Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1645 | 1646 | (Page 1647) | 1648 | 1649 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Bw. Ramadhani Mkeyenge  akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu dhana nzima ya utaratibu wa uwekaji akiba kwa hiari kwenye Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwenye mkutano uliofanyika Makao makuu ya Mfuko mjini Dodoma .
  Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. James Mlowe akizungumza na waandishi wa Habari mjini Dodoma kuhusu umuhimu wa matumizi ya teknolojia ikiwemo huduma za M-pesa na Tigo-pesa katika kuwafikia Watanzania walio wengi ili wajiunge na kuweka akiba kupitia “LAPF Jiongeze Scheme”.
  Meneja mwenye dhamana na Skimu ya uchangiaji wa hiari (LAPF Jiongeze Scheme) Bi. Hanim Babiker akizungumzia taratibu mbalimbali zinazotakiwa kufuatwa ili kuweka akiba kwa njia ya M-pesa na Tigo-pesa wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dodoma.


  0 0

  Na beatrice Lyimo-MAELEZO

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeutaarifu Umma juu ya kuendelea na taratibu za kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mbunge wa Viti  maalumu(CCM) Sophia Simba  aliyefukuzwa uanachama wa Chama cha Mapindizi (CCM) Machi 11,  mwaka huu.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji(R) Semistocles Kaijage imeeleza  kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemjulisha Mwenyekiti wa Tume kuwa kufuatia Mbunge huyo kufukuzwa uanachama wa CCM hivyo kiti cha Mbunge huyo kiko wazi.

  Alisema kuwa Ibara ya 67(1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inaeleza kuwa ili mtu ateuliwe au achaguliwe katika nafasi ya ubunge ni lazima awe mwanachama aliyependekezwa na Chama chake husika cha siasa.


  “Kwa kuwa ndugu Sophia Mnyambi Simba amefukuzwa uanachama wa Chama kilichomdhamini, Ibara ya 67(2)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaelekeza kuwa mbunge huyo amepoteza sifa za kuteuliwa au kugombea Ubunge” alisema Jaji(R) Semistocles Kaijage.

  Aliendelea kwa kusema kuwa kutokana na kuwepo kwa nafasi hiyo taratibu za kujaza nafasi hiyo zinaendelea kwa kuzingatia kifungu cha sheria 86(8) cha Sheria ya Uchaguzi Sura ya 343.

  Kifungu hicho kinasema, orodha ya majina wanawake wagombea waliopendekezwa na tume kwa mujibu wa Ibara 78(4) ya Katiba na kila chama cha siasa kwa uchaguzi mkuu, kwa kuzingatia Ibara  76(3) ya Katiba, itakuwa orodha sawa na ile itakayotumiwa na tume kwa madhumuni ya kujaza nafasi yoyote iliyowazi katika ofisi ya mbunge wa viti maalum vya wanawake wakati wa kipindi kizima cha uwahi wa Bunge.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Yanga Chrles Mkwasa.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Kuelekea mechi ya marudiano ya mchezo wa hatua ya mtoano wa Kombe la Shirikisho baina ya wawakilishi wa Tanzania  klabu ya soka ya Yanga na Mc Alger ya Algeria imeweka wazi kikosi cha wachezaji 20 watakaoondoka kesho kueleo nchini Algeria.

  Yanga wanatarajiwa kuondoka kesho majira ya saa 12 jioni kuelekea nchini Algeria ambapo watacheza na MC Alger siku ya Jumamosi katika Jiji la Alger.

  Akitaja kikosi hicho, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya kwenda kupambana nchini Algeria na tunafahamu ni mchezo mgumu lakini pia ni muhimu sana kwao wakihitaji ushindi wa aina yoyote au sare ili kusonga mbele na kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

  Mkwasa amesema kuwa anapenda kuwa msafara wa wachezaji 20, benchi la ufundi na viongozi utaondoka kesho jioni majira ya saa 12 kwa ndege ya shirika la Emirate kupitia Dubai.

  Wachezaji watakaondoka ni Makipa; Deogratius Munishi na Beno Kakolanya . Nafasi ya ulinzi ni ; Nadir Haroub , Vicent Bossou , Juma Abdul , Vicent Andrew, Oscar Joshua , Juma Abdul , Mwinyi Haji, Hassan Kessy na Kelvin Yondani. 

