Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1635 | 1636 | (Page 1637) | 1638 | 1639 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) mkoani Dodoma Aprili 3, 2017.

  Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) wakifuatilia taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa Baraza hilo (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa baraza hilo Aprili 3, 2017 katika Ukumbi wa Mikutano Dodoma.
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) wakifuatilia taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa Baraza hilo (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa baraza hilo Aprili 3, 2017 katika Ukumbi wa Mikutano Dodoma.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Erick Shitindi akiwasilisha hotuba yake wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyazi Ofisi hiyo uliofanyika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma Aprili 3, 2017.
  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Peter Kalonga akichangia hoja wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyazi uliofanyika Aprili 3, 2017 Dodoma.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyazi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) mara baada ya kufungua mkutano huo katika Ukumbi wa mikutano Ofisi hiyo Dodoma.

  (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA)

  0 0


  Beki wa Timu ya Taifa ya Vijana ya Ghana (U17) , Yusif Abdulrazak akiondosha mpira mbele ya Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Vijana - Serengeti Boys, Yohana Mkomola, katika Mchezo wa kimataifa wa kirafiki, uliopichezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka sare ya kufungana goli 2-2.
  Mshabuliani wa Timu ya Taifa ya Vijana - Serengeti Boys, Kelvin Naftal akitafuta mbinu za kumtoka Beki wa timu ya Beki wa Timu ya Taifa ya Vijana ya Ghana, Antah Isaac, katika Mchezo wa kimataifa wa kirafiki, uliopichezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka sare ya kufungana goli 2-2.
  Mshambuliaji wa Serengeti Boys, Muhsin Malima akiipatia timu yake bao la pili, dhidi ya wageni wao Ghana, katika Mchezo wa kimataifa wa kirafiki, uliopichezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka sare ya kufungana goli 2-2.
  Wachezaji wa Serengeti Boys wakishangilia baada ya kupata goli la pili na kufanya matokeo kuwa 2-2 dhidi ya Ghana, katika Mchezo wa kimataifa wa kirafiki, uliopichezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.


  0 0


  0 0


  0 0

  Ni simanzi kubwa, baba yetu mdogo, Profesa Lloyd Manamba Binagi, amefariki dunia hii leo Jijini Dar es salaam.
  Taratibu za kuusafirisha mwili kwenda nyumbani Tarime zinafanyika. Pumzika kwa amani baba. Ulikuwa nguzo muhimu kwetu. Daima tutakukumbuka. 
  Mola ailaze roho yako mahali pema peponi - Amina.
  George Binagi.

  0 0  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika New York, Marekani na kupitisha Azimio la kuongeza muda kwa vikosi vya usalama vilivyopo DRC. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb). akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Picha ya pamoja ya wajumbe wa Tanzania na Uganda  ambao nchi zao zimetakiwa kushirikiana kwa pamoja kutumia rasilimali walizonazo kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa pande zote mbili katika  Kikao cha Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya nchi hizo mbili. Taarifa kamili BOFYA HAPA


  0 0

  Jumuiya ya waTanzania Rome- Italia 
  Picha kwa hisani ya Tanzania Community Rome- Italy


  Na Vijimambo Blog
  Natumaini wote hamjambo na mnaendelea vizuri na majukumu ya kila siku ya maisha yanayotukabili kila siku ya uhai wetu. Baada ya salamu ningependa kuanza moja kwa moja na swala ya jumuiya za waTanzania nje ya nchi tuipendayo Tanzania, kumekuwepo na migogoro mingi kwenye hizi jumuiya na mishikamano inayoleta umoja kupungua siku hadi siku mpaka inasikitisha na kutia huruma.
  Jumuiya za waTanzania ughaibuni zilikua imara sana wakati zilipoanzishwa miaka ya nyuma hasa mwanzoni mwa miaka ya 80 na jumuiya zilikua imara sana wakati huo ikiwemo wanajumuiya wanachama kuwa hai kwa kuchangia michango yao ya kila mwezi hadi mwaka.
  Sababu moja wapo kubwa ya jumuiya hizi kuwa hai ni idadi ndogo ya waTanzania iliyokuwepo ughaibuni iliyofanya urahisi wa mawasialino kwa kujuana na kutembelea kama ndugu waliotoka nchi moja tofauti na sasa waTanzania wamekua wengi mpaka wengine imekua vigumu kujuana.

