Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1671 | 1672 | (Page 1673) | 1674 | 1675 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0

  Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mohmoud Thabit Kombo akipokea maandamano ya Wakunga na Wauguzi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.

  Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiwa na Viongozi wa Wizara ya Afya na Jumiya ya Wakunga, Wauguzi na Wadau wa Afya Tanzania wakati wakipokea maandamano ya Wakunga na Wauguzi katika viwanja vya ZBC Redio rahaleo Zanzibar.  
  Wauguzi na Wakunga wakipita mbeli ya mgeni rasmin Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombe katika viwanja vya ZBC Redio rahaleo wakati wa maadhimishi ya siku hiyo maalum kwao.

  0 0

   Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, wakiwa na kifaa cha kukatia umeem, tayari kwa kazi kwenye transfoma ya kupeleka umeme kwenye eneo la kiwanda eneo la Vingunguti 
   Mfanyakazi wa TANESCO kivaa gloves tayari kukata umeme
   Meneja wa TANESCO mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, MhandisiAthanasius Nangali, (kulia), akiwa na Afisa kutoka idara ya fedha TANESCO makao makuu, akizungumza na waandishi wa habari 
   Mhandisi wa kudhibiti mapato TANESCO mkoa wa Ilala, Daniel Kimaro, akizungumza na waandishi baada ya kusitisha huduma ya umeme kwenye kampuni ya Iprint. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

    U.S. Chargé d’Affaires Virginia Blaser speaking with Tanzanian game scouts at the Pasiansi Wildlife Training Institute in Mwanza on May 3, 2017.  Chargé Blaser observed students at the Institute demonstrating the law enforcement, military, natural history, and field training they receive.  The U.S. Government has contributed to the Institute by supporting the training of nine Pasiansi staff members, helping to build capacity to protect wildlife in Tanzania. 

   U.S. Chargé d’Affaires Virginia Blaser visiting the Pasiansi Wildlife Training Institute in Mwanza on May 3,2017.   The students demonstrated for the Chargé the medicalfield training they receive.  The U.S. Government has contributed to the Institute by supporting the training of nine Pasiansi staff members, helping to build capacity to protect wildlife in Tanzania. 
   U.S. Chargé d’Affaires Virginia Blaser with Tanzanian game scouts at the Pasiansi Wildlife Training Institute in Mwanza on May 3, 2017.  Chargé Blaser observed students at the Institute demonstrating the law enforcement, military, natural history, and field training they receive.  The U.S. Government has contributed to the Institute by supporting the training of nine Pasiansi staff members, helping to build capacity to protect wildlife in Tanzania. 
  U.S. Chargé d’Affaires Virginia Blaser at the Mwanza Maritime Academy on May 3, 2017.  During the visit, Chargé Blaserwatched a patrol demonstration from onboard a U.S.-donated Defender Boat provided to Tanzania’s maritime police through the African Partnership for Rapid Response Peacekeeping.  In addition to donating two boats to the Maritime Police, the United States also donated nine other boats to Tanzania and facilitates the repair and maintenance of all the boats.
  U.S. Chargé d’Affaires Virginia Blaser with Police Inspector Wenceslaus Muchuguzi at the Mwanza Maritime Academy on May 3, 2017.  During the visit, Chargé Blaserwatched a patrol demonstration from onboard a U.S.-donated Defender Boat provided to Tanzania’s maritime police through the African Partnership for Rapid Response Peacekeeping.  In addition to donating two boats to the Maritime Police, the United States also donated nine other boats to Tanzania and facilitates the repair and maintenance of all the boats.

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa maelekezo Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Eng. Mgeni Mwanga juu ya upandaji nyasi kwenye eneo la katikati ya barabara wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Sakina hadi Tengeru jijini Arusha
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari wakati alipokwenda kukagua ujenzi wa barabara ya Sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei 4, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, bw. Mrisho Gambo. 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Cheil Engineering ambayo inajenga barabara ya Sakina-Tengeru, Bw. Shin Pil Soo (wa pili kushoto). Kulia ni Mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari na wa pili kulia ni Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Eng. Mgeni Mwanga. 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa tahadhari juu ya gema lililopo kwenye daraja la mto Ndoruma mara baada ya kukagua ujenzi wa daraja hilo katika barabra ya kutoka sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei 4, 2017. Kushoto kwake ni Meya wa Arusha, Bw. Calist Lazaro. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar.

  Hospitali na Vituo vya Afya vya Wilaya vinaweza kupunguza idadi ya akinamama kujifungulia Hospitali kuu ya Mnazimmoja iwapo juhudi za kuandaa mazingira mazuri zitachukuliwa na wakunga na wauguzi  wa vituo hivyo.

