Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1629 | 1630 | (Page 1631) | 1632 | 1633 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo amefika mbele ya kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kufuatia wito wa Kamati hiyo kumtaka afike mbele ya kamati kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matashi aliyoyatoa mapema mwezi februari 2017 jijini Dar es Salaam yaliyokuwa na madai ya kudharau Bunge.

  Wito wa kufika mbele ya Kamati hiyo unafuatia Azimio la Bunge lilitolewa tarehe 8 Februari 2017 ambapo Bunge liliazimia Mhe. Spika aweze kukubali Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexandra Mnyeti na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Paul Makonda wahojiwe kutokana na Matamshi yao ya Kudharau Bunge.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akipokelewa katika Viwanja vya Bunge na Mkuu wa Kitengo cha Babari, Elimu na Mawasiliano Ndg. Owen Mwandumbya.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akihojiwa mbele ya ya kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kufuatia wito wa Kamati hiyo kumtaka afike mbele ya kamati kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matashi aliyoyatoa mapema mwezi februari 2017 jijini Dar es Salaam yaliyokuwa na madai ya kudharau Bunge. Picha na Deonisius Simba - Bunge

  0 0


   Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Elisante ole Gabriel akiteta jambo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe na wakati waziri huyo alipowasili Ofisini kwake Mjini Dodoma.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura wakati alipowasili Ofisini kwake Mjini Dodoma.
    Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akisalimiana na baadhi ya wakurugenzi na wakuu wa Taaisi zilizo chini ya Wizara yake wakati alipowasili Ofisini kwake Mjini Dodoma.
    Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisini kwake Mjini Dodoma.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0


  0 0

  KAMATI ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge ya Bunge la Jamhuri ya Uganda imetembelea Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo mafao yanayotolewa na Mfuko kwa wanachama wake.

  Ujumbe wa watu 6 kutoka nchini Uganda ulifanya ziara ya mafunzo katika Ofisi za Makao Makuu ya Mfuko jana (28/3/2017) ambapo walipata fursa ya kuona na kuelezwa mbinu na mafanikio ya Mfuko huo.

  Wabunge hao ni pamoja na Amos Lugoloobi (Mb), Muwanga Kivumbi (Mb), Kaberuka James (Mb), Felix Kaluyigye (Mb), Opolot Isiagi (Mb) na Ofisa wa Ubalozi wa Uganda nchini Tanzania Doroth Kalema.

  Akiukaribisha ujumbe huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF, Mama Anne Makinda alisema kuwa Mfuko unajisikia faraja kubwa kupata ugeni huo ambao umetambua kazi kubwa inayofanywa na NHIF na kuona umuhimu wa kufika na kujifunza ama kupata uzoefu wa namna ya utekelezaji wa shughuli hasa za utoaji wa mafao.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko Bw. Bernard Konga alitaja makundi yanayohudumiwa na Mfuko kuwa ni pamoja na Waajiriwa wa sekta rasmi, Kampuni binafsi, wanachama binafsi, wajasiliamali, watoto chini ya umri wa miaka 18, wanafunzi pamoja na viongozi wa madhehebu ya dini.

  “NHIF imefanikiwa kuwa na mtandao mkubwa wa vituo vya kutolea huduma ambapo kwa sasa ni zaidi ya vituo 6,000 na mafao wanayopata wanachama ni mengi ambayo kwa kiasi kikubwa yanaondoa usumbufu wote wakati anapopata ugonjwa,” alisema Bw. Konga.