  0 0
  0 0

  Na Lydia Churi-MAHAKAMA, ARUSHA

  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Ferdinand Wambali amewataka Majaji wa Mahakama Kuu nchini kufanya kazi zao kwa kuzingatia Maadili, kuwa waaaminifu na kushirikiana katika kuwahudumia wananchi ili kesi zimalizike kwa haraka katika Mahakama mbalimbali.

  Akifungua Mafunzo ya siku tano ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tazania kuhusu Uongozi katika shughuli za Mahakama  leo jijini Arusha, Jaji Kiongozi amesema lengo la Mafunzo hayo ni kujadiliana kwa kina nini kifanyike ili kesi zimalizike mapema kwenye mahakama mbalimbali nchini.

  Jaji  Wambali alisema katika mkutano huo, Majaji watapata nafasi ya kujifunza Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania wenye nguzo tatu ambazo ni pamoja na masuala ya Utawala, Upatikanaji wa haki kwa wakati na imani ya wananchi kwa Mahakama na ushirikishwaji wa wadau katika shughuli za Mahakama.

  Katika Mafunzo hayo pia Majaji watajadiliana ni nini kilifanyika mwaka jana katika umalizwaji wa mashauri, changamoto zilizojitokeza na nini kifanyike ili kutatua changamoto zinazojitokeza katika utendaji wao wa kazi wa kila siku.

  Naye Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Katarina Revokati akizungumza na Waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo  alisema  yamegawanyika katika makundi matatu ambapo kundi la kwanza ni la Majaji wa Mahakama ya Rufani, kundi la pili ni la Majaji  Wafawidhi  wa Kanda 14 za Mahakama Kuu ya Tanzania na  kundi la Tatu ni la Majaji wengine wote.

  Alisema Majai wa Mahakama ya Rufani watapatiwa Mafunzo kuhusu namna ya kutoa maamuzi ya Mahakama katika usikilizwaji wa kesi ngazi ya Rufaa, ambapo Majaji Wafawidhi watapewa mafunzo kuhusu Usimamizi wa uendeshaji wa kesi wakati Majaji wengine watapatiwa mafunzo kuhusu uongozi na usimamizi wa kuleta mabadiliko.

  Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Benki ya Dunia ni Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania na yanalenga katika kuboresha utendaji kazi na kuleta mabadiliko ndani ya Mahakama.

  Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma (wa pili kushoto) akiwasili katika ukumbi wa AICC jijini Arusha kuhudhuria Mafunzo ya Majaji yaliyoanza  jijini humo.Kushoto kwake ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali. Kushoto kwa Jaji Wambali ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revokati na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Mahakama Bibi Wanyenda Kutta.

  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akifungua Mafunzo ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania katika Ukumbi wa AICC leo jijini Arusha. Mahakama inaendesha Mafunzo kwa Majaji wote wa Tanzania ambapo Majaji wa Mahakama ya Rufani wanahudhuria Mafunzo kuhusu namna ya kutoa maamuzi ya Mahakama katika usikilizwaji wa kesi ngazi ya Rufaa, Majaji Wafawidhi kuhusu Usimamizi wa uendeshaji wa kesi wakati Majaji wengine wanapatiwa mafunzo kuhusu uongozi na usimamizi wa kuleta mabadiliko.

  Waheshimuiwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa kwenye ufunguzi wa Mafunzo yao yaliyoanza  jijini Arusha.


