Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1619 | 1620 | (Page 1621) | 1622 | 1623 | .... | 3284 | newer

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme akizungumza na Kamati ndogo ya Mkoa inayoratibu Ujenzi wa mradi wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa utakojengwa katika kata ya Nala Mjini Dodoma.
   Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Mkoa ya Uratibu Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimatafa Bw.Salum Mkuya akitoa mrejesho wa mambo yaliyofanywa na Kamati yake kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme (Hayupo Pichani)   katika kuhakikisha Mradi huo unafanikiwa.
    Mjumbe wa hiyo ambaye ni Mwanasheria kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Evordy Kyando akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme (Hayupo Pichani)  wakati Kamati hiyo ilipokutana na Mkuu huyo wa Wilaya. 
   Mjumbe wa kamati hiyo ambaye ni Afisa Tawala Wilaya ya Dodoma Bw. Hashimu Kitambuliyo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme (Hayupo Pichani) kuhusu mipango na mikakati iliyoweka na Kamati hiyo katika kufanikisha Mradi huo. 
  Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma


  0 0


  0 0  SWAZ1
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu wa Swaziland Mhe. Barnabas Sibusiso Dlamini katika uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Afrika kwenye hoteli ya Westin mjini Port Louis, Mauritius, Machi 20, 2017.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  SWAZ2
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wa nchi za Afrika walioshiriki katika uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Afrika kwenye Hoteli ya Westin mjini Port Louis nchini Mauritius Machi 20, 2017.(Picha na 0fisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Cliford Tandari akifafanua jambo katika Mkutano wake na Baadhi ya Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kituo hicho, Jijini Dar es salaam leo.
   Kiongozi wa Msafara wa Mabalozi hao, Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Balozi Omar Yussuf Mzee akifafanua jambo katika kikao kati yao na uongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), walipotembelea leo ili kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji zinatolewa na Kituo hicho. ambapo amewataka TIC kuhakikisha wanaandaa maeneo ya viwanda kulingana na uzalishaji unaopatikana katika eneo husika.
  Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Matilda Masuka akizungumza jambo katika kikao kati yao na uongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), walipotembelea leo ili kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji zinatolewa na Kituo hicho.
  Mkutano baina ya Baadhi ya Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje na uongozi wa Kituo cha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Cliford Tandari, ukiendelea.
  Balozi wa Tanzania nchini Oman, Balozi Abdallah Kilima (katikati) akizungumza katika kikao kati yao na uongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), walipotembelea leo ili kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji zinatolewa na Kituo hicho.


  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akivuta kitambaa pamoja na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi katika Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za Juu Ubungo Interchange jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipiga makofi.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Crispianus Ako aliyekuwa akielezea nama ya ujenzi huo makutano ya barabara za juu za Ubungo(Ubungo interchange) zitakavyokuwa.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi hawapo pichani kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi  wa ya  barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati akiwa ndani ya basi la Mwendokasi pamoja na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim (anayetazama kadi yake ya DART) wakati wakitokea kituo kikuu cha BRT-Kivukoni kuelekea Ubungo kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.

  0 0


  0 0

  Dar es Salaam, Tuesday March 21, 2017. In the matter of Moto Matiko Mabanga vs Vodacom Group Limited Vodacom Tanzania PLC  ("VCT"); Vodacom International Limited  ("VIL"), and Vodacom Congo s.p.r.l ("VDRC") where Mr. Moto Mabanga has filed for the attachment of shares in Vodacom Tanzania PLC purportedly to recover a debt owed to Namemco Energy PTY Limited by VIL.  

