Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1634 | 1635 | (Page 1636) | 1637 | 1638 | .... | 3278 | newer

  0 0


  Spika wa Bunge  Mhe. Job Ndugai akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa Mhe. Elly Macha, uliotokea juzi katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton nchini Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu, katika tukio lililofanyika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma

  Naibu Spika wa  Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa Mhe. Elly Macha, uliotokea juzi katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton nchini Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu, katika tukio lililofanyika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Do.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili uwanja wa Karume Pemba leo kwa ziara ya kikazi
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Do.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili uwanja wa Karume Pemba leo kwa ziara ya kikazi
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Do.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili uwanja wa Karume Pemba leo kwa ziara ya kikazi

  0 0


  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoani Tanga kimepata pigo baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Muheza, Rwebangira Mathias Karuwasha kuamua kutangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) leo kwa kile anachodai kuwa  chama hicho kupoteza dira na mwelekeo.

  Hatua ya mwenyekiti huyo kutangaza kujiuzulu inakuja siku chache baada ya maamuzi wa mkutano mkuu wa viongozi wa chama kanda ya kaskazini mjini Tanga uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe kuridhia kuvunja uongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya ya mkoa wa Tanga.
  Akitangaza uamuzi huo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ukumbi wa BMK uliopo Sahare Jijini Tanga,  Rwebangira Karuwasha alisema hayo ndio mambo makubwa yaliyopelekea kuamua  kujiunga na CCM ambako amesema kuna sera makini zinazotekelezeka.
  Alisema kutokana na matukio mbalimbali anayoyafanya Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe sitegemei kuendelea kubaki kwenye chama hiki cha watumwa na watwana hivyo nimeamua kujiunga na CCM kwani ndio chama kinachoweza kutekeleza sera makini na zenye mafanikio.

  “Kwa mfumo wa uongozi unaoongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe haukubaliki na hakuweza kuvumilia.... sitegemei kuendele kuwepo kwenye chama hicho kilichokuwa cha watwana na watumwa hivyo nimeridhia kujiunga na CCM “Alisema.

  “Kuanzia leo mimi sio mwanachama wa Chadema na nitajiungha na CCM ya sasa chini ya Rais Dokta John Magufuli sababu Chadema wameacha sera na makini kwa ajili ya kuwapa maendeleo wananchi.

  Alisema pia sababu nyengine ni kutokana na utendaji wa Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM ambao umekuwa mstari wa mbelea kujali wanyonge na kusaidia harakati za kimaendeleo hapa nchini.

  Aidha alisema wameshindwa kuelewa kuwa Mwenyekiti Mbowe alipangua gia angani kumuondoa dkta Slaa wakati alipokuwa kwenye chama hicho jambo ambalo ni hatari kwa ukuaji wa chama hicho. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Muheza, Rwebangira Mathias Karuwasha akizungumza na waandishi wa habari mapema leo kutangaza azma ya kuondoka Chadema na kuhamia CCM 

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara,  Mhe. James Ole Millya na mbunge wa viti maalum Zanzibar  Mhe. Tauhida wakiwa kwenye mkutano wa 134 wa umoja wa mabunge duniani mjini Dhaka nchini Bangladesh, ambapo Tanzania iliwakilishwa na wabunge tisa na makatibu wawili

  Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mkoani Simiyu Mhe. Andrew Chenge akiwaongoza wabunge tisa na makatibu wawili wa Bunge la Tanzania kwenye mkutano wa 134 wa umoja wa mabunge duniani mjini Dhaka nchini Bangladesh (wa pili kulia mstari wa nyuma) ni mbunge wa jimbo la Simanjiro, mkoani Manyara, James Ole Millya.

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi akisoma taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara katika mwaka wa fedha 2016/17 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2017/18 kwa kamati ya kudumu ya bunge ya ardhi, Maliasili na Utalii - Dodoma. 
  Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii; Mhe. Atashasta Ndetiye akiongoza majadiliano wakati wa kujadili bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ilioshirikisha Kamati yake na watendaji wakuu wa Wizara na taasisi zake - Dodoma.
  Mbunge wa Korogwe mjini, Mhe. Mary Chatanda akishiriki mjadala wakati wa kujadili bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ilioshirikisha Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na watendaji wakuu wa Wizara na taasisi zake – Dodoma. 

  Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-
  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi amezipa kongore timu za JKT Oljoro ya Arusha, Mawenzi ya Morogoro na Transit Camp ya Shinyanga kwa kufanikiwa kupanda daraja la kwanza  baada ya kufanya vema kwenye hatua ya Nne Bora (Play off) iliyofikia kikomo jana Aprili mosi, mwaka huu.

  Katika salamu zake za pongezi, Rais Malinzi amezitaka timu hizo sasa kujiimarisha katika nyanja za usajili na maandalizi mengine ili kuwa timu za ushindani katika Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambako watashiriki kuanzia msimu mpya utakaoanza Julai, mwaka huu.

  “Nichukue nafasi hii kuzipongeza timu zote ambazo zimepanda daraja kutoka Ligi Daraja la Pili na kwenda Ligi Daraja la Kwanza. Pongezi nyingi ziwaendee wanafamilia wote kuanzia viongozi, wachezaji, waamuzi walioamua mechi zao, mashabiki nakadhalika,” amesema Malinzi na kuongeza:
  “Huu ni uthibitisho kuwa timu zote ziliajianda vya kutosha na kupata matokeo,naamini hata Cosmopolitan nayo ilijiandaa lakini kwa bahati mbaya pointi hazijatosha kwa msimu huu. Ni imani yangu kuwa itapambana msimu ujao na kufanikiwa.”
  Hali Kadhalika Rais Malinzi alizitakia kila la kheri timu zote katika kumaliza msimu na kuanza msimu ujao.

  0 0

  Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys, kesho Jumatatu itapambana na Black Starlets ya Ghana kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Katika mchezo huo utakaoanza saa 10.00 jioni, Serengeti Boys itautumia kama ni ishara ya kuwaaga mamilioni ya Watanzania kabla ya kusafiri kwenda kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14, mwaka huu.

  Lakini kabla ya kutua Gabon, Serengeti Boys itakwenda Rabat, Morocco kufanya kambi ya takribani mwezi mmoja kuanzia Aprili 5, mwaka huu. Ikiwa huko angalau itacheza mechi za kirafiki zisizopungua mbili dhidi ya wenyeji morocco na timu nyingine ya jirani ama Tunisia au Misri. Kambi hiyo ya Morocco itamalizika Mei mosi, mwaka hu ambako timu itasafiri hadi Cameroon.

  Ikiwa Cameroon, timu itacheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya wenyeji yaani Mei 3 na 6, mwaka huu kabla ya kusafiri Mei 7, mwaka huu kwenda Gabon ambako Serengeti Boys imepangwa kundi B pamoja na timu za Mali, Niger na Angola.

  Vipimo vya mechi dhidi ya Ghana kadhalika hapo baadaye Cameroon, vitakuwa mwafaka kwenye kufanya tathmini ya uwezo wa Serengeti Boys kwani wapinzani hao wamekuwa na rekodi nzuri kwenye soka la vijana na kwa kipindi hiki zimepangwa kundi A pamoja na wenyeweji Gabon na Guinea.

  Kila la kheri Serengeti Boys katika mapambano ya kuwania ubingwa wa Afrika kadhalika kucheza fainali za Kombe la Dunia hapo Novemba, mwaka huu zitakazofanyika India. Serengeti Boys inaweza na Mtanzania tunakuomba kuichangia timu hii kwa namna ya 223344 kupitia mitandao yote ya simu.

  0 0

  Na: Genofeva Matemu – WHUSM, Katavi 

  Wananchi wameombwa kuiunga mkono Serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na kujenga uchumi wa viwanda nchini. 

  Rai hiyo imetolewa na Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru Mkoani Katavi na kusema kuwa Uchumi wa viwanda uliodhamiriwa ni ule utakaolifanya taifa kuzalisha bidhaa bora na zenye ushindani wa soko la kimataifa badala ya kuwa chanzo cha malighafi na soko la bidhaa za viwanda vya mataifa mengine. 

  “Tanzania tumeazimia kutoka katika kundi la uchumi duni na kwenda kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda, Ujenzi na uimarisha wa viwanda nchini ambao utahusisha wadau mbalimbali wa Maendeleo, wananchi wenyewe, sekta binafsi na Mashirika Mbalimbali ya Kimataifa yanayo nafasi kubwa hususan katika uwekezaji mkubwa, ukuzaji wa mitaji, masoko, Teknologia na upatikanaji wa rasimali watu wenye ujuzi maalum” amesema Mhe. Balozi Iddi. 