  Nafasi ya viungo ni; Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deusi Kaseke,Said Makapu, Juma Mahadhi, Saimoni Msuva, Geofrey Mwashuiya na Emmanuel Martin.
   Upande wa washambuliaji ni Amissi Tambwe na Donald Ngoma

  Wachezaji wafuatao wataukosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali ambao ni Justine Zulu, Malimi Busungu, Matheo Antony, Ally Mustapha, Pato Ngonyani, Obrey Chirwa na Yusuph Mhilu.


  0 0

  Na Karama Kenyunko

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekubali maombi ya Waziri wa Katiba na Sheria ya kuwasafirisha watanzania watatu  wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya kwenda nchini Marekani kusikiliza tuhuma zinazowakabili.

  Hakimu Mkazi mfawishi Cyprian Mkeha ametoa uamuzi huo leo. Wajibu maombi hao ni Ally Hatibu Hassan maarufu kama Shkuba, Iddi Salehe Mafuru, na Lwitiko Emmanuel Adam.

  Akisoma uamuzi huo, Hakimu Mkeha amesema, wajibu maombi hao watakaa rumande hadi kibali kutoka kwa Waziri wa Katiba na Sheria kitakapotolewa. Aidha mahakama imesema kuwa wajibu maombi wanahaki ya kukata rufaa ndani ya siku 15 kabla ya Waziri wa katiba na Sheria hajatoa Kibali cha  kuwasafirisha.

  Mapema wiki hii Waziri wa Katiba na Sheria  kupitia Wakili Mkuu wa Serikali Edwin Kakolaki aliwasilisha maombi ya kuwasafirisha wajibu maombi hao kwenda nchini humo kujibu tuhuma za kusafirisha na kusambaza dawa za kulevya.

  Katika maombi hayo, wajibu maombi wanadaiwa kuhusika kwenye njama za kusafirisha na kusambaza zaidi ya kilo moja ya Heroine nchini humo.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Cosms Nshenye akiwaonesha waandishi wa habari hawapo pichani mashina ya bangi yaliyolimwa katika shamba la mkulima wa kijiji cha Liweta ambaye hakufahamika jina lake walipokuwa katika msakao wa kuyabaini na kuteketeza mashamba ya Bangi.
  Baadhi ya Askari Polisi kutoka kituo kikuu cha Polisi Wilayani Songea wakindelea na kazi ya kung'oa bangi katika moja ya shamba katika kijiji cha liweta katika halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoni Ruvuma, halmashauri hiyo ni miongoni mwa halmashauri ambazo wananchi wamekithiri katika kilimo hicho.
  Afisa Masoko wa Kampuni ya Pannar Seed (T) ltd, Sabasaba Manase akiwaonesha wakulima wa kijiji cha mletele katika manispaa ya songea mkoani Ruvuma shamba lililotumia mbegu aina ya pan 15 zinazosambazwa na kampuni hiyo.mbegu hizo zinatajwa kuleta mafanikio makubwa kwa wakulima kutokana na kukomaa haraka,kujaa vizuri na hata kuhimili hali ya hewa ikilinganishwa na mbegu za makampuni mengine.

  0 0

  Katibu mkuu wa Chama cha Tennisi nchini , Irene Jackson Mwasanga akizungumza na waandsihi wa habari juu ya mpango wa kuiwezesha timu ya mchezo wa Tennisi kwa walemavu.
  Meneja Masoko wa TV 1 Tanzania , Gllian Rugumamu akizungumza na waandishi wa habari juu ya mpango wa T V 1 Kusaidia timu hiyo hili iweze kusafiri kwenda Italy kushiriki mashindano ya Dunia.
  Promotion Meneja wa kituo cha radio cha Times Fm, Namiundu Ngutupari akizungumza juu ya kituo hicho kujiingiza katika kusaidia kupatikana kwa fedha za wachezaji hao kuwawezesha kufika nchini Italy katika mashindano ya Dunia.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Timu ya Magongo ya Tennis inahitaji milioni 120 ili kuweza kushiriki mashindano ya kimataifa yanayotarajia kutimua vumbi Mei 1 hadi Mei 6 nchini Italy.

  Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Rais wa timu hiyo, Denis Makoi amesema kuwa hadi sasa wamepata dola 3500 ambazo dola 3000 zimetolewa na Kampuni ya TPS na dola 1500 zimetolewa na shirikisho la Tenis la Kimataifa.

  Amesema mashindano hayo ni mhimu kwa timu hiyo kwani wao ndio mabingwa wa Afrika hivyo kushiriki kwao kutaongeza kuwa na uwezo na kuiletea Taifa heshima ya mchezo huo.

  Makoi amesema kuwa TV One wamejitoa kuungana na katika kutafuta fedha hizo ili timu hiyo iweze kushiriki mashindano hayo yatayoifanya Tanzania kuingia katika ramani mchezo wa Tenis.

  Meneja wa Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu amesema wamejitoa katika kuhamasisha watanzania kuchangia timu hiyo ili iweze kushiriki mashindano hayo.

  Gillian amesema kama chombo cha habari wanawajibu wa kuhamasisha mchezo wa tenis kutokana na vjana kuwa na uwezo wa mchezo huo.

  Amewaomba watanzania kuchangia kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa M-Pesa kwa kuingiza namba 5590901 kwa Benki ya NIC kwa fedha ya Kitanzania A/C No.2000021086 na dola za Kimarekani kwa akaunti A/C NO. 2000021094.
  Mcheza Tenisi Vosta Piter akijaribu kurudisha mpira uliopigwa na mwenzie katika mazoezi ya mchezo huo katika Viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam
  mcheza Tennisi akiwa katika mazoezi ya kawaida katika uwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Sehemu ya Makaburi ya Mashujaa wa Tanzania, waliokuwa mstari wa mbele kuitetea Tanzania, kuhakikisha wanamuondoa Nduli Idd Amini, hapa wakiwa wamelazwa 


  MWISHO WA VITA VYA KAGERA.

  Jumatano ya Aprili 11, 1979,

  Rais wa Uganda Idi Amin Dada Oumee aliikimbia nchi yake na kwenda Libya na baadaye Saudi Arabia,  baada ya kushindwa vita dhidi ya Tanzania.

  KISA CHA VITA

  Uhusiano wa Tanzania na Uganda ulidorora tangu Januari 25, 1971, Idd Amin Dada(tamka Dadaa) alipoipundua serikali halali ya Rais Milton Obote aliyekuwa nchini Singapore kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola.

  Rais wa Tanzania, Julius Nyerere, akampa Obote na wenzake 2000 hifadhi ya kisiasa. Idd Amin hakufurahishwa na hilo kwani aliamini kwamba Nyerere anamuandaa Obote aje kumpindua, kwa hiyo akapanga kumdhibiti kabla hajampindua...akaivamia Tanzania.

  MIKAKATI

  Kanali, Abdu Kisuule, aliyekuwa mshirika wa karibu wa Idd Amin na kiongozi wa moja ya vikosi vya Uganda kwenye vita hiyo, aliongea na mtandao wa www.thecitizen.co.tz kwenye mfululizo wa makala za 'hadithi ambayo haikuwahi kusimuliwa ya vita vya Kagera' (The untold story of Kagera War by TZ Uganda top soldiers).

  "Nilitumwa Ulaya kununua silaha, nilikuwa na wenzangu, Yekoko na meja Ndibowa. Tulikwenda Bilbao Hispania. Tulitumwa kununua vifaru, bomu aina ya Napalm ambalo ni maalumu kwa ajili ya kupambana na saba saba ya Tanzania(mtambo wa kurushia maroketi uliotengenezwa Urusi uliokuwa ukiitwa BM Katyusha rocket launcher), na ndege 112 za kuangushia mabomu.