  VCT hereby notifies its customers, the public and other stakeholders that its Initial Public Offering (IPO) is still underway. The IPO has a closing date of April 19, 2017. The management of Vodacom Tanzania PLC will continue to work with all stakeholders in order to ensure the transaction is completed successfully.  
  According to Vodacom Tanzania PLC, Managing Director Ian Ferrao,Mr. Mabanga's claim is principally against VIL and not VCT.
  The case was originally initiated in the Johannesburg High Court and eventually settled amicably following a ruling of the Kinshasa/Gombe Commercial Court, Democratic Republic of the Congo ("DRC"). 
  Following this settlement, Mr. Moto Mabanga's  purported repudiation of the settlement agreement was dismissed by the arbitral tribunal of the International Chamber of Commerce ("ICC") which not only found that the settlement agreement was valid, but also directed Mr. Mabanga to pay damages which, over time,  have accumulated to an amount in excess USD 7 million. Namemco is challenging the ICC ruling in the Court of Appeals in Paris, France.
  We believe that the Tanzania high court will act swiftly to resolve this matter which is related to an ongoing case between VIL and Mr Mabanga,Said Managing Director of Vodacom Tanzania Ian Ferrao.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Takwimu zinaonyesha kuwa wanaume ndio wengi katika nyanja mbalimbali za kiutawala na uongozi kuliko wanawake hali ambayo inahitajika kuwepo kwa taarifa za wanawake katika masuala kufanyiwa kazi.

  Hayo yamesemwa na mtakwimu wa Chuo cha Taifa cha Takwimu, Chiskel Masaki wakati wakitoa ripoti ya uwiano wa takwimu kati ya wanawake na wanaume waliofanyia kazi kutokana na mafunzo waliyopata nchini Swiden kwa ufadhili wa Sida, amesema kunahitaji taarifa za wanawake ili kuweza kuwasukuma washiriki katika masuala mbalimbali kuendana na wanaume.

  Chiskel amesema kuwa mafunzo hayo ya mwezi mmoja yalishirikisha nchi tano ambazo ni Tanzania, Uganda, Rwanda, Pakstan pamoja na Bangladesh ambapo baada ya mafunzo walifanya takwimu za uwiano wa wanaume na wanawake kwa kila nchi.

  Aidha amesema kuwa kutokana na kufanya takwimu wameweza kuona umuhimu wa kuwa na takwimu mbalimbali ambazo zinaweza kusaidia nchi kuweza kutatua matatizo likiwemo suala la uwiano wanaume na wanawake ambapo wanaume ndio wanaoneka katika ajira , uongozi pamoja na uatwala.
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Sylvia Meku akitoa maada katika katika uzinduzi wa ripoti ya uwiano kati ya wanaume na wanawake leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Ufatiliaji na Tathimini wa TACAIDS, Dk. Jerome Kamwela akitoa maada katika uzinduzi wa ripoti ya uwiano kati ya wanaume na wanawake leo jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Sylvia Meku akikabidhi kitabu kwa Mkurugenzi wa Ufatiliaji na Tathimini wa TACAIDS, Dk. Jerome Kamwela katika uzinduzi wa ripoti ya takwimu ya uwiano kati ya wanaume na wanawake leo jijini Dar es Salaam.
  Picha ya pamoja ya wasimamizi wa kusimamia Takwimu zilizofanywa pamoja na watakwimu waliofanya takwimu ya uwiano wa wanaume na wanawake.Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha sukari cha Kampuni ya Alteo ya Nchini Mauritius chenye uwezo wa kukamua tani 400 za miwa kwa saa na kuzalisha tani 170,000 za sukari kwa mwaka.

  Kampuni ya Alteo inamiliki kiwanda cha sukari cha TPC mkoani Kilimanjaro kwa ubia na Serikali ya Tanzania na kinazalisha tani 110,000 kwa mwaka.

  Waziri Mkuu ametembelea kiwanda hicho leo (Jumanne, Machi 21, 2017) na kujionea namna wanavyozalisha sukari kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
  Aidha, Waziri Mkuu amefanya mazungumzo na uongozi wa kiwanda hicho na kuwashawishi waongeze maeneo ya uwekezaji nchini.

  “Tekonolojia wanayoitumia katika uendeshaji wa kiwanda chao ni nzuri hivyo tumewashawishi waje kuongeza maeneo ya uzalishaji wa sukari nchini ili tuweze kukidhi mahitaji,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema Tanzania kuna viwanda vitano vya sukari ambavyo ni Mtibwa, Mahonda (Zanzibar), TPC, Kilombero na Kagera vinavyozalisha tani 320,000 kwa mwaka huku mahitaji ni tani 420,000.

  Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed amesema Zanzibar kuna kiwanda kimoja cha sukari ambacho uzalishaji wake haukidhi mahitaji kutokana na
  uhaba wa malighafi.

