Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110176 articles
Browse latest View live

Article 17


WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA MAELEZO ONLINE TV MJINI DODOMA

$
0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe ameipongeza Idara ya Habari-MAELEZO kwa ubunifu mkubwa  katika kuitangaza Serikali. ameyasema hayo jana mjini Dodoma wakati akizindua televisheni ya mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO inayoitwa MAELEZOTV.
“Napenda nichukue fursa hii kwa kuwapongeza Idara ya Habari kwa kazi nzuri mnayoifanya katika Wizara hii,nawapongeza kwa ubunifu mkubwa na leo tunazindua Televisheni ya mtandaoni ya Idara hii  kwa mara ya kwanza katika historia ya Wizara yetu na Idara ya Maelezo kwa ujumla kuwa na” Alisema Waziri Mwakyembe.
Amesema kuwa kwa kazi ya kwanza ambayo imeonekana katika televisheni hiyo imeonyesha weledi wa hali ya juu na kuwataka viongozi wengine wa Wizara hiyo kuiga mfano mzuri na kuwa wabunifu na kusisitiza kuwa nchi yetu ina vipaji na ubunifu wa hali ya juu ikiwemo timu yetu ya Vijana ya Serengeti Boys na n.k
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO,amesema  kuanzishwa kwa televisheni hii ya mtandaoni itasaidia kwa kiasi kikubwa Serikali katika kutangaza matamko mbalimbali na uzinduzi wake wa mapema utasaidia kufikisha taarifa mbalimbali kwa jamii husika.
“Sisi kama Serikali tumekuwa makini katika kuimarisha mawasiliano kati yetu na wananchi na hii televisheni ya mtandaoni itatusaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha dhima ya Serikali ya awamu ya tano katika kutekeleza kazi zake”,Aliongeza Dkt Abbas.
Mbali na hayo amesema kuwa kipindi cha kwanza kabisa kuwekwa katika televisheni hii itakuwa mahojiano ya maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya muungano  waliyofanya na Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano Mhe.Samia Hassan Suluhu.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe akibonyeza kitufe kuzindua Televisheni ya mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO jana mjini Dodoma.Televisheni iyo itaonyesha kazi mbalimbali za Wizara,Taasisi na Idara za Serikali.Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Anastazia Wambura.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe,Naibu Waziri wake Anastazia Wambura,Katibu Mkuu Prof.Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbas wakifurahi mara baada ya kuzindua Televisheni ya mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO jana mjini Dodoma.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe akiangalia mahojiano yaliyofanyika kati ya Mkurugenzi wa Idara ya Maelezo Hassan Abbas na Makamu wa Rais Mhe.Samia Hassan Suluhu kuhusu maadhimisho ya Muungano yatakayofanyika mjini Dodoma.Mahojiano hayo ni ya kwanza kupitia televisheni ya mtandaoni ya Idara ya habari-MAELEZO.

Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Harrison  Mwakyembe akizungumza na menejimenti ya Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo(Hawapo Pichani) na kuipongeza Idara ya habari kwa kuwa wabunifu.Kulia kwake ni Naibu Waziri wake Anastazia Wambura,Katibu Mkuu Prof.Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbas. Picha na Daudi Manongi-MAELEZO,DODOMA.





INTRODUCING "SINA KINYONGO" BY SALUM SIMBA

$
0
0


Audio produced by Laizer (WCB records)
Video directed by Benjamin Busungu
for any interviews please call

Salum Simba-0756-440-401
                    -0653-158-156


BREAKING: HAJI MANARA AFUNGIWA MIEZI 12 NA FAINI YA SHILINGI MILIONI 9 KWA UTOVU WA NIDHAMU

$
0
0
Msemaji wa Simba Haji Sunday Manara amefungiwa kutojihusisha na mchezo wa soka kwa muda wa miezi 12 na kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni tisa , kwa utovu wa nidhamu wa kutoa matamshi yasiyo na staha kwa viongozi wa TFF pamoja na vyombo vya uongozi wa mchezo huo. Makamu  Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya TFF Wakili msomi Jerome Msemwa pia amesema Haji Manara anaweza kukata rufaa.

