Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

KIKOSI KAZI CHA KUNUSURU IKOLOJIA YA MTO RUAHA CHATEMBELEA BONDE LA IHEFU

$
0
0
 Wajumbe wa Kikosi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha (kikundi namba 2) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakisubiri kupanda boti ya upepo ili kutembelea eneo la bonde la Ihefu lililoko Mbalari- Mkoani Mbeya kugagua ikolojia ya Bonde hilo.
 Wajumbe wa Kikosi kazi wakiwa ndani ya boti katikakti ya bonde la Ihefu wakiakagua ikolojia ya bonde hilo. Kuanzia kulia ni Mkurugenzi Tume ya Umwagiliaji Injinia Seth Lusweme, Mkurugenzi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Richard Muyungi na Mkurugenzi wa Bonde la Rufiji Idris Msuya.
 Afisa Mkuu toka TANAPA Kanda ya Arusha Vitalis Uruki akiongea na Wanahabari mara baada ya ziara ya kikosi kazi katika bonde la Ihefu katika Wilaya ya Mbalari Mkoani Mbeya.



Picha ikionyesha hali ya ikolojia katika bonde la Ihefu inavyoonekana kwa sasa

RAIS MAGUFULI AONGOZA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO WA TANZANIA

$
0
0

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika gari maalum na kuwapungia mkono Wananchi mbali mbali wa Mji wa Dodoma wakati wa sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri. Kulia kwake ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Salvatory Mabeho.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. 
Kulia kwake ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Salvatory Mabeho.
Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ, pamoja na Wananchi mbali mbali wa Mji wa Dodoma wakiwa katika Uwanja wa Jamhuri,wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika leo,Mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanzania katika Uwanja wa Uhuru zilizofanyika leo,ambapo Mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.Picha na Ikulu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na mjane wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume pamoja na mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono ya pongezi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na walioshiriki katika zoezi la kuchanganya udongo kuasisi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. Wananchi hao ni Bw. Hassan Omary Mzee (hayupo pichani), Bw. Hassaniel Elisael Mrema (kushoto), Bi. Sifael Kunda Shuma (anayepewa mkono) na Bi. Khadija Abbas Rashid 
Gadi ya “Komando” la vijana likiwajibika kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Onesho la ndege vita kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma 
Onesho la mbwa wa polisi kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma 
Onesho la Komandoo wawili kuvuta lori la tani 7 kwa mikono kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Kikosi cha Komandoo cha  JWTZ kikitoa heshima kwenye sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma


PICHA NA IKULU

HOTUBA YA RAIS DKT MAGUFULI KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA MUUNGANO MJINI DODOMA

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS APRIL 27,2017

WAAJIRI TEKELEZENI SHERIA YA KAZI ILI KULINDA HAKI ZA WAFANYAKAZI-NAIBU WAZIRI MAVUNDE.

$
0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.


Waajiri wote nchini yakiwemo makampuni ya Madini wametakiwa kutekeleza matakwa ya Sheria ya kazi kwa lengo la kulinda haki za wafanyakazi.


Hayo yamesemwa na Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira Kazi na watu wenye Ulemavu  Mhe. Anthony Mavunde wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge leo Mjini Dodoma.


“Makampuni haya yana wajibu mkubwa wa kulinda haki za wafanyakazi,kupunguza migogoro isiyo ya lazima sehemu za kazi na kuongeza tija na uzalishaji mahala pa kazi.”Aliongeza Mhe.Mavunde.


Aidha amesema Ofisi yake imeendelea kutekeleza majukumu yake ya usimamizi wa Sheria kwa kufanya kaguzi sehemu za kazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa waajiri wanazingatia matakwa ya Sheria,elimu ya Sheria za kazi inatolewa kwa waajiri,wafanyakazi na vyama vyao ili kuongeza uelewa wao katika kutekeleza Sheria.


Kuhusu ukaguzi wa mikataba kwa kampuni zinazofanya kazi migodini amesema  Serikali iliunda kikosi ambacho kilishirikisha Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,NSSF,SSRA,OSHA ,Mamlaka ya Mapato Tanzania na Wakala wa Ukaguzi wa Madini.


Amesema kikosi kazi hiki kilipewa jukumu la kufanya ukaguzi wa kina kwenye migodi iliyopo kanda ya ziwa na kaskazini kwa lengo la kuangalia hali halisi ya utekelezaji wa Sheria za kazi,afya na usalama mahali pa kazi,masuala ya hifadhi ya jamii,fedha na kodi.