  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo ameeleza hayo katika maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Wasanii Rahaleo.
  Amesema akinamama  wengi wamejenga imani ya kujifungua  Hospitali kuu ya Mnazimmoja na kupelekea upungufu wa nafasi katika Hospitali hiyo huku vituo vya Afya vijijini vikiwa na akina mama  wacheche wanaokwenda kwa huduma ya kuzaa.

  Ameongeza kuwa Hospitali ya Mnazimmoja inazalisha zaidi ya akinamama 50 kwa siku na Mwembeladu wanawake 30 wengi wao kutoka vijijini wakati vituo vya afya vya huko vinazallisha wanawake wawili hadi watano kwa siku.
  Waziri Mahmoud amewataka wakunga na wauguzi wa vituo vya afya vya Wilaya vinavyotoa huduma ya kuzalisha  kuandaa mazingira yatakayowavutia wanawake kujifungua katika vituo vyao.

  Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea na mkakati wa kuandaa mazingira mazuri na kuweka miundo mbinu bora  ikiwemo vifaa vya kisasa hivyo amewataka wafanyakazi nao kubadilika na kuwapa faraja wagonjwa ili wajenge imani kwao.
   Brass band ya Chipikizi ikiongoza maandamano ya wakunga na wauguzi kupita mbele ya mgeni rasmi Waziri Afya Mhmoud Thabit Kombo katika maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Wasanii Rahaleo Mjini Zanzibar. 
    Mama Mariyam Othmani Mihale akiongoza wakunga na wauguzi katika wimbo maalum wa maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani katika ukumbi wa Wasanii Rahaleo.
   Mwenyekiti wa Baraza la Wuguzi na Wakunga Zanzibar Amina Abdulkadir Ali akitoa maelezo juu ya siku ya Wuguzi duniani katika maadhimisho yaliyofanyika ukumbi wa wasanii Rahaleo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
 • 05/05/17--00:55: HII NI HATARI
 • Nguzo ya umeme ikiwa inaning'inia katika barabara ya Moshi Bar Gongolamboto jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi kama ilivyonaswa na mdau wa Globu ya Jamii Zourha Malisa.

  0 0

  Havas Group ni moja kati ya mawakala wakubwa wa matangazo ya biashara yenye mtandao mpana duniani kote. Ikiwa na makao makuu nchini Ufaransa, Havas inapatikana katika nchi 149 zikiwemo nchi 19 barani Afrika ambapo wana ubia na kampuni nyingine. Havas Group,imegawanyika mara mbili katika Afrika - Havas Media Africa & Arena Media Afrika.
  Kihistoria, Havas imejikita kwa nguvu zaidi kwenye nchi zinazoongea lugha ya kifaransa zikiwemo,Cameroon, DRC, Ivory Coast & Senegal kuwa ndio nguzo yao katika ukanda huo. Nyingine ni pamoja na Gabon, Niger, Burkina, Benin, Togo. 
  Hivi karibuni,Havas imekuwa kwa kasi katika ukanda wa Afrika Mashariki, ikianzia na Kenya kwa miaka 5 iliyopita. Uganda na Rwanda zilifunguliwa mwaka jana wakati Zambia ipo kwenye  mipango ya kufunguliwa mwishoni mwa mwaka  huu. Ofisi za Tanzania zimekuwa zikifanya kazi tangu mwaka 2015 na tangu wakati huo hakuna kurudi nyuma. Hadi sasa tayari ina wateja wa kimataifa kama vile Emirates, Airtel & DTCM, biashara ya Tanzania inakua kulingana na mahitaji ya soko la media linaloongezeka siku hadi siku. 
  Shughuli za Havas Africa huratibiwa na kusimamiwa na kitengo cha Havas Afrika chenye makao makuu mjini Paris,ikikuza utaalamu kimataifa, zana na maarifa kwa masoko yote.Mtindo wao wa kufanya kazi huhakikisha kwamba kuna uthabiti na utendaji bora  katika matawi yao yote, ili kuinua na kuleta mawakala wote kwenye kiwango cha ubora kilicho sawa. 
  Kinachoitofautisha Havas  ni mbinu za utumiaji wa takwimu na namna yao ya kipekee ya kuweka matangazo ya bidhaa kwenye mtandao. Ndani ya mazingira ya Afrika, Havas  tayari imepiga hatua mbele na kuona umuhimu wa  vitu hivi viwili  katika kufanya mapendekezo na maamuzi. 
  Meneja uendeshaji wa Havas Tanzania anasema mwaka jana umekuwa ni mwaka wa kusisimua sana katika suala la maendeleo ya ofisi yake na timu kwa ujumla inaona fursa kubwa mwaka 2017. Mbinu kubwa wanayoitumia kwa mteja wao,ni kuwa na uelewa wa soko la Tanzania, mteja wake anataka nini na namna pekee wanayotumia kutangaza bidhaa kupitia mtandao, na namna wanavyoweza kujenga fikra  kimkakati kwa kuongozwa na  takwimu.