  Kwa bahati mbaya, kila tulipoenda, Tanzania ilitufuatilia na kuzima jaribio letu la kununua(Tanzania were tracking us and blocking our orders). Endapo tungefanikiwa kununua bomu la Napalm, habari ingekuwa habari nyingine kwa sababu Napalm ni bomu la moto ambalo huunguza kila kitu, linapotua. Wakati bado tukiwa Hispania, Tanzania ikavamia Uganda"
  VITA YENYEWE

  Januari 30, 1978, majeshi ya Idd Amin yalivamia Tanzania na kuvunja daraja la mto Kagera linalouunganisha mkoa wa Kagera na sehemu nyingine ya Tanzania. Amin akautangaza mkoa wa Kagera kama sehemu ya Uganda.

  Rais wa Tanzania, Julius Nyerere akamsihi Amin kuondoa majeshi yake...Amin akakataa. Nyerere akaziomba jumuia za kimataifa kulaani uvamizi wa Idd Amin lakini dunia ikakaa kimya.

  Nyerere akatangaza vita vilivyoanza Oktoba 30, 1978.

  UWANJA WA MAPAMBANO

  Nyerere alikusanya jeshi la wananchi lililoanza na askari pungufu ya 40,000 na kuongezeka mpaka 100,000 wakiwemo polisi, askari magereza, JKT na migambo

  Jeshi hilo likaungana na vikundi mbalimbali vya waganda vilivyokuwa vikimpinga Amin ambavyo vilikutana mjini Moshi kwenye mkutano wao waliouita Moshi.

  Mkutano huo ndiyo ulioanzisha jeshi lililoitwa Uganda National Liberation Army (UNLA).

  Makundi haya ni pamoja na  Kikosi Maalum kilichokuwa chini ya Tito Okello( huyu ndiye aliyeongoza Mapinduzi ya Zanzibar 1964) na David Oyite Ojok. Pia kulikuwa na kikundi cha FRONASA kilichokuwa chini ya Yoweri Museveni, pamoja kikundi kingine kama Save Uganda Movement.

  Majeshi ya Tanzania yalikuwa na mzinga kutoka Urusi ulioitwa BM Katyusha rocket launcher (nchini ulikuwa ukifahamika kama saba saba) ambao ulivurumishwa moja kwa moja kwa majeshi Uganda. Majeshi ya Uganda yarudi nyuma.
  MUAMMAR GADDAFI NA PALESTINA WAMSAIDIA IDD AMIN

  Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, alituma wanajeshi 2,500 kumsaidia Idd Amin. Wanajeshi hao walikuwa na silaha za kisasa kama vifaru vya T-54 na T-55, BTR APC, BM-21 Grad MRL, artillery, MiG-21, pamoja na kombora la Tu-22.

  Hata hivyo, walibya hao na wapalestina wakajikuta peke yao mstari wa mbele huku wanajeshi wa Uganda wakirudi nyuma. Askari wa Libya pamoja na Palestina wakatekwa

  MWISHO WA VITA

  Vita hiyo ilianza Oktoba 30, 1978 na kumalizika Aprili 11, 1979.
  Baada ya vita hii, Gaddafi akamuomba Nyerere awaachie askari wake na yeye atampa pesa nyingi au mafuta. Nyerere akakataa akisema binadamu halinganishwi na chochote, akawaachia bure askari wale ambao walisifu sana jinsi walivyotendewa wakati walipokuwa mateka.
   Hayati Muammar Gaddafi akisalimina na wanajeshi wa jeshi la Idd Amin wakati wa vita ya Kagera. Idd Amin (katikati) akiwa anashuhudia.
   

  Baadhi ya mabaki na kumbukumbu ya magari na mabomu yaliyotumika katika Vita ya Idd Amin mwaka 1978-79.

  0 0

  Na Benny Mwaipaja-Wizara ya Fedha na Mipango.

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekutana na Taaasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) kwa lengo la kujadili namna ya kuboresha mazingira ya biashara nchini na kukuza uchumi ili kuiwezesha Tanzania kutimiza azma yake ya kuwa na uchumi wa viwanda.

  Mkutano huo uliongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Dkt. Philip Mpango pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji (MB), Mh. Charles Mwijage ulifanyika mkoani Dodoma katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango.

