Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1643 | 1644 | (Page 1645) | 1646 | 1647 | .... | 3278 | newer

  0 0


  Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi akiongea na wanafunzi wa kidato cha tatu kutoka shule mbalimbali walioingia kwenye fainali za mashindano ya ICT nchini yanayosimamiwa na UCSAF (Universal Communications Services Access Funds) wakati walipotembelea Airtel makao makuu kujifunza zaidi kuhusu technologia ya mawasiliano.
  Wanafunzi hao wa kidato cha tatu kutoka shule mbalimbali walioingia kwenye fainali za mashindano ya ICT nchini yanayosimamiwa na UCSAF (Universal Communications Services Access Funds) wakitumia komputa kubwa iliwekwa kwaajili ya wateja katika duka la Airtel Makao Makuu kuangalia bidhaa na huduma mbalimbali wakati walipotembelea Airtel makao makuu kujifunza zaidi kuhusu technologia ya mawasiliano.
  Kaimu Mkuu wa kitengo cha Uendeshaji wa Mitambo wa Airtel , Frank Munale akiongea na wanafunzi wa kidato cha tatu kutoka shule mbalimbali walioingia kwenye fainali za mashindano ya ICT nchini yanayosimamiwa na UCSAF (Universal Communications Services Access Funds) wakati walipotembelea Airtel makao makuu kujifunza zaidi kuhusu technologia ya mawasiliano. Akishuhudia ni Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi
  Afisa Huduma kwa wateja wa Airtel, Stephen Makongoro akiwaonyesha baadhi ya wanafunzi jinsi ya kupata huduma mbalimbali kupitia komputa kubwa iliyopo katika duka la kisasa la Airtel wakati wanafunzi hao wa kidato cha tatu kutoka shule mbalimbali walioingia kwenye fainali za mashindano ya ICT nchini yanayosimamiwa na UCSAF (Universal Communications Services Access Funds) walipotembelea Airtel makao makuu kujifunza zaidi kuhusu technologia ya mawasiliano.

  0 0


  Na Dotto Mwaibale

  MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Machi, 2017 umeongeza hadi kufikia asilimia 6.4 kutoka asilimia 5.5 mwezi Februari 2017.

  Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

  Taarifa hiyo ilieleza kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Machi 2017 imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi wa Februari 2017.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 108.44 mwezi Machi 2017 kutoka 101.93 mwezi Machi 2016.Mfumuko wa Bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Machi 2017 umeongezeka hadi asilimia 11.0 kutoka asilimia 8.7 ilivyokuwa mwezi Februari 2017.

  Taarifa hiyo imeonesha kuwa kuongezeka kwa mfumuko wa Bei wa mwezi Machi 2017 kumechangiwa na kuongezeka kwa bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Machi 2017 zikilinganishwa na bei za mwezi Machi 2016.

  Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa ukumbi wa mikutano Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) jijini Dar es Salaam leo kupata taarifa ya mfumuko huo wa bei kwa mwezi Machi.
  Ofisa Habari wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Veronica Kazimoto (kulia), akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwapatia taarifa hiyo.

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akiwasili katika kikao ,kati yake na wazee Maarufu wa Kata ya Mtama na Majengo A, kilichofanyika kwenye ukumbi wa kanisa katoliki kijiji cha Majengo A huku akiwa ameongozana na Katibu Msaidizi wa Wilaya ya Lindi Vijijini Bw. Shaibu Bakari Ngatiche .
  Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akizungumza na Wazee maarufu wa Kata ya Mtama na Majengo A ,katika kikao chao kilichofanyika katika ukumbi wa kaniasa la Katoliki,Mtama Lindi Vijijini.Mh Nape alizungumza mambo mengi ikiwemo na kuwaomba Wana Mtama kusameheana kwa mambo yote mabaya yaliyokuwa yametokea na kuanza ukurasa mpya wa kujenga undugu wa kupendana na kushirikiana katika mampo mbalimbali,amewaomba kuziweka kando itikadi zao za kisiasa na badala yake wakae kwa umoja wao wafirie namna ya kuliletea maendeleo jimbo la Mtama.