  0 0


  0 0


  0 0


   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Crispin Prospher Mwombeki wa kampuni ya Ujenzi wa Barabara ya Mecco wakati Rais alipotembelea ukarabati wa barabara ya Chwale (Madenjani) mpaka Mzambarautakao  inayojengwa na kampuni hiyo yenye urefu wa kilomita tano (5km) katika Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba akiwa katika ziara ya kikazi (kulia) katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Miundombinu Ndg. Mustafa Aboud Jumbe
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto)akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Miundombinu Ndg. Mustafa Aboud Jumbe (katikati) alipokuwa akiangalia mashine ya kutilia lami (PAVER) ya kampuni ya Mecco wakati alipotembelea ukarabati wa ujenzi wa Barabara ya Chwale (Madenjani) mpaka Mzambarautakao inayojengwa na Kampuni hiyo   yenye urefu wa kilomita tano (5km) katika Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba,  akiwa katika ziara ya kikazi 
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati)akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya ZECON ya Zanzibar Ndg. Ali Mbarouk Juma (kulia) wakati alipofika Daya Mtambwe Kaskazini Pemba kuangalia hatua za Ujenzi wa Chuo cha  Mafunzo ya Amali  akiwa katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kasakazini Pemba,(wa pili kulia)Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Mmanga Mjengo Mjawiri
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akizungumza na Wananfunzi wa Skuli ya Daya Mtambwe alipotembelea   Ujenzi wa Chuo cha  Mafunzo ya Amali unaojengwa na Kampuni ya kizalendo ya ZECON ya hapa Zanzibar,   akiwa katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kasakazini Pemba

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati)akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Rashid Hadid Rashid alipotembelea Ukunjwi katika  sehemu ya kupokelewa Umeme unaopelekwa kisiwa cha Fundo, Mkoa wa kaskazini Pemba akiwa katika ziara ya kikazi. Picha na Ikulu.
  Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dr. Anna Peter Makakala amefanya mabadiliko makubwa ya Viongozi wa Uhamiaji wa Mikoa mbalimbali hapa nchini pamoja na kuwateua Wakuu Wapya wa mikoa kushika nyadhifa hizo katika Mikoa iliyopo Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.

  Katika Mabadiliko haya Naibu Kamishna wa Uhamiaji Sixstus Faustine Nyaki aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza amehamishiwa  mkoa wa  Simiyu wakati aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa Naibu Kamishna  wa Uhamiaji Selemani  Bandiho  Kameya amehamishiwa Mkoa wa Tabora.
  Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Asumsio  Paulus Achacha amehamishiwa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa  Manyara  Naibu Kamishna  Peter Jerome Kundy amehamishiwa Mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya  Kamishna Msaidizi  Ali Mohamed ambaye amehamishiwa   kuwa Mkuu wa Uhamiaji mkoa wa  Arusha. 
  Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Mkemi Mhina Seif  ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja, Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Muhsin Abdallah Muhsin ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja,  Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Said Omary Hamdani ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji  Mkoa wa Mjini Magharibi na  Naibu Kamishna wa Uhamiaji Othman Khamis Salum  ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mjini Magharibi Unguja.
  Katika mabadiliko hayo baadhi ya Wakuu wa Uhamiaji wa Mikoa wamebaki katika Vituo vyao vya kazi vya awali akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Morogoro Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Safina Muhindi, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Lindi Naibu Kamishna wa Uhamiaji George Kombe, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma  Naibu Kamishna wa Uhamiaji Hilgaty Laurent  Shauri, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Singida Naibu Kamishna wa Uhamiaji Faith Alexander Ihano  na Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mara  Naibu Kamishna  Fredrick Eustace  Kiondo.
   Wengine waliobaki kwenye vituo vyao vya awali ni pamoja na  Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Abdallah  Ramadhani Towo  mkoa wa Kagera na  Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Anastazia  Gasper Ngatunga mkoa wa Shinyanga.
  Katika mabadiliko hayo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Makakala pia amewateua  Viongozi wa Uhamiaji wa Mikoa wapya katika baadhi ya mikoa hapa nchini ambapo Naibu Kamishna wa Uhamiaji Mary Francis Palmer   kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam,  Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Plasid  Mazengo,  Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa  Pwani, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji  James Andrew Mwanjotile, Mkuu wa Uhamiaji  Mkoa wa  Mtwara,  Kamishna Msaidizi Mwandamizi  Hope Jaffer Kawawa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa  Iringa,  na  Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji  Hosea Alphonce Kagimbo  Mkoa wa Njombe.  Wengine ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Rashid Salum Magetta  Mkuu wa Uhamiaji  Mkoa wa Songwe,  Naibu Kamishna wa Uhamiaji Carlos John Haule,  Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa,  Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Julieth Deodatus Sagamiko Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa  Manyara,  Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Albert Joseph Rwelamila, Mkuu wa Uhamiaji  Mkoa wa Kilimanjaro na  Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Paul Laurent Eranga,  Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa  Mwanza.
  Naibu Kamishna wa Uhamiaji Crispin Crispin Ngonyani ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa  Tanga,  Naibu Kamishna wa Uhamiaji  Shaban Omar Hatibu  Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa  Katavi,  Naibu Kamishna wa Uhamiaji   Remigius Ibrahimu Pesambili Mkuu  wa Uhamiaji  Mkoa wa Kigoma na Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Novaita Edmund Mrosso ameteuliwa kuwa  Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya.
  Aidha Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Bakari Mohamed Ameir ameteuliwa kuwa Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume [AAKIA] na Kamishna Msaidizi  Mwandamizi wa Uhamiaji Fulgence Andrew Mutarasha  kuwa  Mkuu wa Uhamiaji Kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere[JNIA].