  Katika mkutano huo Serikali ilipata nafasi ya kusikiliza baadhi ya changamoto ambazo zinaikabili Sekta hiyo na kuahidi kuandaa namna bora ya kuzitatua kwa manufaa ya Taifa.Akizungumza katika mkutano huo Dkt. Mpango alisema kuwa mkutano huo umelenga zaidi katika kuboresha mahusiano na uaminifu kati ya Sekta Binafsi nchini na Serikali.

  “Sekta Binafsi na Sekta za Umma inabidi zifanyekazi kwa pamoja kwa maendeleo ya Taifa, niwaombe wafanyabiashara mtoe taarifa za watumishi wa Umma wasio waadilifu ili kuondoa hali ya kutoaminiana”, alisema.Dkt. Mpango aliongeza kuwa Serikali inaahidi kutatua kero mbalimbali zinazoikabili Sekta hiyo hususani suala la utitiri wa kodi na marejesho ya kodi ili kupunguza maumivu kwa wafanyabiashara na kukuza uchumi wa nchini.

  Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Dkt. Philip Mpango akisisitiza jambo mbele ya wadau wa Sekta Binafsi katika mkutano maalum wa Sekta hiyo na Serikali iliokuwa na malengo ya kuweka mazingira bora ya uhusiano na ushirikiano mwema katika kukuza uchumi wa nchi na kuiwezesha Tanzania kutimiza azma yake ya kuwa na uchumi wa viwanda ifikapo 2025.
  Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Dkt. Philip Mpango akimsikiliza mdau wa Sekta Binafsi, Bw. David Mwaibula kabla ya kupokea kitabu cha utafiti wa masuala ya Sekta hiyo, katika mkutano kati ya Serikali na Sekta Binafsi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dkt. Reginald Mengi akizungumza na wadau kutoka Serikalini na Sekta Binafsi ambapo ameiomba Serikali iwaamini wawekezaji wazawa kwa maendeleo ya Taifa na kuongeza kuwa Taifa lolote haliwezi kujengwa na wageni.


  Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Serikali wakifuatilia kwa makini maelezo ya wadau wa Sekta Binafsi wakati wa mkutano maalum wa Serikali na Sekta Binafsi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.


  0 0

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetoa vifaa vya michezo kwa timu ya taifa ya wanawake ya Kilimanjaro Queen kwa lengo la kuiwezesha timu hiyo kuwa na vifaa bora vitakavyowawezesha kuendelea kufanya vizuri katika michuano mbalimbali ndani na nje ya nchi 

  Vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na viatu vya mpira pair 20 na socks pair 40 vitawawezesha wachezaji hao kuondoka na changamoto ya vifaa vya michezo hususani viatu bora vya kuchezea mpira ambavyo ni nyenzo muhimi katika mchezo wa soka.

  Akiongea baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo kwa niaba ya timu ya Kilimanjaro Queens, Mwenyekiti wa soka la wnawake Amina Karuma alisema “ Tunajisikia furaha kupokea vifaa hivi na nawapongeza sana Airtel kwa kutimiza ahadi yao yakutupatia vifaa lakini pia kwa kuunga mkono jitihada za kukuza soka la wanawake nchini.

   Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchochea kukua kwa soka la wanawake kwa kushirikisha timu  za wasichana katika michuano ya Airtel Rising Stars kila mwaka na kwa kupitia michuano hii tumeweza kupata vipaji tunavyoviona leo katika timu zetu za wanawake.

  “Tunawahakikishia vifaa hivi vitatusaidia saana kwani viatu vya mpira ni nyenzo muhimu sana lakini pia ni moja kati ya changamoto kubwa kwa wachezaji wetu. Tunayo mipango mingi na michuano mbalimbali iliyopo mbele yetu na tumejipanga kufanya vizuri lakini pia kujiandaa vyema kwa michuano ya AFCON inayotegemea kuanza Februari Mwakani. “Aliongeza Karuma
  Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kushoto), akikabidhi vifaa vya michezo kwa Mwenyekiti wa Soka la Wanawake Tanzania, Amina Karuma, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kusadia timu ya taifa ya wanawake ya Kilimanjaro Queens, ili kuiwezesha timu hiyo kufanya vizuri katika michuano mbalimbali ndani na nje ya nchini. Kulia ni Kocha Mkuu wa timu hiyo, Sebastian Nkomwa na Nahodha, Sophia Mwasikili.


