Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 29.03.2017


RAIS DKT. MAGUFULI ATEUA KAMATI YA UCHUNGUZI WA SHEHENA YA MCHANGA WA KUTOKA MIGODINI

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MAWAZIRI WA TANZANIA NA UGANDA juu ya mradi wa ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi TANGA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha pamoja cha Mawaziri wa Serikali za Tanzania na Uganda pamoja na wadau kuzungumzia mradi wa ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Mkutano huo, uliofanyika Ikulu, Dar es salaam, Jumanne Machi 28, 2017, ulihudhuriwa na Mawaziri wa Nishati na Madini pamoja na Mawaziri wa Ardhi wa nchi hizo mbili, Wanasheria wa Serikali na kampuni washirika wa mradi huo Lake Albert (CNOOC, TOTAL na TULLOW). 
Pamoja na mambo mengine, Mawaziri, Maafisa na Wataalam wa pande zote husika walikaa na kukubaliana kwamba rasimu ya makubaliano rasmi ya kuanza kwa mradi yawe yamekamilika na kuwa tayari katika kipindi cha wiki mbili ili kuwezesha Marais wa Tanzania na Uganda kuweka jiwe la msingi kuashiria kuanza ujenzi wa kihistoria wa mradi huo wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga, Tanzania. PICHA NA IKULU

DEATH ANNOUNCEMENT: Prof. Philip Robert Hiza

$
0
0
It is with great sadness, we announce the death of Prof. Philip Robert Hiza, of Makongo Juu, which occurred on Monday, March 27, 2017, at Muhimbili Medical Centre.
The deceased's body will be moved to The Late Prof. Hiza's residency on Friday, March 31, 2017,  for last respects vigil, to be followed by a special mass at St. Alban's Church on Saturday, April 1, 2017, 13:00Hrs. 
The  burial event will take place at Misalai, 
Amani,  Tanga on Sunday April 2, 2017.

Prof. Hiza leaves to mourn, his wife, Eileen Hiza, 3 sons, 4 daughters 15 grandchildren and 3 great grandchildren. Our heartfelt support and prayers go to the family of Late Prof. Philip Robert Hiza.

For more information, please contact:

1) Caroline Hiza  +1 (952) 215-6690
2) David Hiza  +1 (952) 649-2474
3) Roby Hiza  +255 745555554
4) Paul Meela  +255 767909090

KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII YAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA HABARI.

$
0
0
Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii pamoja na Waziri, Naibu Waziri na watendaji wakuu wa Wizara na Taasisi zilizo chini yaWizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakijadili Bajeti ya Wizara hiyo Mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza katika kikao cha kujadili Bajeti ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mjini Dodoma.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa kikao cha kujadili Bajeti ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akieleza juu ya mikakati ya Wizara katika kushirikisha Sekta binafsi katika kuleta maendeleo katika Sekta za Wizara wakati wa kikao cha kuijadili Bajeti ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mjini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakifuatilia hoja mbalimbali wakati wa kikao cha kujadili Bajeti ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mjini Dodoma.


Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma

Naibu Waziri Wa Mambo Ya Nje Apokea Nakala Za Utambulisho Za Mabalozi Wateule Kutoka Ethiopia Na Vietnam Nchini

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Kim Doanh. Tukio hilo limefanyika Wizarani tarehe 30 Machi, 2017

Dkt. Kolimba akizungumza na Balozi Mteule wa Vietnam, Mhe. Nguyen Kim Doanh mara baada ya kupokea nakala zake za hati za utambulisho  
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ethiopia nchini, Mhe. Dina Mufti Sid.Tukio hilo lilifanyika Wizarani tarehe 30 Machi, 2017.  
Picha ya pamoja.

JPM APONGEZWA KUIWEZESHA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE

$
0
0

Frank Mvungi-Maelezo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amepongezwa kwa kuiwezeshaTaasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kufanya upasuaji wa kihistoria tangu kuanzishwa kwake.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo na Daktari Bingwa wa Moyo Dkt. Bashir Nyangassa wakati wa hafla fupi ya kuwaaga madaktari bingwa wa moyo kutoka Hospitali ya Saifee ya Mumbai nchini India waliosaidia kufanikisha upasuaji huo wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kupandikiza katika mishipa ya moyo iliyoziba (CABG-Coronary Artery Bypass Graft) kwenye moyo .