  Kwa upande wa ujumbe huo waliupongeza Mfuko kwa kazi kubwa inayofanya lakini pia kwa ushirikiano ambao imekuwa ikionesha kwa nchi yao wakati wowote wanapokuwa na nia ya kuja kujifunza.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bernard Konga akitoa uzoefu wa huduma za Mfuko kwa Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge la Uganda ambao walitembelea kwa lengo la kupata uzoefu. Kati kati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF, Mama Anne Makinda.
  Wabunge wakipata maelezo katika Kituo cha Huduma kwa Wateja cha NHIF.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF, Mama Anne Makinda akiwa na wageni katika picha ya pamoja.
  Wageni wakiagana na Mwenyekiti wa Bodi Mama Anne Makinda baada ya kumaliza ziara yao.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

  Wafanyabiashara watatu akiwemo raia wa Zambia mmoja  wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za uhujumi uchumi ikiwemo kusafirisha bidhaa kwa  kificho

  Washtakiwa hao ambao wamefikishwa mbele ya Mahakimu wawili tofauti ni Sultani Ibrahimu, (36), mwarabu Mkazi wa Usalama Temeke, Augustino Kalumba (39) raia wa Zambia na Ramadhani Hamisi maarufu kama Ukwaju (48) anaishi Kinondoni Hananasifu.

  Wanadaiwa kutenda makosa hayo kinyume na sheria ya Umoja wa nchi za Afrika Mashariki ya kudhibiti ushuru. Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba washtakiwa Sultan Ibrahimu na Augustino Kalumba wamesomewa mashtaka matatu, la kula njama,  kusafirisha Mali iliyofichwa na kuitia hasara serikali ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania zaidi ya  shilingi milioni 287.8.

  Mwendesha mashtaka Nassoro Katuga akisaidiana na Wakili Batlida Mushi amedai kuwa kati ya Decemba 1 mwaka jana na Machi 1 mwaka huu katika eneo lisilojulikana washtakiwa hao wakiwa na wenzao ambao bado hawajakamatwa walikula njama ya kusafirisha mali.

  Katika shtaka la pili imedaiwa kuwa kati ya Decemba 1 hadi 31, mwaka jana katika makao makuu ya Bandari ya Tanzania yaliyopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam washtakiwa waliingiza magari matatu ambayo ni Range Rover sports, Zenye naomba tofauti tofauti.

  Imedaiwa kuwa magari hayo yalikuwa yamepakiwa pamoja na nguo za mitumba na viatu kwenye kontena namba MSKU 9914168 kwa nia ya kuwadanganya maafisa wa ushuru.

  Aidha washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuingiza Mali hizo wakiwa wamezificha na kuisababishia serikali ya Tanzania kuingia hasara zaidi ya shilingi 287.8.  Mbele ya Hakimu Respiciou Mwijage washtakiwa Sultan Ibrahim na Ramadhani Hamis wamesomewa mashtaka matatu.

  Imedaiwa kuwa kati ya Decemba Mosi mwaka jana na March 4 mwaka huu jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao walikula njama ya kutenda kosa la Kuficha Mzigo wakati wakiuingiza nchini.
   Imeendelea kudaiwa kuwa, kwa pamoja washtakiwa hao waliingiza Mzigo wa magari matatu wakiwa wameyaficha ili kuweza kuwaficha maafisa ushuru.

  Wakili Katuga amedai kuwa kitendo hicho kimeikosesha serikali ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania mapato zaidi ya shilingi milioni 190.9. Hata hivyo washtakiwa hao hawakuruhisiwa kujibu kitu chochote na wamerudishwa rumande kwa kuwa mashtaka dhidi yao yako chini ya sheria ya uhujumu uchumi ambayo Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kutoa dhamana.Aidha Wakili Katuga aliiarifu mahakama kuwa DPP bado hajatoa kibali kwa mahakama ya Kisutu kusikiliza kesi hiyo.

  Kesi hiyo itatajwa mahakamani hapo Aprili 12 mwaka huu. Upelelezi bado haujakamilika.

  0 0  0 0  Na Theresia Mwami – TEMESA Mwanza.

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt. Mussa Iddi Mgwatu, leo amepokea boti nne zilizokuwa zikijengwa na kampuni ya Songoro Marine Boatyard ya jijini Mwanza. Dkt. Mgwatu amesema kukamilika kwa boti hizi ni utekelezaji wa ahadi za Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa alizozitoa kwa wananchi wa Pangani Tanga pamoja na Kilambo na Msangamkuu Mtwara kwa nyakati tofauti.

