Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1621 | 1622 | (Page 1623) | 1624 | 1625 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye, amekabidhiwa taarifa  dhidi ya uvamizi wa kituo cha utangazaji cha Clouds na kuwashukuru kwa jitihada kubwa walizofanya bila malipo.

  Waziri Nape ameipongeza kamati hiyo kwa kufanya kazi kwa uaminifu mkubwa na kuahidi Kuipeleka taarifa hiyo katika ngazi za juu na kuishukuru kamati hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Mwenyekiti wake Hassan Abbas ambaye pia ni mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo.

  Akipokea taarifa hiyo kutoka kwa Abbas amesema amekabidhiwa taarifa hiyo ikiwa na vielelezo vya picha za mnato (video) na sauti kwa watu waliohojiwa na amewaahidi kuwa atalifikisha mbele zaidi kwani ana wakubwa wengine ambapo yuko Waziri Mkuu, Makamu na Rais Mwenyewe, kwa hiyo kama kuna ushauri, au maelekezo wao ndio wenye mamlaka ya kusema.
   Akisoma ripoti hiyo Katibu wa kamati iliyoundwa na waziri Nape, Deodatus Balile amesema katika kukamilisha ripoti hiyo, walifanya mahojiano na wafanyakazi 14 wa kituo hicho cha radio waliokuwa zamu usiku huo.

  Taarifa hiyo ya kamati ya watu watano imeeleza, ili kukamilisha taarifa hiyo walifanya jitihada za kumtafuta Mkuu wa Mkoa bila mafanikio. "Tulimpigia simu lakini hakupokea, tulimpelekea ujumbe wa maneno lakini hakujibu, na hata tulipoenda ofisini kwake alitokea mlango wa nyuma na kuondoka." amesema Balile.
  Balile ameongeza kuwa baada ya kushindwa kuonana naye, tukajiridhisha kuwa amechagua mwenyewe kutotumia fursa ya kuhojiwa. Taarifa hiyo ilieleza zaidi  kuwa katika uchunguzi wao, walijiridhisha kuwa ni kweli Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  alivamia kituo cha utangazaji cha Clouds akiwa anaendesha gari mwenyewe  akiambatana na askari wenye silaha.
  Akisoma taarifa hiyo ameongeza kuwa, uchunguzi huo walioifanya umeonyesha kuwa Mkuu wa mkoa aliwatisha wafanyakazi hao na kuwalazimisha kurusha kipindi ama sivyo angewaingiza kwenye tuhuma za dawa za kulevya na kuongeza kuwa, kitendo kile kilionyesha kuwa RC aliingilia taratibu zinazofanywa na wahariri kwa kulazimisha Habari anayoitaka irushwe hewani.
  Aidha akiendelea kusoma taarifa hiyo, Balile amesema kamati yao haikupata udhibitisho wowoe kuonyesha kuwa wafanyakazi walipigwa na vitako vya bunduki na kupigwa mitama.
  Kamati hiyo imetoa mapendekezo matatu, likiwemo la kumtaka RC aombe radhi kwa Clouds na kwa wanahabari wote kwa kuingilia Uhuru wa Habari.

  Katika pendekezo lingine kamati  imewataka vyombo vya usalama kufanya uchunguzi dhidi ya askari waliovamia kituo hicho kwa silaha ili waweze kuchukuliwa hatua.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari baada ya  kupokea ripoti ya uchunguzi wa  taarifa  dhidi ya uvamizi wa kituo cha utangazaji cha Clouds baada ya tume ya saa 24 teule kuikamilisha.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akipokea ripoti ya uchunguzi wa  taarifa  dhidi ya uvamizi wa kituo cha utangazaji cha Clouds  kutoka kwa Mwenyekiti kamati hiyo Hassan Abbas ambaye pia ni mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, kulia ni katibu wa kamati hiyo teule Deodatus Balile aliyeisoma ripoti hiyo leo Jijini Dar es salaam.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo amezindua visima vitatu vya Maji vilivyopo Mbagala Maji matitu shuleni, amesema kuwa uzinduzi wa miradi hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Maji Ulimwenguni ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 22 ya mwezi wa tatu.

