Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1656 | 1657 | (Page 1658) | 1659 | 1660 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imezindua jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi kwa wanawake wa Wilaya ya Handeni  kwenye ukumbi wa maount Ilulu uliopo Kabuku mjini lenye ujumbe wa “Wezesha wanawake kiuchumi ili kujenga uchumi wa kati na Tanzania ya Viwanda”.

  Jukwaa hili linalengo la kuwakutanisha wanawake pamoja na kujadili fursa, changamoto na jinsi ya kushiriki kikamilifu katika biashara na shughuli nyingine za kiuchumi katika Wilaya ya Handeni.

   Akizungumza kwenye uzinduzi wa Jukwaa hilo Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni  Bw. John Mahali aliyekuwa mgeni rasmi akimwakilisha mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe alisema kuwa jukwaa la wanawake hilo  litasaidia  kuongeza uelewa kwa wanawake katika upatikanaji  wa mitaji , sheria za nchi katika masuala ya kiuchumi na jinsi ya kujitegemea.

  Aliongeza kuwa wanawake wamekuwa hawapati fursa za kutosha za kiuchumi hapa Nchini hata na duniani kote kutokana na kutokuwa na usawa katika fursa , uwezo wa kupata mitaji.

  “jukwaaa litasaidia kuondoa matabaka na sheri ambazo zitasaidia kupunguza ubaguzi wa kiuchumi kwa wanawake, ambalo ni jambo la muhimu sana katika kuleta maendeleo ya usawa katika pato la Taifa, jamii na familia” alisema Bw. John. 
   Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw William Makufwe wakwanza kulia akifuatiwa na Katibu tawala Wilaya Bw John Mahali wakitazama Moja ya bidhaa ya vikapu vinavyotengenezwa na kikundi cha wanawake tupendane cha segera
   Katibu tawala Wilaya Bw John Mahali akizungumza na wanawake waiojitokeza kwenye Uzinduzi wa jukwaa Hilo.
   Mwenyekiti wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi Wilaya Bi Fatuma Zuberi akipokea katiba kutoka Kwa mgeni rasmi Katibu tawala Wilaya Bw John Mahali.
   Baadhi ya wanawake wakishiriki wa Uzinduzi wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi Wilaya  ya Handeni.


  0 0

  Na Catherine Sungura, WAMJW             
   Ujumbe wa wawekezaji toka nchini Misri umewasili nchini kufanya mazungumzo na serikali ya Tanzania kwa nia ya kujenga  viwanda vya dawa za binadamu zikiwemo za majimaji pamoja na zile za antibiotic.
  Ujumbe huo ulikutana jana na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  pamoja na wawakilishi toka wizara Viwanda,Biashara na Uwekezaji na Kituo cha Uwekezaji cha Taifa (TIC) kwenye ofisi ndogo ya wizara ya afya, maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto iliyopo jijini Dar es Salaam

  Ujumbe huo ulisema kuwa kiwanda walichokusudia kujenga nchini hapa kitazalisha  dawa za majimaji yaani “IV Fluids” pamoja na “antiobiotics” za aina mbalimbali  ikiwemo "Paracetamol IV” na dawa za kutibu Malaria

  Aidha, walisema lengo lao ni kujenga kiwanda kikubwa ambacho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha dawa ambazo zitawahudumia watanzania pamoja na nchi za Afrika Mashariki na ya kati. Wawekezaji hao pia wanatarajia kuisaidia Tanzania katika uzalishaji wa chanjo ya ugonjwa wa homa ya Ini (Hepatics B na C ).

  Kwa upande wake Waziri Ummy amewaahidi wawekezaji hao kuwasaidia katika mipango ya ujenzi huo na kutoa ushirikiano wa dhati katika kufanikisha viwanda hivyo vinajenga nchini kwa muda uliopangwa.

  “Naelekeza kwa taasisi zote zitakazoguswa na uanzishwaji wa viwanda hivi watoe ushirikiano wa hali ya juu ili lengo hili lifikiwe,soko la dawa hapa nchini lipo naomba niwahakikishie hili”alisema waziri Ummy.

