Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1631 | 1632 | (Page 1633) | 1634 | 1635 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Na Othman Khamis Ame, OMPR
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewasili Zanzibar mapema leo asubuhi akitokea nchini India ambako alifanya ziara ya wiki moja.Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Balozi Seif aliyeambatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi alipokewa na Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Watendaji wakuu wa Serikali pamoja na baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Siasa.Balozi Seif ambae aliuongoza Ujumbe wa Mawaziri wawili, Naibu Waziri  na Makatibu wakuu alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Viongozi wa Taasisi na Makampuni mbali mbali ya vitega uchumi.Miongoni mwa Taasisi na makampuni hayo ni yale yanayojishughulisha na sekta ya Afya,Kilimo pamoja na Makampuni ya ujenzi.Ziara ya Balozi Seif na Ujumbe wake imeonyesha matumaini makubwa kutokana na Taasisi na baadhi ya Makampuni kuonyesha nia na muelekeo wa kutaka kuzitumia fursa za uwekezaji zilizopo Visiwani Zanzibar.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokewa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud alipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar baada ya kumaliza ziara yake ya Wiki Mopja Nchini India. Kulia ya Mh. Ayoub ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Issa Haji Gavu na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi Dr. Sira Ubwa Mamboya.
    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Issa Haji  Ussi Gavu akimkaribisha Balozi Seif mara tu baada ya kuwasili Zanzibar. Wa kwanza kutoka Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Rashid Ali Juma.
   Mjumbe wa Baraza na Mapinduzi ambae pia ni Waziri asiye na Wizara Maalum Mh. Said Soud akimlaki Balozi Seif katika mapokezi hayo.
  Kulia ya Mh. Soud ni Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiye na Wizara Maalum Mh. Ali Juma Khatib na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib.
  Balozi Seif na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi wakimalizia kusalimiana na Viongozi mbali mbali wa serikali waliofika kuwapokea wakitokea Nchini India. Picha na OMPR – ZNZ.

  0 0

   Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba,  akitoa ufafanuzi  kuhusu utekelezaji wa majukumu ya wizara yake kwa Bajeti ya mwaka wa fedha wa  uliopita katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa Mapitio ya Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma. 

   Katibu Mkuu wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira wa kwanza kulia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo, Balozi  Hassan Simba Yahaya anayemfuatia wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa ukitolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini [IGP] Ernest  Mangu aliyesimama  kuhusu Oparesheni mbalimbali za kuzuia uhalifu hapa nchini, wakati wa Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa Mapitio ya Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma. 

   Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr.  Anna Peter Makakala, akiwa pamoja na watendaji wengine wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, akimfuatilia kwa makini Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Balozi  Adad Rajab wakati Mwenyekiti huyo hayupo pichani, akiwaongoza Wajumbe wa Kamati hiyo kuipitia Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bjeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma.   
   Katibu Mkuu wa Wizara Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira wa kwanza kulia na Naibu Katibu Mkuu wake, Balozi  Hassan Simba Yahaya wakifuatilia kwa makini Bajeti ya Jeshi la Polisi ya mwaka ujao wa fedha,  katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa Mapitio ya Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo, ambapo kwa siku ya leo Kamati hiyo imepitisha Bajeti za Jeshi la Polisi na Fungu Hamsini na Moja inayobeba Idara Saidizi ndani ya wizara, hatua ambayo ni muhimu kufikiwa kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma. 


  Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba,  akisoma taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha wa  uliopita katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kabla ya Mapitio ya Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma  mkoani Dodoma.
  PICHA ZOTE NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YANCHI


  0 0

   Jumapili March 26,2017 ilikuwa siku muhimu kwa mwanahabari wa 102.5 Lake Fm Mwanza na mwanablogu wa BMG, George Binagi wa Tarime Mara pamoja na Miss Upendo Kisaka wa Moshi Kilimanjaro baada ya kuuaga ukapera.
  Wapendanao hao walifunga pingu za maisha katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza na baadaye hafla kufanyika Ukumbi wa Sun City Hotel, Ghana Green View Jijini Mwanza.
  Tazama video hii chini.

