Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1615 | 1616 | (Page 1617) | 1618 | 1619 | .... | 3283 | newer

  0 0


  Waziri wa michezo wa Zanzibar, Rashid Ali Juma (pili kulia) akiwa na viongozi wa ZFA mara baada ya Zanzibar kutangazwa kuwa mwanachama wa 55 wa CAF.


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Chama cha mpira wa miguu Zanzibar (ZFA) wilaya ya Magharibi A Unguja kimewapongeza wajumbe wa mkutano mkuu wa shirikisho la soka barani Afrika CAF kwa uamuzi wao wa kukubali ombi la chama hicho kuwa mwanachama wa 55 wa shirikisho hilo.

  Mwenyekiti wa ZFA wilaya hiyo Kheri Adam Aliy ameitaja hatua hiyo kuwa ni mafanikio makubwa katika historia ya soka la Zanzibar na Tanzania mwa ujumla.

  Katika taarifa yake mara baada ya kupokea taarifa za kupatiwa uwanachama kamili kwa Zanzibar, Adam aliwapongeza pia viongozi wa shirikisho la soka Tanzania TFF, Chama cha soka Zanzibar ZFA, serikali zote mbili (Zanzibar na jamhuri ya muungano wa Tanzania) kwa kuendelea kufuatia haki hiyo toka lilipowasilishwa ombi hilo mwaka 2004 na kupelekea mwaka 2006 kupatiwa uanachama mshiriki.

  Aliitaja hatua hiyo iliongeza matumaini na subra kwa wadau wa Soka la Zanzibar, subira ambayo imezaa matunda baada ya sehemu hiyo ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa mwanachama wa kamili.

  Adam aliwataka wadau wa soka kuongeza mashirikiano kati yao na kuwasaidia viongozi wa chama cha soka wa ngazi zote kuweza kusimamia shughuli za mpira kama inavyotakiwa na CAF na mashirikisho mengine ya kimataifa.

  Amesema ipo haja kwa viongozi wa wilaya kujiandaa kisaikolojia na kupokea mabadiliko mbali mbali ya uongozi na utendaji ili kuendana na matakwa ya shirikizho hilo linalosimamia masuala ya soka barani.

  Katika hatua nyengine Mwenyekiti huyo alimpongeza Ahmad Ahmad kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa CAF akichukua nafasi ya  Issa Hayatou ambae amelitumikia shirikisho hilo kwa muda mrefu kwa kipindi cha miaka 29.
  Waziri wa michezo wa Zanzibar, Rashid Ali Juma akiwa ameshikilia bendera ya Tanzania mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Shirikisho la soka wa Barani Afrika na kuipitisha Zanzibar kuwa mwanachama kamili wa 55.

  0 0

  Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu,alipokuwa akiwafafanulia jambo wakati   kamati hiyo ilipofanya ziara ya kikazi  makao makuu ya kampuni ya hiyo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali  zinazofanywa na kamapuni hiyo.
   Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge,Mhe Anna Lupembe (katikati)akifurahia jambo na Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu(kushoto)na Mkuu wa kitengo cha Uendeshaji wa Mtandao Andrew Lupembe, wakati   mwanakamati huyo na wenzake walipofanya ziara ya kikazi  makao makuu ya kampuni ya hiyo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali  zinazofanywa na kamapuni hiyo.
   Baadhi ya wajumbe wa  kamati ya kudumu ya Bunge wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa kitengo cha Undeshaji wa Mtandao wa Vodacom Tanzania PLC, Andrew Lupembe,alipokuwa akiwafafanulia jambo wakati   kamati hiyo ilipofanya ziara ya kikazi  makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali  zinazofanywa na kamapuni hiyo.
   Mwenyekiti wa kamati ya  kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu Mhe.Prof Norman Sigalla (katikati)akisisitiza  jambo kwa Uongozi wa Vodacom Tanzania PLC wakati   kamati hiyo ilipofanya ziara ya kikazi  makao makuu ya kampuni ya hiyo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali  zinazofanywa na kamapuni hiyo,kushoto  ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani  na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa kampuni hiyo,Alec Mulongo.
  Kaimu Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC,Alec Mulongo akimsomea waraka wa matarajio (Prospectus) Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu, Mhe.Prof Norman Sigalla wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kikazi  makao makuu ya kampuni ya hiyo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali  zinazofanywa na kamapuni hiyo.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(wa pili kulia) akiwa katika meza kuu na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kushoto) kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza, uliofanyika leo katika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam . Wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (wa kwanza kulia) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Edith Mallya.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba kufungua rasmi Mkutano huo.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba akiwasilisha hotuba yake kwenye Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza.
  Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba fupi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (hayupo pichani).