  Waziri Ummy aliwaomba wawekezaji hao kuharakisha ujenzi wa viwanda huo na kujengwa ndani ya miezi kumi na nane kama walivyoahidi ili watanzania waanze kunufaika mapema. 

   Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika mazungumzo na Ujumbe huo wa wawekezaji toka nchini Misri kwenye ofisi ndogo ya wizara hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam
   Wawakilishi toka wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Kituo cha Uwekezaji cha Taifa (TIC) wakiwa katika mazungumzo hayo kwenye ofisi ndogo ya wizara ya afya, maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto iliyopo jijini Dar es Salaam
   Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja  na Ujumbe huo wa wawekezaji toka nchini Misri  na Wawakilishi toka wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Kituo cha Uwekezaji cha Taifa (TIC) baada ya mazungumzo kwenye ofisi ndogo ya wizara hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam

  0 0


   Balozi wa Norway hapa nchini,  Mhe. Hanne-Marie akiongea      katika hafla ya fupi ya makabidhiano ya jengo la Afya ya Akili Hospitali ya Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na Kituo cha Tanga International Conference Centre (TICC), Shighela alisema vita ya madawa itakuwa endelevu.                                       
  MKUU wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shighela akizungumza katika hafla ya fupi ya makabidhiano ya jengo la Afya ya Akili Hospitali ya Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na Kituo cha Tanga International Conference Centre (TICC), Shighela alisema vita ya madawa itakuwa endelevu.
  vita ya madawa itakuwa endelevu.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighela (katikati), Balozi wa Norway wa kwanza kulia, Hanne-Marie Karstand na Mganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita (kushoto) wakifungua jengo la Afya ya Akili hospitali ya Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na kituo cha Tanga International Comperence Centre Tanga.


  0 0

  Gari ikiwa imejikinga na mwamvuli ili mvua isiingie ndani.

  0 0

   Vurugur  zimeibuka wakati Wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) kupambana na  wenzao wanaosadikiwa kuwa wapinzani wao baada ya kundi hilo  kuvamia mkutano   na waandishi wa habari katika Hotel ya Vinna Hotel maeneo ya  Mabibo jijini Dar es salaam, na kuzua taharuki kubwa kwa waandishi wa habari na wakaazi wa eneo hilo.  Wanahabari kadhaa walijeruhiwa na mmoja kuharibiwa kamera yake ya video.
  Mashuhuda wamesema watu kadhaa wasiojulikana walifika hapo wakiwa wamefunika nyuso zao kwa vitambaa huku wakiwa na silaha za jadi na kuanza vurugu.
  Baada ya mkutano kuvurugika baadhi ya  waliokuja kufanya vurugu walikimbia huku wakikimbizwa na wanachi wenye hasira kali ambao walifanikiwa kumkamata mmoja wao na kumjeruhi  kwa kumkata maungio ya kisigino ya mguu wake wa kulia.
  Juhudi za kuwapata wasemaji wa pande mbili hizo zinaendelea.
  Taharuki  katika Hotel ya Vinna maeneo ya  Mabibo jijini Dar es salaam
   Mmoja wa watuhumiwa  wa uvamizi huo akiwa anapambana
   Mmoja wa watuhumiwa  wa uvamizi huo akiwa anapambana
   Mmoja wa watuhumiwa wa uvamizi akiwa chini ya ulinzi mara baada ya kudhibitiwa na na wananchi kisha kumkata mguu na kushindwa kutembea
  Mtuhumiwa akiwa amekatwa mguu wa kulia akiugulia maumivu  baada ya kujeruhiwa


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama ameeleza kukamilika kwa maandalizi ya kuadhimisha sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zitakazofanyika Viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma, siku ya jumatano Aprili 26, 2017.
  Ameyasema hayo leo wakati akizungumza waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Aprili 22, 2017 katika Ofisi yake Dodoma.
  “Nipende kuwaeleza Watanzania wote kuwa hadi sasa maandalizi ya kuifikia siku ya Maadhimisho ya Sherehe za Muungano tayari yamekamilika kwa kuangalia mambo yote yaliyopangwa katika ratiba ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli.”Alisema Waziri Mhagama.
  Amesema sherehe hizo zitakuwa na  upekee wa aina yake ukizingatia kuwa  ni mara ya kwanza tangu Serikali ilipotimiza adhma yake ya kuhamia Dodoma.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika Mkoani Dodoma 26 Aprili 2017.Kulia kwake ni  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Januari Makamba na kushoto  ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Jordan Rugimbana.

