Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1670 | 1671 | (Page 1672) | 1673 | 1674 | .... | 3285 | newer

  0 0    Ndugu Catherine Nyakao Ruge 


  KUHUSU UTEUZI WA CATHERINE NYAKAO RUGE KUWA MBUNGE WA VITI MAALUM KUPITIA
  CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
  Kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 04 Mei, 2017 imemteua Ndugu Catherine Nyakao Ruge kuwa Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Dkt. Elly Marco Macha. 


  Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemteua Ndugu Catherine Nyakao Ruge baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa mujibu wa Kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwepo nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, baada ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Dkt. Elly Marko Macha kufariki dunia na hivyo kuwepo nafasi wazi. 

  Imetolewa leo tarehe 04 Mei, 2017 na:- 

  Kailima, R.K 

  MKURUGENZI WA UCHAGUZI

  0 0

  Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

  Serikali imesema kuwa haina mpango wowote wa kusitisha mbio za Mwenge wa Uhuru na kusisitiza kuwa dhana hii ni endelevu na itaendelea kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa kusisitiza misingi hii bila kuchoka.

  Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama wakati akijibu hoja mbalimbali  Mjini Dodoma.

  “Kutokana na faida na Mafanikio makubwa yanayopatikana kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru Serikali inaamini kuwa zipo faida nyingi ndani yake na mwenge huu utaendelea kudumu”,Alisisitiza Mhe.Muhagama.

  Amesema kuwa Kimataifa Mwenge wa Uhuru umeendelea kusimamia dhana na maudhui yake ya kumulika hata nje ya mipaka yetu kwa kuwa msuluhishi wa Amani Afrika na mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine Afrika na Dunia kote.

  Aidha amesisitiza kuwa Umoja ,Mshikamano ,Upendo na Ukarimu wa Watanzania  ni matunda ya Mwenge wa Uhuru.

  Mhe.Muhagama ametoa takwimu ambazo zinaonyesha kuwa Miradi ya Maendeleo iliyozinduliwa pamoja na kuwekewa mawe ya msingi kupitia Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2015 ni miradi 1342 yenye thamani ya bilioni 463,519,966,467.

  Pamoja na hayo amezitaja faida za Mwenge wa Uhuru kuwa ni kuendelea kuamasisha ari ya wananchi kujitegemea na kuwekeza katika maeneo mbalimbali katika Taifa letu,pia kimekuwa ni chombo pekee cha kujenga umoja na mshikamano na kudumisha amani pale unapopita bila kujihusisha na itikadi za kisiasa.

  Aidha Mwenge wa Uhuru umeendelea kuhamasisha na kuimarisha umuhimu wa Muungano kwa Watanzania wa pande mbili za nchi yetu na kila mwaka huweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi na kuhamasisha uzalendo wa kuendelea kujitolea.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi ,Vijana ,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.

  0 0

  Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar.

  Hospitali na Vituo vya Afya vya Wilaya vinaweza kupunguza idadi ya akinamama kujifungulia Hospitali kuu ya Mnazimmoja iwapo juhudi za kuandaa mazingira mazuri zitachukuliwa na wakunga na wauguzi  wa vituo hivyo.

  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo ameeleza hayo katika maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Wasanii Rahaleo.
  Amesema akinamama  wengi wamejenga imani ya kujifungua  Hospitali kuu ya Mnazimmoja na kupelekea upungufu wa nafasi katika Hospitali hiyo huku vituo vya Afya vijijini vikiwa na akina mama  wacheche wanaokwenda kwa huduma ya kuzaa.

  Ameongeza kuwa Hospitali ya Mnazimmoja inazalisha zaidi ya akinamama 50 kwa siku na Mwembeladu wanawake 30 wengi wao kutoka vijijini wakati vituo vya afya vya huko vinazallisha wanawake wawili hadi watano kwa siku.
  Waziri Mahmoud amewataka wakunga na wauguzi wa vituo vya afya vya Wilaya vinavyotoa huduma ya kuzalisha  kuandaa mazingira yatakayowavutia wanawake kujifungua katika vituo vyao.

  Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea na mkakati wa kuandaa mazingira mazuri na kuweka miundo mbinu bora  ikiwemo vifaa vya kisasa hivyo amewataka wafanyakazi nao kubadilika na kuwapa faraja wagonjwa ili wajenge imani kwao.
   Brass band ya Chipikizi ikiongoza maandamano ya wakunga na wauguzi kupita mbele ya mgeni rasmi Waziri Afya Mhmoud Thabit Kombo katika maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Wasanii Rahaleo Mjini Zanzibar. 
    Mama Mariyam Othmani Mihale akiongoza wakunga na wauguzi katika wimbo maalum wa maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani katika ukumbi wa Wasanii Rahaleo.
   Mwenyekiti wa Baraza la Wuguzi na Wakunga Zanzibar Amina Abdulkadir Ali akitoa maelezo juu ya siku ya Wuguzi duniani katika maadhimisho yaliyofanyika ukumbi wa wasanii Rahaleo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Mwenyekiti wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Andrew Chenge  akiongoza kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.
    Wabunge wa CCM wakijadili  jambo katika  kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.
   Waziri wa Sera,Bunge,Kazi ,Vijana ,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama wakizungumza jambo na Mbunge wa Iringa Mjini Mhe.Peter Msigwa  katika kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.
   Mbunge wa Konde,Khatib Said Haji(CUF) akiuliza swali katika kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Na Asteria Muhozya, Arusha.

   Jumla ya Wanafunzi 55 kutoka  Shule za Sekondari za Arusha Day, Arusha Sekondari na Wining Sprit wenye  umri kati ya miaka 12- 15 wamepatiwa mafunzo ya Jemolojia katika Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito yanayoendelea jijini Arusha.

  Mafunzo hayo yanayojulikana kama GemKids yametolewa na  Wakufunzi kutoka  Taasisi ya Gemological Institute of America (GIA) na kuratibiwa na Kituo cha Jimolojia  Tanzania  Cha Arusha, (TGC).

  Akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo, Mratibu wa TGC,  Erick Mpesa amesema kuwa, mafunzo hayo  ya Jemolojia, yanalenga kuwapa ufahamu wanafunzi ili kuwa na uelewa wa madini ya vito, kujua matumizi yake, kuyatumia na baadaye kuwawezesha  kuingia katika biashara ya madini huku wakiwa na uelewa mzuri na rasilimali hizo ambazo zinapatikana katika maeneo mbalimbali nchini.

  Akizungumzia mahusiano ya TGC na Taasisi ya GIA, Mpesa amesema kuwa, TGC imelenga kuendeleza ushirikiano na Taasisi hiyo kwa siku za baadaye hususani katika masuala ya utafiti na mafunzo na kuongeza kuwa, uhusiano uliopo baina ya taasisi hizo, umewezesha baadhi ya watumishi wa kituo hicho kupata mafunzo katika taasisi hiyo.

  Kuhusu mpango wa TGC kutoa mafunzo  kwa Watanzania, alisema kuwa, tayari kupitia Maonesho ya Vito ya Arusha, kituo hicho kuanzia mwaka 2014 kimetoa mafunzo ya ukataji na unga'rishaji wa madini ya vito kwa  jumla wanawake 47 na kueleza kuwa,  hivi sasa jumla ya wanawake 18 wanaendelea na mafunzo hayo na wanatarajiwa kuhitimu ifikapo tarehe 19 ya mwezi huu.

  "Kutokana na changamoto ya ajira wahitimu wetu tunawashauri kujiunga katika vikundi ili kuwawezesha kupata ruzuku pale zinapotolewa na Serikali. Hii inawezesha rasilimali inayotumika kuwafundisha kuwawezesha vijana hawa isipotee bure. Lengo letu ni kuwawezesha waweze kujiajiri na kuajiriwa," alisisitiza Mpesa.

  Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Vito ya Arusha yalianza  rasmi tarehe 3 Mei na yanataajiwa kufungwa tarehe 5 Mei,2017. 
  Wanafunzi wa Shule wa Sekondari ya Arusha wakimsikiliza Mkufunzi kutoka  Taasisi ya  Gemological Insitute of America (GIA) , Elizabeth  Bokaba (hayupo pichani). Wanafunzi hao wamepata mafunzo kuhusu mafunzo ya Jimolojia.
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha wakifuatilia mafunzo kwa vitendo kuhusu elimu ya madini ya vito yanayopatikana chini, wakati wa Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito yanayoendelea jijini Arusha.
  Mratibu wa Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), Eric Mpesa akiwaeleza jambo wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha wakati wa mafunzo ya Jemolojia yaliyotolewa na Taasisi ya GIA wakati wa Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Vito Arusha yanayoendelea jijini Arusha.
  Mkufunzi kutoka Taasisi ya Gemological Institute of America (GIA), Elizabeth  Bokaba, akiwafundisha elimu ya Jemolojia wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha.
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha wakiangalia madini ya Tanzanite katika Banda la Kampuni Gliters Gems Limited  wakati walipotembelea mabanda ya maonesho baada ya kupata mafunzo ya Jemolojia.

