Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

RC MAKONDA: WAFANYABIASHARA WASIOFATA UTARATIBU KUKIONA


TUNISIA YARIDHIA TAMKO KURUHUSU WATU BINAFSI KUPELEKA KESI ZAO MOJA KWA MOJA KWENYE MAHAKAMA YA AFRIKA IILIYO JIJINI ARUSHA

0
0
Tunisia imesema Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) ni lazima itangazwe kwa nguvu zote ili kuwawezesha wananchi barani Afrika kufahamu uwepo wake,malengo ya kuanzishwa kwake pamoja na shughuli zake.
Akipokea ujumbe wa Mahakama hiyo katika Ikulu ya Tunisia,Rais wa Nchi Hiyo ,Mh.Beji Caid Essebsi alipongeza uanzishwaji wa Mahakama hiyo na kuongeza  kuwa inahakikisha ulinzi wa Haki za Binadamu Barani Afrika.    
 “Kwa njia hii,Haki za Binadamu Barani Afrika zitalindwa na kuhakikisha maendeleo endelevu ya demokrasia kwa wananchi” Aliuambia ujumbe huo uliohusisha majaji watatu akiwemo Rais wa AfCHPR,Jaji Sylvain Ore’.
Kwa upande wake Rais wa AfCHPR, Jaji Ore’ aliishukuru serikali ya Tunisia kwa kukubali kuupokea ujumbe wake na kukutana na Viongozi na Maafisa mbalimbali wa nchi hiyo na pia kuendesha semina kwa wadau mbalimbali nchini humo kwa lengo la kuitangaza Mahakama.
Wakati wa ziara hiyo,Tunisia ilitia saini tamko la kuruhusu watu binafsi na Mashirika yasiyo ya kiserikali(NGO’s) katika nchi hiyo kupeleka kesi zao moja kwa moja katika Mahakama hiyo yenye Makao yake makuu Jijini Arusha.
Hatua hiyo ya Tunisia ambayo ni utekelezaji wa kifungu cha 34(6),Inalifanya Taifa hilo kuwa Nchi ya nane Barani Afrika kukubali makundi hayo kupeleka kesi katika Mamlaka za Mahakama hiyo.
 Rais wa Tunisia Mh.Beji Caid Essebsi akimlaki Rais wa AfCHPR Jaji Sylvain Ore katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Tunis
Rais wa AfCHPR Jaji Sylvain Ore akionesha kwa wanahabari tamko la kuruhusu watu binafsi na Mashirika yasiyo ya kiserikali(NGO’s) katika nchi hiyo kupeleka kesi zao moja kwa moja katika Mahakama hiyo yenye Makao yake makuu Jijini Arusha. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

TAASISI ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) YAPIMA MOYO WA MTOTO ALIYE TUMBONI MWA MAMA YAKE

0
0
Na Veronica Romwald, Dar es Salaam
TAASISI ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mara nyingine tena imefanya upimaji wa moyo wa mtoto aliye tumboni mwa mama yake, kuchunguza magonjwa mbalimbali ya moyo.
Upimaji huo umefanywa katika taasisi hiyo na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Watoto wa JKCI, Naiz Majani.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dk. Naiz amesema kuna faida lukuki iwapo mjamzito ataamua kufanya kipimo maalumu.
"Tunatumia Ultra sound kama kawaida kufanya kipimo hiki, lakini inakuwa ina tofauti kidogo... hatutumii mionzi yoyote, hivyo hakuna madhara anayoweza kuyapata mama au mtoto wake aliye tumboni," amesema. 

Ametaja faida hizo kuwa ni kupunguza idadi ya vifo vya watoto wanaozaliwa na magonjwa ya moyo, na kuwaondoa kwenye masumbufu wanayoweza kuyapata kutokana na kuchelewa kupata matibabu.
"Kwa mara ya  kwanza tuliwafanyia kipimo hicho wajawazito 25 mwishoni mwa mwaka jana ambapo watano kati yao mimba zao zilikutwa na matatizo.

 Dk. Naiz akionesha jinsi wanavyofanya upimaji kuchunguza magonjwa ya moyo wa mtoto aliyeko tumboni. 

Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi (pichani) akielezea dhumuni  la kuanzisha huduma hiyo ili kugundua matatizo mapema.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 19.04.2017

SIMBA WAJA JUU, WADAI WAMECHOKA KUONEWA NA TFF

0
0

Ofisa habari wa Simba  Hajji Manara akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji kukaa na kupitia hukumu ya kupokwa alama tatu kwa timu ya Kagera Sugar na kupatiwa wao.