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Januari Makamba akizungumza na waandishi wa habari leo Mjini Dodoma kuhusu matukio mbalimbali yatakayokuwepo katika Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika Mkoani Dodoma 26 Aprili 2017.Kushoto kwake ni  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe,Jenista Mhagama na mwishoni ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw.Jordan Rugimbana.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Jordan Rugimbana akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika Mkoani Dodoma 26 Aprili 2017 na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi.Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe,Jenista Mhagama na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Januari Makamba.


  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe amekutana na na uongozi wa klabu ya Simba ukiongozwa na Rais wake Bw. Evans Aveva kwenye Ofisi zake Mjini Dodoma.
  Uongozi wa Simba umeitikia wito wa Mhe. Mwakyembe wa kukutana naye na kujadili masuala mbalimbali ya mpira wa Miguu zikiwemo fursa na changamoto katika mabadiliko na maendeleo ya uendeshaji wa timu.
  Aidha  Mhe. Mwakyembe  amepokea maoni ya Uongozi wa samba na kusahauri kuendelea kutoa ushirikiano na wadau wa mpira wa miguu nchini.
  Kikao hicho pia kilihudhuriwa  na Katibu Mkuu Wizara husika prof Elisante Ole Gabriel, Mkurugenzi wa Michezo Yusufu Omary, Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja, na Msajili wa Vilabu na Vyama nchini.
    Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harison Mwakyembe akizungumza na uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wake Bw. Evans Aveva Mjini Dodoma. 
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja  na uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wake Bw. Evans Aveva Mjini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WHUSM Dodoma.

  0 0  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa Uchangiaji wa Madawati kwa ajili ya Skuli za Msingi na  Sekondari za Zanzibar kwa Viongozi mbali mbali katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mnazi mmoja Mjini Unguja
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea mfano wa Hundi ya Shilingi za Kitanzania Millioni Arobaini na Mbili kutoka kwa Kanishna wa ZRB Amour  Hamil Bakari  (katikati)  wakati wa Uchangiaji wa Madawati kwa ajili ya Skuli za  Serikali, katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi-Zanzibar  Mnazi mmoja Mjini Unguja,(kulia) Mwenyekiti wa Kamati ya Uchangiaji Madawati na Waziri wa  nchi Ofisi ya Rais,Sheria,Katiba,Utumishi wa Umma na Utawala Boro Mhe.Haroun Ali Suleiman,(kushoto) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali pia naibu Mwenyekiti wa kamati Mhe,Riziki Pembe Juma akifuatiwa na Naibu Kamishna wa ZRB Hadija Shamte

   Wakuu wa Mikoa na Viongozi wengine mbali mbali wakiwa katika hafla ya Uzinduzi wa Uhamasishaji Uchangiaji wa Madawati kwa ajili ya Skuli za Msingi na  Sekondari za Zanzibar
   Baadhi ya wajumbe wa Kamati wa Uchangiaji wa Madawati iliyoteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakimsikiliza Rais alipokuwa akifanya uzinduzi na uhamasishaji huo 
  Baadhi ya Viongozi wengine mbalimbali wakiwa katika hafla ya Uzinduzi wa Uhamasishaji Uchangiaji wa Madawati kwa ajili ya Skuli za Msingi na  Sekondari za Zanzibar katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. 
  Picha zote na IKULU. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0  0 0


  0 0  0 0

   Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akiruka juu sambamba na kipa wa Tanzania Prisons, Andrew Ntala katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Yanga imeshinda 3-0.
  Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo lililofungwa na Amis Tambwe.
   Wachezaji wa Tanzania Prisons wakiomba dua kabla ya mchezo.


  Godfrey Taita akichuana na mchezaji wa Yanga.


  Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa, akimtoka kipa wa Tanzania Prisons, Aron Kalambo, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 3-0. (Picha na Francis Dande).