  Dkt. Mgwatu ameongeza kuwa boti hizo nne zitatoa huduma za dharura hasa wakati wa usiku kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa na pia kutoa usafiri mbadala wakati vivuko vikubwa vinapokuwa haviwezi kutoa huduma kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kupungua kwa kina cha maji katika maeneo ya Kilambo mkoani Mtwara pamoja na Utete Mkoani Pwani.

  Nae Mkurugenzi kutoka kampuni ya Songoro Marine Boatyard Mhandisi Major Songoro amesema kuwa boti tatu kati ya nne zilizokabidhidhiwa zimejengwa kwa kutumia “fibre Glass” na boti moja imejengwa kwa kutumia chuma. Boti ya MV Kuchele ambayo itapelekwa katika eneo la Msangamkuu Mtwara ina uwezo wa kubeba abiria nane, sawa na boti ya MV Bweni itakayopelekwa katika eneo la Pangani mkoani Tanga. MV Mkongo itakayopelekwa Utete mkoani Pwani ina uwezo wa kubeba abiria 40 na MV. Tangazo itakayopelekwa Kilambo/Namoto Mtwara ina uwezo wa kubeba abiria 25.

  Aidha Dkt. Mgwatu ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kuwezesha ujenzi wa boti hizo na tayari amemuagiza mkandarasi huyo kuhakikisha anazisafirisha boti hizo kwenye maeneo husika haraka iwezekanavyo ili wanachi waanze kunufaika na huduma mbadala itakayotolewa na boti hizo. Ujenzi wa boti hizo umefanywa kwa kutumia fedha za ndani na umegharimu jumla ya shilingi milioni 415.
   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Ukodishaji na Huduma za Vivuko TEMESA Mhandisi Japhet Maselle, nyuma yao ni Meneja wa TEMESA mkoani Mwanza Mhandisi Ferdnand Mishamo wakati wa majaribio ya boti Mpya ya MV Mkongo  iliyojengwa kwa ajili ya kutumika katika eneo la Utete Rufiji Mkoani Pwani. Boti hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 40.
  ZA 1
  Boti tatu kati ya nne mpya zilizokabidhiwa leo kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na Kampuni ya Songoro Marine Boatyard baada ya kukamilika kwa ujenzi wake. Makabidhiano yamefanyikia jijini Mwanza na boti hizo zitasafirishwa kuelekea Pangani Tanga, Kilambo Mtwara na Msangamkuu Mtwara ili zianze kutoa huduma kwa wananchi.
  ZA 2
   Boti Mpya ya MV Kuchele iliyokabidhiwa leo kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na Kampuni ya Songoro Marine Boatyard baada ya kukamilika kwa ujenzi wake. Boti hii iliyojengwa kwa “fibre glass”ina uwezo wa kubeba abiria nane na itakuwa ikitumika nyakati za dharura katika eneo la Msangamkuu Mtwara. Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Mwanza.
  ZA 3
   Boti Mpya ya MV Tangazo  iliyokabidhiwa leo kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na Kampuni ya Songoro Marine Boatyard baada ya kukamilika kwa ujenzi wake. Boti hii iliyojengwa kwa “fibre glass”ina uwezo wa kubeba abiria 25 na itakuwa ikitumika nyakati za dharura katika eneo la Kilambo Mtwara. Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Mwanza.
  ZA 4
   Boti Mpya ya MV Bweni iliyokabidhiwa kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na Kampuni ya Songoro Marine Boatyard baada ya kukamilika kwa ujenzi wake. Boti hii iliyojengwa kwa “fibre glass”ina uwezo wa kubeba abiria nane na itakuwa ikitumika nyakati za dharura katika eneo la Kilambo Mtwara. Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Mwanza.
  Picha na Theresia Mwami – TEMESA Mwanza.

  0 0

  Na Mary Gwera, Mahakama.

  MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Mwanza imejipanga kuondoa Mashauri yote yenye umri zaidi ya miaka miwili yaliopo katika Kanda hiyo ili kuendana na azma ya Mahakama ya Tanzania ya kutokuwa na mlundikano wa kesi katika Mahakama za ngazi zote nchini.