  Hii ndiyo sababu inayowafanya wateja wengi kuchagua Havas.

   Kwa mawasiliano na Havas Tanzania: fey.mallonga@tanzania.havasafrica.com  0 0


   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  akiongea wakati wa hafla ya ununuzi wa hisa za Vodacom Tanzania PLC iliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ambapo alinunua hisa  zake pamoja na mke wake Mary Majaliwa zenye thamani ya shilingi Milioni 20, wapili kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwekezaji Bi.Beng’i Issa , Mkurugenzi  Mtendaji  wa Vodacom Tanzania  PLC,Ian Ferrao na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn Mworia.

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  akielekezwa jinsi ya kujaza fomu  za kununua hisa  za Vodacom Tanzania PLC na Mkurugenzi wa wakala wa hisa wa Orbit Securities,Gerase Kamugisha  (kushoto) wakati alipokuwa akinunua hisa zake na mke wake Mary Majaliwa(hayupo pichani)zenye thamani ya shilingi milioni 20 katika hafla fupi  iliyofanyika ofisini kwake  jijini Dar es Salaam leo.Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwekezaji, Bi.Beng’i Issa  na Mkurugenzi  mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao.

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akikabidhiwa fomu ya kununua hisa za Vodacom Tanzania PLC   na Mkurugenzi wa wakala wa hisa wa Orbit Securities ,Gerase Kamugisha   wakati wa hafla fupi ya kununua hisa zake na mke wake,Mary Majaliwa(hayupo pichani) zenye thamani ya shilingi Milioni 20.Hafla hiyo ilifanyika  ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo,Anaeshuhudia kulia ni Mkurugenzi  Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC,Ian Ferrao.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akipongezwa na Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao  baada ya kununua hisa zake na za mke wake Mary Majaliwa(hayupo pichani) kutoka Vodacom Tanzania PLC kampni hiyo zenye thamani ya Shilingi Milioni 20.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na wadau wakati wa hafla ya ununuzi wa hisa Vodacom Tanzania PLC iliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ambapo alinunua hisa  zenye thamani ya shilingi Milioni 20 pamoja na mke wake Mary Majaliwa.

  0 0


  0 0

  Wanasiasa wameshauriwa kuacha kuwakatisha tamaa wananchi kwa kuwaita masikini hali inayosababisha washindwe kuchangia na kushiriki kikamilifu katika miradi na shughuli za maendeleo hususani miradi ambayo ina ufadhili kidogo wa serikali na wahisani.

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ametoa katazo hilo kabla ya kugawa vyeti kwa waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama waliofuzu mafunzo kuhusu jitihada za jamii kupitia mbinu shirikishi ya fursa na vikwazo kwa maendeleo iliyoboreshwa na usimamizi wa miradi ya maendeleo.

  Dkt. Nchimbi amesema wanasiasa akitoa mfano wa madiwani wamekuwa wakisema wananchi ni masikini na wa chini kauli zilizokuwa zikiwakatisha tama ya kuchangia maendeleo kwa kiwango kikubwa na kujiona hawana uwezo huo.

  “Mnawaita wananchi wa chini nani amewaweka ninyi juu? Inapofika wakati wa michango ya maendeleo mnasema wananchi ni masikini hawawezi kuchangia, nawaambia mkitoka hapa kwenye mafunzo mkatubu na muifute kauli ya kuwaita masikini, wananchi hawa ni msingi wa maendeleo na wana mchango mkubwa kwa maendeleo ya halmashauri” amesisitiza.

  Ameongeza kuwa kumekuwa na kutokuaminiana kati ya madiwani na watendaji hali inayowafanya kutupiana lawama pale jambo linapoharibika badala ya kutafuta suluhu kwa pamoja ili wananchi wapate huduma na maendeleo kwa haraka.

  Dkt. Nchimbi amesema mafunzo hayo waliyopewa yaonyeshe tofauti kati ya zamani na sasa huku akisisitiza kutumia fursa zilizopo vizuri na halmashauri kusimamia na kuhakikisha wananchi wananufaika na fursa zilizopo katika halmashauri yao.