  0 0
  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza wanafunzi kote nchini kupenda kusoma masomo ya Sayansi hasa watoto wa kike ili Taifa liweze kujitosheleza kwa wataalamu wa fani mbalimbali nchini hasa wakati huu ambao Taifa linaelekea kwenye uchumi wa Viwanda.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo katika hotuba yake kwenye mahafali ya Pili ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wa shule ya sekondari ya WAMA- NAKANYAMA Jijini Dar es Salaam, mahafali ambayo imehudhuriwa na wake wa Marais Wastaafu.
  Makamu wa Rais amesema haitapendeza hata kidogo ajira nyingi nchini kuchukuliwa na wataalamu mbalimbali mataifa ya nje hasa kipindi hiki wakati Serikali inahimiza ujenzi wa viwanda hivyo amesisitiza wanafunzi wajikite kwenye kusoma masomo ya sayansi ili taifa liweze kujitosheleza kwa ajili ya manufaa ya maendeleo ya taifa. Amesema katika kuhakikisha taifa lipata wanasayansi wengi, Serikali inaendelea na mpango wa ujenzi wa maabara na kununua vifaa vya maabara ili kuhamasisha wanafunzi wengi zaidi kupenda kusoma masomo ya sayansi kote nchini.
  Makamu wa Rais pia amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya Tano inakusudia kuimarisha ufundishaji wa masomo ya Teknolojia ya habari na Mawasiliano –TEHAMA- katika shule za Sekondari na kujenga maabara za kompyuta nia ikiwa ni kuongeza wataalamu wa fani hiyo nchini. Kuhusu mila na desturi kandamizi kwa wanawake na wasichana zilizopo kwenye baadhi ya jamii nchini, Makamu wa Rais ameitaka jamii kukomesha mila hizo na iwashirikishe wanawake katika mipango na mikakati ya maendeleo ya nchi kwani watakuwa ni chachu ya maendeleo katika jamii husika.

  “Wote tunajua wanawake ni chachu na kiungo muhimu katika maendeleo ya jamii, Taifa na Dunia kwa ujumla hivyo ni wajibu wa jamii kushirikisha wanawake katika kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo kote nchini” amesisitiza Makamu wa Rais.
  Makamu wa Rais pia ameipongeza Taasisi ya Wanawake na Maendeleo – WAMA- kwa kujenga shule Mbili za Sekondari na kusomesha watoto wanaotoka kwenye familia maskini na yatima na kusema huo ni mfano wa kuingwa na wadau wengine wa maendeleo katika kusaidia kundi hilo ili watoto wanaotoka kwenye familia maskini nao waweze kuapata elimu itakayowasaidia katika maisha yao ya baadae. Kuhusu changamoto zinazoikabili shule ya WAMA – NAKAYAMA, Makamu wa Rais ameahidi kushughulikia changamoto hizo ikiwemo uhaba wa maji, ubovu wa barabara kuelekea kwenye shule hiyo na tatizo la uhaba wa mabweni
  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama SALMA KIKWETE amesema aliamua kuanzisha taasisi hiyo ambayo inamiliki shule Mbili mpaka sasa ili kusaidia watoto wa maskini na yatima kupata elimu bure ambapo mpaka sasa kuna idadi kubwa ya wanafunzi wanaliohitimu katika shule hizo ambao wamejiunga na masomo ya elimu ya juu. Mama Salma Kikwete ameshukuru ushirikiano mkubwa anaopata kutoka Serikalini unaolenga kuhakikisha shule zinazoendeshwa na taaisisi hiyo ikiwemo ya Wama – Nakayama zinafanya vizuri.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi wengine wakiangalia kwa vitendo majaribio ya kiyasansi kutoka kwa wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya sekondari ya WAMA NAKAYAMA kwenye sherehe za mahafali yao ambapo wanafunzi 45 wamehitimu. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete(kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa WAMA Bi.Zakhia Meghji wakiimba wimbo maalumu wa shule ya Sekondari ya WAMA NAKAYAMA wakati wa mahafali ya pili ya kidato cha sita ambapo wanafunzi 45 wamehitimu.
  Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu kidato cha sita katika shule ya sekondari WAMA NAKAYAMA.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba amekutana na kufanya mazunguzo na Mabalozi Wateule wanaoenda kuiwakilisha Tanzania maeneo mbalimbali Duniani.Mazungumzo hayo yaliyofanyika ofisini kwake Makao Makuu ya Nchi mjini Dodoma, yalijikita katika kujadili namna bora ya kuiwakilisha Tanzania ughaibuni kwa kuzingatia sera ya nchi ya mambo ya nje, kwa lengo la kuboresha mahusiano ya Kidiplomasia baina ya Tanzania na nchi hizo, na kwa kuzingatia maslahi mapana ya kiuchumi ya nchi yetu ikiwemo kutangaza shughuli za utalii zinazopatikana nchini. 
  Naibu Waziri Mhe. Dkt. Susan Kolimba akisisitiza jambo 

