Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1654 | 1655 | (Page 1656) | 1657 | 1658 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Na Daudi Manongi-MAELEZO.

  Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imelipa madeni ya fedha za likizo kwa walimu 86,234 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na 2016/17.

  Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Stella Manyanya wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.

  “Serikali inaendelea kulipa madeni mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha za likizo kwa walimu/Watumishi katika sekta ya Elimu”,Aliongeza Mhe.Manyanya.

  Amesema kuwa katika kipidi cha mwaka wa fedha 2015/16 hadi mwezi Juni, 2016 jumla ya shilingi bilioni 22,629,352,309 zililipwa kwa walimu 63814, na pia katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 hadi kufikia mwezi Machi, 2017 jumla ya shilingi bilioni 10,505,160,275 zimelipwa kwa walimu 22420.

  Aidha katika malipo haya jumla ya shilingi 13,415,410 zimelipwa kwa ajili ya madeni ya fedha za likizo kwa watumishi wa chuo cha ualimu Korogwe.Akizungumzia upande wa upandishaji madaraja Mhe.Manyanya amesema kuwakwa sasa uhakiki wa watumishi unaendela na ukikamilika watapandisha madaraja kama inavyotakiwa.

  Aidha amesisitiza kuwa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imekuwa ikiwapandisha vyeo watumishi wake wenye sifa kila mwaka ambapo katika mwaka 2015/16 Wizara iliwapandisha vyeo watumishi 2272 kati yao watumishi 71 ni wa chuo cha ualimu korogwe.

  Uhakiki wa madeni ya miaka ya nyuma unaendelea kuratibiwa na mamlaka husika na taratibu za malipo zitakamilishwa kwa wale wanaostahili.
  Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Stella Manyanya

  0 0  has1
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mahojiano maalumu  na Mkurugenzi  Idara ya Habari (MAELEZO)  Dkt. Hassan Abbasi  kuhusu  masuala ya Muungano kwa ujumla kuelekea maadhimisho ya Miaka 53 ya Muungano.
  has2
  Mkurugenzi  Idara ya Habari (MAELEZO)  Dkt. Hassan Abbasi  akimkabidhi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  Jarida la Nchi yetu linalotolewa na Idara ya Habari ( MAELEZO). Jarida hilo liliandaliwa kwa ajili ya maadhimisho ya Miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika.
  has3
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) katika picha ya pamoja na watumishi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mara baada ya mahojiano maalumu kuelekea Maadhimisho ya Miaka 53 ya Muungano( kutoka kushoto ni Beatrice Lyimo, Dkt. Hassan Abbasi, Jonas Kamaleki na Hassan Silayo.

  0 0

  Na Daudi Manongi-MAELEZO.

  Wizara ya Maji na Umwagiliaji imesema kuwa mkandarasi ameanza kazi ya ujenzi wa mabomba ya usambazaji katika maeneo ya Malamba Mawili,Msigani,Mbezi Luisi,Msakuzi,Kibamba,,Kiluvya,Mloganzila na Mailimoja na atakamilisha kazi hiyo mwaka huu 2017.

  Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe wakati akijibu hoja mbalimbalia za wabunge.

  “Baada ya kukamilika kwa mradi maeneo mengi ndani ya kilomita 12 ya pembezoni mwa bomba kuu la Ruvu Juu yameanza kupata huduma ya Maji”,Aliongeza Mhe.Kamwelwe.

  Amesema kuwa maeneo ambayo yanapata maji kwa sasa kutoka Bomba la Ruvu Juu ni pamoja na Mlandizi na vitongoji vyake, Visiga, Misugusugu, Soga, Korogwe, Picha ya Ndege, Kwa Matiasi,Tumbi, Mailimoja, Pangani, Kiluvya, Kibamba, Mloganzila, Mbezi kwa Yusufu,Mbezi Mwisho, Kimara, Mavurunza, Baruti, Kibo, Kibangu,Tabata, Segerea, Kinyerezi na Karakata.

  Aidha maeneo ambayo bado hayajaanza kupata huduma ya maji yatapata huduma hiyo baada ya utekelezaji wa miradi mipya ya kujenga mtambo wa mabomba ya kusambaza maji katika maeneo yote ambayo hayana huduma hiyo, Amesema kuwa miradi hii itatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha .

  0 0


  Na: Frank Shija – MAELEZO.

  TPDC kwa kushirikiana na Sekta binafsi wanatarjia kutekeleza miradi mbalimbali ya usambazaji wa gesi asilian katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na baadhi ya mikoa mingine itakayoidhinishwa.

  Hayo yamebainishwa na Kiamu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.

  Mhandisi Musomba amesema kuwa miradi hiyo imeanza kwa kupitia upya taarifa ya awali ya upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa mtandao wa bomba la kusambazia gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo mnamo mwezi machi 22, 2017 TPDC ilikaribisha jumla ya makampuni 9 ambayo yalikidhi vigezo vya kimanunuzi kwa ajili ya kazi hiyo.
  “Napenda kuutaarifu umma kuwa TPDC inatarajia kutekeleza miradi mbaimbali ya usambazaji wa gesi asilia katika mikoa ya Dar es Salaam, Bagamoyo na Mkuranga Mkoani Pwani, Lindi na Mtwara pamoja na baadhi ya mikoa mingine,” alisema Mhandisi Muyomba.
  Aliongeza kuwa lengo la kupitia upya taarifa za awali ni kuboresha zaidi taarifa za kifedha, mahitaji ya kiufundi na utambuzi wa njia za kupitisha bomba na ugawaji wa kanda za usambazaji.
  Aidha alisema kuwa ili kuharakisha usambazaji wa gesi, TPDC inakaribisha na kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika uendelezaji wa miundombinu itakayowezesha usambazaji wa gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam mara tu mapitio ya upembuzi yakinifu utakapomalizika.
  Mtandao huo unakadiriwa kuwa na urefu wa takribani kilomita 65 ambao utahudumia, kwa kuanzia, nyumba 30,000, viwanda na vituo vya kushindilia gesi asilia pamoja na vituo vya kujazia gesi hiyo.
  Katika hatua nyingine Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema kuwa hadi sasa TPDC imefanikiwa kukiunganisha na mtandao wa gesi asilia Kiwanda kimoja cha kutengeneza Vigae cha Goodwill kilichopo Mkuranga, Mkoani Pwani huku likiendelea na majadiliano na viwanda vingine vitatu kwa ajili ya kuunganishwa na mtandao huo.
  Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015 TPDC inatambuliwa kuwa Shirika rasmi la taifa linalojiendesha kibiashara, ambapo sheria hii inaipa mamlaka TPDC kuruhusu makampuni mbalimbali kuendesha shughuli za sekta, zitakazokuwa zainadhibitiwa kwa utaratibu maalum chini ya usimamizi wa Mdhibiti anayetoa leseni.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uunganishwaji na usambazaji wa gesi asilia leo Jijini Dar es Salaam. 
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uunganishwaji na usambazaji wa gesi asilia leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusinano na Mipango wa TPDC, Nathan  Mnyawami. 
  Baadhi ya waaandishi wa habari wakifuatilia mkutano baina yao na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba (hayupo pichani) uliofanyika Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO. 

  0 0


  0 0


  Na Nuru Juma-Maelezo

  Taasisi ya Tanzania Health Summit yaandaa mbio za nusu Marathon na Upimaji wa afya kwa lengo la kusaidia juhudi za serikali katika kupunguza magonjwa yasioambukiza, mbio hizo zinazotarajia kufanyika Aprili 26 katika barabara ya Kaole iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.

  Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo Rebecca John wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhamasisha jamii kushiriki.

  “Kamati ya maandalizi ya ya mbio za Heart Marathon inapenda kuwa taarifu wadau wote wa sekta ya afya hapa nchini na jamii kwa ujumla juu ya mbio za Heart Marathon na upimaji wa afya ili kuungana na serikali katika juhudi za kupunguza magonjwa yasiyoambukiza” alisema Rebecca.

  Aliongeza kuwa kwa mwaka huu mbio hizi zitashirikisha washiriki zaidi ya elfu mbili kutoka rika mbalimbali wakiwemo vijana, watoto, wazee, makundi ya watu wenye ulemavu na watu wenye magonjwa yasiyoambukiza.