  0 0


  0 0

  Na Faustine Ruta, Bukoba
  Timu ya Vijana U17 ya Burudi leo kwenye uwanja wa Kaitaba imeanza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki kwa kichapo cha bao 3-0 na Timu ya Vijana maarufu kwa jina la Serengeti Boys.
  Bao la kwanza lilifungwa dakika ya 20 na Muhsin Malima Makame bao la pili lilifungwa dakika ya 38 na Nickson Clement Kibabage huku bao la tatu likifungwa kwa mkwaju wa penati na kepteni  Kevin Nashon Naftal dakika ya 72 baada ya beki wa Burundi kujichanganya kwa kuunawa mpira ndani ya boksi.
  Mchezo wa marudiano wa timu hizi utachezwa Jumamosi hapa hapa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, kabla ya Serengeti kupanda ndege kwenda Jijini Dar es Salaam kucheza na U-17 ya Ghana Jumatatu  kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera. 

  Kikosi cha Burundi chini ya Miaka 17 kilichoanza dhidi ya Serengeti Boys ya Tanzania. Picha  na habari/ Faustine Ruta.
  Kikosi cha Serengeti Boys kilichoanza leo kwenye mchezo wa kirafiki kwenye Uwanja wa Kaitaba.

  0 0

  C
   Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akimpa pole   Mama Janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe na Waziri wa Kwanza wa Ushirika na Masoko katika Baraza la Mawaziri chini ya Serikali ya Madaraka na baadaye Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Ndani baada ya  Uhuru, Marehemu Clement George Kahama maarufu kama `Sir George Kahama’ aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam. 
  C 1
  Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akishiriki katika sala na Mama Janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe Marehemu Clement George  Kahama maarufu kama `Sir George Kahama’ na ndugu, marafiki na jamaa wa familia ya marehemu aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam.
  C 2
   Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akiweka saini kitabu cha maombolezo baada ya kumfariji  Mama Janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe na Waziri wa Kwanza wa  Ushirika na Masoko katika Baraza la Mawaziri chini ya Serikali ya  Madaraka na baadaye Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Ndani baada ya Uhuru, Marehemu Clement George Kahama maarufu kama  `Sir George Kahama’  aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mama Janeth Kahama, Mama Evelyn Warioba, Anna Kahama-Rupia, Mama Rahma Bomani,Mama Getrude Luangisa, Mama Ishengoma, Mama Feruzi na Mama Tunu Mwapachu.
  C 3
  Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akiagana na  Mama Janeth Kahama, baada ya kumpa pole Mjane huyo wa mwanasiasa  mkongwe Marehemu Clement George Kahama maarufu kama `Sir George Kahama’ aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam.  PICHA NA IKULU

  0 0


  *Amtaka Waziri wa Maji avunje mkataba ifikapo Mei 31
  *Ni mkandarasi aliyenyang’anywa pasipoti na Rais Magufuli