  Kutokana na hali hiyo, Dkt. Khalid ameikaribisha kampuni ya Alteo kwenda Zanzibar kushirikiana na Serikali katika uwekezaji hususani kwenye viwanda vya sukari. Naye Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Patrick de Labauve amesema wamekubali kuongeza maeneo ya uwekezani wa mashamba ya miwa nchini.

  Pia ameomba Serikali iwapatie fursa ya uwekezaji katika sekta ya utalii mkoani Kilimanjaro. “ Kuna vivutio vingi vya utalii ukiwemo mlima Kilimanjaro,”.

  Akizungumzia kuhusu ajira amesema kiwanda cha TPC kimeajiri wafanyakazi 3,000 wakiwemo 1,900 wa kudumu.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMANNE, MACHI 21, 2017.

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mfumo wa kompyuta wa kiwanda cha sukari cha Alteo nchini Mauritius Machi 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akikagua shamba la miwa wakati alipotembelea kiwanda cha sukari cha Alteo nchini Mauritius Machi 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha sukari cha Alteo nchini Mauritius Machi 21, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha sukari cha Alteo nchini Mauritius Machi 21, 2017.

  0 0


  Na: LilianLundo – MAELEZO

  Serikali imefuta usajili wa vibali vya uzalishaji na Uingizaji wa aina 20 ya pombe kali za viroba zilizokuwa zimesajiliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).

  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo, Jijini Dar es Salaam kuhusu usitishaji wa uzalishaji na uingizaji, uuzaji na matumizi ya pombe zilizofungwa katika mifuko ya plastiki (Viroba).

  “Tumefuta usajili wa vibali vya uzalishaji na uingizaji kutoka nje, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizofungashwa katika mifuko ya plastiki (viroba) chini ya ujazo wa milimita 200,” alifafanua Ummy Mwalimu.

  Aliendelea kwa kusema kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa tamko la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alilotoa Februari 02, 2017 la kusitisha uzalishaji, uingizaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe hiyo kali kuanzia Machi 01, 2017.

  Ummy amesema kuwa usitishaji huo unazingatia kanuni za kukataza uzalishaji, uingizaji na matumizi ya vifungashio vya plastiki kufungashia pombe kali za mwaka 2017 (The Environmental Management (Prohibition of Manufacturing, Important and Use of Plastic Sachets for Packakging Distilled and other alcoholic beverages) Regulations 2017) imekatazwa kutumia vifungashio vya plastiki kufungashia pombe kali. Badala yake wazalishaji watapaswa kufungasha pombe kali hizo katika chupa zenye ujazo usiopungua mililita 200.

  Aidha amesema kuwa uamuzi wa kupiga marufuku matumizi ya pombe za aina hiyo unatokana na athari mbalimbali ikiwa ni pamoja na za kiafya na kijamii. Matumizi mabaya ya pombe hizo yamesababisha ajali nyingi, vifo, ulemavu na mzigo mkubwa kwa Serikali wa kutoa huduma kwa wahanga wa pombe hizo na ongezeko la makosa ya jinai.

  Ummy amesema kwamba Viroba vilivyokamatwa na kuzuiwa vinasubiri maelekezo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu namna ya kuviteketeza.

  0 0

  Na Karama Kenyunko,blogu ya jamii.

  Wanachama nane wa chama cha CUF, akiwemo mbunge wa Jimbo la Kaliua Tabora, Magdalena Sakaya Leo wamewasilisha pingamizi la awali dhidi ya kesi ya madai iliyofunguliwa na bodi ya wadhamini ya CUF

  Pingamizi hilo la awali limewasilishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili wa wadaiwa, Mashaka Ngole na litasikilizwa Mbele ya Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri.

  Katika pingamizi hilo, wakili  Ngole amedai kuwa, maombi  yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Bodi ya wadhamini ya CUF kupitia Wakili Hashimu Mziray hayawezi kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

  Amedai kuwa maombi hayo yanashughulikiwa  katika maombi namba 23 ya 2016 yaliyopo Mahakama Kuu Masijala ya Dar es Salaam.

  Ngole ameendelea kudai kuwa,  muombaji hana mguu wa kusimamia (mamlaka) ya kufungua kesi dhidi ya wajibu maombi na kwamba maombi hayo hayana msingi  kwa sababu yameshindwa kubainisha jina  la mwandishi wa masula ya fedha. Aidha wameomba mahakama itupilie mbali maombi hayo kwa garama.

