Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

Mawaziri Wastaafu Wakutana

$
0
0
Leo Prof. Mark Mwandosya, aliyekuwa Kamisha, Katibu Mkuu, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Waziri wa Nchi(Mazingira), Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Waziri wa Nchi(Ofisi ya Rais-Kazi Maalum) amemtembelea Mhe. Stephen Masato Wasira nyumbani kwake Mbweni, Dar es Salaam kumjulia hali na kubadilishana uzoefu. Mheshimiwa Wasira ni mmoja ya wanasiasa wa siku nyingi nchini. Amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa, Naibu Waziri, Waziri wa Wizara mbalimbali, akimalizia kama Waziri wa Nchi(Ofisi ya Rais) na hatimaye Waziri wa Kilimo.

SUZA and China's Southwest University (SWU) join hands in educational related issues

$
0
0

 The State University of Zanzibar (SUZA) and Southwest University (SWU) of Chongqing, China have on Thursday 4th May, 2017 established a tie up intended to maintain friendship for the purpose of promoting mutual understanding and academic, cultural and educational cooperation based upon the principle of reciprocity, agree to work together towards the internationalization of higher education. 
On academic arena, the partnership will focus on the programmes offered by the institutions which are felt desirable and feasible for the development and strengthening of cooperative relationships between them. 
The five members SWU delegation led by Prof. Liu Meng, the Party Secretary and Deputy Dean of International College met their host Prof. Idris Rai, the SUZA Vice Chancellor at Tunguu Campus where their conversation was held.

 In the memorandum of understanding prepared by the institutions, SUZA and SWU have reached agreement to cooperate in research, exchange of students, short-term academic programmes, invitation for participation in academic conferences and seminars and other educational endeavours. 
The memorandum will enter into force from the date of its signature and will remain valid for a period of five (5) years and is extendable after its termination upon mutual consent of the parties. 

Southwest University (SWU) is a key comprehensive university, under the direct administration of the Ministry of Education of the People’s Republic of China. It was newly established in July 2005 through the incorporation of former Southwest China Normal University and Southwest Agricultural University upon the approval of the Ministry of Education. SWU is situated nearby the beautiful Jialing River, and is located at the foot of Jinyun Mountain, a state level scenic spot, in Beibei District, Chongqing Municipality. 

Zulfiqar Manzi at it, again - Dating App for Ugly People...

MAMA SAMIA AWATAKA WAKUNGA KUFANYA KAZI KWA BIDII

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameziagiza Halmashauri zote nchini zihakikishe zinajenga nyumba kwa ajili ya watumishi wa afya hasa maeneo ya vijijini na kipaumbele kitolewe kwa wakunga ambao mara nyingi ndio wanatoa huduma za dharura kwa wanawake wajawazito na watoto.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo mjini Dodoma katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani sherehe ambazo zimehudhuriwa na Mamia ya wakunga kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Makamu wa Rais amesema kuwa halmashauri zikijenga nyumba karibu na vituo vya kutolewa huduma za afya zitasaidia kupunguza matatizo ya mama na watoto wanaotaka kupata huduma za dharura ikilinganishwa na hali ilivyo sasa ambapo baadhi ya watumishi wa afya hasa wakunga wanakaa mbali na maeneo yao ya kazi hivyo utoaji wa huduma za dharura kuwa duni.

Makamu wa Rais amewahimiza Wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia ujenzi huo kikamilifu kama walivyoshughulikia matatizo ya madawati katika maeneo yao ili kuhakikisha Taifa linafikia malengo yake ya kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na uzazi nchini.

Kuhusu changamoto zinazoikabili sekta ya afya nchini, Makamu wa Rais amewahakikishia wakunga na watumishi wengine wa sekta ya afya nchini kuwa Serikali inaendelea kufanyia kazi changamoto hizo ikiwemo uboreshaji wa maslahi kwa watumishi wa kada hiyo pamoja na kuongeza maradufu vifaa tiba,dawa na vitendanishi ili kuhakikisha wananchi kote nchini wanapata huduma bora za afya.