UZINDUZI WA MRADI WA GARI 8 ZA CCM JIMBO LA MFENESINI UNGUJA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Gari Nane(8) ya CCM aina ya Dyna ikiwa ni ahadi ya Mbunge wa CCM wa Jimbo la Mfenesini Col.Mstaafu Masoud Khamis (wa pili kulia) katika viwanja vya Z. Ocean Hotel iliyopo kihinani Wilaya ya Magharibi Jimbo la Mfenesini leo.
Gari nane (8) aina ya Dyna zilizonunuliwa na Mbunge wa Jimbo la Mfenesini  Mhe.Col.Mstaafu Masoud Khamis ambazo leo amezikabidhi kwa Chama cha Mapinduzi CCM zitakazotumika na kutoa huduma katika Matawi ya Chama cha CCM katika jimbo hilo,ambazo zimegharimu jumla ya shilingi za kitanzania Millioni Mia moja na Tisiini na Mbili,[Picha na Ikulu] 23/o4/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akipokea kadi za Gari Nane (8) aina ya Dayna ambazo Rais amezindua Mradi huo wa CCM zitakazotumika katika Matawi ya Chama Jimbo la Mfenesini,Gari hizo ini ahadi aliyoitoa Mbunge Mhe.Col.Mstaafu Masoud Khamis katika ukumbi wa Hoteli ya Z. Ocean iliyopo kihinani Jimbo la Mfenesini leo katika sherehe Jimboni humo, 
Baadhi ya Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Mfenesini wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza katika sherehe za Uzinduzi wa Mradi wa Gari Nane (8)za CCM zilizokabidhiwa leo kwa Rais ikiwa ni ahadi ya Mbunge wa jimbo hilo Col.Mstaafu Masoud Khamis,ikiwa ni ahadi ya kwa Wananchi hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Z. Ocean Hoteli iliyopo kihinani Jimbo la Mfenesini.

TAMISEMI YABARIKI MICHUANO YA COPA UMISSETA 2017 – COCA-COLA KUENDELEA NA UDHAMINI KAMA KAWA

$
0
0
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na SerikalizaMitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akitoa hotuba ya ufunguzi kwa washiriki wa semina elekezi kwa Maafisa Elimu na Maafisa Michezo wa mikoa yote nchini, ikiwa ni maandalizi mahsusi ya uzinduzi rasmi wa mishindano ya michezo ya Copa UMISSETA 2017, ambapo kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola imeendelea kudhamini mashindano hayo.

 Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki Dodoma na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini na Coca-Cola Tanzania. Ufunguzi rasmi wa michuano hii utafanyika katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma siku ya Ijumaa Aprili 28, 2017.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Bw Yusuf Singo akizungumza na washiriki wa semina elekezi kwa Maafisa Elimu na Maafisa Michezo wa mikoa yote nchini, ikiwa ni maandalizi mahsusi ya uzinduzi rasmi wa wamishindano ya michezo ya Copa UMISSETA 2017, ambapo kampuni yavinywajibaridiya Coca-Cola imeendelea kudhamini mashindano hayo. 

Katikati ni Naibu Waziri wa Tawala za Mikoana SerikalizaMitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akiwa pamoja na Afisa Msimamizi wa Copa Cola-Cola, Pamela Lugenge (kushoto). Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki Dodoma na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini na Coca-Cola Tanzania. Ufunguzi rasmi wa michuano hii utafanyika katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma siku ya Ijumaa Aprili 28, 2017.
Afisa Msimamizi wa Copa Cola-Cola, Pamela Lugenge (kushoto) akizungumza na washiriki wa semina elekezi kwa Maafisa Elimu na Maafisa Michezo wa mikoa yote nchini, ikiwa ni maandalizi mahsusi ya uzinduzi rasmi wa mashindano ya michezo ya Copa UMISSETA 2017, ambapo kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola imeendelea kudhamini mashindano hayo. 

Katikati ni Naibu Waziri wa Tawalaza Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Bw Yusuf Singo (kulia). Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki Dodoma na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini na Coca-Cola Tanzania. Ufunguzi rasmi wa michuano hii utafanyika katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma siku ya Ijumaa Aprili 28, 2017.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BABA WA SHOKA ANAYESTAHILI TUZO!