  Madiwani na watendaji kwa kauli moja wamekubali kuwa kabla ya mafunzo kumekuwa na kutokuaminiana na kusababisha shughuli kutofanikiwa kwa kukosa ushirikiano wa wananchi, wanasiasa na watendaji wenyewe ila baada ya mafunzo wanasiasa na watendaji watafanya kazi kwa kushirikiana na kuwahusisha wananchi ili wao ndio waibue miradi na kuimiliki.

  Diwani Viti Maalumu kutoka kata ya Kinyangiri Eunice Kalaila amesema mafunzo hayo yatawafanya waweze kusimamia fedha zinazotolewa na serikali ili ziweze kukamilisha miradi kwa gharama na ubora sahihi.

  Kalaila ameongeza kuwa kutokana na mafunzo hayo utoaji wa taarifa utakuwa yakinifu huku miradi yote iliyosimama kwa kukosa ushirikiano wa wananchi itaendelea na kukamilika huku wananchi wataelimishwa kutambua fursa zilizopo na kuibua miradi yao watakayoikamilisha wenyewe na si kuitegea serikali.

  Kwa upande wake Diwani Viti Maalumu kutoka Kata ya Ibaga Habiba Issa amemkabidhi mkuu wa mkoa matunda ya asili aina ya furu huku akisisitiza kuwa sasa vijana wataelekezwa kutambua fursa zilizopo kuliko kusubiria ajira za serikali huku akitoa mfano wa fursa ya kutengeneza juice kutokana na matunda hayo ya asili.

  Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkalama Godfrey Sanga amesema atahakikisha anasimamia maelekezo yote ili wananchi wake wapate huduma nzuri na maendeleo kwa haraka huku akiamini lawama na malalamiko yatapungua.

  Sanga amesema sasa hakuta kuwa na uhasama kati ya watendaji na wanasiasa na hivyo ushirikiano huo utasaidia katika kuibua na kusimamia miradi pamoja na kutambua na kuzitumia fursa za maendeleo zilizopo Mkalama.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimkabidhi Diwani Viti maalum kata ya Ibaga Habiba Issa cheti cha mafunzo ya usimamizi wa miradi na jitihada za jamii za mbinu za kutambua fursa na vikwazo.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na madiwani kabla hajawapatia vyeti vya mafunzo ya usimamizi wa miradi na jitihada za jamii za mbinu za kutambua fursa na vikwazo.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhandisi Jackson Masaka zawadi ya matunda asilia aina ya furu aliyopewa na Diwani Viti maalum kata ya Ibaga Habiba Issa, matunda hayo yanaweza kutengenezwa juice na kuwa fursa ya ajira kwa vijana.
  Madiwan na watendaji kutoka halmashauri ya Mkalama wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi alipokuwa akizungumza nao kabla hajawapatia madiwani vyeti vya mafunzo ya usimamizi wa miradi na jitihada za jamii za mbinu za kutambua fursa na vikwazo.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
  MSANII wa Sanaa za Maonyesho Amani Kipimo  anataraji kufanya onesho la  Igizo la Jukwaani linalokwenda kwa jina la Untoldy Story litakalo fanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa  jijini Dar es Salaam.
  Akizungumza na Michuzi  blogu muandaji wa enesho  hilo Amani Kipimo amesema kuwa enesho ambalo litakuwa la bure  hivyo anawaomba kila mtu aliyopo nje na ndani ya Dar es Salaam  kufika katika ukumbi wa makumbusho Mei 18  mwaka huu.
  Kipimo  amesema kuwa eneo hilo alina kiingilio  hivyo kuwaomba watu kufika kwa wingi kujionea namna ya wataalamu na manguli wa sanaa za jukwani watakavyokuwa wanatoa burudani na ujumbe kwa jamii.

  0 0

  Jitihada za Wizara ya Nishati na Madini za kuhakikisha umeme unafika na kusambaa maeneo ya vijijini zimetambuliwa kimataifa hali iliyopelekea Serikali kupokea Tuzo ya Uwezeshaji wa Mazingira Bora ya Upatikanaji wa Umeme Vijijini kwa Nchi zinazoendelea.

  Serikali imetunukiwa Tuzo hiyo mwezi Machi, 22 na Taasisi ya Kimataifa ya Alliance for Rural Electrification yenye Makao Makuu yake nchini Ubelgiji ambayo ilipokelewa na Meneja Miradi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali kwa niaba ya Serikali katika hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika Lisbon, Ureno. Magali pia ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA).
  Meneja Miradi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali (kushoto) akipokea Tuzo ya Uwezeshaji wa Mazingira Bora ya Upatikanaji wa Umeme Vijijini kwa Nchi zinazoendelea kwa niaba ya Serikali kutoka kwa Mwenyekiti wa Sera ya Mtandao wa Kimataifa wa Nishati Mbadala (REN21) yenye makao makuu yake nchini Ufaransa, Profesa Arthouros Zervos.