  "Ndugu zangu,Wazee Wangu siasa kwa sasa zimekwisha,niwaombe tu,itikadi zetu za kisiasa tulizokuwa nazo tuziweke kando,tuanze upya kwa pamoja kuijenga Mtama yetu ili ipige hatua katika suala zima la Maendeleo,na mie kwa vile nimepata nafasi ya kuhakikisha jimbo la Mtama linapata maendeleo,basi ntahakikisha yale yote niliyo yaahidi wakati wa kampeni,ndani ya miaka mitano niwe nimemaliza ama kuyakupunguza kwa kiasi kikubwa",alisema Nape.Picha na MichuziJr.
   Baadhi ya wazee wakimsikiliza Mbunge wa jimbo la Mtama Mh. Nape Nnauye alipokuwa akizungumza nao mambo mbalimbali ya kuhakikisha jimbo la Mtama na kusini kwa ujumla inaanza kupiga hatua kimaendeleo.


  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lindi vijijini Bw. Mohamed Nanyali akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wakati akimkaribisha Mbunge wa jimbo hilo Mh. Nape Nnauye ili kuzungumza na wapiga kura wake kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo Wazee maarufu wa jimbo hilo. 
   Baadhi ya akina Mama waliofika kumsikiliza Mbunge wao
   Mmoja wa Wananchi wa jimbo la Mtama akielezea moja ya changamoto ndani ya jimbo hilo,ambalo amemuomba Mh Nape alifanyie kazi
  Mh.Nape akiwa katikati ya Wazee Maarufu wa jimbo la Mtama wakisubiri chakula cha pamoja


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  amekutana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa nyumbani kwake mjini Dodoma akiwa njiani kuelekea mkoani Iringa kuzindua kikosi kazi cha Taifa cha bonde la mto Ruaha Mkuu.


  0 0


  0 0  0 0


  0 0

                       
   Watanzania na taasisi mbalimbali za kitanzania mmebakiza muda wa siku 9 tu kuwa miongoni mwa wamiliki wa kampuni yetu nunua hisa zako sasa!
   Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yetuwww.vodacom.co.tz/investor-relations


  0 0


  The family of Sir JK Chande (ANDY) wishes to announce the sad demise of their beloved JK Chande who passed away on Thursday 6th APRIL 2017 in Nairobi.

  The funeral cortege will leave from their residence along Msasani Road plot number 366A, at 10:30a.m, on Tuesday 11/4/2017 for Hindu cemetery.  
  This will be preceded by last respects to be paid at the family residence from 8:30a.m.
  The prayer meeting will be held on the same day 11/4/2017 at 5:30p.m at Shree Lohana Mahajan Hall along PRAMUKH SWAMI STREET.
  OM SHANTI SHANTI SHANTI OM.

  0 0  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Msaidizi wa Pembejeo wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bw. Shenal Nyoni ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili kwa kuongeza gharama za pembejeo kwa kushirikiana na baadhi ya mawakala wa pembejeo za kilimo.

