Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1662 | 1663 | (Page 1664) | 1665 | 1666 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Na Karama Kenyunko blogu ya jamii


  Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla, amewatunuku vyeti wanafunzi wa kike 25 wa shule mbalimbali za sekondari waliofanya vizuri katika mafunzo ya uchambuzi wa takwimu.

  Dk. Kigwangallah ametoa vyeti hivyo leo kwa wanafunzi hao baada ya mafunzo ya siku tatu ya namna ya kutumia takwimu.

  Mafunzo hayo yameandaliwa na kufadhiliwa na DataLab-dlab kwa kushirikiana na UDICTII, Apps Girls and She Code for change na yamelenga kuwajengea uwezo kwenye eneo la kutumia takwimu, kuzitafsiri na kuziweka kwenye taarifa ambazo zinaweza kutumika na walaji kama vile wanahabari, wabunge, watunga sera na wengine wenye uhitaji.

  Dk. Kigwangallah amewapongeza waandaji na kueleza kuwa yatawajenga watoto kwenye utamaduni wa kutumia takwimu.

  Mkuu wa Mafunzo wa Mradi wa Takwimu, Tanzania, Mahadia Tunga, ambaye ni Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, amesema wameamua kutoa mafunzo hayo ya uchambuzi wa takwimu kwa watoto wa kike sababu mara nyingi mwamko wao huwa ni mdogo tofauti na wanaume.

  Amesema kuwa mafunzo hayo wanayatoa kwa watoto kuanzia umri wa miaka 15 hadi 20 ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto na kuzipatia ufumbuzi.

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikabidhi Zawadi kwa Mwanafunzi wa kidato cha tano shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa ambaye ni mshindi wa kwanza wa Data Innovation, Asha Abbas.
  Wasichana Walioshiriki katika Mafunzo wakifatilia hotuba ya Naibu waziri.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameziagiza halmshauri zote za Mkoa wa Singida kuanzisha mabwawa ya ufugaji wa samaki ili kutunza mazingira, kuongeza kipato na kuwa darasa la kufundishia vikundi na wananchi wengine.

  Dkt. Nchimbi ametoa agizo hilo mapema asubuhi ya leo katika shamba ya ufugaji wa samaki la Mikumbi lililopo manispaa ya Singida linalomilikiwa na Bwana Charles Kidua wakati wa uzinduzi wa mavuno ya kwanza ya samaki aina ya kambare katika mabwawa matatu kati ya sita yaliyopo katika shamba hilo.

  Amesema halmashauri zionyeshe mfano kwa kuiga mbinu ya ufugaji wa samaki katika kutunza mazingira kwakuwa itaongeza kipato cha halmashauri pia halmashauri iangalie namna ya kufundisha ufugaji wa samaki vikundi vya vijana kuliko kuwapa mikopo ya pesa ambayo huishia kutumika vibaya.

  Dkt. Nchimbi ameongeza kuwa uwepo wa mabwawa hayo ya ufugaji wa samaki unaonyesha kuwa Mkoa wa Singida sio kame na wala sio mkoa masikini na uko tayari kuandaa chakula kulisha mikoa ya jirani hasa makao makuu ya nchi ambayo ni Dodoma.

  “Tumejipanga na tuko vizuri kuhakikisha Dodoma inapata chakula kizuri na cha uhakika, Singida sio kame wala masikini, samaki hawafugwi kwenye ukame, Singida sio kame hata kidogo” amesisitiza Dkt. Nchimbi.

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wa pili kulia) akishiriki kuvua samaki aina ya kambare kwenye bwawa lililopo kwenye shamba la samaki la Mikumbi mjini hapa ikiwa ni sehemu ya uzinduzi uvuvi kwenye shamba hilo.Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa mmiliki wa shamba la ufugaji samaki la Mikumbi Bw. Charles  Kidua (wa pili kulia) wakati akikagua shamba hilo lenye mabwawa sita yaliyofungwa samaki aina ya sato na kambare.
  Mmiliki wa shamba la samaki Mikumbi mjini Singida na afisa maliasili Mkoa wa Singida Charles Kidua (aliyenyoosha mkono) akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wa kwanza kulia) muda mfupi kabla ya kuzinduliwa kwa uvuvi kwenye shamba hilo asubuhi ya leo.
  Baadhi ya samaki aina ya kambare waliovuliwa mapema leo kwenye uzinduzi wa uvuvi shamba la samaki la Mikumbi lililopo mjini hapa.