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
 • 03/17/17--08:40: NBS NEWS LETTER

 • 0 0

  Droo ya robo fainali ya ligi ndogo ya Ulaya (Europa League) imepangwa leo mchana.


  0 0

   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (aliyesimama) akiwaeleza jambo wajumbe wa kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakati  Kamati  hiyo  ilipotembelea Azam Media jana Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Azam Media Bw.Tido Muhando.
   Mkurugenzi wa Azam Media Bw. Tido Muhando (aliyesimama) akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii (hawapo pichani) utendaji kazi wa Chombo hicho wakati  Kamati  hiyo  ilipotembelea Azam Media jana Jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura.
   Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mhe. Faustine Ndugulile akizungumza  jambo  kwa Kamati hiyo na uongozi wa Azam Media wakati Kamati ilipotembelea chombo hicho jana Jijini Dar es Salaam.

   Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakimsikiliza Mkurugenzi wa Azam Media Bw. Tido Muhando(hayupo pichani ) wakati Kamati ilipotembelea chombo hicho jana Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wa kwanza kushoto akizungumza na wasikilizaji wa Uhai Radio wakati  Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii ilipotembelea studio hizo jana Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na wanachi wa Kata ya Boko NHC wakati wa makabidhiano ya mradi wa maji katika Kata hiyo  leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja  akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda wakati wa makabidhiano ya mradi wa maji katika Kata hiyo  leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana.

   Mwenyekiti wa Kamati ya Maji Boko NHC ,Dk. Alexander Kyaruzi akizungumza wakati wa kukabidhiwa mradi wa maji ya Dawasco  Boko  leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji wa Dawasco  Boko NHC, leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO,  Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) akisaini makubaliano na mwenyekiti wa kamati ya Maji Boko NHC, Dk. Alexander Kyaruzi leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisalimiana na wananchi baada ya kuzindua mradi wa maji wa Dawasco  Boko NHC, leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza jana.
  Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.


  0 0  0 0

  Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ameeleza kufurahishwa kwake baada ya kuhojiwa na Mamlaka ya kuzuia na Kupambana na Dawa za kulevya nchini.
  Mbunge huyo amezungumza hayo  jijini Dar es salaam baada ya kuhojiwa na Mamlaka hiyo, ambapo alisema roho yake imesuuzika kwani jamii imeamini kwamba hahusiki kwa namna yoyote ile na biashara hiyo haramu.
  "nashukuru kwa kuhojiwa huku nimepata nafasi ya kueleza ukweli juu ya jambo hili ambalo lilishaanza kuleta taharuki katika jamii, sasa umma umejua kuwa siuzi wala sihusiki na dawa za kulevya roho yangu imesuuzika "alisema Ridhiwani
  Alisema vita ya dawa ya kulevya ni kubwa na inapaswa kupigwa na kila mmoja ili kuokoa kundi kubwa la vijana ambao wanaathirika kutokana na suala hilo na kwamba kuhojiwa kwake kumemfanya awe na amani.
  Msikilize hapa:

  0 0


  In Tanzania, there are these cab drivers called, "Dala Dala". They are the most bootleg and unsafe cab drivers I've ever seen in my life. I started to ponder and think to myself...how would a Dala Dala driver be like, if he was an Uber Driver??? Subscribe to ZMaster Productions!
  ---------------------------------------
  Social Media: 
  YouTube: Subscribe Link: http://www.youtube.com/subscription_c...