  Amesema Serikali italipa madeni yote ya mawakala wa pembejeo za kilimo mara baada ya kukamilisha uhakiki na kujiridhisha juu ya uhalali wake, sababu bado inawahitaji mawakala ili kushirikiana nao katika kuhudumia wakulima kwenye maeneo mbalimbali nchini.
  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Aprili 10, 2017) katika kikao alichokiitisha kwenye Makazi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma kati yake na mawakala wa pembejeo za kilimo pamona na Maofisa kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
  “Gharama ya madeni ni kubwa kuliko pembejeo zilizosambazwa. Hii inatokana na udanganyifu mkubwa unaofanywa na mawakala kwa kushirikiana na watendaji wa Serikali wanaohusika na masuala ya pembejeo,”
  Amesema kuwa kwenye eneo la pembejeo kuna matatizo makubwa kutokana na baadhi ya Maofisa kuzungumza na mawakala na kuongeza gharama za pembejeo kwa lengo la kuibia Serikali na kisha kugawana fedha. “Sasa Serikali haiwezi kulipa madeni ya kutengenezwa bali tutawalipa stahili zenu baada ya uhakiki kukamilika kama nilivyosema awali,”.
  Waziri Mkuu ameongeza mawakala wa pembejeo waliwasilisha Serikali deni la sh. bilioni 65.4 kwa huduma waliyoitoa katika mikoa 25 ambapo Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imekamilisha uhakiki wa madeni hayo kwa mikoa 10 ya Morogoro, Iringa, Njombe, Ruvuma, Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma, Kilimanjaro na Arusha ambayo madeni yake ni asilimia 70 ya madeni yote.
  Amesema ripoti ya uhakiki wa mikoa nane kati ya 10 imetoka (imebaki Katavi na Kigoma) na kubainisha kuwa mikoa hiyo inadai sh. bilioni 36 kati ya hizo sh. bilioni 11 bado zinaendelea kuhakikiwa, sh. bilioni 14 zimekataliwa hivyo siyo madeni halali, sh. bilioni 8.2 ndiyo deni halali na sh. bilioni 2.3 zinachungizwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
  Waziri Mkuu amesema uhakiki wa madeni kwa mikoa 15 iliyobakia ambayo madeni yake ni asilimia 30 unaendelea ambapo amewasihi mawakala hao kuwa wavumilivu katika kipindi ambacho Serikali inafanya uhakiki kwa kuwa inataka itende haki kwa kila mtu kulipwa deni lake kwa kiwango kinachostahili na watakaobainika kufanya udanganyifu watachukuliwa hatua za kisheria.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S.L.P 980, DODOMA

  JUMATATU, APRILI 10, 2017.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Bw.Alvero Rodriguez Mratibu wa Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini pia Mwaklilishi Mkaazi wa Shirika la Maendeleo la Umoaja wa Mataifa (UNDP) Nchini Tanzania akiongoza Ujumbe wa Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanyia kazi zake Nchini walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe wa Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanyia kazi zake Nchini ukiongozwa na Bw.Alvero Rodriguez Mratibu wa Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini pia Mwaklilishi Mkaazi wa Shirika la Maendeleo la Umoaja wa Mataifa (UNDP) Nchini Tanzania walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.(Piccha na Ikulu.)

  0 0

   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali(hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kueleza mipango mbalimbali ya jeshi hilo ikiwemo uzinduzi wa klabu katika shule za sekondari nchini, zitakazotoa elimu ya uzimaji moto kwa wanafunzi. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(Maelezo), jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Afisa Habari Mwandamizi, Casmir Ndambalilo.
   Mmoja wa waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa kuelezea mipango mbalimbali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  ikiwemo uzinduzi wa klabu  katika shule za sekondari, zitakazotoa elimu ya uzimaji moto kwa wanafunzi, akiuliza swali kwa Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye(hayupo pichani), wakati wa mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(Maelezo), jijini Dar es Salaam leo.
  Waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa kuelezea mipango mbalimbali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  ikiwemo uzinduzi wa klabu  katika shule za sekondari nchini, zitakazotoa elimu ya uzimaji moto kwa wanafunzi, wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye  wakati wa mkutano huo uliofanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari(Maelezo), jijini Dar es Salaam leo.Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  BARAZA la Uongozi la Dini na Amani Tanzania  (IRCPT), limesema ipo haja mchakato wa Katiba Inayopendekezwa kufikia tamati kwa kuwa ina mambo ya msingi kwa Watanzania.


  Mkurugenzi wa Baraza hilo, Mchungaji Thomas  Godda amesema ni vema viongozi wa dini  wakatimiza wajibu wao  kwa kuihamasisha  Serikali imalize mchakato huo sanjari na kuhamasisha wananchi kusoma Katiba iliyopo ili kuwajengea uelewa mpana.


  Ametoa kauli hiyo leo Dar es Salaam kwenye semina ya siku mbili ya kuhamasisha uhiishaji wa Katiba Mpya kwa viongozi wa dini inayoendelea kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam ambayo imeandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC). 