  Amesema kuwa rasilimali hiyo ni adhimu na ni miongoni mwa rasilimali zinazoathirika sana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

  "Naomba nitoe rai kwa kila mmoja wetu kwa nafasi na majukumu aliyonayo katika sekta ya maji, kuanzia watendaji wa Mamlaka zinazohusika na utoaji wa huduma mpaka mtumiaji mmoja mmoja ahakikishe analinda na kutunza vyanzo vya maji,"amesema Makonda.

  Aidha, kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni "Maji na Majitaka; punguza uchafu yatumike kwa uangalifu" Makonda amewaomba wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinafamu kwenye vyanzo vya Maji kama kando kando kwa mto Kizinga uliopo Temeke.

  Hata hivyo, Makonda ameipongeza Serikali kupitia DAWASA na wadau wa maendeleo wanaosaidia ujenzi wa miradi hiyo, kwani mbali na kuboresha mazingira ya kiafya, itapunguza matumizi ya maji safi kwa shughuli zisizo za lazima.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizindua kisima cha maji Mbagala Maji matitu leo jijini Dar es Salaam. Kuliani Mkuu wa Wilaya Temeke Mh.Felix Lyaniva.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza na na baadhi ya akina Mama wa Mbagala Maji matitu mara baada ya kuzindua visima hivyo,katika maadhimisho ya wiki ya Maji Ulimwenguni leo jijini Dar es Salaam.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimtwisha mama ndoo ya maji marabadaa ya uzinduzi huo.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizindua kisima cha maji Mbagala Maji matitu leo jijini Dar es Salaam. Kuliani Mkuu wa Wilaya Temeke Mh.Felix Lyaniva.

  0 0


  Na Dotto Mwaibale

  SERIKALI ya Tanzania na China zimetiliana saini mkataba wa makubaliano wa utamaduni wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020.

  Nchi hizo zimetiliana saini za mkataba huo kupitia kwa Mawaziri wa wizara husika katika masuala ya utamaduni ambapo kwa China Naibu Waziri wa Utamaduni, Gong Wei alihusika katika tukio hilo.Kwa Upande wa Tanzania Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alishiriki kutia saini.

  Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo, Gong Wei alisema kwa muda mrefu nchi ya China imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika mambo mengi ikiwepo sanaa na utamaduni hivyo akaomba ushirikiano huo uendelee kudumu.

  Alisema katika kudumisha ushirikiano huo Serikali ya China itatoa kiasi cha Yuan laki nne (400,000) kwa ajili ya kununua samani kwa Wizara hiyo ambazo zitatumika katika maofisi ambapo alimuomba Waziri Nape kueleza ni samani gani zitakazo hitajika ili ziletwe.

  Waziri Nape aliishukuru China kwa msaada huo na kusema Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi hiyo katika nyanja mbalimbali.Katika hafla hiyo mawaziri hao waliweza kupeana zawadi mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu.


  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto) na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei (kulia) wakibadilishana mkataba wa makubaliano utekelezaji wa masuala ya Utamaduni baina ya nchi hizo wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Serena ijini Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati), akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei (kulia). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Profesa, Elisante Ole Gabariel.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto), na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei wakiangalia zawadi.
  Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto), na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei wakisaini mkataba huo.
   

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  Klabu ya soka ya Azam fc, iliyokuwa  imelaani vikali  vitendo vya vurugu zilifanywa na timu ya Mbabane swallows katika mchezo ulifanyika nchini Swazland mchezo ambao walikubali kipigo cha goli 3-0, na kusema wao wanaliachilia mbali suala hilo wakijua CAF ndio wenye maamuzi ya mwisho.

   Azam ilikuwa ikishiriki kwenye ikishiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF iliondolewa kwenye michuano hiyo baada ya kushindwa kulinda ushindi wao wa nyumbani wa goli 1-0  na kutolewa kwa jumla ya goli 3-1 mwishoni mwa wiki hii.

