Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1642 | 1643 | (Page 1644) | 1645 | 1646 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Abdalah Pazi maarufu kama Dullah Mbabe (kushoto) akitunishiana Misuli na mpinzani wake Abdi  Kivu anayataraji kuzichapa nae kesho katika ukumbi wa Mwananyamala Mwinjuma Kinondoni katika pambano lisilokuwa na ubingwa.
   Khalid Chokoraa akiwa na Mpinzani wake wakitunishiana misuli baada ya kumaliza kupima uzito kwa ajili ya pambano la kesho. katikati ni Kocha wa Masumbwi nchini, Rajab Mhamila a.k.a Super D.
   Mabondia Chipukizi  wakitambia kwa ajili ya pambano la kesho
   Mashabiki wa Abdi Kivu wakiwa wanaimba mara baada ya bondia wao kumaliza kupima uzito
  Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Abdalah Pazi maarufu kama Dullah Mbabe akiwa na Mashabikiwa wake akiondoka ndani ya ukumbi wa Mwananyamala Mwinjuma mara baada ya kumaliza kupima uzito.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Taraba amewataka wananchi wilayani humo kuchukua tahadhari na baa la ndege waharibifu wa mazao mashambani aina ya kwelea. Amesema tayari baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo yamevamiwa na ndege hao waharibifu wa mazao yakiwemo ya mtama, uwele, alizeti na mahindi yanayoanza kustawi.

  Taraba ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama alitoa tahadhari hiyo kwa wananchi mwishoni mwa wiki alipofanya ziara ya katika vijiji vya kata sita zilizopo wilayani humo. Akiwa amembatana na Ofisa Kilimo, Ushirika na Umwagiliaji Wilaya, George Kessy na Ofisa Nyuki na Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya (OCD), Emmanuel Gariyamoshi aliwatembelea wananchi wa kata za Uchunga, Mwadui Lohumbo, Idukilo, Ukenyenge, Mwamasele na Mwaweja.

  Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi kulinda mashamba yao na kuwafukuza ndege hao wakati Serikali inaendelea kuchukua hatua za haraka ili kuwasaidia. Alisema tayari wilaya imeagiza ndege maalumu kwa ajili ya kumwaga sumu kwenye mazalia ya ndege hao ili wasiongezeke na kuleta madhara zaidi kwa mashamba ya wananchi.

  “Serikali haijawatupa nawaomba wananchi tukae mashambani mwetu tulinde na kuwafukuza ndege hao wasile mazao yetu kwani tutapata hasara kubwa, hatujui hao kwelea kwelea watakuja lini, na hatujui hiyo ndege itakuja lini,” alisisitiza.

  Aidha, aliwataka wananchi kuvuna haraka iwezekanavyo mazao ambayo tayari yamekomaa ili kutowapa mwanya ndege hao kufanya uharibifu wao na hivyo kuwapa hasara wakulima. Aliwataka wakulima wasihadaiwe na kuuza mazao yote kwa wafanyabiashara hali inayoweza kuwasababishia kukosa chakula baadaye na kulazimika kununua chakula kwa bei ya juu. Aliwaonya watu wanaofanya hivyo kwani huwaacha nyuma wakulima waliotoka jasho kulima mazao wakati wao wakineemeka kwa kuyauza mazao hayo kwa bei ya juu na kupata faida.