  Aliongeza kuwa viongozi wa dini si wanaharakati bali ni watu wanaotoa uamuzi wao kwa hekima huku wakiaminiwa na wafuasi wao wakiwemo viongozi wa serikali.
   Mkurugenzi wa Baraza la Dini na Amani Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Godda, akihutubia wakati akifungua semina ya siku mbili ya viongozi wa dini kuhamasisha uhiishaji wa katiba mpya inayoendelea Hoteli ya Golden Tulip Posta jijini Dar es Salaam leo. Semina hiyo imeandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
  Mwenyekiti wa Taifa wa Wanawake wa Baraza la Kiislam Tanzania (Bakwata), Shamim Khan (kulia), akizungumza katika semina ya siku mbili ya viongozi wa dini kuhamasisha uhiishaji wa Katiba mpya iliyofanyika Dar es Salaam leo. Semina hiyo imeandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
   Semina ikiendelea.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Kwenye muungano huo ambao unaitwa Taifa Moja, makampuni matatu makubwa ya kutoa huduma za simu za mkononi ya Tigo Tanzania, Airtel Tanzania na Zantel, wateja wanaweza kutuma pesa na kupokea kutoka kwenye moja ya mitandao hiyo kwa gharama zile zile.

   Hapo awali, kutuma pesa au kupokea pesa kutoka mtandao tofauti mteja alikuwa akipokea ujumbe mfupi ambao ilikuwa ni lazima apeleke kwa wakala wa mtandao ambao amepokea fedha kutoka na ilikuwa izizidi siku saba tofauti na hapo fedha hiyo ilikuwa inarudi kwa aliyetuma. 

  Kwa huduma hii, mteja anapaswa kuchangia huduma ya kutuma pesa kutoka kwa menu ya kawaida, halafu anachangua kutuma pesa kwenda mitando mingine. 

  Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa kutembelea watumiaji wa huduma za kutuma na kupokea pesa, Meneja wa Airtel Money kutoka kampuni ya Airtel Tanzania Moses Alphonce alisema kupitia muungano wa Taifa Moja wameweza kuwafanya wateja wapate njia rahisi ya kutuma na kupokea fedha.

  Tunajua hapo zamani kuna baadhi ya wateja walikuwa wanapata wakati mgumu linapokuja suala la kutuma na kupokea fedha. Ilikuwa aidha upokee fedha kwa ujumbe mfupi au uwe na laini ya simu zaidi ya moja. Ukipokea fedha kwa ujumbe na kwa bahati mbaya ukaufuta ilikuwa inamaanisha fedha imepotea, alisema Alphonce. 
  Meneja wa Airtel Money kutoka kampuni ya Airtel Tanzania Moses Alphonce akitoa elimu kwa mmoja wa watumiaji wamitandano ya simu kwa namna Makampuni ya simu za mikononi nchini yameungana kwa kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha kwenda mitandao yeyeto nchini kwa kiwango cha gharama ile ile.
  Makampuni ya simu za mikononi nchini yameungana kwa kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha kwenda mitandao yoyote nchini kwa kiwango cha gharama ile ile.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  UPATIKANAJI wa huduma za Benki ya NMB umezidi kuboreshwa na sasa umesogezwa zaidi mtaani kwako. Mteja wa NMB na asiyekuwa mteja kupitia huduma ya NMB Wakala sasa anaweza kuweka kutoa fedha na hata kulipia huduma mbalimbali akiwa mtaani kwake bila ya uhitaji wa kufika katika tawi la benki ya NMB. 

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari alipokuwa akitambulisha huduma hiyo iliyoboreshwa zaidi, Mkuu wa Idara ya Huduma Mbadala za Kibenki wa NMB, George Kivaria alisema kuboreshwa kwa huduma hiyo sasa kunawawezesha wateja kupata huduma za benki hiyo kwa haraka na kwa usalama na uhakika popote walipo.

  Alisema huduma hiyo pia inamwezesha mteja wa NMB kuweza kuweka fedha, kutoa, kujua salio lake kwa gharama nafuu zaidi, huku ikitolewa na mawakala zaidi ya 2000 ambao wanapatikana maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo maeneo ya vijijini. 