  Website: www.zmasterproductions.com

  Twitter: @ZulfiqarManzi

  Facebook: Zulfiqar Manzi

  Instagram: @zulfiqarmanzi29

  Snapchat: ZulfiqarManzi

  Playlist Link: https://www.youtube.com/playlist?list...

  Channel Link: https://www.youtube.com/user/SuperZ29  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys imepangwa  Kundi B katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, zitakazofanyika nchini Gabon kuanzia Mei 14 hadi 28, mwaka huu.

  Serengeti walifuzu kuingia katika fainali hizo baada ya kushinda rufaa yao dhidi ya Congo Brazaville kushindwa kumpeleka mchezaji wao aliyechezeshwa kwenye kikosi cha vijana lakini akisadikiwa kuwa ni mkubwa kiumri tofauti na kanuni za mashindano hayo. 
  Congo Brazaville walishindwa kumuwasilisha kwa vipimo zaidi ya mara tatu walipohitajiwa na CAF na hivyo CAF kuamua kuwaondoa kwenye nafasi hiyo na kuchukuliwa na Tanzania..
  Kundi B, Serengeti Boys wamepangwa na Angola, Niger na Mali ambapo kwa sasa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limewafungia baada ya Serikali ya nchi hiyo kuingilia masuala ya soka na  kuwafukuza viongozi wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo (FEMAFOOT).  
  Kundi A lina timu za wenyeji Gabon, Guinea, Cameroon na Ghana na ikumbukwe timu mbili za juu kila kundi zitafuzu moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia za U-17 nchini India baadaye mwaka huu.


  Awali  fainali hizo zilitakuwa kufanyika nchini Madagascar lakini Gabon aliyekuwa rais wa  Shirikisho la Soka Afrika (CAF)  Issa Hayatou wa Cameroon alisema  nchi hiyo haikukidhi vigezo vya kuandaa mashindano hayo.

  Kikosi cha timu ya Tifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys.


  0 0


  0 0  0 0

  Mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Graca Machel amesema mapinduzi yanayotakiwa kufanyika hapa nchini kwa sasa ni ya kuwainua wanawake kiuchumi, kiafya na kijamii.
  Mama Machel, ambaye ni mke wa Hayati Nelson Mandela amesema hayo leo Ijumaa wakati wa mkutano na wanahabari alipozindua mpango wa kuwainua wanawake Afrika."Mapinduzi ya kwanza yalifanikiwa wakati ule tunatafuta uhuru lakini,"amesema.
  Mama Machel amesema wanawake hawana budi kushika usukani katika kuhakikisha wanafanikiwa kiuchumi na katika sekta zote za maendeleo.
  Kwa upande wake Mwanzilishi wa Tanzania Women Chambers, Anjelina Maleko amesema kama wanawake wamebarikiwa kwa jambo moja hawana budi kuwa baraka kwa wenzao.
  Mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Graca Machel akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa kuhusu changamoto wanazozipata wanawake kiuchumi na katika sekta zote za maendeleo wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuwainua wanawake Afrika uliofanyika katika leo jijini Dar es Salaam.
  Rais wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction Limited Bi. Maida Waziri akiongea akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchango wa Mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini mama Graca Machel alivyomsaidia kufikia malengo hasa kwenye suala la elimu.
  Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Jacqueline Mneney Maleko akizungumzia mafanikio yake pamoja na njia wanazoweza kuzitumia wanawake ili kufikia malengo waliyojiwekea.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  BALOZI wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Richard Lupembe, ameweka wazi kuwa Azam FC ni moja ya timu zinazowatia moyo  Watanzania wanoishi nje ya nchi, huku akiipa mkono wa ushindi kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Mbabane Swallows ya Afrika Kusini.