  Akikabidhi Tuzo hiyo Jijini Dar es Salaam, kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo; Magali alisema Tuzo hiyo imetolewa kwa kutambua mchango wa Serikali ya Tanzania wa kufikisha huduma ya umeme maeneo ya vijijini pamoja na uwezeshaji wa mazingira bora na rafiki kwa wawekezaji wanaosambaza umeme katika maeneo ya vijijini.

  “Kwa mwaka huu, Serikali yetu imetambuliwa kwa kufikisha umeme vijijini na juhudi zake za kuhakikisha kunakuwa na mzingira rafiki kwa watoaji na wasambazaji wa huduma ya umeme vijijini,” alisema Magali.
  Meneja Miradi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali pamoja na washiriki kutoka nchi mbalimbali wakionesha Tuzo walizopokea kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Alliance for Rural Electrification katika hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika Lisbon, Ureno.

  Kwa upande wake Dkt.Mhandisi Pallangyo aliipongeza kampuni ya Ensol kwa kupokea tuzo kwa niaba ya Serikali na kuahidi kuendeleza ushirikiano na kampuni zote zinazojihusisha na usambazaji wa umeme maeneo ya vijijini.

  Alisema Serikali itaendelea kuandaa mazingira rafiki kwa wawekezaji ili kutimiza azma ya kuhakikisha vijiji vyote vinafikiwa na huduma ya Nishati ya Umeme.
  Aidha, Dkt. Mhandisi Pallangyo alizitaka kampuni nyingine zinazoshughulika na uzalishaji na usambazaji wa umeme vijijini kujiunga na Taasisi za Kimataifa ikiwemo ya Alliance for Rural Electrification ili kunufaika na fursa zinazopatikana kwenye Taasisi hizo.

  Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na watendaji wa Wizara na Taasisi zake wakiongozwa na Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ensol, Hamis Mikate.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akipokea Tuzo kutoka kwa Meneja Miradi wa Kampuni ya Umeme ya Ensol, Prosper Magali.


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga jana alifungua hafla ya maadhimisho ya 69ya uhuru wa Taifa la Israeli yaliyo fanyika mjini Dodoma katika Hoteli ya Morena.

  Hafla hiyo ya maadhimisho ya 69 ya uhuru wa Taifa hilo na uhusiono mzuri wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Israeli yaliratibiwa na Ubalozi wa Israel wenye makazi yake jijini Nairobi, Kenya. Waziri Mahiga akizungumza katika hafla hiyo aliupongeza Ubalozi wa Israel kwa uamuzi wake wa kufanyia hafla ya maadhimisho ya 69 ya uhuru wao, Makao Mkuu ya Serikali mjini Dodoma. 

  Waziri Mahiga aliongeza kusema Mataifa haya mawili Tanzania na Israel yana mahusiano mazuri ya kidiplomasia, ikidhihirishwa wazi na idadi kubwa ya raia wa nchi hizi mbili kutembeleana na kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo utalii. 

  Aidha Mahiga aliipongeza Serikali ya Israel kwa hatua kubwa ya maendeleo waliyofikia katika maeneo mbalimbali ikiwemo sayansi na teknolojia na kwa kuchangia maendeleo ya Tanzania katika nyanja mbalimbali. 

  Balozi wa Israeli nchini Mhe. Yahel Vilan mwenye makazi yake Jijini Nairobi, Kenya akitoa hotuba yake alisema Ubalozi wa Israeli umechukua maamuzi ya kufanyia hafla hiyo Mjini Dodoma ikiwa nikuunga mkono maamuzi ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhamishia Makao Makuu ya Serikali Dodoma. 