  Akizungumzia tuhuma zilizokuwa juu yao kuwa waliwafanyia fujo Mbabane kwenye mechi ya awali iliyochezwa  jijini Dar es saalm, katika uwanja wa Chamazi complex, Ofisa habari wa Azama Jaffar Iddy amesema kuwa hizo taarifa hazina ukweli.

  Iddy amesema sababu ambazo zimesambaa kuwa waliwafanyia fujo Mbabane  sio za kweli bali waliamua tu kutengeneza sababu kwao kuhakikisha wanatimiza azma yao,ambayo  anaamini ndiyo iliyopelekea klabu hiyo kupata matokeo hasi.

  Amesema kwa matokeo waliyoyapata ya kufungwa mabao 3-0, kimpira wameyakubali lakini walicheza katika mazingra magumu sana kwa kuwa waliwachezesha wachezaji ambao walikuwa na majeraha kama Salum abubakari( sure boy) ,akisumbuliwa na dole gumba, Himid mao bega na Frank Domayo akisumbuliwa na Malaria..

  Amesema katika mchezo wa mpira, yote huwa yanatokea katika uhalisia wa matokeo ya mpira ambayo yapo matatu, kufungwa, kushindwa na kutoka sare, hivyo basi wamekubali wamashindwa lakini wao kama Azam fc, jukumu la nini? Kifanyike! baada ya wao kufanyiwa vurugu zile ni jukumu la mechi kamishna maana ndiye alikuwa msimazi wa mchezo hule.

  Pia amesema ingawa wameingia kambini na wachezaji wachache waliopo huku nane(8) wakiitwa kikosi cha timu ya Taifa, (Taifa stars), tayari kwa mchezo wao  na Yanga, unaotarajia kufanyika April mosi mwaka huu, na FA CUP, wanasumbuliwa na baadhi ya wachezaji ambao anaamini wanaweza kukosa michezo kaza inayowakabili, kama Kingu na John bocco, ambaye walimuacha Afrika kusini kwa matibabu Zaidi.

   Ofisa habari wa Azama Jaffar Iddy 

  0 0

   Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
  Jana  kulisambaa habari zisizokuwa za kweli kuhusu kifo cha Diwani wa kata ya Kijichi Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Tausi Milanzi.
  Habari hizo ambazo zililikuwa zinasambaa kwa kasi  kwenye mitandao ya kijamii jambo lililopelekea Globu ya Jamii  kutafuta ukweli wa jambo hilo na kuwasiliana na watu wanaohusika.
  Globu ya Jamii  ilimtafuta Diwani huyo kwa njia ya simu ya kiganjani na kuzungumza nae ambapo amekanusha uwepo wa taarifa hizo na kueleza kuwa yeye ni mzima wa afya na anaendelea na shughuli zake kama kawaida na kuwataka wananchi wake waendelee kumuunga mkono na kupuuza uvumi huo.
  "Mimi mzima na shangaa hao amabo wamezusha kuwa mimi nimefariki Dunia hivyo wanatakiwa  kujua kwamba wao sio Mungu kiasi cha kuamua kukatisha maisha yangu na katika hili nitawachukulia hatua  wale wote walihusika katika uzushi huu kwa mujibu wa sheria"amesema  Tausi Milanzi. 
  Amesema kuwa swala la matumizi ya mitandao limekuwa kubwa sana kwa sasa hivyo lazima niwafikishe  katika vyombo vya sheria wote  waliohusika kusambaza ujumbe huu wa kifo changu jambo ambalo si kweli.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) leo tarehe 22 Machi, 2017 amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Mabalozi Wateule 7 wanaowakilisha nchi zao nchini kutoka Hungary, Belarus, Guinea, Botswana, Niger, Cyprus na Bangladesh. Pichani Balozi Mahiga akipokea nakala za hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Hungary nchini, Mhe. Laszlo Eduard Mathe mwenye makazi yake Nairobi, Kenya.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akipokea nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Belarus nchini, Mhe. Dmitry Kuptel mwenye makazi yake Addis Ababa, Ethiopia. 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa na Balozi Mteule wa Guinea nchini Mhe. Sidibe Fatoumata KABA mwenye makazi yake Addis Ababa, Ethiopia mara baada ya kupokea Nakala zake za Hati za Utambulisho.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Botswana nchini, Mhe. Lebonaamang Thanda Mokalake mwenye makazi yake Lusaka, Zambia.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwasha mshumaha mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Kampuni ya Ujenzi wa Nyumba za Mkopo katika Jimbo la Chennai Nchini India. Kushoto ya Balozi Seif ni Rais wa Jumuiya ya Makampuni ya Nichan Nchini India Bwana Manohar Nichani, Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi Dr.
  Sira Ubwa Mambora, Kayibu Mkuu Wizara ya Kilimo Nd. Juma Ali na Kaimu Balozi wa Tanzania Nchini India Balozi Mohamed Hija. Kulia ya Balozi Seif ni Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini India Bibi Haika Msuya na  Mwakilishi wa Taasisi ya Kitaifa ya mpango wa kilimo kinachotumia mbolea za Asili India Bwana Satyajit Kittur Mjini Chennai.
   Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akizungumza na Mwakilishi wa Taasisi ya Kitaifa ya mpango wa kilimo kinachotumia
  mbolea za Asili India Bwana Satyajit Kittur Makao Makuu ya Kampuni ya Ujenzi ya Nchini India Mjini Chennai.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiongea na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Kimataifa ya Miot Dr. Malika Mohandazaz kwenye Hotelli ya Crowne Plaza Mjini Chennai kabla ya kurejea Mjini New Delhi.
   Mke wa Makamu wa Pili wa Raios wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akibadilishana mawazo nammoja wa Viongozi Wandamizi wa Hospitali ya Miot Mjini Chennai kabla ya Kuelekea Mjini New Delhi. 
  Picha na – OMPR – ZNZ. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0


