Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1633 | 1634 | (Page 1635) | 1636 | 1637 | .... | 3285 | newer

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya kuchunguza kiwango cha aina ya madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya makontena yaliyozuiliwa na Serikali sehemu mbalimbali hapa nchini  Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo Profesa Justinian Rwezaura Ikungula Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo Profesa Joseph Buchweishaija Ikulu jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Kamati Maalum ya kuchunguza kiwango cha aina ya madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya makontena yaliyozuiliwa na Serikali sehemu mbalimbali  hapa nchini mara baada ya kuwaapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
  0 0

  Kocha Msaidizi wa timu ya Maji Maji (Wanalizombe) , Habibu Kondo amewahakikishia wanachama wa Club ya Maji Maji na wadau wa soka mkoani Ruvuma kuwa timu hiyo haitashuka daraja , hivyo wawe na amani katika michezo hii iliyobakia lazima Maji Maji itashinda na kubaki ligi kuu Tanzania bara.

  0 0  Kufuatia uteuzi wa Bibi Blandina S.J. Nyoni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) tarehe 25/02/2017. Mhe. William V. Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 5(2) cha Sheria Na. 2 ya Mwaka 1990, amewateua Wajumbe 7 wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa. 

  Aidha, uteuzi huu ni wa kipindi cha miaka mitatu (3), kuanzia tarehe 23 Machi, 2017.

  Majina ya wajumbe hao ni kama ifuatavyo: 

  Prof. John M. Lupala
  Bwn. Gabriel Malata
  Bi. Mary Mlay
  Bi. Subira Mchumo
  Bwn. Ally Hussein Laay
  Bwn. Pius Maneno
  Bwn. Kesogukwele Masudi Issa Miraji Msita 


  Imetolewa na: 

  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

  0 0


  Msongola, Dar es Salaam.

  MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewataka watendaji wa Manispaa kuhakikisha wanazuia shughuli za kibinadamu ikiwemo ujenzi na kilimo katika maeneo oevu ili kulinda mazingira.

  Amewasisitizia wananchi umuhimu wa kupanda miti mingi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuzuia magonjwa mbalimbali ambayo yamekuwa yakisababishwa na hali ya hewa.Mjema amesema hayo leo wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti duniani, ambayo wilaya ya Ilala iliyafanya shule ya msingi Yangeyange katika Kata ya Msongola wilayani humo.


  Alisema mbali na kutunza mazingira na kuleta mvua, miti imekuwa ikitumika kama dawa na jambo la muhimu ni kuwa miti hiyo inafyonza mionzi inayotoka katika jua. “Miti hii inafyonza mionzi mikali inayotoka kwenye jua, ile mionzi badala ya kuja kutugonga moja kwa moja kwenye ngozi zetu inapita kwanza kwenye miti, miti hii inatukinga na maradhi hasa ya kansa. Lakini sasa mkiangalia maradhi ya kansa yanazidi hasa ya ngozi, miti tunakata sana, tupande na tutunze miti,” alisema mjema.

  Akizungumzia kuhusu wananchi wanaojenga katika maeneo oevu na mabondeni, aliwataka watendaji na wenyeviti wa maeneo mbalimbali ya Manispaa hiyo kuhakikisha wanazuia mapema ujenzi huo badala ya kusubiri mtu anamaliza ujenzi na ndipo waende kumhoji.
  Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akipanda mti wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Upandaji Miti, kilichofanywa na Wilaya ya Ilala katika shule ya Msingi, Yangeyange, Kata ya Msongola wilayani humo mkoani Dar es Salaam. Wapili kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo ya Ilala Edward Mpogolo na Kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando.  0 0


  Walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wamepongezwa kazi nzuri na kupata matokeo mazuri ya shule zao za msingi katika mtihani wa taifa wa mwaka jana.

  Pongezi hizo zilitolewa jana na mwakilishi wa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Sigisbert Rwezaula wakati wakati wa hafla ya kupongeza shule kumi zilizofanya vizuri katika mitihani ya mwaka jana.

  Katika hafla hiyo iliyofanyika Mwadui wilayani Kishapu ikiambatana na utoaji vyeti kwa walimu wakuu, Rwezaula ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema hakuna muujiza wa kufanya vizuri bali ni walimu kujituma.

