Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

ILALA YAZINDUA MRADI WA MAJI WA MAMILIONI PUGU

$
0
0
"Nikizindua kisima  tu nawashukuru wananchi kwa sapoti yao tunamshukuru mbunge wa ukonga Mh Waitara aliechangia Milioni tatu  katika fedha za mfuko wa jimbo,niliwasisitiza wananchi watunze mradi huo wa maji kwani ni ukombozi kwa kata yao ya pugu",alisema Kumbilamoto.
 Naibu Meya akizindua mradi mkubwa wa kisima cha maji katika jimbo la ukonga kata ya pugu mtaa wa bombani na kigogo B ,Mradi huo wa maji umegharimu kiashi cha fedha Milioni  67.610.000 kama sehemu za juhudi za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Wananchi pamoja na mfuko wa Jimbo
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akifungua  bomba la Maji kuashiria kuwa Maji yanaanza kutumika katika eneo la Pugu Kajiungeni
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akimtwisha ndoo ya Maji mmoja wa wakazi wa Pugu mara baada ya Maji ya kisima kilichochimbwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza na wakazi wa Jimbo la ukonga kata ya Pugu mtaa wa bombani Kigogo B.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ,Omary Kumbilamoto  akishuka bondeni kuangalia chanzo cha maji katika eneo la Pugu

KITABU CHA UWIANO WA TAKWIMU ZA WANAWAKE NA WANAUME CHAZINDULIWA JIJIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

WANAUME wameonekana kuwa wengi katika nafasi mbalimbali ukilinganisha na wanawake.

Hayo yamebainishwa na Mhadhiri wa Chuo cha Takwimu Afrika Mashariki, Chisker Masaki wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo katika hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Uwiano wa Taarifa za Takwimu kwa Wanawake na Wanaume Tanzania.

Alisema kitabu hicho kimeandaliwa na washiriki wa mafunzo ya ukusanyaji wa taarifa za takwimu kutoka Tume ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Hakielimu , Ofisi yaTaifa ya Takwimu (NBS) na Chuo cha Takwimu cha AfrikaMashariki, chini ya wakufunzi wa masuala ya ukusanyaji wa taarifa kutoka nchini Sweden. 

Masaki alisema utafiti unaonesha kuwa kuna tofauti kubwa za uwiano kati ya mwanamke na mwaume katika nyanja za kimaendeleo na kijamii, ambapo maeneo mengi yanaonekana kutwaliwa na wanaume kuliko wanawake.
Meneja wa Takwimu za Watu na Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Sylvia Meku (katikati) akiwa na wadau wakionesha kitabu cha uwiano wa takwimu za wanawake na wanaume wakati wa hafla ya kuzindua kitabu hicho iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Habari na Ulaghibishi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Jumanne Issango, Ofisa wa Takwimu kutoka nchini Sweden, Cath Craiger, Mtakwimu kutoka Sweden, Ana Morkuda na Mwanahabari Philip..Kitabu hicho kimeandikwa na wanafunzi watano kutoka Tanzania waliopata mafunzo ya miezi 11 nchini Sweden.
Mada kuhusu mafunzo hayo zikitolewa kabla ya uzinduzi.
Wafadhili wa mafunzo hayo kutoka nchini Sweden wakifuatilia mada kuhusu mafunzo hayo.

Airtel yazindua HATUPIMI bando, Ongea bila kikomo

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua OFA kabambe   ijulikanayo kama HATUPIMI Bando itakayowawezesha wateja wake wote nchini kuongea bila kikomo mara tu baada ya kujiunga. 

“Airtel HATUPIMI Bando” itapatikana katika vifurushi mbalimbali ikiwemo kifurushi cha siku, wiki na mwezi vilivyosheheni dakika zisiso na kikomo zinazowawezesha wateja wa Airtel kuongea na kufanya mengi zaidi bila kuwa na wasiwasi wa kuishiwa muda wa maongezi kwa kuwa hakuna kupimiwa dakika za maongezi.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa ofa hii kabambe, Mkurugenzi wa Masoko, Isack Nchunda alisema “ Airtel Hatupimi, sasa Hatupimi dakika zenu za maongezi, tunaleta huduma hizi nafuu kwa kuwa tunaamini katika kuendelea kuboresha huduma zetu ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu kwa kuwapatia thamani ya pesa zao katika huduma na bidhaa zetu.