  Imetolewa na

  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini

  Dr. A. P. Makakala


  3 Machi 2017


  0 0

  Na Daudi Manongi - MAELEZO
  Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imesaini msaada wa shilingi Bilioni 490 usiokuwa na masharti yeyote kutoka Umoja wa Ulaya ikiwa ni msaada wa kibajeti kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka wa bajeti wa 2017/18.
  Mkataba huo umesainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James kwa niaba ya Serikali na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Bw.Roeland van de Geer kwa niaba ya Umoja wa Ulaya.
  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mkataba huo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James amesema Umoja wa Ulaya umetoa msaada huo kutokana na kuvutiwa na juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika maeneo mbalimbali ikiwemo kupambana na rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.
  “Nadhani mmeshuhudia utiaji saini huu ulioisha hivi punde na Umoja wa Ulaya wametuhakikishia kuendelea kutusaidia katika masuala ya misaada ya kibajeti pamoja na kuwa bega kwa bega na Serikali katika masuala mbalimbali ya maendeleo”, aliongeza Katibu Mkuu huyo.
  Pamoja na hayo mpango wa pili wa maendeleo wa Taifa wa Bajeti ya mwaka 2017/18 pia utapewa msaada na umoja huo kwani wameuona mpango huo una tija na kuweka mkazo katika viwanda na kilimo.
  Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Roeland Van de Geer amesema kuwa wameliangalia zaidi suala la utawala kama eneo kuu katika mpango wa ushirikiano na Tanzania na vilevile wanatazamia maendeleo zaidi katika maeneo ya kilimo,ujenzi wa barabara za vijijini na nishati.
  “Mkataba ambao tumeusaini utaiwezesha Wizara ya Fedha na Mipango katika ukusanyaji wa mapato,zitaboresha uwajibikaji na utumiaji mzuri wa mali za Serikali, na Umoja wa Ulaya unasapoti azma ya viwanda ya Serikali ya Awamu ya Tano,”Aliongeza Roeland Van de Geer.
  Amesema kuwa ushirikiano uliopo katika ya Tanzia na Umoja wa Ulaya ni mpana sana na utaendelea kuimarika zaidi katika kipindi hiki ambacho mageuzi ya sera yanahitajika.
   Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Dotto James akibadilishana mkataba wa kibajeti na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Bw.Roeland van de Geer mara baada ya kusaini mkataba huo Jijini Dar es Salaam.

   Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Bw.Roeland van de Geer akizungumza jambo na waandishi wa habari juu ya msaada wa shilingi bilioni 486.9 uliotolewa na umoja huo kwa Serikali ya Tanzania ili kusaidia Bajeti.Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Dotto James.

  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Dotto James akitoa ufafanuzi kwa wahandishi wa habari juu ya msaada wa shilingi bilioni 486.9 ambao Serikali imeupata kutoka umoja wa ulaya (EU) kwa ajili ya kusaidia Bajeti.Kushoto kwake ni Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Bw.Roeland van de Geer.Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.

  0 0


  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Ndugu Andrew W. Massawe yuko mkoani Iringa kukagua maendeleo ya zoezi la Usajili na Utambuzi wa watu; ambapo pamoja na mambo mengine anatazamiwa kushuhudia sherehe za uzinduzi wa utoaji Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Wilaya ya Mufindi na kuzinduliwa kwa kampeni ya Usajili wa wananchi na wageni wenye umri wa miaka 18 na kuendelea wanaoishi mkoani humo.
  Katika ziara yake; leo amekutana na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William, ambaye amemweleza Mkurugenzi huyo hatua kubwa ambayo Wilaya yake imefikia mpaka sasa katika kuwasajili wananchi, ambapo takribani asilimia 60 ya wananchi wameshasajiliwa, kuchukuliwa alama za vidole na baadhi Vitambulisho vyao kuzalishwa, mbali na kukamilika kwa zoezi la kuwasajiliwa Watumishi wa Umma.
   Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Wilaya ya Mufindi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Ndugu Andrew W. Massawe