  Maofisa wa Jeshi la Polisi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambyo ni Mwanza, Kigoma, Kagera,Geita, Mara, Shinyanga, Simiyu pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka  nchini (DPP) Biswalo Mganga, wamenufaika na elimu kuhusu sheria namba 4 ya mwaka 2010, kwenye sekta ya ujenzi.
  Elimu hiyo imetolewa leo katika ufunguzi wa mkutano wa   mashauriano kati ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi,Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Mashitaka,  uliofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall Jijini Mwanza.
  Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi Mbunifu Majengo Dkt. Ambene Mwakyusa amesema, malengo ya mkutano huo ni kubadilishana uzoefu,ili kuongeza ufanisi katika kusimamia utekelezaji wa Sheria Na. 4 ya mwaka 2010 bila vikwazo  pamoja na kujitambulisha kwa wadau,shughuli za bodi,kuelimisha umuhimu wa kuwatumia wataalamu katika shughuli za ujenzi.
  Kamishna wa Polisi (Operesheni na Mafunzo), Nsato Marijani akiongea katika mkutano huo jijini Mwanza.
  Mwenyekiti wa Bodi Mbunifu Majengo Dkt. Ambene Mwakyusa, akizungumza na wanahabari nje ya ukumbi wa mkutano wa   mashauriano kati ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi,Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Mashitaka,  uliofanyika Jijini Mwanza.

  0 0

  Na MatukiodaimaBlog Same 

  MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Mhe. Rosemary Sitaki Senyamule ambae ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ameendelea na mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kukamata shamba la mirungi. 
   Mkuu huyo wa wilaya amesema  kuwa Shamba hilo limekamatwa leo kata ya Vudee, kijiji cha Kisesa wilayani humo pamoja na mtuhumiwa aliyekuwa mmiliki wa shamba hilo. 
   "Tunaendelea na utekelezaji wa agizo la Rais Dkt John Magufuli la kupambana na dawa za kulevya na mbali ya misako endelevu tumekamata pia miche 1450 iliyokuwa ikimwagilia..... analitunza sana shamba lama kama vile ni la  mazao ya chakula"
  "Tumewapa siku 2 ndugu zao wahakikishe wameng'oa mirungi hiyo na kuiteketeza" mkuu huyo alisema na kuongezea kwamba  bado kazi ya kuwasaka wote wakulima wa bangi, mirungi na Viroba inaendelea 
   "Watu wamekuwa wagumu sana kuacha hii biashara. Na sisi tutapambana kwa kutolala mpaka mirungi inaisha Ardhi ya Same" alitoa wito kwa wana Same kulima mazao sahihi ya chakula na biashara badala ya kulima bangi na Mirungi ambayo amesema mwisho wake ni jela

  Mkuu wa wilaya ya Same Mhe. Rosemary Sitaki Senyamle akiwa na mtuhumiwa mkulima wa Mirungi. 


