Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

BREAKING NEWZZZ: RAIS DKT. MAGUFULI AFUTA AGIZO LA KUFUNGA NDOA KWA SHARTI LA KUWA NA CHETI CHA KUZALIWA

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari Mkoani Dodoma kuhusiana na kufuta agizo lililotolewa jana na Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu Wananchi wanaohitaji kufunga ndoa kuanzia mwezi Mei mwaka huu kuwa na vyeti vya kuzaliwa. Rais Mhe. Dkt. Magufuli ameagiza utaratibu wa awali uendelee kutumika kwasababu wananchi wengi wa Tanzania hawana vyeti, hivyo wangekosa haki hiyo ya kufunga ndoa. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana. PICHA NA IKULU


KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII YAIPONGEZA TASUBA.

0
0
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imeipongeza Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) kwa juhudi zake inazozifanya katika kuibua na kukuza vipaji vya Vijana nchini.

Pongeza hizo zimetolewa leo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani na Wajumbe wa Kamati hiyo wakati walipoitembelea taasisi hiyo kwa ajili ya kukagua mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo.

Akiongea wakati wa kikao na Watendaji wa Taasisi hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Peter Serukamba amesema kwamba, suala la muziki, filamu na utamaduni ni suala la kipaji, hivyo halihitaji elimu kubwa kwa vijana, bali kuwepo na mazingira mazuri yatakayowezesha wenye vipaji na wasio na vipaji waweze kupata fursa ya kujifunza na kuonyesha vipaji vyao.

Mhe. Serukamba amelishauri Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kuweka mazuri ambayo hayatawabana vijana ambao hawakupata fursa ya elimu lakini wana vipaji, hivyo ameshauri vijana nchini wapewe fursa ya kujifunza na vipaji vyao viendelee kuibuliwa.

Sambamba na hilo, Mhe. Serukamba ameishauri taasisi hiyo kutoa elimu ya lugha mbalimbali kama vile lugha za Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kijerumani, Kichina na nyinginezo ili ziweze kuwasaidia vijana hao wawapo nje ya nchi na pindi wanapokuwa wameiva katika masomo yao ndani ya chuo hicho.

“Chuo hiki naomba kione namna ya kufundisha lugha pamoja kwamba mnafundisha muziki, basi vema mkawafundisha vijana wetu lugha mbalimbali ili waweze kwenda Duniani, kwasababu kama watakuwa na tatizo la lugha itawapa shida”, alisema Serukamba.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, wakionyeshwa vifaa vitumikavyokatika uhariri wa kazi za sanaa walipoingia katika moja ya Studio ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) kujionea utendaji kazi wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Peter Serukamba akiongea na Wafanyakazi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) mara baada ya kuwasili katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kukagua mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017. 
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii pamoja na Wafanyakazi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakijadiliana wakati wa kikao 17 Machi, 2017. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiongea na Wafanyakazi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakati wa kikao cha kukagua mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017. 

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHUDHURIA MKUTANO WA ASASI YA SIASA ULINZI NA USALAMA SADC

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, usiku huu anahudhuria Mkutano wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama unaojulikana kama SADC Double Troika, mjini Mbabane Swaziland. Mkutano ambao unajadili kwa kina hali tete ya usalama katika Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo( DRC) na Nchi ya Lesotho, ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Asasi hiyo.