  Hayo yalisemwa na Jaji Mfawidhi, Kanda ya Mwanza, Mhe. Robert Vincent Makaramba katika Mahojiano maalum aliyofanya na Mwandishi wa habari hii hivi karibuni ofisini kwake, Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza.

  “Mbali na agizo la Mahakama la kutaka kila Mahakama ishughulikie mashauri ya muda mrefu Mahakamani, Mahakama, Kanda ya Mwanza tayari tulishajipanga katika kuondosha Mashauri haya, na kila Jaji amejipangia namna ya kusikiliza na kutolea maamuzi mashauri hayo,” alisisitiza Jaji Makaramba.

  Aliongeza kuwa ili suala hili liweze kufanikiwa ni vyema kuwa kitu kimoja na Wadau wa Mahakama kuwezesha zoezi hili kufanikiwa na vilevile kuwa na rasilimali wezeshi kama fedha.

  Aidha; ili kuweza kufanyika kwa zoezi hili la kuondoa mlundikano wa Mashauri Mahakamani, Majaji wote saba (7) wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza pamoja na Viongozi wengine wa Mahakama hiyo ikiwa ni pamoja na Naibu Msajili na Mtendaji wa Mahakama walikutana na Wadau wa Mashauri ya Jinai na Madai ili kujadili namna bora ya kuondosha mashauri yenye umri wa miaka miwili Mahakamani.

  Kwa upande wake, Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza, Mhe. Eugenia Rujwahuka alisema kuwa zoezi la kuondosha mashauri haya linatakiwa liwe limekamilika kufikia mwezi wa tano mwaka huu.

  “Kikao hicho kilichojumuisha Wadau mbalimbali kama Mawakili, Waendesha Mashitaka, Magereza n.k, kililenga katika kujipanga ili kufanikisha usikilizaji wa Mashauri ya Mauaji katika vikao maalum vitakavyoanza Aprili, 24, mwaka huu hadi hadi Mei, 24 mwaka huu,” alisema Naibu Msajili.

  Mhe. Rujwahuka aliongeza kuwa jumla ya Mashauri 107 yamepangwa kusikilizwa katika vikao hivyo ambavyo vitafanyika Tarime, Sengerema, Magu, Geita, Mwanza na Musoma.

  Hata hivyo; katika kikao hicho kati ya Mahakama na Wadau wake walikubaliana kushirikiana ili kufanikisha zoezi zima la uondoshaji wa mrundikano wa mashauri.

  Katika muendelezo wa uboreshaji wa huduma ya Utoaji haki nchini Mahakama ya Tanzania imedhamiria kuondoa mlundikano wa kesi katika Mahakama zake.
  Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Mwanza akiongea jambo katika kikao hicho, pamoja nae wanaoonekana katika picha ni baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza ambayo ina jumla ya Majaji saba (7).   Baadhi ya Watumishi wa Mahakama na Wadau wakiwa katika kikao hicho.
  Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza wakiwa katika kikao pamoja na Wadau wa Mahakama wa Kanda hiyo (hawapo pichani) kilichofanyika hivi karibuni, wa kwanza kulia ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza, Mhe. Eugenia Rujwahuka.


  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akizungumza wakati wa uzinduzi wa Warsha ya umuhimu wa taasisi katika Maendeeo ya Viwanda nchini kwa watafiti iliyoandaliwa na taasisi ya REPOA
   Mkurugenzi mkuu wa REPOA Tanzania, Dr Donald Mmari akizungumza juu ya taasisi hiyo na mudhui ya mkutano kwa watafiti
   Baadhi ya wabunge wa Bunge la jamhuri ya Muungano Tanzania wakiwa katika mkutano huo
   Kiongozi wa umoja wa Ulaya  Roeland Van De Geer akizungumza wakati wa mkutano huo
   Profesa Lant Pritchett  kutoka chuo kikuu cha Havard Marekani akizungumza mara baada ya ufunguzi wa Warsha hiyo Prof Lant ni mmoja wa watoa mada wakuu waliofika katika mkutano huo
   Baadhi ya Washiriki wakiwa katika mkutano huo wakisikiliza mada kutoka kwa Prof Lant.