  Alisema lengo la NMB ni kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja ili kurahisisha upatikanaji wa huduma zake tena kwa gharama nafuu. Alisema huduma zingine ambazo wateja wengine hata wasiokuwa na akaunti za NMB wanaweza kufanya kwa mawakala hao ni pamoja na kulipa ada za shule, kulipia tozo za luku, ving'amuzi, malipo ya TRA, leseni na bili za maji.
  Meneja Uwakala wa Benki ya NMB, James Wanyama (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) walipokuwa wakizinduwa huduma za NMB Wakala zilizoboreshwa zaidi zenye gharama nafuu. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Huduma Mbadala za Kibenki wa NMB, George Kivaria. Kwa huduma hizo mteja wa NMB anaweza kuweka na kutoa fedha mtaani kwake, kuangalia salio na hata kufanya malipo ya tozo mbalimbali akiwa katika mawakala wa NMB popote alipo.
  Mkuu wa Idara ya Huduma Mbadala za Kibenki wa NMB, George Kivaria (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizinduwa huduma za NMB Wakala zilizoboreshwa zaidi. Kulia ni Meneja Uwakala wa Benki ya NMB, James Wanyama.

  0 0

  Serikali ya awamu ya tano nchini imezindua rasmi usambazaji wa vifaa vya hospitali kwa halmashauri zote nchini  katika kutekeleza mkakati wa kuboresha huduma za afya nchini kwa kuhakikisha wananchoi wanapata huduma kwa kiwango stahiki.

  Akizindua usambazaji huo  leo wilayani Kongwa, Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema serikali imetekeleza ahadi iliyotoa kwa wananchi ambapo serikali inawekeza katika afya ya wananchi  hivyo kuweza kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

  Akizungumza kwenye hadhara ya wanachi wa Wilaya ya Kongwa,Waziri Ummy alisema serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwa baadhi ya maeneo ikiwemo ya upatikanaji wa dawa ambapo bajeti ya dawa imeongezeka kutoka shilingi bilioni 31 mwaka 2015/16 hadi shilingi bilioni 251 mwaka 2016/17.

  “Hatua hii imeleta mapinduzi makubwa katika upatikanaji wa dawa,vifaa na vifaa tiba kwenye vituo vya Umma vya kutolea huduma za afya,hivyo wanaomba wananchi kuhakikisha mnafika kwnye vituo vya kutolea huduma za afya ili kupata matibabu sahihi”.

  Aidha, Waziri Ummy alisema kufuatia ahadi ya Mhe. Rais ya kununua na kusambaza vitanda kwenye vituo vya Umma ,Wizara yake kwa bajeti ya mwaka 2016/17 ilitenga kiasi cha shilingi biliuoni 4 za kuwezesha kununua pamoja na kusambaza  vifaa hivyo kwa halmashauri 184 nchini.

  Alivitaja vifaa vilivyonunuliwa na kuvikabidhi kwa Mhe. Job Ndungai (Mb), Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungazo wa Tanzania  Mhe. John Ndugai  ni pamoja na  vitanda vya hospitali (20),vitanda vya kujifungulia wajawazito (5), magodoro (25) na mashuka (50).

  Vifaa vya Hospitali vitakavyopasambazwa kwenye Halimashauri zote 184 nchini ni pamoja na vitanda vya hHospitalini 3,680; vitanda vya kujifungulia akinamama wajawazito 920; magodoro 4,600; na mashuka 9,200. Thamani ya vifaa hivi ni shilingi bilioni 2,933, 125,600. Zoezi la kugawa vifaa hivi linatarajiwa kukamilika kabla ya Juni 30, 2107.