  Mfanyabiashara wa Madini wa Kampuni ya Abdulhakim Mulla akiwaonesha wanafunzi wa Shule ya Sekondari Madini ya Tanzanite. Mulla alitumia nafasi hiyo kuwafundisha tofauti ya madini yaliyonakishiwa na ambayo bado hayajakatwa.

  0 0

  Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi ametembelea Ubalozi wa Tanzania Nairobi Kenya na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Mheshimiwa Balozi Mteule Dkt. Pindi Hazara Chana.

  Prof. Kabudi alifanya ziara hiyo tarehe 4/5/2017 wakati akihudhuria Mkutano wa 56 wa Mwaka wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria ya Nchi za Asia na Afrika (Asian-African Legal Consultative Organisation –AALCO) unaofanyika mjini Nairobi.

  Katika ziara hiyo Prof. Kabudi aliongozana na Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda Balozi Mteule wa Tanzania Nchini India yalipo makao makuu ya Jumuiya hiyo na maafisa wengine wa Wizara ya Mambo ya Nje.

  Prof. Kabudi alimpongeza Balozi Pindi Chana kwa uteuzi na alishukuru kwa maandalizi waliyoyafanya kuhakikisha ujumbe wa Tanzania unashiriki ipasavyo mkutano huo. Vile vile alimuhakikishia kuwa Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na taasisi zake zitampa ushirikiano stahiki katika utekelezaji wa majukumu yake, na kwamba Ubalozi uwe tayari kwa kufuata taratibu zilizopo kiserikali kuwasiliana na Wizara pindi yanapoibuka masuala yanayohitaji ushiriki wa Wizara.

  Kwa upande wake Balozi Dkt. Pindi Chana alimshukuru Prof. Kabudi kwa kutenga muda kuja kuutembelea Ubalozi na kumpongeza kwa uteuzi alioupata. Balozi Chana alimuahidi Prof. Kabudi kuwa Ubalozi utaendelea kushirikiana ipasavyo na Wizara kwa kutumia taratibu zilizopo utahakikisha kuwa masuala ya Wizara yanaifikia Wizara kwa wakati. 
  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, kushoto akifurahia jambo katika Sikukuu ya Muungano wa Tanzania iliyoadhimishwa nchini humo kwa kukutanisha Watanzania wanaoishi Saudi Arabia, wazawa na viongozi mbalimbali kama sehemu ya kuitangaza vyema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hisani ya Ubalozi wa Tanzania Saudi Arabia.

  Na Mwandishi Maalum, Riyadh Saud Arabia

  SHEREHE za Sikukuu ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zimetumika kama sehemu ya kutangaza utalii wa Tanzania katika tukio maalum lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wan chi hiyo.

  Akizungumza hivi karibuni katika sherehe hizo za Sikukuu ya Muungano wa Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, alisema kwamba Tanzania ni eneo zuri la uwekezaji kutokana na sera zake nzuri pamoja na dhamira njema za viongozi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli kwa Tanzania Bara pamoja na Dr Ali Mohamed Shein kwa upande wa Visiwani Zanzibar.
  Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza wa nane kutoka kushoto mstari wa mbele akiwa na wageni mbalimbali katika maadhimisho ya Sikukuu ya Muungano nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kusherehekea pamoja katika siku hiyo muhimu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Picha kwa Hisani ya Ubalozi wa Tanzania Saudi Arabia.
  Balozi Mgaza akiwa na mgeni rasmi Prince Muhammad bin abdullahman wakikata keki ya sherehe.
  Balozi Mgaza kushoto akikata keki
  Balozi Mgaza akihutubia katika hafla hiyo

  Alisema kutokana na sera hizo pamoja na kusimamia vyema rasilimali za utalii kama vile Mlima Kilimanjaro, mbuga mbalimbali za wanyama ni sehemu thabiti ya utalii kwa wageni, wakiwamo wananchi wa Saudi Arabia.

  “Nchi yetu ina mbuga za wanyama 16 ambazo zimekuwa zikitunzwa na kuhifadhiwa vema kama sehemu ya kuhakikisha kwamba rasimali hiyo inakuza uchumi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  “Nchi yetu ina wakaribisha wote kutembelea kujionea mambo mbalimbali yanayovutia katika utalii pamoja na kuwekeza katika sekta muhimu zikiwamo za viwanda ambazo ndio agenda kuu kwa sasa nchini mwetu,” Alisema Balozi Mgaza.

  Sikukuu ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeadhimishwa wiki iliyopita Aprili 26 ambayo hutumiwa kama kioo cha kuangalia matunda yanayojitokeza kutokana na Muungano huo kati ya Tanzania Bara na Visiwani.