Upasuaji huu uliwahusisha madaktari 6 toka Hospitali ya Saifee umesaidia kuwaongezea ujuzi wataalamu wa Taasisi hiyo na kuokoa fedha nyingi ambazo zingetumika kuwasafirisha nje wagonjwa ili waweze kupata matibabu.

“Kama wagonjwa hawa wangeenda kutibiwa nchini India Serikali ingelipia zaidi ya shilingi bilioni 2.1 kama gharama za matibabu” Alisisitiza Dkt. Nyangassa. “

Akizungumzia upasuaji mwingine uliofanyika kwa wagonjwa 8 Dkt. Nyangassa amesema kuwa ni upasuaji wa milango miwili hadi mitatu ya moyo ambayo ilikuwa na matatizo kwa kuibadilisha. 
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo Dkt. Bashir Nyangasa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini Sheikh Tayabali Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kutoka Hospitali ya Saifee, ya Mumbai nchini India Dkt. Aliasgar Behranwala. 
Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge akifafanua jambombele ya waandishi wa habari kuhusu kumalizika kwa kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo iliyofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 Machi katika Taasisi hiyo ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016. Katikati ni Mwakilishi Mkazi wa Madhebu ya Mabohora nchini Sheikh Tayabali Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upandikizaji wa Mishipa kutoka Hospitali ya Saifee ya Mumbai, India Dkt. Yunus Loya. 
Daktari Bingwa wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo kutoka Hospitali ya Saifee, ya Mumbai nchini India Dkt. Yunus Loya akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016. Kutoka kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini, Sheikh Tayabali Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo Dkt. Bashir Nyangasa (kulia). 
Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa moyo kuzibua njia mbili, Athumani Waziri akielezea namna alivyofarijika baada ya kupata matibabu hayo wakati wa kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo iliyofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 mezi Machi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktari hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016.Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini Sheikh Tayabali Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kutoka Hospitali ya Saifee, ya Mumbai nchini India Dkt. Aliasgar Behranwala. 

KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII YAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA HABARI


WAZIRI MKUU AWASHAWISHI WAWEKEZAJI KUTOKA MAURITIUS KUWEKEZA NCHINI,Awataka waje kujenga viwanda vya sukari, nguo na samaki

$
0
0

SERIKALI imepanga kuondoka katika uchumi wa chini na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 ambapo katika kufikia azma hiyo imeweka juhudi kwenye uanzishwaji wa viwanda mbalimbali kuanzia vidogo hadi vikubwa.

Mpango wa kufikia uchumi wa kati unalenga kuiwezesha serikali kujitegemea na tayari hatua mbalimbali zimechukuliwa ili kuweza kufikia azma hiyo.

Dira ya Taifa ya Maendeleo, imeainisha malengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujenge uchumi imara wenye uwezo wa kukabiliana na ushindani.

Katika kuhakikisha mkakati huo unafanikiwa Serikali imeweka sera na mazingira mazuri kwa ajili ya kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza kwenye viwanda.

Hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikwenda nchini Mauritius kumwakilisha Rais Dk. John Magufuli kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi Barani Afrika (AEP).

Baada ya kumaliza uzinduzi huo Waziri Mkuu alipata fursa ya kutembelea viwanda mbalimbali nchini Mauritius na kuhamasisha wawekezaji waje nchini ili kuongeza uzalishaji utakaokuza uchumi na kuongeza pato la taifa.

KUSOMA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WATANZANIA WAASWA KUJITOLEA KUCHANGIA DAMU

$
0
0
Frank Mvungi-Maelezo

Watanzania wametakiwa kujitolea kuchangaia Damu ili kuwasaidia wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa moyo wanaohitaji kuongezewa damu wakati wa kupatiwa mat

ibabu.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo na Daktari Bingwa wa Moyo Dkt. Bashir Nyangasa kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

“Tunatarajia kuwa na kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto itakayoanza tarehe 3/4/2017 hadi tarehe 7/4/2017 ambapo Taasisi yetu itashirikiana na Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Healinga Little ya London Uingereza.”Alisisitiza Dkt. Nyangasa

Akifafanua Nyangasa amesema kuwa wagonjwa 12 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kipindi hicho kwa ushirikiano na Madaktari hao kutoka Taasisi ya Healing Little ya London Uingereza.

