Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

MATOKEO YA LIGI YA KIKAPU MKOA WA DSM

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Matokeo ya michezo ya mpira wa kikapu iliyochezwa wikiendi hii ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam RBA Wiki  ya tisa.

 7/4/2017

Jogoo 75/61 Chui


Jkt 74/79 Kurasini heat

Pazi 58/54 Ukonga k.

Trh 8/4/2017

Chui 62/69 Youngstars 

Magnet 60/88 Jogoo 

Mgulani 44/68 Mabibo

Abc 83/50 Outsiders 

Jkt 72/49 Ukonga k.

Trh 9/4/2017

Mgulani 47/52 Chui

Michezo mingine haikuchezwa kwa sababu ya mvua pamoja na kukatia kwa umeme.

SERIKALI YAANDA UTARATIBU WA KUUNDA BODI MPYA YA TUMBAKU

$
0
0

Naibu Waziri wa Kilimo Uvuvi na Ufugaji Mhe. William Ole Nasha akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.

Na Daudi Manongi-MAELEZO DODOMA.
Serikali imesema kuwa inaandaa utaratibu wa kuunda Bodi mpya ya wakurugenzi ya Tumbaku  kwa kuwa ina umuhimu mkubwa katika ukuaji wa Sekta ya Tumbaku nchini.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge mjini Dodoma.

“Serikali ilivunja Bodi ya Tumbaku kwa lengo la kufanya maboresho katika utendaji kazi wa Bodi,na hatua hii ya kuvunja Bodi ya wakurugenzi haihusu kusitisha shughuli zinazotekelezwa katika sekta hii ya tumbaku kwani wapo wataalamu wanaoendeleza utekelezaji wa mpango uliopo wa kuendeleza zao la tumbaku”. Aliongeza Mhe.Ole Nasha.

Aidha amesisitiza kuwa upatikanaji wa pembejeo za zao hilo zitapatikana kupitia vyama vikuu vya ushirika kwa kila eneo kwa kupitia mchakato wa zabuni unaosimamiwa na kuratibiwa na vyama vikuu vya ushirika.

Amezitaja pembejeo za muhimu kwenye zao la tumbaku kuwa ni mbolea aina ya NPK, Mbolea aina ya CAN, nyuzi za kufungia tumbaku wakati wa kuvuna na wakati wa masoko zote zitapatikana kupitia vyama vikuu vya ushirika.

Ameeleza kuwa kwa kuzingatia kuwa wakulima wanahitaji huduma muhimu  hasa katika kipindi hiki cha kuelekea masoko ya tumbaku kwa msimu wa 2017/18, Serikali imeateua timu kwa ajili ya uratibu na kusimamia masuala hayo.

“Tuna timu tayari iko mkoani Tabora ambayo itasimamia na kuratibu masuala mbalimbali ya wakulima ikiwa ni pamoja na kuandaa upatikanaji wa pembejeo kwa msimu ujao,hivyo pamoja na WETCU kuvunjwa kazi za chama hicho zinaendelea kama kawaida”Alisema Mhe.Ole Nasha.

PROF. MUHONGO AKUTANA NA KAMPUNI YA WAZALISHAJI UMEME KWA NISHATI YA JUA YA JUMEME

$
0
0
Na Veronica Simba - Dodoma.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na ujumbe kutoka kampuni ya JUMEME inayojishughulisha na uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati ya jua.

Ujumbe huo ulijumuisha baadhi ya wakurugenzi wa kampuni ya JUMEME ambao ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), Padre Dk. Thadeus Mkamwa na Leo Schiefermueller.
Ujumbe huo ulifika ofisini kwa Waziri Muhongo mjini Dodoma, kumweleza mipango na mikakati yao ya kuendelea na uzalishaji wa umeme wa jua katika maeneo ya Tanzania yaliyo nje ya gridi ya Taifa ya umeme.
Kampuni hiyo, inaendesha mradi wa kuzalisha umeme wa jua katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe na imelenga kuwafikia watu milioni moja ndani ya Tanzania kupitia mitambo 300 katika vijiji vilivyo nje ya gridi ya Taifa ifikapo mwaka 2022.
Profesa Muhongo, kwa upande wake, aliwahakikishia JUMEME kuwa Serikali itawapa ushirikiano unaotakiwa ili kuhakikisha wananchi wa vijijini wanapata umeme kwa kutumia njia mbalimbali muafaka kama ilivyodhamiriwa.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akisisitiza jambo kwa Ujumbe kutoka Kampuni ya JUMEME, waliomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma kuzungumzia masuala ya uzalishaji umeme wa jua. Kutoka kulia ni Leo Schiefermueller, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), Padre Dk. Thadeus Mkamwa na Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga.
 Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya JUMEME, Leo Schiefermueller (kulia), akifafanua jambo kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto). Wengine pichani ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), Padre Dk. Thadeus Mkamwa (wa pili kutoka kulia) na Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kushoto), akitoa maelekezo kwa Ujumbe kutoka kampuni ya JUMEME ambao ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), Padre Dk. Thadeus Mkamwa (kushoto) na Leo Schiefermueller kutoka Ujerumani (kulia). Wa pili kutoka kulia ni Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga.

Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya JUMEME, Leo Schiefermueller (kushoto), akifafanua jambo kwa Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga (kulia). Pamoja nao pichani, ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), Padre Dk. Thadeus Mkamwa.

KUNA MWENENDO MZURI KATIKA SOMO LA KISWAHILI-TWAWEZA

$
0
0
Na Hassan Silayo

Mwenendo wa somo la Kiswahili nchini umeendelea kuimarika na hii ni kutokana na jitihada mbalimbali ziliwekwa na serikali katika somo hilo.

Akitoa ripoti matokeo ya utafiti wa Uwezo,Meneja wa Uwezo Tanzania Zaida Mgalla alisema kuwa kwa watoto walikuwa darasa la tatu walioweza kufauli majaribio ya Kiswahili mwaka 2011 walikuwa asilimia 29 tofauti na asilimia 56 ya mwaka 2015.

Bi. Zaida Aliongeza kuwa kwa darasa la saba kumekuwa na ongezeko la watoto kujifunza na kufanya vizuri zaidi ikiwa kwa mwaka 2011 asilimia 76 walifaulu majaribio ya Kiswahili ikilinganishwa na asilimia 89 ya mwaka 2015.

“Tunaipongeza Serikali ka jitihada zake za kuhakikisha watoto wanapiga hatua katika somo la Kiswahili tunaona ongezeko la ufaulu limeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka na  hii inatia moyo na serikali inatakiwa iendelee kuweka jitihada katika kimarika zaidi na kuacha kuridhika na matokeo haya”.Alisema Zaida.

Aidha Zaida aliongeza kuwa Taarifa ya Tafiti ya Uwezo inaonesha kuwa uwiano kati ya Wanafunzi na vitabu umeendelea kuboreka kutoka wanafunzi 30 kutumia kitabu kimoja mwaka 2013 hadi wanafunzi 8 kwa mwaka 2014, hadi kufikia wanafunzi 3 kutumia kitabu kimoja kwa mwaka 2015.

Akiongelea kuhusu ufaulu katika somo la Kiswahili Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza Aidan Eyakuze  alisema kuwa inatia moyo kuona watoto wetu wanapata matokeo mazuri zaidi kuliko miaka ya nyuma kwenye somo la Kiswahili.

Wakichangia mijadala katika halfa hiyo baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameishauri serikali kuendelea kuweka mazingira mazuri ya watoto kufanya vizzuri katika masomo pamoja na kuboresha maslahi ya walimu ili kuwajengea morali katika kufundisha.
 Meneja Uwezo Tanzania Zaida Mgalla akiongea na wageni waalikwa wakiwamo wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa hafla ya utoa wa matokeo wa Tafiti za Uwezo ambapo mbali na changamoto nyingine takwimu mpya za uwezo zinaonesha mwenendo mzuri katika somo la Kiswahili na uwiano mzuri uliopo kati ya wanafunzi na vitabu,Leo Mjini Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Seleman Jafo akiongea na wageni waalikwa wakiwamo wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa hafla ya utoa wa matokeo wa Tafiti za Uwezo ambapo alipongeza tafiti za TWAWEZA na kuwataka watendaji serikalini kuzitumia tafiti hizo ili kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya elimu,Leo Mjini Dodoma.

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAJIZATITI KUIMARISHA HUDUMA ZAKE

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kueleza mipango mbalimbali ya jeshi hilo ikiwemo uzinduzi wa klabu katika shule za sekondari nchini, zitakazotoa elimu ya uzimaji moto kwa wanafunzi. Kushoto ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kueleza mipango mbalimbali ya jeshi hilo ikiwemo uzinduzi wa klabu katika shule za sekondari nchini, zitakazotoa elimu ya uzimaji moto kwa wanafunzi. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Afisa Habari Mwandamizi, Casmir Ndambalilo. 
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano Mkuu wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Kamishna Jenerali Thobias Andengenye  Leo Jijini Dar es Salaam kuhusu mikakati ya Jeshi hilo kuboresha huduma wanazotoa  kwa kushirikisha wadau wa Maendeleo.