  Aidha Mhe. Balozi Iddi amesema kuwa wananchi wanayo fursa kubwa sana katika kujenga na kuendeleza viwanda nchini kwani ukuaji wa uchumi wa Viwanda unaanza kwa jitihada za wananchi wenyewe katika kuanzisha na kuendesha viwanda vidogo vidogo vinavyoweza kuongeza thamani ya mazao na bidhaa wanazozalisha kila siku katika maeneo yanayowazunguka. 
  : Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi (wapili kushoto) akiwasha Mwenge wa Uhuru wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi. Watatu kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Bw. Amour Hamad Amour (kushoto) akimhaidi mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi (kulia) kuulinda na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri zote 195 Tanzania bara na Zanzibari wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Bw. Amour Hamad Amour akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga Mwenge wa Uhuru baada ya kukabidhiwa mwenge huo na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi kuukimbiza mwenge huo katika halmashauri 195 Tanzania bara na Zanzibar wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
  Watumbuizaji kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari wakitoa burudani wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM, Katavi.

  0 0


  0 0

  Mmoja wa mafundi akiweka mabomba ya maji sawa hili aweze kumwagilia vizuri eneo la uwanja wa Bandari, Temeke, jijini Dar es salaam ambao umepandwa nyasi za kisasa kwa ajili ya mazoezi pamoja na kuchezea mashindano ya soka, yakiwemo ya Ndondo Cup.
  Mabomba ya kisasa yakimwagilia maji katika uwanja huo wa Bandari ambao unatarajiwa kuwa wa kisasa katika eneo lake la kuchezea kwa kufanana na uwanja wa Taifa.
  Bomba jingine lililopo upande wa mashariki ya uwanja likimwagilia maji.
   Jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja huo liliwekwa na balozi wa China Dkt. Lu Younqing
  Sehemu ya upande wa goli ambayo imewekwa sawa na kupandwa nyasi za kisasa. Picha na HunphreyShayo wa Globu ya Jamii

  0 0

  Timu ya Maji Maji ( WANALIZOMBE) imeutumia vyema uwanja wake wa nyumbani kwa kuichapa Toto African Bao 4-1  katika mchezo uliochezwa uwanja wa MAJI MAJI uliopo mjini Songea, mkoani Ruvuma.

  0 0


  0 0


  0 0

  Mtanange ulipomalizika Kipa Kaseja alipewa zawadi na Mashabiki wa Kagera Sugar pamoja na Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawilo akikaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

  Na Faustine Ruta, Bukoba
  Timu ya soka ya Kagera Sugar imefanikiwa kuichapa timu ya Simba kwa bao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, uliopigwa katika dimba la Kaitaba, Mjini Bukoba Mkoani Kagera.

  katika mchezo huo ulishuhudia timu ya soka ya Simba wakishindwa kutumia nafasi zao vyema walizopata na kujikuta wakifungwa bao 2-1 ambapo mabao ya Kagera Sugar yalifungwa na Mbaraka Yusuph na bao la pili likifungwa na Edward Christopher huku bao la kufutia machozi kwa Simba likifungwa na Mzamilu Yasin dakika 61 ya kipindi cha pili. 

  Kwa matokoe hayo Yanga wanaendelea kuwa kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na jumla ya pointi 56 wakifuatiw na Simba wenye pointi 55 huku Kagera Sugar wakifikisha jumla ya pointi 45 huku nafasi ya nne ikishikwa na Azam wenye pointi 44.
  Kikosi cha Simba kilichoanza.
  Kikosi cha Kagera Sugar kilichoanza dhidi Simba ya Jijini Dar es salaam.
  Mshambuliaji wa timu ya Simba Mrundi Laudit Mavugo akijaribu kumtoka Beki wa Kagera Sugar Juma Ramadhan .
  Kichuya Akiambaa na Mpira.
  Kiungo wa timu ya Simba Said Ndemla akiachia Shuti kali ambalo lilipanguliwa na Kipa Juma Kaseja
  Kiungo wa timu ya Simba James Kotei raia wa Ghana  ambaye anauwezo wa kucheza namba zaidi ya moja Uwanjani akipambana kupata mpira mbele ya wachezaji wa kagera Sugar leo hii uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