  0 0

  Mkuu wa masoko wa  Benk ya TIB Corporate ltd  Bi. Theresia Soka akipokea hati ya shukran toka Kwa mgeni rasmi Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudiwa na Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa bodi ya makandarasi Mama Consolata Ngimbwa na  msajili mkuu wa  bodi ya makandarasi Bw. Reuben  Nkori. Hiyo ikiwa ni baada ya kudhamini mkutano mkuu wa mwaka wa Bodi ya Makandarasi unaofanyika katika ukumbi wa Jakaya  kikwete convention center  mjini Dodoma leo. 
  TIB corporate ni benki  ya biashara  inayotoa huduma mbalimbali za kibenki katika sekta mbali mbali. Kupitia benki hiyo, Makandarasi wanapatiwa huduma mbalimbali kama vile project financing, overdraft na bank guarantees, unsecured bid bonds, advance payment guarantees na performance guarantees.

  0 0


  Katika azma yake ya  kuhakikisha Watanzania wengi wanapata matangazo yake, Kituo cha Utangazaji cha EFM  kimetanua matangazo yake kwa kuongeza masafa ya 91.3 fm Mkoani Mwanza huku Uongozi ukibainisha kuwa matarajio ni kuhakikisha Matangazo hayo yanafika katika mikoa mingine kumi, ikifuatiwa na Mkoa wa Mbeya, Singida, Kilimanjaro, Manyara, Mtwara, Tanga , Kigoma na  Dodoma.
  Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa EFM Radio Bwana Denis Ssebo, amesema lengo la kuanza na Mkoa wa Mwanza ni baada ya kuangalia idadi ya watu ambao wanapatikana kupitia Kanda ya Ziwa Victoria lakini pia ukubwa wa jiji hilo baada ya jiji la Dar es salaam.
  "Lengo la Efm Radio ni kuhakikisha inahabarisha, inaburudisha, kuwezesha pamoja na kuwapa elimu wasikilizaji wake wote katika kila mkoa itakaposikika.  Hivyo mikoa mingine ikae mkao wa kula - tutawafuata mlipo…" amesema Denis Ssebo”, akimalizia na EFM NI KWIKWI!

  0 0
 • 05/05/17--00:00: KUMBUKUMBU
 • MAREHEMU MWALIMU NOVATI SIMEON RUTAGERUKA


  TAREHE 5 - MEI - 2017, UMETIMIZA MIAKA SABA TANGU MWENYEZI MUNGU ALIPOKUTWAA TOKA HAPA DUNIANI.  PAMOJA NA KWAMBA KIMWILI HAUPO NASI, KIROHO TUNAKUKUMBUKA DAIMA.

  UNAKUMBUKWA DAIMA NA WATOTO WAKO FLORIDA, ILLUMINATA, LIBERATA, DUNSTAN, JOYCE NA EDWIN PAMOJA NA WAKWE, WAJUKUU, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.

  IBADA YA MISA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU MWALIMU NOVATI RUTAGERUKA ITAADHIMISHWA SIKU YA IJUMAA TAREHE  5 - MEI - 2017, KATIKA KANISA LA MTAKATIFU GASPER, MBEZI BEACH, DAR-ES-SALAAM SAA 12.00 ASUBUHI NA KANISA LA MTAKATIFU MAURUS, KURASINI DAR-ES-SALAAM SAA 12.30 ASUBUHI.

  BWANA ALITOA, BWANA ALITWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE. AMINA

  0 0


  0 0

  Aliyekuwa Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta  ambaye anajiandaa kustaafu, Bw. Fortunatus Kapinga akizungumza wakati wa kuwatuza wafanyakazi hodari wa shirika. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu mpya, Deo Kwiyukwa na kulia ni Meneja wa Fedha, Cyprian Mugemuzi.
  Kaimu Postamasta Mkuu mpya wa Shirika la Posta, Bw. Deo Kwiyukwa akiwa na baadhi ya watendaji washirika hilo, wakiimba wimbo wa wafanyakazi wa mshikamano.  
  Mmoja wa wafanyakazi wa shirika la Posta, Zainabu Ukwaju akigogesha glasi na Kaimu Postamasta Mkuu mpya wa Shirika la Posta, Deo Kwiyukwa.
  Baadhi ya wafanyakazi wa shirika la Posta wakiwa katika hafla ya kuwatunuku wafanyakazi hodari.