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitavumilia wakandarasi wasio na uwezo na ambao wanapewa kazi lakini wanashindwa kuzimaliza katika muda uliopangwa.
  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo, leo (Alhamisi, Machi 30, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa Halmamshauri ya Chalinze na wale wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (CHALIWASA) katika ofisi zao, karibu na daraja la mto Wami, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.
  Alikuwa ameenda kukagua mradi wa upanuzi wa mtambo wa maji Chalinze na ujenzi wa mfumo wa kusafirisha na kusambaza majisafi pamoja na matenki ya kuhifadhia maji ambao umechukua muda mrefu lakini haujakamilika. Awamu ya kwanza ilianza mwaka Septemba mosi 2001 na kukamilika Desemba mosi 2003.
  Amemuagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge ahakikishe kuwa kazi ya ujenzi wa mradi huo inaimarika na kufikia asilimia 80 la sivyo, wakamilishe taratibu za kukatisha mkataba na kutafuta mkandarasi mwingine.
  Agizo la Waziri Mkuu linafuatia taarifa aliyopewa kwamba mkandarasi wa mradi huo, Overseas Infrastructure Alliance (OIA) Pvt Ltd ya India alipaswa kumaliza kazi hiyo Februari 22, mwaka huu lakini hadi sasa mradi huo umekamilika kwa asilimia 23 tu.
  “Nimeelezwa kwamba mmempatia nyongeza ya siku 100 ambayo inaisha tarehe 31 Mei 2017, kama kazi yake haitakuwa ya kuridhisha na kufikia walau asilimia 80, itabidi Mheshimiwa Waziri uendelee na taratibu zako za kukatisha mkataba, tuanze kutafuta mkandarasi mwingine,” amesema.


  0 0

  Na Salum Vuai, MAELEZO - Zanzibar
  JUMATATU ya tarehe 27 Machi, 2017, niliamua kuakhirisha mambo yangu mengine yaliyokuwemo kwenye ratiba yangu na kuamua kufunga safari hadi mtaa wa Chumbuni, Wilaya ya Mjini Unguja.


  Nia yangu ilikuwa kwenda kumjulia hali msanii mkongwe wa Zanzibar, Mzee Haji Gora Haji (pichani), ambaye kwa miezi kadhaa sasa nyendo zake zimekatika kutokana na kusumbuliwa na maradhi.


  Gwiji huyu wa sanaa mbalimbali ikiwemo ushairi, uandishi wa vitabu vya hadithi fupi, tenzi na mashairi ya nyimbo, ni miongoni mwa watu muhimu katika historia na tasnia ya usanii hapa nchini.


  Kwangu mimi, na ninaamini kwa wengine wanaopenda sanaa, Mzee Gora aliyezaliwa mwaka 1933 kijijini Tumbatu, ni mwalimu na mlezi katika kuwafinyanga washairi chipukizi na wa makamu ambao bado wanaendelea kujifunza kwa kuamini kwamba sanaa ni utamaduni endelevu unaokuja kivyengine kadiri siku na mambo yanavyobadilika.


  Ingawa nilikuwa nikipanga kumtembelea siku nyengine isiyokuwa tarehe 27 Machi niliyoitaja awali, lakini nililazimika kubadili mpango huo na kuamua kuwahisha ziara yangu hiyo kutokana na jambo maalumu liliougusa mtima wangu usiku wa Machi 26, mwaka huu.

  Ni jambo gani hilo? Endelea kusoma makala haya mstari kwa mstari, neno kwa neno, herufi kwa herufi ili ulijue.

  0 0


  Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe ametoa wito kwa wasanii nchini kutovuka mipaka katika utengenezaji wa kazi zao mpaka kufikia hatua ya kuvunja Sheria na taratibu za nchi.

  Ameyasema hayo Mjini Dodoma jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego kwa mwaliko wa Waziri huyo.

  Amesema kuwa wasanii ni nguzo muhimu katika nchi sio kwa kufanya kazi ya kuburudisha na kuelimisha bali katika kuujenga Utamaduni wa nchi ambao ndio nguzo muhimu sana kwa malezi na makuzi ya wanajamii.

  “Niwaombe wasanii nchini kuzingatia Sheria na taratibu za nchi katika utunzi wao na utenegenezaji wao wa kazi zao” Alisisitiza Mhe. Dkt Mwakyembe.

  Aidha ameongeza kuwa Serikali haina nia ya kuwanyima uhuru wa kujieleza bali watambue kuwa nchi inaendeshwa kwa taratibu na Sheria ambazo zinatakiwa zifuatwe na watu wote.