BOFYA HAPA KWA HABARI ZAIDI


NA

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia kwenye kilele cha siku ya Wakunga Duniani ambapo Kitaifa imefanyika mjini Dodoma. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Samia akihutubia Wakunga kwenye kilele cha Sherehe za Siku ya Wakunga Duniani iliyofanyika Kitaifa mkoani Dodoma kwenye ukumbi wa Julius K. Nyerere Chuo cha Mipango.
Wakunga wakirekodi hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa sherehe za Siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa zimefanyika mjini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akihutubia Wakunga waliojitokeza kwa wingi kwenye kilele cha Siku ya Wakunga Duniani ambayo Kitaifa imefanyika mkoani Dodoma na mgeni rasmi ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Zulia Jekundu S1 Ep 122: Ciara Wilson, Met Gala, Keith Holland, David Adjaye ,na Gifte Ngoepe

Dr. Ntuyabaliwe Foundation yahimiza wanafunzi kusoma vitabu

$
0
0
Wananafunzi wa Shule za Msingi jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla, wametakiwa kujenga utamaduni wa kupenda kusoma vitabu vikiwemo vya kiada na ziada, ili waweze kupanua wigo wa uelewa wa mambo mbalimbali.
 
 Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi, alipozungumza na wanafunzi, walimu na wajumbe ya Kamati ya Shule ya Msingi Makumbusho, wakati akizindua maktaba iliyokarabatiwa na mfuko huo. Amesema upo umuhimu mkubwa kwa wanafunzi kusoma vitabu vya kielimu, historia na pia hadithi.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi katika picha na walimu pamoja na wajumbe wa kamati shule
 Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la maktaba katika shule ya msingi Makumbusho jana jijini Dar es Salaam.(Picha zote na thebeauty.co.tz).
 
 Awali Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo, alitoa shukrani kwa Dr. Ntuyabaliwe Foundation kwa mchango wake wa vitabu kwa ajili ya maktaba hiyo, na kuomba kupatiwa mtaalam wa kutunza maktaba, ikiwezekana mwalimu mmoja akasomeshwe taaluma hiyo. Naye Afisa Taaluma Fatma Mwiru akimwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni, amewataka waalimu kuwasaidia wanafunzi kupata vitabu mbalimbali, kwa kuwashirikisha wadau wa elimu, wachapishaji vitabu pamoja na wahisani. Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akizungumza alipokuwa akimkaribisha Mama Jacqueline Mengi.[/caption] Aidha Mama Jaqueline Mengi amesema Dr. Ntuyabaliwe Foundation ilianzishwa mwaka jana ikiwa na lengo la kuchangia katika sekta ya elimu, ambapo iligundua shule nyingi za msingi zinakabiliwa na uhaba wa maktaba na vitabu. Shule ya Msingi Makumbusho inakuwa ya shule ya pili katika wilaya ya Kinondoni na ya kwanza katika kata ya Makumbusho, kusaidiwa ujenzi wa maktaba na msaada wa vitabu na Dr. Ntuyabaliwe Foundation, ikitanguliwa na Shule ya Msingi Hananasifu. Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi pamoja na Afisa Taaluma Fatuma Mwiru, aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la maktaba hiyo.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akifurahi na kuimba na wanafunzi wa shule ya msingi Makumbusho baada ya kukamilika kwa shughuli ya uzinduzi wa maktaba shuleni hapo. 

WAZIRI MWAKYEMBE AMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI KAMA UTAMBULISHO WA KITAIFA

SAFARI ZA ATCL MKOANI TABORA ZAZINDULIWA RASMI

$
0
0
Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), imeanzisha safari zake kutoka Tabora kwenda mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam kwa lengo la kurahisisha huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo katika mikoa hiyo na mikoa jirani. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za kampuni hiyo mkoani Tabora, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, amesema kuwa kuanzishwa kwa safari hizo katika mikoa hiyo kutatanua wigo wa kibiashara na kukuza uchumi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo za utalii na kilimo.

“Naamini wananchi wa mkoa wa Tabora na mikoa ya jirani, sasa mtanufaika kwa ujio wa ndege hii, matumaini yangu kwamba mtatumia usafiri huu ambao hautumii muda mrefu katika kurahisisha shughuli zenu za kibiashara na kijamii”, amesema Eng. Ngonyani.

Aidha, Naibu Waziri Ngonyani amewataka wananchi wa mkoa wa Tabora kutumia fursa ya ujio wa ndege hiyo kama chachu ya kuleta maendeleo katika mkoa huo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri, wakikata keki kama ishara ya kuzindua rasmi safari za Ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), mkoani humo. 
Baadhi ya viongozi na wabunge wakiingia kwenye ndege aina ya Bombardier Dash 8 Q400 ya Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), iliyotua kwa mara ya kwanza mkoani Tabora katika uzinduzi wa safari za ndege mkoani humo. 