  Kwa upande wake, Kessy alisema idara yake inawasisitizia wananchi wajenge utamaduni wa kuhifadhi chakula cha kutosha ghalani ili kiwasaidia katika siku zijazo na kuuza tu ile ziada inayobaki baada ya kutosheka. Aliwapa mbinu za kufukuza kwelea kwelea kwa kuweka vitambaa mithili ya bendera, sanamu za watu na kupiga madebe ili kuwafukuza ndege hao ili wapiti mbali ya mashamba wasiweze kufanya uharibu.
  Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (katikati) akikagua mashamba katika vijiji vya Kata ya Mwadui Lohumbo. Wengine pichani kushoto ni Mkuu wa Polisi Kishapu, Emmanuel Gariyamosho na Afisa Nyuki, Revocatus Mboya.
  Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akiwapungia mikono wakulima waliokuwa wakiendelea na shughuli shambani katika Kata ya Mwadui Lohumbo.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa kofia) akifanya mazoezi na vikundi vya michezo kutoka Zanzibar na Tanzania Bara kabla ya kufungua Bonanza kubwa la michezo lililofanyika katika viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi, Zanzibar. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka wanamichezo hao pamoja na wananchi hapa nchini kwa ujumla, kudumisha mazoezi zaidi ili waweza kupata afya bora.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akifanya mazoezi na vikundi vya michezo kutoka Zanzibar na Tanzania Bara kabla ya kufungua Bonanza kubwa la michezo lililofanyika katika viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi, Zanzibar. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka wanamichezo hao pamoja na wananchi hapa nchini kwa ujumla, kudumisha mazoezi zaidi ili waweza kupata afya bora.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wanamichezo wa vikundi mbalimbali kutoka Zanzibar na Tanzania Bara mara baada kiongozi huyo kufanya mazoezi ya viungo na wanamichezo hao katika Viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi, Zanzibar. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka wanamichezo hao pamoja na wananchi hapa nchini kwa ujumla, kudumisha mazoezi zaidi ili waweza kupata afya bora.
  Msoma Risala wa Kikundi cha Michezo cha Island Erercise Club cha mjini Unguja, Zanzibar, Ally Mussa, ambacho ndio waratibu wa Bonanza la Vikundi vya Michezo kutoka Visiwani humo pamoja na Tanzania Bara, akitoa historia fupi ya kikundi hicho pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili, kabla ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) kukariboishwa kuzungumza na mamia ya wanamichezo ambao walifanya mazoezi mbalimbali katika Viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi, Zanzibar leo. Wapili kulia ni Bregedi Kamanda KV101 kambi ya nyuki, Kanali Fadhili Nonda.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiumwagilia maji mti wa kumbukumbu alioupanda katika eneo la Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi, Zanzibar, mara baada ya kufanya mazoezi ya viungo katika Bonanza la Vikundi vya Michezo kutoka visiwani humo pamoja na Tanzania Bara. Masauni aliwakilisha Makamu wa Rais, Sami Suluhu katika sherehe hiyo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza Kampeni ya kunusuru Bonde la Mto Ruaha Mkuu lililopo Iringa kutokana uharibifu mkubwa unaendelea, huku akiambatana na Mawaziri watano ambao watasaidia kuokoa uharibifu wa Mazingira.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Januari Makamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo Jijini Dar es salaam, amesema kuwa Ofisi hiyo imeanzisha Kampeni hiyo kwa sababu Hifadhi ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu ni kubwa kuliko yote hapa Afrika Mashariki.

  Amesema kuwa uharibifu unafanywa kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu katika Bonde hilo unasababisha kukauka kwa Mto Ruaha ambao ni tegemezi katika nyanja za kiuchumi.

  Aidha, Makamba amewataja Mawaziri watakaoongozana na Makamu wa Rais kuwa ni pamoja na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge, Waziri wa Ardhi, William Lukuvi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Jumanne Maghembe, Waziri wa Kilimo, Charles Tizeba.

  Vile vile, ameongeza kuwa hali ya mazingira kwa sasa ni mbaya sana kwenye bonde hilo kwani ukifika wakati wa kiangazi mto huo wa Ruaha Mkuu hautirirshi tena maji kama ilivyokuwa zamani.

  "Hali hii inasababisha kupungua kwa watalii, shughuli za kiuchumi na uzalishaji wa umeme ambao unamrahishia mwananchi wa kawaida kupata umema nafuu, pia uhalibifu huu wa Mazingira unahatarisha maisha ya wanyama,"amesema Makamba.

  Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi wote kutunza vyanzo vya maji, Mazingira ili viweze kuwaletea manufaa kwa sasa na vizazi vijavyo.​
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba  akizungumza na Waandishi wa habari ofsini kwake mapema leo juu ziara ya Makamu wa Rais nchini Mama Samia Suluhu Hassan katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu linakabiliwa na uharibifu mkubwa wa mazingira kushoto Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustin Kamuzora
   Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira wa Ofisi hiyo Bw. Richard Muyungi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari  juu ya athari za kuchepusha mto
   Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakimskiliza waziri makamba

  0 0

      Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt. Julius Mwaisalage misaada ambayo ametoa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa  wagonjwa waliolazwa katika Taasisi hiyo jijini Dar es salaam.
     Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi zawadi kwa mmoja wa wagonjwa katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na   wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya saratani ya Ocean Road jijini Dar es salaam.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiomba dua na baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya saratani ya Ocean Road jijini Dar es salaam.
     Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt. Julius Mwaisalage misaada ambayo ametoa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa  wagonjwa waliolazwa katika Taasisi hiyo jijini Dar es salaam.
     Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi msaadammoja wa wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya saratani ya Ocean Road jijini Dar es salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
  0 0

  BONANZA la Michezo la siku sita litakalohusisha walimu wa michezo na wadau mbalimbali linatarajiwa kufanyika Mei 20 mwaka huu kwenye viwanja vya Halmashauri ya Korogwe .