  0 0


  0 0

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuutarifu Umma kuwa; kwa mujibu wa Kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Mhe. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemjulisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa; kufuatia Mbunge wa Viti Maalum, SOPHIA MNYAMBI SIMBA kufukuzwa uanachama wa Chama cha Mapinduzi tarehe 11 Machi, 2017 kiti cha Mbunge huyo wa Viti Maalum Wanawake kwa tiketi ya CCM kiko wazi.

  Kwa mujibu wa Ibara ya 67 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ili mtu ateuliwe au achaguliwe katika nafasi ya Ubunge ni lazima awe mwanachama aliyependekezwa na Chama chake husika cha Siasa.

  Kwa kuwa Ndg. SOPHIA MNYAMBI SIMBA amefukuzwa uanachama wa Chama kilichomdhamini, Ibara ya 67 (2) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaelekeza kuwa Mbunge huyo amepoteza sifa za kuteuliwa au kugombea Ubunge.

  Kutokana na kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge wa Viti Maalum, taratibu za kujaza nafasi hiyo zinaendelea kwa kuzingatia kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

  Jaji (R) Semistocles Simon Kaijage
  Mwenyekiti
  TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
  12 Aprili, 2017
  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akisalimiana na familia ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Israel, Mhe. Ehud Barak (kulia) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jana kwa ajili ya ziara ya kutembelea vivutio vya utalii nchini. Waziri Mkuu huyo wa 10 wa Israel aliliongoza taifa hilo mwaka 1999 - 2001.
  Waziri Mkuu Mstaafu wa Israel, Ehud Barak (wa pili kushoto) akimueleza jambo Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe muda mfupi baada ya kuwasili na ndege ya shirika na ndege la Israel (Israel Air) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro jana kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akimuongoza mgeni wake, Waziri Mkuu Mstaafu wa Israel, Ehud Barak (kushoto kwake) kuelekea kwenye maandalizi ya ziara yake ya kitalii nchini baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro jana. (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)

  0 0

   Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuhitimisha  Hoja yake ya Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2017/2018, bungeni mjini Dodoma Aprili 12, 2017.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kushoto) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri  Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohitimisha  Hoja yake ya Makadirio ya matumizi ya Ofisi ya Waziri  Mkuu kwa Mwaka 2017/2018, bungeni mjini Dodoma Aprili 12, 2017 
   Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuhitimisha  Hoja yake ya Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2017/2018, bungeni mjini Dodoma Aprili 12, 2017.


  0 0

   Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt Asha-Rose Migiro mapema mwezi huu aliwasilisha hati ya utambulisho (letter of credence) kwa Rais wa Ireland, Mhe. Michael D. Higgins.
  Akiwasilisha hati hiyo katika Ikulu ya Ireland, Balozi Migiro alimfikishia Rais Higgins salam za Mhe. Rais John Magufuli na wananchi wa Tanzania pamoja na kumuahidi kufanya kazi itakayoimraisha uhusiano wa kihistoria baina ya Serikali za Tanzania na Ireland pamoja na kuanzisha maeneo mapya ya ushirikiano kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda. Kabla ya kuagana na Rais Higgins, Balozi Migiro alikagua gwaride rasmi liliondaliwa na kikosi cha Jeshi la Anga la nchi hiyo.  
  Akiwa Ireland, Balozi Migiro pia alikutana kwa mazungumzo na wanadiaspora wa Tanzania waishio katika miji mbalimbali ya Ireland.
  Katika mkutano huo aliwasihi wanadiaspora kushikamana, kuwa wamoja na kuunda Jumuiya ya Watanzania waishio Ireland akiwakumbusha kauli ya wahenga isimayo kuwa 'Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu'.
  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt Asha-Rose Migiro  akimkabidhi Rais Michael D. Higgins hati ya utambulisho kutoka kwa Mhe.Rais John Pombe Magufuli.
  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt Asha-Rose Migiro  akikagua gwaride la heshima la kikosi cha jeshi la anga la Ireland
  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt Asha-Rose Migiro  akiagana na Rais Higgins.
   Michael D. Higgins akimuaga Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt Asha-Rose Migiro baada ya kupokea hati yake ya utambulisho 
  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Dkt Asha-Rose Migiro  alikutana kwa mazungumzo na wanadiaspora wa Tanzania waishio katika miji mbalimbali ya Ireland.