  Aliwataka walimu wakuu wa shule ambazo hazikufanya vizuri kuhakikisha wanaweka mikakati ili ziweze kuibuka vinara kama walivyo wenzao na kuwataka kuendelea kujituma.

  ”Najua kuna changamoto nyingi kwa walimu kama upungufu au ukosefu wa fedha lakini nawaomba tuvumilie na tukabiliane nazo, jambo kubwa ni kutoa elimu bora kwa wanafunzi wetu na hatimaye wafanye vizuri,” alisisitiza.

  Mgeni rasmi, Sigisbert Rwezaula akitoa cheti kwa mmoja wa walimu wakuu wa shule zilizofanya vizuri. Wengine pichani kulia ni Afisa Ugavi Wilaya, George Ngwesa. 
  Walimu wakifurahia cheti walichopewa kwa kutambua kufanya vizuri kwa shule yao. 
  Wageni waalikwa wakiserebuka muziki ikiwa ni moja ya shamrashara za kupongezana kwa kazi nzuri. 
  Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na walimu wakuu wa shule kumi bora pamoja na maofisa elimu mbalimbali. 


  0 0


  Mwenyekiti wa KILIFM Sports Center akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kuhusu KILIFM International Marathon yanayolenga kuzuia mauaji ya Albino, utunzaji wa mazingira na uoto wa asili pia kuzuia mauaji ya Tembo nchini,leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mjumbe wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Bw. Peter Mwita.
  D 1
  Mratibu wa Mashindano ya mbio za KILIFM akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu mashindano ya KILIFM International Marathon yanayotarajiwa kufanyika Augusti 13, Mwaka huu Mkoani Kilimanjaro.

  Picha na: Beatrice Lyimo – MAELEZO.

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja.

  Baadhi ya Wahariri wa Habari na waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wanahabari hao katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja. 
   

  Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Mhe,Rashid Ali Juma alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali katika wengine alipowasili katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja.


  Wakuu wa Wilaya za Zanzibar na Waandishi wa habari wakiwa katika Semina ya siku moja ya Viongozi na Waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani). 

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud mara alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja katika Semina ya Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo.


  0 0

  Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Elizabeth Titus Munthali, wakati wa sherehe ya mahafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba. 
  Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Honest Amedeus Matem, wakati wa sherehe ya mahafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba. 
  Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Annastacia Mbunda, wakati wa sherehe ya mahafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO). 
  Mgeni rasmi Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga, akimkabidhi cheti mhitimu, Salim Ngailo, wakati wa sherehe ya mahafali ya kwanza ya Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania, iliyofanyika leo katika Jengo la kibiashara la Haidary Plaza, jijini Dar es Salaam. Kulia kwa mgeni rasmi, ni Rais wa Taasisi hiyo, Pius Maneno (kulia) ni Mkaguzi msaidizi Mkuu wa hesabu za Serikali, Emmanuel Subi. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo, Buyamba Buyamba. 


  0 0


  Na Faustine Ruta, Bukoba
  Timu ya Vijana U17 ya Burudi leo kwenye uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba imepoteza mchezo wake wa pili tena wa kirafiki baada ya kukubali kuchapwa bao 2-0 na Timu ya Serengeti Boys ya jijini Dar es salaam inayojiandaa na safari ya Gabon. Mchezo wake wa kwanza wa kirafiki walinyukwa bao 3-0 na Timu ya Vijana maarufu kwa jina la Serengeti Boys katika uwanja huo huo wa Kaitaba. 
  Katika mchezo wa leo bao la kwanza lilifungwa na Issa Abdu Makamba dakika ya 36 kipindi cha kwanza jezi namba 6 mgongoni aliyelifunga kwa mpira wa adhabu (frii kiki) na kuzama moja kwa moja. Bao la pili  lilifungwa dakika za majeruhi dakika ya 89  na Ibrahim Abdallah na mtanange kumalizika kwa bao 2-0 ikiwa ni jumla ya bao 5-0 ikiwa ni jumla ya mchezo wa kwanza na wa pili. Serengeti sasa baada ya kuvuna ushindi huo mkubwa wanapanda ndege kwenda Jijini Dar es Salaam kucheza na Timu ya U-17 ya Ghana Jumatatu mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.