“HATUPIMI Bando” itawapatia wateja wetu nchi nzima uhuru wa kuongea na familia, marafiki na wadau wa biashara zao kulingana na aina ya kifurushi mteja alichochagua ikiwemo kifurushi cha siku, wiki na mwezi bila kujali vifurushi vyao kuisha muda wa maongezi. Kuna vifurushi vya Hatupimi kwa siku vya hadi shilingi 1000/= pia vipo vya wiki kwa shilingi 5000, na vilevile unaweza kujiunga na HATUPIMI kwa mwezi kwa shilingi 10,000/= ili ufurahie huduma yakutopimiwa dakika zako ongea bila kikomo 
 Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya (wa pili kushoto)  na wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini (kulia), Niki wa Pili(wa pili kulia) na Gnako kwa pamoja  wakizindua Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja wake kuongea bila kikomo.  Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isack Nchunda.

 Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati) akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja wake kuongea bila kikomo.  Wa (pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isack Nchunda na wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini (kulia), Niki wa Pili(wa pili kulia) na Gnako 
 Wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini (kulia) ,  Niki wa Pili (katikati) na Gnako wakitumbuiza jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Ofa kabambe ya Airtel ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja Airtel kuongea bila kikomo.

KUSOM ZAIDI BOFYA HAPA


TAARIFA KWA UMMA KUTOKA VODACOM TANZANIA

$
0
0
Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC imetoa ufafanuzi kuhusiana na suala la kesi iliyofunguliwa na Moto Matiko Mabanga dhidi ya Vodacom Group Limited , Vodacom Tanzania PLC  ("VCT"); Vodacom International Limited  ("VIL"), na Vodacom Congo s.p.r.l ("VDRC") Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo,Ian Ferrao inasema ,Bwana Moto Mabanga amehusisha suala hilo na hisa za kampuni ya Vodacom PLc zinazoendelea kuuzwa kwa umma kwa lengo la kutaka kulipwa deni la Namemco Energy PTY Limited inayodai kuidai Vodacom International Limited (“VIL”)

Vodacom Tanzania PLC inapenda kuufahamisha umma kwamba suala hilo halihusiani na uendeshaji wa shughuli za Vodacom hapa nchini na zoezi la kuuza hisa  kwa umma lililozinduliwa hivi karibuni,Zoezi hili linaendelea kama kawaida na litafikia mwisho mnamo Aprili 19,2017,na uongozi wa Vodacom nchini utaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa kama ilivyokusudiwa.

Madai ya Bw.Mabanga yanahusiana na kampuni ya Vodacom International Limited (“VIL”) na sio Vodacom Tanzania PLC  ("VCT").Kesi hiyo ilianzia katika Mahakama kuu ya Johannesburg na kumalizika vizuri kutokana na hukumu  ya Mahakama ya Biashara ya Kinshasa/Gombe katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo (DRC).Kutokana na kumalizika kesi hiyo kwa njia ya mahakama,Bw.Moto Mabanga ,alifikisha malalamiko yake tena kwenye Baraza la kusuluhisha kesi zinatotokana na migogoro ya kibiashara (ICC) ambalo liliridhia uamuzi wa awali wa hukumu ya mahakama na kumwamuru,Bwana Mabanga kulipa gharama za kesi hiyo kiasi cha USD 7 milioni.Kampuni ya Namenco Energy PTY Limited inapinga uamuzi wa kulpa ghrarama hizo katika Mahakama ya Rufaa ya Paris,nchini Ufaransa.

Mkurugenzi huyo alisema kampuni yake ina imani kubwa na mahakama kuu ya  Tanzania kwani  itaelewa suala la kesi hii inayoendelea inayoihusu Vodacom International Limited na Namenco Energy PTY Limited ambayo  Vodacom Tanzania PLC  ("VCT"); haihusiki nayo,Alisema Ferrao.