(Picha zote na Frank Mvungi)

MABALOZI WAPYA WA JAMHURI YA MUUNGANO WAMUAGA RAIS WA ZANZIBAR DKSHEIN

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mabalozi wapya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioteuliwa kuiwakilisha  Tanzania  katika Nchi mbali mbali walipofika kumuaga Rais Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe Mabalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioteuliwa kuiwakilisha  Tanzania katika Nchi mbali mbali,  walipofika kumuaga Rais Ikulu Mjini Zanzibar. Picha na Ikulu.

Maziko ya Sir ANDY CHANDE Yatikisa Dar

Masanja Mkandamizaji azungumza katika kongamano la Diaspora jijini Dar es salaam


Harmorapa ft. Juma Nature - Kiboko Ya Mabishoo

uamuzi dhidi ya maombi ya Serikali ya Marekani ya kuwataka raia watatu wa Tanzania waodaiwa kuhusika na dawa za kulevya kutolewa kesho Mahakama ya Kisutu

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam kesho inatarajia kutoa uamuzi dhidi ya maombi ya Serikali ya Marekani ya kuwataka raia watatu wa Tanzania wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya kama waende nchini humo kusikiliza tuhuma hizo ama la.

Wajibu maombi wanaotuhumiwa nchini humo ni mfanyabiashara bilionea, Ally Khatib Hajj maarufu kama Shkuba, mfanyabiashara Idd Mafuru na Lwitiko Emmanuel Adam maarufu Tiko.
Katika maombi hayo, serikali inaiomba mahakama itoe amri ya kuwakamata na kuwazuia watuhumiwa hao ambao ni wajibu maombi ianzishe utaratibu wa kuwasafirisha kwenda nchini humo. 

Uchunguzi unaonyesha kuwa mshtakiwa Shkuba, na wenzake walihusika kwenye njama za kusambaza zaidi ya kilo moja ya dawa za kulevya aina ya Heroine ambazo zimezuiliwa nchini humo.
Maombi ya Marekani, yaliyosikilizwa mbale ya hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha, yaliwasilishwa na aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe kupitia, Wakili wa Serikali Mkuu, Edwin Kakolaki.
Wajibu maombi wanatetewa na jopo la Mawakili watatu, wakiwemo Edson Ndusyepo, Majura Magafu na Adinan Chitare.
Wakati wa usikilizwaji Kakolaki alieleza kuwa Waziri wa sheria wakati huo Mwakyembe alipelekewa maombi ya kutakiwa kwa wajibu maombi hao ambapo Aprili 4, mwaka huu mahakama ilitoa amri ya kukamatwa kwao na Aprili 6 walikamatwa na jana walifikishwa mahakamani hapo ambapo maombi hayo yaliwasilishwa.
Kakolaki ameendelea kudai kuwa maombi ya kuwasafirisha wajibu maombi ni halali kwani kumekuwa na mahusiano ya Tanzania kubadilishana wahalifu na nchi za Ulaya tangu enzi za ukoloni wakati Tanzania inaitwa Tanganyika.


Wajibu maombi ambao wanatuhumiwa nchini Marekani ambao ni mfanyabiashara bilionea, Ally Khatib Hajj maarufu kama Shkuba (fulana nyekundu), mfanyabiashara Idd Mafuru (wa pili kulia) na Lwitiko Emmanuel Adam maarufu Tiko (kulia) wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.a