  Wachezaji wa Timu ya Serengeti Boys wakimpongeza mfungaji wao wa bao la pili Ibrahim AbdallahShangwe kwa Vijana maarufu kwa Jina Serengeti Boys baada ya kuibuka Kidedea kwa bao 2-0 kwa kuitandika Burundi (U17) kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba leo.


  0 0

  Beki wa Yanga, Deus Kaseke akijarimu kumdhibiti Mshambuliaji wa Azam FC, Salum Abubakar "Sureboy", katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara, uliochezwa jioni ya leo kwenye dimba la Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 1-0.

  Mabingwa watetezi wa Ligi ya Vodacom Tanzanja Bara Yanga wamefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Azam katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa.  Mpira huo ulioanza majira ya sa 10 alasairi ulichezeshwa na Mwamuzi Jonesia Rukyaa akisaidiwa na John Kanyenye na Soud Lila ulikuwa na ushindani mkubwa huku Azam wakionekana kutawala sehemu ya kiungo.

  Azam katika dakika 45 za kipindi cha kwanza walishindwa kutumia nafasi walizozipata kutokana na kutokuwa makini kwa safu yao ya ushambuliaji.

  Kipindi cha pili kimeanza kwa kila upande kutafuta goli la kuongoza na katika dakika ya 71 mshambuliaji wa kimataifa kutoka Zambia Obrey Chirwa anaiandikia Yanga goli la kuongoza akitumia uzembe wa mabeki wa Azam kuurudisha mpira kwa golikipa Aishi Manula.

  Yanga wanaamka na kuanza kulishambulia lango la Azam lakini nao wanakuwa makini na kusaka goli la kusawazisha na mpaka dakika 90 mwamuzi Jonesia anapuliza filimbi ya mwisho Yanga wanatoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 1-0.

  Baada ya matokeo hayo, Yanga wanafikisha alama 56 wakiwa mbele kwa alama moja dhidi ya mahasimu wao Simba wenye alama 55 ambao wanacheza na Kagera Sugar katika Uwanja  wa Kaitaba mkoani Kagera.

  Kikosi cha Yanga kilichoanza leo.
  Kikosi cha Azam FC kilichoanza leo.
  Mshambuliaji wa Azam, Shaban Idd akiipokea pasi kwa kisigino mbele ya Mabeki wa Yanga, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara, uliochezwa jioni ya leo kwenye dimba la Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 1-0.


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akiagana na Waziri Mkuu wa Shirikisho la Kidemokrasia la Jamhuri ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Dessalegn mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini. Wakati wa ziara hiyo pamoja na mambo mengine alimaliza kwa kutembelea Bandari ya Dar es Salaam na Mhe. Dessalegn ameahidi kuitumia Bandari hiyo kupitisha mizigo ya nchi yake pamoja na kufanya biashara na nchi za Afrika Mashariki.Ziara hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 31 Machi hadi 01 Aprili, 2017.
  Mhe. Dessalegn akiagana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb) akiagana na Mhe. Dessalegn.
  Waziri Mkuu, Mhe. Dessalegn akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Naimi Aziz mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini
  Waziri Mkuu, Mhe. Dessalegn akiagana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Innocent Shiyo mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini
  Waziri Mkuu Dessalegn akiagana na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Zulekha Tambwe.
   Mhe. Dessalegn akimpungia mkono wa kwaheri Rais Magufuli, viongozi mbalimbali wa Serikali na wananchi (hawapo pichani) waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kumuaga  mara baada ya kumaliza rasmi ziara yake nchini.
  Rais John Pombe Magufuli (wa kwanza kulia), Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda kwa pamoja wakimpungia mkono wa kwaheri kumuaga Mhe. Dessalegn,

  0 0


  Na Freddy Macha 
  Jumuiya ya Wasanii wa Tanzania Uingereza (WASATU) leo inazinduka kwa onesho la muziki Northampton.