Pamoja na hayo amesema kuwa Serikali inatambua umhimu wa uwekezaji katika kukuza fursa za ajira kwa watanzania na kuchangia kukua uchumi kwa ujumla.


“Serikali itaendelea kusimamia sheria za kazi ili kuhakikisha kuwa waajiri wote nchini wanatimiza wajibu wao na wawekezaji wamepata nafasi ya kuwekeza na kuchangia kukua kwa uchumi wa nchi yetu kwa kufuata sheria zilizoko nchini”Alisisitiza Mhe.Mavunde.

YANGA KUIFUATA MBAO BILA NYOTA WAO WATATU WA KIMATAIFA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MABINGWA watetezi wa kombe la Shirikisho la Azam HD Yanga wanaondoka jioni ya leo kuelekea Jijini Mwanz akwa ajili ya mchezo wa nusu fainali ya kombe hilo dhidi ya Mbao FC.

Yanga wanatarajia kuvaana na Mabo Jumapili ya April 30 katika Uwanja wa CCM Kirumba ikiwa ni nusu fainali ya pili ambapo mchezo wa kwanza utakuwa ni baina ya Simba na Azam utakaofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa Jumamosi.

Msafara wa wachezaji utaondoka majira ya saa 11 jioni smabamba na benchi la ufundi na viongozi wakitumia usafiri wa anga kwa ndege ya shirika la ndege la ATC.

Wakitoa taarifa hiyo kupitia Kitengo cha habari na mawasiliano ya klabu hiyo, msafara wa wachezaji wa Yanga utakuwa na jumla ya wachezaji 21 huku wakiendelea kuwakosa noya wao kadhaa akiwemo Mzimbabwe Donald Ngoma, Vicent Bossou, Justine Zullu walio majeruhi, Malimi Busungu, Pato Ngonyani na Yusuph Mhilu.

Deogratius Munishi ,Beno Kakolanya na Ally Mustapha. Nafasi ya ulinzi ni ; Nadir Haroub,Vicent Andrew, Oscar Joshua , Juma Abdul , Mwinyi Haji, Hassan Kessy na Kelvin Yondani. Wachezaji watakao ondoka ni Makipa ni 

Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deusi Kaseke,Said Makapu, Juma Mahadhi, Saimoni Msuva, Geofrey Mwashuiya na Emmanuel Martin. 

Katika nafasi ya viungo ni pamoja na Upande wa safu ya washambuliaji itaongozwa na ni Amissi Tambwe , Matheo Antony na Obrey Chirwa.





MBUNGE WA KIBAHA VIJIJINI AENDELEA KUTEKELEZA AHADI KWA VITENDO JIMBONI KWAKE

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa (kushoto) akisaidia kushika kamba kwenye maandalizi ya awali ya ujenzi wa soko Mlandizi.

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha Vijijini

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Mkoani Pwani, Hamoud Jumaa, amesema 2017/2018 anajikita kutekeleza ahadi na vipaumbele alivyojiwekea kwenye za huduma za kijamii hasa afya, elimu na soko. Katika utekelezaji huo, ameanza maandalizi ya kujenga soko la Mlandizi awamu ya kwanza litakalogharimu kiasi cha mil. 180 hadi kukamilika kwake. 

Jumaa alisema watafanya ujenzi kwa awamu ambapo awamu ya kwanza itagharimu mil. 50. Alieleza kuwa, soko la Mlandizi ni soko linalotegemewa na wakazi wengi wa mji huo hivyo kuna kila sababu kulijengea mazingira bora na kuwa la kisasa. Aidha Jumaa alisema ,wafanyabiashara wamejipanga kumuunga mkono kwa kuchangia sh. 5, 000 kila mmoja ambazo zitakuwa zikichangishwa kupitia ofisi ya soko. 

"Simaanishi kuwa hakuna kero nyingine lakini ninafanya kwa awamu na mengine ninatekeleza pale napopata fedha ama wafadhili na wadau mbalimbali "alisema Jumaa. 

Jumaa alibainisha, masuala hayo ni utekekelezaji wa ilani ya CCM na atahakikisha hadi ifikapo 2020 awe amemaliza ahadi zake na vipaumbele alivyojiwekea.  Mbunge huyo alisema, ni jukumu lake kuwatumikia wananchi na aliwaomba washirikiane kwa kufuata kauli mbiu yake ya SISI KWANZAA SERIKALI BAADAE. 
Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa, akishiriki kuchimba mashimo ya maandalizi ya ujenzi wa soko Mlandizi.