Na Zainab Nyamka, 
Globu ya Jamii.
Wakati Maamuzi ya kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ikitarajiwa kulipua bomu muda wowote kutoka sasa juu ya hatma ya pointi tatu na mabao matatu waliyopewa Simba kufuatiwa malalamiko yao, Uongozi wa Simba umekuja juu na kuishutumu Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).
Sakata hilo limeendelea kushika hatamu .kutokana na Kamati hiyo kupokea barua ya kukata rufaa kutoka timu ya Kagera kupinga maamuzi ya kamati ya saa 72 kuipoka timu hiyo pointi na kuwapa Simba.
Katika maamuzi ya kamati hiyo iliyokaliwa jana ikiongozwa na Katibu Mkuu wa wa TFF Selestine Mwesigwa na kuita mashahidi akiwemo mchezaji husika Mohamed Fakhi, Mwamuzi wa mezani katika  mchezo huo wa African Lyon dhidi ya Kagera Jonesia Rukyaa, waamuzi wa pembeni pamoja na Meneja wa Kagera Mohamed Husein.
Kufuatia hilo,  Uongozi wa klabu ya Simba umesema hakukuwa na haja ya Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za wachezaji kuitisha kikao kwa ajili ya kujadili marejeo (Review) ya shauri la timu ya Kagera Sugar kwa madai kuwa haina uhalali huo.
Kauli hiyo inakuja siku moja baada ya Kamati hiyo kukutana jana kwenye Hotel ya Protea kupitia shauri hilo ambapo mpaka sasa bado maamuzi yake hayajatangazwa.

Ofisa habari wa Simba  Hajji Manara ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari  kuwa licha ya kutokuwa sahihi kwa Kamati hiyo kuketi kwakua suala hilo lilitakiwa lipelekwe bodi ya ligi lakini pia kwa mujibu wa sheria za nchi shauri la mrejeo halipaswi kufanyika kwa kuita mashahidi wapya kama ilivyotokea jana.
Manara amesema haijawahi kutokea duniani kote kuwa mtuhumiwa anaitwa kwenye Review au mwamuzi wa nne (Fouth Official) ambaye hata haandiki ripoti anaitwa kutoa ushahidi kwenye kamati jambo ambalo halijawahi kutokea na zaidi ameitaka TFF kutenda haki kwani wamechoka kuonewa. "TFF endapo watashindwa kupata haki yao suala hilo litafika mbali kwa maelezo kuwa tumechoka kuonewa  kwani mara nyingi wamekuwa wakiipendelea Yanga,"
Manara amemshutumu Rais wa TFF Jamal Malinzi kuwa  Wanafahamu kinachoendelea kati yake na mwamuzi Donisia Rukyaa na  wanao ushahidi wa kutosha kuhusu wao.


UHAMIAJI YAZINDUA MFUMO WA KUHAKIKI VIBALI VYA UKAAZI KI - ELEKTRONIKI

0
0

Frank Mvungi-Maelezo.

Serikali imezindua mfumo wa Kielektroniki wa Uhakiki  wa Vibali vya ukazi “e-verification” hapa nchini ili kuongeza tija na kudhibiti upotevu wa mapato. Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mfumo huo.
Akizungumzia mfumo huo Kamishna Jenerali Makakala amesema utasaidia Makampuni, Taasisi,  Mashirika na watu binafsi kuhakiki vibali vya watumishi wao ili kuona kama ni halali ama  si halali na idara hiyo itakuwa tayari kuwasaidia wale wote watakaokuwa na matatizo kupata ufumbuzi wa changamoto zao.
“Idara inatoa siku 90 kwa watu wote kuhakiki vibali vyao vya ukazi ili kama wana matatizo wasaidiwe kupata ufumbuzi” Alisisitiza Dkt Makakala.