   Mshindi wa pikipiki katika shindanola Shika ndinga la EFM kwa wanawake kutoka wilaya ya Temeke ambaye aliondoka na pikipiki ya Sanmoto katika Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es salaam siku ya Jumapili.
  Mshindi kwa wanaume washindano la Sjika ndinga, Abdallah Twaha akiangukia gari mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa pikipiki ya Sanmoto viwanja wa Mwembe Yanga, Temeke, jijini Dar es salaam.
   Meneja wa EFM Radio Dennis Ssebo  akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa washindi
   Meneja Masoko wa kampuni ya Mosan ya hapa nchini Tanzania,Jakson Stephen akikabidhi pikipiki aina ya Sanmoto kwa washindi Pili Hassna na Abdalah Twaha mara baada ya kuibuka washindi katika shindano la Shika ndinga Wilaya ya Temeke liliandaliwa na EFM. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Na  Bashir  Yakub. 
  Ni  wangapi  wamefanyiwa  utapeli  katika  harakati  za  kununua  viwanja  au  nyumba.  Ni  wangapi  wamepata  hasara  kubwa  kutokana  na  michezo  ya  utapeli   iliyotamalaki  katika  ardhi  nchini.  Ni  kesi  ngapi  ziko  mahakamani  zinazohusisha  utapeli   katika  mauzo na  manunuzi  ya  ardhi.  Idadi  ni kubwa  mno  na huu  ndio  ukweli.

  Siku  zote  huwa tunasema  ni  vigumu  kujua   ukubwa  na  hatari  ya  jambo   hili  mpaka  likukute  au  limkute  mtu  wako  wa  karibu. Lakini  swali  ni  ikiwa  watu   wamekuwa  wakijifunza  kupitia  wenzao  ambao  wamekutwa  na  haya. Kama  na wewe  bado  hujajifunza  basi ni  muhimu  sasa  kujifunza.

  Mtu   anauza  ardhi  moja  kwa  watu hata   zaidi  ya  wanne tofauti, mtu  anauza  ardhi  asiyokuwa  yake  huku  akijua  kabisa  sio  ya kwake, mtu  anaghushi  hati  au  leseni  ya  makazi  kisha  anauza  kiwanja  au  nyumba ya  mtu, kiongozi  wa  serikali  ya  mtaa   anashiriki  kuuza  ardhi  ya mtu   huku akijua  kuwa  juzi  mtu  mwingine  alinunua  ardhi  hiyohiyo, kwa  ufupi  hali  ni  mbaya  na  ni  vema  kusema  ili  watu  wachukue  tahadhari.

  Wizara  ya  ardhi  imeshasema mara  nyingi  kuwa  moja  ya  sababu  kubwa  inayopelekea  watu   kutapeliwa  katika  manunuzi  ya  ardhi  ni  wanunuzi  wenyewe  kutozingatia  taratibu  za  kisheria  za  manunuzi. Migogoro  mingi  imezalika  hapa. 

  Mara  kadhaa  tumewahi  kueleza  kwenye  makala mbalimbali  namna  salama  ya  kununua  ardhi  kwa  kuepuka  utapeli.  Zipo  makala nyingi  ambazo  zimeeleza  hatua  za  kufuata  ili  uwe  salama.  Hata  hivyo  leo  kitaelezwa  kitu  kingine  ambacho  hakikuwahi  kuelezwa.  Ni  namna  ya kuhakiki  hati  au  leseni  ya  makazi   ili  kujua  ikiwa ni  halisi (original)  au  feki kabla  ya  kununua  kiwanja  au  nyumba. 

  1.UHAKIKI  ULIOWAHI  KUSHAURIWA.
  Kabla  ya  kueleza  njia  nyingine  ya uhakiki  inayotakiwa  kuelezwa  leo hebu  tujikumbushe  njia iliyowahi  kuelezwa  katika  makala  zilizopita. Ni  uhakiki  wa  hati  kwa  njia  ya   upekuzi  rasmi( official  search).  Tulisema  kuwa  kupitia  njia  hii  utaandaa  maombi  kwenda  kwa   msajili  wa  hati(Registrar of Title)   ukitaka  kujua  ikiwa  nyumba /kiwaja  unachotaka  kununua  kama kina  mgogoro  au  ikiwa kuna  mtu  mwingine  mwenye  maslahi  juu  yake.