  0 0


  SIMU.TV: Waziri wa Nishati na Madini Prof Muhongo amesema kukosekana kwa uaminifu kwa baadhi ya wanasheria wa wizara hiyo kumepelekea mikataba mibovu kwa Taifa; https://youtu.be/QyUuuGhgY5s

  SIMU.TV: Fuatilia mahojiano maalumu baina ya TBC na Dr Hellen Ottaru kuhusu ujenzi wa Reli ya Kisasa na manufaa yake kwenye uchumi wa Tanzania; https://youtu.be/5he3ovQaAz4

  SIMU.TV: Baadhi ya wakazi mkoani Kigoma wameonesha hofu ya kujiunga kwenye vikundi vya Ushirika ili waweze kukopeshwa fedha kwa ajili ya maendeleo; https://youtu.be/U4A_gGZvKPM

  SIMU.TV: Sekta ya Utalii visiwani Zanzibar inasemekana kuwa chachu ya vijana wengi visiwani humo kufahamu Lugha zaidi moja; https://youtu.be/fQ8rFRJ4P_I    

  SIMU.TV: Kampuni binafsi zinazofanya biashara katika maeneo hatarishi kwa uharibifu wa mazingira yametakiwa kuhakikisha wanalinda mazingira; https://youtu.be/C52_tvXJbug

  SIMU.TV: Taasisi inayohusika na utoaji Barcode imetiliana saini na halmashauri za mkoa wa Kigoma kuanza kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo mkoani humo; https://youtu.be/qaJJ2QEA1I0

  SIMU.TV: Afisa mtendaji mkuu wa benki ya Afrika hapa nchini amesema wametenga zaidi ya shilingi bilioni 500 kwa ajili ya kuwakopesha wafanyabiashara; https://youtu.be/qTCLH_zy2yM  

  SIMU.TV: Klabu ya soka ya Yanga inatarajia kuondoka hapo kesho kuelekea nchini Algeria kurudiana na wapinzani wao katika kombe la shirikisho klabu ya MC Alger; https://youtu.be/UZwv8YZcDYQ

  SIMU.TV: Fahamu hapa baadhi ya mapambano ya Masumbwi yatakayopigwa katika sikukuu ya Pasaka nchini Tanzania ; https://youtu.be/RYbgFhOHNFs

  SIMU.TV: Fahamu hapa jinsi mchezo wa kubashiri matokeo mbalimbali ya soka barani Ulaya unavyowanufaisha mashabiki wa soko nchini Tanzania; https://youtu.be/H4q-3AoQXkw


  0 0


  0 0

  Mbunge wa Nkasi Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ali Mohamed Keissy amefunguka na kusema wasanii ambao wanaandika nyimbo za kumtukana na kumkashfu Rais Magufuli wanapaswa kupata kibano zaidi ili waache tabia hiyo.
  Mbunge huyo amesema hayo leo bungeni na kusema angeaachiwa yeye dakika mbili tu wangeona ni nini angewafanya, hivyo kuendelea kuwatetea wasanii hao ni jambo ambalo si sawa, na kusema wasanii hao wajaribu kwenda Rwanda au nchi za kiarabu waone jinsi watakavyonyongwa. 

  "Mtu anaimba wimbo wa matusi kumtukana Rais mwanzo mpaka mwisho harafu anaachiwa nchi gani hii? Utawala gani huu? Wewe mtu unamtukana Rais unaachiwa aende Rwanda kule au nchi za kiarabu watakunyonga. Unamtukana Rais wa nchi wewe umekuwa nani? Uhuru gani huu, Demokrasi gani hii? Unaimba wewe nyimbo na mtu wa studio anarekodi ama kweli huu si utawala wangeniachi mimi dakika mbili ili niwaoneshe hawa" alisema Mbunge Kessy.
  Keissy anasema ni jambo ambalo haliwezekani mtu kumuimba Rais anamtukana na wewe kuendelea kushabikai huku akidai kuwa yeye ameusikiliza wimbo wa Roma na kusikitishwa na kile kilichoimbwa.
  "Ukiusikia huo wimbo wa Roma Mkatoliki ndugu zangu ni wimbo wa aibu sana, haiwezekani mtu na akili yako unasikia wimbo kama ule harafu unashabikia mtu, haiwezekani kusema kweli ni makosa, ni kukosa adabu Rais wa nchi hatukanwi popote pale haiwezekani nendeni nchi zingine, nenda Rwanda hapo nenda Burundi nenda DRC Congo ukaangalie watakushugulikia, nyinyi mnacheka cheka hapa. Rais haiwezekani kumchezea namna hii huu ni utovu wa nidhamu" alisisitiza All Keissy 