Akizungumzia lengo la mfumo huo Makalala amesema utasaidia kuimarisha udhibiti wa wageni wanaoishi hapa nchini na kuzuia mianya ya upotevu wa maduhuli ya Serikali na mfumo huo ni rahisi na unatoa fursa kwa wageni wote wenye vibali vya ukaazi kuhakikiki kumbukumbu za vibali vyao ili kujua kama vimetolewa na Idara hiyo.
Aidha,Idara ya Uhamiaji inawaomba wadau wa huduma zake kufika wao wenyewe katika Ofisi zao katika  ngazi ya Wilaya, Mikoa na Makao Makuu kwani huduma za Uhamiaji hazina uwakala.
Mfumo huo wa uhakiki wa vibali vya ukaazi kwa kutumia njia ya kielektroniki “e-verification” unapatikana kupitia tovuti ya uhamiaji ya www.immigration.go.tz
  Kamishna Jenerali  wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akifafanua jambo kwa  waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki  vibali vya ukaazi ujulikanao kama  “E – Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali  wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akizungumza na maafisa Uhamiaji na  waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki vibali vya ukaazi ujulikanao kama  “E – Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maafisa Uhamiaji na waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishna Jenerali  wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki  vibali vya ukaazi ujulikanao kama  “E – Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Afisa TEHAMA, Mkaguzi wa Uhamiaji Sokolo Kaseko akifafanua na kuelekeza mbele ya Waandishi wa Habari jinsi ya kufanya Uhakiki wa Vibali Ki- elektroniki wakati wakati wa Uzinduzi wa Mfumo Uhakiki wa Vibali vya Ukaazi ki-elektroniki uliofanyika Ukumbi wa Mikutano, Makao Makuu ya Uhamiaji, Dar es Salaam.

 Kamishna Jenerali  wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akifuatilia jambo wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki vibali vya ukaazi ujulikanao kama  “E – Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Afisa Utawala na Fedha wa Uhamiaji Edward Chegero na kushoto ni Afisa wa vibali na Pasi wa Uhamiaji Musanga Etimba.

Vodacom yaongeza muda wa kuuza hisa

0
0
Akiongea jijini Dar es Salaam mapema leo, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia amesema “Vodacom Tanzania PLC inatarajia kupokea maombi mengi ya kununua hisa katika kipindi cha wiki hii.
Pia kutokana na ushauri kutoka Serikali ya Tanzania na  makundi mbalimbali muhimu ya kijamii yanayohitaji kuwekeza wakiwemo Wabunge, makundi ya watumishi wa kada mbalimbali wa serikali na maofisa wa vyama  vya Ushirika kutoka sehemu mbalimbali za nchi, tumewasilisha maombi na kupata idhini kutoka Mamlaka ya Soko la mitaji na dhamana(CMSA) kuongeza muda wa zoezi la kuuza hisa kwa kipindi cha wiki tatu hadi kufikia Alhamisi ya tarehe 11 Mei, 2017. 
Mkurugenzi huyo alisema kuongezeka kwa muda wa mwisho wa kununua hisa utawezesha wanaohitaji kununua hisa  kwa makundi binafsi na taasisi zilizoomba muda uongezwe kushiriki kikamilifu katika mchakato huu. Tunatoa shukrani za dhati kwa watanzania ambao wamejitokeza kuwekeza kupitia kununua hisa na tunawakaribisha ambao bado hawajanunua hisa kuchangamkia fursa hii katika kipindi cha muda mfupi wa nyongeza.

Mgawanyo na mchanganuo wa umiliki wa hisa inapendekezwa utafanyika kuanzia Mei 19, 2017 na kuendelea kabla ya kumaliza mchakato wa mwisho wa kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam katika tarehe iliyopangwa ya Juni 6, 2017.”
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati alipokuwa akitangaza kwa kampuni yao kuongeza muda wa zoezi la kuuza hisa kwa kipindi cha wiki tatu hadi kufikia Alhamisi ya tarehe 11, Mei 2017.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kwenye mkutano huo.

JEWELRY FASHION SHOW 2017


TAASISI YA VICTORIA YAZINDULIWA NA KUTOA MAFUNZO KWA WAJANE

0
0
Mafunzo hayo yalitolewa kwa lengo la kupunguza pengo la elimu ya masuala ya fedha kwa wanawake hao kwa kuwafundisha mbinu mbali mbali za biashara, namna ya kuweka akiba na kulipa mikipo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga alimpongeza Kamata kwa jitihada zake kwa kuinua wanawake hususani wajane na wasiojiweza kiuchumi na kuwataka wanawake kujenga utamaduni wa kufuatilia taarifa mbali mbali kuhusiana na masuala ya fursa za kibiashara ili kuzitumia katika kupanua wigo wa shughuli zao.