$
0
0
 Hivi majuzi Globu ya Jamii katika pitapita zake ilikutana na Bw. Yusuph Hamisi, baba wa mtoto wa miezi 5 aitwaye Ilham Yusuph akiwa amembeba mwanae katika Kituo cha Afya cha Nagaga alipokuwa amempeleka Kliniki, baada ya kumtaka mama yake apumzike ili kazi hiyo afanye yeye. Watoto wanaopelekwa na Baba zao katika kituo hicho wanapata kipaumbele katika huduma kwani hawakai foleni. Kituo cha Afya  Nagaga kipo Kilometa 40 kutoka Mjini Masasi. Hakika wazazi wa kiume wa aina hii inabidi watafutiwe tuzo zao
Bw. Yusuph Hamisi, na  mtoto wake wa miezi 5 aitwaye Ilham Yusuph wakiwa katika kliniki ya Kituo cha Afya cha Nagaga, Masasi.

NGORONGORO: KITOVU CHA UTALII KINACHOWAVUTIA WATU MASHUHURI DUNIANI

$
0
0
Na Jumia Travel Tanzania
Inaonekana mwaka 2017 umeanza vizuri katika sekta ya utalii nchini Tanzania kutokana na watu kadhaa mashuhuri kuzuru vivutio vyake. Sehemu ambazo zimeonekana kuwavutia watu wengi zaidi ni hifadhi ya mbuga ya Serengeti na bonde la Ngorongoro.

Alianza mwigizaji maarufu wa filamu kutokea Hollywood nchini Marekani, Will Smith na mkewe Jada Pinkett-Smith. Mwanzoni mwa mwezi Machi walitua nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kujivinjari katika mbuga ya Serengeti. Wakiwa huko familia ya Smith walikutana na msanii mwingine kutokea huko huko Marekani, lakini huyu yeye ni mwanamitindo na mrembo, Chanel Iman.
Haikupita muda mrefu sana tangu watu hao mashuhuri kuwepo nchini, kwani siku chache zilizopita aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Taifa la Israel, Bw. Ehud Barak naye alitembelea mbuga ya Serengeti pamoja na Ngorongoro.


Hii ni ishara nzuri kwa sekta ya utalii nchini ambapo kupitia watu hawa maarufu wengine nao wanapata taarifa na kuhamasika kutembelea pia.

Kusoma zaidi BOFYA HAPA

INTRODUCING "KAZA MOYO" BY PETTY BARAKA

$
0
0
Wimbo mpya wa Petty Baraka unaitwa Kazi ya Moyo uliotengezwa Studio ya Pamoja Records ya Nas B 
Petty Baraka ni msanii anayefanya kazi nzuri ya muziki,awali alikuwa Mabatini jijini Mwanza sasa anapatikana Temeke jijini Dar es salaam. Wasiliana naye kwa simu namba 0653 710 388 
Petty Baraka anawaalika wapenzi wa muziki kumpokea kwa mikono miwili ili kutimiza ndoto zake katika muziki. 
Sikiliza wimbo Kazi ya Moyo ya Petty Baraka hapa chini

ISRAELI TOURISTS ACKNOWLEDGES TANZANIA AS BEST TOURISM DESTINATION

MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRIL 24,2017

HAFLA YA KUCHANGIA SERENGETI BOYS IJUMAA APRIL 28,2017

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeandaa hafla maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni ya timu ya Serengeti Boys inayojiandaa kucheza fainali za kuwania Kombe la Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchini Gabon. Fainali hizi zitafanyika kufanyika kuanzia Mei 14 hadi 28, 2017. 
TFF inatambua kuwa wadau mbalimbali wamekuwa wakichangia timu hiyo kupitia mitandao ya simu kama vile namba 0687 333 222 kadhalika Selcom kwa namba 22 33 44 pia kuweka fedha kwenye akaunti Na. 00 866 280 03 katika Benki ya Diamond Trust (DTB).
Sasa siku ya Ijumaa Aprili 28, 2017 TFF imeandaa hafla maalumu ya kupokea michango hiyo, lakini pia kuchangisha fedha zaidi maana lengo ni kukusanya shilingi bilioni moja (Sh. 1 Bil.) Hafla hiyo itafanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam kuanzia saa moja jioni.
TFF imeamua kutumia fursa kuwakaribisha wawakilishi wa makundi mbalimbali ili wawasilishe michango yao na kumkabidhi mgeni rasmi.