  0 0  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

  Watanzania wenye vipaji wametakiwa kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza na wamewataka wajitokeze kwa wingi katika mafunzo ya kucheza yatakayoendeshwa na Mtanzania Emanuel Houston anayeishi Nchini Ujerumani.

  Emanuel ameambatana na baba yake Luis Houston ambao wote wanaishi nchini Ujeruami na wataendesha mafunzo hayo kupitia taasisi ya Unleashead Academy iliyo chini ya Halila Mbowe.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Emanuel amesema kuwa anafurahi kuja kuwafundisha vijana wa kitanzania namna ya kucheza na watapata fursa ya kumuuliza kitu chochote.

  Emanuel amesema kuwa, kuja kwake nchini Tanzania anategemea kuona vijana wengi kuja kujifunza kwani katika nchi za Ulaya watu wanaanza kujifunza mapema zaidi wakiwa na umri mdogo ndiyo maana wanaweza kufika mbali katika sekta mbalimbali.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Unleashed Academy Halila Mbowe amesema wanafuraha sana kuweza kuwakaribisha vijana katika kituo chao na pia kushirikiana na Emanuel Houston pamoja na Ben Pol kuja kuandaa mafunzo hayo kwa vijana.

  Halila amesema kuwa kituo chake kinajihusisha na masuala ya kuinua vipaji katika kucheza mziki na kuandika mashairi na wameweza kupata vijana wengi na na takribani 25 tayari wameshaingia katika mashindano makubwa.

  Baba yake na Emanuel, Luis Houston amesema kuwa alianza kukijua kipaji cha mwanae toka alivyokuwa mdogo na akamwambia kuwa utakuja kuwa mcheza mziki (dancer) na kweli mpaka sasa ameweza kuendesha maisha yake kupitia kucheza na ameshafungua kituo cha mafunzo nchini Ujerumani na ana wanafunzi takribani 15000.

  Mafunzo hayo yanatarajiwa kuwa kesho katika studio za Unleashead zilizopo Mikocheni B na itaanza saa 9-11 alasiri na hakutakuwa na kiingilio chochote.

  Mtanzania Emanuel Houston akizungumza na waandushi wa habari kuhusiana na mafunzo ya kucheza yatakayoendeshwa nae hapo kesho chini ya Unleashed Academy, kushoto ni msanii na mratibu wa mafunzo hayo Bernad Paul 'Ben Pol' na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Unleashed 

  Academy Halila Mbowe.


  Mkurugenzi Mtendaji wa Unleashed Academy Halila Mbowe akizungumzia jinis kituo chake kinavyofanya kazi katika kuinua vipaji vya vijana wa kitanzania katika kucheza na kutunga mashairi, Kulia ni Luis Houston ambaye ni baba yake na Emanuel Houston (wa pili kushoto) na    msanii na mratibu wa mafunzo hayo Bernad Paul 'Ben Pol' 

  0 0

   Waahidi kuendelea kusaidia sekta ya nishati nchini

  Na Veronica Simba – Singida

  Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hamme-Hanie Kaarstad na Balozi Katarina Rangnitly anayewakilisha Sweden hapa nchini, wameipongeza Serikali kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa miradi ya umeme vijijini, hivyo wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano hususan katika sekta ya nishati.

  Wakizungumza hivi karibuni, kwa nyakati tofauti, katika uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Usambazaji wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kwa Mkoa wa Singida, Mabalozi hao walisema Serikali za nchi zao zinafurahi kuona jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha wananchi, hususan wa vijijini wanapata umeme wa uhakika na wa bei nafuu.