  Kufuatia pingamizi hilo, wakili Mziray aliiomba mahakama iwapatie muda wa kujibu pingamizi hilo kwa kuwa  walikwisha patiwa nakala ya pingamizi hilo.

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 12 mwaka huu ambapo mahakama itasikiliza pingamizi hilo. Kesi ya msingi imepangwa kutajwa Mei 8,2017.

  Awali, Bodi ya wadhamini ya CUF, kupitia wakili Mziray ilifungua kesi ya madai mahakamani hapo ikiomba  zuio la muda ili Sakaya na wenzake saba wasiweze kujihusisha na uongozi wa chama na kufanya mikutano na waliwasilisha maombi hayo chini ya hati ya dharura.

  Katika maombi hayo iliyofunguliwa chini ya hati ya dharula, wajibu maombi ni  Magdalena Sakaya na wenzake Thomas Malima, Maftah Nachumu, Omar Masoud, Abdul Kambaya, Salama Masoud, Zainabu Mndolwa na Jafari Mneke.

  Katika maombi ya  bodi ya wadhamini wanaiomba  mahakama itoe zuio la muda kwa kuwazuia wajibu maombi ama  mawakala wao au watu wao kujihusisha katika masuala yoyote ya uongozi ama kufanya mikutano ya chama hicho, hadi maombi yatakaposikilizwa.

  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango , Dk. Philip Mpango akisaini mkataba wa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Chahua hadi Chaya  kwa mkopo wa Dola Milioni 51 za kimarekani, katika shughuli iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hazina, jijini Dar es salaam leo.
   Naibu Mkurugenzi wa mfuko wa wa Kuwait , Hamad Al-Omar  akiabadilishana mkataba na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk .Philip Mpango.
   Baadhi ya wajumbe kutoka nchini Kuwait wakishuhudia tendo hilo la utiaji Sahii
   Viongozi wa ngazi za juukutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakishuhudia kitendo hicho cha utiaji Sahini.

  0 0

  BODI ya ligi kuu ya Tanzania Bara (TPBL) imefanya mabadiliko ya ratiba ya ligi Kuu kama ifuatavyo

   Ratiba hiyo itahusiana na mechi za timu ya Yanga na Prison (MNO 224) utakaochezwa Mei 06, Yanga na Kagera (MNO 214) Mei 09, Yanga na Mbeya City (MNO 231)Mei 13, Yanga na Toto (MNO 206)Mei 16 zote zitakazochezwa Katika Uwanja wa Taifa.

  Katika mechi zingine ni Ruvu Shooting  na Kagera (MNO 223) Mei 05 kwenye Uwanja wa Mlandizi, Azam na Toto Afrika (MNO 227) Mei 12 uwanja wa Azam Complex, Simba na African Lyon (MNO 219) Mei 07 Uwanja wa Taifa.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Bw. Luca Neghesti kutoka SportPesa Tanzania leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Bw. Neghesti amefuatana na wawakilishi wa timu ya Mpira wa Miguu ya Everton ya nchini Uingereza kumpa taarifa Mhe. Waziri kuhusu maandalizi ya kuileta timu hiyo kucheza mechi za kirafiki nchini Tanzania hivi karibuni. 
  Mhe. Waziri Mahiga akiwa katika mazungumzo na wawakilishi wa timu ya mpira ya Everton ya nchini Uingereza. Timu hiyo ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya kuja Tanzania kwa ajili ya kucheza mechi za kirafiki. Mhe. Waziri alisema ziara hiyo itasaidia kuitangaza Tanzania duniani pamoja na kuhamasisha mchezo wa mpira wa miguu kwa vijana wa Kitanzania. Anaozungumza nao kutoka kulia ni Mkuu wa Uendeshaji wa Mpira wa Miguu (Head of Football Operations) wa timu hiyo, Bw. David Harrison; Mkuu wa Ulinzi na Usalama (Head of Safety and Security) wa timu, Bw. Dave Lewis na Bw. Alan Chisholm kutoka Thomas Cook. 
  Waziri Mahiga akifurahia zawadi ya jezi aliyokabidhiwa na Mkuu wa Uendeshaji wa Mpira wa Miguu (Head of Football Operations) wa timu ya Everton, Bw. David Harrison. Jezi hiyo ni ya Mchezaji wa Timu hiyo ambaye pia ni Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ireland, Bw. Coleman. 
  Picha ya pamoja.   0 0

  Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim, ameondoka nchini baada ya ziara ya kikazi ya siku tatu na kuagwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

  Katika ziara yake ya Siku tatu Dkt. Jim Yong Kim, pamoja na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jonh Pombe Joseph Magufuli, alishiriki tukio la uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya juu (Ubungo Interchange) katika makutano ya barabara Ubungo itakayogharimu Sh.188.7 Bilioni kati ya hizo Benki ya Dunia itatoa Sh186.8 kwa ajili ya ujenzi na usanifu na Sh1.9 Bilioni zitatolewa na Serikali kwa ajili ya kulipa fidia.

  Aidha umma umeshuhudia utiwaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo itakayo fadhiliwa na Benki ya Dunia hapa nchini, yenye thamani ya shilingi Trilioni 1.74.

  Miradi hiyo ni ile ya Uboreshaji Miundombinu ya Usafiri Jijini Dar es Salaam ikiwemo awamu ya tatu na ya nne ya mradi wa mabasi yaendayo haraka-DART, Mradi wa kusambaza maji safi, mazingira na ukusanyaji wa maji taka, na mradi wa uendelezaji wa miji ya Arusha, Dodoma, Tanga, Kigoma, Mwanza, Mbeya, na Mtwara.

  Pia katika ziara hiyo, Dkt. Kim alipata fursa ya kutembelea Shule ya Msingi Zanaki iliyopo Manispaa ya Ilala, ambayo ni moja ya Shule zinazonufaika na mpango wa kuboresha elimu ya msingi. 
  Rais wa Benki ya Dunia (WB) Dkt. Jim Yong Kim (wa pili) na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa pili kushoto), wakitoka katika eneo la kupumnzikia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Waziri Mpango amemuaga Rais huyo baada ya kuwepo nchini kwa takribani siku tatu.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akiagana na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim (wa pili kushoto) baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi hapa nchini, ambapo alishiriki uwekaji wa jiwe la Msingi katika ujenzi wa barabara za juu eneo la Ubungo.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (aliyevaa tai) akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati wa kumuaga Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim aliyekuwepo nchi kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.


  0 0

  Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika kuhakikisha kuwa linaboresha mawasiliano yake baina ya wananchi wanaoishi maeneo jirani na hifadhi wameamua kuwapa mafunzo maalum ya wiki moja yanayolenga kuwajengea uwezo Wahifadhi Ujirani Mwema katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku hususan utoaji wa Elimu ya Uhifadhi kwa wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya hifadhi nchini.Miongoni mwa mammbo ambayo wameweza kujifunza ni utoaji taarifa kwa njia ya habari. Ilikufanikisha hilo TANAPA imewapa mafunzo ya kitaalam maofisa wake hao katika mafunzo yanayoendelea mjini Dodoma. Pichani juu ni Mhariri wa Habari Mwandamizi wa Machapisho ya Mwisho wa wiki ya Gazeti la Habarileo, kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Oscar Mbuza akitoa mafunzo ya uandishi bora wa habari za kijamii kwa maofisa hao.
   Maranyingi habari huendana na picha, ili somo hilo la Habari liwezuri na liende sawa maofisa hao pia walipewa mafunzo ya namna ya upigaji picha bora za Habari na namna ya kutumia Kamera. Mpigapicha Mwandamizi wa Magazeti ya Serikali (TSN), Mroki Mroki alitoa mafunzo hayo kikamilifu.
   Muda wa majadiliano ulikuwepo baada ya kutoa mada, ambapo pia maswali yaliulizwa na kujibiwa.
   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi nae alishiriki mafunzo hayo kama mwenyekiti wa mafunzo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


  Mshambuliaji na Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Ally Samatta anatarajiwa kuwasili nchini leo kuanzia Saa 4:00 usiku kujiunga na kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mchezo ya kirafiki ya kimataifa wiki ijayo.

  Taifa Stars inatarajiwa kucheza mechi mbili, kwanza na Botswana Machi 25 na baadaye Burundi Machi 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na pamoja na Samatta, mchezaji mwingine wa Tanzania anayecheza Ulaya, Farid Mussa anatarajiwa pia kuwasili leo.