Alisema wanawake wengi nchini wanashindwa kusonga mbele kibiashara kwa kuwa wanakosa taarifa ambazo zingetumiwa kuwawezesha kusonga mbele na kujikwamua kiuchumi.

"Ni wakati sasa kwa wanawake nchini kutafuta taarifa zitakazoinua biashara, mafunzo kama haya mmeyapata bure myatumie vema kuhakikisha mnatimiza malengo yenu.”alisema.

Kwa upande wa muandaaji wa mafunzo hayo, Vicky Kamata alisema mfuko wake mbali na kutoa misaada mbali mbali kwa walemavu, ni wakati sasa wa kusaidia elimu kwa wanawake na kuwawezesha mitaji ili waweze kufikia lengo.

“Naamini mwanamke ni jeshi kubwa, ukimuwezesha mwanamke mmoja umewezesha jeshi kubwa lililopo nyuma yake hata watoto watasoma vizuri.”alisema Kamata

Awali  kupitia mfuko huo wa Victoria Foundation, awamu wa kwanza ya utekelezaji wa ahadi zake kwa wakazi wa Geita waliomsaidia kuchaguliwa kwake kuwa mbunge kupitia CCM , Kamata alitoa misaada ya  vyakula, mavazi, magodoro na viti vya walemavu (Wheel Chair) 30 kwa wakazi wa tarafa ya Bugando.

Alisema kupitia mfuko wa Victoria Foundation  wakazi wa Geita watanufaika kwa misaada mbali mbali itakayowawezesha watu hususani wanawake wajane na yatima na wale wasiojiweza kuondokana na adha walizonazo na kufurahia maisha kama watu wengine.
Source:DailyNews-Habarileo Blog
Picha mbalimbali zikionesha matukio wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Victoria Foundation uliofanyika hivi karibuni katika mji wa Geita ulioenda sabambamba na utoaji vyeti kwa washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali.
MAFUNZO ya ujasiriamali yametolewa kwa wanawake wajane na wasiojiweza wa mkoa wa Geita kupitia mfuko wa Victoria Foundation unaomilikiwa na mbunge wa viti maalum CCM, Vicky Kamata.

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA BMT, BODI YA LIGI NA TFF MJINI DODOMA

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WATAKAOSHINDWA KUSIMAMIA AFYA YA MAMA NA MTOTO KUKIONA

0
0
 Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya imesema itawashughulikia wakurugenzi wote wa halmashauri ambao wataonekana kuwa chanzo cha ukosefu wa huduma bora za mama na mtoto katika hospitali za Wilaya na vituo vya afya kote nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu alipokuwa akifungua mkutano wa 24 wa Madaktari bingwa wa magonjwa ya Wanawake na Watoto (AGOTA) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

“ swala la afya ya mama na mtoto ni lililopewa kipaumbele kwa serikali ya Tanzania na Dunia kwa ujumla hivyo wakurugenzi wa halmashauri wanao wajibu wa kuhakikisha wanaboresha huduma hizi kwani ni vitu vidogo ambavyo vipo ndani ya bajeti yao, tutawachukulia hatua wakurugenzi wote ambao watashindwa kutimiza wajibu wao katika kulinda afya ya mama na mtoto” amesema Waziri Ummy.

Amesema zipo changamoto nyingi katika huduma hizi hivyo katika bajeti ya 2017/2018 wizara yake imetenga fedha za kutosha kwa ajili ya huduma za uzazi wa mpango ili ziwe bora na kuepuka kero ya wanawake wanaopata huduma hii kupanga foleni.

Ametaja kuwa katika tafiti inaonyesha kuwa ni wanawake 32 tu kati ya 100 ndio ambao wanatumia huduma ya uzazi wa mpango hivyo serikali itatumia njia nzuri zaidi kuwafikia wanawake wengi.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Madaktari bingwa wa masuala ya afya ya Mama na Mtoto (AGOTA), Prof Andrea Pembe amesema kuwa serikali imefanya kazi kubwa sana katika utoaji wa huduma katika vituo vya afya Tanzania .