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho, wakiwa ndani ya ndege kuelekea katika uzinduzi wa safari za ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), mkoani Tabora. 


SINGIDA INAZALISHA NUSU YA ASALI YOTE INAYOZALISHWA NCHINI; WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA AELEZA.

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda Mkoa wa Singida kwa kuzalisha nusu ya asali yote inayopatikana nchini Tanzania. 

Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda ametoa pongezi hizo wakati akifunga mafunzo ya ufugaji nyuki kibiashara wa kikundi cha wafugaji nyuki wa kijiji cha Kisaki Manispaa ya Singida ambapo aliwatunuku vijana 23 vyeti vya mafunzo hayo.

Amesema Singida imekuwa ikizalisha tani elfu 17 kwa mwaka huku uzalishaji kwa nchi nzima ukiwa ni tani elfu 34 kwa mwaka hivyo basi wananchi watumie fursa ya hiyo kuzalisha asali bora ili ipate soko la kimataifa.

Mheshimiwa Pinda amesema asali ina faida kubwa kwakuwa imekuwa ikitumika kama chakulana pia dawa huku akiongeza kuwa baadhi ya wazalishaji wameweza kutumia nta kuzalisha mshumaa na gundi ijapokuwa bado si kwa kiwango cha kutoshelesha hata soko la ndani.

Ameongeza kuwa kuwa wananchi watumie fursa ya nchi ya Tanzania kuwa na misitu hekta milioni 35 kufuga nyuki kwa wingi ili misitu hiyo iwezwe kutunzwa huku ikiwafaidisha kwa kuvuna asali na mazao yake.
 
 Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akizindua kikundi cha wazalishaji nyuki cha Kisaki katika manispaa ya Singida. 

Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akiwa anatazama asali inayozalishwa na kikundi cha wazalishaji nyuki Kisaki, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa kikundi hicho Philemon Kiemi.  

Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akimpongeza Jacob Edward Mashimba kwa kuhitimu mafunzo ya ufugaji nyuki kibiashara kabla ya kumtunuku cheti cha mafunzo hayo. 
Eneo la kikundi cha wafugaji nyuki kibiashara likiwa na mizinga ya nyuki ya  kutosha katika kijiji cha Kisaki, Manispaa ya Singida. Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akipata maelezo ya ukamuaji na upakiaji wa asali kisasa kutoka kwa Mkurugenzi wa kikundi cha uzalishaji nyuki Philemon Kiemi. 

ISEMAVYO SHERIA YA MIPANGO MIJI NA. 8 YA MWAKA 2007

$
0
0
Prof. John Lupala, Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewataka wanachi kuzingatia Sheria Na. 8 ya mwaka 2007 kuepuka adha zinazotokana na kutozingatia sheria hiyo.

Akitoa ufafanuzi wa Sheria ya Mipango Miji, namba 8 ya mwaka 2007; Prof. Lupala alisema; Sheria imetungwa ili kutoa muongozo namna ya kupanga miji nchini. Prof. Lupala amefafanua maeneo matatu ya Mipango katika sheria hiyo. 

Mipango Kabambe/ General Planning; Mipango ambayo huandaliwa kuongoza ukuaji wa miji kwa muda wa miaka 20. Ambapo sheria inasisitiza ushiriki wa maoni ya Wananchi.

Mipango Kina; Mgawanyo wa viwanja au shamba unaofanywa katika eneo fulani, hutakiwa kuandaliwa kulingana na taratibu za viwango vya upangaji ndani ya miji, alieleza hata kama mpangaji binafsi anatumika ni lazima viwango vya kisheria vizingatiwe.

Urasimishaji; Unalenga kutambua miliki za watu, kutengeneza viwanja vya milki za maeneo yao na kupangilia miji kwa kuweka huduma za msingi au miundombinu ya msingi kama; maji, barabara n.k.

Pro.Lupala alisema iwapo mwananchi hatazingatia taratibu za uendelezaji Miji bila kupata kibali cha ujenzi, Mamlaka za Miji huchukua hatua kwa Kusimamisha ujenzi au kubomoa.

Wananchi hawana budi kushiriki katika maoni wakati wa upangaji miji na kutojenga katika maeneo hatarishi, ya hifadhi au oevu.


Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Prof. John Lupala akitoa ufafanuzi wa Sheria ya Mipango Miji, Na. 8 ya Mwaka 2017.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MAY 6, 2017

TFF, WILDAID WASAINI MAKUBALIANO KUPIGA VITA UJANGILI

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Taasisi ya kupigania uhai wa maisha ya wanyama wa mbugani ya Wildaid Alhamisi Mei 4, mwaka huu kwa pamoja wamesaini makubaliano ya vita dhidi ya ujangili. Makubaliano hayo yalisainiwa jijini Dar es Salaam kati ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Mwakilishi wa taasisi hiyo, Lily Massa.

Akizungumza kabla ya kusaini makubaliano hayo, Rais wa TFF Jamal Malinzi alisema kwamba, “Hii ni sehemu nyingine ya TFF kujihusisha na shughuli za kijamii licha ya kuwa na majukumu ya kusimamia maendeleo ya mpira wa miguu katika kukuza na kuendesha mashindano.”

Malinzi amesema TFF inaendeleza utamaduni wa shughuli mbalimbali za jamii kwani hata kwa Rais wa Heshima wa TFF, Leodegar Tenga enzi za utawala wake akiwa kiongozi mkuu wa mpira wa miguu, alifanya hivyo katika kampeni za kupinga maambukizi mapya ya UKIMWI.

“Wengi mtakumbuka kuwa kulikuwa pia na vita vya kupigania afya za watoto na kupigania uhai wao pia kampeni za amani ambazo mpira wa miguu umetumika kuelimisha,” amesema.

Kwa hatua hii ya sasa, Rais Malinzi amesema kwamba TFF, inaingia makubaliano hayo na kuiteua timu ya taifa ya vijana Tanzania maarufu kama Serengeti Boys kusimama kidete kupinga uwindaji haramu wa wanyama mbugani kwa kuwa ni hazina kubwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Kwa upande wa Mwakilishi wa WildAid, Lily Massa, alishukuru kuingia kwa makubalino hayo akisema kwamba ndoto zao za kupiga vita uwindaji haramu na ujangili, itafanikiwa.

“Tunashukuru kuingia programu hii na ninaamini Mungu atatusaidia,” amesema Massa ambaye taasisi yake iko karibu kila nchi yenye wanyama wa mbugani.

Katika hatua nyingine, Rais Malinzi aliitakia kila la kheri Serengeti Boys ambayo kwa sasa inajiandaa kuingia Gabon kwa ajili ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika. Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Mei 14, mwaka huu ambako Serengeti Boys ambayo iko Kundi B itakuwa Libreville - Mji Mkuu wa Gabon. Timu nyingine za Kundi B ni Mali, Niger na Angola.

BREAKING NYUZZZZZZ....: WANAFUNZI ZAIDI YA 20 NA WALIMU WAO WADAIWA KUPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA GARI WILAYANI KARATU LEO

$
0
0
Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde, inaeleza kuwa kuna ajali imetokea muda huu katika eneo la Rhotia Wilaya ya  Karatu Mkoani Manyara, iliyohusisha Basi lililokuwa limebeba wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St Lucky ya jijini Arusha, inayodaiwa kuwa ilipoteza mueleo na kupinduka wakati wakiwa safarini kuelekea Karatu waliokuwa wakienda kufanya mitihani na wanafunzi wenzao wa Shule ya Tumaini English Medium ya Karatu. Inadaiwa kuwa wanafunzi zaidi ya 20 na walimu wao wamepoteza maisha huku wengine wakiwa wamejeruhiwa. jitihada za kumtafunda Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara zinaendea ili kupata kauli yake juu ya ajali hii. Pichani ni baadhi ya wasamalia wakitoa msaada wa uokozi kwa wanafunzi hao.
Zoezi la uokoaji kwa wanafunzi hao likiendelea. 

TTCL KUZIMA TEKNOLOJIA YA CDMA

INTRODUCING: Linah & Mr kesho - Upweke


RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA NCHINI, IKULU JIJINI DAR LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara, Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Mkutano wa Baraza la kumi la Biashara Tanzania, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 6, 2017. Wengine ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto), Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Reginald Mengi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara, Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Mkutano wa Baraza la kumi la Biashara Tanzania, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 6, 2017. 
Baadhi ya Mawaziri, pamoja na Wajumbe, wakimsikililiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara, Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiongea katika Mkutano wa Baraza la kumi la Biashara Tanzania, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 6, 2017. PICHA NA IKULU

MWAKYEMBE AWASIHI WANAMICHEZO KUPATA CHANJO YA HOMA YA MANJANO KABLA YA KUSAFIRI

$
0
0
NA Ally Daud –WAMJW Dodoma.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewasihi wanamichezo wa Tanzania wapate chanjo ya homa ya manjano kabla ya kusafiri ili kujikinga dhidi ya ugonjwa wa homa ya manjano wanapokwenda nchi ambazo zina maambukizi ya ugonjwa huo.