(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

DK.SHEIN AZUNGUMZA NA WANA CCM PEMBA

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCm Zanzibar Dk.Ali Mohamed Sheuin (katikati) akimkabidhi Mwakilishi wa Jimbo la Mkoani Pemba CCM pia Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Mmanga Mjengo Mjawiri (kulia) vifaa vya Michezo kwa niaba ya Jimbo lake vitakavyotumika katika mashindano ya mpira wa miguu kwa majimbo 18 ya Pemba,chini ya ufadhili wa Mfanya bishara na Kada wa CCM Mohamed Raza Daramsi (kushoto) hafla iliyofanyika ukumbi wa Fidel Castro leo.
Miongoni mwa Vijana wa CCM wa Majimbo 18 ya mikoa ya Pemba CCM wakiwa katika sherehe za kubabidhiwa vifaa vya Michezo vya Mpira wa Miguu vitakavyofanikisha mashindano ya Majimbo hayo,vilivyotolewa na Mfanya bishara na Kada wa CCM Mohamed Raza Daramsi na kukabidhiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCm Zanzibar Dk.Ali Mohamed Sheuin (hayupo pichani) katika ukumbi wa Fidel Castro wilaya ya Chake chake Pemba leo
Miongoni mwa Vijana wa CCM wa Majimbo 18 ya mikoa ya Pemba CCM wakiwa katika sherehe za kubabidhiwa vifaa vya Michezo vya Mpira wa Miguu vitakavyofanikisha mashindano ya Majimbo hayo,vilivyotolewa na Mfanya bishara na Kada wa CCM Mohamed Raza Daramsi na kukabidhiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCm Zanzibar Dk.Ali Mohamed Sheuin (hayupo pichani) katika ukumbi wa Fidel Castro wilaya ya Chake chake Pemba leo,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Sheuin (katikati) akimkabidhi Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani Suleiman Makame Ali (kulia) vifaa vya Michezo kwa niaba ya Jimbo lake vitakavyotumika katika mashindano ya mpira wa miguu kwa majimbo 18 ya Pemba,chini ya ufadhili wa Mfanya bishara na Kada wa CCM Mohamed Raza Daramsi (kushoto) hafla iliyofanyika ukumbi wa Fidel Castro leo,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCm Zanzibar Dk.Ali Mohamed Sheuin akizungumza na Viongozi wa CCM na Vijana UVCCM wa Majimbo 18 ya Mikoa ya Pemba katika hafla ya kukabidhi vifaa vya Michezo vilivyotolewa na Mfanyabishara na Kada wa CCM,pia Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Unguja, Mohamed Raza Daramsi, hafla iliyofanyika ukumbi wa Fidel Castro leo,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCm Zanzibar Dk.Ali Mohamed Sheuin akipiokea Kombe la Mashindano ya Mpira wa miguu katika Timu mbali mbali za majimbo 18 ya Mikoa ya Pemba,kutoka kwa Mwanamichezo, Mfanyabishara na Kada wa CCM,pia Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Unguja, Mohamed Raza Daramsi,(kushoto) katika hafla ya kukabidhi vifaa vya Michezo vilivyotolewa na Raza katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Fidel Castro leo,

[Picha na Ikulu.]

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KWA KUSHIRIKIANA NA MRADI WA SPANEST YAFANYA MAFUNZO YA SIKU TATU KATIKA FANI YA UTALII NA UKARIMU KWA WAHITIMU 74 MKOANI MBEYA

0
0
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Constantine Mushi amewataka wamiliki wa hoteli kuajiri wafanyakazi wenye ujuzi katika fani ya ukarimu na utalii baadala ya kuajiri ndugu zao wasio na ujuzi wowote na kuwalipa ujira mdogo hali inayochangia kuzorotesha huduma za utalii mkoani hapo.

Alisema wahudumu walio wengi katika hoteli hizo wamekuwa kero katika utoaji wa huduma kwa watalii pindi wanapotembelea kuja kuona vivutio vya utalii vilivyopo mkoani hapo.

Ametoa raia hiyo jana wakati akifunga mafunzo hayo kwa jumla ya wahitimu 74 yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wa SPANEST unaotekelezwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

Amesema mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa siku tatu kwa lengo la kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa katika sekta ya ukarimu na utalii ili kukidhi mahitaji ya soko, pamoja na kukuza hadhi ya huduma za malazi zilizopo chini ya kiwango kwa mikoa ya Nyanda za juu kusini.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Constantine Mushi akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufunga mafunzo ya jumla ya wahitimu 74 waliopewa mafunzo ya siku tatu katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST Mkoani Mbeya, lengo likiwa ni kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa katika sekta hiyo ili kukidhi mahitaji ya soko, pamoja na kukuza hadhi ya huduma za malazi zilizopo chini ya kiwango. Wengine ni Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki (kushoto) Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskas Mwiru (kulia).