  Kwa upande wake Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa kuwaunga mkono wasanii nchini na kuahidi kuongeza baadhi ya mambo katika wimbo wake wa “Wapo” na kuwaalika watanzania kama kuna kero zingine zinazowasumbua katika jamii wasiwasilishe kwake ili azizungumzie katika wimbo huo.

  “Namshukuru Mhe. Rais kwa kutuunga mkono pia naahidi kufanya “remix” ya wimbo wa “Wapo” kwa kuongeza maneno niliyoshauriwa na Mhe Rais na Mhe. Waziri na kama kuna mengine kutoka kwa wananchi pia niko tayari kuyapokea na kuyafanyia kazi” alisema Bw. Elibariki.

  Hivi karibuni wimbo wa “Wapo” wa Msanii Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego ulifungiwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kosa la kutozingatia maadili na baadae kufunguliwa kwa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kupitia Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe.


  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akisalimiana na Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego kwa mwaliko Ofisini kwake Mjini Dodoma kufanya mazungumzo yahusuyo mambo ya Sanaa ya Muziki.

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa  Mitego akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe Mjini Dodoma kwa mazungumzo.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego mara baada ya mazungumzo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mazungumzo na Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego Ofisini kwake Mjini Dodoma. 
  Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mazungumzo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe Mjini Dodoma.Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma

  0 0


   A stop order issued by Tanzania Government on March 3rd 2017 barring mining companies to export copper concentrates for smelting outside the country has significantly exposed Acacia, which exports the stuff from Buzwagi and Bulyanhulu mining projects.

  Acacia statement opens a can of worms
  On March 15th 2017 Acacia Chief Executive Officer (CEO), Brad Gordon responded officially pertaining to the Government order. The CEO is quoted expressing jittery for Acacia incurring loss of US$17 million (Tzs. 37 billion) in just two weeks of executing Government stop order.

   He is concerned if the stop order is maintained Acacia may fail to continue running operations because export of copper concentrates accounts for 50 percent of Acacia earnings from Buzwagi and Bulyanhulu mining projects. This statement exposes the vital information not previously disclosed to Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI). Actually, it opens a can of worms. Acacia is TEITI member with obligation to correctly disclose material production and Government payments information pertaining to its mining operations in Tanzania.

  But reading Acacia statement we note the implication that Acacia had since TEITI launch (2009) disclosed only half the production and payments value data from Buzwagi and Bulyanhulu mining projects. And this sends bad signal to TEITI because it discounts material information and data compiled and published in the successive annual reports since 2011. The credibility of TEITI reports’ data and integrity of entire EITI work in Tanzania is exposed to irreparable risk if corrective remedies are not done in real time. Acacia has the obligation and should therefore come out immediately to patch up the anomaly.   

  Acacia statement exposes a gap in the TEITI reports.

  The quantity of gold or money value declared as having been produced or earned by Acacia and therefore payments made to government in the form of royalties, taxes, fees, levies, duties and statutory contributions should be correctly captured and documented in the TEITI reports. However, that may not be the case when we evaluate inherent logic exposed by Acacia statement. The payment data documented in the TEITI reports from Pangea Minerals Ltd (Buzwagi) and Bulyanhulu only present half the story. None of the six TEITI reports (2008/09 – 2013/14), has documented either quantity or value of copper concentrates, which according to Acacia, account for 50 percent of Bulyanhulu and Buzwagi revenue combined.

  The documented evidence available at TEITI indicates during the 2012/13 fiscal year, Pangea Minerals Ltd (Buzwagi goldmine) produced 205,240 ounces of gold worth Tzs. 520.9 billion (US$328,025,425) while Bulyanhulu goldmine produced 197,571 ounces of gold worth Tzs. 477.1 billion (US$300,413,402) (TEITI Report 5th, 2015:11). Again, the data documented during the subsequent fiscal year show no difference. 