   Ndugu George Mushi Afisa Usajili Mkoa wa Iringa (RRO), akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA,  Ndugu Andrew W. Massawe kuhusu vifaa vinavyotumika kwenye usajili wa wananchi alipotembelea ghala la kuhifadhi vifaa wilayani Mufindi

   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA  Ndugu Andrew W. Massawe akiwa na Kanali Hamisi Maiga Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha Mafinga namba 841, wakati alipotembelea kambi hiyo.

   Mtendaji wa Kata ya Boma; Joseph Kiwele akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la usajili wananchi kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA  Ndugu Andrew W. Massawe. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0


  Na  Bashir  Yakub
  Transfer  ni  kubadilisha  hati  au  leseni  ya  makazi  kutoka  jina  la  mmiliki  wa awali  kwenda  kwa  mmiliki  mpya.  Transfer  inaweza  kufanyika  kutokana na mauzo, kupewa  zawadi, fidia, n.k.  Kwahiyo  kuzuia  transfer  ni  kuzuia   kubadilishwa  kwa  hati  kutoka  mmiliki wa  awali  kwenda  mmiliki  mpya. Mara   nyingi  tumezoea   kuzuia   transfer  kwa  kutumia  mahakama ( court  injuction).

  Sasa  yatupasa tufahamu kuwa  ipo  njia nyingine  nyepesi  ambayo  haihusishi  mahakama.  Ni  njia  ya  maombi  kwa  kamishna  wa  ardhi   kwa  mujibu  wa  Sura  ya  113 ,  sheria  ya ardhi ,namba  4, ya mwaka  1999  vifungu  vya  38, 39  na  41 . Kabla  ya kuona  ufanyeje  kutumia  njia  hii ni  vema  tuone    mazingira  ambayo   yakikutokea unaweza  kutumia  hiyo  njia.


  1.HAYA  YAKITOKEA  UNAWEZA  KUPELEKA  MAOMBI  KWA  KAMISHNA.

  ( a ) Mme  wako  au  mke  wako  ameuza   kiwanja  au  nyumba  yenu  na  kuna  namna  ambavyo  mauzo  hayo   unadhani  sio  halali  kwasababu  yoyote  ile  ya  kisheria pengine ya  kutokushirikishwa,  au  kushirikishwa  lakini  baadae  kunyimwa  haki  yako  kwa  mujibu  wa  makubaliano au  vinginevyo. Lakini   wakati  huo   unadhani  huna  la  kufanya  kwakuwa  mauzo  tayari  yamefanyika  na  pengine  hata  wewe  ulishasaini.

  ( b ) Una  maslahi  na  haki  katika nyumba/kiwanja  cha  mirathi .  Mali  hiyo  imeuzwa  bila  wewe  kushirikishwa  au  umeshirikishwa  lakini  haki  zako  za  msingi  hazikuzingatiwa  au  namna  nyingine  yoyote  ambayo  kwayo  unahisi  mchakato  haukwenda  sawa.  Lakini   wakati  huo   unadhani  huna  la  kufanya kwakuwa  mauzo  tayari  yamefanyika  na  pengine  hata  wewe  ulishasaini.

  ( c ) Umemuuzia  mtu  nyumba/kiwanja  lakini  amekataa  kutekeleza  baadhi  ya  makubaliano  ya  msingi yaliyo  katika  mkataba  wenu  wa  mauziano  na  sasa  anafanya  mchakato  wa  kubadili  hati.

  ( d ) Na mazingira  mengine  yoyote ambayo  tayari  nyumba/kiwanja  kimeuzwa  lakini  ukaona  kuna  haja  ya  kuzuia  mchakato  wa  kubadilishwa jina  la  mmiliki  ili  baadhi  ya mambo yawekwe  sawa  kwanza.
  0 0


older | 1 | .... | 1635 | 1636 | (Page 1637) | 1638 | 1639 | .... | 3286 | newer