WAZIRI UMMY ASISITIZA WANAFUNZI WANAOPATA UJAUZITO WAENDELEE NA MASOMO

$
0
0
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesisitiza kuwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa mashuleni waendelee na masomo yao ili kufikia malengo walioyanayo nchini.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa maswala ya kijinsia ulioandiliwa na Chuo Cha Ualimu (DUCE) alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri8 ya Muungano waq Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo jijini Dar es salaam.

“Tunapokataza watoto wa kike wasiendelee na masomo pindi wanapopata ujauzito wakiwa mashuleni tunawaadhibu watoto wa masikini washindwe kutimiza malengo yao kwa wakati waliotarajia”alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa anaunga mkono uamuzi wa Rais wa Tanzania Dkt. Jonh Pombe Magufuli kwa kutoa elimu bure nchini kwani kunaongeza idadi ya watoto wa kike kuwepo mashuleni tofauti na kipindi cha nyuma.

Mbali na hayo Waziri Ummy ametoa wito kwa wazazi kuwahamasisha watoto wao wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kukuza rasilimali watu katika kujenga uchumi unaotokana na viwanda nchini.

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha DUCE Prof. William Anangisye amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kuleta chachu ya kuwatia moyo wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kupata wanasayansi wanawake nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu akimuwakilisha Makamu wa Raisi Bi Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Masuala ya Usawa wakijinsia ulioandiliwa na Chuo Cha Ualimu (DUCE) jijini Dar Es salaam.
Prof Rwekaza Mukandala Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar Es Salaam akihutubia wadau na wanafunzi waliojitokeza katika mkutano wa kwanza wa masuala ya Jinsia na Usawa yaliyofanyika katika chuo kikuu cha Uwalimu DUCE jijini Dar Es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha DUCE Prof. William Anangisye akihutubia jopo la Wadau na wanafunzi katika mkutano wa masuala ya Usawa na huku akisisitiza wazazi na walezi kuwatia moyo wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kupata wanasayansi wanawake nchini.
Wadau wa Masuala ya Usawa wa kijinsia wakifuatilia kwa ukaribu ujumbe uliokuwa ukitolewa na Mh.Ummy Mwalimu Waziri wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na watoto aliyekuwa akimuwakilisha Makamu wa Raisi Bi Samia Suluhu Hassan katika viunga vya Chuo cha Uwalimu DUCE jijini Dar Es Salaam.
Picha ya pamoja ya wadau wa masuala ya Usawa wakijinsia katika mkutano wa kwanza wa masuala ya Usawa wakijinsia uliowakutanisha kujadili na kuhamasisha juu ya kumlinda mtoto wa kike ili apate Elimu sawa kama ile apatayo mtoto wakiume katika jamii yetu.

Rais Magufuli mgeni rasmi Siku ya Uhuru wa Habari Duniani

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamio.

Rais wa Jamuhuri y Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli anatarajiwa Kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Habari Mei mwaka huu.

Maadhimisho hayo ya mwaka huu, yatafanyikia jijini Mwanza kwa Siku mbili mfululizo kuanzia Mei 2 na 3 mwaka huu yakiwa na maudhui yanayosema fikra yakinifu kwa wakati muhimu'.

Akizungumzia madhimisho hayo, Mwenyekiti wa Misa Tanzania Salome Kitomary amesema lengo la siku hiyo ni kuwakutanisha wadau wa Habari kuweka msukomo wa mataifa kutunga sheria za vyombo vya habari ambazo zinahakikisha Uhuru wa habari katika nchi husika.

 Amesema lengo lingine ni kufikia makubaliano ya kitaifa juu ya kuanzisha utaratibu wa usalama na ulinzi wa wanahabari na wafanyakazi wa vyombo vya habari kwenye mtandao na nje ya mtandao.
Aidha Aliongeza kuwa lengo lingine ni kutetea Sera na mfumo wa mageuzi ya kisheria kwa ajili ya vyombo vya Habari na maendeleo endelevu.