  Bulyanhulu is recorded to have produced 192,550 ounces of gold worth Tzs. 430.5 billion (US$265,884,907) while Pangea Minerals (Buzwagi) produced 198,995 ounces of gold worth Tzs. 384,539,239,000 (US$237,516,516) (TEITI Report 6th, 2015:10). Not only are the quantity and value of copper concentrates exported from Buzwagi and Bulyanhulu missing from the duo fiscal years’ TEITI reports, but also are entirely not documented in the previous four reports.

  There is one more controversial issue, which previously, Acacia hadn’t disclosed yet, but it is implied in the statement. The statement underscores that Acacia exports (sells) copper concentrates to foreign buyers rather than sending the stuff for smelting outside the country where appropriate technology is available. This means the ownership title of copper concentrates changes from Acacia to a foreign buyer immediately the stuffs are exported. 

  This notion is new to Tanzanians, who hitherto held common knowledge that Acacia sends copper concentrates to foreign countries with appropriate technology for smelting the stuff, which whatsoever, wouldn’t involve ownership title transfer from Acacia to a foreign entity. That being the case, Acacia would be expected to report such significant transaction to TEITI because copper concentrates and gold are materially different. The local media quoting persons involved in the export of copper concentrates from the Tanzania Mineral Audit Agency (TMAA), Tanzania Ports Authority (TPA) and Acacia officials estimate 50,000 [8ft (2.43m) x 8.5ft (2.59m) x 40ft (12.2m)] containers of copper concentrates have had been shipped annually.    

  Our Position and recommendations
  The Coalition of Tanzania Civil Society Members of global EITI Association (TEICS) considers the amount of money raised from export of copper concentrate but Acacia hadn’t reported to TEITI for public scrutiny is significant enough to alter both TEITI reports and Government records of payment received from Acacia. Disclosure of these payments is even more urgent than ever considering Acacia nonpayment of Corporate Income Tax (CIT) since the company started (1998) operating in Tanzania up to 2016, on the ground that the company is still recuperating losses incurred during the investment startup phase.
           
  We, TEICS, recommend and call upon:-

  1.That Acacia should disclose all details related to quantity and proceeds obtained from exports of copper concentrates since 2001 to 2017. Data presentation should comply with the EITI recommended pattern of data disaggregation – project by project and year by year – to allow and facilitate ease use by TEITI and Government.

  2. That TETI Committee should immediately start retrospective review and upscale all previous TEITI reports’ data to accommodate significant material information disclosed by Acacia reflecting proceeds from annual exports of copper concentrates.

  3. That the Government of the United Republic of Tanzania should assume leadership to evaluate the Mineral Development Agreement (MDAs) entered with Acacia to establish parties’ consistency and compliance with agreed terms therein, and thereafter, in consultation with Acacia, correct inconsistencies in the MDAs, if any, and ensure Acacia repays all the unpaid royalties, taxes, fees, levies, duties and statutory contributions resulting from exports of copper concentrates for entire period effectively from 2001 to 2017.    

  4.  That the media should follow up and report to public about the actions taken by Acacia, TEITI Committee and the Government to correct the anomaly caused by Acacia not disclosing copper concentrates export business to TEITI and Government.


  Issued and signed on behalf of TEICS members today, 30th March 2017, by

  Bubelwa Kaiza
  Coordinator

  0 0
  0 0

  Wanawake na vijana ni nyenzo muhimu katika uhamasishaji wa kumaliza machafuko yanayoendelea nchini Somalia, wakati kundi hilo pia likilengwa zaidi na vikundi vya kigaidi kutumika katika matukio ya kigaidi. 

  Hayo yamebainishwa na Bi. Mane Ahmed, Afisa Jinsia kutoka African Union Mission in Somalia (AMISOM), wakati wa mkutano wa siku tatu unaomalizika leo (Ijumaa) jijini Dar es Salaam jana.

  Mkutano huo ulioandaliwa na AMISOM kwa ushirikiano na serikali ya Somalia unalenga kutafuta njia stahiki za kuzuia vijana kudahiliwa na vikundi vya kigaidi nchini humo.