  0 0

  Mkuu wa wilaya Iringa Mhe Richard Kasesela leo amefanya ziara ya kukagua madarasa na mabweni katika shule ya sekondari Tagamenda ikiwa ni maandalizi ya kupokea kidato cha 5 mwezi wa 7. Katika ziara yake aliyo ambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Bwana Omar Mkangaa, Mhe Kasesela aliagiza kasi ya ujenzi wa madarasa hayo na mabweni iongezeke ikiwezekana wajenge hata usiku ili tuweze kupokea wanafunzi wa kidato cha 5, huku akisisitiza kwamba mpaka sasa fedha za ujenzi zimeishapatikana kinachotakiwa ni kasi ya ujenzi. 
  Kwa sasa shule ya sekondari ya Tagamenda ina wanafunzi 882 wakiwemo wasichana 503 na wavulana 379. Inatarajia kupokea wasischana 120 kidato cha tano. Ujenzi wa madarasa 4 kwa thamani ya shilingi milioni 80, mpaka sasa kiwanja kimoja kipo katika hatua ya kupaka rangi na vyumba 3 na ofisi ya mwalimu vipo katika hatua ya kupiga kenchi. Akitoa taarifa fundi mjenzi Bwana Emmanuel Mhelamvi alisema mpaka sasa kiasi cha shilingi 56,447,102.40 zimekwisha tumika bado shilingi 23,552, 897.60 .  Pia Mabweni 2 ambayo yako katika hatua za kenchi yatagharimu kisi cha shilingi 150,000,000. 
  Changamoto kubwa ni gharama ya vifaa bei zake kubadilika mara kwa mara, pia gharama za ujenzi zimeonekana kuwa juu kutokana na eneo lenyewe kuwa mlimani . Mkuu wa wilaya aliaomba wadau na wananchi wajitokeze kusaidia ujenzi na vifaa vya shule hiyo. “nia yetu ni kuifanya shule ya mfano ili iweze kushindana na shule kama Feza na St Francis na zinginezo zinazo fanya vizuri, la msingi ni kuboresha miundo mbinu” 
  Mhe Kasesela pia alimshukuru sana Bwana Tibba Guyayi kutoka Dar Es salaam ambaye ameahidi kutoa kompyuta 2 kwa ajili ya shule na kuwaomba wengine waige mfano wa bwana Guyayi.
   Ujenzi wa madarasa na mabweni katika shule ya sekondari Tagamenda 
   Mkuu wa wilaya Iringa Mhe Richard Kasesela akiwa katika  ziara ya kukagua madarasa na mabweni katika shule ya sekondari Tagamenda
   Mkuu wa wilaya Iringa Mhe Richard Kasesela akitoammaagizo wakati wa ziara yake ya kukagua madarasa na mabweni katika shule ya sekondari Tagamenda

   Mkuu wa wilaya Iringa Mhe Richard Kasesela akiendelea  kukagua madarasa na mabweni katika shule ya sekondari Tagamenda

  0 0

  Na Khalfan Said
  “MANENO ni mawili tu “KA na TA” ukiunganisha Kata, asiyelipa kateni umeme” Hayo yalikuwa ni maneno ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, wakati akitoa hotuba ya uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme mkoani Mtwara miezi michche iliyopita.

  Kufuatia maagizo hayo ya Rais, Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wake, Dkt. Tito Mwinuka, aliitisha mkutano na waandihi wa habari na kutoa ilani kwa wadaiwa wote “sugu” wa bili za umeme kuwa walipe madeni yao vinginevyo huduma ya umeme itasitishwa.

  Baada ya tangazo hilo, baadhi ya taasisi za serikali likiwemo Jesho la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, kupitia kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo, naye aliitisha mkutano na wanahabari na kueleza kuwa JWTZ italipa sdeni lake na kuagiza wahusika wafanye hivyo mara moja.

  Leo hii Mei 4, 2017, Meneja wa TANESCO mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali, aliwaita waandishi wa habari ofisini kwake na kuwaeleza kuwa taasisi za umma na binafsi zilizo katika mkoa wake, zilikuwa zikidaiwa jumla ya shilingi Bilioni 7, ambapo taasisi za serikali pekee zilikuwa na deni la  shilingi bilioni 6 na kwa sasa tayari zimelipa jumla ya shilingi bilioni 2 na kubaki deni la shilingi bikioni 4.

  “Hizi taasisi za umma tumeingia nazo mkataba na kwakweli wameanza kulipa na tunaendelea kuwahimiza wafanye hivyo ili wasije kukosa huduma ya umeme.” Alisema Mhandisi Nangali.