  Aliongeza kusema kuwa hafla hiyo ni ishara ya Israel kuanziasha Ubalozi wake nchini Tanzania. Balozi Vilan ameihakikishia serikali ya Tanzania kuwa Israel itaendelea kuwa mshirika mzuri wa maendeleo ya Taifa katika maeneo ya kilimo, afya, elimu, sayansi na teknolojia na usalama. Israeli ilifungua kituo cha kushughulikia masuala ya viza nchini Tanzania tarehe 3 Novemba, 2016. 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 69 ya uhuru wa Taifa la Israel iliyofanyika kwenye Hoteli Morena Mjini Dodoma.
  Meza Kuu wakiwa wamesimama wakati wimbo ya Taifa unakipigwa kweye maadhimisho ya 69 ya uhuru wa Israel.
  Balozi wa Israeli nchini mwenye makazi yake Nairobi, Kenya Mhe. Yahel Vilan akizunguza kwenye hafla ya maadhimisho ya 69 ya uhuru wa Israel iliyofanyika mjini Dodoma.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani (Mwinyi kulia) akifuatilia jambo, kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Job Masima.
  Picha ya pamoja.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dokta Binilith Mahenge akisoma taarifa ya mkoa pamoja na miradi ambayo mwenge wa Uhuru 2017 utafanya kazi ya kufungua, miradi itakayozinduliwa, itakayowekwa mawe ya msingi na itakayo kaguliwa TAARIFA KAMILI HII HAPA

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sophia Mjema akizungumza hivi karibuni na Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/17. Kwa Dar es Salaam, utafiti huu unatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi Mei, 2017.

  Na: Veronica Kazimoto.

  Wito umetolewa kwa Wananchi wote wa mkoa wa Dar es Salaam ambao kaya zao zimechaguliwa kitaalam kwa ajili ya  Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI wa mwaka 2016/17 kutoa ushirikiano kwa wadadisi wataokusanya taarifa za utafiti huo utakaofanyika mwishoni mwa mwezi Mei, mwaka huu.

  Akizungumza hivi karibuni katika  Mkutano wa Wadau wa Utafiti huo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sophia Mjema amesema Utafiti huu ni muhimu sana kwani husaidia kujua hali halisi ya ugonjwa wa UKIMWI na hivyo kuongeza nguvu zaidi ya kuondokana na ugonjwa huo.

  "Mimi niwaeleze tu kwamba, utafiti huu ni muhimu sana katika mkoa wetu wa Dar es Salaam kwa kuwa utatusaidia kujua hali halisi ya maambukizi ya VVU na hatimaye kupata nguvu zaidi za kuondokana na ugonjwa huu, hivyo nawaagiza kusimamia zoezi hili na kuwahimiza Wananchi wote ambao kaya zao zimechaguliwa kutoa ushirikiano kwa wadadisi watakaofanya taarifa za utafiti huu", amesema Mjema.
  Mkurugenzi Msahauri, Dkt. Cecilia Makafu kutoka Shirika la ICAP Tanzania akiwasilisha mada kuhusu Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI wa mwaka 2016/17 kwa wadau wa Utafiti huo wa Mkoa wa Dar es Salaam.

  Mjema amefafanua kuwa, utafiti huu ni wa kwanza kukusanya taarifa zinazohusiana na maambukizi mapya ya VVU, kiwango cha VVU mwilini kwa watu wanaoishi na VVU na wastani wa maambukizi ya VVU kwa watu wa rika zote pamoja na wingi wa chembechembe za kinga mwilini (CD4 T-cell count).

  Aidha,  utafiti huu utapima uwepo wa viashiria vya usugu wa dawa, kiwango cha maambukizi ya kaswende pamoja na homa ya ini (Hepatitis B).

  Akizungumzia kiwango cha maambukizi ya VVU katika tafiti zilizopita, Mkuu wa Wilaya huyo ameeleza kuwa, maambukizi yamepungua kutoka asilimia 7 mwaka 2003 mpaka asilimia 5.1 mwaka 2011 na kuifanya Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha chini cha maambukizi ya nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo nchi nyingi za ukanda huo zina kiwango cha zaidi ya aslimia 10.
  Baadhi ya Washiriki waliohudhuria Mkutano wa Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/17 uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

  Nae Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Grace Magembe amesema kuwa, kwa mkoa wa Dar es Salaam, utafiti huu utahusisha kaya zisizozidi 1,000  na Wananchi watakuwa na hiari ya kukubali kupima ambapo kwa wale watakaogundulika kuwa na maambukizi, watapata rufaa ya kwenda kupatiwa matibabu bure katika vituo vya kutolea huduma za afya.

  "Utafiti huu wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI hauhusishi watu wote bali ni kaya chache tu ambazo zimechaguliwa kitaalam ili ziweze kuwakilisha kaya nyingine na kwa hapa Dar es Salaam kaya zilizochaguliwa hazizidi 1000", amesema Dkt. Magembe.

  Utafiti wa aina hii ni wa mara ya nne (4) kufanyika nchini Tanzania ambapo wa kwanza ulifanyika mwaka 2003, wa pili mwaka 2007 na wa tatu mwaka 2011.

  Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016 /17 unafanyika nchini, chini ya usimamizi wa  Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kwa Tanzania Bara, Wizara ya Afya Tanzania Zanzibar, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS), Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS)  na Tume ya UKIMWI Zanzibar (ZAC). 