  0 0

  Hivi karibuni Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dkt Asha Rose Migiro alifanya ziara mjini Leicester ambapo alikutana na Diaspora wa Tanzania waishio katika mji huo na vitongoji pamoja na kujionea shughuli za kiuchumi na kimaendeleo zinazofanywa na Diaspora hao. 

  Katika mazungumzo yake na Diaspora Balozi Migiro aliwakumbusha dhamira ya dhati ya Rais John Pombe Magufuli na Serikali yake katika Kuwashirikisha Diaspora katika agenda ya Maendeleo ya Serikali na Nchi kwa ujumla. Aidha aliwakumbusha kuwa pamoja na shughuli zao ughaibuni ni Vyema wasisahau kuendeleza nyumbani. 

  Balozi pia alitumia fursa hiyo kufafanua masuala ya uraia pacha na umiliki wa ardhi kwa Diaspora ambapo aliwaeleza kuwa Sera na Sheria zilizopo ndizo zinazotekelezwa na Serikali katika kuyashughulikia masuala hayo. 

  Balozi Migiro anatarajiwa kuendelea kuwatembelea Watanzania walio katika miji mingine ya Uingereza kama sehemu ya mpango Kazi wa Ubalozi wa London wa kuwatambua Diaspora wa Tanzania waishio Uingereza na Kuwashirikisha katika Agenda ya Maendeleo ya Serikali ya Awamu ya Tano.
   Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dkt Asha Rose Migiro akipata  maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Diversity Health and Social Care Bi Frida Kusamba kuhusu huduma ya afya inayotolewa na kampuni yake. 
   Balozi akijionea mavazi yanayoshonwa  katika duka la Bi. Farhiya Mayo, Mkurugenzi wa zanzibar fashion house.
   Balozi akiongea na wamiliki wa Kampuni ya uandaaji vyakula ya Diaspora Kisk Catering' .
  Balozi katika hali ya kufurahia jambo na Diaspora wa Leicester walioshiriki Mkutano wake

  0 0

  Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini kupitia (TSSA) inayoundwa na Mifuko ya NSSF, PPF, LAPF, PSPF, GEPF, NHIF, WCF pamoja na ZSSF imefanya ziara ya kutembelea kiwanda cha nyama kilichopo mjini Shinyanga ambacho hakikuwahi kufanya uzalishaji tangu kibinafisishwe, lengo la Ziara hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kuona hali halisi ya kiwanda hicho ambacho kwa sasa kipo chini ya mikono ya Serikali, Mifuko hiyo kwa pamoja kupitia umoja wao wa TSSA wamedhamiria kuwekeza kwa pamoja katika sekta ya ngozi, nyama na nguo katika kiwanga hivyo. wanaonekana mbele ni  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa GEPF, Daud Msangi (wa pili kulia).
  Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini kupitia (TSSA) inayoundwa na Mifuko ya NSSF, PPF, LAPF, PSPF, GEPF, NHIF, WCF pamoja na ZSSF wakipatiwa maelezo wakati walipotembelea kiwanda cha nyama kilichopo mjini Shinyanga, ambacho hakikuwahi kufanya uzalishaji tangu kibinafisishwe. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa GEPF, Daud Msangi akisaini kitabu wakati walipotembelea kiwanda cha nyama kilichopo mjini Shinyanga, ambacho hakikuwahi kufanya uzalishaji tangu kibinafisishwe. Kulia ni Mratibu wa ziara hiyo kutoka TSSA, Meshack Bandawe.
  Wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini kupitia Jumuiya yake ya TSSA (Tanzania Social Security Association) wakiendelea na ziara yao katika kiwanda cha nyama kilichopo mjini Shinyanga.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 

  0 0


  Na .Vero Ignatus,Arusha.

  WAKAZI wa Olasiti jijini Arusha wamesusia maji yanayotolewa na Idara ya maji na kudai kuwa maji hayo hayafai kwa matumizi ya aina yoyote.

  Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanywa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wananchi hao walisema maji yaliyosambazwa na Idara ya maji yana chumvi kiasi cha kuharibu hata mimea wanapojaribu kumwagilia.

  Mmoja wa wakazi hao Meck Mollel alisema wanahofia baada ya miaka ijayo kutokuwa na nguvu za kiume kutokana na kuendelea kutumia maji hayo ambayo yanaladha ya magadi.

  "Kweli haya maji yanatupa hofu baadaye tutajikuta wanawake wote kwa mpango huu hatuyahitaji haya maji tuleteeni maji yaliyorafiki kwa binadamu" alisema Mollel.