  .
  mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamle akiwa katika shamba la Mirungi baada ya kukamata kwa watuhumiwa wakulima wa zao hilo haraamu 


  0 0

  MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella, amesema Utafiti mpya wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi kwa kutumia mfumo wa (CD4T-cell count) utasaidia kupunguza maambukizi ya Ukimwi.

  Amesema Utafiti huo utaangazia pia kuwepo kwa Viashria vya Usugu wa dawa, kiwango cha maambukizo ya Kaswende na homa ya Ini kwa watu wenye umri wa miaka 15 na zaidi.

  Amesema Tafiti tatu zilizotangulia zimekuwa zikiwahusiha wananchi wenye umri wa miaka 15 hadi 49 tofauti na utafiti wa mwaka 2016/ 2017 ambao ni wa kipekee ambapo kwa mara ya kwanza wananchi wa rika zote katika kaya zilizochaguliwa watahusihwa.

  Kwa upande wake, Meneja Takwimu Mkoa wa Tanga, Tonny Mwanjoto, aliwataka Makatibu Tawala kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi pamoja na wanafunzi shuleni kutokomeza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

  Alisema kufanya hivyo itasaidia juhudi za Serikali kuhakikisha maambukizi ya VVU yanapungua ikiwa na pamoja na kuyatokomeza moja kwa moja.
  Baadhi ya Wajumbe wa mkutano wa Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi 2016/17 wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwa Makatibu Tawala kutoka Wilaya za Tanga na Wawakilishi wa TACAIDS pamoja na Wadau wa Maendeleo uliofanyika leo ukumbi wa mikutano jengo la Mkuu wa Mkoa.

  0 0
  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah  Kairuki amesema kwamba serikali itahakikisha kwamba Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) tawi la Mbeya kinakuwa na majengo yake ili kupunguza gharama za uendeshaji.

  Kwa sasa chuo hicho kinatumia majengo ya kukodi ambayo ni mali ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya,majengo hayo yapo eneo la  soko Matola, Chuo kinahudumia wakazi wa Nyanda za Juu Kusini.

  Akiwasilisha taarifa ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania tawi la Mbeya mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge  Utawala na Serikali za Mitaa  Waziri Kairuki alisema gharama ya kodi ya shilingi milioni 24 kwa mwezi ni kubwa na kwamba serikali iko katika mchakato wa kuhakikisha kwamba chuo hicho kinamilikishwa mjengo hayo ili kupunguza gharama za uendeshaji.

   Aidha Waziri huyo alisema kwamba serikali itahakikisha kwamba chuo kinakuwa na wakufunzi wa kutosha ili kuendesha kozi zake kwa ufanisi.

  Mkuu wa TPSC Dk.Henry Mambo aliiambia kamati hiyo kuwa tawi la Mbeya linakua kwa kasi kwani kwa sasa lina wanafunzi 1236, tawi hilo lilizinduliwa mwaka 2014 likiwa na wanafunzi 453.

   Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge  Utawala na Serikali za Mitaa  Mhe. Jason Rweikiza akizugumza na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) tawi la Mbeya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo hawapo pichani katika Ukumbi wa chuo hicho Jijini Mbeya, kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah  Kairuki, kulia ni Mkuu wa TPSC Dk.Henry Mambo. Picha na Kenneth Ngelesi
  Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Tawi la Mbeya Dk. Heriel Nguvava katikati akiwaonyesha chumba cha Kompyuta wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge  Utawala na Serikali za Mitaa  walipofanya ziara chuo hapo kushoto ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Jason Rweikiza kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah  Kairuki. Picha na Kenneth Ngelesi. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA


  0 0
 • 03/22/17--12:47: KANUSHO
 • Tunapenda kutaarifu Umma kuwa kuna mtu aliyefungua ukurasa katika mtandao wa kijamii wa ‘Twitter’ kwa kutumia jina la Mhe. Charles Mwijage(MB), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji na kuweka taarifa kuwa “Kilichotokea kwa Clouds Media ni kitendo cha kinyama na wala si uungwana kabisa tunajenga nchi ya viwanda na si ya kutishana”

  Wizara inakanusha taarifa hiyo ya kizushi iliyosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii yenye lengo la kuleta chuki na kuchafua jina la Waziri pamoja na Wizara yetu kwa ujumla.