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI MGENI RASMI UZINDUZI WA RELI YA KISASA KESHO

$
0
0
RAIS Dk. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa  uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi reli ya kisasa itakayofanyika  kesho Pugu, Ilala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika sehemu ya uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa watanzania waunge mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Amesema reli hiyo ni ya kisasa ambayo itarahisisha usafiri wananchi kuondokana na adha ya kusafiri kwa muda mrefu.Makonda amesema baada ya uzinduzi ajira zitatoka katika ujenzi wa reli hiyo na kuwataka wataopata ajira kuwa walinzi reli hiyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli (TRL)  Mhandisi Massanya Kadogosa amesema kuwa ujenzi huo utaanza kwa awamu .Amesema miundombinu hiyo hiyo ikikamilika gari moshi litatembea kilomita 160 kwa sasa hivyo kwa safari zote zitakuwa ni fupi na wananchi wanaweza kujenga uchumi.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akioneshwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema   maandalizi ya uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi wa reli ya kisasa Standard Gauge Pugu jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  akipata maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika la Reli Tanzania (TRL),  Mhandisi ,Massanja Madogosa  juu ya katika maandalizi ya a uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi wa reli ya kisasa Standard Gauge Pugu jijini Dar es Salaam.
 .Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitoa maelekezo  kwa watendaji walipotembelea  maandalizi ya uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi wa reli ya kisasa 'Standard Gauge' kesho Pugu jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Mhandisi Massanja Kadogosa akizungumza na waandishi wa habari juu  ya uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi wa reli ya kisasa utaofanyika kesho  Pugu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi waliofika kushuhudia eneo hilo la tukio hapo kesho

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA WAJUMBE WA KAMATI YA PILI YA UCHUNGUZI WA MADINI YALIYOMO KWENYE MCHANGA KUTOKA MIGODINI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Nehemiah Eliachim Osoro kuwa mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Pili itayofanya Uchunguzi wa Madini yaliyomo kwenye Mchanga kutoka kwenye migodi mbalimbali hapa nchini kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 11, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Longinus Kyaruzi Rutasitara kuwa mjumbe wa  Kamati Maalum ya Pili itayofanya Uchunguzi wa Madini yaliyomo kwenye Mchanga kutoka kwenye migodi mbalimbali hapa nchini kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 11, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt Oswald Joseph Mashindano  kuwa mjumbe wa  Kamati Maalum ya Pili itayofanya Uchunguzi wa Madini yaliyomo kwenye Mchanga kutoka kwenye migodi mbalimbali hapa nchini kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 11, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Casmir Sumba Kyuki kuwa mjumbe wa  Kamati Maalum ya Pili itayofanya Uchunguzi wa Madini yaliyomo kwenye Mchanga kutoka kwenye migodi mbalimbali hapa nchini kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 11, 2017.
 


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

RAIS DKTMAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UTENDAJI KAZI YA TAKUKURU YA 2016/2016

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola akitoa muhtasari wa Taarifa ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU ya mwaka 2015/2016 Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne 11, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea toka kwa Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola Taarifa ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU ya mwaka 2015/2016 Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne 11, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kupokea Taarifa ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU kwa mwaka 2016/2017 Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne 11, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola na watendaji wa taasisi hiyo baada ya kukabidhiwa Taarifa ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU kwa mwaka 2015/2016 Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne 11, 2017.
PICHA NA IKULU

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 11.04.2017

JIANDIKISHE SASA KUSHIRIKI MAONESHO YA SITA YA VITO JIJINI ARUSHA


JESHI LA POLISI LAPOKEA PIKIPIKI 20 KUTOKA KAMPUNI YA HUAWEI TANZANIA

$
0
0
 Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini, D-IGP Abdulrahman Kaniki (katikati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Gaomeng Dong (kushoto) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa makabidhiano ya pikipiki 20 zilizotolewa na Kampuni ya Huawei kwa Jeshi la Polisi nchini zitakazosaidia katika shughuli mbalimbali za kukabiliana na uhalifu hapa nchini. Pikipiki hizo ni sehemu ya pikipiki 56 zilizokuwa zimeahidiwa na Kampuni hiyo kwa Jeshi la Polisi ili ziweze kusaidia ufanisi wa kazi kwa Jeshi hilo.

 Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini, D-IGP Abdulrahman Kaniki akiwa amepanda kwenye moja ya pikipiki hizo alipokuwa akiijaribu, muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Gaomeng Dong (wa pili kushoto) katika hafla fupi ya makabidhiano hayo, iliyofanyika katika viwanja vya Polisi Oysterbay, Kinondoni jijini Dar es salaam leo.

 Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini, D-IGP Abdulrahman Kaniki akizungumza katika hafla hiyo.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

KAMBI YA VIPIMO NA MATIBABU YA MACHO MKOANI KIGOMA

TIB Corporate bank (TIB CBL) yashiriki katika jukwaa la biashara jijini Mwanza

$
0
0

TIB Corporate bank (TIB CBL) wameshiriki katika  jukwaa la biashara linalofanyika katika  ukumbi wa Rock City, jijini Mwanza.
Jukwaa hili limehusisha wadau mbalimbali Ili kujadili na kutambua fursa mbali mbali ktk mkoa wa mwanza Na namna ya kuwezesha maendeleo ktk Fursa hizo.
"TIB CBL ikiwa Ni benk ya serikali inalenga kufanikisha lengo la kuwezesha maendeleo ya nchi hivyo kuhakikisha kuwa watanzania wengi na wadau mbalimbali wanapata huduma Bora kabisa za kibenki Kwa gharama nafuu" amesema Ni Bi Theresia Soka mkuu WA kitengo Cha masoko Na mahusiano ya kampuni wa benki hiyo.
Akiwasilisha mada juu ya huduma zinazopatikana TIB Corporate bank (TIB CBL) ni Bi Theresia Soka mkuu  kitengo Cha masoko na mahusiano ya kampuni wa benki hiyo
 Wadau mbali mbali katika picha ya pamoja baada ya kufanyika kwa  jukwaa la biashara jijini Mwanza

SERIKALI KUFANYIA MAREKEBISHO SHERIA YA NDOA YA MWAKA 1971 - PROFESA KABUDI

$
0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imesema inaendelea na mchakato wa ndani wa kufanyia marekebisho ya kuhuisha na kuimarisha maeneo yaliyo mazuri ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 na kuwasilishwa Bungeni ili kuendana na wakati.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Prof.Palamagamba Kabudi wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.

“Serikali inaendelea na mchakato huu wa mapendekezo ya marekebisho ya Sheria hii Bungeni ili iweze kuendana na wakati kwa kuondoa upungufu uliopo kwa maslahi mapana ya nchi yetu”,Aliongeza Mhe.Kabudi.

Amesema kuwa baada ya miaka 20 kupita tangu sharia hiyo ya ndoa itungwe,Serikali kupitia tume ya kurekebisha Sheria iliifanyia mapitio ya sheria hiyo na kubaini maeneo kadhaa yenye udhaifu na hivyo kuhitaji kufanyiwa marekebisho.
Amebainisha kuwa  Kutokana na maoni hayo ya tume,mwaka 2008 Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria iliandaa waraka  wa baraza la Mawaziri uliokuwa na mapendekezo ya marekebisho ya sharia ya ndoa ya mwaka 1971,hata hivyo desemba 2010 kabla waraka huo kujadiliwa na kuridhiwa na baraza la Mawaziri mchakato wa mabadiliko ya katiba ya jamhuri ya muungano ukaanza na kulilazimu Baraza kusitisha kwa muda mchakato huo.
“Serikali ilikuwa na matarajio kuwa wakati tume ya mabadiliko ya katiba inakusanya maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko ya katiba,wananchi wangetoa maoni kuhusu Sheria ya ndoa  pamoja na sheria  nyingine zinazofanana na hiyo na hivyo maoni yaliyotolewa wakati wa Sheria ya Ndoa yalikuwa machache sana”Alifafanua Mhe.Kabudi.
Sheria ya ndoa mwaka 1971 ni matokeo ya mjadala mpana na shirikishi kupitia waraka wa Serikali namba moja wa mwaka 1969.

WANATAALUMA WAMUAGA MAREHEMU PROFESA SAMWEL MASELE ALIYEWAHI KUWA MKURUGENZI MKUU HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

$
0
0
 Mwili wa aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ukiwasili katika kiwanja cha Graduation Square MUHAS  ukisindikizwa na wanataaluma jana April 11, 2017 ambapo mazishi yamefanyika katika makaburi ya Kinondoni leo April 12, 2017 Jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)


 Mwili wa aliyewahikuwa Mkurugenzi Hospitali ya Taifa Muhimbili Ukiwasili katika kiwanja cha Graduation SQuare Muhas ambapo taratibu za kutowa heshima za mwisho zilifanyika jana April 11, 2017 na leo April 12, 2017 mwili huo unatarajiwa kupumzishwa katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam
 Wanataaluma mbalimbali wakiwa wanaushusha mwili wa mpendwa wao marehemu Profesa, Samuel Maselle kwa maandalizi ya kutowa heshima za mwisho jana
 Baadhi ya viongozi katika meza Kuu akiwemo Profesa, Ephata Kaaya (wa tatu kushoto) wapilikushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa, Lawrence Museru na wa kwanza kushoto ni Profesa Ayub Magimba
 Baadhi ya wanafamilia na wana Taaluma wa MUHAS.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images