  Naye mkazi mwingine alisema maji hayo akiwapa vifaranga wanapata matege kutokana na hali ya chunvi iliyozidi ambapo pia alisema akimwagilia mimea inakuwa ya njano.

  Hata hivyo mkuu wa mkoa aliwataka wananchi hao kufahamu kuwa serikali haiwezi kuruhusu maji yasiyo faa kwa matumizi ya binadamu hivyo maji hayo yalipimwa na kuonekana yanafaa ndio maana yakaruhusiwa.

  "Serikali yoyote duniani haiwezi kuruhusu kitu chenye madhara kwa wananchi wake hivyo tutaleta tena wataalamu kuyapima tena na majibu yatakayopatikana tutajua cha kufanya" alisema Gambo.

  Naye Mkurugenzi wa maji jiji la Arusha Ruth Koya alisema kiwango cha maji salama hakipimwi kwa macho bali kinapimwa maabara hivyo wataalam wamepima na wakaona yanafaa kwa matumizi.

  Koya alisema maji wanayolilia wananchi hao yanafloride lakini hayo yaliyopo pamoja na kuwa na chumvi hayana madhara kwa matumizi Kama wanavyolalamika wao.
  Baadhi ya wananchi Wa Kara ya Olasiti kama wanavyoonekana pichani.Picha na Vero Ignatus blog.

  0 0

  NAHODHA Msaidizi wa klabu ya  Azam Himid Mao ‘Ninja’, ameweka wazi kuwa wana morali kubwa ya kupata matokeo mazuri kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Sports) dhidi ya Simba utakaopigwa siku ya Jumamosi.

  Mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza kati ya Simba na Azam utapigwa katika dimba la UWanja wa Taifa ukichezeshwa na mwamuzi Mathew Akrama kutoka Jijini Mwanza na unatarajiw akuwa moja ya mechi ngumu sana kwa kila upande.

  Kikosi cha Azam FC kipo kwenye maandalizi makali kuelekea mchezo huo, ambapo tayari kimeshaingia kambini mapema wiki hii  katika makao makuu ya klabu hiyo ndani ya viunga vya Azam Complex kujiandaa na mchezo.

  Himid amesema  kikosi chote cha wachezaji wana ari kubwa na wapo vizuri  na watanufaika na urejeo wa wachezaji wao muhimu waliokuwa majeruhi.

  “Morali iko juu, timu ipo vizuri bahati nzuri wachezaji wenzetu karibia asilimia 90 wapo vizuri na wapo fiti na wako tayari kwa mchezo na naamini kocha atakuwa na nafasi nzuri ya kuchagua timu yake ya kwenda kucheza mchezo huo,” alisema Mao.

  Kiungo huyo wa timu ya Taifa alisema kuwa mchezo huo utakuwa mgumu licha ya kufanikiwa kuwafunga mara mbili katika mechi mbili zilizopita.

  “Usidhani kama mchezo huu wa tatu utakuwa mrahisi kama mara mbili zilizopita tulizoshinda, kwani Simba nayo inajipanga, lakini naamini sisi tutajipanga vizuri zaidi ili kuweza kushinda mechi hiyo inayokuja,” alisema.

  Himid ambaye amekulia kwenye timu hiyo kwa takribani miaka tisa sasa, alitoa wito kwa mashabiki wa Azam FC kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo ili kuwapa sapoti kwani wao ni sehemu muhimu sana katika timu na uwepo wao utawaongezea nguvu zaidi uwanjani ya kuibuka kidedea.


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  0 0  0 0
  0 0

   Mratibu wa Shindano la Miss Grand  Tanzania , Rasheedah  Jamaldin akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar, juu ya uzinduzi wa shindano la urembo litakalo tambulika kama Miss Grand Tanzania  2017 linalotarajia kuanza mapema mwezi Juni  mwaka huu, ambapo imeelezwa kuwa mchujo wake utaanzia katika ngazi ya vitongoji mpaka Taifa .
   Meneja Matukio wa Miss Garand  Tanzania 2017 ,Abraham Mahimbo akizungumza na waandishi jisni mawakala watakavyohusika katika kuwapata warembo nchi nzima
  Waandishi mbalimbali waliofika katika mkutano huo wa uzinduzi wa shindano la Miss Garand 2017 jijini Dar es Salaam leo

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Mtandao wa Vikundi vya Wakulima nchini (MVIWATA) umeiomba Serikali kutunga sheria ndogo ndogo zitakazowabana wafanyabiashara wa zao la ufuta ili wakulima wapate faida ya uzalishaji wa zao hilo.

