Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1655 | 1656 | (Page 1657) | 1658 | 1659 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Meneja Masoko wa kampuni ya Sun King nchini Tanzania, Albert Msengezi, akizungumza na wanahabari kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini, uliofanyika hii leo Buzuruga Plaza Jijini Mwanza.
  #BMGHabari
  Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King Tanzania, Judie Wu, akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza hii leo.
  Mgeni Rasmi, Afisa Tawala wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Zubeda Kimaro, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza hii leo.
  Afisa Tawala wilayani Nyamagana, Zubeda Kimaro (mwenye kofia), akizindua ofisi ya Sun King Jijini Mwanza ikiwa ni uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo kimataifa hii leo. Kulia ni Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King Tanzania, Judie Wu.

  0 0  Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya TBL Afrika Mashariki, Thomas Kamphuis akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bia ya Castle Lite 'Castle Lite Unlocks' jijini Dar es Salaam. 


  0 0

  Mchezo wa Robo Fainali ya Nne ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup 2016/2017), kati ya Young Africans na Tanzania Prisons FC utafanyika kesho Aprili 22, 2017 saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
  Mchezo huo utatoa mshindi ambaye ataungana na timu nyingine tatu ambazo tayari zimefuzu kwa hatua ya Nusu Fainali. Timu zilizotangulia Nusu Fainali ya ASFC ni za Mbao FC, Simba SC na Azam FC.
  Jumapili Aprili 23, mwaka huu kutakuwa na droo ya wazi kwa timu nne zitakazokuwa zimefuzu kwa hatua ya Nusu Fainali ya ASFC, itakayofanyika Kituo cha Televisheni cha Azam ambao ni wadhamini wakuu wa jina la michuano na haki ya kuonesha mubashara michuano hii ambayo inafanyika kwa msimu wa pili mfululizo.
  Azam FC ilikata tiketi ya kucheza Nusu Fainali ya ASFC baada ya kuifunga Ndanda FC mabao 3-1, kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam Aprili 5, 2017 ikitanguliwa na Mbao iliyoishinda Kagera Sugar mabao 2-1 katika mchezo ulifanyika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera Machi 18, 2017 ilihali Machi 19, mwaka huu Simba iliwatoa Madini ya Arusha kwenye mchezo uliofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
  Nusu Fainali inatarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu, kabla ya fainali ambako Bingwa wa michuano hii ambayo msimu huu ilishirikisha timu 86 ikiwa ni pamoja na za Ligi Kuu ya Vodacom (timu 16); Ligi Daraja la Kwanza (timu 24); Ligi Daraja la Pili (timu 24) na mabingwa wa mikoa timu 22, atazawadiwa Sh. 50 milioni na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho - CAF.  0 0  0 0

  Mining industry equipment 

  TANZANIA Chamber of Minerals and Energy (TCME) notes with concern the false allegations that Mining Companies have not been paying taxes in Tanzania. The Chamber represents member companies in the formal mining sector, from junior explorers to large-scale producers as well as medium scale miners. 

  The Chamber and its members support a well-regulated local industry and place great emphasis on compliance with all relevant local and international laws and rules, including tax codes governing its members. 

  Mining companies in Tanzania are highly regulated and remain to be significant contributors to the economy of the country in many ways, among them being through tax payments and employment creation. Between 2009 and 2015, the Tanzania Minerals Audit Agency, an arm of the Ministry of Energy and Minerals, reported that these companies collectively paid over USD390 Million (TZS 870 Billion) in Royalties, and USD 305 Million (TZS680 Billion) in Corporation Taxes, along with other significant taxes. In 2015 alone, the five major gold mines and one diamond mine paid a total of USD65.5 Million (TZS 146 Billion) in royalties to Tanzania’s coffers, and over USD 170 Million (TZS380 Billion) in other taxes. 