  Lupembe alitoa kauli hiyo wakati alipoitembelea timu hiyo jana kwenye kambi yake katika Hoteli ya Acardia jijini Pretoria, nchini humo ikijiandaa na mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa wa Somhlolo nchini Swaziland Jumapili hii saa 10.30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

  “Kwa kweli nimefarijika sana kwa kuiona Azam FC tena kama nakumbuka mlikuja hapa mwaka jana, mlikuja hapa kucheza na  Bidvest nikawa mgeni rasmi na mkono wangu ukawa wa kheri mkashinda, nawahakikishieni nitawashika tena mkono na ninauhakika mtashinda tena,” alisema Lupembe

  Balozi  wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Richard Lupembe akiwa pamoja na wachezaji wa Azam wakati alipoitembelea timu hiyo jana kwenye kambi yake katika Hoteli ya Acardia jijini Pretoria, nchini humo ikijiandaa na mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa wa Somhlolo nchini Swaziland Jumapili hii saa 10.30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.alip

  Kocha wa Azam ... akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi  ya kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku ya Jumapili.
  Beki wa Kulia wa Azam, Shomari Kapombe akiwa anagombania mpira na Kingue wakati wa mazoezi ya timu hiyo  kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku  ya Jumapili.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa Msumbiji Mhe. Carlos Agostinho do Rosario walipokutana na kufanya mazungumzo ya kikazi mjini Mbabane Swaziland leo March 17,2017

  0 0

  Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu Mhe.Prof Norman Sigalla (katikati)akisisitiza jambo kwa Uongozi wa Vodacom Tanzania PLC wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kikazi makao makuu ya kampuni ya hiyo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kamapuni hiyo,kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa kampuni hiyo,Alec Mulongo.
  Kaimu Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC,Alec Mulongo akimsomea waraka wa matarajio (Prospectus) Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu, Mhe.Prof Norman Sigalla wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kikazi makao makuu ya kampuni ya hiyo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kamapuni hiyo.
  Baadhi ya wanakamati ya kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu,alipokuwa akiwafafanulia jambo wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kikazi makao makuu ya kampuni ya hiyo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kamapuni hiyo.
  Mwanakamati wa kamati ya kudumu ya Bunge,Mhe Anna Lupembe (katikati)akifurahia jambo na Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu(kushoto)na Mkuu wa kitengo cha Uendeshaji wa Mtandao Andrew Lupembe, wakati mwanakamati huyo na wenzake walipofanya ziara ya kikazi makao makuu ya kampuni ya hiyo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kamapuni hiyo.
  Baadhi ya wanakamati ya kamati ya kudumu ya Bunge wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa kitengo cha Undeshaji wa Mtandao wa Vodacom Tanzania PLC, Andrew Lupembe,alipokuwa akiwafafanulia jambo wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kikazi makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kamapuni hiyo.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Iran Nchini, Mhe. Mousa Farhang kabla ya mazungumzo yao, kwenye Makazi yake, Oysterbay jijini Dar es salaam, Machi 17, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Iran Nchini, Mhe. Mousa Farhang kwenye Makazi yake, Oysterbay jijini Dar es salaam, Machi 17, 2017

  0 0


  Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Jim Yong Kim (pichani), atafanya ziara ya kikazi nchini kuanzia tarehe 19 hadi 21 Machi 2017. 
  Akiwa nchini, Dkt. Kim atafanya mazungumzo na Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu Jijini Dar es Salaam siku ya Jumatatu, tarehe 20 Machi 2017 pamoja na kushiriki uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara za Juu katika eneo la Ubungo (Ubungo Interchange). 
  Katika mazungumzo yao, Viongozi hao watajadili namna bora ya kuimarisha zaidi uhusiano uliopo kati ya Tanzania na benki hiyo. Vilevile, watazungumzia miradi mikubwa inayotarajiwa kutekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia katika kipindi kijacho. 
  Aidha, baada ya mazungumzo hayo, Rais Magufuli na mgeni wake watashuhudia uwekwaji saini wa mikataba mitatu:  (i) Uboreshaji Miundombinu ya Usafiri Jijini Dar es Salaam ikiwemo awamu ya tatu na ya nne ya mradi wa DART pamoja na ujenzi wa barabara ya juu katika eneo la Ubungo (Dar es Salaam Urban Transport Project (DUTP); (ii) Awamu ya pili ya mradi waUboreshaji wa Upatikanaji wa Maji safi na uboreshaji wa miundombinu ya maji taka (Water and Sanitation Project) na (iii) Uboreshaji wa Miundombinu na Hudumaza msingi katika baadhi ya miji (Tanzania Strategic Cities Project). 
  Wakati wa ziara hiyo, Dkt. Kim atapata pia fursa ya kutembelea Shule ya Msingi Zanaki ambayo ni moja ya Shule zinazonufaika na mpango wa kuboresha ubora wa elimu ya msingi unaogharamiwa na Benki ya Dunia. 
  Ziara ya Dkt. Kim inafuatia ziara iliyofanywa nchini na Makamu wa Rais wa Benki hiyo wa Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop mwezi Januari 2017 ambapo alishiriki uzinduzi wa mradi wa mabasi ya mwendo kasi (BRT) uliofanyika kwenye kituo kikuu cha mabasi hayo kilichopo Kariakoo jijini Dar Es Salaam. 
  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,