  Aidha alisema taasisi binafsi zinadaiwa shilingi Bilioni 1 na nyingi kati ya hizo hazijaingia mkataba wa malipo ya madeni yake na TANESCO kwa hivyo akatahadharisha kuwa TANESCO haitasita kuchukua hatua za kusitisha huduma ya umeme na kwa kuonyesha kuwa Shirika halifanyi mzaha, leo hii kampuni mbili moja ikimilikiwa na mfanyabiashara maarufu Fida Hussein iliyoko Vingunguti wilayani humo imesitishiwa huduma ya umeme kufuatia deni la shilingi Milioni 29.

  Kampuni nyingine iliyoonja joto ya jiwe ni Iprint iliyoko eneo la Banda la Ngozi kandokando ya barabara ya Nyerere, kampuni hiyo hadi kufikia leo Mei 4, 2017 ilikuwa ikidaiwa jumla ya shilingi Milioni 16,95.
  Maafisa wa TANESCO waliokuwa kwenye operesheni ya “kukata” umeme kwa wadaiwa sugu, walikuwa na stakabadhi zinazoonyesha kuwa kufikia leo Mei 4, 2017 kampuni hizo mbili zikikuwa zikidaiwa madeni hayo.  

   Mfanyakazi wa TANESCO kivaa gloves tayari kukata umeme
   Meneja wa TANESCO mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, Mhandisi Athanasius Nangali, (kulia), akiwa na Afisa kutoka idara ya fedha TANESCO makao makuu, akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Mei 4, 2017.
   Mhandisi wa kudhibiti mapato TANESCO mkoa wa Ilala, Daniel Kimaro, akizungumza na waandishi baada ya kusitisha huduma ya umeme kwenye kampuni ya Iprint.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Klabu ya Rotary nchini uangalie uwezekano wa kuisaidia Serikali kupambana na ugonjwa wa Malaria.

  Waziri Mkuu Majaliwa ambaye leo hii (Alhamisi, Mei 4, 2017) amekuwa mwanachana wa 651 kujiunga na klabu hiyo,  ametoa wito huo wakati akifungua mkutano wa 92 wa mwaka wa Rotary unaojumuisha nchi za Uganda na Tanzania (District 9211) katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.

  "Ninatambua kazi nzuri inayofanywa na Rotary Club katika kuisaidia jamii kwa vile na mimi mwenyewe nimekuwa nikisaidia jamii. Kwa hiyo mimi na mke wangu Mary Majaliwa tunajiunga tukiwa ni wanachama wa 651 na 652 ili kuongeza nguvu ya Rotary kusaidia jamii," alisema huku akishangiliwa na washiriki zaidi ya 1,000 waliohudhuria mkutano huo kutoka Uganda, Tanzania, India, New Zealand na Australia.

  Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa klabu hiyo uongeze mikakati ya kutangaza kazi wanazozifanya ili kuondoa dhana iliyojengeka miongoni mwa watu wengi kwamba wanaojiunga na klabu hiyo ni watu matajiri na watu maarufu.

  "Kazi mnazozifanya ni kubwa na nzuri mno kwa jamii. Lakini itabidi mjitangaze zaidi ili watu wengi zaidi watambue kazi zenu na waweze kuwaunga mkono," alisema.

  Waziri Mkuu aliahidi kuwashawishi viongozi wengine wa Serikali, taasisi za umma pamoja na Wabunge wajiunge kwa wingi na klabu hiyo. Tanzania ina klabu za Rotary 36 zenye wanachama 650 wakati Uganda ina klabu za Rotary 93 zenye wanachama 2,700. Tanzania na Uganda zinaunda District 9211 katika mfumo wa kimataifa wa rotary.

  Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwapongeza wana-Rotary kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kusaidia jamii hasa kwenye sekta za maji, elimu, na afya.

  Alisema Rotary inatambulika duniani kwa kampeni yake ya kutokomeza ugonjwa wa polio; na kupitia michango ya wana-Rotary, Tanzania hivi sasa haina mgonjwa yeyote wa polio.

  "Licha ya uchache wenu, natambua mchango mkubwa unaotolewa na Rotary Club hapa nchini. Hivi karibuni, Rotary Club saba ziliungana na Benki M na kujenga hospitali kubwa ya watoto pale Muhimbili (MNH) na Kituo cha Ujasiriamali kwa Vijana pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)," alisema.

  "Miradi mingine inayofadhiliwa na Rotary Club ni ujenzi wa hospitali ya akinamama wajawazito mkoani Dodoma, utoaji wa vitabu vya ziada 20,000 kwenye shule za sekondari zaidi ya 40 mkoani Tanga pamoja na miradi ya maji safi kwenye  wilaya za Same na Mwanga mkoani Kilimanjaro.