  These amounts are expected to have increased in 2016. Concerns have been raised about Mining Companies incorrectly benefitting by getting VAT refunds. This is simply not true. As Mining Companies export all that they produce, they, like any other exporting industry, are categorized as zero rated under the VAT Laws and are therefore eligible to get refund of input VAT incurred on their purchases.
  It should however, be noted that Mining companies still pay VAT on specific categories not allowable to be claimed under the VAT law. For example, mining companies have continued to pay VAT on catering services, on purchase of spares parts or repairs and maintenance services for light vehicles categorized as passenger vehicles under the VAT Act, 2014 which form large part of the Mining companies fleet. 

  It should be noted that the VAT regime under which mining companies are operating is the same as for any other exporting company in other sectors. In addition, the formal mining sectors employs 7,355 people directly and more than 3,000 people indirectly, in support industries. Given that each of these people in formal jobs supports roughly 11 people, the industry provides a direct livelihood to an estimated 114,000 people. The taxes paid provide funding for among other things, construction of crucial infrastructure required for the development of the country. 


  0 0


  Kituo cha mazoezi cha Bodyline Health& Fitness kimeandaa tamasha la mazoezi litakalofanyika kesho jumamosi Mayfair Msasani jijini Dar es Salaam.
  Akizungumza mkurugenzi wa Bodyline Health& Fitness, Abbas Jaffer Ali alisema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuwajenga watanzania wapende kufanya mazoezi ili kuimalisha afya zao.
  Aliongeza kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na michezo mbali mbali ikiwemo shindano la kutunisha mishuli, kuogelea na viungo vya mwili.
   Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano.
  Katibu Mkuu - Shirikisho la Watunisha Misuli Tanzania, Francis Mapugilo (katikati) akisisitiza Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki mazoezi.
  Mkurugenzi wa kituo cha mazoezi ya Bodyline Health &Fitness, Abbas Jaffer Ali  (katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati akitangaza tamasha la michezo linalotarajiwa kufanyika Aprili 22, 2017  ukumbi wa Mayfair Plaza jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Katibu Mkuu - Shirikisho la Watunisha Misuli Tanzania, Francis Mapugilo (kulia) na mwalimu wa mazoezi.  0 0

   Msanii wa muziki wa kizazi kipya,ambaye amekuwa akifanya vyema ndani na anga za Kimataifa Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platinumz akizungumza mbele ya Waandishi wa habari pamoja na wadau wengine waliohudhuria hafla fupi iliyohusu uzinduzi wa manukato (Pafyum) yake iliyoitwa CHIBU,mapema leo jijini Dar.

  Wakati wa uzinduzi huo Diamond alisema kuwa ameamua kuingia kwenye soko la kutengeneza manukato 'pafyum' yenye nembo yake CHIBU ili kusaidia serikali katika suala zima la kutatua changamoto ya uhaba wa ajira nchini lakini pia kuongeza pato la Taifa kwa kulipa Kodi.

  Amesema kuwa kuanza kutengenezwa na kuuzwa kwa pafyum hizo kutaongeza ajira kwa vijana wengi lakini pia kutasaidia kukuza uchumi wa nchi kupitia kodi zitakazotozwa kutokana na bidhaa hiyo ambayo wanaume na wanawake wote wanaweza kuitumia, Pafyum ya CHIBU itapatikana katika maduka yote ya GSM na itauzwa bei ya rejareja kiasi cha shilingi 105, 000/-  kwa moja.
  Katika mkakati mwingine wa soko Meneja wa Msanii huyo Bw. Salaam Mendes amesema wako katika mazungumzo na mashirika kadhaa likiwemo shirika la ndege la Kenya Airways kwa ajili ya kuitangaza bidhaa hiyo na kuifikisha kwenye soko la kimataifa ikiwa ni pamoja na kuuzwa katika maduka makubwa kwenye viwanja vya ndege katika nchi mbalimbali ambako ndege za shirika hilo zinafika
  Msanii Nasseb Abdul a.k.a Diamond Platnumz akimkabidhi chupa ya Pafyum,mteja wake wa kwanza aliyejitambulisha kwa jina la Aisha Azori,wakati wa uzinduzi huo.Mwana mama huyo alionekana kujisikia fahari kununua bidhaa ambayo imetengenezwa na Msanii wa hapa nyumbani,ambae pia anafanya vyema katika kazi zake za Muziki,kushototo ni Mmoja wa mameneja wa Diamond Plutnamz almaarufu kwa jina la Babu Tale. 
   Msanii Diamond akifafanua jambo kwa Wanahabari
   Msanii Diamond akionesha moja ya Pafyum yake mbele ya Wanahabari na wadau mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo fupi iliofanyika jijini Dar Es Salaam mapema leo.
  Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Diamond alipokuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Pafyum hiyo ambayo tayari imekwisha sambaza kwenye maduka mengi jijini Dar.
  Meneja wa Diamond Platnumz  Babu Tale akiwakaribisha wana habari na wadau mbalimbali waliofika kushuhudia tukio hilo adhimu la uzinduzi wa Pafyum ya msanii huyo iliyojulikana kwa jina la CHIBU.  0 0

   Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Dkt. Omary Chillo (kulia) akifafanua jambo  kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maandalizi ya mbio za HEART MARATHON  na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza magonjwa yasiyoambukizika, jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Lucas Nkungu na kushoto ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John. Mbio hizo zitaanzia na kuishia barabara ya Kaole Oysterbay jijini Dar es salaam. Muda wa kuanza ni saa 12 asubuhi.
   Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Riadha Tanzania Bi. Ombeni Zavara akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ya mbio za heart marathon na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza magonjwa yasiyoambukizika  jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John.
  Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John (katikati) akisisitiza jambo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maandalizi ya mbio za heart marathon na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza magonjwa yasiyoambukizika, jana jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Riadha Tanzania Bi. Ombeni Zavara na kulia ni Katibu Mkuu Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Lucas Nkungu.


  0 0


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na wabunge katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Dkt. Elly Macha aliyefariki Machi, 31, 2017 katika hospitali ya New Cross Wolverhampton nchini Uingereza.
  Akizungumza katika tukio hilo Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, familia marehemu pamoja na wabunge wote. Amesema enzi ya uhai wake marehemu Dkt. Elly alitoa mchango mkubwa na ushauri mzuri katika masuala ya elimu na uboreshaji wa maeneo ya watu wenye ulemavu.
  Awali akisoma wasifu wa marehemu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mheshimiwa Mchungaji Peter Msigwa alisema Dkt. Elly alipata ulemavu wa macho akiwa na umri wa miezi mitano baada ya kuugua ugonjwa wa surua.
  Mchungaji Msigwa alisema pamoja na kuwa na ulemavu huo wa macho lakini haukuwahi kuwa kikwazo kwake kwani aliweza kufanya jambo lolote lililokuwa ndani ya uwezo wake.
  Mwili wa marehemu Dkt. Elly umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwake Usa River mkoani Arusha na anatarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwa wazazi wake katika kijiji cha Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro.
  Dkt. Elly alizaliwa Juni 18, 1962 kwenye kijiji cha Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro, ambapo mbali na wadhifa wa ubunge pia  aliwahi kuwa Mshauri Mwelekezi wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu vya Afrika Mashariki.
   Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Kulia), Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (wa pili kulia) wakishuhudia mwili wa Marehemu Mhe. Elly Macha ukiwasili, Marehemu aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton, nchini Uingereza  baada ya mwili kuwasili  leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
   Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza  wakati wakati wa kuagwa kwa mwili wa marehemu Mhe. Elly Macha aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton, nchini Uingereza na mwili umeagwa  leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
   Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza  wakati wa kuagwa kwa  mwili wa Mhe. Elly Macha aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton nchini Uingereza na mwili wake umeagwa  leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiaga mwili wa marehemu Mhe. Elly Macha aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton, nchini Uingereza na mwili umeagwa  leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiaga mwili wa marehemu Mhe. Elly Macha aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton, nchini Uingereza na mwili umeagwa  leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
  Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiaga mwili wa marehemu Mhe. Elly Macha aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross,Wolverhampton nchini Uingereza na mwili wake umeagwa leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
   Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe, Kassim Majaliwa wakati wa kuagwa kwa mwili wa Mhe. Elly Macha aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton nchini Uingereza na mwili wake umeagwa leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.