Wanafunzi wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Northwestern Pritzker Chicago Illinois nchini Marekani wamtembelea kaimu jaji mkuu jijini Dar es salaam

$
0
0
Wanafunzi wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Northwestern Pritzker Chicago, Illinois nchini Marekani wakiwa wamemtembelea Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma, Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam. Wanafunzi hao wako nchini kwa ajili ya Utafiti wao kuhusu hali ya  sasa ya Makosa ya Mauaji ya Wanyamapori  na Usimamizi wa Rasilimali ya Wanyamapori Tanzania

 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma, Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam akiongea na Wanafunzi wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Northwestern Pritzker Chicago, Illinois nchini Marekani. Pamoja naye ni Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Wambari
 Badi ya Wanafunzi wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Northwestern Pritzker Chicago, Illinois nchini Marekani wakisikiliza Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma walipomtembelea kwenye ofisi zake katika Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam.
Picha na LYDIA CHURI-MAHAKAMA YA TANZANIA


Pikniki Adui wa Mazingira Ukanda wa Utalii - amber resort, zanzibar

$
0
0

Pikiniki zinazofanywa na watu mbalimbali  katika fukwe zilizoko kwenye ukanda wa utalii visiwani Zanzibar, zinachangia uharibifu mkubwa wa mazingira unaotishia kuwakimbiza watalii.


Shughuli ya kusafisha mazingira iliyofanywa juzi katika eneo dogo kwenye ufukwe wa Muyuni ulioko Matemwe mkoa wa Kaskazini Unguja, ilikusanya karibu tani moja ya takataka zikiwemo chupa za plastiki.

Operesheni hiyo iliyochukua saa moja, ilijumuisha wafanyakazi wa Amber Resort na Best of Zanzibar, na kusafisha eneo linaoandaliwa kwa ajili ya mradi mkubwa wa kitalii utakaofanywa na kampuni ya Pennyroyal.

Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, Meneja Mradi wa Amber Resort Murtaza Hassanali, alisema vijana wanaotembeza watalii (mapapasi) pamoja na wageni wanaofika hapo, huondoka wakiacha vitu vingi visivyofaa ambavyo hugeuka kuwa taka na sumu kwa viumbe wa baharini.

Aidha alieleza kuwa, pikiniki zinazofanywa na watu kutoka mjini na maeneo mengine hasa vijana, ni chanzo kikuu cha uharibifu wa fukwe hizo. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

WAFANYABIASHARA MACHINGA COMPLEX JIJINI DAR ES SALAAM WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA

$
0
0
NaFrank Shija – MAELEZO, Dar es Salaam.

WAFANYABIASHARA ndogondogo katika Soko la Machinga Complex Jijini Dar es Salaam wameshauriwa kubadilika na kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia sheria badala ya kufanya biashara zao kimazoea.

Wito huo umetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene alipofanyaa ziara ya kikazi katika Soko hilo ili kusikiliza changamoto wanazokumbana nazo wafanyabiashara wa soko hilo.

“Nawapa pole sana ndugu zangu wafanyabiashara wa Machinga Complex mnaendesha biashara zenu bila kuzingatia sheria jambo linalo wagharimu hivi sasa katika biashara zenu leo nimekuja kuwarejesha kwenye mstari,” alisema Simbachawene.

Aidha Waziri Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuwachukulia hatua baadhi ya viongozi wa menejimenti ya Machinga Complex kwa kile kinachodaiwa utendaji wao mbovu na kujaza nadfasi zote zilizo wazi.

Wakati huohuo amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuteua Wajumbe wa Bodi ya Machinga Complex ili kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa Soko hilo.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene (wapili kutoka kushoto) akitembelea baadhi ya vizimba vya wafanyabiasha katika soko la wafanyabiashara wadogowadogo la Machinga Complex leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Meneja wa Soko hilo, na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Machinga Complex alipofanya ziara kwa ajili ya kusikiliza changamoto zao leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Sipora Liana, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema.
 Mmoja wa wafanyabiashara katika Soko la Machinga Complex akielezea changamoto wanazokumbana nazo katika soko hilo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene (hayupo pichani) alipotembelea katika soko hilo leo Jijini Dar es Salaam. Waziri Simbachawene amefanya ziara katika Soko hilo hili kusikiliza changamoto kutoka kwa wafanyabiashara hao na kukagua utekelezaji wa agizo alilolitao wakati wa ziara yake ya kwanza sokoni hapo.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI


UBALOZI WA MAREKANI WATOA MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI KWA WANAMITANDAO

$
0
0
USA8
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada zilizotolewa.
USA9
Maofisa wa Ubalozi wa Marekani pamoja na Mkufunzi huyo wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo .
USA10
Mkufunzi wa Mafunzo hayo Ricci Shryock akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