  Maombi hayo yamebainishwa hivi karibuni na Afisa Masoko kutoka MVIWATA, Acquiline Wamba wakati wa warsha ya uboreshaji wa matumizi ya vipimo sahihi katika biashara ya mazao ya kilimo iliyofanyika mkoani Dodoma.

  Bi. Acquiline amesema Serikali inatakiwa kuchukua hatua madhubuti kwa kuweka sheria kali dhidi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kwani Sheria hizo  zitawasaidia kuwapa maelekezo ya namna ya kuweka vipimo sahihi kwenye mazao ili kuongeza ushindani kwenye biashara.

  “Wafanyabiashara wasio waaminifu wamekua ni chanzo cha kukwamisha soko la nje kwa kupeleka mazao yenye uchafu nje ya nchi, hii sio sahihi ndio maana tunaomba Serikali itusaidie” alisema Bi. Acquiline. 

  Aliongeza kuwa ili kuboresha soko la nje la zao la ufuta Serikali inatakiwa kuhakikisha panakwepo na mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mazao yanayoenda nje ni masafi.

  Aidha, Bi. Acquiline alifafanua kwamba kuwabana wafanyabiashara wa zao hilo kutumia vipimo sahihi vya mizani itasaidia kukomesha  wafanyabiashara wanaowaibia wazalishaji hao kwani lengo halisi la kuweka mizani ni kupunguza tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kuongeza mchanga kwenye zao la ufuta kwa lengo la kuongeza uzito.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Danford Chisomi alisema kuwa Halmashauri bado haijawa na mizani ya mazao kutokana na ufinyu wa bajeti hivyo aliahidi kushiriki katika kutatua changamoto hizo.

  “Halmashauri itatafuta nafasi ya kuweka mizani pamoja na kuunda sheria mpya ndogondogo za kuwadhibiti wafanyabiashara wa zao hilo”, alisema Chisomi. 

  Akiongea katika warsha hiyo, mzalishaji wa ufuta Wilayani Bahi, Fikiri Bernard, alisema kukosekana kwa mizani katika Halmashauri hiyo kunaathiri moja kwa moja jitihada za wazalishaji pamoja na kusababisha upotevu wa mapato kwa halmashauri hiyo. 

  “Vipimo vingi vinavyotumiwa na wafanyabiashara huwa haviko sahihi kwa sababu havijahakikiwa na Mamlaka husika kwa matumizi ya biashara hivyo wafanyabiashara wamekua wakitumia mwanya huo wa ukosefu wa mizani kuweka vipimo vyao wenyewe vya kununulia zao la ufuta,” alisema Bernard.

  Ameongeza kuwa Halmashauri hiyo imekua ikipoteza mapato mengi kwa kushindwa kukusanya ushuru kutokana na kuwepo kwa wafanyabiashara wasio waaminifu wanaopenyeza mazao yao bila kulipa ushuru.

  Vile vile, mkulima huyo ameiomba Halmashauri kutenga vituo mbalimbali vya kupimia mazao kwa ajili ya kupata vipimo sahihi vya mazao ili kuepuka kuwaibia wakulima.

  0 0

  Hospitali ya Taifa Muhimbili imetoa msaada wa baiskeli na matibabu kwa Mwalimu Joyce Kantande ambaye alipata ulemavu kutokana na ajali aliyoipata akiwa na umri wa miaka saba.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili , Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga, Agnes Mtawa amesema wameguswa na tatizo la Joyce na hivyo uongozi wa hospitali umeamua kumpatia baiskeli hiyo ili kumwezesha kufanya shughuli zake akiwa amekaa .

  ‘’ Tuliona stori yake kwenye gazeti moja na kiukweli tumeguswa na tatizo lake kwani Joyce alikaa miaka 18 akiwa amelala baada ya kupata ajali iliyosababisha apate ulemavu kutokana na hali hiyo Mkurugenzi Mtendaji Profesa Lawrence Museru ameona ni vema tukampatia msaada wa baiskeli, lakini pia kama Hospitali tutampatia msaada wa matibabu na tutakua tukimfuata na kumrudisha nyumbani kwa kipindi chote atakachokua akija hospitalini hapa kwa ajili ya matibabu,‘’ amesema Mtawa .

  Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura na Ajali, Juma Mfinanga amesema kwa kushirikiana na wataalam wengine wa MNH watamfanyia vipimo mbalimbali ili kujua tiba gani anastahili .

  Naye Mkuu wa Idara ya Tiba na Utengamao katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Rosemary Kauzeni amesema watatumia utaalam wao kumsaidia Bi Joyce ili aweze kufanya shughuli zake akiwa amekaa badala ya kulala hususani shughuli zake za kufundisha watoto ambazo huzifanya akiwa amelala .

  ‘’Tutatumia utalaam wetu kwa kumpatia tiba ya mazoezi ya viungo ili aweze kukaa wakati anapofanya shughuli zake badala ya kulala na hatimaye aweze kutawala mazingira yake,” amesema.

  Kwa upande wake Bi Joyce ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa msaada alioupata na kuwaomba watu wengine kujitokeza kumsaidia kwani ana mahitaji mengi.

  Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agness Mtawa akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kumpatia Joyce Kanitande msaada wa baiskeli na matibabu ambayo yatamwezesha kufanya shughuli zake za kila siku. Joyce anatapatiwa matibabu katika hospitali hiyo baada ya kupta ajali na kuvunjika mgongo wakati akiwa na umri wa miaka saba.
  Bi. Joyce akiwa amekaa kwenye baiskeli baada ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kumpatia msaada huo leo.
  Mkuu wa Idara ya Utengamano, Rosemary Kauzeni akiwaeleza waandishi wa habari jinsi Joyce akavyokuwa akipatiwa matibabu yakiwamo mazoezi ambayo yatamsaidia kufanya shughuli zake.

  Bi. Joyce akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako amefikishwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Joyce alipata ulemavu wa mgongo baada ya kupata ajali wakati akiwa na umri wa miaka 7 na hivyo kushindwa kuendelea na shughuli zake za kawaida.

  0 0


  Na Karama Kenyunko

  Mshtakiwa Mary Amokowa, ameiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imuachie huru kwani hakuhusika na tuhuma za kusafirisha wasichana 10 kutoka Tanzania Kwenda Kenya kwa ajili ya biashara ya ngono.

  Mshtakiwa huyo ambaye ni raia wa Kenya ameiomba mahakama imuachie huru kwa kuwa madai ya kesi hiyo ni ya uongo na ya kutengenezwa.

  Ameyasema hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godifrey Mwambapa wakati akitoa utetezi wake dhidi ya kesi hiyo inayomkabili yeye,Jackline Milinga na Simon Alex Mgawe.

  Akiongozwa na wakili wake Nehemia Nkoko,Mary amedai kuwa yeye ni mfanyakazi wa kampuni ya simu ya safari Com iliyopo Nairobi Kenya. Amedai kuwa, Septemba 4,2015 akiwa na rafiki yake Jackline walisafiri kwa kutumia basi la Mordem Coast kutoka Dar es Salaam kwenda Nairobi.

  Ameongeza kuwa walikuwa na tiketi na pasi za kusafiria lakini walipofika Namanga mpakani mwa Kenya na Tanzania, akiwa tayari amekwisha gongewa mhuri wa kutoka Tanzania na akiwa katika foreni ya kusubiri kugongewa muhuri wa kuingia Kenya, askari wawili wa Uhamiaji wa Tanzania walimkamata Jackline.

  Amedai walipomkamata walimwambia wana wasiwasi na hati yake ya kusafaria kwa sababu alikuwa na hati ya kusafiria ya kidiplomasia na baadaye walibaini haijaghushiwa ni halali.

  Amedai kuwa, baada ya pasi ya rafiki yake kuonekana kuwa ni halali na wote wakati huo walikuwa chini ya ulinzi aliomba waachiwe huru, baada ya kutuchukua maelezo lakini hawakutuachia. Badala yake wakatuweka sehemu moja na hao wasichana 10, ambao tulikaa nao siku nne Uhamiaji Makao Makuu na kwamba walipohamishiwa uhamiaji mkoa hawakuwa na hao wasichana.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Wankyo Gati,,ARUSHA

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha, leo imemuachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Lengai Ole Sabaya baada ya kuona upande wa Jamuhuri wazembe wa kushindwa kuleta mashahidi katika kesi ya kujifanya Afisa Usalama wa Taifa (TISS).