  0 0

  Baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha Corporate Support cha NMB wakipiga picha na mmoja wa wanufaika wa wanufaika wa upasuaji wa mdomo Sungura uliotolewa na wafanyakazi wa kitengo cha Corporate Support cha Benki ya NMB.

   WAFANYAKAZI wa Benki ya NMB katika kitengo cha Corporate Support wamedhamini upasuaji wa watoto wanne wenye midomo Sungura waliokuwa wamelezwa katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam. Akizungumzia udhamini huo, Meneja Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Majengo NMB, Elizabeth Lukaza alisema ufadhili huo ni sehemu ya utaratibu ambao wamejiwekea wao kama wafanyakazi wa kitengo cha Corporate Support kusaidia jamii kwa sehemu yenye uhitaji.

  Alisema ufadhili huo ulikuwa wa Dola 1,200 (Tsh. 2.6 milioni) na hiyo siyo mara ya kwanza wao kutoa ufadhili kwa kuchangia huduma mbalimbali za kijamii kwani kila mwaka hufanya hivyo angalau mara tatu. 

  “Kila mwaka tunatoa msaada kwa jamii, kwa mwaka huu tumekuja CCBRT tumesaidia watoto wanne ambao walikuwa wanatakiwa kufanyiwa upasuaji wa mdomo Sungura, upasuaji wa kila mtoto tumetao Dolla 300,"“Pesa hizi tumejichangisha katika kitengo na ofisi imetuchangia sehemu ya fedha ili kufanikisha lengo letu, tumekuwa tukifanya mambo mbalimbali, tumewahi hata kutoa damu kwenye kituo chao kilichopo Mwananyamala,” alisema Elizabeth. Mmoja wa wanufaika wa ufadhili wa wafanyakazi wa kitengo cha Corporate Support cha NMB, Emmanuel Isdor (mtoto), akiwa amebebwa na mama na mamae, Maines Ephrahim.[/caption] Pia alizungumzia mipango ya kitengo chao kwa siku zijazo, “Kuna vitu vingi vya kufanya, kama kitengo chetu tumemua kuunga mkono juhudi za benki kupitia kitengo cha masuala ya uwajikikaji kwa jamii (CSR). 

  Pia tutaendelea kufuatilia maendeleo ya afya za watoto hawa kupitia wazazi wao,” Naye mmoja wa wazazi ambao mtoto wake amefanyiwa upasuaji wa mdomo Sungura kwa ufadhili wa NMB kupitia kitengo cha Corporate Support, Maines Ephrahim alionyesha Furaha na kuwashukuru NMB kwa ufadhili huo na kueleza kuwa kabla ya upasuaji huo hali ya mtoto ilikuwa tofauti na ilivyo sasa. 

  “Nawashukuru NMB kwa msaada ambao wamempatia mtoto wangu (Emmanuel Isdor), amefanyiwa upasuaji vizuri…kabla ya upasuaji mtoto alikuwa analialia, lakini sasa hali ni nzuri nimefurahi,” alisema Maines. Kwa upande wa nesi aliyewahudumia katika wodi ya watoto wenye mdomo sungura na walemavu, Joyce Cosmas alisema, “Nawashukuru NMB kwa msaada waliotoa, kwa sisi kama manesi tuliwapokea vizuri na kuwapa huduma zote ambazo walikuwa walistahili kuzipata.” 

  0 0

  Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameshiriki Mkutano wa World Economic Forum for Africa unaofanyika Durban, Afrika Kusini. Mkutano huo muhimu unaokutanisha wafanyabiashara, wanasiasa na viongozi wa kiserikali unalengo la kutoa fursa kwa wadau wa maendeleo barani Africa kukutana na kujadili mustakhabali wa maendeleo na uwekezaji barani Afrika.
  Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Rais Mstaafu aliwakilisha Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu (The Education Commission) ambapo alikutana na wadau wa elimu na vyombo vya habari kuelezea Mpango wa Kizazi cha Elimu barani Afrika.
  Rais Mstaafu pia alipewa heshima ya kuhutubia hafla ya chakula cha jioni kutathmini mafanikio ya mpango wa Kilimo wa Grow Africa ambao chimbuko lake ni Mkutano wa WEF Africa uliofanyika Tanzania Mei, 2010 na Mpango wa Uwekezaji wa Kilimo wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT). 
  Katika hotuba yake, Rais Mstaafu alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuchochea ushiriki wa Sekta Binafsi na uwekezaji katika Kilimo barani Afrika. Alitoa angalizo kuwa mafanikio ya mapinduzi ya kilimo hayawezi kufanikiwa kwa kuondoa wakulima wadogo bali kuwaongezea tija. Alitoa rai kwa viongozi wa Afrika kuhakikisha kuwa kilimo cha Wakulima wakubwa kinashamirisha na kustawisha kilimo cha wakulima wadogo na kuwa ni vitu vinavyoweza kwenda pamoja.
  Akiwa Durban, Rais Mstafu amehudhuria pia amefanya mazungumzo na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Profesa Klaus Shwab ambaye ni Mtendaji Mkuu wa World Economic Forum. 
   Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika mdahalo wakati wa Mkutano wa World Economic Forum for Africa unaofanyika Durban, Afrika Kusini. 
    Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini pembezoni mwa mkutano huo mjini Durban