Kufuatia upasuaji huo Dkt. Nyangasa amewaomba wananchi kuendelea kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha ya wale wanaohitaji kuongezewa damu.

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imekuwa Moja ya Taasisi Bora katika ukanda wa Afrika mashariki na Kati katika kutoa matibabu moyo kwa wagonjwa kutoka hapa nchini na katika mataifa mbalimbali yanayoizunguka Tanzania.

Upatikanaji wa damu yakutosha imekuwa moja ya changamoto zinazoikabili Sekta ya afya kutokana na mwitikio mdogo wa wananchi kujitolea damu ili kusaidia wale wenye uhitaji hivyo ni wajibu wa kila mtanzania kuunga mkono juhudi za Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika kuhamasisha wananchi kujitolea kuchangia damu.

Chama cha Mchezo wa “Baseball/Softball” Tanzania – TaBSA kutoa kombe siku ya kimataifa ya michezo ya amani

$
0
0

Umoja wa Mataifa (UN) pamoja na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa(IOC) kwa pamoja mnamo tarehe 23 Agosti, 2013 walitiliana saini na kukubaliana kuanzishwa rasmi kwa tarehe 6 April ya kila Mwaka iwe ni SIKU YA KIMATAIFA YA MICHEZO KWA AJILI YA AMANI NA MAENDELEO. “International Day of Sport for Development and Peace” 

Chama cha Mchezo wa “Baseball/Softball” Tanzania – TaBSA, kimeamua kushiriki siku hii kwa kutoa Kombe Maalum la AMANI ambalo litashindaniwa na timu mbili zitakazojumuisha watu wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea bila kujali viwango vya wachezaji katika kuucheza mchezo huu wa Baseball. Mechi hiyo itakuwa katika mfumo wa Bonanza. 

Timu zitakuwa ni TIGERS na GIANTS. 

Kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya Chama, ninachukua fursa hii kuwaalika wote kuhudhuria na kushiriki Bonanza hili la AMANI katika viwanja vya Azania Sekondari kuanzia saa 13:30 mchana siku ya Jumamosi ya tarehe 8 April, 2017. 

Karibuni wote!. 
Alpherio Moris Nchimbi – KATIBU MKUU. 
Tumeamua kuifanya tarehe 8 April kwa kuwa tarehe 6 April ni siku ya Kazi!
Alpherio Moris Nchimbi Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa “Baseball/Softball” Tanzania – TaBSA .

CITY FM RADIO 91.1 ya Dar-es-Salaam Yapokea Muziki wa Ngoma Africa band aka FFU UGHAIBUNI

$
0
0
Baada ya wadau wa muziki wa dansi kutaka kusikia mdundo wa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni inayongozwa na mwanamuziki Kamanda Ras Makunja uchezwe redioni, nyimbo hizo zimekabidhiwa leo katika studio za CITY FM RADIO 91.1 ya jijini Dar-es-Salaam.
Hivyo basi kutoka sasa wadau wa muziki wa dansi
watapata burudani ya kusikia nyimbo za bendi hiyo iliyojijengea umaarufu wa kimataifa na kuteka nyoyo za washabiki katika majukwaa ya kimataifa.
Ngoma Africa band imedumu katika medani ya muziki kwa takribani miaka 23 tangu ianzishwe mwaka 1993 na kiongozi wake Kamanda Ras Makunja.
pia unaweza kuwasikiliza 

UJENZI WA KIWANDA CHA DAWA ZA BINADAMU CHA ZINGA PHARMACEUTICALS KUPUNGUZA GHARAMA ZA UNUNUAJI WA DAWA KUTOKA NJE YA NCHI

$
0
0
SERIKALI imesema ujenzi wa kiwanda cha dawa za binadamu cha Zinga Pharmaceuticals katika kitongoji cha Zinga mkoa wa Pwani utasaidia sana katima kupunguza gharama za ununuaji wa dawa kutoka nje ya nchi.

Pia imesema gharama ambazo hutumia kwa mwaka kwa ajili ya ununuaji wa dawa kwa mwaka ni dola za kimarekani milioni 100.

Taarifa hiyo imetolewa na Mfamasia wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Siana Mapunjo kwa niaba ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, wakati wa mkutano wa wadau wa mradi wa kiwanda cha dawa cha Zinga, uliofanyika Bagamoyo mkoani, Pwani leo.