  Akipokea vifaa hivyo, Mhe. Ndugai ameishukuru Serikali kwa msaada wa vifaa vilivyotolewa kwa Hospitali na vituo vya Afya katika mkoa wa Dodoma ikiwemo Halmashauri Kongwa. Vifaa hivyo vitaboresha afya ya wananchi wa jimbo la Kongwa na maeneo mengine nchini na hivyo kusaidia kuwawezesha wananchi kukutumia mudao wao mwingi katika shughuli za kiuchumi.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amezindua Kikosi Kazi Maalum kwa ajili ya kuokoa mfumo wa ikolojia katika bonde la mto Ruaha Mkuu ambalo lipo katika hatari ya kutoweka kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea kwenye bonde hilo kutokana na shughuli za Kibinadamu.

  Kikosi kazi hicho ambacho kimezinduliwa mjini Iringa kitafanya kazi chini ya usimamizi wa Makatibu Tawala wa mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe kwa kuchambua kwa kina tafiti na matokeo ya tafiti hizo ili kupendekeza hatua za haraka zitakazochukuliwa katika kudhibiti uharibifu kwenye bonde hilo ambao umechangia kupungua kwa maji kwenye mto Ruaha Mkuu.

  Akizindua Kikosi kazi hicho mjini Iringa ambacho ambacho kimehudhuriwa na Mawaziri kutoka Wizara Tano, Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema ofisi yake imeamua kuunda kikosi hizo ili kuokoa hali mbaya ya uharibifu wa mazingira unaoendelea kufanyika hivi sasa katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu.

  Amesema kutokana hali kuwa tete kwenye bonde hilo ndio maana hatua ya haraka na za dharura zimechukuliwa na ofisi yake kwa kuunda kikosi kazi hicho ambacho kinaundwa na wataalamu mbalimbali wa serikali, washirika wa maendeleo ambao wana uwezo wa kufanya maamuzi ya kisera na kiutendaji ili kutoa suluhu ya kudumu ya kuhifadhi bonde hilo.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiongoza mkutano wa uzinduzi wa kikosi kazi cha kuokoa mfumo-ikolojia wa bonde la mto Ruaha Mkuu uliofayika kwenye ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa. 
  Mhe. January Makamba akithutubia juu ya umuhimu wa mto Ruaha ambao unahudumia watu zaidi ya milioni 6 na namna ambavyo umeathirika na shughuli za binadamu kwenye warsha ya uzinduzi wa kikosi kazi cha kuokoa mfumo- ikolojia wa bonde la mto Ruaha Mkuu uliofayika kwenye ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi (MB) Mhe. Wiliam Lukuvi (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Amina  Masenza wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kikosi kazi cha kuokoa mfumo-ikolojia wa bonde la mto Ruaha Mkuu uliofayika kwenye ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa.  Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Tanzania Mhandisi Gerson Lwenge akihutubia wakati wa warsha ya uzinduzi wa kikosi kazi cha kokoa mfumo -ikolojia wa bonde la mto Ruaha mkuu.


  0 0

    Mkuu wa kitengo Cha masoko na mahusiano ya Benki ya TIB CBL ,  Bi Theresia Soka akiwasilisha mada juu ya huduma zinazopatikana katika benki hiyo kwa washiriki wa jukwaa la biashara lililofanyika katika ukumbi wa Rock City jijini Mwanza.

  Jukwaa hili limehusisha wadau mbalimbali ili kujadili na kutambua fursa mbalimbali zinazopatikana katika mkoa wa Mwanza.
  Wadau mbalimbali wa kiwa kwenye picha ya pamoja walioshiriki kwenye jukwaa la biashara lililofanyika katika ukumbi wa Rock City jijini Mwanza.

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  WAJUMBE wa kamati ya Utendaji wa Yanga wameweka wazi maamuzi yao ya kutakuwa na imani na maamuzi na utendaji wa kamati ya saa 72 kwa rufaa mbalimbali zilizowakilishwa wao kubwa ikiwa rufaa ya Simba SC kwa Kagera Sugar.

  Viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Yanga Mhandisi Paul Malume , wamesema hawana imani na kamati hiyo na kinachoendelea ni kutaka kuvuruga utulivu wa ligi kuu na soka kiujumla .

  Mjumbe wa kamati ya Utendaji Salumu Mkemi mjumbe kamati kuu Yanga SC amesema kamati hiyo haina usawa pia ni kamati inayoundwa na zaidi ya wanachama 6 wandamizi wa Simba SC na wao kama Yanga wakiwa na wanachama wawili tu.