    Rais Mstafu amehudhuria pia amefanya mazungumzo na Profesa Klaus Shwab ambaye ni Mtendaji Mkuu wa World Economic Forum.  
  Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho akiwa na Mkurugenzio wa World Economic Forum kanda ya Afrikakwenye mkutano huo  unaofanyika Durban, Afrika Kusini. Kabla ya hapo Bi kanza alikuwa mshauri wa Uchumi wa Rais Mstaafu Kikwete wakati wa uongozi wa awamu ya nne.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) (katikati), akipokea funguo za Magari aina ya Toyota Land Cruiser  kutoka kwa  Balozi wa Omani hapa nchini, Mhe. Ali Abdullah Al Mahruqi. Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Ramadhan Mwinyi. 

  Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam leo. Baada ya kukabidhiwa magari hayo yenye thamani ya takriban milioni 400 za Tanzania, Waziri Mahiga alisema kuwa msaada huo umetolewa na Serikali ya Oman kwa ajili ya kusaidia masuala ya usafiri katika kipindi hiki cha mpito ambapo Serikali inahamia Dodoma. 
  Waziri Mahiga akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Serikali na Wizara yake kwa ujumla mara baada ya kupokea msaada huo. 
  Waziri akiendelea kuongea huku Watumishi wa Wizara yake wakimsikiliza kwa makini.
  Balozi Al Mahruqi naye akizungumza na kuishukuru Tanzania kwa ushirikiano anaoumpata kwenye utendaji kazi wake hapa nchini. Alisema Serikali yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo huduma za kijamii. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan –JAICA- wametoa mrejesho wa utekelezaji wa mpango wa kuboresha huduma na kutatua matatizo madogo kwa kutumia rasimilimali zilizopo –KAIZEN. 
   Mbali na kutoa mrejesho huo pia wameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuboresha utoaji wa huduma. 
  Mpango huo ambao unahusisha watoa huduma umesaidia watumishi kutoa huduma bora, kuzingatia muda wa utoaji huduma na hivyo kupunguza malalamiko kwa wateja. 
   'Tumefanya tathimini tumeona jinsi ambavyo mmeboresha utoaji wa huduma na kupunguza mlalamiko kwa wananchi , wauguzi wanahudumia wagonjwa kwa upendo na wanatumia lugha nzuri lakini hata mazingira ya Hospitali ni safi’’ amesema Noriyuki Miyamoto. 
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utumishi wa MNH Bwana Makwaia Makani amesema tangu kuanza kutekelezwa kwa mpango huo mwaka 2008 kumekua na mabadiliko mengi hospitalini hapo na kusisitiza kuwa hospitali hiyo itahakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma bora.
  Baadhi ya wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakimsikiliza Mkurugenzi wa Utumishi wa MNH  Bwana: Makani katika  mkutano huo uliofanyika  leo.
  Bi Rose  Mpayo  Muwezeshaji kutoka Hospitali ya  Rufaa Kanda ya Mbeya akielezea umuhimu wa utoaji huduma bora kwa wateja.


  Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakifuatilia maelezo kutoa kwa mtoa mada.
  Mtaalam wa usimamizi wa huduma  bora kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan- JICA  -Noriyuki  Miyamoto akitoa mrejesho kuhusu  mpango wa kuboresha huduma . Zoezi lililofanywa na JAICA kwa kushirikiana na  wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
  Mkurugenzi  wa  Utumishi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Makwaia Makani akitoa neno kwa wauguzi wa  Hospitali hiyo katika mkutano wa kupokea mrejesho kuhusu mpango wa kuboresha huduma na kutatua matatizo madogo  kwa kutumia rasilimali zilizopo-KAIZEN .

older | 1 | .... | 1671 | 1672 | (Page 1673) | 1674 | 1675 | .... | 3272 | newer