  Pamoja na mambo mengine, mkutano huo umebainisha umuhimu wa ujengaji uwezo kama hatua madhubuti katika kueneza hali ya kuvumiliana ndani ya jamii na kuwapa sifa mbaya Al-Shabaab.

  Akizungumza mkutanoni hapo, Bi Mane amesema kuwa Serikali ya Somalia imeanzisha ofisi ijulikanayo kama Counter-Violent Extremism (CVE) ikiwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na kukamilisha rasimu ya kwanza ya Sera ya Kuzuia na Kupambana na Vikundi vyenye msimamo mkali.

  Bi Mane alisema kuwa AMISOM imeanzisha Mtandao wa Kijinsia ambao umelenga katika kuzuia na kupambana na vikundi vyenye msimamo mkali kwa lengo la kusaidia juhudi za Shirikisho katika kuunganisha mtazamo wa kijinsia katika mpango na mikakati yake.

  Bi Muna alisema: "Mkutano huu utawajengea uwezo viongozi wa dini, watendaji wa Somalia na kuongeza ufahamu wao juu ya umuhimu wa kuwajumuisha wanawake katika njia yao za kupambana na siasa kali na kubadilishana uzoefu na mbinu bora na wataalamu, watafiti, watendaji kutoka barani ambao wana ufanisi mkubwa katika kukabiliana na masuala yahusuyo vikundi vyenye misimamo mikali."

  Bi. Mane Ahmed, Afisa Jinsia kutoka African Union Mission in Somalia (AMISOM) akizungumza na waandishi wakati wa mkutano huo.

  Washiriki wa mkutano huo wakifatilia mada zilizowasilishwa wakati wa mkutano huo  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL, Bw. Lasislaus Matindi anasema wamefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 9 kwa Miezi minne tu kwa kutumia ndege hizo mbili zilizonunuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, nakuleta utata mkubwa na wapinzani wa siasa nchini waliodai kuwa hazikuwa na tija kwa Taifa. 
  Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania Corporation, ATC); katika Shirika hilo, Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC. Hata hivyo ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya kiuendeshaji na kulazimika kusitishwa mwezi Agosti 2006 na ATCL kurejeshwa tena Serikalini kwa asilimia 100.
  KUMBUKUMBU:
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa na viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam Jumatano Septemba 28, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na maafisa wengine waandamizi wakiwa kwenye ndege mojawapo baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam Jumatano Septemba 28, 2016. PICHA NA IKULU.

  0 0  0 0


  0 0

  Mgeni rasmi; Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dr. Moses Kusiluka akiongoza maandamano na viongozi wa Chuo cha Ardhi – Morogoro, pamoja na Mkuu wa Chuo cha Ardhi – Tabora, Bwn. Justo Lyamuya, wakati wa maafali ya 35 ya chuo cha Ardhi – Morogoro.
  Mgeni rasmi; Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dr. Moses Kusiluka akitoa hotuba katika maafali ya 35 ya Chuo cha ardhi Morogoro, kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ardhi – Morogoroius; Bwn. Desderius Kimbe, anayemfuatia ni Mkuu wa Chuo cha Ardhi – Tabora; Bwn. Justo Lyamuya.
  Katika picha ya pamoja na wahitimu na baadhi ya wanafunzi, katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dr. Moses Kusiluka, kushoto kwake ni; Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ardhi – Morogoro Bwn. Desderius Kimbe na kulia kwake ni Mkuu wa Chuo cha Ardhi – Tabora, Bwn. Justo Lyamuya. 
  Mkuu wa Chuo cha Ardhi – Tabora, Bwn. Justo Lyamuya akitoa maelezo ya kina kuhusu matumizi ya kifaa cha upimaji Ardhi kwa baadhi ya waalikwa wa Maafali ya 35 ya Chuo cha Ardhi – Morogoro.
  Mgeni rasmi; Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dr. Moses Kusiluka akifuatilia kwa makini maelekezo ya Mwanafunzi wa Chuo cha Ardhi – Morogoro, ambaye alikuwa akionyesha jinsi ya kutumia kifaa cha upimaji Ardhi, wakati wa maafali ya 35 ya chuo cha Ardhi – Morogoro.