INTRODUCING "SINUNUI STRESS" BY CYRILL KAMIKAZE

Legendury Beatz Team Up With Veemoney to Serve Some SwagHili

$
0
0
Figisu ndiyo kitu mi sinaga are the opening lines to this immediately captivating track. This Swahili line describes VeeMoney to the tee. It translates as; Trouble/Drama is what I don't have. The latest video off of the Legendury Beatz mixtape Afropop 101 features East Africa's leading female act Vanessa Mdee and they opt for a vibrant lyric video for this one. Mainly to bring their fans from across the globe together and unite irrespective of where they are from. With one belief, 'Together we are CHAMPIONS!' Needless to say Legendury Beatz went IN on the production of this guaranteed club banger seen in the various elements of the production. So sit back and learn some SwagHili
For more information
Twitter: @vanessamdee
Instagram: @vanessamdee

Snapchat: moneymondays

Twitter: @legendurybeatz


 

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA SUKARI CHA ALTEO NCHINI MAURITIUS

WATANZANIA WAASWA KUBADILIKA LA SIVYO WAKENYA NA WAGANDA WATAENDELEA KUAJIRIWA KATIKA HOTELI ZETU

$
0
0
Serikali kupitia Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amesema raia wa Kenya na Uganda wataendelea kuajiriwa katika hoteli zetu kama Watanzania hawataweza kubadilika kwa kuachana na tabia sizizofaa ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na watalii wengi wanaofikia katika hoteli hizo.

Amesema baadhi ya wafanyakazi katika hoteli hizo wamekuwa na tabia za udokozi, uvivu na kiburi akitolea mfano amesema unaweza ukafika katika hoteli ukakaa zaidi ya nusu saa bila kusikilizwa huku wahudumu wakikupita tu kana kwamba hawajakuona, hali inayochangia kwa watalii wanaotembelea vivutio vya utalii kwa mara ya kwanza kutokurudi tena.

Sendeka aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo yaliyofanyika kwa muda siku tatu mkoani Njombe kwa wahitimu 90 katika fani ya ukarimu na Utalii, alisema ni lazima wabadilike kwa kufanya kazi kwa kujituma pasipo kusimamiwa na mameneja wa hoteli hizo la sivyo wataendelea kulalamika huku nafasi zao zikiendelea kuchukuliwa na wageni.

Amesema wamiliki wengi wa hoteli wamekuwa wakipenda kuajiri wafanyakazi kutoka nchi hizo kutokana na uchapakazi wao na si kwa ajili ya wanajua lugha ya kiingereza ‘’Wamiliki wananchohitaji ni kupata faida na sio kung’ang’ania kuajiri wazawa ambao hata kumkaribisha mgeni kwa bashasha imekuwa ni shida’’ alisisitiza Sendeka

Kwa upande wa Mratibu Msaidizi wa Mradi wa SPANEST, Edmund Murashani alisema mradi huo umeamua kujikita katika kuwezesha wahudumu wa hoteli, migahawa na nyumba za kulala wageni wanapata mafunzo kwa kuwa wao ni mojawapo ya nguzo muhimu katika kuhakikisha utalii unakua katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

‘’ Tunataka mtalii akifika katika hoteli hizo kitu cha kwanza kabla hajatembelea vivutio vya utalii vinavyopatikana katika ukanda huo awaze kuongeza siku za kulala katika hoteli zetu kutokana na huduma stahiki anazopata kutoka kwa wahudumu hao’’ Murashani alisema Naye, Mhitimu wa Mafunzo hayo, Tulizo Sanga aliomba siku za mafunzo hayo ziweze kuongezwa kwani siku tatu hazitoshi kutokana na umuhimu wa mafunzo hayo kwao.