  Onesho hilo litajumuisha wanamuziki wakongwe wa Kitanzania wakiwemo Saidi Kanda ( na bendi Mvula Mandondo), mwimbaji sauti chiriku Fab Moses na bendi ya Afrika Jambo ikihusisha mpiga sax RamaSax. Ramasax aliwahi kupuliza “madude” na Simba wa Nyika. Mwingine ni mpiga gitaa Kawele Mutimanwa aliyeshiriki wimbo maarufu wa Mambo Bado na bendi ya Makassy miaka ya 80. Wengine ni pia wanamuziki walemavu kama  mpiga gitaa John Londo, Kea nk...


  Mwenyekiti wa WASATU, Bi Neema Kitilya , mcheza dansi, Khadija ( Kibisa zamani) wasanii wengine wameeelezea mori wao kutangaza na kujumuiha wasanii wetu duniani.

  TUTAWALETEA HABARI ZAIDI INSHALLAH MUNGU AKIPENDA


  Tuko pamoja!


  Tanzania oyeee !!!


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Duniani Mtukufu Mahant Swami Maharaj mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Kiongozi huyo Mkuu wa Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Mtukufu Mahant Swami Maharaj mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa Dua na kiongozi huyo wa Jumuiya ya Kihindu Duniani Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Mtukufu Mahant Swami Maharaj aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake kiongozi huyo Mkuu wa Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Mtukufu Mahant Swami Maharaj mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na kiongozi huyo wa Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Mtukufu Mahant Swami Maharaj Ikulu jijini Dar es Salaam. 

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Kiongozi huyo Mkuu Duniani wa  Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Mtukufu Mahant Swami Maharaj Ikulu jijini Dar es Salaam. 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kiongozi huyo Mkuu Duniani kutoka Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha(BAPS) Mtukufu Mahant Swami Maharaj Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


  0 0  0 0


  0 0


  Na Jumia Travel Tanzania

  Kama kuna kitu ambacho wafanyakazi wengi wanapenda kusikia basi ni sikukuu au mapumziko. Kwani hupata fursa ya kutokwenda kazini, haimaanishi kwamba ni wavivu bali kutokana na ufinyu wa likizo ukiachana na wikendi.
  Kwa upande wa watanzania hali hiyo hutokea kwa baadhi ya miezi na wa Aprili ni mmojawapo. Kutokana na utafiti mdogo uliofanywa na Jumia Travel, zifuatazo ni sababu zinazoufanya mwezi huu kupendwa zaidi nchini.
  Sikukuu ya Karume. 
  Hii siku huadhimishwa kila ifikikapo April 7 ya kila mwaka ikiwa ni kumbukumbu ya kuuawa kwa aliyekuwa Rais wa kwanza wa visiwa vya Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume mwaka 1972 katika eneo la Mji Mkongwe, Unguja. 


  Hivyo basi kama taifa huiadhimisha siku hiyo kwa wananchi kupumzika na kutofanya shughuli yoyote na badala yake kumkumbuka shujaa huyo aliyeongoza mapinduzi dhidi ya waarabu waliokuwa wakivikalia visiwa hivyo kwa mabavu. Kwa mwaka huu ni tofauti kidogo kwani siku hiyo itaangukia Ijumaa na hivyo kutoa fursa kwa watu kupumzika kwa siku tatu ukijumuisha na wikendi. Kwa wenye mipango mifupi kwenye mapumziko hayo wanaweza kutekeleza azma zao, kama vile kusafiri nje kidogo ya mji. 

  Sikukuu ya Pasaka. 
  Kwa wakristo wengi nchini Tanzania na duniani kote kwa sasa wapo kwenye mfungo wa Kwaresma ambao ulianza tarehe mosi ya mwezi Machi na kudumu kwa siku 40. Kwa mujibu wa kalenda mfungo huo utaisha siku ya Alhamisi ya tarehe 13 ya mwezi Aprili. Maandalizi ya sikukuu ya Pasaka huanza siku ya Ijumaa Kuu, tarehe 14, ambayo ni siku ya mapumziko huku sikukuu yenyewe ya Pasaka itakuwa ni Jumapili ya tarehe 16. Lakini haiishii hapo kwani shamrashamra za Pasaka zitaendelea mpaka siku ya Jumatatu ya tarehe 17. Hivyo, kwa haraka haraka watu watakuwa na mapumziko ya siku nne mfululizo na ndio maana husubiriwa kwa hamu kubwa huku kukiwa na mipango lukuki ndani yake. 