  Akisoma uamuzi wake jana uliotokana na ombi la Wakili wa Serikali Grace Madikenya la kuomba Mahakama hiyo kuiondoa kesi hiyo kwa sababu ya kukosa shahidi muhimu katika kesi hiyo na kupingwa na Upande wa Utetezi kuwa wanatumia vibaya mahakama kumtesa mteja wao, Gwantwa

  Mwakuga, alisema Mahakama inasikitika kuona mwendesha mashitaka wa serikali, anatumia kigezo cha kuondoa kesi na kumkamata mshitakiwa kwa maslahi yake mwenyewe.

  Alisema kesi hiyo imekuja mara ya pili baada ya kufunguliwa kesi namba 376/2016 na ilipofika katika utoaji wa ushahidi wa mpelelezi wa kesi hiyo, Mwendesha mashitaka aliomba Mahakama kuiondoa kesi hiyo kwa madai hawana nia ya kuendelea nayo na na mahakama ilikubaliana naye na kumwachia huru, lakini siku hiyo hiyo Desemba 14 Mshitakiwa alikamatwa.

  “Kinachosikitisha Mahakama ilishuhudia kwa macho yake baada ya kumwachia mshitakiwa alipotoka nje alikamatwa tena na kuletwa tena Mahakamani hapa, kwa hakimu Mfawidhi Augustino Rwezile na mashitaka yalikuwa yale yale hakuna kilichorekebishwa na sasa wanaomba tena kuondoa kwa kigezo shahidi muhimu yupo nje ya nchi kwa miezi 18, hii ni utumiaji vibaya ofisi ya mwendesha mashitaka, ili kutesa watu,”alisema.

  Gwantwa alisema Mahakama inatambua nguvu ya Mkurugenzi wa Mashitaka aliyonayo, lakini nguvu hiyo isitumike vibaya ni muhimu kuzingatia maslahi ya umma,haki na utedaji kazi wa Mahakama.Alisema Mahakama hiyo imejiuliza kipya kilichorekebishwa katika kesi hiyo ya pili namba 493/2016 na kuona hakuna, isipokuwa upande waJamuhuri wamefanya kwa kukidhi mataka yao wenyewe.


  0 0

  Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

  Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara ametoa wito kwa wanawake mkoani hapa kuungana na kushirikiana pamoja katika shughili za mbalimbali za ujasiriamali ili iwe rahisi kwao kunafaika na fursa mbalimbali mikopo ikiwemo asilimia tano inapaswa kutolewa na Halmashauri zao.

  Dkt. Ntara alitoa kauli hiyo jana mjini Tabora wakati akizindua Jukwaa la Uwezeshaji wanawake kiuchumi la Mkoa huo.Alisema kuwa wanawake wakiendelea kufanyakazi kwa ubinafsi hawataweza kuendelea bali wataendelea kubaki nyuma.

  Katibu Tawala huyo wa Mkoa alisema kuwa wanawake wakiungana na wakaunda vikiundi vinavyoaminika watapata fursa ya kukopeshwa na Taasisi za fedha zilizopo mkoani Tabora na hivyo kukuza mitaji yao ambapo hatimaye wanaweza kuwa na uwezo wa kuanzisha viwanda vyao.

  Dkt. Ntara aliongeza kuwa wakiungana watapata fursa ya wao kuwa kichocheo cha kuleta maendeleo kuanzia ngazi za familia hadi taifa kutokana na wao kuwa wataalam wazuri wa matumizi ya fedha kidogo wanazopata.

  Alisema kuwa mwanamke licha ya baadhi yao kutokwenda shule au kutopata fursa ya kusoma lakini bado Mungu amewajalia maarifa ambayo yanasaidia jamii kama vile kufahamu kuwa mtoto wake anaumwa wakati hajasomea udaktari, kufahamu umuhimu wa kilimo cha mboga mboga kuzungumza nyumba yake licha ya kutosomea ubwana au ubibi shamba, kuwa mtunza fedha mzuri licha ya kutosomea uhasibu.


  0 0

  Na Tiganya Vincent-RS-Tabora.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama katika kijiji cha Mabama wilayani Uyui mkoani Tabora.

  Taarifa hiyo imetolewa leo mjini Tabora na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye pia ni Mkuu wa Wialaya ya Tabora Queen Mlozi imesema kuwa sherehe za uzinduzi wa mradi huo zitaanza asubuhi siku ya Jumamosi ya tarehe 29 Mwezi huo.

  Amesema kuwa baada ya uzinduzi wa mradi huoi , Makamu wa Rais atapata fursa ya kuwahutubia wananchi na viongozi mbalimbali katika viwanja vya Shule ya Msingi Mabama.