  Bonanza hilo limefadhiliwa na asasi ya Inuka wenye lengo la kupiga vita madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo na nidhamu kwa jamii 

  Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mratibu wa Inuka Kanda ya Ziwa, Gaudance Msuya alisema lengo kubwa litakuwa kuiamsha jamii na kupenda kushiriki kwenye michezo ili kuimarisha afya zao.

  Alisema katika bonanza hilo michezo itakayokuwepo ni mpira wa miguu,riadhaa ,mpira wa pete,kuvuta kamba na kukimbiza kuku na kutembea na magunia.

  Aidha alisema washindi kwenye michezo hiyo wata zawadiwa zawadi mbalimbali ambapo zaidi ya milioni mbili zimetengwa kwa ajili ya zawadi kwa washiriki watakofanya vizuri.

  “Ndugu zangu watu wa Korogwe hii ni fursa ya kipekee hivyo ninawaomba mjitokeze kwa wingi kushiriki kwenye bonanza hili ambalo litakuwa na faida kubwa licha ya kuwepo kwa zawadi hizo”Alisema.

  Hata hivyo alisema kwa washiriki ambao wangependa kushiriki wawasiliane na Ofisa Michezo wilaya ya Korogwe ili kuweza kuthibitisha ushiriki wao.

  Mratibu huyo aliyataka mashirika mbalimbali ikiwemo mabenki kuona namna ya kuunga mkono jambo hilo kwa kuona namna ya kufadhili ambapo wanaweza kuwasiliana na mratibu huyo kwa simu namna 0683122320/0683122340.

  0 0

  Na Mwandishi wetu, Vijimambo Blog

  Nianze kwa kukusabahi wewe msomaji wangu, nikitumaini upo mzima wa afya kwa uwezo wake Mola.

  Nakukaribisha tena katika makala nyingine, na hii ya leo itazungumzia suala la uraia pacha. Hili ni suala ambalo kwa mtazamo wangu, Watanzania waliochukua uraia wa nchi nyingine wamekatishwa tamaa na namna serikali ya nchi yao inavyolipuuzia, licha ya kuwa ni suala muhimu na lenye faida kubwa kwa taifa letu.

  Viongozi wengi sio kwamba hawaelewi umuhimu wake bali wanafanya jitihada za makusudi za kuwatia uoga na kukataa kuwaelimisha ndugu zetu WaTanzania juu ya faida ambazo nchi itapata kutokana na ndugu zao ambao waamehamishia maisha na kuchukua uraia nje ya nchi. Kuna sababu mbalimbali za waTanzania hawa kufikia maamuzi haya, lakini sote tunatambua kwamba sababu kuu ni moja tu, kutafuta maisha, kitu ambacho hakina tofauti na mtu aliyetoka kijijini na kuhamia mjini.

  Viongozi wetu wamekua mstari wa mbele kuwaita WaTanzania wenzao waliokwenda ughaibuni kutafuata maisha, na wengine kulazimika kuchukua ukaazi wa huko kutokana na kubanwa na sheria kuwa WAMEJILIPUA, ilhali tunatambua kuwa lengo ni kuweza kurejesha matunda ya ukaazi huo nchini Tanzania.

  Neno kujilipua tafsiri yake hasa ni mtu aliyejifunga bomu na baadae kujilipua ili afe. Hiyo ndio maana yake halisi na kwa viongozi wetu kufananisha mtu aliyebadili uraia na mfu, inasikitisha.
  Binafsi napinga kuhusishwa kwa tafsiri hiyo na kinachofanywa na WaTanzania sisi, kwa sababu mtu aliyekufa hawezi kutoa huduma yeyote kwa jamii. Watanzania waliobadili uraia wanasaidia sana ndugu zao nyumbani na kuwakumbusha tu viongozi ni kwamba, uraia anaopewa mTanzania ni wa karatasi kamwe hautaweza kufuta nchi aliyozaliwa.