  Mkemi amesema kuwa tayari wameziangazia harufu na fununu ya kubadilishwa kwa ripoti za michezo ambayo Simba wanasema mlinzi wa Kagera Mohamedi Fakhi alipata kadi 3 za njano .

  " kamati hii imechelewa kutoa maamuzi kwa kuandaa ripoti za uongo za michezo dhidi ya Fakhi pia tuna taarifa za kughushiwa email na nyaraka zingine ili kuipa alama tatu Simba SC yenye zaidi ya wajumbe 6 katika kamati hiyo sisi kama Yanga tumeanza uchunguzi wetu na kutoa taarifa kwa vyombo husika vya dola pia maamuzi yoyote ya kuibeba Simba tutakwenda mahakamani licha ya sheria za FIFA kukataza hivyo kama hawataki tufike huko lazima haki itendeke. .." alieleza mjumbe huyo.

  Mkemi amesema kuwa tayari wameshavijulisha vyombo husika yaani Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na watu wa makosa ya mtandao (cyber crime) na Mamlaka ya mawasiliano Nchini (TCRA)  juu ya uchunguzi wa mawasilano ya waamuzi wote waliosika na kutajwa kwenye rufaa hiyo.

  " tuache kumtafuta bingwa wa mezani na sisi tumefungwa karibu mechi tatu na hatujalilia alama za mezani kwanini wao,  mbona jana wamecheza mchezo mzuri mwishoni na kupata ushindi wa jioni dhidi ya Mbao na hakuna kelele tena na tunawapongeza kwa come back ile . Hiki ndicho mashabiki wa timu hizi wanakitaka . Ushindi wa uwanjani sio figisu . "


  Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga Salum Mkemi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamkom lao juu ya maamuzi na utendaji wa kmati ya saa 72 dhidi ya rufaa ya timu ya Simba dhidi ya Kagera. Kushoto ni Katibu  Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa.

  Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga Salum Mkemi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamkom lao juu ya maamuzi na utendaji wa kmati ya saa 72 dhidi ya rufaa ya timu ya Simba dhidi ya Kagera. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga, Siza Lyimo, shoto ni Katibu  Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa na Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Yanga Mhandisi Paul Malume .


  0 0

  Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

  Serikali kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeandaa Rasimu ya Muswada wa Sheria itakayoweka bayana taratibu na mfumo wa usimamizi na udhibiti wa bishara ya chuma chakavu katika hatua mbalimbali za uzalishaji, ukusanyaji, usambazaji, uuzaji na uyeyushaji wake kwa kuzingatia uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwa manufaa ya Taifa.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.

  “Biashara ya Chuma chakavu imeshamiri hapa nchini na duniani kwa ujumla,na hili limetokana na mahitaji ya vyuma chakavu ambapo kumetumiwa na wahalifu kuaharibu miundombinu iliyojengwa kwa vyuma kwa nia ya kupata chuma ili waiuze kama chuma chakavu”Alisema Mwijage.

  Amesema ili kukabiliana na hujuma hizi Mamlaka husika zikiwemo TANESCO, TANROADS  na  RAHACO wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na jeshi la Polisi ikiwemo kutumia walinzi wa Taasisi husika ili kulinda rasilimali hizo.

  Amesisitiza kuwa Muswada huu umeweka wazi na bayana adhabu itakayotolewa kwa mtu atakayebainika kuharibu miundombinu.
  Aidha Mhe.Mwijage ametoa wito kwa watanzania kutoa taarifa pindi waonapo mtu anayehujumu  miundombinu kwa namna yote ile.

  “Natoa wito kwa wenye viwanda na wafanyabiashara wa vyuma chakavu jiepusheni na ununuzi wa vyuma  ambavyo asili yake ina mashaka na tutaharakisha sheria  hii ili kutatua tatizo hili”Aliongeza Mwijage.

  Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.

older | 1 | .... | 1643 | 1644 | (Page 1645) | 1646 | 1647 | .... | 3278 | newer