Mafunzo kama hayo yanatarajiwa kufanyika mkoani Iringa na Songwe chini ya Usimamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia Mradi wa SPANEST unaotekelezwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka akizungumza na jumla ya wahitimu 90 wakati alipokuwa akifunga jana mafunzo katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na Mradi wa SPANEST yaliyofanyika Mkoani Njombe kwa muda wa siku tatu. na Wengine ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Njombe, Joseph Choya (kulia) Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskasi Mwiru (kushoto).
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka akikabidhi cheti kwa Mhitimu wa mafunzo katika fani ya ukarimu na utalii wakati alipokuwa akifunga mafunzo hayo jana yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na Mradi wa SPANEST yaliyofanyika Mkoani Njombe.
Mkufunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), Dawson Kyungai akiwaelekeza Washiriki 90 wa Mafunzo ya Ukarimu na Utalii namna ya kumimina mvinyo kwenye glasi pamoja na kuwaonyesha kiwango kinachotakiwa. Mafunzo hayo yametolewa kwa muda wa siku tatu katika fani ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Mradi wa SPANEST ambayo yamefungwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka . 
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher  Ole Sendeka akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na Maofisa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Mradi wa SPANEST na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe mara baada ya kufunga mafunzo ya muda wa siku tatu kwa jumla ya wahitimu 90 katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na Mradi wa SPANEST. (Picha na Lusungu Helela- WMU).

BENKI YA KCB TANZANIA YAZINDUA WARSHA YA BIASHARA CLUB KWA WATEJA WAKE AMBAO NI WAJASIRIAMALI WADOGO NA WAKATI

$
0
0
Benki ya KCB Tanzania imeendelea kuwekeza kwa wajasiriamali wadogo na wakati kupitia kitengo chake cha “Biashara Club”, kitengo kinachohudumia wajasiriamali wadogo na wakati yaani (SME) kwa kuwapa huduma za kibenki na huduma endelevu za kimaendeleo kwa wateja wake. 

Zaidi ya wanachama 100 wa Biashara Club wamekutana kujifunza jinsi ya kutunza fedha, jinsi ya kufanya kwa vitendo uwekaji wa kumbu kumbu za hesabu , jinsi gani taarifa ya fedha za biashara yako na taarifa za kifedha za mtu binafsi zinavyokusanywa na kukaguliwa, na kwa njia gani taarifa hizi zinapatikana kwenye taasisi za mikopo kupitia taasisi za kifedha. 

Kwa kuongezea, maelezo mafupi yalitolewa na Taasisi ya biashara, Viwanda na kilimo Tanzania kuhusu utolewaji na uthibitishwaji wa vyeti halali kwa bidhaa zinazo zalishwa hapa Tanzania, wao wamebobea katika kufanya tafiti mbalimbali nchi nzima kwa kutumia mtandao wao na kuanzisha mfumo maalumu kwa wajasiriamali wadogo na wakati, 

kuzisaidia taasisi za wajasiriamali wadogo na wakati, na kuwakutanisha wadau wa misitu kwa pamoja na kufanya ushirika wa biashara kwa wadau na kuwaunganisha wanachama na fursa zilizopo kwa washirika wa kibiashara wa kimataifa. Akiongea kwenye warsha ya KCB Biashara Club iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya KBC, Godfrey Ndalahwa akizungumza machache wakati wa warsha ya KCB Biashara Club iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa Kitengo cha Kiislamu wa Benki ya KCB, Rashid Rashid akitoa machache kwa wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club' iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa kitengo kinachohudumia wajasiriamali wadogo na wakati (SME) ,Edgar Masatu akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kuhudhuria Warsha hiyo iliyoandaliwa na benki hiyo ya KCB mapema leo jijini Dar.

Wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club' wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ukumbi humo mapema leo.
Wanachama wa Jukwa la Kibiashara 'Biashara Club' wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo mapema leo asubuhi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA SAMAKI CHA MAURITIUS

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama usindikaji wa samaki katika kiwanda cha MER Des Mascareignes nchini Mauritius Machi 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akitazama makasha yenye minofu ya samaki wakati alipotembelea kiwanda cha samaki cha MER Des Mascareignes nchini Mauritius Machi 21, 2017. Wapili kulia ni Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha samaki cha MER Des Mascareignes nchini Mauritius Machi 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


WAZIRI NAPE APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA UCHUNGUZI WA TUKIO LILILOTOKEA CLOUDS MEDIA

$
0
0
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amepokea taarifa ya kina kuhusu chanzo, sababu na namna tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda alivovamia kituo cha Utangazaji cha Clouds Media akiwa na walinzi wenye silaha Machi 17, 2017.

Akipokea taarifa hiyo leo Jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Dkt.Hassan Abbas ameishukuru Kamati kwa utulivu wao na kuifanya kazi hiyo kwa utaalamu na umakini mkubwa huku jamii ikitaka matokeo kwa haraka.