  Katika uongozi wa awamu ya Nne Rais mstaafu Mhe. Jakaya Kikwete alishawahi kutamka na kutoa mwamko wa WaTanzania waliopo nje warudi nyumbani kuwekeza na hii ni kutambua umuhimu wake na sio kwamba alikua haelewi sheria inasemaje kwa mTanzania anayebadili uraia. Naamini Rais alisema vile kwa kuwa aliona umuhimu wa WaTanzania wanaoishi nje ya Tanzania na kwamba alijua wanaweza kutumia ujuzi na maarifa ya Dunia ya kwanza katika kuletea maendeleo ya nchi yetu.

  Rais mstaafu Kikwete alijitahidi kukutana na WaTanzania kila nchi aliyoenda na kuwapa ujumbe wa kutosahau kuwekeza nyumbani na wakati Fulani alinukuliwa akisema " WaTanzania Diaspora na WaTanzania mliobadili uraia wote ni jamii moja, rudini nyumbani mkawekeze. Ni fedheha unakaa huku ukirudi unafikia hoteli kule ni nyumbani hata kama huna fedha nyingi za kuwekeza, jenga hata kibanda"

  WaTanzania wengi waliitikia wito huo na kuanza kupeleka vitega uchumi nyumbani na wengine kujenga nyumba pasipo kufikiria ipo siku wataitwa WaTanzania waliojilipua au kuukana uraia wa nchi yao. Kwa mimi binafsi, meneno hayo hayapaswi kutumiwa kwani yanapandikiza na kujenga chembechembe za chuki na WaTanzania wengine kuona kwamba WaTanzania wenzetu kwanza hawaitaki nchi yao na sasa wanarudi kuomba uraia pacha kusudi wale huku na kule.

  Binafsi naamini kuna faida kubwa sana za raia wa nchi husika walio nje ya nchi kushiriki maendeleo kwa uhuru na bila hofu. Nchi kama Kenya, Sudan, Ethiopia na nyingine barani Afrika ni mfano tosha. Na naamini faida za hili ni kati ya sababu zilizopelekea nchi karibia zote jirani zinazotuzunguka kuruhusu uraia pacha. Kwanini inakuwa ngumu kwetu sisi ambao tunaungana na nchi hizo lakini tunatengana na wazawa wetu? Kwani tunaona ugumu gani?

  Wenzetu Kenya wamejiwekea lengo la mwaka 2017- 2018 wakusanye kodi ya Kshs 300 bilioni ambayo ni sawa na $3 bilioni kutoka kwenye uwekezaji unaofanywa na Diaspora wa Kenya nchini humo. Serikali yetu ikiamua kufuatilia fedha zinazoingia Tanzania kutoka Diaspora na kuzitoza kodi ambayo kodi hiyo inaweza kutumika kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.

  Sasa wakati umefika kwa viongozi kuwaelimisha au kuwaambia wananchi ukweli kuhusu uraia pacha na faida zake, badala ya kuwapotosha na kuwatisha kwa kauli kama “tukiruhusu uraia pacha siku moja nchi nii itakuja kutawaliwa na Rais mzungu"?
  Kwanini wananchi pia wasiambiwe “tukiruhusu uraia pacha nchini itapata Madaktari, Wahandisi, Wawekejazi WaTanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo wanamichezo wa KiTanzania watakaoamua kuja kuiwakilisha nchi yao katika mshindano ya kimataifa na hatimae kuliletea Taifa sifa”?.

  Pamoja na kuchukua uraia wa nchini nchingine mbona inapotokea hitaji la misaada, WaTanzania hao hao wanaowaitwa wameukana uraia wanaipeleka Tanzania, na viongozi wanaipokea kwa mikono miwili?

  Misaada mingi itolewayo na diaspora kama vile Madaktari, vifaa mbalimbali vya mahospitalini, mashuleni mitambo ya kuchimbia visima na kadha wa kadha yote ni kuonyesha mapenzi makubwa waliyonayo na nchi yao walikozaliwa.

  Hizo ni faida chache mbali na fedha zinazoingizwa nchini kutoka Diaspora ambazo hazina idadi kwasababu hakuna ufuatiliaji wa fedha hizo.

  Tunaomba Viongozi wetu mlifikirie upya swala hili kwa faida ya Taifa letu na kwa mwendo kasi wa Rais wetu Mhe. John Pombe Magufuli ingekua vizuri kuwashirikisha WaTanzania nje ya nchi ili kusaidiana na ndugu zetu nyumbani ili wachangie nguvu ya kuleta maendeleo ya nchi kwa kasi zaidi.