Kwa kutambua michango mbalimbali ambayo imekusanywa kupitia makundi ya mitandao ya jamii kama WhattsApp, facebook hivyo TFF inaomba wawakilishi wa makundi yote ya mitandao ya jamii (admins) ambao wamekusanya michango hii wajiorodheshe ili wapate fursa ya kukabidhi michango ya makundi yao kwa mgeni rasmi katika hafla hii.
Admins hawa wanaombwa wajiorodheshe kwa kutuma email kwenda fdf@tff.or.tz, kwa kupiga simu 0787 176767 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda 0787 176767 ambayo pia inapatikana kwenye mawasiliano ya WhattsApp.
Aidha wawakilishi wa makundi mengine kama idara za Serikali, mashirika ya umma na binafsi kadhalika watu binafsi ambao nao wamechangia nao pia  tunaomba wajioredheshe ili wapewe fursa pia ya kukabidhi michango yao siku hiyo ya Ijumaa.
TFF inashukuru sana kwa ushirikiano.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu ibariki Serengeti Boys


Engine za Land Rover Discovery, Defender, Range Rover na Puma zinauzwa

$
0
0
Tuna Engine za Land Rover Discovery , Defender Range Rover, Puma Engine Tdci 2.4, Td5,Tdi300,Tdi200,P38, pia tunaweza kukupatia Spare ya aina yoyote kutoka Europe kwa bei nafuu. 
Bei ya hiyo Land Rover Discocery  Engine Td5 ni T.sh.4.7 Milion; Gear Box T.sh. 2.7 Milion. 
Tunaleta kutoka U.K. zipo Dar es Salaam kwa maelezo zaidi wasiliana nasi 
Tel.+255674782666 +255652444311 
 on whatswap +447723550406

Leo ni siku ya kuzaliwa Sensei Rumadha Fundi "romi"

$
0
0
Leo ni siku ya kuzaliwa Sensei Rumadha Fundi (Romi) ambaye ni Mtanzania mtaalam na mwalimu wa ngazi za kimataifa  wa karate na Yoga. 
Tunapozungumzia watanzania waliozaliwa na vipaji na kufanikiwa kuvipigania na kuviendeleza vipaji hivyo hadi kufikia kiwango cha kimataifa jina la Sensei Rumadha Fundi aka Romi hatuwezi kulikwepa
Mtanzania huyu makazi yake ni nchini marekani. Kabla ya kujikita huko yeye  alikuwa ni mmoja ya wanafunzi wa karate katika dojo lililopo shule ya Sekondari ya wasichana ya  Zanakaki jijini Dar es salaam  chini ya mwalimu wake Sensei Natambo Guru Kamara Bomani (RIP). Baada ya hapo Sensei Rumadha akaenda kwa mafunzo zaidi nchini Japan,Sweden na Denmark. Pia akachaguliwa kwenda nchini India kwa mafunzo ya kuwa mtaalamu wa Yoga,
Kwa vipaji hivi vya Karate na Yoga vya ngazi ya kimataifa, Sensei Rumadha Fundi anaiwakilisha Tanzania kuwa nchi ya wenye vipaji .Sensei Rumadha Fundi ni mwalimu wa karate na yoga 
mwenye utalaamu na upeo wa hali ya juu sana,tena mwenye nidhamu.
Sensei Rumadha ni  mmoja wa walimu wa Kitanzania wa karate ambao wanafanya vizuri katika fani hii  ughaibuni.  
Sensei Rumadha ana mkanda mweusi ngazi ya tatu (Black belt 3rd Dan ya mtindo wa Goju Ryu, ambayo ni chimbuko la  dojo iliyojengwa na Master Eiichi Miyazato miaka 63 iliyo pita huko mjini Naha, Okinawa baada ya  kifo cha mwanzilishi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu , Master Chijun  Miyagi , ambayo hivi sasa  inaendeshwa na mtoto wake Yoshihiro Kancho Miyazato. Sensei Rumadha Fundi, kwa sasa ndiye  mwakilishi wa "JUNDOKAN SO HONBU" tawi la Tanzania. 
Pichani wa nne kushoto waliosimama ni Sensei Rumadha akiwa nchininUreno akishiriki katika kongamano la Karate la kimataifa la " European Jundokan  Gasshuku 2016" mwaka jana akiwa mjumbe wa  kitengo kinachosimamia ubora na uthabiti wa  sanaa asili ya mitindo ya  karate toka Okinawa kiitwacho " OKINAWA BODOKAN & KARATE FEDERATION" ambacho kimefanya mabadiliko ya kutofautisha  karate asilia na ile ya  kimichezo itayokuwa katika michezo ya  Olympiki.