Ameongeza kuwa uelewa mdogo wa jamii juu ya masuala ya afya ya uzazi yamechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa vifo vya Mama na mtoto.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Watoto na wanawake nchini AGOTA wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 24 wa Taasisi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar leo.
Rais wa Shirikisho la Madaktari bingwa wa masuala ya afya ya Mama na Mtoto (AGOTA), Prof Andrea Pembe, akizungumza kabla ya kumkaribisha waziri Ummy Mwalimu kwa ajili ya ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar leo.
 Daktari Gileard Masenga kutoka Hospitali ya KCMC Moshi akitoa taarifa fupi juu ya tafiti iliyofanywa kuhusiana na Afya ya Mama na Mtoto nchini kwenye mkutano wa 24 wa Madaktari bingwa wa magonjwa ya Wanawake na Watoto (AGOTA) uliofanyika leo.
 Baadhi ya Madaktari walioshiriki mkutano wa 24 wa Madaktari bingwa wa magonjwa ya Wanawake na Watoto (AGOTA) wakifutilia mada zilizokuwa zinatolewa leo.
Waziri Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari 

PROF. MUHONGO AZINDUA BODI YA REA

0
0
Na Veronica Simba – Dodoma.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, amezindua Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kuiagiza kufanya kazi kwa kutanguliza maslahi ya Taifa na Watanzania kwa ujumla.
Profesa Muhongo alizindua Bodi hiyo jana, Aprili 19, 2017 Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.

Akizungumza na Wakurugenzi wa Bodi hiyo mpya, wakati wa hafla ya uzinduzi, Profesa Muhongo aliwaagiza kuhakikisha wanawasimamia wakandarasi waliochaguliwa kutekeleza miradi ya umeme vijijini ili wanunue vitendea kazi ikiwemo nguzo, transfoma na nyaya za umeme kutoka kwa wazalishaji wa ndani ya nchi.

“Wakandarasi ni lazima wanunue vifaa hivyo ndani ya nchi. Vikiisha hapa nchini, ndiyo waagize nje. Hatutavumilia kuona mkandarasi ananunua vitendea kazi nje ya nchi wakati hapa nchini vipo tele.”

Hata hivyo, Profesa Muhongo alisisitiza suala la ubora ambapo alifafanua kuwa, ni lazima vitendea kazi vinavyonunuliwa viwe katika ubora unaostahili. “Japokuwa tunataka vitu kutoka ndani ya nchi lakini ni lazima tuzingatie suala la ubora wake.”

Akiendelea kutoa maagizo kwa Bodi hiyo, Waziri Muhongo pia alielekeza kwamba, Kampuni zote za kigeni ambazo zimeshinda Tenda ya kutekeleza miradi ya umeme vijijini awamu ya Tatu (REA III), ni lazima zifanye kazi na wakandarasi wadogo (sub-contractors) wa kitanzania.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akizungumza na Wakurugenzi wa Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini - REA (hawapo pichani), wakati alipokuwa akiizindua rasmi Bodi hiyo Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Aprili 19, 2017.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (kulia), akiwasomea majukumu yao ya kazi, Wakurugenzi wa Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Bodi hiyo, uliofanyika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Aprili 19, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya REA, uliofanyika hivi karibuni mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa tano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), mara baada ya kuizindua rasmi hivi karibuni mjini Dodoma. Kulia kwa Waziri ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa James Mdoe na kushoto kwa Waziri ni Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Gideon Kaunda. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga..

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA APOKEA TAARIFA YA KAMATI YA MGOGORO WA LOLIONDO

0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo Taarifa ya Kamati Shirikishi (Teule) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye pori tengefu la Loliondo kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati Shirikishi (TEULE) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye pori tengefu la Loliondo kabla ya kupokea taarifa ya kamati hiyo kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kuhusu ramani ya pori tengefu la Loliondo kabla ya kupokea taarifa ya kamati Shirikishi (TEULE) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumishi ya ardhi kwenye pori hilo. Taarifa hiyo ilikabidhiwa kwa Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Spika mjini Dodoma Aprili 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, mrisho Gambo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Shirikishi (TEULE) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye pori tengefu la Loliondo kabla ya kupoke taarifa ya kamati hiyo kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati Shirikishi (TEULE) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye pori tengefu la Loliondo kabla ya kupokea taarifa ya kamati hiyo kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MTOTO AKRAM MBAROUK AMEPOTEA ANATAFUTWA NA WAZAZI WAKE

0
0



Mtoto Arkam Salim Mbarouk (anayeonekana kwenye picha) mwenye umri wa miaka 12 amepotea tokea tarehe 19 April, 2017 mida ya jioni (alasiri) wakati anakwenda madrasa (maeneo ya Makongo Juu) na hajaonekana mpaka sasa.