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Constantine Mushi akizungumza na wahitimu kabla ya kufunga jana mafunzo hayo fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu na kuhudhuriwa na jumla ya wahitimu 74. Wengine ni Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki (kushoto) Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskaz Mwiru (kulia)

Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki akizungumza na   wahitimu waliohitimu jana mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu na kuhudhuriwa na jumla ya washiriki 74.

Baadhi ya wahitimu waliohitimu jana mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu na kuhudhuriwa na jumla ya washiriki 74.

KIKAO CHA UPITIAJI/UHAKIKI WA MIPANGO KABAMBE YA AFYA YA MWAKA 2017/18 CHAFANYIKA MJINI DODOMA

0
0
 Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya , Dkt Zainabu Chaula akizungumza na  baadhi ya wajumbe wa timu za uendeshaji wa huduma za afya,waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na waganga wafawidhi wa Hospitali za Rufaa na Mikoa nchini juu ya Upitiaji/Uhakiki wa Mipango Kabambe ya Afya ya mwaka 2017/18 kwa kuhusisha ngazi za Mikoa, Halmashauri na Wizara ,Mjini Dodoma. 
 Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya , Dkt Zainabu Chaula akiwaonyesha  Ilani ya Uchaguzi baadhi ya wajumbe wa timu za uendeshaji wa huduma za afya,waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na waganga wafawidhi wa Hospitali za Rufaa na Mikoa nchini juu ya Upitiaji/Uhakiki wa Mipango Kabambe ya Afya ya mwaka 2017/18 kwa kuhusisha ngazi za Mikoa, Halmashauri na Wizara ,Mjini Dodoma. 
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya, Dkt Zainabu Chaula akizungumza na  baadhi ya wajumbe wa timu za uendeshaji wa huduma za afya,waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na waganga wafawidhi wa Hospitali za Rufaa na Mikoa nchini juu ya Upitiaji/Uhakiki wa Mipango Kabambe ya Afya ya mwaka 2017/18 kwa kuhusisha ngazi za Mikoa, Halmashauri na Wizara ,Mjini Dodoma.

 Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Huduma za Afya   Idara ya Afya Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI), Dkt Anna Nswira  akizungumza na  baadhi ya wajumbe wa timu za uendeshaji wa huduma za afya,waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na waganga wafawidhi wa Hospitali za Rufaa na Mikoa nchini juu ya Upitiaji/Uhakiki wa Mipango Kabambe ya Afya ya mwaka 2017/18 kwa kuhusisha ngazi za Mikoa, Halmashauri na Wizara ,Mjini Dodoma.

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya ,Dkt Doroth Gwajima  akizungumza na  baadhi ya wajumbe wa timu za uendeshaji wa huduma za afya,waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na waganga wafawidhi wa Hospitali za Rufaa na Mikoa nchini juu ya Upitiaji/Uhakiki wa Mipango kabambe ya Afya ya mwaka 2017/18 kwa kuhusisha ngazi za Mikoa, Halmashauri na Wizara ,Mjini Dodoma.

HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI NAPE NNAUYE KWENYE KIKAO KAZI CHA MAAFISA HABARI MKOANI DODOMA

LAPF WATOA REFLECTOR JACKET 500 KUSAIDIA BODA BODA WILAYANI KISARAWE MKOANI PWANI

0
0
 Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe (wa pili kulia), akimkabidhi moja ya jaketi angavu (Reflector Jacket) kati ya majaketi 500 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda katika hafla iliyofanyika wilayani humo jana. LAPF imetoa majaketi hayo kwa ajili ya kusaidia waendesha bodaboda ili waweze kutambulika wakiwa katika shughuli zao za kila siku.Kutoka kushoto ni Meneja wa Mfumo wa Uchangiaji wa Hiari wa LAPF, Hanim Babiker, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, William Gama na Meneja wa LAPF, Kanda ya Mashariki,  Lulyalya Sayi. 
 Waendesha boda boda wa Wilaya ya Kisarawe wakiwa kwenye mkutano huo.
  Waendesha boda boda wa Wilaya ya Kisarawe wakiwa kwenye mkutano huo.
  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe, akionesha moja ya jacket katika mkutano huo. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Kisarawe, Abel Mudo na kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri wa wilaya hiyo, Khamis Dikupatile.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Rais wa Uganda alaani mauaji ya Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini humo, aagiza kufungwa kamera za usalama katika Miji mikubwa