Kwa upande wake makamu wa rais kutoka umoja wa clabu za waandishi Tanzania, UTPC, Janne Mihanji amewataka waandishi wawe ndio wapangaji wa ajenda za taifa badala ya kutumiwa na wanasiasa.
Aidha amewaasa waandishi wakiwa katika maeneo yao kazi, kuchukua tahadhari wakiangalia usalama wao zaidi kwani hakuna habari bora kuliko uhai wa mtu mwenyewe. Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Tanzania, Salome Kitomari akizungumza kwenye mkutano wa wanahabari kutambulisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Tanzania, Salome Kitomari akizungumza kwenye mkutano wa wanahabari kutambulisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Makamu Rais wa UTPC, Bi. Jane Mihanji na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandushi Dar es Salaam akizungumza katika mkutano wa wanahabari kutambulisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanahabari na wageni waalikwa wakiwa katika mkutano na Kamati ya maandalizi ya WPFD-2017 kutambulisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

SALUM MKEMI KIKAANGONI APRIL 30,AITWA KAMATI YA NIDHAMU YA TFF

$
0
0
Mjumbe wa kamati ya Utendaji wa Yanga Salum Mkemi (kulia) akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mjumbe wa kamati ya Utendaji wa Yanga, Salum  Mkemi ameitwa mbele ya kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kujibu tuhuma zinazomkabili dhidi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPBL).

Kwa mujibu wa barua hiyo, Mkemi anakabiliwa na tuhuma za kuishutumu bodi ya ligi na kuidhalilisha kamati ya utendaji na usimamizi wa kanuni wa ligi (kamati ya saa 72) ya bodi ya ligiu kuwa inaendeshwa kwa unazi na imegubikwa na rushwa katika kushughulikia suala la kadi tatu za njano kwa mchezaji Mohamed Fakhi.

Mbali na kamati, shutuma hizo pia alizielekeza kwa TFF na kuwa na kudai kuwa tayari amesharipoti suala hilo Taasisi ya kuzuaia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU ili kuwachunguza viongozi wa TFF na kamati hiyo.

Kikao hicho kitakachokaliwa siku ya Jumapili kitatoa maamuzi kulingana na utetezi wa Mkemi kutokana na tuhuma zake pia atahitajika kwenda na ushahidi wake atakaouwasilisha mbele ya kamati ya nidhamu.

MASHABIKI WA YANGA NA SIMBA KUKIPIGA DUBAI KATIKA SHEREHE ZA MUUNGANO

$
0
0
Assalam aleykum ndugu Watanzania wote muishio UAE.
Naomba kuwalika wote kwenye shughuli yetu ya kusherekea sikukuu ya Muungano itakayo fanyika pale Al Ahly club mjini  Dubai siku ya Jumamosi tarehe: 29/04/2017 saa mbili unusu (8:30pm).
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi na pia Bi Samira Diria Balozi mdogo kutoka ubalozini Abu Dhabi atakuwepo. Kwenye sherehe hizo tutacheza friendly match  ya Simba vs Yanga wa Dubai. Pamoja na hayo kutakuwa na chakula, BBQ na kadhalika. KARIBUNI WOTE

- MRATIBU MKUU
 Yanga ya Dubai
 Simba ya Dubai
Wachezaji wa Simba ya Dubai

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 27.04.2017

SONGWE WAJIPANGA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI MAPYA YA UKIMWI

$
0
0
Serikali ya Mkoa wa Songwe imeanza kuchukua hatua madhubuti kwa lengo la kupambana na changamoto zinazotokana na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi ili kuweza kufikia malengo ya taifa baada ya kuanza kutekeleza mwongozo mpya wa matibabu kwa wote wanaogundulika na VVU kuanzia Oktoba 2016.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Ndg. Eliya Ntandu katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. John Ernest Palingo kwenye kikao cha wadau wa afya kilicholenga kutambulisha mradi unatoa huduma mbalimbali za kupunguza maambukizi ya ukimwi ujulikanao kama SAUTI unaofadhiliwa na shirika la Misaada ya Kimataifa ya Maendeleo la Marekani(USAID) na kutekelezwa na shirika la Jhpiego.

Akielezea Mradi wa SAUTI katika Mkoa wa Songwe, Mhe. Palingo amesema anatambua malengo ya mradi huu kuwa ni kusaidia jitihada za serikali katika kuboresha afya za wananchi na kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ambapo mkoa wa Songwe ni wanufaika wakubwa kupitia wilaya mbili za Mbozi na Tunduma ambako mradi huu unatekelezwa.