  0 0

  Wateja wa mtandao wa mawasiliano wa Vodacom Tanzania Plc, kuanzia leo wataanza kunufaika na programu mpya  na ya kisasa zaidi katika kufanya miamala yao kupitia huduma ya M-Pesa ambayo itawezesha watumiaji wa huduma hii wenye simu za intanenti kuifurahia zaidi kwa kuwa imerahisishwa na kuboreshwa zaidi.

  Programu hii inawezesha watumiaji wa huduma ya M-Pesa kufanya mihamala kwa haraka bila kufuata mlolongo mrefu wa programu ya awali - kwa mfano mtumiaji anaweza kuangalia akiba ya salio lake kwa kubonyeza mara moja maelekezo ya kupata huduma hii bila gharama yoyote.Pia programu hii imekuja na mfumo wa kufanya mihamala ya malipo kwa teknolojia ya kisasa na haraka inayomrahisishia maisha mtumiaji.

  Katika programu hii mpya pia inawezesha mteja kuona jina la wakala au jina la kampuni au biashara kabla ya kutoa au kutuma hususani katika mihalama ya kulipa kwa kutumia huduma ya Lipa kwa M-Pesa.

  Mkurugenzi wa huduma za biashara kwa njia ya mtandao wa Vodacom Tanzania Plc, Sitoyo Lopokoiyit,amesema kuwa  programu hii imezinduliwa rasmi leo baada ya kufanyiwa utafiti  katika soko na kujiridhisha kuwa italeta mapinduzi ya matumizi ya kufanya mihamala ya fedha kwa M-Pesa kwa kuifanya kuwa rahisi zaidi kwa watumiaji hususani wanaotumia simu za intanenti (Smart Phones).

  0 0


  Mabadiliko ya mazingira ya ufanyaji biashara yanayoletwa na maendeleo ya uchumi wa viwanda pamoja na mnyororo wa thamani, yameelezwa kuwa changamoto kubwa katika jitihada za kuimarisha hali ya usalama na afya za wafanyakazi katika sehemu za kazi hapa nchini.

  Changamoto hiyo imetolewa na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Bw, Eric Shitindi, wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) mjini Dodoma leo.

  Amesema mabadiliko hayo yanahusisha matumizi ya teknolojia za kisasa na ongezeko kubwa la idadi ya wafanyakazi katika sekta zote za umma na za binafsi jambo ambalo linahitaji utaalamu mkubwa katika kuweka na kusimamia mifumo ya kulinda afya na kuwahakikishia usalama wafanyakazi wote wanapokuwa katika sehemu zao za kazi.

  “Hivyo mkiwa kama wataalamu katika masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi mnatakiwa kuwa na mikakati mipya ya kukabiliana na changamoto hizo. Hii itakuwa ni pamoja na kubadilika kifikra na kimtazamo katika utendaji kazi,” alisema Katibu mkuu Shitindi.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, akiwahutubia wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) katika kikao chao cha baraza. Kulia ni Kaimu  Mtendaji Mkuu wa Wakala Bi. Khadija Mwenda na viongozi wa baraza hilo. 
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) mara baada ya kufungua kikao chao cha baraza.) 
  Wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi (hayupo pichani) alipofungua kikao cha baraza lao mjini Dodoma jana. 


  0 0


  Tunawashukurukwa kupokea wito wetu na kuja, karibuni sana tunawaahidi kwamba tutaendelea kushirikiana nanyi katika kila hatua.