Akizungumza hayo mara baada ya kupata chanjo hiyo katika viwanja vya bunge mjini Dodoma Dkt. Mwakyembe amesema kuwa wanamichezo wanastahili kupata chanjo hiyo ili wasipate ugonjwa pindi wanapotembelea nchi zenye ugonjwa huo.

“Nawaomba wanamichezo na watanzania kwa ujumla wapate chanjo hii ili kusudi wajilinde kutokupata ugonjwa huu kwani tumezungukwa na nchi wanachama ambao wana ugonjwa wa homa ya manjano” alisema Dkt. Mwakyembe.

Aidha Dkt. Mwakyembe amesema kuwa wanamichezo wanastahili kupata chanjo hiyo kwani huwa wanasafiri mara kwa mara kuwakilisha Taifa katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas Amesema kuwa ugonjwa wa homa ya manjano una madhara hivyo ni vyema kwa wafanyakazi,wafanyabiashara pamoja na wanafunzi wanaosafiri nje ya nchi hususani nchi zenye ugonjwa huo ni vyema wakajitokeza kupata chanjo.
WAZIRI wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kulia akipata maelekezo juu ya nchi zenye ugonjwa wa homa ya manjano barani Afrika na Duniani kutoka kwa Afisa Habari Msaidizi Wa Wizara ya Afya Bw. Ally Daud kushoto mara baada ya kupata chanjo ya homa ya manjano katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
Msemaji Mkuu wa Serikali na ambaye ni Mkurugenzi Idara ya Habari Dkt Hassan Abbas wa kwanza kulia akipokea cheti cha homa ya manjano kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Afya Mazingira Dkt. Khalid Massa wa kwanza kulia mara baada ya kupata chanjo hiyo katika viwnja vya Bunge mjini Dodoma katikati ni Afisa Afya Remidius Kakulu.

LIGI KUU YA VODACOM BARA KUENDELEA LEO NA KESHO KWA JUMLA YA MICHEZO SITA

$
0
0
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea leo Jumamosi Mei 6 na Jumapili Mei 7, mwaka huu kwa jumla ya michezo sita.

Kwa mujjibu wa ratiba, michezo ya Jumamosi kutakuwa na michezo mitano ilihali Jumapili kutakuwa na  mechi moja.

Michezo ya Jumamosi itakuwa ni kati ya Toto African na JKT Ruvu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza  wakati Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mwadui kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.

Kagera Sugar itaalikwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Young Africans ya Dar es Salaam itaialika Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Siku hiyo ya Jumamosi Mei 6, mwaka huu Azam FC itaialika Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Mbagala, Dar es Salaam ilihali Jumapili kutakuwa na mchezo kati ya Simba SC na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

UPDATE: TAARIFA YA KAMANDA WA POLISI MKOANI ARUSHA KUFUATIA AJALI YA GARI ILIYOPOTEZA MAISHA YA WANAFUNZI ZAIDI YA 30 HUKO KARATU LEO

$
0
0

Zoezi la uokoaji kwa wanafunzi hao likiendelea. 
Zoezi la uokoaji likiendelea. 
 
Majina ya Baadhi ya wanafunzi waliotambulika mpaka sasa.

VODACOM TANZANIA PLC YASHEREHEKEA MIAKA 23 YA UHURU WA AFRIKA YA KUSINI JIJINI

$
0
0
Balozi wa Afrika ya Kusini nchini, Thamsanga Dennis Msekelu akipongezwa na Meneja Ruzuku wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald,kuhusiana na sherehe ya maadhimisho ya miaka 23 ya Uhuru wa Afrika ya Kusini iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki,Sherehe hiyo ilidhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC.

Balozi wa Afrika ya Kusini nchini, Thamsanga Dennis Msekelu akicheza muziki aina ya Kwaito na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa kusherehekea maadhimisho ya miaka 23 ya Uhuru wa Afrika ya Kusini,Hafla hiyo iliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meneja Ruzuku wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald(kushoto)akiwa na wageni waalikwa kwenye sherehe ya maadhimisho ya miaka 23 ya Uhuru wa Afrika ya Kusini,Hafla hiyo iliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC na kufanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images