  Tembelea Jumia Travel kujua sehemu zilizo karibu nawe ambazo unaweza kwenda na kufurahia kwa siku hizo chache pamoja na wapendwa wako.

  Sikukuu ya Muungano. 
  Ifikapo tarehe 26 ya mwezi wa Aprili pia watanzania watakuwa na sherehe nyingine muhimu katika historia ya taifa lao. Siku hiyo inakumbukwa kwa Tanganyika kuungana na visiwa vya Zanzibar (Unguja na Pemba) mnamo mwaka 1964 na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama ilivyo ada siku hii nayo ni mapumziko kwa watanzania wote, watu hawaendi kazini na badala yake kusherehekea siku hiyo kwa kuutafakari umuhimu wa Muunganao na faida zake kwa wananchi wa pande zote mbili kwa pamoja.

  0 0


  Na: Genofeva Matemu – WHUSM, Katavi

  Vijana Mkoani Katavi wametakiwa kujitambua, kuchukua fursa na kuchangia maendeleo ya mkoa na taifa kwa kutumia malighafi zinazopatikana mkoani humo kuwekeza na kuacha kusubiria wawekezaji kutoka mikoa mingine ama nchi za nje kufaidika na malighafi za mkoa huo.

  Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama alipokua akifungua kongamano la Vijana kuelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi na kuwataka vijana hao kuacha uvivu kwani maendeleo huletwa na jitihada za mtu binafsi.

  Mhe. Jenista amesema kuwa vijana wanaweza wakajiwekeza katika sekta isiyo rasmi kwani sekta hiyo huajiri asilimia kubwa na kuwagusa vijana wengi katika kutengeneza ajira na kuwafanya vijana wasiwe tegemezi ndani ya jamii. 
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akifungua kongamano la Vijana kuelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.
  JENI2
  Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga akizungumza na Vijana (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kongamano la Vijana kuelelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.
  JENI3
  Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico akizungumza na Vijana na watendaji wa Mkoa wa Katavi (hawapo katika picha) juu ya matumizi ya Tovuti ya Mkoa kabla ya kuzindua Tovuti hiyo leo Mkoani Katavi.
  JENI4
  Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico (katikati) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Tovuti ya Mkoa wakati wa kongamano la Vijana kuelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.
  JENI5
  Baadhi ya Vijana wa Mkoa wa Katavi wakifuatilia kwa makini mada zilizokua zikitolewa wakati wa kongamano la vijana kuelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.
  Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM.
  0 0

  *Waziri Mkuu amtaka amalize migogoro ya wakulima, wafugaji 

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Eng. Evarist Ndikilo apige kambi katika kata ya Miono wilayani Bagamoyo na kuwasaka wafugaji wanaopiga wakulima.

  Waziri Mkuu alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wakazi wa kata hiyo ambao walisimamisha msafara wake wakati akienda kukagua miundombinu ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani iliyoko wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.

  Akitoa kero za eneo hilo, Diwani wa Kata ya Miono, Bw. Juma Mpwimbwi alisema kata hiyo inakabiliwa na tatizo la wakulima kupigwa na wafugaji na wakipelekwa kituo cha polisi hawachukuliwi hatua yoyote.

  “Wafugaji wanatupiga lakini wenzetu hawachukuliwi hatua na hata ukienda kushtaki polisi, hawakai kwa sababu wanadai wao wana fedha,” alisema diwani huyo.

  Pia alisema mbali ya kero sugu ya maji, waliahidiwa barabara ya lami tangu miaka saba iliyopita lakini hadi sasa hawana hata kipande kidogo tu cha barabara hiyo.
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa (pichani kulia) akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Eng. Evarist Ndikilo alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.  0 0

  Na Jumbe Ismailly,Iramba Apr,02,2017 Maafa 

  MVUA kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha kwa takribani nusu saa imeezua mapaa ya majengo ya shule ya sekondari New Kiomboi,iliyopo wilayani Iramba,Mkoani Singida imesababisha zaidi ya wanafunzi 150 kukosa vyumba vya kusomea na hivyo kulazimika kutumia majengo mawili ya vyumba vya maabara viliyopo katika shule hiyo.