  Aidha Umoja wa Vijana wa CCM unavipongeza sana vyombo vyote vya habari nchini kwa juhudi zenu za kuhabarisha, kuelimisha, kuwaasa, kuwaelekeza na kuihabarisha jamiii katika masuala kadhaa yanayohusiana na mipango ya maendeleo, mikakati, sera na malengo ya Serikali na mipango ya vyama vya siasa.

  Ndugu Waandishi wa habari.

  Tumewaita leo kuzungumzia mambo 2 makubwa, na suala zima la mtikisiko wa demokrasia katika mchakato wa uteuzi wa wagombea Ubunge katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulivyoendeshwa ndani ya vyama vya upinzani nchini.

  Bunge la Afrika Mashariki kama mjuavyo ni chombo kikubwa na chenye heshima ya pekee katika kanda yetu. Kuwepo kwake kunaashiria muendelezo wa kufufua dhana, dhamira, mikakati, fikra na malengo ambayo yaliasisiwa na waasisi wa Mataifa yote yaliyomo katika Kanda yetu ili hatimaye siku moja ishuhudiwe Kanda hii na Bara zima la Afrika likiunda dola moja.

  Ni jambo la heri na faraja kuona EAC ya sasa ikiwa ni yenye kufikia
  malengo ya utengamano na mafanikio hususan katika nyanja za kiuchumi na kiusalama kama vile kuwa na Pasi moja ya kusafria, miingiliano ya
  wananchi wake katika ufanyaji wa biashara pia mkakati kuelekea kupata
  viwango sawia vya ushuru wa Forodha.

  Masuala mengine ni kuona maeneo ya mipaka yetu kukiendelea kuwa na ustawi wa hali ya utulivu na usalama, wakati huo EAC ikifanya kila linalowezekana kumaliza migogoro yake ya kisiasa ambapo mazungumzo ya upatanishi huko Burundi yamekuwa yakiendelea chini ya mpatanishi mkuu Rais mstaafu Benjamin Mkapa sambamba na wananchi wa pande zote za nchi wanachama tukishuhudia wakiishi kwa maelewano, umoja, udugu na mafahamiano.
  Kaimu Katibu Mkuu UVCCM,Shaka Hamdu Shaka .


  0 0

  Na Khadija Khamis –Maelezo 

  Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt Fadhil Moh’d Abdalla ameitaka jamii kubadili tabia kwa kuweka mazingira yaliyowazunguka safi na kuhakikisha wanatumia maji safi na salama ili kujiepusha na maradhi ya mribuko .

  hayo ameyasema wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa ya kuandaa mpango mkakati wa kudhibiti maradhi ya kipindupindu hasa kipindi hichi ambacho mvua za masika zimeanza kunyesha.

  Alisema lengo kuu la kamati hiyo ni kufanya tadhmini ya muendelezo wa mpango kazi wa kudhibiti maambukizi ikiwemo kutoa elimu ya usafi wa mazingira kwa jamii na kupambana na mazingira hatarishi katika maeneo mbali mbali ya Manispaa ya Zanzibar.

  Ameishauri Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kuhakikisha maji yanayotumiwa na wananchi yapo katika hali ya safi na salama kwa kutia dawa vianzio vyote vya maji na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kufanya uharibifu kwenye njia za maji kwa kutoboa mabomba yanayosamba maji .
  Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afaya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohammed Abdalla akieleza mipango iliyoandaliwa ya kukabiliana na maradhi ya kipindupindu iwapo yatatokezea katika kikao kilichofanyika Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongo chekundu Mjini Zanzibar. 
  Mkuu wa Kitengo cha Afya ya Mazingira Rukaiya Mohamed Said akiwasilisha taarifa ya kikao kilichopita cha Kamati hiyo kilichofanyika mwezi uliopita. 
  Afisa kutoka Jumuia ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi Zanzibar Jokha Masoud Salim akitoa mchango wakati wa kikao hicho.


older | 1 | .... | 1631 | 1632 | (Page 1633) | 1634 | 1635 | .... | 3348 | newer