Aidha Mhe. Waziri amesema kuwa ripoti hiyo ataiwasilisha kwa mamlaka husika kwa ajili ya uamuzi na maelekezo.“Nimeipokea ripoti na ninawahakikishia kuwa nitaikabidhi ripoti hii kwa wakubwa zangu wao ndo wenye mamalaka ya kufanya chochote”,Alisema Mhe. Nape.

Kamati aliyoiunda Mhe Waziri ilikuwa na wajumbe wanne ambao ni Bw.Deodatus Balile kutoka Jamhuri,Bw.Jesse Kwayu wa Gazeti la The Guardian,Bibi Nengida Johanes wa Upendo Media na Bibi Mabel Masasi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) walioongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt.Hassan Abbas .
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Hassan Abbass.
Katibu wa Kamati ya Kuchunguza Sakata la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia ofisi za Kituo cha Televisheni cha Clouds Media, Deodatus Balile akielezea yaliyomo katika ripoti yao kabla ya kumkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nauye (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye (katikati) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO Dkt. Hassan Abbass na Katibu wa Kamati hiyo Deodatus Balile.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akikabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds Media na Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi wa sakata hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan Abbass leo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi wa tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia kituo cha Televisheni cha Clouds Media ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan Abbass (kushoto) akimwelezea Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye ushahidi wa CCTV uliombatanishwa katika CD aliyomkabidhi leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia makabidhiano ya ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam.Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.

YANGA YAWAONDOA HOFU MASHABIKI, WASEMA MC ALGER NI KAMA TIMU NYINGINE

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa wanashukuru wamepata ratiba kwa wakati ya hatua ya mtoano wa kombe la Shirikisho na mechi ya kwanza wanaanzia hapa nyumbani dhidi ya wapinzani wao MC Alger toka Algeria. 

Akizungumzia hilo, Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema kuwa hawana hofu na MC Alger kwani ni kama timu nyingine na kikubwa zaidi amewaondoa hofu mashabiki na kuwataka watulie kwani benchi la ufundi linaendelea kukinoa kikosi kwa ajili ya maandalizi.

" Yanga SC ni timu kongwe na bora na tumejipanga kupata matokeo nyumbani na ugenini. Tumezungumza na wachezaji wetu pamoja na benchi la ufundi kujiandaa vyema kimbinu , kiufundi na kisaikolojia kushinda mchezo huu. Mechi kama hizi unapopata ushindi mzuri wa nyumbani , basi unapunguza mlima wa kuupanda ugenini,"amesema Mkwasa.

Mkwasa amesema kuwa MC Alger ni timu nzuri na amekuwa bingwa wa Afrika hivyo kila mtu atataka kuiona na sisi tunawaheshimu kwa historia yao lakini tunakwenda kupambana kutafuta ushindi na zaidi ameweka wazi msisitizo kuwa hivi karibuni wame

"muda ukifika tutawajuza wapi mechi itafanyikia kama ni hapa jijini au popote Tanzania. Kwa sasa bado hatujaamua lolote katika hilo hivyo uwanja wa taifa unabaki kutambulika kama uwanja wa nyumbani." 

Mkwasa akizungumzia sapoti ya mashabiki katika mchezo wao , alieleza kinagaubaga jinsi gani klabu inahitaji sapoti yao mwanzo mwisho , " mashabiki na wadau wote wa soka nchini tunawaomba kuipa sapoti timu yetu muda wote wa dakika 90 itakapokuwa uwanjani.

"tunawafahamu vyema wenzetu kwa fitina zao hususani mechi za kwao . Mara nyingi huzipanga usiku ili wapate fursa ya kuwasha miale yao na vitochi kuumiza macho ya wachezaji . Tunawaandaa wachezaji wetu katika hali zote pia umakini wa kuripoti kila tukio kwa mamlaka husika . " alimaliza katibu mkuu huyo wa Yanga SC ndugu Charles Mkwasa. 
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa 

MAKACHERO SARPCCO WAJADILI UHALIFU UNAOVUKA MIPAKA.

$
0
0
Na. Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
Wakuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai kusini mwa Afrika wametakiwa kuongeza ushirikiano katika kubadilishana taarifa za wahalifu na uhalifu unaovuka mipaka ili kuufanya ukanda wa kusini mwa Afrika kuwa salama.