“Mradi huu utasaidia sana kupunguza hatari za maambukizi ya Ukimwi katika makundi maalum yenye hatari zaidi ya kuambukiza au kuambukizwa VVU hususani wanawake wanaoanya biashara ya ngono, Vijana wa Kike nje ya shule walio katika mazingira tete kama ilivyoanishwa katika mwongozo mpya wa serikali wa 2017 unaosimamia huduma za VVU na Ukimwi kwa makundi maalum” alisema Mhe. Palingo
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. John Ernest Palingo akifungua kikao cha wadau wa afya Mjini Songwe kilicholenga kutambulisha mradi unatoa huduma mbalimbali za kupunguza maambukizi ya ukimwi ujulikanao kama SAUTI unaofadhiliwa na shirika la Misaada ya Kimataifa ya Maendeleo la Marekani(USAID) na kutekelezwa na shirika la Jhpiego.
Mkurugenzi wa mradi wa SAUTI Dkt. Albert Komba akiwasilisha mada kuhusu Mradi wa Sauti ambao ni Mradi wa miaka mitano unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) kupitia Mpango wa dharura wa raisi wa Marekani kwa ajili ya UKIMWI (PEPFAR) katika kikao cha wadau wa afya kwa lengo la kuutambulisha mradi huo.
Mratibu wa kudhibiti Ukimwi kutoka TACAIDS katika Mkoa Songwe Ndg. Emanuel Petro akiwasilisha mada kuhusu mikakati ya Mkoa katika mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI, Mafanikio na changamoto katika kikao hicho.

WAZIRI LUKUVI AANZA KUBAINI WADAIWA WA KODI YA PANGO LA ARDHI

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi amefanya ukaguzi wa mfumo wa kodi ya ardhi katika manispaa ya Musoma Mjini mkoa wa Mara ambapo amebaini wananchi 231 wanadaiwa Kodi ya Pango la Ardhi kiasi cha shilingi milioni 271.

Mhe Lukuvi amemtaka Afisa Ardhi wa manispaa ya Musoma bwana Joseph Kamonga kuwasilisha majina ya wadaiwa hao katika Mahakama ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupiga mnada majengo na mali zao kawa wakikaidi kulipa kodi hiyo.

“Nimeagiza kesi za madai ya kodi zitolewe hukumu ndani ya siku moja tu ili wadaiwa waweze kuchukuliwa hatua ya kuuzwa kwa mali zao haraka” Mhe Lukuvi aliyasema hayo wakati alipo fanya ziara ya kukagua mfumo wa kodi wa manispaa ya Musoma mjini ili kuhakikisha wamiliki wote wa ardhi nchini wanalipa kodi kwa hiari kabla ya hatua za kisheria hazijafuata dhidi yao.

Aidha, Waziri Lukuvi amefanya uzinduzi wa mpango kabambe (Master Plan) wa Manispaa ya Musoma na kuwapongeza viongozi na watendaji wa manispaa ya Musoma kwa kuwa manispaa ya kwanza nchini kuweza kuzindua mpango kabambe wa mji wao. Pia aliwapongeza kwa uzalendo wao wa kutumia kampuni za ndani katika utekelezaji wa mpango huo.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akikagua mfumo wa kodi wa Manispaa ya Musoma Mkoani Mara. Kushoto kwake Afirsa Ardhi wa Manispaa hiyo Ndugu Joseph Kamonga akimuonesha mfumo wa kodi unavyofanya kazi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akikambidhi Mpango Kabambe wa Manispaa ya Musoma Meya wa Manispaa ya hiyo Mh. Patrick Gumbo.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akizindua Mpango Kabambe (Master Plan) Manispaa ya Musoma Mkoani Mara.

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akiongea na viongozi na wananchi wa Manispaa ya Musoma katika uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Manispaa hiyo.

Baadhi ya Wananchi na Watendaji wa Manispaa ya Musoma wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi katika uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Manispaa hiyo mkoani mara. 

IVORY BAND YAPANIA KUPAA KATIKA ANGA ZA KITAIFA NA KIMATAIFA

$
0
0
Ijumaa hii na kila Ijumaa ni siku ya raha na starehe kwa wakazi wa Tabata na vitongoji vyake, maana mara tu baada ya jua kuzama kiota maarufu cha NEXT DOOR kilichopo katika kitongoji hicho cha wastaarabu huwaka moto wa midundo ya aina mbalimbali inayoporomoshwa na IVORY BAND iliyosheheni vipaji visivyo vya kawaida. 

Ripota wa Globu ya Jamii alipotembelea hapo katika ukumbi wa NEXT DOOR Ijumaa hakuweza kuamini macho na masikio yake kukuta ukumbi umefurika mashabiki wakipata burudani toka kwa vijana hao. Akaamua kuhoji wahusika. 