  Wizara inachukua hatua za kisheria kuwatambua wale wote waliohusika na kutengeneza ukurasa huo bandia.

  Tunatoa wito kwa wahusika wote kuacha mara moja kusambaza taarifa hii potofu.


  IMETOLEWA NA

  KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI,

  WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI

   22 March, 2017

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Droo ya makundi ya klabu Bingwa Afrika inatarajiwa kupangwa  kwa timu 16 kuingia kwenye makundi manne.

  Timu hizo zimepangwa kwenye vyungu vinne kulingana na alama zao ndani ya miaka mitanoi kulingana na ushiriki wao kwenye michuano ya kimataifa.

  Makundi yatakuwa manne kila POT Itatoa  timu moja ili kuunda makundi manne timu zimepangwa kwenye Pot kulingana na Pointi zao za CAF Kwa miaka Mitano.  

  DROO YA MAKUNDI 

  POT 1
  -Al Ahly (Misri) 
  -Zamalek (Misri) 
  -Etòile du Sahel (Tunisia) 
  -Mamelodi Sundowns (Africa kusini) 

  POT 2
  -Al Hilal (Sudani) 
  -Espèrance de Tunis (Tunisia) 
  -Wydad Casablanca (Morroco) 
  -USM Alger (Algeria) 

  POT 3
  -Al Merreikh (Sudani) 
  -Cotton Sports -Ivory Coast 
  -As Vita Club (Congo) 
  -Al-Ahli Tripoli (Libya) 

  POT 4
  -St George(Ethiopia)
  -Ferroviario Maputo (Msumbiji)  
  -Zanaco Fc (Zambia) 
  -CAPS United (Zimbambwe) 


  0 0


   Baadhi ya watanzania waishio nchini Mauritius na maofisa wa serikali ya Tanzania wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye hoteli ya Meridien, nje kidogo ya mji Port Louis Machi 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Baadhi ya watanzania waishio nchini Mauritius na maofisa wa serikali ya Tanzania wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye hoteli ya Meridien, nje kidogo ya mji Port Louis Machi 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Baadhi ya watanzania waishio nchini Mauritius na maofisa wa serikali ya Tanzania wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye hoteli ya Meridien, nje kidogo ya mji Port Louis Machi 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na watanzania wanaosoma na wale wanaoishi nchini  Mauritius kwenye hoteli ya Meridien, nje kidogo ya mji wa Port Louis.
   Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na watanzania wanaosoma na wale wanaoishi nchini  Mauritius kwenye hoteli ya Meridien, nje kidogo ya mji wa Port Louis, Machi  22, 2017.  Kulia ni Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed na kushoto ni Balozi wa heshima wa Tanzania nchini Mauritius, Merday Venkatasamy.

  0 0  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akimkaribisha Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong Ikulu jijini Dar es salaam kwa mazungumzo leo Jumatano Machi 22, 2017 .
  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akitambulishwa kwa ujumbe aliofuatana nao Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Machi 22, 2017 
  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli katika mazungumzo na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Machi 22, 2017 
  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongozana na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Machi 22, 2017 
  Rais Dkt John Pombe Magufuli akifurahia wakati Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong alipokuwa akisalimia viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Machi 22, 2017 
  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Machi 22, 2017 .