  Kwa upande wake, District Gavana wa Rotary 9211 ambaye anamaliza muda wake, Bw, Jayesh Asher wana-Rotary duniani wanaamini kwamba Serikali za nchi mbalimbali haziwezi kutekeleza majukumu yote kwa wananchi wake kwa hiyo wanajiunga na kutoa rasilmali zao ili kusaidia jamii zenye uhitaji.

  Akizungumzia kuhusu uchahe wa wanachama hapa nchini, Bw. Asher alisema Rotary Club ya Uganda imepata umaarufu kwa sababu viongozi wengi wamejiunga na klabu hiyo wakiwemo Mawaziri, Spika wa Bunge la Uganda, wabunge na mabalozi.

  “Hapa Tanzania itabidi tutangaze zaidi kazi zetu ili tuweze kuwavuta viongozi wa kisiasa na wa umma na pia kuongeza wanachama zaidi,” alisema.

  Mkutano huo wa siku tatu, utamalizika Juni 6, mwaka huu.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa 92 wa mwaka wa Rotary unaojumuisha nchi za Uganda na Tanzania (District 9211) katika ukumbi wa AICC jijini Arusha Mei 4, 2017.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akivishwa beji ya uanachama wa Rotary Club na Dk. Manoj Desai kwenye mkutano wa 92 wa mwaka unaojumuisha nchi za Uganda na Tanzania (District 9211) katika ukumbi wa AICC jijini Arusha Mei 4, 2017.
  aziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Rotary Club kwenye mkutano wa 92 wa mwaka unaojumuisha nchi za Uganda na Tanzania (District 9211) katika ukumbi wa AICC jijini Arusha Mei 4, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Serikali iko katika hatua za mwisho za kukamilisha mradi wa kufunga Taa za kuongozea ndege ili kuruhusu Uwanja wa Ndege wa Dodoma kuweza kutumika masaa 24. Akizungumza hayo mjini Dodoma mara baada ya kukagua Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light) zilizofungwa uwanjani hapo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema kuwa hatua hiyo ni muendelezo wa uboreshaji wa uwanja huo katika kuruhusu ndege za aina zote kutua masaa 24 kwa wiki.

  “Hii ni hatua ya pili ya uboreshaji wa uwanja huu ambapo hatua ya kwanza tumeimaliza ya upanuzi wa barabara za kuruka na kutua ndege (runway) hadi kufikia KM 2.5”, amesema Waziri Profesa Mbarawa. Aidha, ameongeza kuwa ufungaji wa taa hizo umegawanywa kwa hatua tatu ambapo awamu ya kwanza imekamilika kwa kujumuisha ufungaji wa Mfumo wa Kisasa wa Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light), katika barabara za kuruka na kutua ndege na maeneo ya maegesho, hatua ya pili ni kufunga taa za kumsaidia Rubani kuweza kuona uwanja wote na hatua ya mwisho ni taa zitakazofungwa mita 400 kila upande uwanjani hapo.

  Amefafanua kuwa Taa hizo za kisasa (Aviation Solar Powered Light) zitapunguza gharama za uendeshaji uwanjani hapo ikiwemo matengenezo yake kwani zinadumu muda mrefu. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara, Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho, amesema kuwa nia ya Serikali ni kuendelea kurefusha uwanja huo ambapo italipa fidia kwa nyumba zilizopo pembeni ya uwanja huo ili kuongeza usalama wa uwanja na ndege kwa ujumla.

  “Tutaweka uzio katika uwanja huu kulingana na matakwa ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na pia kupitia uzio huu taa zitakuwa salama”, amesisitiza Dkt. Chamuriho. Naye, Msimamizi wa mradi Bw. Samwel Mruma kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), amesema mfumo wa taa hizo za kisasa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light), zimefungwa kwa siku 14 na zina uwezo wa kufanya kazi kwa miaka 12 na kuwaka kwa masaa laki moja ukilinganisha na nyingine ambazo zinawaka kwa masaa elfu kumi.

  Mfumo wa uwekaji Taa za Kisasa ni mkakati wa Serikali katika kuhakikisha inaendelea kuboresha viwanja vyake vya ndege ili kukidhi viwango vianavyostahili katika usafiri wa anga.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa mradi Bw. Samwel Mruma kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), wakati alipokagua mfumo wa Kisasa wa Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light), zilizofungwa katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara, Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho na kulia ni Meneja wa Uwanja huo Julius Mlungwana.
  Msimamizi wa mradi Bw. Samwel Mruma kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), akionesha Taa za Kisasa za Umeme Jua (hazipo pichani), kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), zilizofungwa kwa ajili ya kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akionesha kifaa (Remote Controller) cha kuwashia Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light), zilizofungwa katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma kwa waandishi wa habari, wakati akikagua Taa hizo uwanjani hapo.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara, Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho (katikati), na Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Leonard Chimagu (kushoto), wakati alipokagua mfumo wa kisasa wa Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light), katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma.
  Muonekano wa Mfumo wa Kisasa wa Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light), zilizofungwa katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma. Taa hizo zitatumika kuongozea ndege nyakati za Usiku na zina uwezo wa kuwaka masaa laki moja.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ina mkakati wa kufanya Majiji yote nchini yawe na barabara za viwango vya kimataifa na zinazopitika kwa urahisi.