“Bendi hii tulianzisha mwaka jana (2016) mwezi wa tano na wamiliki wake ni sisi wanamuziki wenyewe tukishirikiama na wenzetu kadhaa ambao tumewaajiri”, alisema mmoja wa wamiliki wa IVORY BAND, Rama Pentagone, wakati wa mapumziko mafupi. Alisema waliamua kujiita IVORY BAND sababu ya kuangalia jina fupi litalokuwa rahisi kushikika na pia hakuna asiyefahamu thamani ya "IVORY" (Pembe ya ndovu).
Pentagone, anayepiga kinanda, gitaa na kuimba alisema wamiliki wa bendi hiyo ni yeye, mwanamuziki mkongwe mwenye sauti tamu Saleh Kupaza, Omari Kisila na Amina Juma. “IVORY BAND bado hatujatoa mtindo wa kutumia kwa sababu sisi tunapiga muziki tofauti na wengie wengine, hasa ukizingatia kwamba hatupigi “Sebene”, alisema Pentagone. 

Saleh Kupaza aliyekuwa pembeni akipoza koo na maji alisema hatua ya kwanza ya kuanzisha bendi na kujiajiri wao wenyewe imefanikiwa kwa asilimia 100, na kwamba sasa wako katika hatua ya pili ambayo ni kuazalisha nyimbo kibao zenye mtazamo wa kitaiafa na kimataifa. 
“Malengo yetu ya mbeleni ni kuwa kundi la muziki la Kimataifa na endapo Mungu atatujalia kutimiza malengo yetu ni kufanya maonesho makubwa ndani na nje ya nchi”, alisema Kupaza. 


Omari Kisila akaongezea kwamba kwa kuwa inakaribia watimize mwaka mmoja toka waanze rasmi, IVORY BAND imepanga kufanya bonge la onesho litakaloandamana na sherehe za bendi hiyo kutimiza mwaka mmoja mnamo mwezi wa Julai. 

“Tumeamua kufanya onesho hilo kabambe mwezi wa Saba kwa sababu mwezi Mei na Juni utakuwa ni Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Mei na kumalizikia mwezi Juni”, alisema Kisila. 
Amesema ukumbi pamoja na tarehe rasmi ya kufanyika tukio hilo vitatangazwa muda utapokaribia, na kwamba kwa sasa wako katika hatua za mwisho za kuanza kupasua anga za redio na TV kwa kutoa kibao chao cha utambulisho kiitwacho SHIKA MOYO unachokisikia hapo chini. Hicho ni moja ya vibao takriban kumi ambavyo husisimua mashabiki kila wapigapo.

ALPHONCE SIMBU ATINGA BUNGENI-BUNGE LAZIZIMA KWA SHANGWE

$
0
0
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo tarehe 27 April limezizima kwa nderemo na shangwe pale alipotambulishwa rasmi mwanariadha Alphonce Simbu, Mshindi wa medali ya dhahabu wa Mumbai Marathon, na moja ya washindi wa London Marathon.

Mwanariadha huyo ambaye pia ni balozi maalum wa DStv, alilitembelea Bunge kama mgeni maalum wa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Harison Mwakyembe akiambatana na muwakilishi wa DStv Johnson Mshana na maafisa kadhaa waandamizi wa Jeshi la kujenga Taifa akiwemo Kanali K.J Mziray – Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa JKT

Mara baada ya naibu spika wa Bunge Dk. Tulia Akson kumtaja Simbu, bunge lilizizima kwa shangwe kwa muda hali iliyoashiria kuraha kubwa kwa wabunge kuweza kumshuhudia mwanariadha huyo ambaye ni tegemeo kubwa la Tanzania katika mashindano ya riadha ya Dunia yatakayofanyika mwezi Agosti mwaka huu jijini London.

Baada ya ziara hiyo, Simbu alipata fursa ya kusalimiana na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa na kisha kuwa na mazungumzo mafupi na Waziri Mwakyembe.

Akiongea wakati wa kupiga picha ya pamoja na Simbu, Waziri mkuu Kassim Majaliwa alimpongeza sana mwanariadha huyo na kusema kuwa Serikali inatambua na kuthamini sana jitihada zilizofanywa na wadau wote katika kufanikisha ushindi wa Simbu. Pia alimtakia kila la heri katika maandalizi na kisha ushiriki wake katika mashindano ya Dunia yanayomkabili mwishoni mwa mwaka huu.