Mapunjo amesema kutokana na gharama ambayo serikali hutumia kunulia dawa kwa mwaka inakadiriwa kuwa hadi ifikapo mwaka 2021 kiasi cha dola za Kimarekani 350 zitatumika kwa ajili ya ununuzi huo.

“ Hadi sasa nchini tuna viwanda vya dawa za binadamu 13 ambavyo uwezo wake wa kuzalisha ni asilimia 20 na kuisababishia serikali kupoteza sh. milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa dawa,” alisema.

Amesema kiwanda cha Zinga Pharmaceuticals kitasaidia kupata dawa muhimu kwa wakati na kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania.

Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Dkt. Mary Mayige alisema kiwanda hicho kitagharimu kiasi cha sh.bilioni 70 za Kitanzania na kutarajiwa kukamilika baada ya mwaka mmoja na nusu.

“Uzalishaji wa dawa za binadamu nchini bado ni upatikanaji wake kwa hospitali binafsi na serikali umeshuka kwa kiwango mkubwa ukilinganisha na miaka iliyopita kwa hiyo kupitia kiwanda hiki tutafikia malengo,” amesema.

Dk. Mayige alizitaja dawa zitakazotengenezwa kuwa ni dawa wa kufubaza makali ya virusi vya ukimwi, antibiotiki, dawa za maumivu, malaria, magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza, shinikizo la damu na kisukari.

Naye Mwakilishi tokaWizara ya Viwanda na Uwekezaji, Elly Pallangyo, amesema uwekezaji huo umejizatiti kuweka mazingira mazuri kwa kutafsiri Tanzania ya viwanda kwa vitendo. “ Hatutaweza kufikia malengo ya Tanzania ya Viwanda kama watu wake hawatakuwa na afya nzuri,” alisema.

Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dk. Shukuru Kawambwa alisema atahakikisha anashirikiana na wawekezaji hao ili serikali iweze kutekeleza mradi huo kwa wakati.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Happyness Seneda alisema mkoa wa Pwani una jumla ya Viwanda vikubwa na vidogo 264 kati ya hivyo 88 ni vikubwa na kati, na ameahidi kwamba mkoa wa Pwani utatoa ushirikiano utakaotakiwa ili kufanikisha mradi huo ni mingine yote.

Mwakilishi wa Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto,Siana Mapunjo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa kiwanda cha dawa ya binadamu cha Zinga Pharmaceuticals mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Happyness William Seneda akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa kiwanda cha dawa ya binadamu cha Zinga leo mkoani Pwani
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa kiwanda cha dawa ya binadamu cha Zinga leo mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha zinga Dkt.Mary Mayige akiwaeleza wageni mipangilio ya Zinga Pharmaceuticals watakavyotumia utaalam wao kuzalisha dawa nyingi za binadamu zenye viwango vya kimataifa hapa nchini.
Mshauli Mkuu wa kiwanda cha dawa za binadamu Zinga kutoka Ujerumani Mhandisi Bernt Kleinmann akifafanua jambo.
Wadau wa mradi katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa ujenzi wa kiwanda cha dawa ya binadamu cha Zinga Pharmaceuticals mkoani Pwani.

Habari na picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

TEHAMA inavyoboresha utendaji kazi na uboreshaji wa huduma kwa umma katika Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania


MICHUZI TV: TUME YA HAKI ZA BINADAMU YAKEMEA VITENDO VIOVU DHIDI YA WATU WENYE UALBINO

RC MAKONDA AONGEA NA WANAHABARI MJINI DODOMA JUU YA UJIO WA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA

MASHINDANO MAKUBWA YA 18 ya KUHIFADHI QUR'AAN TUKUFU BARANI AFRIKA KUFANYIKA DAR ES SALAAM JUNI 11, 2017

TPSF YAKUTANA NA WADAU WAKE KUJADILI MAENDELEO YA UTEKELEZAJI WA SOKO LA PAMOJA LA AFRIKA MASHARIKI.

$
0
0

Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii

Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) imekutana na wadau wake kujadili utekelezaji wa Soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika  Mashariki (Common Market Protocol 2010)  tangu ilipoanzishwa upya mwaka 2010.

Wanachama wa Jumuiya hiyo walingia makubaliano ya pamoja ili kuongeza utengamano ambao ulilenga zaidi kuongeza uhuru wa watu kupita nchi za Afrika Mashariki, Kuongeza uhuru wa kusafirisha Mizigo na Biashara pamoja Uhuru wa Mitaji (Free Movement of Capital).

