na Ujumbe wake akielekea Nchini Djibout kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Brigedier General Bishoge mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nchini humo akiwa na Ujumbe wake akielekea Nchini Djibout kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu,(katikati ) Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifuatana na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Brigedier  General Bishoge mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nchini humo akiwa na Ujumbe wake akielekea Nchini Djibout kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu,(katikati ) Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifuatana na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Brigedier General Bishoge mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa nchini humo akiwa na Ujumbe wake akielekea Nchini Djibout kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu,(katikati ) Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein. Picha na Ikulu

  0 0  Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Singida Rashid Mandoa ameagizwa kuhakikisha ofisi za halmashauri hiyo zinahamia ndani ya eneo la halmashauri hiyo na kutoka walipo sasa katika manispaa ya Singida. 

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ametoa agizo hilo jana wakati akikabithi vyeti kwa madiwani wa halmashauri ya Singida walipohitimu mafunzo kuhusu jitihada za jamii kupitia mbinu shirikishi ya fursa na vikwazo kwa maendeleo iliyoboreshwa na usimamizi wa miradi ya maendeleo.
  Dkt. Nchimbi amesema endapo mkurugenzi atahamishia ofisi na watendaji katika halmashauri yake watapata ubunifu wa kutatua shida na kero za wananchi na hivyo kuiendeleza halmashauri.
  “Ukikaa kwenye nyumba inayovuja ndipo utapata akili na ubunifu wa kutatua changamoto hiyo, ukiangaia wanufaika wa Tasaf wameweza kufanya mambo mazuri kwa pesa kidog waliyonayo, mkurugenzi uige mfano huo, mhamie katika halmasahuri yenu, wananchi hawafurahii kuwaona ninyi na watendaji wengine mkiishi manispaa” amesisitiza Dkt. Nchimbi.

  Ameongeza kuwa kusitasita kwao kutohamia katika halmashauri yao kutasababisha halmasahuri hiyo ikavunjwa na hivyo kukosa ajira kwa watumishi huku akiwaeleza madiwani kuwa wataponzwa wa kukosa kura katika uchaguzi ujao kwani wananchi wangependa kupata huduma kwa ukaribu.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akisisitiza jambo katika baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Singida. 
  Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Singida wakifuatilia kikao cha baraza hilo. 
  Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Singida Rashid Mandoa (katikati) akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (kulia kwake) na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Singida Eliya Digha. 
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akitunuku cheti kwa mmoja wa madiwani waliohitimu mafunzo ya jitihada za jamii kupitia mbinu shirikishi ya fursa na vikwazo kwa maendeleo iliyoboreshwa na usimamizi wa miradi ya maendeleo. 

  0 0


  0 0


  0 0  0 0older | 1 | .... | 1673 | 1674 | (Page 1675) | 1676 | 1677 | .... | 3272 | newer