 Mara ya mwisho alivaa kanzu ya msikitini rangi ya kijivu na pensi nyekundu. Tafadhali tunaomba utakapomuona popote au kupata taarifa zake uwasiliane nasi kwa namba hizi zifuatazo



 0782412840 AU 0659296329 AU 0713251344,

0718237250 AU 0713484838 AU 0655188918 AU 0658023243 AU 0713483436 AU 0784675774.

 TAFADHALI TUNAOMBA SAMBAZA UJUMBE HUU KWENYE MAGROUP MENGINE KADRI IWEZEKANAVYO.

ZURICH GROUP, JUBILEE INSURANCEWAZINDUA BIMA MPYA YA GHARAMA NAFUU 'AFYA WOTE

0
0
  Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wzee na Watoto, Edward Mbanga (Wa pili Kulia) akipokea Tisheti kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zurich Group, Sudi Simba, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bima mpya ya Afya, inayojulikana kwa jina la Afya Wote, iliyo chini ya Jubilee Insurance, Zurich Group waanzilishi wa Afya Wote Medical Insurance Scheme, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe yanga Manispaa ya Temeke jijini Dar esSalaam, leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Jubilee Insurance, Rogation Selengia (kushoto) ni Mkuu wa Idara ya Afya Jubilee Insurance, Kenneth Agunda. Picha zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Wakionyesha Vipeperushi na fomu zinazoelezea huduma za Bima hiyo, baada ya uzinduzi huo.

 Na Ripota wa mafoto Blog, Dar

WITO umetolewa kwa  wananchi wa kipato cha chini na kati kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya mpya unaojulikana ‘Afya Wote’, uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo.



Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Sera na Mipango Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wzee na Watoto, Edward Mbanga, alisema kuwa uzinduzi wa mfuko huo wenye gharama nafuu ni  kimbilio la wanyonge kutokana na kuwajali wananchi wa aina zote.




Aidha alisema kuwa wananchi wataona umuhimu wa mfuko huo pindi wanapopatwa na tatizo la ugonjwa na kwa wakati huo wakawa hawana pesa za kukidhi matibabu.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

BANDA RUKSA KUICHEZEA SIMBA MECHI ZILIZOBAKI

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Hatimaye kamati  ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekaa leo na kumsikiliza beki wa Simba Abdi Banda aliyesimamishwa na kamati ya saa 72 baada ya klabu ya Kagera Sugar kutuma malalamiko dhidi yake.


Kamati hiyo, imefikia maamuzi ya kumfungia  mechi mbili kwa kosa la kumpiga ngumi kiungo wa Kagera Sugar, George Kavilla Aprili 2, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.


Adhabu hiyo inamuweka huru Banda kuweza kuendelea kucheza mechi tatu zilizosalia za timu hiyo baada ya kuwa nje kwa mechi mbili dhidi ya Mbao na Toto Africa zilizochezwa mapema wiki iliyopita.

Katika mchezo huo dhidi ya Kagera Banda alimpiga ngumi Kavila pasi na kuwa na mpira lakini mwamuzi wa mchezo huo hakumpa kadi na kupelekea adhabu yake kuwa nyepesi kulingana na ushahidi alioupeleka katika kamati hiyo.

Kamati iliweza kubaini kuwa Banda  hakupewa adhabu yoyote na refa kwa sababu hakuona tukio hilo, alifanya kitendo cha aina hiyo kwenye mechi namba 169 kati ya Simba na Yanga iliyofanyika Februari 25, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam akimpiga kiungo Said Juma ‘Makapu’.


Awali, Klabu ya Kagera Sugar iliwasilisha malalamiko dhidi ya kitendo cha beki wa Simba, Abdi Banda kumpiga ngumi kiungo wao George Kavilla wakati akiwa hana mpira, na Mwamuzi wa mechi hiyo kutochukua hatua yoyote.