  0 0

  Bonge la supermarket jipya lipo katika jengo la kituo kikuu cha daladala  cha Makumbusho jijini Dar es salaam ambako utapata  BIDHAA KIBAO kwa bei  poa kabisaaa kama vile Mikate, keki,  biscuit wanazopika wenyewe pamoja na vyakula vya kila aina vinapatikana hapo
  Usipitwe...Fanya uwatembelee CHOPPIES ukajipatie vitu vingi kwa bei ya kiwandani na wapo wazi kuanzia saa 12:00 kamili asubuhi mpaka saa tatu usiku siku za Jumatatu mpaka Ijumaa.Siku za weekend wako wazi kuanzia saa 03:00 kamili asubuhi mpaka saa 3 usiku. 

  KARIBUNI SANA!
  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack ameagiza wakurugenzi wa mamlaka za Serikali za Mitaa na Maji kuhakikisha hakuna mtu anayefanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji.

  Telack alitoa agizo hilo juzi wilayani hapa katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese wakati wa kilele cha maadhimisho Wiki ya Maji yaliyofanyika kijiji cha Sekeididi.

  Aliagiza wakurugenzi hao kuhakikisha vyanzo hivyo vinapandwa miti ili kutunza uoto wa asili ambao mara nyingi huathiriwa na ukame kutokana na kukosekana kwa miti.Mkuu huyo wa mkoa aliwataka viongozi hao wasimamie utekelezaji wa sheria ya utunzaji wa mazingira ili kunusuru vyanzo vya maji, kwani Serikali inatumia fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya maji.

  “Utunzaji wa vyazo vya maji ni jambo muhimu katika upatikanaji wa maji na hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kutunza vyanzo vya maji kwa kupanda miti eneo linalozunguka vyanzo.“Kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004, kifungu cha 57, kifungu kidogo cha 1 kinakataza mtu yeyote kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kwenye vyanzo vya maji,” alisema.

  Maadhimisho hayo yaliambatana na zoezi la upandaji miti kwenye bwawa la Sekeididi ambalo litakuwa likitoa huduma ya maji kwa wananchi wa maeneo hayo.Telack aliwataka wananachi kuiunga mkono Serikali katika jitihada zake za kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yao.
  Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maji kimkoa
  Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akipanda mti wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maji kimkoa.
  Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese (katikati) akiongozwa na Kaimu Mhandisi wa Maji, Wilaya, Bernad Bwire (wa pili kushoto) kutembelea bwawa la maji na kupanda miti katika kilele cha Wiki ya Maji. Wengine pichani kushoto ni mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mohamed Mlewa (kushoto) na Kaimu Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari, Steven Cleophace (kulia).


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Standard Chartered Kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati Bw. Sunil Kaushal pamoja na ujumbe wake uliomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Standard Chartered Kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati Bw. Sunil Kaushal ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
  Picha ya pamoja.

  0 0

  Mgeni rasmi wa Mkutano wa 26 wa Mwaka wa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango akitoa hotuba yake wakati akiufungua Mkutano huo, unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, Jijini Arusha. Akifungua Mkutano humo, Waziri Mpango ameupongeza Mfuko huo kwa kwa kutekeleza kwa vitendo Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka mitano na kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2015 kupitia kwenye uwekezaji wa viwanda. akilizungumzia swala la waajiri wenye tabia ya kutowaunganisha wafanyakazi wao na mifuko ya jamii, Waziri Mpango amesema kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria ya nchi, hivyo amewataka Waajiri wenye tabia hiyo kuacha mara moja.
   Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua Mkutano wa 26 wa Mwaka wa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, Jijini Arusha.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Hijjah akihutubia katika ufunguzi wa Mkutano wa 26 wa Mwaka wa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, Jijini Arusha.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akitoa taarifa fupi ya Mfuko kwa Wadau na Wanachama, katika Mkutano wa 26 wa Mwaka wa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, Jijini Arusha.
   Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. Martin Mmari akiwasilisha mada katika Mkutano wa 26 wa Mwaka wa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, Jijini Arusha.

   Sehemu Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakifatilia Mkutano huop katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, Jijini Arusha. 
  Sehemu wa Wakurugenzi wa Mifuko ya Jamii, wakiwa katika Mkutano huo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

older | 1 | .... | 1621 | 1622 | (Page 1623) | 1624 | 1625 | .... | 3283 | newer