  Wakati Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji atatua kwa ndege ya Shirika la Uturuki Saa 4:00 usiku, Farid wa DC Tenerife anatarajiwa kutua kuanzia 9:00 Alfajiri kwa ndege ya KLM.Taifa Stars itamkosa mchezaji mwingine wa Ulaya, Thomas Ulimwengu wa AFC Eskilstuna ya Sweden, ambaye hayuko fiti.

  Taifa Stars inaingia kambini leo kwenye Hoteli ya Urban Rose, Dar es Salaam na kikosi hicho cha kocha Salum Mayanga aki

  saidiwa  na kocha wa Makipa, Patrick Mwangata, Meneja wa timu Danny Msangi, Mtunza Vifaa Ally Ruvu wakati Daktari wa timu atakuwa Richard Yomba na Daktari wa viungo akiwa ni Gilbert Kigadya.  Nyota wengine walioitwa Taifa Stars ni walinda milango
  Aishi Manula (Azam FC), Deogratius Munishi (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).

  Walinzi wa pembeni upande wa kulia aliwataja 
  Shomari Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael (Azam FC).

  Walinzi wa kati ni 
  Vicent Andrew (Yanga SC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Erasto Nyoni (Azam FC) ilihali aliwataja viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC).

  Viungo ni 
  Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Frank Domoyo (Azam FC) na Muzamil Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga SC) na Shizza Kichuya (Simba SC), 

  Farid Mussa (Teneriffe, Hispania) na Hassan Kabunda (Mwadui FC)

  Wakati washambuliaji ni 
  Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yussuf (Kagera Sugar) na Abdul-Rahman Mussa (Ruvu Shooting).


  0 0

  Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ameshinda tuzo ya Afisa Mtendaji Mkuu Bora wa mwaka 2017 inayotolewa na Jukwaa la Wakurugenzi Watendaji Afrika (Africa CEO Forum). Dewji ameshinda tuzo hiyo kwa kuwashinda Abdulsamad Rabiu (CEO wa BUA Group), Issad Rebrab (CEO wa Cevital), Naguib Sawiris ( CEO wa OTMT Investments), Said Salim Awadh Bakhresa (CEO wa Bakhresa Group) na Strive Masiyiwa (CEO wa Econet). Akizungumza kuhusu ushindi huo, Dewji ameishukuru Africa CEO Forum kwa kutambua mchango wake kwa kumchagua kuwa mshindi tuzo hiyo lakini pia kuwashukuru Watanzania na Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwa kazi nzuri ya kudhibiti na kubana matumizi mabaya ya pesa ya umma. 

  “Ninashukuru sana Africa CEO Forum kwa heshima hii ambayo mmenipa, napenda kutoa tuzo hii kwa nchi yangu Tanzania, bila wao nisingekuwa hapa na MeTL Group isingekuwa katika nafasi iliyonayo sasa, nawashukuru sana kwa kuniruhusu mimi na familia nzima ya MeTL kukua na kufika hapa,“Pia napenda kutoa heshima kwa Rais wangu John Pombe Magufuli anafanya kazi nzuri na wote tunajua Afrika inavyokabiliwa na vitendo vya rushwa lakini yeye ni mmoja wa watu ambao wanapambana na rushwa, kubana matumizi mabaya na wenye mwono katika kazi yake.” alisema Dewji. 

  Aidha Dewji alisema kwa sasa bara la Afrika uchumi wake unakua kwa kasi huku akitolea mfano wa ripoti yam waka 2015 ambayo ilionyesha uchumi wa Afrika unakua kwa asilima 4 kwa mwaka kulinganisha na Ulaya inayokua kwa asilimia 1.5 hivyo kuwashauri wanachama wa Afrika CEO Forum kutumia vyema fursa hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii na kuzisaidia nchi za Afrika kukua kiuchumi. Washindi wengine wa tuzo zilizotolewa na Africa CEO Forum ni; CEO of the Year


  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akimkaribisha Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Guo Jinlong, alipowasili na ujumbe wake, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga. (Picha na Bashir Nkoromo).
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Guo Jinlong, baadaya kumookea na ujumbe wake, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

older | 1 | .... | 1619 | 1620 | (Page 1621) | 1622 | 1623 | .... | 3284 | newer