  Mkuu wa shule hiyo,Lameck Ayeiko alisema kuwa tukio hilo lilitokea Machi,24,mwaka huu saa kumi jioni ambapo mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali ilinyesha kwa muda wa takribani nusu saa na hivyo kusababisha pia ofisi ya Mkuu wa shule na ofisi za walimu kuezuliwa paa na kujaa maji kwenye vyumba hivyo na kwamba zaidi ya shilingi milioni 20 zinahitajika kurudisha majengo hayo katika hali ya kawaida.

  “Ili kurudisha yale majengo katika hali yake ilivyokuwa zilikuwa zinahitajika jumla ya shilingi milioni 13,648,lakini kuboresha yale madarasa ili yakae vizuri sasa, kulikuwa kunatakiwa kuwe na ongezeko la kama shilingi milioni 6,511,000/= karibu milioni ishirini”alisisitiza mwalimu huyo.

  Kufuatia tukio hilo Mkuu wa shule huyo alisema walilazimika kufanya mkutano wa hadhara kwa kuwashirikisha wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo na kufikia makaubaliano kwa kila mzazi kuchangia shilingi 10,000/=ambapo papo kwa papo zilipatikana zaidi ya shilingi laki tano kwa ajili ya ukarabati wa majengo hayo.

  Alipotakiwa kuzungumzia maafa hayo,Mkuu wa wilaya ya Iramba,ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa kamati ya maafa wa wilaya hiyo,Emmanuel Luhahula alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kwamba baada ya kufanyika kwa tathimini ya uharibifu huo walibaini zaidi ya shilingi milioni 20 zinahitajika kurejesha majengo hayo katika hali yake ya kawaida.

  Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba,Mariether Kasongo aliweka wazi kuwa kati ya shilingi milioni 30 hadi 35 zinahitajika kukarabati majengo yaliyoathirika kutokana na mvua hiyo iliyonyesha kwa muda wa nusu saa.

  Shule ya sekondari New Kiomboi iliyoezuliwa mapaa ya baadhi ya majengo yake kwa zaidi ya wiki moja sasa,lakini hakuna kiasi chochote cha fedha kilichotengwa na Halmashauri hiyo kwa ajili ya kurejesha hali ya majengo ya shsule hiyo.

  Shule ya sekondari New Kiomboi,iliyopo Tarafa ya Kisiriri,wilayani Iramba,Mkoani Singida ipo katika Programu ya SEDP na fedha kwa ajili ya kuhakikisha shughuli za kuboresha majengo ya shule hiyo yanatekelezwa kupitia mpango huo zinapatikana.
  baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari New Kiomboi,wilayani Iramba,Mkoani Singida wakifanya mitihani yao kwenye majengo ya vyumba vya maabara baada ya vyumba vya madarasa yao kuezuliwa na upepo mkali.(Picha zote Na Jumbe Ismailly) .
  baadhi ya vyumba vya madarasa ya shule ya sekondari New Kiomboi,wilayani Iramba,Mkoani Singida vilivyoezuliwa paa kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo iliyonyesha kwa takribani nusu saa na hivyo kuwakosesha zaidi ya wanafunzi 150 vyumba vya kusomea.
  baadhi ya vyumba vya madarasa ya shule ya sekondari New Kiomboi,wilayani Iramba,Mkoani Singida vilivyoezuliwa paa kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo iliyonyesha kwa takribani nusu saa na hivyo kuwakosesha zaidi ya wanafunzi 150 vyumba vya kusomea.
  Ni baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tatu na nne katika shule hiyo waliokuwa wakijisomea nje ya vyumba vya madarasa wakisubiri kuingia kwa zamu darasani kufanya mitihani yao
  Ni baadhi ya bati za majengo ya shule ya sekondari New Kiomboi,iliyopo wilayani Iramba,Mkoani Singida yaliyoezuliwa katika vyumba vya madarasa,ofisi ya mkuu wa shule pamoja na ofisi za walimu wa shule hiyo.

  0 0

older | 1 | .... | 1633 | 1634 | (Page 1635) | 1636 | 1637 | .... | 3285 | newer