  Hainingii akilini unamyang'anya uraia mTanzania mwenzako aliyechukua uraia nchi nyingine hafafu unampa uraia mwananchi wa nchi ngingine hii sio sawa hata kidogo inabdi tukae chini na kuliangalia upya swala hili. Hii sheria ilitungwa 1995 ya Immigration Act and Citizenship Act  hii ni 2017 ni zaidi ya miaka 10 tangia kutungwa kwke tunaomba iangaliwe upya iendane na muda uliopo kwa manufaa ya nchi yetu.

  Kwa pamoja, walio nyumbani na ugenini, tutaijenga Tanzania njema, Tanzania bora, Tanzania ya viwanda ambayo serikali inaitaka, na wazawa wake walio nje wanaishi na kutumika vilipo viwanda

  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Diaspora

  0 0

  Meneja wa SIDO Mkoa wa Mtwara, ndugu Joel Chidabwa akiwatunukia vyeti wahitimu wa mafunzo ya ujasiriamali na matumizi ya vipodozi kwa wanawake wa mkoa wa Mtwara. Ndg. Chidabwa alifunga rasmi mafunzo hayo ya wiki mbili yaliyoandaliwa na kutolewa bure na taasisi ya Manjano Foundation mkoani Mtwara.Katika mafunzo hayo ya ujarisiamali na matumizi sahihi ya vipodozi, yalitolewa kwa wanawake 30 walionufaika na mafunzo hayo kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano vilivyo dhaminiwa na kampuni ya Shear illusions. 

  Mafunzo hayo yaliendeshwa na wataalamu wa mambo ya biashara wakishirikiana na maofisa wa taasisi ya Manjano. Lengo ya mafunzo hayo ni kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuweza kujiajiri na kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kujikita katika tasnia ya urembo na vipodozi. Mafunzo hayo yameshafanyika kwenye mikoa saba nchini, nayo ni Dar es Salaam, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Zanzibar, Dodoma na Arusha. Mpango endelevu wa taasisi ya Manjano Foundation ni kufikia mikoa 30 nchini ndani ya miaka mitano.  

  Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo hayo, taasisi ya Manjano Foundation inawaunganisha na Taasisi za Fedha zinazotoa mikopo bila riba au yenye masharti nafuu ili  waweze kupata mtaji wa kununua bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa Taasisi hiyo kwa mwaka mzima. Lengo ni kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea na kusaidia familia yake.

  Washiriki walionufaika kwenye Mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa SIDO Mkoa wa Mtwara, ndugu Joel Chidabwa.
  Wanawake wa mkoa wa Mtwara walionufaiki na mafunzo ya ujasiriamali na urembo wamemshukuru afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions na muasisi wa Taasisi ya Manjano Foundation mama Shekha Nasser kwa moyo wake wa kujitolea na kuwajali wanawake wengine hususani wakazi wa Mtwara. Wakiongea zaidi wanawake hao ambao wamepatiwa elimu ya biashara kutambua nafasi yao katika jamii inayowazunguka pamoja na namna ya kupamba maharusi, ueledi na jinsi ya kupata masoko na kuongeza mauzo kwenye biashara na matumizi sahihi ya vipodozi. Wamemshukuru mama Shekha kwa moyo wenye kuwajali na kuwabeba wanawake wenzake na kutoa elimu ya bure aliyokuwa nayo kwa wengine ili waweze nao kujiongezea kipato na kupunguza ukali wa maisha. Wameahidi kuyatumia mafunzo hayo kwa lengo la kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira kwa wanawake na pia kujiongezea kipato.

  0 0

  The President’s Manufacturer of the Year Awards (PMAYA) 2016 winners have been finalized yesterday in Dar es salaam during the prestigious awards ceremony which was graced by the Vice President of Tanzania Hon. Samia Suluhu Hassan as a chief guest.
  The event revealed the 2016 winners being Tanzania Breweries, other companies scooped the top most positions were Kioo Ltd and Mufindi Paper Mills. Others are Petrolube, Alliance Insurance Corporation, Hanspaul Automechs, Nyanza Mines Tz, Tanpak Tissues, DPI Simba, Alliance Life Assurance, Prisons Corporation Sole, Chemi Cotex Ind, Said Salim Bakhresa, Jambo Plastics, Nida Textiles, Ital shoe, Dharam Singh Hanspaul & sons and Tanelec.
  The President’s Manufacturer of the year Awards is an annual event that is organized by the Confederation of Tanzania Industries (CTI) to award the outstanding manufacturers of the preceding year. The Awards are given to companies in small, medium and large manufacturer categories that exhibit a high degree of economic impact. Bank M Tanzania plc is the main sponsor of this year’s event for a second year in a row.
  Speaking during the event, the Vice President congratulated CTI for the initiative and mostly by inviting the non members to participate this year as well as Bank M for sponsoring the event. In addition, Hon. Samia assured CTI and the stakeholders that the government is always ready to work with the private sector in order to boost the industrial sector.