  Pia washiriki watapata nafasi ya kupima afya magonjwa mbalimbali kama vile shinikizo la damu ,wingi wa sukari katika damu, kiasi cha mafuta mwilini, uchunguzi wa uvimbe katika matiti na kupata ushauri wa wataalam kuhusiana na vyakula bora, magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.

  Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John (katikati) akisisitiza jambo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maandalizi ya mbio za heart marathon na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza magonjwa yasiyoambukizika mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Riadha Tanzania Bi. Ombeni Zavara na kulia ni Katibu Mkuu Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Lucas Nkungu. 
  Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Riadha Tanzania Bi. Ombeni Zavara akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ya mbio za heart marathon na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza magonjwa yasiyoambukizika mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John. 
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Dkt. Omary Chillo (kulia) akifafanua jambo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maandalizi ya mbio za heart marathon na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza magonjwa yasiyoambukizika mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Katibu Mkuu Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Lucas Nkungu na kushoto ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John.   0 0
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Dkt. Musafiri Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda na Mjumbe maalumu wa Rais Paul Kagame alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 20, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Dkt. Musafiri Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda na Mjumbe maalumu wa Rais Paul Kagame alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 20, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Dkt. Musafiri Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda na Mjumbe maalumu wa Rais Paul Kagame alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 20, 2017. Wengine ni Balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Kayihura na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi Bw. Issa Mugabutsinze.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais Paul Kagame wa Rwanda uliowasilishwa kwake na kt. Musafiri Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda  alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 20, 2017
  PICHA NA IKULU  0 0

  Pata ticket yako ya Mother and Child Gala Event katika vituo vifuatavyo :Mr Price Mlimani City :Maznat Bridal saloon Mikocheni :
  :MAK bookshop Mliman City.
  :Kinyago trave &tour NHC HOUSE MJINI :OMY GIFT Shop City Mall :Rose Brasilian saloon mikocheni
  Au piga no. 0718 769010/0754 291 291 uhudumiwe.
  #motherandchildgala2017
  #mtokoamazingkwamwanao
  #maongeziyaleomsingiwakesho
  #vunjaukimya
  @dotty_kipeja @chrismauki @diana_gasper @rosebrazilian @auntsadaka  0 0
 • 04/20/17--13:55: Introducing KABUMA

 • 0 0


  Asalaamu alaykum. 
  Mtoto wetu Arkam Salim Mbarouk (anayeonekana kwenye picha) mwenye umri wa miaka 12 amepotea tokea tarehe 19 April, 2017 mida ya jioni (alaasiri) wakati anakwenda madrasa (maeneo ya Makongo Juu) na hajaonekana mpaka sasa. 
  Mara ya mwisho alivaa kanzu ya msikitini rangi ya kijivu na pensi nyekundu. Tafadhali tunaomba utakapomuona popote  au kupata taarifa zake uwasiliane nasi kwa namba hizi zifuatazo 0782412840 
   AU 0713251344,

  0 0  0 0

  Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

  Fundi simu, Juma Maulid (30) mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam, leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kuingilia na kuchezea simu zilizofungiwa.

  Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa imedaiwa na mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali,  Elizabeth Mkunde kuwa, mshtakiwa ametenda kosa hilo Novemba 8, 2016 katika maeneo ya Kariakoo mtaa wa Aggrey wilaya ya Ilala. 

  Mkunde amedai kuwa mshtakiwa huyo alighushi IMEI za simu aina ya Tecno L8 zenye namba 357085075221523 na 357085075221531 ambazo zilifungiwa na TCRA  na kuzibadilisha namba hizo zikasomeka  kama 352167055726443 na 352167055726450.

  Mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Hakimu Mwambapa alimtaka mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho watakaosaini hati ya dhamana ya maneno ya milioni tano kila mmoja. 

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 4 mwaka huu, kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali(PH) baada ya upande wa mashta kuileza mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

  Akizungumza nje ya mahakama,  Mwanasheria Mkuu Mwandamizi wa TCRA, Johannes Kalungula akiwa nje ya mahakama aliwaonya wale wote wanaojihusisha na kuingilia na kuchezea  Imei za Simu zilizofungiwa ama kuibiwa watachukuliwa hatua za kisheria.

  Ameongeza kuwa kitendo hicho kinarudisha nyuma zoezi  lililofanyika la kufungia simu na kudhibiti wizi wa simu.