  Aidha , Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora ametoa wito kwa viongozi wa dini zote, vyama vyote vya siasa, viongozi wa serikali na wananchi wa maeneo yaliyopo karibu na mradi huo kujitokeza kwa wingi kwenda kusikiliza hotuba ya Makamu wa Rais.

  Uzinduzi wa mradi huu utasaidia kuondoa tatizo la maji safi na salama kwa wakazi wa eneo hilo na ni jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwaondole matatizo mbambali wananchi likiwemo la upatikanaji wa maji safi na salama.

  Mradi huo wa maji ambao umefadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan(JICA) umewezesha umesaidia uchimbaji wa visimana ujenzi mitandao ya mabomba katika eneo hilo wilayani Uyui.

  0 0


  I do not pretend to be older than many but the truth is that, I'm old enough to confess that life is indeed a mystery.

  I've seen a Landlord becoming a tenant of his former tenant before his death. 


  I know a student who became the Vice Chancellor in his former University with most of his lecturers still teaching under him.


  I have seen a rejected person becoming the bread winner for a whole community. A victor becoming a victim. A driver conductor buying the bus of his master. And A borrower recruiting his erstwhile credit bank manager. 
  In life, no one knows tomorrow & you can never trust life, because it is mysterious. 


  Never ever forget. U may not know the full story, Don't be quick to judge. Every coin has two sides. 


  Treat everyone during your life time fairly like your own & love and forgive as much as you live. 


  So let us be humble, kind, love more & do not try to be smart in anything; for we do not know what tomorrow holds for us.


  Five years ago, on 28th April 2012, my Guardian Angel Isabella Benita Bulengo was laid to eternal rest at Makongo Juu, Dar es Salaam at the Age of 5 years. RIP! My Guardian Angel Isabella.

  Fr. James Byebazo Rugemalira Rutakwabyera. 

  0 0

  Na Nuru Juma na Beatrice Lyimo-MAELEZO .

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka watumishi 9932 waliogushi vyeti, kuondoka maeneo yao ya kazi haraka iwezekanavyo kabla hawajadhibiwa kwa mujibu wa sheria. 

  Rais Magufuli ameyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akikabidhiwa taarifa ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma sambamba na uzinduzi wa maadhimisho ya miaka kumi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). 

  “Watumishi 9932 wenye vyeti vya kugushi na feki mishahara yao ya mwezi huu ikatwe na waondoke kazini mara moja na hizo nafasi zitangwazwe ili wasomi waweze kuziomba na majina yao yawekwe kwenye magazeti ili wajulikane” amesema Rais Magufuli 

  Aidha amesema kuwa hadi kufika tarehe 15 Mei, 2017 kila mkuu wa Idara mahali pake pa kazi ahakikishe watumishi hao wameondoka na watakao kaidi agizo hilo amevitaka vyombo vya usalama kuwashughulikia.
  Hata hivyo Rais Magufuli ameongeza kuwa watumisi 1538 wanaotumia cheti zaidi ya mtu mmoja kutopewa mshahara hadi pale itakapojulikana nani mwenye cheti halali na kuwataka watumishi 11,769 kuwasilisha vyeti vilivyopungua. 

  Mbali na hayo Rais Magufuli amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kuachana na masuala ya siasa kwa lengo la kujenga nchi kwani watanzania wanahitaji maendeleo. 

  Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angela Kairuki amesema kuwa mpaka sasa vyeti vilivyohakikiwa ni 435,000 ambapo imefanyika kwa awamu tatu iliyojumuisha Serikali za Mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma, Tume na Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi na Wakala wa Serikali pamoja na Serikali Kuu. 

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Jane Kajiru akitoa maelekezo ya kumchagua mfanyakazi bora wa ofisi wa mwaka 2017.
  Wawakilishi wa wafanyakazi bora wa Idara/Vitengo vya Ofisi ya Rais-Utumishi wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Jane Kajiru wakishuhudia kura zikihesabiwa ili kumpata mfanyakazi bora wa ofisi wa mwaka 2017.
  Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakisikiliza maelekezo ya uchaguzi wa mfanyakazi bora wa ofisi wa mwaka 2017 uliofanyika leo katika ofisi hiyo.

  0 0

  Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma

  Mikoa mitatu ya Tanga, Morogoro na Iringa, imenufaika na kiasi cha shilingi bilioni 6.5 zilizotolewa kama mkopo na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) tangu benki hiyo ianzishwe mwaka 2015.

  Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, wakati akijibu swali na msingi lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Felister Aloyce Bura, aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaanza kutoa huduma kwa wakulima wadogo wadogo wa mkoa wa Dodoma.

  Dkt. Kijaji ameeleza kuwa hadi kufikia mwezi Desemba, 2016, TADB imetoa mikopo ya jumla ya shilingi 6,489,521,120 kwa ajili ya kutekeleza miradi ishirini (20) ya kilimo katika mikoa hiyo mitatu ya Iringa, Morogoro na Tanga.

  “Sambama na utoaji mikopo, Benki inatoa mafunzo kwa wakulima ambapo hadi sasa vikundi 336 vya wakulima wadogowadogo vyenye jumla ya wanachama 44,400 wamepatiwa mafunzo hayo katika mikoa hiyo mitatu” aliongeza Dkt. Kijaji

  Amesema kuwa Benki hiyo inatarajia kuanza kutoa huduma hiyo kwa wakulima wadogowadogo wa Mkoa wa Dodoma na mikoa mingine jirani wenye sifa.

  “Benki imepata nafasi kwa ajili ya kufungua ofisi katika jengo la PSPF mjini Dodoma na itakabidhiwa ofisi hiyo mwezi Julai, 2017, baada ya mkandarasi kukamilisha ujenzi wa jengo hilo” Alisisitiza Dkt. Kijaji

  Dkt. Kijaji amesema kuwa tayari Benki hiyo imemwandikia barua Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma ili kuomba aipatie miradi mizuri ya kilimo ambayo mkoa unapendekeza Benki iifikirie katika zoezi la kutoa mikopo itakayoanza kutolewa mwishoni mwa mwaka 2017.

  0 0  Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharikialifanya ziara ya kikazi jijini Seoul, Jamhuri ya Korea tarehe 24 Aprili 2017 kwa mwaliko kutoka kwa Mhe. Yun Byung-se, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea. Ziara hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea mwaka 1992.

  Wakati wa ziara hiyo, Mheshimiwa Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Mhe. Yun Byung-se ambapo Waziri Mahiga aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kumpatia mwaliko wa kutembelea taifa hilo hususan wakati huu inapoadhimishwa jubilee ya miaka 25. Mhe. Mahiga aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kuichagua Tanzania kuwa nchi ya kimkakati  katika uwekezaji kwa kipindi cha kuanzia 2016 -2020.

  Kwa kipindi cha miaka 25, Serikali ya Korea imeisaidia Tanzania kufanikisha utekelezaji wa miradi mikubwa ikiwemo Ujenzi wa Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi unaojumuisha madaraja matatu yenye jumla ya urefu wa meta 275  pamoja na barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 48; Ujenzi wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Kampasi ya Mloganzila yenye uwezo wa kulaza wagonjwa 600imejengwa na kufungwa vifaa tiba vya kisasa vya digitali, vinavyotumia zaidi teknolojia ya Tehama zikiwemo mashine za X-ray, MRI, CT-Scan, mashine maalum kwa ajili ya kupimia magonjwa ya wanawake. 

  Vilevile, Ujenzi wa Hospitali ya mama na mtoto Chanika yenye uwezo wa kulaza wagonjwa 160 inatarajiwa kufunguliwa siku za karibuni.Aidha, Watanzania zaidi ya 1000 wamenufaika kwa kupata ufadhili wa kusoma katika vyuo mbalimbali vya Jamhuri ya Korea.

  Waziri Mahiga pia alikutana na baadhi ya Wanachama wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Jamhuri ya Korea ambapo alitumia fursa hiyo kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania mathalani ujenzi wa Reli ya Kati katika viwango vya kimataifa; uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme; ujenzi wa maeneo ya viwanda; na huduma ya kutoa ushauri katika miradi mikubwa.

  Aidha, Mhe. Waziri aliwahakikishia wawakilishi wa  makampuni ya Jamhuri ya Korea kuwa, Tanzania imeboresha mazingira ya uwekezaji na biashara pamoja na taasisi muhimu zinazotoa huduma mbalimbali katika sekta hiyo. 


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea, Mhe. Yun Byung-se. Mhe. Mahiga alikuwa nchini humo kwa ziara ya kikazi ikiwa pia ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 25 ya ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea.

older | 1 | .... | 1662 | 1663 | (Page 1664) | 1665 | 1666 | .... | 3284 | newer