  Balozi Mteule Baraka H. Luvanda akichangia jambo wakati wa mazungumzo. Punde baada ya mazungumzo na Mhe. Naibu Waziri, Mabalozi walikutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 
  Katibu Mkuu Wizara Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.Aziz P Mlima akiongea na Mabalozi ofisini kwake mjini Dodoma 
  Mazunguzo yakiendelea 

  0 0

  Na: Athumani Shariff

  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo amesaini kandarasi zenye thamani ya dola za Marekani Milioni 268.35 ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 600 za Tanzania mjini Tabora kwa mkopo wa benki ya Exim ya nchini India kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzani kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji kutoa Ziwa Victoria na kupeleka katika Manispaa ya Tabora na Halmashauri za Igunga, Uyui, Shinyanga Vijijini na Nzega. 

  Utekelezaji wa mradi ni wa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ya Mradi ilikuwa kufanya usanifu na kuandaa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya ujenzi, kazi ambayo ilifanywa na Kampuni ya WAPCOS Ltd ya India na ilikamilika mwezi Desemba 2015. 

  Awamu ya pili ni ujenzi wa mradi ambao umegawanyika katika sehemu tatu. Sehemu ya kwanza itaanzia Kijiji cha Solwa (kilichopo Wilaya ya Shinyanga Vijijini) hadi Mji wa Nzega, ujenzi utafanywa na Kampuni ya Megha Engineering Infrastructures Ltd ya India. Sehemu ya Pili inaanzia Mjini Nzega mjini hadi Manispaa ya Tabora kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, ujenzi utafanywa na Kampuni ya L&T ikishirikiana na kampuni ya Shriram zote kutoka India. 

  Sehemu ya tatu inaanzia Nzega mjini hadi Igunga mjini, ujenzi utafanywa na Kampuni ya Afcons ikishirikiana na kampuni ya SMC zote kutoka India. Usimamizi wa mradi unafanywa na Kampuni ya WAPCOS Ltd ya India. 

  Katibu Mkuu Wizara ya maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo na Visay Uplenchwar wa Kampuni ya Megha Engineering Infrastructures Ltd akisaini Mikataba ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka kijiji cha Solwa Shinyanga na kupeleka maji Nzega.
   Mbunge wa Nzega Hussein Bashe akimsalimia waziri wa Maji na Umwagiliaji Eng. Lwenge
   Waziri wa maji na Umwagiliaji Eng. Gerson Lwenge akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakati alipowasiri katika viwanja vya Furahisha Tabora.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh.Amos Makalla amepokea msaada wa mifuko 400 ya saruji,kutoka kwa Benki ya AKIBA Commercial Bank Ltd ,kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa njia za Wagonjwa,yenye urefu wa mita 175 katika hospitali ya Mkoa wa Mbeya.

  Akizungumza hayo jana jijini Mbeya wakati wa kupokea msaada huo,RC Makalla aliwashukuru Wadau hao kwa kujitolea na kulishughulikia ombi lake kwa haraka na kwa uzito wa juu kabisa.

  "Nawashukuru sana Wadau AKIBA Commercial Bank Ltd , kwa kulishughulikia ombi langu hili, ambalo sikutarajia kama lingechukua muda mfupi hivi,nawashukuru sana na nawaomba msichoke na  tuendelee kuijenga Mbeya yetu kwa pamoja",alisema Makalla.