  0 0  0 0

  VOTE for Mt Kilimanjaro #Tanzania as Africa's Leading Tourist Attraction in World Travel Awards 2017.

  DID YOU KNOW? Mt Kilimanjaro is the 2016 Africa's Leading Tourist Attraction.
  HOW TO VOTE? Click link below, register&vote
  Pigia kura Mt Kilimanjaro katika Tuzo za World Travel Awards 2017 kama Kivutio Bora Afrika. 
  JE WAJUA? Mlima Kilimanjaro ndio kivutio bora Afrika mwaka 2016.
  Jinsi ya kupiga kura: bonyeza link hapa chini, jisajili (register), fungua link hapo chini kisha nenda kwenye majina (Africa nominees) kisha piga kura kwa kubonyeza kiduara pembeni mwa jina


  0 0
  0 0
 • 04/22/17--00:13: Article 24

 • 0 0

  Na Humphrey Shao, 
  Globu ya Jamii

   Kundi la Waandishi wa habari kumi na Muigizaji mmoja kutoka nchini Israel lililokuja katika utalii wa maeneo mbalimbali nchini limeondoka leo  mara baada ya kumaliza ziara yao ya siku tano nchini.
  Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) Bi. Devotha Mdachi amesema kundi hilo ambalo lilitembea sehemu mbalimbali nchini limewasili jijini Dar es Salaam leo kutoka Kigoma na linataraji kuondoka nchini leo majira ya saa tisa kurudi nchini kwao kwa ndege maalumu ya kukodi.

  “Waandishi hawa wa Habari waliofika kufanya utalii nchini ni moja ya matunda yaliyotokana na Rais John Pombe Magufuli kurudisha diplomasia baina ya Islael na Tanzania mara tu walipofungua ubalozi wao hapa nchini hivyo watalii hawa walipata fursa ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti, visiwa vya Zanzibar na hifadhi ya Sokwe iliyopo Gombe mkoani Kigoma” amesema Bi. Mdachi.

  Kwa upande wake afisa habari wa Shirika la Hifadhi ya Taifa nchini (TANAPA), Bw. Pascal Shelutete amesema kuwa watalii hao wamejionea vivutio vingi sana hapa nchini na kusema kuwa kweli nchi hii inahitaji kuitwa nchi ya Asali na Maziwa kama ilivyo kwao.

  Amesema kuwa watalii hao wamefuraishwa na jinsi uoto wa asili ulivyo hifadhiwa hapa nchini na kikubwa zaidi kuona sokwe ambao kisayansi inasemekana kuwa wana mahusiano makubwa na wanadamu kwa asilimia 98%.

  Kwa upande wake kiongozi wa kundi hilo la watalii hao, Ronit Hershkovitz, amesema kuwa amefurahishwa sana na vivutio vilivyopo hapa na kwa sasa kundi hilo linakwenda kuwa mabalozi kwa watalii wengine wanaotoka ukanda wa Magharibi hasa nchi za Mashariki ya kati.   Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Bi. Devotha Mdachiakiaga na kiongozi wa kundi la Waaandishi wa habari na watali kutoka nchini Israel Bi. Ronit Hershkovitz kabla ya kuondaka kurudi nchini kwao


   Kiongozi wa kundi la Waaandishi wa habari na watali kutoka nchini Israel Bi. Ronit Hershkovitz  akizungumza  na vyombo vya habari vya hapa nchini kabla ya kuondaka kurudi nchini kwao
   Afisa Habari Shirika la Hifadhi ya Taifa nchini (TANAPA), Bw. Pascal Shelutete akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam wakati akiagana na kundi hilo la Watalii kutoka nchini Islael
   Afisa Habari Shirika la Hifadhi ya Taifa nchini (TANAPA), Bw. Pascal Shelutete akiagana na Kiongozi wa kundi la Waaandishi wa habari na watali kutoka nchini Israel Bi. Ronit Hershkovitz 