  She also commented on the challenges facing the industrial sector and assured CTI that the government is working on the challenges to find out solutions ” I fully understand there are several challenges facing the industrial sector such as tax issues on raw material, infrastructure etc, but be assured that the government is working on them”, said the Vice president.

  Speaking on behalf of Bank M, the Deputy CEO Ms. Jacqueline Woiso expressed the Bank’s satisfaction to the whole process, “we congratulate the president for your efforts to boost the economy, we also congratulate CTI for this initiative, as well as the winners. PMAYA plays a central role in the economic growth of Tanzania.

  By recognizing the industrial sector contribution, we believe that they will be encouraged to do even more. By so doing, such industries will prosper increase productivity as well as its contribution to the social welfare of the people by creating more employment opportunities and most importantly boosting our economy.”

  Commenting on the event success, the CTI Executive Director, Leodeger Tenga, said the companies competing in this competition will enable the East Africans business community to expand the market space, and make the region more competitive via larger economies of scale. “Congratulations to all the winners”, Mr. Tenga said.

  Apart from Bank M, other sponsors, who have joined hands with CTI in this year’s event include GIZ, Motisun Group, Alaf, ITV, The Guardian, Nipashe, Radio One, Serena Hotel, Cocacola, Mwananchi, The Citizen, Siemens and Clouds Media.
  Bank M CEO Jacqueline Woiso receiving a trophy as the main sponsors from The Vice president of the United republic of Tanzania HE Samia Suluhu Hassan during the President's Manufacturer of the year awards ceremony held in Dsm over the weekend. Bank M sponsored the event for a second year in a row. Others from left are Minister of Industries, Trade and Investment Charles Mwijage,TPSF Chairman Reginald Mengi, CTI 2nd vice chairman Zavery Shabbir, CTI Executive Director Leodegar Tenga and Permanent Secretary Min. of Industries, Trade & Investment Dr Adelhelm Meru.

  0 0


  Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
  MVUA kubwa iliyoambata na upepo mkali,imekata mawasiliano ya miundombinu ya barabara eneo la Buyuni, na kusababisha wakazi kutoka kata ya Vigwaza na Mwavi jimbo la Chalinze,kupata shida.
  Hali hiyo inasababisha wakazi hao,kuvushwa kwa kupata msaada wa kubebwa mgongoni na shingoni kwa gharama ya sh.3,000 na 2,000 na pikipiki kupitishwa kwa sh.5,000 huku magari yakishindwa kupita kabisa.
  Baadhi ya wakazi hao,akiwemo Zaina Zuberi aliekuwa akienda Mwavi,alisema wapo katika hali ngumu.
  “Mvua hapa bado haijanyesha,maji haya yanatokea maeneo ya Msoga huko na kufika huku daraja la  Mbiki,Buyuni na kukatiza katika hii barabara,sipati picha mvua ikipiga hapa kwa mwezi huu”
  MBUNGE wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,akiangalia barabara kutoka Vigwaza-Mwavi iliyoharibika vibaya eneo la Buyuni hali inayosababisha magari kushindwa kupita.

   Mkazi wa Mwavi ,Zainab Zuberi akivushwa  kwenye maji yaliyokata barabara eneo la Buyuni,kwa kubembwa shingoni .
  Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,akizungumzia kero ya kuharibika kwa baadhi ya  miundombinu ya barabara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha,ambapo mvua iliyonyesha april 7 na 8 imesababisha kuharibu barabara ya Vigwaza-Buyuni-Mwavi na ya Milo-Kitonga-Ruvu.


  0 0
  0 0

  Leo Aprili 10 ni siku ya kuzaliwa kwa Blogger Cathbert Angelo Kajuna mmiliki wa Kajunason Blog (www.kajunason.com), ambaye ameyaandika haya katika ujumbe wake mfupi "Namshukru sana mwenyezi Mungu kwa kunilinda mpaka kufika hapa nilipo na kunipa nguvu, ujasili wa kupambana na misukosuko ya hapa na pale, hakika yeye ndiye muweza wa kila jambo.