  Makala alisema kuwa kupitia kwa marafiki wa hospitali ya Mkoa,wanaoishi ndani na nje ya mkoa huo,kupitia harambee walioifanya hivi karibuni wamefanikiwa kukamilisha ujenzi wa mita 55 na na kuwa awamu ya pili inaendelea kwa ujenzi wa mita 175.

  Mh.Makalla alisema kuwa katika awamu ya kwanza ya ujenzi huo,zilitumika fedha jumla ya shilingi milioni 600,kutokana na mahitaji kuwa makubwa ya ujenzi,ujenzi  ukasimama. kwa sababu zilikuwa zikihitajika fedha nyingine kiasi cha shilingi milioni 55,ndipo wakachukua hatua za kuomba msaada zaidi kwa wadau ambao ni AKIBA Commercial Bank Ltd .

  "Kukamilika kwa ujenzi huu kutaondoa tatizo la wagonjwa kupelekwa au kwenda wodini kwa taabu, kwani wakati wa mvua tatizo linakuwa kubwa ",alisema Mh Makalla.

  Kwa upande wa Akiba Commercial Bank kupitia kwa Afisa Masoko na Uendeshaji Bi Dora Saria amesema waliguswa sana baada ya kuombwa na Mkuu wa Mkoa kutokana na wananchi kupata shida hasa wagonjwa kwenda wodini au kupeleka maiti kwenye chumba cha kuhifadhia maiti

  Hivyo wao kama taasisi ya Benki waliguswa na jambo hilo,na wakachukua hatua ya kuchangia shilingi milioni 5 sawa na Mifuko 400 ya saruji na kuahidi kutoa Mafunzo na mikopo kwa wajasiriamali 

  Aidha Akiba wamevutiwa na jitihada za Mkuu wa Mkoa kuliweka jiji safi hivyo watatoa Vifaa vya usafi na kushiriki kufanya usafi mwisho wa mwezi huu.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh.Amos Makalla akikabidhiwa mifuko 400 ya saruji na Bi. Dora Saria ambaye ni Afisa Masoko wa Akiba Commercial Bank Jijini Mbeya.Na Mr.Pengo wa Globu ya jamii Mbeya
  RC Makalla akitoa neno la shukrani mbele ya Viongozi na wafanyakazi wa Benki ya Akiba na Serikali kwa ujumla.

  0 0  0 0

  Hapa Kazi Tu!! Ndivyo Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Bi. Rehema Madusa anafanya mara baada ya yeye pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya yake kuungana kwa pamoja na kuamua kuanza kuitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya miundombinu kama barabara na majengo mengine ya kiserikali na ya kijamii kama Ujenzi wa Zahanati, Kituo cha Afya na Ujenzi wa maabara kwa shule za Sekondari. 

  Katika Ziara hiyo aliyoianza hivi karibuni,DC Madusa alibaini changamoto mbalimbali na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi wa haraka ili kuwezesha gurudumu la maendeleo kusonga mbele. 

  Aidha, DC Madusa akizungumza na mtandao huu amesema amejipanga kikamilifu kuhakikisha Shule za Sekondari za Wilaya hiyo zinakua za mfano kwenye mitihani kwa ngazi ya Mkoa, Kanda na Taifa kwa Ujumla, hivyo amewataka wananchi wake kumuunga mkono ikiwemo kuhakikisha nidhamu ya wanafunzi inatazamwa kwa jicho la karibu ili kuwasaidia walimu kufanya majukumu yao pasi na matatizo yeyote
  Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Rehema Madusa akitoa maelekezo  kwa mfadhili kuondoa bati zisizotakiwa (G. 30) na kupaua kwa bati zenye viwango vilivyopitishwa na serikali (G. 28) katika moja ya shule huko mjini Chunya mkoani Mbeya.Na Mr.Pengo wa Globu ya Jamii Mbeya.

older | 1 | .... | 1656 | 1657 | (Page 1658) | 1659 | 1660 | .... | 3270 | newer