Wito huo umetolewa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki mjini Bagamoyo alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa Wakuu wa Upelelezi wa Polisi kutoka Shirikisho la Wakuu wa Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO) unaofanyika sambamba na kamati za ufundi za SARPCCO kwa lengo la kupanga mikakati ya kupambana na uhalifu na wahalifu.
Kaniki alisema ili kuwabaini wahalifu kwa urahisi ni vyema ushirikiano wa kubadilishana taarifa ukafanyika kwa haraka hasa kwa kuimarisha teknolojia ya habari na mawasiliano na mafunzo kwa maafisa wa Polisi ili kuwajengea uwezo wa kubaini mapema viashiria vya uhalifu katika maeneo yao.
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahmani Kaniki akisaluti kwa wimbo wa taifa kabla ya kutoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kamati ndogo za kiufundi za shirikisho la wakuu wa Polisi wan chi za kusini mwa afrika SAPRCCO. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika Bagamoyo mkoani Pwani kujadili mikakati ya kukabili uhalifu unaovuka mipaka. Kushoto ni Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya Jinai DCI, Robert Boaz. Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Abdulrahmani Kaniki akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kamati ndogo za kiufundi za shirikisho la wakuu wa Polisi wan chi za kusini mwa afrika SAPRCCO. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika Bagamoyo mkoani Pwani kujadili mikakati ya kukabiliana uhalifu unaovuka mipaka. Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Abdulrahmani Kaniki akionyesha zawadi kutoka kwa Mkuu wa Interpol kanda ya kusini (kulia) baada ya kutoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kamati ndogo za kiufundi za shirikisho la wakuu wa Polisi wan chi za kusini mwa afrika SAPRCCO. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika Bagamoyo mkoani Pwani kujadili mikakati ya kukabiliana uhalifu unaovuka mipaka. Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE IMEITAKA SERIKALI KUHAKIKISHA INATOA FEDHA ZA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA ABIRIA NAMBA TATU

$
0
0
KAMATI ya Kudumu ya Bunge imeitaka serikali kuhakikisha inatoa fedha za mradi wa ujenzi wa jengo la abiria namba tatu (terminal III) kwa wakati ili mradi huo uweze kukamilika kama ilivyopangwa. 

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Norman Sigalla aliyasema hayo wakati wa kufanya majumuisho baada ya kutembelea mradi huo leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA). 

Alisema kukamilika kwa jengo hilo kwa wakati uliopangwa utawapa heshima Watanzania lakini pia kupunguza msongamano katika jengo la sasa la Terminal II. 

“Nchi inapoenda kwa sasa ni kuzuri, lakini ili kukamilika ujenzi huu kwa wakati tunaomba serikali itoe fedha ili kufanikisha hilo, baada ya kukamilika kila ndege itatua hapa nchini na hivyo kuongeza pato la Taifa,” alisema Profesa Sigalla. 
01.Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu Mhe.Prof Norman Sigalla akizungumza na wana kamati wakati wa ziara ya mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abria (terminal) katika kiwanja cha ndege cha kimataifa Julius Nyerere leo jijjini Dar es Salaam. 
02.Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akizungumza wana kamati wakati wa ziara ya mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abria (terminal) katika kiwanja cha ndege cha kimataifa Julius Nyerere leo jijjini Dar es Salaam. 
Wana kamati wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu Mhe.Prof Norman Sigalla
.Wana kamati wa kamati ya kudumu ya Bunge wakitembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abria (terminal) katika kiwanja cha ndege cha kimataifa Julius Nyerere leo jijjini Dar es Salaam. 
Ujenzi ukiendelea wa jengo la abiria namba tatu (Terminal. ).Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE YA ULINZI NA USALAMA YAKAGUA MRADI WA UJENZI -OFISI ZA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu (wakwanza kushoto), akiongozana na wajumbe wengine wa kamati hiyo baada ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahaya, akijibu baadhi ya hoja zilizoelekezwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama (hawapo pichani), wakati wajumbe hao walipotembelea mradi wa ujenzi ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Ziara hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa ofisi za jeshi hilo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama(hawapo pichani), wakati wajumbe hao walipotembelea mradi huo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Balozi Adadi Rjabu na anayefuatia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahaya.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama,Kapteni Mstaafu George Mkuchika, akichangia hoja wakati wa ziara ya kamati hiyo kukagua ujenzi wa ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, jijini Dar es Salaam leo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images