  Natoa shukrani kubwa kwa familia yangu, ndugu, jamaa na marafiki wote ikiwa na member wa TBN members na wote waliweza kuwa nami katika safari yangu ya maisha mpaka hii leo namuomba Mwenyezi Mungu aniongezee uhai na uzima ..."

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akikabidhiwa kombe na Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Ali Mussa baada ya timu ya mpira wa miguu ya Polisi Tanzania kuchukua ubingwa katika Michezo ya Majeshi iliyomalizika hivi karibuni Visiwani Zanzibar (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi).

  0 0

   Msamalia akiipiga kibega gari iliyokuwa imezimika ghafla kwenye maji yaliyotuama katika Barabara ya Umoja wa Mataifa, Upanga jijini Dar es salaam mchana wa leo. Hali hii imefikia hivyo, kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali hapa nchini.
   Gari ikipafua maji katika Barabara ya Umoja wa Mataifa, Upanga jijini Dar es salaam mchana wa leo.
  Hivi ndivyo hali ilivyo katika Barabara ya Umoja wa Mataifa, Upanga jijini Dar es salaam mchana wa leo.

  0 0

  Kifimbo cha Malkia wa Uingereza maarufu (Qeens Baton) chatembezwa katika maeneo mbalimbali ya Daraja la Nyerere jijini Dar es salaam, Uongozi wa Shirika la taifa la Hifadhi ya Jamaii (NSSF) uliupokea msafara unaokitembeza Kifimbo hicho ambacho kinatarajiwa kuzungushwa maeneo mbalimbali ya Dar esalaam na Arusha.
  Kaimu Meneja wa Miradi wa Shirika la taifa la Hifadhi ya Jamaii (NSSF), Radhia Tambwe akiwa ameshikilia kifimbo cha Malkia baada ya msafara wa Kifimbo hicho kufanya ziara katika Daraja la Kigamboni.
  Baadhi ya wafanyakazi wa NSSF wakikitembeza kifimbo cha Malkia kitika maeneo mbalimbali ya Daraja la Nyerere.
  Baadhi ya wafanyakazi wa NSSF wakikitembeza kifimbo cha Malkia baara ya kutembezwa katika maeneo mbalimbali ya Daraja la Nyerere.


  0 0

  Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB –Richard Makungwa (kulia) akimpongeza mwenyekiti wa jukwaa la wahariri TEF- Teophil Makungwa mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni ishirini kutoka benki ya NMB. NMB imetoa kiasi cha fedha hiyo kama sehemu ya ufadhili wa mkutano wa mwaka wa jukwaa la wahariri ambao umefanyika mkoa wa Kilimanjaro. Wengine katika picha ni maofisa wa benki wakishuhudia tukio hililililofanyika mwishoni mwa wiki hapa Kilimanjaro. Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wakizungumza katika mkutano huo uliofanyika Mkoa wa Kilimanjaro. Wengine katika picha ni maofisa wa benki wakishuhudia tukio hililililofanyika mwishoni mwa wiki hapa Kilimanjaro. Benki ya NMB imetoa kiasi cha sh 20,000 kama sehemu ya ufadhili wa mkutano huo. Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wakizungumza katika mkutano huo uliofanyika Mkoa wa Kilimanjaro. Wengine katika picha ni maofisa wa benki wakishuhudia tukio hililililofanyika mwishoni mwa wiki hapa Kilimanjaro. Benki ya NMB imetoa kiasi cha sh 20,000 kama sehemu ya ufadhili wa mkutano huo.

  BENKI ya NMB imedhamini mkutano mkuu wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofanyika kwa siku moja ya Aprili 4, 2017 mkoani Kilimanjaro na kuhudhuriwa na wahariri wa vyombo mbalimbali nchini ambao ni wanachama wa TEF. 

  Akizungumza katika uzinduzi wa mkutano huo, Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali, Richard Makungwa alisema NMB inathamini mchango wa waandishi wa habari nchini na imekuwa ikishikiana nao kwa muda mrefu hivyo kudhamini mkutano huo ni sehemu ya kuendeleza ushirikiano ulipo baina ya NMB na waandishi wa habari. 

  “Kwa niaba ya uongozi wa Benki ya NMB, napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati kabisa kwa kutambua kuwa NMB ni benki iliyo karibu na jamii yote ya Watanzania na kugusa mahitaji ya kila jamii ya watanzania wa kila kada. 