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika majadiliano hayo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sera – Taasisi ya Sekta Binafsi, Gilead Teri amesema kuwa wamekutana kufanya tathmini kujua changamoto pamoja na uboreshaji katika soko hilo.

Amesema wamekutana kujadili  ili baadae kutoa maoni kwa Serikali pamoja na viongozi wa Jumuiya hiyo, pia ni jinsi gani Tanzania inaweza kunufaika zaidi na soko la pamoja.

Katika soko hilo Tanzania inanufaika zaidi kupata Kodi,Wananchi kupata ajira kutokana na soko kubwa, familia kupata kipato pamoja na kukua kwa Teknolojia ya uzalishaji.
 
 Sehemu ya Wadau wa Taasisi ya Sekta Binafsi wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Sera wa TPSF, Gilead Teri.
 Mkurugenzi wa Sera – Taasisi ya Sekta Binafsi, Gilead Teri akizungumza na baadhi ya wadau wa Taasisi hiyo juu ya kujadili utekelezaji wa Soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika  Mashariki (Common Market Protocol 2010)  tangu ilipoanzishwa upya mwaka 2010.

UONGOZI MPYA WA CHAMA CHA MAWAKILI TANGANYIKA (TLS) WAJITAMBULISHA KWA KAIMU JAJI MKUU WA TANZANIA

$
0
0
Na Mary Gwera, Mahakama

KAIMU Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof.  Ibrahim Juma ameutaka Uongozi mpya wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kuusoma na kuuelewa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania ili umoja huo uweze kuchangia katika utekelezaji wake.

Prof. Juma aliyasema hayo mapema leo, Ofisini kwake, Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam alipotembelewa na Uongozi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) ukiongozwa na Rais wa Chama hicho, Mhe. Tundu Lissu.

Alisema kuwa ni vyema kuusoma Mpango Mkakati huo ili kufahamu ni wapi Mahakama inatoka na wapi inapotaka kuelekea hususani katika suala zima la maboresho ya huduma ya utoaji haki nchini.

Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania (2015/2016-2019/2010) umegawanyika katika nguzo kuu tatu ambazo ni Utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali,  Upatikanaji na utoaji haki kwa wakati na Kurejesha imani ya jamii na ushirikishwaji wa wadau,  umejikitika katika kuboresha huduma za utoaji haki kwa ujumla.

Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), amemueleza Mhe. Kaimu Jaji Mkuu kuwa lengo la ujio wao ni kujitambulisha kwake na pia kumpa pongezi Mhe. Kaimu Jaji Mkuu kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo.

Mbali na utambulisho, Mhe. Tundu Lissu alipata wasaa wa kueleza baadhi ya changamoto zinazowakabili Mawakili nchini ikiwa ni pamoja na baadhi ya Mahakama kutokuwa na Ofisi kwa ajili ya Mawakili, taratibu za usajili wa Mawakili n.k

Akijibu kuhusu hoja ya Rais wa TLS; Msajili; Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ilvin Mugeta alisema kuwa Mahakama Kuu inaendelea kufanyia kazi changamoto zote zinazowakabili Mawakili na vilevile kuona uwezekano wa taratibu za malipo kufanyika kielektroniki.

 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma (aliyeketi mbele) akiwa pamoja na baadhi ya Viongozi wapya wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) waliomtembelea kwa lengo la kujitambulisha kwake kama Uongozi mpya na pia kumpongeza Mhe. Kaimu Jaji Mkuu kwa uteuzi wake, aliyeketi kushoto kwa Mhe. Kaimu Jaji Mkuu ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali na aliyeketi kushoto kwa Kaimu Jaji Mkuu ni Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Mhe. Tundu Lissu.

 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akiongea jambo na Uongozi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) walipomtembelea Ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha.
 Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika, Mhe. Tundu Lissu akiongea jambo, Ofisini kwa Mhe. Kaimu Jaji Mkuu walipofika kwa ajili ya utambulisho wa Uongozi  mpya wa Chama hicho.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania (wa sita kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) walipomtembelea Ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha, wa tano kushoto ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, wa kwanza kushoto ni Msajili, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta na wa tano kulia ni Rais wa Chama hicho, Mhe. Tundu Lissu.(Picha na Mary Gwera)
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images