0
0
Raisi wa Uganda, Yoweri Kaguta Museven amelaani mauaji ya Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda ambaye pia alikuwa ni Naibu Mkuu wa Jeshi hilo, Andrew Kaweesi na walinzi wake wawili ambao walishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana katika eneo la Kulambiro, Kisaasi kaskazini mashariki mwa mji mkuu Kampala, Nchini Uganda jana. 

Bado haijajulikana sababu hasa ya kutekelezwa mauaji hayo ingawa serikali imeagiza kufungwa kwa kamera za usalama katika miji mikubwa yote nchini humo wakati huu uchunguzi ukifanywa.

Katika kipindi cha miaka saba iliyopita takribani matukio ya mauaji 12 yametekelezwa na washambuliaji waliokuwa wakiendesha pikipiki maarufu kwa jina la boda boda ambao walitoroka eneo la tukio na kutopatikana licha ya jitihada za polisi kuendelea kufanyika kuwatafuta.

Kwa mujibu wa Luteni Jenerali, Henry Tumukunde, mara nyingi vitendo hivi hufanyika kwa umakini kujiamini na ujasiri huhakikisha wameua kabisa kabla ya wauaji kutokomea.

Hotuba ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari wakati wa ufungaji wa Kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano.

AJALI YA GARI YATOKEA KIMARA SUKA JIJINI DAR ES SALAAM, WAMSHAMBULIA MWANDISHI ALIYEKUWA AKICHUKUA PICHA ZA TUKIO

0
0
Gari aina ya Mark II Grand yenye namba za usajili T145AMZ likiwa limeivaa daladala lenye namba za usajili T992DGZ lililokuwa limepaki kituoni KIMARA -SUKA jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa wapo eneo la tukio ilionyesha dereva wa gari hilo dogo alikuwa amelewa na ndipo aliposhindwa kukamata breki na kujikuta uvunguni kwa daladala hilo.
Vijana wakijaribu kuiba katika gari ndogo iliyokuwa imepata ajali eneo la Kimara Suka jijini Dar es Salaam.
Vijana ambao walivamia gari ndogo na kuanza kuiba wakishangaa kuona kamera ya Kajunason Blog imetinga eneo hilo na ndipo walipoungana na mwenye gari kumfanyia fujo na kumpiga kwa kumshambulia mwandishi wa habari Cathbert Angelo Kajuna aliyekuwa eneo la tukio. 

Kwa msaada wa wasamalia wema waliweza kumnasua mwandishi huyo na kumshika kijana aliyekuwa mmiliki wa gari ndogo ambaye ndiye alitoa amri ya kumshambulia mwandishi wa habari.

 Kijana aliyemshambulia mwandishi wa habari Cathbert Angelo Kajuna amekamatwa na kufunguliwa jarada la KMR/RB/3987/2017 na mpaka sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kituo cha Mbezi kwa Yusuph.

DK. AYUB RIOBA AWANOA KWA SEMINA YA WELEDI WAANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA UHURU, JIJINI DAR ES SALAAM, LEO

0
0
 Mwandishi wa habari nguli wa siku nyingi,Dk. Ayub Ryoba, akiendesha semina ya kunoa weledi wa taaluma ya uandishi wa habari kwa waandishi wa habari na baadhi ya watumishi wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd, Wachapishaji wa Magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, leo katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam. Dk. Ryoba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), ana shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) katika Sayansi ya Jamii aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 Mwandishi wa habari nguli wa siku nyingi,Dk. Ayub Ryoba, akiendelea kutoa 'nondoz' kwa wafanyakazi hao wa UPL, huku wafanyakazi hao wakimsikiliza kwa makini sana
 Mwandishi wa habari nguli wa siku nyingi,Dk. Ayub Ryoba, akifafanua mada zake kwenye semina hiyo ya kunoa weledi wa kitaaluma
 Washiriki wa semina hiyo wakiwa ukumbini.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Ujenzi wa barabara za juu Ubungo kugharimu shilingi bilioni 188.71