Kutokana na mabadiliko ya  kimbinu na ufasaha yanayoonekana katika michezo hiyo, shirikisho hilo limeamua kutofautisha kabisa jinsi  Karate asilia itavyozidi kuimarika na kutochujwa na kuwa sanaa nyepesi, na pia, kuhakikisha kiundani zaidi kwamba  mbinu halisi za sanaa hiyo zinazingatiwa na ma- Sensei wote wa mitindo ya  Karate waliopata mafunzo visiwani Okinawa duniani kote. 

Hivyo Sensei Rumadha kwa sasa ni mjumbe wa timu hiyo ya Karate ya Okinawa ( Masters) toka mitindo mbalimbali inayotambulika na " BUDOKAN" kusambaza uadilifu wa mitindo hiyo kama jinsi ilivyokuwa  inafundisha na waasisi wake asilia.

KARIAKOO FAMILY DEVELOPMENT FOUNDATION CHAPATA UONGOZI MPYA

$
0
0
Wanachama wa chama cha  Kariakoo Family Development Foundation (KFDF) wamejipatia uongozi mpya baada ya kufanya mkutano mkuu wa uchaguzi siku ya Jumapili Aprili 23, 2017 katika ukumbi wa shule ya Msingi ya Jamhuri jijini Dar es salaam. Jumla ya wanachama hai na halali  41 walishirki katika uchaguzi huo, ambapo wanachama 23 walikuwepo ukumbini na wanachama 18 waishio nje ya nchi walipiga kura kwa njia ya mtandao. 
Bw. Alkarim Bhanji alishinda nafasi ya Uenyekiti akiwa mgombea pekee, wakati Bw. Mohamed Irapo alinyakua nafasi ya Makamu Mwenyekiti. Katibu Mkuu wa kipindi cha mpito Bw. Wahid Abdulghafoor aliweza kutetea kiti chake akiwa mgombea pekee. Nafasi ya Katibu Mkuu msaidizi imechukuliwa na Bw. Fabian Kimongw wakati Bw. Bakari Simba ametetea tena nafasi ya Mweka Hazina Msaidizi aliyokuwa akishika wakati wa kipindi cha mpito.
Katika uchaguzi huo uliokuwa umesimamiwa vyema na Katibu Mkuu wa klabu ya michezo ya Saigon,  Bw. Boi Juma,  jumla ya wajumbe watano kati ya sita wanaotakiwa kikatiba walichaguliwa. Hao ni  Bw. Shaaban Kessy Mtambo,  Bw. Abdallah Kizua,  Bw. Idrissa Jumbe, Bi. Sophia Muccadam na Bi. Salma King.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa KFDF Bw. Wahid Abdulghafoor, nafasi mbili za Mweka Hazina na Mjumbe mmoja zilizo wazi baada ya kutotokea mgombea zitajazwa baadaye katika uchaguzi mdogo.
KFDF ni chama kinachojumuisha wananchi  wanaoishi  ama waliopata kuishi eneo lote Kariakoo, dhumuni kuu likiwa ni kuwaunganisha upya na kufanya shughuli za kijamii kimaendeleo kwa lengo la kudumisha na kuendeleza umoja, mshikamano na undugu uliokuwepo miongoni mwa wakaazi wa eneo hilo maarufu la jiji la Dar es salaam toka enzi za mababu.

Msimamizi wa uchaguzi Bw. Boi Juma (mwenye bahasha mkononi) akipata picha ya pamoja na safu mpya ya uongozi wa KFDF pamoja na wanachama waliopo nchini baada ya kuhitimisha zoezi hilo siku ya Jumapili Aprili 23, 2017 katika ukumbi wa shule ya Msingi ya Jamhuri jijini Dar es salaam

Msimamizi wa uchaguzi Bw. Boi Juma (kati) akipata picha ya pamoja na safu mpya ya uongozi wa KFDF siku ya Jumapili Aprili 23, 2017 katika ukumbi wa shule ya Msingi ya Jamhuri jijini Dar es salaam.
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

MATUKIO KATIKA PICHA: KIKAO CHA 11 MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO APRIL 24, 2017

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu akiongoza kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017.
 Naibu Waziri wa Ujenzi uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Nyonyani akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017. 

UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU

$
0
0
Image result for umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
Na Mwandishi wetu, Vijimambo Blog
Nimekuja tena leo nimaitumaini yangu kuwa wote hamjambo na kwa kudra zake mola mtakua mnaendelea vyema na mihangaiko ya kila siku.

Na kama nilivyoandika wiki mbili zilizopita kuhusiana na swala la uraia pacha na katika kuchunguza kwangu maisha ya DIASPORA hasa WaTanzania nimegundua umoja wetu katika kulipigania swala hili la uraia pacha ni mushkeli, nadhani ni kutokana na tofauti tulizo nazo katika mafanikio na nafasi ya kila mmoja wetu ughaibuni na wengine kutoona umuhimu wa swala zima la uraia pacha.

Kuna aina mbili ya Watanzania DIASPORA, kwanza ni wale Watanzania ambao wanaishi nje ya Tanzania na bado wanashikilia pasi za kusafiria za Tanzania na kundi la pili ni lile la WaTanzania waliobadili uraia wao kwa ajili ya kubanwa na sheria za ukaazi wa nchi walizopo, kundi hili la pili kisheria halitambuliki kama Tanzania DIASPORA kwani ni raia tayari wa nchi walizochukua uraia. Tofauti hizi ndio kikwazo kikubwa cha umoja na mshikamano wa msukumo na nia ya kupigania uraia pacha.

WaTanzania ambao bado wanapasi za kusafiria za Tanzania ukumbuke kwamba swala hili la uraia pacha ni kwa faida ya vizazi vyetu unapolipuuzia ulitendehi haki swala lenyewe wakiwemo watoto wetu ambao wanapozaliwa ughaibuni uwezekano ni mkubwa wa kuchukua uraia wa nchi aliyopo na nchi kama Marekani watoto wakibahatika kuzaliwa huko wanakua raia moja kwa moja.

Kitu kitakachosaidia kwa mtoto kurithi mali zako Tanzania ni swala hili la uraia pacha litakapopatiwa ufumbuzi. Japo kuwa wewe unaefikiria halikuhusu kwa sababu tu hujabadili uraia lakini una miaka zaidi ya 20 unaishi ughaibuni na una watoto hiyo ni kujidanganya, pigania uraia pacha upatikane ili mali zako zisipotee kwani sheria iliyopo sasa kama wewe sio raia wa Tanzania huwezi kumiliki ardhi, kesho na keshokutwa usipokuwepo nani atarithi mali zako Tanzania? kama sio mtoto wako ni nani tena. Tupiganie kwa pamoja swala hili ni letu sote.

Pamoja na kwamba baadhi ya WaTanzania  wamebadili uraia kumbuka kwa huo ni kwenye karatasi tu asili yao ya kuzaliwa daima itabaki Tanzania. Ni haki ya kila mmoja wetu kupigania kwa nguvu zote, wenzetu Kenya iliwachukua zaidi ya miaka 20 mpaka serikali yao kukubali uraia pacha ipo siku serikali yetu sikivu itaona umuhimu wa uraia pacha na kuwezesha kufanikisha swala hili lakini ukumbuke umoja wetu ndio utakaokua nguzo kuu ya mafanikio haya.

Nakupa mfano mdogo hapa juzi kati kulitokea WaTanzania kuja na wazo la kuanzisha umoja wa WaTanzania Duniani kwa lengo kuu la kupigania uraia pacha na haki za WaTanzania wanaishi nje ya nchi yao, wazo lao ni zuri kama yalivyokua mawazo mengine ya kuanzisha jumuiya zilizopita japo kila chenye mwanzo hakikosi changamoto zake na mimi mwenyewe nilifikiri changamoto zingetokea Tanzania lakini kinyume chake changamoto nyingi zimetokea kwa WaTanzania waishio ughaibuni wakikiwemo baadhi ya WaTanzania wenye Jumuiya zao nchi zilizopo kupiga vita za makusudi kwa lengo la kukwamisha jitihada hizi na kusahau kwamba umoja umeundwa ili kuunganisha nguvu ya WaTanzania Duniani.