  Akizungumzia kuhusu Mradi wa REA III mkoani Singida, Balozi Kaarstad, mbali na kumshukuru Rais John Pombe Magufuli, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo pamoja na watendaji wengine wa Wizara kwa kuwezesha kutekelezwa kwa miradi husika ya umeme vijijini, alisema kuwa ni matarajio yake kwamba Mradi utawezesha maisha ya wananchi wa Singida kuwa mazuri zaidi.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akiwatambulisha Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hamme-Hanie Kaarstad (katukati) na Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitly (kulia); kwa wananchi (hawapo pichani) waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kwa Mkoa wa Singida.

   Kamishna wa Nishati na Masuala ya Mafuta, Mhandisi Innocent Luoga (mwenye suti nyeusi) na Afisa kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) (wa pili kutoka kushoto), wakiwatafsiria kwa lugha ya kiingereza wageni walioambatana na Mabalozi wa Sweden na Norway katika hafla ya uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kwa Mkoa wa Singida.
  Sehemu ya umati wa wananchi waliohudhuria katika hafla ya  uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kwa Mkoa wa Singida.
  0 0

  Na Hassan Matimbwa

  Marehemu TX Moshi alifariki tarehe 29 Machi mwaka 2006 siku ya JUMATANO majira ya saa 3 asubuhi na kuzikwa siku hiyo hiyo makaburi ya Keko machungwa.

  Tarehe na siku ya kifo chake vimejirudia mwaka huu na siku hiyo hua kuna Show ya Msondo ktk ukumbi wa Sugar Ray kwa Sokota. Marehemu TX alijiunga Msondo mwaka 1982 akitokea Polisi Jazz. Miongoni mwa nyimbo alizotunga mara baada ya kujiunga ni pamoja na Ajuza, Asha Mwanaseif, (aliomtungia mkewe), na Ashibaye.
  Alitunga nyimbo nyingi lakini nyimbo zilizotia fora sana ni pamoja na Kilio cha Mtu Mzima, Ndoa Ndoano, Piga Ua Talaka Utatoa, Ndoa ya Isihaka Kibene, Kaza Moyo na Ajali.
  Wimbo wa Ajali aliutunga baada ya kupata ajali ya kuparamia mti wa mvinje pale Mivinjeni Desemba 16, 2005 iliyompelekea kuvunjika mguu.

  Moshi alikua chakaramu na mbunifu wa kutunga vionjo ikiwemo mtindo ujulikanao kama Mambo Hadharani na katika nyimbo alipenda kuchombeza vionjo vyenye kutoa raha na kunogesha wimbo mfano utasikia "we nani", " kidogo tu..kidogo tu", "kwanini lakini", " watoto wanachezea umeme", "dispilin", " fair play" nk.
  Wakati wa uhai wake alipitia katika bendi mbalimbali za muziki ambazo ni pamoja na Safari Trippers, Juwata Jazz. UDA Jazz, na Polisi Jazz, ambayo alitokea wakati anajiunga msondo. Tz pis alijaliwa kupata tuzo mbalimbali mfululizo za muziki kama Kilimanjaro Music Award.
  Marehemu Moshi alibatizwa jina la TX, na Mwandishi wa Habari wa siku nyingi aliyekuwa mtangazaji wa Radio Tanzania, marehemu Julius Nyaisanga. Nyaisanga alimbatiza jina hilo kutokana na tunzi zake za uhakika. Nyaisanga alikua mtangazaji wa RTD na kisha vituo vya IPP Media. Jina halisi la TX ni Shaaban Mhoja Kishiwa ingawa alikuwa akijulikana zaidi kwa jina la Moshi William TX.
  Hakika Tx Moshi, aliyezaliwa mwaka 1958 huko Korogwe, Tanga, ameacha pengo na kumbukumbu isiyosahaulika kwa wapenzi wa Msondo na ulimwengu wa muziki wa Dansi Tanzania. Tarehe 29 wana Msondo tumkumbuke.