0
0




Na. Immaculate Makilika –MAELEZO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kushirikiana na Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Jim Yong Kim wanatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za juu (Ubungo interchange) eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam Machi 20 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inasema kuwa mradi wa ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya Ubungo yatagharimu takribani shilingi bilioni 188.71 ambapo una lengo kupunguza msongamano wa magari katika barabara za Morogoro, Nelson Mandela na Sam Nujoma.

“Mradi huo ni sehemu ya uboreshaji usafiri Jijini Dar es Salaam yaani (Dar es salaam Urban Transport Improvement Project), utakaogharimiwa kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia na mchango wa Serikali ya Tanzania”

Aidha, taarifa hiyo ilisema kuwa, mradi huo utahusisha pia awamu ya tatu na ya nne ya ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (Bus Rapid Transit- BRT), katika barabara ya Nyerere kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam hadi Gongo la mboto na barabara ya Bagamoyo kutoka katikati ya jiji hadi Tegeta.

AFISA USTAWI WA JAMII AWATUPIA LAWAMA WAKUU WA IDARA KUHUSU KUFUMBIA MACHO VITENDO VYAUNYANYASAJI WA KIJINSIA

0
0
AFISA Ustawi wa Jamii Wilaya ya Wete Haroub Suleiman Hemed amewatumia zigo la lawama baadhi ya wakuu wa Taasisi na Idara za Serikali kwa akidai kwamba hawana mchango wowote katika kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji .

Amesema baadhi ya wakuu hao wa Idara na Taasisi za Serikali wameshindwa kuonyesha nguvu zao katika kuunga mkono mapambano dhidi ya matendo hayo yanayoendelea kuiathiri jamii wakiwemo watoto wadogo .

Akizungumza kwenye kikao cha Maofisa wa Serikali ya Wilaya ya Wete , kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya , amesema wakuu hao wa Idara na Taasisi ni kikwazo kinachoviza mafanikio ya kuyatokomeza matendo hayo.

Ameeleza kwamba baadhi ya watumishi wa Serikali wanaokabiliwa na kesi ya udhalilishaji , hawahudhurii kikao wakiitwa huku hata wakuu wao wa taasisi hizo nao pia wameshindwa kushirikiana na Ofisi ya Ustawi wa Jamii kutafuta ufumbuzi wa masuala hayo.

“Baadhi ya wakuu wa Idara NA Taasisi za Serikali wanakuwa ni kikwazo katika kufanikisha mapambano dhidi ya matendo ya udhalilishaji , kwa kuwa wanashindwa kutoa ushirikiano wanapotakiwa kufanya hivyo ”alisema.
Na Masanja Mabula –Pemba

MD KAYOMBO AWAONYA MAAFISA WATENDAJI WA KATA NA MITAA KUTOPOKEA RUSHWA

0
0

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Maafisa Watendaji wa Kata 14, Watendaji wa Mitaa 91 pamoja na Wahasibu wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wameonywa kutopokea Rushwa wala hongo ya aina yoyote kutoka kwa wamiliki wa biashara mbalimbali katika Manispaa hiyo kwani kufanya hivyo watadhoofisha ukusanyaji wa mapato ya serikali kama ilivyokusudiwa.

Kauli ya onyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati akitoa ufafanuzi wa muongozo wa ukusanyaji wa mapato na kutoa maelekezo ya majukumu ya kazi kwa Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa kwenye kikao cha kazi kilichofanyika leo Jumamosi Machi 18, 2017 katika ukumbi wa Ofisi za Manispaa hiyo ilipo Mtaa wa Kibamba CCM.