ZIARA YA KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI PROF. KITILA MKUMBO RUVU JUU

WACHUNGAJI ZAIDI YA 300 WA MADHEHEBU MBALIMBALI KUSHIRIKI SEMINA NA KONGAMANO JIJINI ARUSHA

0
0
Na Pamela Mollel,Arusha

Wachungaji zaidi ya 300 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini bila kujali madhehebu yao wako katika semina maalumu ya neno la Mungu yenye lengo la kusaidia kupeleka ujumbe wa madhihilisho ya nguvu ya kristo katika maeneo mbalimbali ya nchi ili watu waweze kubadilika na kumjua Mungu

Semina hiyo ya siku nane iliyoandaliwa na kanisa la Zion City Church Arusha litafanyika kanisani hapo ikiambatana na Kongamano ambalo limeandaliwa kwa ajili ya wachungaji na watu mbalimbali likiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kupeleka injili kwa watu wa mataifa.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo Mch.George Mngodo alisema kuwa watu ambao wataweza kushiriki wataweza kujifunza mambo ambayo awali hawakuweza kuyafahamu ambayo yatawawezesha kuvuka kutoka hatua moja kwenda nyingine.

Mngodo aliongeza kuwa huduma zitakazo tolewa katika katika kongamano hilo hazitawakugusa kiroho tu bali hata kwenye maisha yao ya kawaida wataweza kubadilika

“Tunaamini kongamnao hili litagusa wachungaji hawa na jamii wanayoihudumia kimwili na kiroho”alisema Mngodo

Kwa upande wake mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo Paul Sulley alisema kuwa matarajio yao ni kuona kila mtumishi anayehudhuria anavuviwa upya ili aweze kumtumikia Mungu kwa bidii.

Mch.Dr.Jerry Williamson kutoka nchi Marekani akiomba katika ibada ya katika kongamano kanisa la Zion lililopo njiro jijini Arusha ambapo kanisa hilo limeendaa semina na kongamano kwa wachungaji pamoja na washirika wengine,kulia kwake ni Ben Mangeni ambaye ni mkalimani wake

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo Mch.George Mngodo akiongea na waandishi wa habari , alisema kuwa watu ambao wataweza kushiriki kongamano hilo wataweza kujifunza mambo ambayo awali hawakuweza kuyafahamu ambayo yatawawezesha kuvuka kutoka hatua moja kwenda nyingine
Mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo Paul Sulley akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa matarajio yao ni kuona kila mtumishi anayehudhuria anavuviwa upya ili aweze kumtumikia Mungu kwa bidii.

kushoto ni Mtume trice Shumbusho akiwa na mkalimani wake akihubiri katika kongamano hilo.
Waumini wakiwa katika maombi.


Onyesho la Harusi Trade Fair kufanyika Mei 12-13

0
0
Maonesho ya tisa ya Harusi Trade Fair yanatarajiwa kufanyika Mei 12 hadi 13 mwaka huu kwenye hoteli ya Golden Tulip Oyststerbay Jiji Dar es salaam ili kuwapatia maharusi uwanja wa kuchagua mahitaji yao yote kwa ukamilifu siku ya harusi yao.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Meneja Biashara Hamis Omary amesema maonesho hayo ni ya kipekee kwa Afrika mashariki na hufanyika mara moja kwa kila mwaka.

"Tunawatangazia jamii kwa ujumla watarajie maonesho yakuvutia kuburudisha pamoja na nyakati rahisi kwa bwana Harusi na bibi harusi kuandaa vitu vyao vya harusi, vilevile kutakuwa na mitindo mipya mingi kutoka kwa wauzaji bora katika sekta ya harusi kila maonesho yanavyoendelea kukua kutoka hatua moja na kwenda hatua nyingine ndivyo ubora unavyoendelea kuongezeka" amesema
Meneja Masoko wa Kampuni ya 361 Degrees, Hamis Omar(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari akizungumza kuhusu maonesho ya tisa ya Harusi Trade Fair yanatarajiwa kufanyika Mei 12 hadi 13 mwaka huu kwenye hoteli ya Golden Tulip Oyststerbay Jiji Dar es salaam.
Kaimu Meneja wa Hoteli ya Golden Tulip, Adele Johnson(kushoto)  akizungumzia na waandishi wa habari leo kuhusu jinsi walivyodhamini maonesho ya tisa ya Harusi Trade Fair yanayotarajiwa kufanyika Mei 12 hadi 13.
Mratibu wa matukio wa Kampuni ya 361 Degrees, Naomi Godwin akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio waliyoyapata kwenye maonesho yaliyopita.
Mmoja wa waandishi wa habari akiuliza swali kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Maelezo jijini Dar leo.

MCHUNGAJI DKT GETRUDE RWAKATARE AAPISHWA KUWA MBUNGE

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images