Umoja huu haukua na lengo ya kuua jumuiya zingine za WaTanzania zilizoanzishwa hapo nyuma kwenye nchini zao kama inavyofikiriwa na baadhi ya wadau ughaibuni, Lengo kama nilipokutaarifu hapo mwanzo ni kuunganisha nguvu ya pamoja ikiwemo juhudi na mawazo za jumuiya hizo ilizoanzisha awali ya kupigania uraia pacha UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU kama nia yetu ni moja kwanini tunatofautiana na kulumbana kwa hili? Bila ya sisi kuondoa tofauti zetu na kuwa kitu kimoja Uraia pacha utachukua muda mrefu zaidi kwa serikali kutuelewa.

Mfano mwingine ni wakati tume ya Warioba ilipokua ikitafuta maoni ya katiba pendekezwa, Diaspora pamoja na kwamba tunakadiriwa tupo zaidi ya milioni 2 lakini waliotoa maoni hawakuzidi elfu sitini, hii ni jinsi gani sisi wenyewe hatuoni umuhimu wa hili swala inabidi tubadilike tuunganishe nguvu ya pamoja popote pale ulipo nje ya Tanzania aidha wewe ni raia wa nchi nyingine au bado unashikilia pasi ya Tanzania kumbuka atakae kula matunda ya jasho lako ni kizazi chako, acha watoto wakukumbuke kwa hili kwamba ulilisimamia kwa ajili yao.

Naomba kwa leo niishie hapa.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Diaspora.

MKUU WA WILAYA MKURANGA AFUNGUA MAFUNZO YA KILIMO BORA

$
0
0
SERIKALI kupitia Bodi ya Korosho Tanzania imejipanga kuhakikisha pembejeo za korosho kwa`msimu ujao wa`mwaka 2017/18 kwa wakulima wa zao la korosho zinawafikia wakuima kwa`wakati kwani mpaka sasa tani 2,890 za Salfa ya unga na lita 30,000 za viatilifu vya maji zimeshawasili katika Bandari ya Dar es Slalaam. 

Akifungua mafunzo ya kilimo bora na matumizi sahihi ya viuatilifu kwa wakulima na wapuliziaji dawa wa Mkoa wa Pwani,Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbeto Sanga amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa nafasi ya kuwafunza wawakilishi wa wakulima na wadau wa zao la korosho namna ya kuhudumia zao hilo.

Alisema katika msimu uliopita wa mwaka 2016/17 upatikanaji na usambazaji wa pembejeo za ruzuku za zao la korosho ulikuwa wa kuridhisha kutokana na kupatikana kwa fedha za ushuru wa mauzo ya korosho nje ya nchi kwa wakati kulikowezesha uagizaji wa pembejeo nao ufanyike kwa wakati.

“Kupatikana kwa fedha za ushuru wa mauzo ya korosho nje ya nchi kwa wakati kuliwezesha uagizaji wa pembejeo ufanyike kwa wakati hivyo kumfikia mkulima kabla ya muda wa kupuliza dawa kwenye mikorosho haujafika,”amesema Sanga.

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filbeto Sanga akizungumza na wakulima,wapuliziaji dawa wa korosho wa mkoa wa Pwani katika mafunzo ya kilimo bora na matumizi sahihi ya viuatilifu, leo mkoani Pwani
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde akizungumza na wakulima,wapuliziaji dawa wa korosho wa mkoa wa Pwani.
Mwakilishi wa Mkurugenzi kanda ya kusini ARI-NALIENDELE Dr Shamte Shomari akizungumza na wakulima,wapuliziaji dawa wa korosho wa mkoa wa Pwani.

wakulima,wapuliziaji dawa wa korosho wa mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filbeto Sanga.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filbeto Sanga akiwa katika picha ya pamoja na wakulima,wapuliziaji dawa wa korosho wa mkoa wa Pwani.picha zote na Emmanuel Massa,Globu ya Jamii.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA PROF KABUDI AKIFAFNUA KUHUSU MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI

PROF. KABUDI AFAFANUA KUHUSU MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI

Viewing all 110176 articles
Browse latest View live




Latest Images