Kayombo ameeleza kuwa kwa mtumishi yoyote wa Manispaa kwa ngazi yoyote atakayebainika kujihusisha na ubadhilifu kwa kuchukua Rushwa kwa walipa kodi atachukuliwa hatua Kali za kisheria kwa kuiibia serikali kwani kuihujumu serikali kwa kuiibia mapato au kuzuia ukusanyaji wa mapato ni kosa kwa mujibu wa taratibu na sheria.

“Nina amini kwamba mnaishi vizuri na wananchi wenu kwahiyo mnawafahamu vizuri wafanyabiashara wanaokwepa kulipa Kodi lakini hata walipaji wazuri hivyo jambo la ukusanyaji mapato litakuwa jepesi sana kwenu kutokana na uzoefu mlionao” Aliongeza Kayombo

Mkurugenzi huyo amewasisitiza Watendaji hao kusimamia vyanzo vyote vya mapato ikiwemo Hotel Levy, Service Levy, Mabango makubwa na madogo (Bill Board), Leseni za biashara na Vileo, Upimaji afya kwa ngazi za Mitaa hususani katika Migahawa.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa ufafanuzi wa muongozo wa ukusanyaji wa mapato kwa Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa
Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
MD Kayombo akisisitiza jambo



Waziri Ummy atoa rai kwa madaktari kuomba nafasi za kazi Nchini Kenya

0
0

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto imebainisha kuwa inatarajia kuwapeleka Madaktari wake waliopo nchini Tanzania kwenda kufanya kazi nchini Kenya kufuatia kuombwa na Rais wa nchi hiyo Mhe. Uhuru Kenyatta.

Akizungumza na vyombo vya habari mapema leo, Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu amesema kuwa, ujumbe maalum kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta kupitia kwa Wiziri wake wa Afya uliokutana na Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na kuomba ombi lao hilo la kutaka madaktari 500, ambao wataajiliwa kwa mikataba maalum ya kuanzia miaka 2 kwa kufanya kazi nchini Kenya.

“Natoa rai kwa madaktari wazawa waliopo nchini kuomba nafasi za ajira ya Udaktari nchini Kenya kwa mkataba maalum. Zoezi hilo limeanza rasmi leo Machi 18 mpaka Machi 27, mwaka huu wawe wameomba.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa waombaji ni wale watakaokidhi vigezo maalum ikiwemo asiwe katika utumishi wa Umma, Asiwe amejiliwa na mashirika ya umma ama mashirika teule ambayo yanalipiwa na Serikali.

Kwa Mujibu wa Waziri Ummy ameeleza kuwa muombaji lazima awe amehitimu mafunzo ya “internalship” na mwisho awe amesajiliwa na baraza la Madaktari nchini.

Aidha, Waziri Ummy ameweka wazi kuwa, ajira hiyo itakuwa ni ya miaka miwili ambapo watapata mishahara na malupulupu mbalimbali katika ajira zao hizo huku akibainisha kuwa, jambo hilo ni jema na linaiingizia Taifa sifa kwa kupeleka wataalamu wake nje ya nchi kupata ajira.

Kwa upande Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa, moja ya vigezo ambavyo vinahitajika kwa madaktari hao ni pamoja na kuwa na digrii ya kwanza na Internal ship huku akiongeza kuwa, kwa upande wao Wizara imejipanga kuimalisha madaktari wa ndani ikiwemo kiwaajili.

Naye Katibu Mkuu Utumishi, Mh. Laulian Ndumbalo amewatoa hofu watanzania licha ya kuwapeleka Madaktari hao nje kupatiwa ajira, nchini bado ina Madaktari wengi wanaofikia zaidi ya 1000, huku kila mwaka wakiajili Madaktari 400 hadi 450.

Imeelezwa kuwa Madaktari hao watakaojitokeza watapata faida kubwa kwani watakuza mahusiano mema ya nchi za Afrika Mashariki kupitia kada hiyo huku pia wakitarajia kuipatia maendeleo nchi ya Tanzania. Jambo ili ndio la kwanza linafanyika huku ikielezwa kuwa idadi hiyo ya madaktari kutoka Tanzania kwenda kupatiwa ajira nje ya mipaka yake ni kubwa, licha ya madaktari wengi kuwepo nchi mbalimbali ikiwemo Malawi, Zambia, Afrika Kusini, Botswana na mataifa mengine.