  Mbunge wa Nkasi Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ali Mohamed Keissy (kulia) na Msanii Roma Mkatoliki
  Courtesy of MCL


  0 0
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye ibada ya kuadhimisha miaka 33 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Marehemu Edward Moringe Sokoine huko Monduli mkoani Arusha leo.
   Wajane wa Marehemu Sokoine Mama Napono Katrika (kati) Mama Nekiteto (kulia), wakiwa na waziri wa maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe nyumbani kwao Wilayani Monduli
   Msaidizi wa Askofu, Prosper Lyimo akihubiri wakati wa ibada ya kuadhimisha miaka 33 ya kifo cha Waziri Mkuu wa Zamani, Marehemu Edward Moringe Sokoine
   Binti wa Sokoine Namelok na Kaka yake, Balozi Joseph Sokoine wakiwa na wageni wengine walioshiriki ibada ya kumbukumbu ya baba yao wilayani Monduli.
   Baadhi ya viongozi walioshiriki ibada ya kumbukumbu ya miaka 33 ya Sokoine, kutoka kushoto ni Askofu wa Dayosisi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Mkoani Arusha, Solomon Masagwa, Mwakilishi wa Shehe Mkuu, Rajab Kiungiza, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe

  Msaidizi wa Askofu, jimbo kuu Katoliki Arusha, Prosper Lyimo akiweka shada la maua kwenye kaburi la Waziri Mkuu wa zamani, Hayati Edward Moringe Sokoine wakati wa ibada ya kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo miaka 33 iliyopita, iliyofanyika nyumbani kwa Sokoine wilayani Monduli. Picha zaote na Pam Mollel wa Globu ya Jamii, Monduli.  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi mikoa ya Kigoma na Mwanza.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiweka jiwe la msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa, Mama Janeth Magufuli wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Masanja Kadogosa wakati akielezea kuhusu ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amechuchumaa kwenye mfano wa Reli ya Kisasa (SGR) na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Masanja Kadogosa, Mwenyekiti wa Kamati  ya Kudumu ya Miundombinu Profesa Norman Sigala mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli hiyo, wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na Hawa Ghasia (Mb).
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa wakati akipita katika katika ya mfano wa Reli hiyo itakayojengwa. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA  0 0

                  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

        WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

   

  Waziri wa Ujenzi, Uchukukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb), kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997 pamoja na marekebisho yake kupitia Sheria Na. 13 ya mwaka 2009 amemteua Dkt. Edward Wilson Ngwale (pichani) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10.04.2017.

  Mhe. Prof. Mbarawa amemteua Dkt. Ngwale kushika nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi baada ya uteuzi wa awali kufika ukomo. 

  Aidha, sambamba na uteuzi huo Prof. Mbarawa amewateua Wajumbe watano (5) wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania kuanzia tarehe 10.04.2017 kama ifuatavyo:-
  1.    Eng. John Bura – Mkandarasi  kupitia Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB)

  2.    Arch. Pius P. Tesha – Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

  3.    Prof. Bakari M. M. Mwinyiwiwa – Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

  4.    Bw. Ntuli Lutengano Mwakahesya – Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  5.    Eng. Amiri N. Mcharo – Wizara ya Fedha na Mipango.


  Imetolewa na;


  Eng. Joseph M. Nyamhanga

  KATIBU MKUU (UJENZI)

  12.04.2017


older | 1 | .... | 1645 | 1646 | (Page 1647) | 1648 | 1649 | .... | 3272 | newer