  0 0


   Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe S. Kebwe akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA ), uliofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa la Magadu, mjini Morogoro.

  Na Ally Changwila

  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt, Kebwe Stephen Kebwe ameipongeza Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa  kufanikisha mchakato wa ununuzi wa Rada nne za kuongozea ndege nchini, kutokana na Mamlaka kubana matumizi yake na hivyo kupata fedha za kununulia mitambo hiyo.  Akizungumza wakati wa kufungua Baraza la wafanyakazi la TCAA lililofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa  la Magadu jijini,Morogoro, Dkt Kebwe aliongeza kuwa Rada hizo nne zitaifanya Tanzania kuwa katika nafasi nzuri ya ushindani katika sekta ya usafiri wa anga kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.  “Mafanikio yenu katika kuyafikia malengo yatategemea kila mmoja wenu kutimiza wajibu wake kwa kadri ya uwezo wake”. Aliongeza.

  Vile vile Dkt. Kebwe ameipongeza TCAA kwa mafanikio iliyoyapata kwa kufaulu ukaguzi wa Shirika la kimataifa la Usafiri wa Anga-ICAO kwa kufikia asilimia 61.  Dkt Kebwe ameongeza kuwa mafanikio ya TCAA ni mafanikio ya sekta nyingine kwani sekta ya usafiri wa Anga ni kiungo muhimu cha kuziwezesha sekta nyingine za uchumi kama utalii, kilimo na madini na kadhalika kuendelea kukua.  Dkt Kebwe pia ameongeza, Usafiri wa Anga si usafiri wa anasa bali ni usafiri wa msingi kwa kuchochea maendeleo, na kwamba Tanzania inapaswa kufanya jitihada za kuongeza  watoa huduma za usafiri wa anga ikiwa ni pamoja na mashirika ya ndege mengi  kutoa fursa kwa wananchi wengi  kuutumia usafiri huo  kwa gharama nafuu.

   Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe S.Kebwe katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa TCAA baada ya  kufungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA ), uliofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa la Magadu, mjini Morogoro. 
   Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe S.Kebwe akibadilishana mawazo na Menejimenti ya TCAA baada ya ufunguzi mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA ), uliofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa la Magadu, mjini Morogoro
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe S.Kebwe akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw.Hamza S.Johari baada ya kufungua  mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA ), uliofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa la Magadu, jijini Morogoro.

  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Wa pili kulia), akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo pamoja na wawakilishi kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.
   Katibu wa Baraza la Wafanyakazi (Sekta ya Ujenzi), Bw. Ramadhani Msafiri(Wa pili kushoto), akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo pamoja na Wawakilishi kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.
   Mmoja wa wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Bw. Shukuru Sikunjema, akitoa maoni yake kwa Mwenyekiti Wa Baraza la Wafanyakazi Eng. Joseph Nyamhanga katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.
   Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) wakifuatilia maelekezo ya Baraza la Wafanyakazi wakati wa kikao hicho kilichofanyika Mkoani Morogoro.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0


  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

  Mshtakiwa Philemon Manase ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa aliteswa sana wakati anatoa maelezo ya onyo katika kituo cha Polisi Osterbay Jijini Dar es salaam.

  Ameyaeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi wakati akitoa utetezi wake katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili yeye, raia wa China anayedaiwa kuwa ni Malkia wa Pembe za Ndovu, Yang Feng Glan (66) na Silvius Matembo.

  Akiongozwa na wakili wake, Nehemiah Nkoko, Manase amedai kuwa, alikamatwa Aprili 20, 2014 wakati akienda kununua vinywaji eneo la njia panda ya Segerea.

  Amedai kuwa, baada ya kukamatwa, alipelekwa kituo cha polisi stakishali na baadae polisi osterbay ambapo wakiwa osterbay Sajenti Beatus aliagiza aandaliwe mazingira ya kumning'iniza kama popo na kwamba anataka amuhoji na taarifa zote wanazo.

  Aliongeza kuwa polisi huyo alimwambia akikataa maelezo aliyokuwa nayo basi asije akamuomba msamaha kwa kitu ambacho wangemfanyia huku wakimuuliza kama alishawahi kukalia chupa.