  “Waandishi wa habari kwa NMB ni wadau muhimu sana kwani mafanikio ya NMB mpaka kufikia hapa kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na vyombo vya habari. Hivyo tunafarijika na sisi kushikiriana nanyi kwenye shughuli zinazowagusa ninyi moja kwa moja,” alisema Makungwa na kuongeza.

   “Kwa NMB, huu ni mkutano muhimu sana na maazimio mtakayoyafikia, yatakuwa yenye tija huku mkiweka mbele uzalendo wan chi yetu. Mkiwa mnaendelea na mkutano huu, tambueni kuwa tunawathamini sana na kazi zenu tunazithamini sana.” 

  Udhamini wa NMB kwa mkutano mkuu wa mwaka wa TEF una thamani ya milioni 20 na hiyo siyo mara ya kwanza kwani hata mwaka jana ilidhamini mkutano wa TEF, mkutano mkuu wa mwaka wa TBN, mkutano wa TAJATI na pia NMB kuwezesha kutolewa kwa tuzo za uandishi mahiri kwa kushirikiana na MCT.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Katiba na Sheria amewasilisha maombi  ya kuwasafirisha washitakiwa watatu akiwemo Ally Hatibu Hassan maarufu kama Shkuba  kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kujibu tuhuma za kusafirishaji dawa za kulevya.

  Washitakiwa wengine ambao wanaungana na Shkuba ni Idd Mafuru na Lwitiko Emmanuel Adam.

  Maombi hayo yamewasilishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya kifungu namba 5 (1) cha Sheria ya Usafirishaji wahalifu sura ya 368 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

  Katika maombi hayo upande wa waziri kupitia DPP wanaiomba mahakama hiyo isikilize ushahidi na itoe amri ya kuwahifadhi washitakiwa ndani wakiwa wanasubiri kibali cha Waziri huyo cha kuwasafirisha nje ya nchi kwa mashitaka hayo.

  0 0
 • 04/10/17--06:33: IN LOVING MEMORY


 • 0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI kwa kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw.   Wambura Sabora (hayupo pichani) wakati Mkurugenzi Mkuu huyo wa NBS alipofanya ziara mkoani humo hivi karibuni kuangalia jinsi zoezi la utafiti huo linavyoendelea.

  Na Veronica Kazimoto
  Imeelezwa kuwa asilimia 97 ya watanzania wanaoishi katika kaya zilizochaguliwa kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI katika mikoa 11 ambayo imeshafikiwa hadi sasa,  wameshiriki kikamilifu katika utafiti huo unaoendelea kufanyika nchini.

  Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa utafiti huo kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Wambura Sabora alipofanya ziara mkoani humo kuangalia jinsi zoezi la utafiti huo linavyoendelea.
  "Ninayo furaha kukutaarifu kwamba,  mpaka sasa utafiti huu umeshafanyika katika mikoa 11 ya Tanzania Bara pamoja  na visiwa vyote vya Zanzibar yaani Pemba na Unguja.  Jambo la kufurahisha zaidi ni mwitikio wa wananchi ambao ni asilimia 97 ya wanaoishi katika kaya zilizochaguliwa kwa ajili ya utafiti kukubali kushiriki," amesema Dkt. Chuwa.

   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (kulia) akiwa na kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Wambura Sabora wakati Mkurugenzi Mkuu huyo wa NBS alipofanya ziara mkoani humo hivi karibuni kuangalia jinsi zoezi la Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI linavyoendelea.
  Mikoa ambayo imekamilisha utafiti huu wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI ni pamoja na Singida, Dodoma, Manyara, Iringa, Njombe na Ruvuma. Mikoa mingine ni Mbeya, Songwe, Katavi, Tabora na Kigoma.
  Nae Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Wambura Sabora amemwambia Mkurugenzi Mkuu wa NBS kwamba, zoezi la utafiti huo mkoani humo linaendelea vizuri na mpaka sasa hakuna tatizo lolote  lililoripotiwa ofisisini kwake.

   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (katikati) akiwa na Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Kukinga na Kuzuia Magonjwa (CDC) Dkt. Eunice Mmari (kulia) wakipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa wadadisi wanaofanya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Bw. Johnmark Obura wakati wa ziara iliyofanyika mkoani Kagera hivi karibuni kuangalia jinsi zoezi la utafiti huo linavyoendelea.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

older | 1 | .... | 1642 | 1643 | (Page 1644) | 1645 | 1646 | .... | 3270 | newer