  Mgogoro  ni  kama  kuna  zuio  la  kifamilia( caveat), zuio  kutoka  mahakamani  na  mengine  yanayofanana  na  hayo.  Na  kuwapo  mtu  mwingine  mwenye  maslahi  ni  kama  kiwanja  au  nyumba hiyo kuwa   imesimama  kama  dhamana   ya  mkopo n.k.  Majibu  ya  vitu  vyote  hivi  utayapata utakapojibiwa   maombi  yako  ya  upekuzi  rasmi ( official  search).


  0 0

  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli  Jumapili  April 2, 2017 ameungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe, Paroko aliyekuwa anahudumu katika Parokia ya  Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia  Parokia ya Chang’ombe, wilayani Temeke.
  Kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rigambwa  wa Kanisa la Mtakatifu Petro na kuongozwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mama Magufuli amemtakia kila la heri Fr. Kaombwe katika kituo chake kipya cha kazi, na pia amempa salamu toka kwa Rais John Pombe Magufuli ambaye naye amemtakia heri na fanaka kwa uhamisho huo.
  Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa alimpongeza Fr. Kaombwe kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati akihudumu katika Paroko hiyo kwa takriban miaka mitatu na nusu, na pia alitumia nafasi hiyo kumtambulisha Fr. Asis Sylvester Mendoca ambaye atakaimu nafasi ya Fr. Kaombwe.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru, amempongeza Fr. Kaombwe kwa mambo mengi aliyoyafanya kanisani hapo, na kwa niaba ya jumuiya ametoa shukurani nyingi kwa huduma alizokuwa akiwapatia.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiongea machache alipoungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa anahudumu katika Parokia ya Oysterbay katika Kanisa la Mtakatifu Petro  jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia  Parokia ya Chang’ombe, wilayani Temeke. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru (kushoto) na Fr. Asis Sylvester Mendoca (wa pili kulia) wakimsikiliza Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke, akiongea kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
  Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa akiongoza sala wakati wa hafla ya kumuaga Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa anahudumu katika  Parokia ya Oysterbay katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Parokia ya Chang’ombe. Kushoto ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli. Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na masista alipoungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe,, Paroko aliyekuwa anahudumu katika Parokia ya Oysterbay katika Kanisa la Mtakatifu Petro  jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Parokia ya Chang’ombe, wilayani Temeke.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja na waumini, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru, Fr. Asis Sylvester Mendoca baada ya kuhitimisha hafla ya kumuaga Fr. Stephano Kaombwe, Paroko aliyekuwa anahudumu Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Parokia ya Chang’ombe, wilayani Temeke. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.

  0 0

  Serikali imesema itakuwa bega kwa bega na Chuo cha michezo Malya ili kuhakikisha chuo hicho kinakuwa kitovu cha kuzalisha walimu bora na wenye weledi katika masuala mazima ya michezo hapa nchini na hata nje ya nchi. 

  Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Harrison George Mwakyembe, alipokuwa akifunga mafuzo ya muda mfupi yanayo tolewa na chuo hicho, ambapo jumla ya wahitimu wapatao sitini na tisa (69) walitunukiwa vyeti na waziri huyo. 

  Mwakyembe amesema, kama wizara, nilazima wakifanye chuo cha Michezo Malya kuwa “Strategic thinking” kwa maana ya stratejia ya wavumbuzi wa vipaji vya watu wa kada mbali mbali hususan katika suala zima la walimu wa michezo “Nilipo tembelea na kukiona chuo nimepata picha kamili ya chuo hiki, hii sasa inanipa shauku yakuwashauri muandae dira endelevu kwa chuo chetu” alisema Mwakyembe. 

  Mwakyembe, amesema katika Ibara ya 161 (G) ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2015-2020, inaweka bayana na kutia msukumo wa masuala ya michezo, lakini pia Rais wa Jamhuri ya Muungano ameonesha dhamira ya dhati katika hilo hata mbele ya Mataifa mengine ndio sababu Morocco, wanataka kujenga ‘Sport Complex’ Makao Makuu ya nchi Dodoma. 

  Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho, amesema katika kuhakikisha chuo hicho kinafanya vema katika siku za usoni wamedhamiria kuongeza idadi ya kozi zitakazo kuwa inatolewa kwa wakurufunzi wanaotaka kujiunga na chuo hicho ukiwepo mchezo wa Whushu ambapo China kupitia ujumbe wake iliowakilishwa na Bi. Amber, uliozulu chuoni hapo wakati wa mahafali, umeonesha nia yakuleta walimu wa Whushu. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Dkt Harrison George Mwakyembe akizungumza katika mahafali ya Chuo cha waalimu Michezo Malya Jijini Mwanza. 
  Mkurugenzi wa Michezo nchini Bw. Yusufu Omary Singo akitoa nasaha kwa wahitimu wa mafunzo katika mahafali ya kuwatunuku vyeti wahitimu wa kozi fupi ya uwalimu wa michezo yaliyofanyika Chuo cha Mwaalimu wa Michezo Malya Jijini Mwanza. 
  Baadhi ya wanafunzi na wahitimu wa kozi fupi ya uwaalimu wa michezo wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Dkt. Harrison George Mwakyembe alipokuwa akizungumza nao katika mahafali ya Chuo hicho Jijini Mwanza. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHUSM .


  0 0

  Wazazi wametakiwa kuwa waangalifu wa watoto wao wanaosoma nje ili kuhakikisha wanasoma na kuhitimu vizuri kama inavyotakiwa.

  Akizungumza na wazazi ambao watoto wao wanasoma nje, Mkurugenzi wa kampuni ya uwakala ya Global Education Link, Abdulmalik Mollel amesema hilo likifanyika taifa litanufaika zaidi.

  “Tuendelee kushirikiana kwa pamoja ili kuona watoto wetu walioko nje kwa masomo wanamaliza masomo yao na kutimiza ndogo zao inavyotakiwa. Sisi wazazi tuna mchango mkubwa sana katika hili,” alisema Mollel mwishoni mwa wiki.

  Alifafanua kwamba kuna watoto wamekuwa wakipewa fedha nyingi na wazazi wao kiasi kwamba nao wanapofika nje huwa bize kufanya matanuzi badala ya kusoma kama ambavyo tunatarajia.

  “Unakuta mtoto anapewa fedha nyingi hadi anashindwa kujua azitumie kwa matumizi gani, ndipo hapo wengine unakuta wanajiingiza kwenye ulevi na mambo mengine kama hayo. Ni lazima tunapowapa fedha tujiridhishe je ni kwa ajili ya nini na wanazitumiaje,” alisema Mollel.

  Mkurugenzi wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel akizungumza jambo kwenye mkutano wa wazazi ambao watoto wao wanasoma nje ya nchi
  Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu, Prof. Simon Msanjila akiwaasa wazazi kwenye mkutano wa wazazi ambao watoto wao wanasoma nje ya nchi

  Robert Shetkintong, Naibu Balozi wa India nchini akifuatilia mijadala katika kikao cha wazazi ambao watoto wao wanasoma nje ya nchiBaadhi ya wazazi walioshiriki mkutano wa wazazi ambao watoto wao wanasoma nje ya nchi mwishoni mwa wiki.  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Joy Sawe akifungua semina ya utoaji elimu kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 kwa Wahariri wa Habari na baadhi ya wamiliki wa Blogs iliyofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.
  Meneja wa Idara ya Takwimu za Kodi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Fred Matola akiwasilisha mada juu ya Takwimu Rasmi wakati wa semina ya utoaji elimu kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 kwa Wahariri wa Habari na baadhi ya wamiliki wa Blogs iliyofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.
  Baadhi ya Wahariri wa Habari na wamiliki wa Blogs wakifuatilia kwa makini semina ya utoaji elimu kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 iliyofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.
  Baadhi ya Wahariri wa Habari na wamiliki wa Blogs wakifuatilia kwa makini semina ya utoaji elimu kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 iliyofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.
  Baadhi ya Wahariri wa Habari na wamiliki wa Blogs wakifuatilia kwa makini semina ya utoaji elimu kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 iliyofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.
  Baadhi ya Wahariri wa Habari na wamiliki wa Blogs wakifuatilia kwa makini semina ya utoaji elimu kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 iliyofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.

older | 1 | .... | 1634 | 1635 | (Page 1636) | 1637 | 1638 | .... | 3278 | newer