  “Tumeanza kujenga barabara za kisasa katika jiji la Arusha ambalo ni jiji la utalii, tutakwenda Mwanza na Dar es Salaam kwa kujenga barabara zenue njia za juu (flyovers) zikiwemo za magari na za waenda kwa miguu,” amesema.

  Ametoa kauli hiyo Alhamisi, Mei 4, 2017 wakati akizumngumza na wananchi wa Tengeru, wilayani Arumeru, mkoani Arusha mara baada ya kukagua barabara ya Sakina- Tengeru yenye urefu wa km. 14.1 ambayo itakuwa na njia nne za magari.

  “Nimekuja kukagua ujenzi wa barabara hii ya Sakina hadi Tengeru lakini mkandarasi akimaliza anajenga barabara nyingine ya kilometa 42.1 na hivyo hapa Arusha tutakuwa na kilometa 56.5 za awamu ya kwanza,” alisema.

  Alisema maboresho ya barabara za Jiji la Arusha yanafanyika ili kuwezesha wafanyabiashara kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi na viwanda vitakapoanza kujengwa, itakuwa hawana shida ya mawasiliano.

  Akizungumzia tatizo la uhaba wa ardhi aambalo lililibuliwa na mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari, Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw, Mrisho Gambo aendelee na zoezi la kuuzungukia mkoa wake ili kubaini maeneo yenye matatizo sugu.

  Mapema, akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo kwa Waziri Mkuu, Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Eng. Mgeni Mwanga alisema ujenzi wa barabara hiyo ambao ulianza Juni 2015, unatarajia kukamilika Juni 2018.

  “Ujenzi wa barara ya Sakina –Tengeru ni wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa km. 230 ya kutoka Arusha –Holili- Taveta –Voi ambayo ujenzi wake unatarajiwa kugharimu sh. bilioni 139.34. Ujenzi huo unagharimiwa na Serikali ya Tanzania pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

  Sambamba na barabara hiyo, Eng. Mwanga alisema mkandarasi wa barabara hiyo ataanza kujenga barabara nyingine ya km. 42.1 inayoanzaia Usa River hadi Kisongo kwa kiwango cha lami ambayo itakuwa na madaraja saba wakati ile ya Sakina hadi Tengeru ina madaraja makubwa mawili.

  Naye mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari alisems uhaba wa ardhi bado ni tatizo kubwa kwenye wilaya hiyo kiasi kwamba hawana hata eneo la kujenga shule au zahanati.

  “Maeneo yote yameuzwa na wenyeviti wa vijiji na madiwani, hivi sasa ukitaka kujenga shule au zahanati hakuna eneo hata moja. Mheshimiwa Waziri Mkuu tunaomba utusaidie kufuatilia suala hilo licha ya kuwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi alishakuja na kuelezwa hali halisi ilivyo,” alisema.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa maelekezo Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Eng. Mgeni Mwanga juu ya upandaji nyasi kwenye eneo la katikati ya barabara wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei 4, 2017.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari wakati alipokwenda kukagua ujenzi wa barabara ya Sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei 4, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, bw. Mrisho Gambo.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Cheil Engineering ambayo inajenga barabara ya Sakina-Tengeru, Bw. Shin Pil Soo (wa pili kushoto). Kulia ni Mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari na wa pili kulia ni Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Eng. Mgeni Mwanga.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa tahadhari juu ya gema lililopo kwenye daraja la mto Ndoruma mara baada ya kukagua ujenzi wa daraja hilo katika barabra ya kutoka sakina hadi Tengeru jijini Arusha, Mei 4, 2017. Kushoto kwake ni Meya wa Arusha, Bw. Calist Lazaro. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0
  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Joelson Mpina anakumbuka siku yake ya kuzaliwa Leo.Heri ya siku ya Kuzaliwa Mhe. Mpina Mungu akupe Maisha Marefu.

older | 1 | .... | 1670 | 1671 | (Page 1672) | 1673 | 1674 | .... | 3285 | newer