  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora Mhe.Angelah Kairuki akizindua Programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa Maofisa wa wa Jeshi la Polisi Mjini Dodoma yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland.Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu na kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora Mhe.Angelah Kairuki (katikati), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu wakionyesha Vitabu vyenye Programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa Maofisa wa Jeshi la Polisi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland mjini Dodoma leo.Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Maofisa wa Polisi katika Uongozi.
   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa Maofisa wa Jeshi la Polisi Mjini Dodoma.Mafunzo hayo yanaendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland.Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora Mhe.Angelah Kairuki na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja.
   Baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Polisi waliopo katika Mafunzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland.Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Maofisa wa Polisi katika Uongozi ambapo baada ya kuhitimu watatunukiwa “Post-Graduate Diploma in Leadership”.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora Mhe.Angelah Kairuki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba na Viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na  Maofisa wa Jeshi la Polisi waliopo katika Mafunzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland.Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Maofisa wa Polisi katika Uongozi ambapo baada ya kuhitimu watatunukiwa “Post-Graduate Diploma in Leadership”. Picha zote na Frank Geofray-Jeshi la Polisi

  0 0

   Kaimu Kamishna wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Wilson Ruge akizungumza na Waandishi wa Habari wakati ufunguzi wa mafunzo wa Waandishi wa habari wa Masuala ya ardhi nchini juu ya kutambua umuhimu wa Kulipa Kodi ya Ardhi kwa Wizara ya Ardhi na Kodi ya Majengo kwa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)
   Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mboza Lwandiko akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara
   Afisa Msaidizi wa huduma kwa mlipa kodi Maya Magimba akitoa somo kwa Waandishi wa Habari juu ya umuhimu wa kulipa kodi ya majengo na kutofautisha kodi hiyo na kodi ya Ardhi maya ambaye aliwataka waandishi wa habari kutumia mafunzo hayo kwa ajili ya kuwa elimisha Watanzania hili waweze kulipa kodi za ardhi kama inavyohitajika kwa mujibu wa sheria
   Afisa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Denis Masami akifafanua masuala muhimu ya Ardhi kwa Waandishi wa Habari
  Mmoja ya Waandishi wa Habari akiuliza swali kwa wakufunzi kuhusu ulipaji wa kodi

  0 0


  NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt, Juliana Palangyo akiongea na wanahabari alipotembelea miradi ya kuzalisha umeme wa  Gesi Asilia ya upanuzi wa Kinyerezi I pamoja na ule wa Kinyerezi II.

  Mafundi wakiendelea na kazi katika moja ya jengo lilopo katika mradi wa kufua umeme wa gesi asili megawati 240 wa Kinyerezi I ambapo unafanyiwa upanuzi.
  Naibu katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo (wa pili kutoka kushoto) akiambatana na viongozi wa TANESCO alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Miradi ya Umeme Kinyerezi I&II.  Kushoto kwake ni kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bi.Joyce Ngahyoma akifuatiwa na Kaimu Meneja Uhusiano Bw. Yasini Didas Slayo Kulia pamoja na Meneja Mradi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephen Manda, (Kushoto)
  0 0
 • 04/22/17--01:03: Article 19
 • For Discounted Accommodation please go to Wyndham Dallas Suites and use Group Code: 04286822TC. You will save $40 per night. This deal is for up two (2) people per room. 
  Registration Website: http://tzdallas.com/register/
  Use promo code SIMBA to save $50
  Using promo code TZDAY2017 you will get a $20 saving with Uber

  0 0
 • 04/22/17--01:23: Article 18
 • AFRICA DIGITAL BANKING SUMMIT 14_15 june 2017. Mlimani City Conference Centre in Dar es salam Tanzania. ADBS is the Africa’s biggest, boldest and best event covering payments and financial services innovation for connected commerce at the intersection of mobile, retail, marketing services, data and technology  With 300+ attendees, including more than 50 CEOs & Presidents, from 100 companies and 9 countries, expected to attend our 2017 Dar es Salaam event. ADBS is critical to realizing the vision of disruptive ways in which consumers and businesses manage, spend and borrow money.  
  Register now @www.afridbs.com 
  #Powered by KONCEPT (ADBS Media partner)

older | 1 | .... | 1655 | 1656 | (Page 1657) | 1658 | 1659 | .... | 3270 | newer