Madaktari hao wenye kutaka kujiunga wanaweza kutembelea tovuti ya wizara ya Afya na kupata maelezo mbalimbali.

DIAMOND AULA UBALOZI WA BIDHAA ZA GSM

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul (Diamond Platnum) amekuwa Balozi wa Bidhaa za GSM na kuwataka watanzania wanunue bidhaa hizo kuacha kutumia gharama kwa kufuata nje ya nchi.

Akizungumza leo na waandishi wa habari, Diamond amesema kuwa licha ya kuwa balozi katika bidhaa za GSM ameweza yeye kununua kutokana vitu mbalimbali katika maduka hayo.

Amesema kuwa GSM walikuwa na uwezo wa kutafuta wasanii wa nje ya nchi lakini wakaona kuna umuhimu wa kuwatumia wasaani wa ndania kama mabalozi katika bidhaa zao. 
 
"Hivyo katika hilo na kuchangia maendeleo kwa wasanii wetu wa hapa nyumbani,wanaojituma na kuonesha mafanikio yao makubwa kwa kile wanachokifanya,sisi kama GSM tumeamua kutimia msanii Diamond Plutnum kuwa Balozi wa bidhaa zetu" alisema

Aidha amesema kuwa ubalozi huo utafanya kutangaza muziki wake kwa mashabiki wa ndani na wan je ya nch. Diamond amesema kuwa balozi hakuadhiri ubalozi mwingine kutokana kuwa kinachotangazwa ni bidhaa ambazo haziingiliani. 

 Msanii wa Bongo Fleva,  Nasibu Abdul (Diamond Platnum) akizungumza na waandishi habari baada ya kukabidhiwa ubalozi wa bidhaa za GSM leo jiiini Dar es Salaam.
 Afisa Masoko wa GSM, Lauma Mohammed  akizungumza na waandishi wa habari juu ya Diamond kuwa Balozi wa Bidhaa za GSM leo jijini Dar es Salaam.
 Waandishi wa habari wakimsikilizwa Msanii wa Bongo Fleva,  Nasibu Abdul (Diamond Platnum)  hawapo pichani leo jijini Dar es Salaam.  

UFUNGUZI WA MASHINDANO YA MAJESHI VISIWANI ZANZIBAR

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 kwa mwaka 2017 leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya SMZ katika Ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 1i kwa mwaka 2017 (BAMATA) yaliyofanyika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja leo.
Maaskari wa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi na Usalama wakiwa katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika sherehe za Ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 kwa mwaka 2017yaliyofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) wakiangalia ratiba Ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 kwa mwaka 2017 (BAMATA) na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance S. Mabeyo (kushoto) katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika sherehe zilizofanyika leo (kulia) Waziri wa Ulinzi Majeshi ya Kujenga Taifa Mhe,Dkt.Hussein Mwinyi. 
Kikosi cha Maaskari Kanda ya JKT wakipita mbele ya Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na kutoa heshima wakati ufunguzi wa Michezo ya Majeshi ya 17 ya mwaka 2017 (BAMATA)katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika sherehe zilizofanyika leo.

DKT SHEIN AFANYA UTEUZI.

0
0
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu namba 17 cha sheria ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia namba 6 ya mwaka 2016, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, amemteua Bwana Omar Zubeir Ismail kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mamlaka ya Kudhibiti Utafutaji na Uchimbaji wa mafuta na gesi asilia, Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo, Bwana Omar Zubeir Ismail alikuwa Ofisa Mwandamizi katika Idara ya Nishati, Zanzibar.

Uteuzi huo uliosainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, umeanza leo tarehe 18 Machi 2017.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO-ZANZINAR

18 Machi 2017

WANAWAKE WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KUTUNZA MAZINGIRA

0
0
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Ruvuma kupitia chama tawala CCM JACKLINE MSONGOZI, amewataka wanawake mkoani humo kuwa mstari wa mbele katika kupambana na uharibifu wa mazingira unaofanywa na baadhi ya wananchi ili kulinda mazingira.
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images