  Manase amedai alimuuliza mbona wanamtisha, lakini Beatus alichukua kalamu na karatasi na kuanza kuchukua maelezo yake binafsi.

  Ameendelea kudai kuwa, wakati akihojiwa alimkabidhi afande Beatus simu mbili na Sh milioni 2.6 na kwamba kuna vijana wawili waliagizwa na afande huyo walikuwa na Bomba na wakamfunga pingu miguuni na bandeji mdomoni.

  Aliendelea kudai kuwa walichukua hilo bomba wakamfunga miguu na mikono wakamuweka juu ya meza na kimning'iniza kichwa chini miguu juu. Akapigwa na rungu mara nne na kwamba alifanyiwa kitendo hicho kwa saa 3.

  Baada alifunguliwa pingu za miguuni wakamuuliza kama yupo radhi kuendelea kutoa maelezo akamwambi ana hali mbaya anajisikia kizunguzungu na  baadae afande Beatusi alimchukua nakumpeleka polisi Kijitonyama ambapo aliwekwa rumande.

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 5, mwaka huu ambapo itatolewa uamuzi wa kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi kama kweli mshtakiwa huyo aliteswa wakati akitoa maelezo ya onyo ama la.

  Kesi hiyo ndogo ndani ya kesi ya msingi imeanza kusikilizwa baada ya Wakili wa upande wa utetezi, Jeremiah Mtobesya kupinga maelezo ya onyo ya Manase yasipokelewe kama kielelezo cha kesi hiyo mahakamani kwa sababu aliyatoa polisi kwa sababu yalichukuliwa nje ya muda na alipigwa na kunyanyaswa.

  Inadaiwa kuwa, kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22,2014 kwa makusudi mshtakiwa Glan aliongoza na kufadhiri vitendo vya kijinai kwa kukusanya na kusafirisha vipande 706 vya Meno ya Tembo bila ya kuwa na kibali chochote kile kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama Pori.

  Ilidaiwa kuwa  washtakiwa Salvius na Manase wanadaiwa kuongoza makosa ya uhujumu uchumi kwa kusaidia biashara ya nyara za serikali kwa kukusanya, Kusafirisha na Kuuza Meno ya Tembo kwa nia ya kujipatia faida.

  Iliendelea kudaiwa kuwa Mei 21, 2014 katika eneo la Sinza Palestina wilaya ya Kinondoni mshtakiwa Manase alitoroka chini ya ulinzi halali wa askari wa Jeshi la Polisi D 7847 Koplo Beatus ambaye alikuwa akimshikilia kwa makosa ya kujihusisha na biashara za nyara za serikali.

  0 0

    Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na uongozi wa Chama cha Ngoma  na Muziki wa Asili Tanzania (CHANGAMATA) wakati alipokutana nao ofisini kwake Mjini Dodoma kujadili masuala mbalimbali ya Sanaa za Ngoma na Muziki Asili Tanzania leo April 21, 2017.
   Mwenyekiti wa Chama cha Ngomana Muziki wa Asili Tanzania (CHANGAMATA) Wanne Salim Kutoka Kikundi cha  Wanne Star  akieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili wasanii wa Ngoma na Muziki Asili kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe wakati walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma Leo April 21, 2017. 
    Katibu wa Chama cha Ngoma  na Muziki wa Asili Tanzania (CHANGAMATA) Richard Muro  akifafanua jambo  kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe wakati  walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma leo April 21, 2017.
    Mmoja wa wasanii kutoka Chama cha Ngoma  na Muziki wa Asili Tanzania (CHANGAMATA) Zuhura Khatib akimueleza jambo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe wakati walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma. 
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akipokea zawadi ya Ngoma kutoka kwa Chama cha Ngoma za na Muziki wa Asili Tanzania (CHANGAMATA) wakati alipokutana nao Ofisini kwake Mjini Dodoma kujadili masuala mbalimbali ya Sanaa za Ngona na Muziki Asili Tanzania leo April 21, 2017.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja  na uongozi wa Chama cha Ngoma za na Muziki wa Asili Tanzania (CHANGAMATA) wakati alipokutana nao ofisini kwake mjini Dodoma kujadili masuala mbalimbali ya Sanaa za Ngona na Muziki Asili Tanzania.

  Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  KUFUATIA sakata la kamati ya katiba, hadhi na wachezaji kuliweka tena mezani suala la Klabu ya Simba kupewa pointi 3 dhidi ya Kagera baada ya kumchezesha Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano, wekundu hao wa Msimbazi wametuma barua kwa Kamanda kwa kanda maalum Mkoa wa Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro kuomba maandamano ya amani.

  Maandamano hayo amb kwa mujibu wa barua hiyo ya leo yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne kuanzia majira ya saa 4 asubuhi mpaka saa 7 mchana yakianzia Makao Makuu ya klabu hiyo kuelekea  Ofisi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

  Dhumuni kuu la barua hiyo ni kupinga namna Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF kufanya vitendo na maamuzi ya uonevu kwa Klabu ya Simba huku malalamiko mengi ya msingi wanayopeleka maombi yakiwa hayasikilizwi kwa wakati.

  Mbali na hilo ni pamoja na leo, Shirikisho hilo kuamua kumpeleka Msemaji wa klabu hiyo Hajji Manara mbele ya kamati ya maadili ikiwa wanaonyesha nia ya kutaka kumfungia na kumziba mdomo ili asioongelee uonevu unaofanywa dhidi yao.

  Barua ya kuomba maandamano hayo ya amani imendikwa na Rais wa klabu hiyo, Evance Aveva na kutuma nakala kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) na maandamanio hayo yatapitia katika barabara za Msimbazi, Nyerere na Chang'ombe.

  0 0


  Tarehe 24 Novemba 2016 Wizara ilizindua Cheti kipya cha Chanjo za Kimataifa kijulikanacho kama Cheti cha Chanjo ya Homa ya Manjano ili kuendana na maboresho ya kipengele cha 7 cha Kanuni za Afya za Kimataifa za mwaka 2005. 

  Lakini pia, zoezi hili lililenga kukabiliana na kusambaa kwa vyeti vya kugushi (feki) ambavyo  watu wamekuwa wakivipata bila kupata chanjo, hali ambayo ilitishia Afya ya Jamii dhidi ya ugonjwa huo. Kwasababu hizo, Wizara iliona ni vema kufanya mabadiliko ya cheti hicho, ambapo wenye vyeti vya zamani wanabadilishiwa na wale  wanaopata chanjo wanapewa cheti kipya.


  0 0

  Mchezo wa Robo Fainali ya Nne ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup 2016/2017), kati ya Young Africans na Tanzania Prisons FC utafanyika kesho Aprili 22, 2017 saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

  Mchezo huo utatoa mshindi ambaye ataungana na timu nyingine tatu ambazo tayari zimefuzu kwa hatua ya Nusu Fainali. Timu zilizotangulia Nusu Fainali ya ASFC ni za Mbao FC, Simba SC na Azam FC.

  Jumapili Aprili 23, mwaka huu kutakuwa na droo ya wazi kwa timu nne zitakazokuwa zimefuzu kwa hatua ya Nusu Fainali ya ASFC, itakayofanyika Kituo cha Televisheni cha Azam ambao ni wadhamini wakuu wa jina la michuano na haki ya kuonesha mubashara michuano hii ambayo inafanyika kwa msimu wa pili mfululizo.

  Azam FC ilikata tiketi ya kucheza Nusu Fainali ya ASFC baada ya kuifunga Ndanda FC mabao 3-1, kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam Aprili 5, 2017 ikitanguliwa na Mbao iliyoishinda Kagera Sugar mabao 2-1 katika mchezo ulifanyika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera Machi 18, 2017 ilihali Machi 19, mwaka huu Simba iliwatoa Madini ya Arusha kwenye mchezo uliofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

  Nusu Fainali inatarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu, kabla ya fainali ambako Bingwa wa michuano hii ambayo msimu huu ilishirikisha timu 86 ikiwa ni pamoja na za Ligi Kuu ya Vodacom (timu 16); Ligi Daraja la Kwanza (timu 24); Ligi Daraja la Pili (timu 24) na mabingwa wa mikoa timu 22, atazawadiwa Sh. 50 milioni na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho - CAF.

  0 0older | 1 | .... | 1654 | 1655 | (Page 1656) | 1657 | 1658 | .... | 3272 | newer