  0 0

   Katibu wa Bodi ya Wadhamini  ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi akisoma taarifa ya Taasisi katika kikao cha kwanza cha Bodi hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ambaye pia ni Daktari Bingwa wa upasuaji wa Magonjwa ya Moyo na mishipa ya damu Prof. William Mahalu.
   Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini  ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia  taarifa ya Taasisi hiyo iliyokuwa  ikisomwa na Katibu ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi katika kikao cha kwanza cha Bodi  kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

   Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini  ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia  taarifa ya Taasisi hiyo iliyokuwa  ikisomwa na Katibu ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi katika kikao cha kwanza cha Bodi  kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  Mwenyekiti  wa Bodi ya Wadhamini  ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Daktari Bingwa wa upasuaji wa Magonjwa ya Moyo na mishipa ya damu Prof. William Mahalu akiongoza kikao cha kwanza cha bodi hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Picha na Anna Nkinda wa JKCI


  0 0  0 0


  0 0

   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kuendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM leo jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti CCM (Zanzibar) Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakiwa pamoja na Wajumbe wengine wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho jijini Dar es Salaam.

   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti CCM (Zanzibar) Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha  Mapinduzi CCM kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha  Mapinduzi CCM Dkt. Salim Ahmed Salim mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha  Mapinduzi CCM kilichofanyika jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


  0 0


  Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri wa miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys Leo Jamatano wamefanya mazoezi kujiweka tayari na mchezo wao wa kesho na Timu ya U17 ya Burundi.
  Serengeti Boys itakuwa kambini Bukoba hadi Aprili 2, mwaka huu ambako inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu vijana ya Burundi kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani hapa Kagera. Michezo hiyo itaanza kuchezwa Machi 30, 2017 na kurudiana Aprili mosi, mwaka huu. 
  Serengeti Boys ambayo inajiandaa na michuano Afrika huko Gabon itarejea Dar es Salaam Aprili 2, mwaka huu ambako imepangwa kucheza na Ghana Aprili 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.


  Serengeti Boys ni timu ya vijana ambayo imefuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14, mwaka huu. Timu hiyo imepangwa Kundi ‘B’ pamoja na mabingwa watetezi Mali, Niger na Angola. Ina lengo la kurejea na Kombe la Afrika kwa vijana. 
  Na ikitokea imekosa nafasi hiyo angalau ikafika nusu fainali ambako kwa mafanikio hayo itakuwa tayari ina tiketi mkononi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia huko India, Novemba, mwaka huu. 


  Serengeti Boys watacheza mchezo wao wa kwanza leo jioni katika uwanja wa Kaitaba na tayari timu ya U17 ya Burundi ambayo imeingia Bukoba hii jana jioni kwenye muda wa saa 11, ila hawakuweza kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Kaitaba kutokana na uchovu wa safari yao na hivyo kutoa taarifa kuwa watafanya asubuhi saa moja. 

  0 0


  0 0


  Picha na habari na Faustine Rutta
  Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburu(wa pili) kutoka kushoto akiwa na  Viongozi wa Tawi la Kichwabuta lililozinduliwa jana kwa shangwe na nderemo mjini Bukoba. 
  Tawi hilo limepewa Jina la Kichwabuta kutokana na kuenzi kazi ya Mwananchama maarufu wa Klabu ya Simba MZEE HUSSEIN OMARY KICHWABUTA ambaye alishiriki kikamilifu kama mpenzi na Mwanachama wa Simba katika maendeleo ya Klabu hiyo ya Simba. 
  Tawi hilo mpaka sasa lina Wanachama 160 waliojiandikisha na taratibu zinaendelea kuhakikisha wanapata kadi za uanachama kulingana na utaratibu wa Klabu. 
  Tawi linaongozwa na Mwenyekiti Ndugu Priscus Isdory Massawe, Katibu ndg. Fauzu BinaMungu, Mhasibu Ndg. Dickson Ishengoma, Msemaji Ndg. Miraji Kichwabuta na Viongozi wengine ili kuhakikisha wanapata Wanachama wengi zaidi.

older | 1 | .... | 1629 | 1630 | (Page 1631) | 1632 | 1633 | .... | 3272 | newer