  Dar es Salaam, 17 Machi, 2017


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Alhaji Majid Mwanga kuwasaka, kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wafugaji wote wanaodaiwa kuhusika katika matukio ya kuwashambulia kwa viboko wananchi wa Kijiji cha Fukayosi kilichopo Wilayani humo.
  Mhe. Dkt. Magufuli aliyekuwa akisafiri kwa gari kutoka Dodoma kwenda Jijini Dar es Salaam ametoa agizo hilo leo tarehe 17 Machi, 2017 aliposimama katika kijiji hicho baada ya kuona wananchi wengi wakiwa wamekusanyika kando ya Ofisi ya Kata.

  Baada ya kusimamisha msafara wake, Mhe. Rais Magufuli aliwaita wananchi waliokuwa wamekusanyika huku wakiwa wameshika mabango yaliyoandikwa ujumbe wa kutaka wafugaji wa jamii ya Wamang’ati waondolewe na kisha akatoa nafasi kwa baadhi yao kueleza dukuduku lao.

  Wananchi hao ambao ni wakulima na mfugaji mmoja aliyejitokeza wakaeleza kuwa Wamang’ati wamekuwa wakiwanyanyasa kwa kuingiza mifugo katika mashamba yao ya mazao na wakithubutu kuwakataza wamekuwa wakichapwa viboko na baadhi kuuawa.

  Katika majibu yake, pamoja na kutaka wote wanaodaiwa kuwashambulia wananchi kwa viboko wakamatwe Mhe. Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kukomesha mara moja vitendo vya wafugaji kuwapiga wakulima na wakulima kuwapiga wafugaji, na pia kukomesha vitendo vya wafugaji kulisha mifugo yao katika mashamba ya wakulima.

  “Kuanzia leo isitokee mfugaji kumpiga mkulima, mkulima kumpiga mfugaji wala mfugaji kulisha mifugo yake kwenye mashamba ya wakulima, na suala hili nitalifuatilia mimi mwenyewe.

  “Kwa hiyo Mkuu wa Wilaya na Viongozi mlishughulikie hili kabla mimi sijawashughulikia nyinyi...Wale waliopiga watu, nataka wote wakamatwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria” amesema Mhe. Dkt. Magufuli.


  Gerson Msigwa

  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

  Dar es Salaam


  17 Machi, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisiliza changamoto za wakulima na wafugaji katika kjijiji cha Fukayosi wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro hiyo akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo akielezea changamoto za wakulima na wafugaji katika kjijiji cha Fukayosi wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro hiyo akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisiliza changamoto za wakulima na wafugaji katika kjijiji cha Fukayosi wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro hiyo akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanakjijiji wa  Fukayosi wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji  akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maagizo kwa Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mhe. Maggid Mwanga baada ya kuongea na wanakjijiji wa  Fukayosi wilayani humo aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji  akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017.
  Wananchi wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  alipokuwa akiongea nao katika kijiji cha  Fukayosi wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji  akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017. PICHA NA IKULU

older | 1 | .... | 1615 | 1616 | (Page 1617) | 1618 | 1619 | .... | 3283 | newer