Naye Waziri mwenye dhamana ya Michezo Harison Mwakyembe ambaye ndiye aliyemualika Simbu Bungeni, alisema kuwa wizara imekuwa ikishirikiana na wadau kwa karibu ambapo hata wakati wa Safari ya Simbu kwenda London, wizara ilihakikisha safari hiyo inafanikiwa. Ameonyesha kufurahishwa kwake na vipaji vilivyopo na kusema nguvu za ziada zitawekwa ili kuhakikisha kuwa vipaji hivyo vinaibuliwa na kukuzwa kwa manufaa ya taifa zima.

Kwa upande wake, Simbu alisema kitendo cha yeye kualikwa bungeni kimempa faraja kubwa na pia alifurahi sana kuona jinsi wabunge walivyomshangilia na kumpongeza. “Kwakweli ujio wangu bungeni umenipa faraja kubwa kuona ni jinsi gani wabunge wote walivyofurahishwa na mafanikio niliyopata na sifa niliyoiletea nchi. Hii imenipa sana moyo na uzalendo kwani ni dhahiri kuwa taifa zima liko nyuma yangu na linanunga mkono kikamilifu” alisema Simbu

Alitoa shukrani za pekee kwa wadhamini wake DStv, pamoja na Waziri Mwakyembe kwa jitihada kubwa anazofanya. Amesema anaamini kwa mwenendo huu yeye, wanariadha wengine na wanamichezo wote wa Tanzania watafika mbali na hatimaye Tanzania itakuwa kinara katika ulingo wa michezo duniani. Pia alilishukuru Jeshi la Kujenga Taifa JKT kwa kumruhusu kufanya mazoezi na kushiriki katika mashindano mbalimbali.

Simbu ambaye ni miongoni mwa wanariadha bora wa Tanzania alivunja rekodi yake aliyoiweka mwaka jana nchini Japan ya muda wa 2:09:19 na hatimaye katika mashindano ya London Marathon mwaka huu alitumia muda wa 2:09:10 ambao ndio muda wake bora zaidi.

Simbu ni miongoni wa wachezaji wa timu ya taifa ya riadha watakaoshiriki mbio za Dunia mwezi Agosti mwaka huu jijini London.

RITA YAMPA TUZO DKT. HARISSON MWAKYEMBE

$
0
0

Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini nchini- RITA umempa tuzo ya heshima aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria mhe. Dkt Harrison Mwakyembe kutambua mchango wake katika kuboresha hali ya usajili wa matukio muhimu ya binadamu nchini.

Tuzo hiyo ya RITA alikabidhiwa Dkt Mwakyembe na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi katika hafla iliyofanyika katika Ofisi za Wizara mjini Dodoma

Akimkabidhi tuzo hiyo Prof. Kabudi alimpongeza DKT Mwakyembe kwa jinsi alivyojitoa na kuhakikisha hali ya usajili inaboreka na hivyo kuinua mwamko wa wananchi na kuona umuhimu wa kujisajili na kuwa na cheti cha kuzaliwa.

Aliwataka watumishi wa RITA na wa Wizara waliokuwepo katika hafla hiyo kuiga moyo wa Dkty Mwakyembe wa kujitoa ili kuhakikisha kazi yake inakuwa na mafanikio.

Akizungumza baada ya kupokea Tuzo hiyo Dkt .Mwakyembe aliwaahidi RITA na Wizara kwa ujumla kuwa ataendelea kuwaunga mkono kupitia Wizara yake mpya ya Habari na kuwataka waendeleze jitihada zao katika usajili ili kuwafanya Watanzania wote wapate vyeti vya kuzaliwa.

“Sina neno kubwa la kuwaambia zaidi ya asante, asanteni sana,niwaahidi kwamba nitaendelea kuwaunga mkono huko nilikoenda, nanyi lazima muendeleze kazi ya kuhamasisha usajili kwa nguvu zenu zote, mjue kwamba mna kazi kubwa mbele yenu na ni lazima ifanikiwe”, alisema Dkt Mwakyembe.

Alisema kazi ya usajili wa matukio muhimu ya binadamu ina umuhimu mkubwa kwa jamii yetu, hii ni kwa ajili ya usalama, uchumi , kijamii na kwa ajili ya maendeleo ya nchi na hivyo ni jukumu lenu kuhakikisha watanzania wote wanasajiliwa ili tuweze kuilinda vyema Tanzania yetu. Kila Mtanzania lazima asajiliwe, lazima ajulikane, hili litasaidia nchi kuhakikisha mgawanyo wa rasilimali zake unakuwa ipasavyo”, alisisitiza Dkt Mwakyembe.


Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Profesa Paramagamba Kabudi akimkabidhi tuzo ya heshima Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo Mh. Dk. Harisson Mwakyembe kutoka umempa tuzo ya heshima aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria mhe. Dkt Harrison Mwakyembe kutambua mchango wake katika kuboresha hali ya usajili wa matukio muhimu ya binadamu nchini Kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini nchini- RITA kushoto ni Naibu  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sgeria Ndugu Amon Anastaz Mpanju.
Waziri wa Katiba na Sheria mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akionyesha tuzo ya heshima aliyokabidhiwa kutoka RITA mara baada ya kukabidhiwa kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sgeria Ndugu Amon Anastaz Mpanju.


SHEIKH SHARIFF MAJINI KUANDAA KONGAMANO KUBWA MJINI DODOMA MWEZI UJAO

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA BALOZI WA IRAN NCHINI TANZANIA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na ugeni kutoka Ubalozi wa Iran nchini Tanzania, katikati ni Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mhe. Mousa Farhang katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto)akikabidhiwa zawadi ya Busati toka kwa Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mhe. Mousa Farhang (Kulia) walipokutana leo katika kikao kilichofanyika ofisini kwake Mjini Dodoma.

UPENDO WOMEN’S GROUP WATOA MSAADA KATIKA WODI YA WAZAZI HOSPITALI YA MWANANYAMALA

$
0
0
Mwenyekiti wa Upendo Women’s Group, Theresia Greca na Mweka Hazina,Begum Chunny kwa pamoja wakikabidhi vifaa hivyo hivyo kwa Afisa Muuguzi wa Hospital ya Mwananyamala,Musa Wambura leo jijini Dar es Salaam.

Umoja wa Wanawake Watanzania waishio nchini Ubeljiji, ‘Upendo Women’s Group’ leo wametoa msaada wa vifaa vya kwenye wodi ya wajawazito ya Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar.


Akizungumza na wanahabari leo wakati wanakabidhi vifaa hivyo, Mwenyekiti wa Upendo Women’s Group, Theresia Greca amesema kuwa changamoto wanazokutana nazo wanawake wa Kitanzania katika wodi mbalimbali wanazokwenda kujifungua ikiwemo uhaba wa vifaa na changamoto nyingine nyingi.

“Wajawazito wana changamoto nyingi sana wakati wa kujifungua, vifaa ni vichache, wahudumu wachache na changamoto nyingine nyingi, hivyo kama Upendo tumekuwa tukikusanya misaada kwetu na wadau mbalimba kwa ajili ya kusaidia wodi ya wajawazito ya Mwananyamala.

“Hii ni awamu ya tatu kwa Upendo kutoa vifaa kwenye wodi ya wazazi hapa Mwananyamala, leo tunatoa vifaa vifuatavyo: Fetal dopler 1, Speculum- SIMS 3, Speculum-cusco 3, Drum (medium)2, Mackintosh Troll 2, Penguin Sucker 2, Needle Holder 10, Sponge Forceps 10, Ambulance Stretcher 1, Ambubag Infant 2, Clinical Thermometer 30, NGT size 8, Drip Stand 3.

Vingine ni Vacuum Extractor 1, Bed Powder Coated 2, Double Step Powder Coated 6 Istrument Trolley 1, Ressuciatian Trolley 1 ambapo vifaa vyote vimegharimu T.Sh.s Mil. 10310000/= (Milioni kumi na laki tatu na elfu kumi).”

Umoja huo unaundwa na wanawake 14; akiwemo mwenyewe, Theresia Greca, Begum Razafinjatovo na Upendo Shoo ambao ni Waweka Hazina. Wengine Ni Fausta Mneney, Dora Maiga, Rosi Kadaga, Linda Shayo, Agnes Kayola, Sedda Maiga, Kimwisho Mndolwa, Hadija Juma, Imbori Na Editha.

Aidha Upendo imewataka Watanzania kujenga utaratibu wa kuwasaidia wodi za wazazi nchini na pia wamewashukuru sana wadau ambao wamekuwa wakishirikiana nao katika kufanikisha misaada hii akiwemo Rais wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin Mkapa, Begum Razafinjatovo, Rosi Kadaga, Chental Ramialimanana,”alisema Grace.

 Mweka Hazina wa Upendo Women’s Group ,Begum Chunny akizungumza wakati wanakabidhi vifaa mablimbaali katika Hospitali ya Mwananyamala leo jijini Dar es Salaam.

Muonekano wa Vifaa hivyo vikiwa katika Hospitali ya Mwananyamala leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images